Mahojiano ya Makongoro Nyerere katika Raia Mwema


CHARLES Makongoro Nyerere (CMN) ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliotangaza nia ya kutaka kuchaguliwa kuwania urais kupitia chama hicho mwaka huu. Raia Mwema lilifanya naye mahojiano wiki hii nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

RAIA MWEMA: Kwanini wana CCM wanatakiwa wakuchague wewe uwe mgombea wao na si mwingine miongoni mwa wenzako 41 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo?

MAKONGORO: Mimi si mwizi, wala mla rushwa. Nina uzoefu wa kutosha na nakijua chama changu. Pia ni mtu ambaye napenda kufuata utaratibu. CCM sasa inahitaji mtu wa namna hiyo.

RAIA MWEMA: Kwanini unadhani uadilifu ndiyo sifa kuu ya Rais ajaye wa Tanzania?

MAKONGORO: Naamini kuwa ni mtu mwadilifu pekee ndiye ambaye ataisaidia nchi yetu kuondokana na matatizo tuliyonayo. Ufisadi, wizi wa mali ya umma na matatizo yote tuliyonayo yataondoka endapo tutampata kiongozi ambaye ni muadilifu. Kinachotakiwa ni kwa chama kujisafisha chenyewe kwanza. CCM ikiwa safi, serikali itakuwa safi tu. Lakini serikali haiwezi kuacha kuwa ya kifisadi wakati chama chetu kina mafisadi na tunawavumilia.

RAIA MWEMA: Ina maana kama utafanikiwa kuwa Rais na hatimaye Mwenyekiti wa CCM unaweza kuwafukuza wanachama wote wenye tuhuma za ufisadi?

MAKONGORO: Hapana, siwezi kumfukuza mwanachama kutoka CCM. Tunachoweza kufanya ni kuwatoa kutoka katika nafasi zao za uongozi. Nitakupa mifano miwili kueleza hili. Kwa mfano wewe ni Mwislamu. Dini yako inataka uwe unaswali swala tano kwa siku. Sasa pale msikitini kwako una Imamu ambaye kwa siku anahudhuria swala moja au asihudhurie kabisa. Lakini kila siku unaambiwa anaonekana klabu ya pombe akinywa. Sasa huyu imamu dawa yake si kumvua Uislamu wake. Unachofanya ni kumtoa kwenye uimamu na kumpa mtu mwingine ambaye hatawakwaza. Kama wewe ni Mkristo na una Paroko ambaye kila kukicha ana kashfa za ngono na wake za watu ingawa hajawahi kukutwa huyo si paroko. Sasa ikitokea siku akanusurika kufumaniwa hadi akaacha mavazi yake ya uparoko kule Guest House lakini akachoropoka bila kukamatwa; huyo humvui Ukristo wake. Unachofanya ni kumtoa kwenye Uparoko wake. Chama ni imani kama zilivyo dini. Huwezi kumwondoa mtu kwenye chama lakini unaweza kumwondoa kwenye nafasi za uongozi. Kwa kifupi, kuna maparoko na maimamu wa aina hiyo ndani ya CCM ambao ni lazima kuwaondoa kwenye nafasi zao kama kweli tunaitakia mema nchi yetu.

RAIA MWEMA: Unasema chama ni imani lakini wewe uliondoka CCM na kuhamia NCCR Mageuzi kwenye miaka ya 1990. Ilikuaje ukahama chama chako?

MAKONGORO: Mojawapo ya matatizo ya chama chetu ambayo ni lazima Rais ajaye apambane nayo ni ukweli kwamba kuna majimbo ya uchaguzi hapa Tanzania ambayo kama mtu hutoi rushwa huwezi kupita. Arusha ni mojawapo ya maeneo hayo. Yaani kama hula hela sahau kuhusu kuchaguliwa. Utafanyiwa mizengwe na viongozi wala rushwa hadi mwenyewe utachoka na kukata tamaa. Mimi mwaka ule wa 1995 nilikumbwa na tatizo hilo. Nilitaka ubunge pale Arusha lakini mtandao wa rushwa ulikuwa ukiniwekea vikwazo. Sasa wazee wawili wa pale; mmoja amefariki dunia na mwingine yuko hai, wakanishauri kuwa kwa vile wananchi wananitaka na shida yao ni kiongozi mzuri, nihamie kwenye chama kingine. Ndiyo nikaenda NCCR Mageuzi na nikapata ubunge. Haya ndiyo mambo ambayo yamenifanya niingie kwenye kinyang’anyiro kwa sababu hali inazidi kuwa mbaya. Kama hali ikiachwa hivi basi hata kwenye urais atakayeshinda atakuwa ni mla rushwa tu na nchi itakwenda vibaya sana.

RAIA MWEMA: Kuna taarifa kwamba Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, aliwahi kutaka kukuteua kuwa mbunge wakati akiwa Rais lakini wewe ulikataa. Kuna ukweli gani katika hili?

MAKONGORO: Katika watu ambao nawaheshimu sana kama viongozi hapa nchini, Mzee Mkapa ni mmoja wao. Aliikuta nchi ikiwa na hali mbaya sana lakini akaicha pazuri. Aliikuta inanuka madeni lakini akaondoka akiiacha na akiba kubwa ya fedha za kigeni. Sasa miezi 18 kabla hajamaliza urais wake, aliniambia anataka kuniteua kuwa mbunge. Ni kweli kuwa nilikataa nafasi hiyo. Nilikataa kwa sababu ingeonekana anampendelea mtoto wa Nyerere. Ingeonekana kama anatoa zawadi. Na pengine ingeweza kujenga picha kuwa nimebebwa. Nilikataa kwa sababu sikutaka mtu ambaye ninamuheshimu sana anyooshewe vidole kwa ajili yangu. Nilimueleza sababu zangu na nashukuru mzee yule alinielewa vizuri.

RAIA MWEMA: Ni kweli kwamba baba yako, Mwalimu Julius Nyerere, hakujua kwamba uko vitani Uganda wakati wa Vita ya Kagera hadi baada ya vita kumalizika?

MAKONGORO: Ni kweli. Unajua mimi nilikwenda vitani nikiwa na umri wa miaka 18 tu ambao ndiyo ulikuwa umri mdogo zaidi kuruhusiwa kwenda vitani wakati huo. Wakati vita inaanza mimi nilikuwa kwenye mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwenye Operesheni iliyojulikana kama Chakaza. Wale waliokuwa JKT walipatiwa mafunzo kidogo na kisha kupelekwa vitani. Mimi pia nikaenda lakini sikumwambia baba. Ulikuwa ni uamuzi wangu binafsi. Kuna kaka zangu walikuwa jeshini tayari wakati huo lakini mimi nilikuwa mdogo sana. Baba alikuwa na mambo mengi ya kufanya wakati wa vita na nadhani alijua naendelea na JKT. Kwa bahati nzuri pale nyumbani Msasani kulikuwa na simu na baada ya vita askari tulikuwa tukirusiwa kupiga simu nyumbani. Sasa nikaanza utaratibu wa kupiga simu nyumbani mara kwa mara kila ilipofika saa kumi jioni. Baba alikuwa na utaratibu wa kurudi nyumbani saa tisa na akirudi moja kwa moja anakwenda mezani ale chakula. Baada ya muda akabaini kuwa kila saa kumi wadogo zangu wakisikia tu simu wanakimbilia ilipo kwenda kusikiliza. Siku moja akawauliza, mbona mnakimbilia simu kila inapofika saa kumi na saa nyingine hamkimbilii? Ndiyo wakamwambia tunaongea na kaka Mako (Makongoro). Akashangaa, akawaambia mnaongea naye kutoka wapi? Wakamwambia yuko Uganda. Nalisikia alishtuka sana na moja kwa moja akaja kwenye simu. Mara nikasikia sauti ya Mwalimu ikiuliza Uko wapi Makongoro? Nikamwambia niko vitani Uganda? Akaniuliza uliendajeendaje? Nikamuuliza kwani vijana wenzangu kama mimi waliendajeendaje? Basi, nikasikia anapumua na akaanza kuniuliza kuhusu habari za Uganda na mambo mengine. Nilikuwa sijawasiliana na baba yangu kwa muda wa miaka miwili tangu kuanza kwa vita.

RAIA MWEMA: Mmoja wa washindani wako kwenye kinyang’anyiro hiki cha kuwania urais, Edward Lowassa, amewahi kuhadithia namna alivyoshuhudia watu wakifa vitani wakati wa vita hiyo. Je, mliwahi kukutana mkiwa Uganda?

MAKONGORO: Sikumbuki kukutana na Lowassa wakati wa Vita ya Uganda. Lakini kulikuwa na askari wengi na inawezekana nilipokuwa mimi yeye hakuwepo. Siwezi kujua askari wote waliopigana vita ile. Baada ya vita kumalizika, wasanii wengi kama vile Zahir Ally Zorro walikuja Uganda kututumbuiza lakini Lowassa pia sikumuona. Nasikia yeye alisomea sanaa Chuo Kikuu labda alikuja wakati huo lakini pia sikumuona. Zorro na marehemu Kapteni John Komba niliwaona wakati ule. Lakini Lowassa sikumbuki kumuona. Labda alipigana mji mwingine au alikuja na wasanii kutumbuiza baada ya vita, lakini mimi sikumbuki kumuona.

RAIA MWEMA: Washindani wako wanadai kuwa wewe hufai kupewa urais kwa sababu ni mlevi na unapenda kunywa pombe. Unazungumziaje shutuma hizi?

MAKONGORO: Mimi pombe nakunywa lakini hilo la kusema kwamba mimi ni mlevi halipo. Mimi si mlevi. Wapo wapinzani wangu ambao ni walevi kiasi kwamba pombe zimeharibu afya zao na sasa wanaumwa. Wanaumwa kwa sababu ya kunywa pombe. Mimi kama unavyoniona niko fiti na sina tatizo lolote la kiafya. Sasa wale ambao ulevi umewasababishia matatizo hawasemwi na kibao kinageuzwa kwangu. Hiki ni kichekesho kwelikweli.

RAIA MWEMA: Kwa hiyo uko tayari kwenda kupimwa afya ili uthibitishe utimamu wa afya yako kama alivyopendekeza mgombea mmoja kwamba wagombea wote mpimwe afya zenu?
MAKONGORO: Tupimwe afya kwani tunataka kwenda kuchezea Real Madrid au Manchester United? Wachezaji wanaotaka kwenda kucheza mpira ndiyo wanapimwa afya zao lakini sijasikia popote watu wanaotaka urais wanaenda kupima afya. Kwani Watanzania hawawezi kuangalia tu wenyewe na wakajua huyu ana afya njema na yule hana?

RAIA MWEMA: Una wito gani kwa wana CCM wenzako kuelekea kuchagua mgombea urais kupitia chama chenu kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu?

MAKONGORO: Mimi nasema wana CCM wanatakiwa watutendee haki wagombea, chama chao na taifa lao. Kwenye uchaguzi huu, CCM inaweza kuamua kufanya mabadiliko chanya au hasi.
Wakichagua mtu ambaye dunia nzima inajua ni mwizi, wajue kwamba Watanzania watawaona na dunia pia itawaona pia. Wana CCM wasibabaike na kauli za vitisho zinazotolewa na baadhi ya wagombea kwamba wasipopitishwa wao, basi patachimbika. Sasa nauliza, patachimbika kwani kuna madini gani yanayotafutwa? CCM imekuwa Mererani ambako wachimba madini wanachimba kutafuta Tanzanite? Kama wana CCM watafanya makosa safari hii, wajue kwamba hawakuwa na wa kumlilia isipokuwa wao wenyewe.

Baada ya kushambuliwa Dogo Jembe ahoji nani anafaa kuwa rais

Tangu mgombea mwenye umri mdogo zaidi kutangaza nia ya kutaka kuwa rais wa Tanzania, Dogo Jembe amejikuta akipambana na upinzani mkali toka kwa wananchi wengi hasa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wengi wamekuwa wakimtaka arudi shule huku wengine wakimshambulia kuwa anatumiwa na mmoja ya wanasiasa.

Mara baada ya kuzongwa na waandishi wa habari waliomuuliza anachukuliaje maoni ya wananchi kuhusu nia yake ya kuutaka urais amelazimika kuitisha mkutano na waandishi wa habari ambapo ameongea kwa hisia akihoji kama hawamtaki yeye ni nani hasa wanaona anafaa. Tazama video hii.
Dk Naiz Majani aelezea hatua iliyopiga Tanzania katika kutibu watoto wenye tatizo la moyo


Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Julai 3, 2015

Polisi yakamata mashine ya BVR kwa kiongozi wa CHADEMA

UPDATE/TAARIFA MPYA Julai 4, 2015 -- Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu wane akiwemo mwenyekiti wa mtaa wa Nyakato na kamanda wa sungusungu ambaye ni wakala wa UKAWA kwa tuhuma za kuandikisha wapiga kura kinyume na taratibu usiku saa nne na nusu katika mtaa wa Nyakato wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga na Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha tukio hilo limetokea Juni 30, 2015 saa nne na nusu usiku katika mtaa wa Nyakato, kata ya Nyasubi wilayani Kahama.

Kamanda Kamugisha amewataja watu wane waliokamatwa ni Nicholaus Kashanga Azalia Mbwambo (40) mjumbe wa serikali ya mtaa wa Nyakato. Kamanda wa jeshi la jadi Sungusungu na wakala wa UKAWA katika zoezi la kuandikisha wapiga kura.

Wengine ni Amos Elias (25), mkazi wa Mhongolo (BVR Operator), Mayunga Alphonce (54) ambaye ni mwenyekiti wa mtaa Nyakato na mkazi wa mtaa huo na Lugina Misango (40) ambaye ni mratibu elimu kata ya Nyasubi.

Kamanda Kamugisha amesema watu hao wanaohojiwa na jeshi la polisi kuhusiana na tuhuma za kuandikisha wapiga kura kinyume cha sheria,ambapo watu hao wanatuhumiwa kuandikisha wapiga kura katika chumba anachoishi Nicholaus Kashanga Azalia Mbwambo kwa kutumia mashine moja ya BVR usiku.

Akifafanua zaidi kuhusu tukio hilo Kamanda Kamugisha amesema kaika mashine hiyo kumekutwa kadi tano ambazo zilikuwa zimechapishwa.
“Katika maelezo ya awali watuhumiwa wanadai mashine mbili zilipelekwa katika chumba hicho ambacho kiko katika nyumba ya Machanya Joshua kwa ajili ya kuchajiwa…”
“Pia tumemkamata Innocent Byamungu (77) Mrundi ambaye baada ya kuhojiwa amedai kutoa Shilingi 5,000/= kwa Nicholaus Kashanga Azalia Mbwambo ili aandikishwe lakini hakuandikishwa kwa madai aliamuriwa na Nicholaus Kashanga Azalia Mbwambo aondoke kwa kuhofia kukamatwa,”
ameeleza Kamanda Kamugisha. 

--------------- MWISHO WA TAARIFA M PYA ---------------------

Jeshi la polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga limekamata mashine moja ya BVR ikitumika kuandikisha wapiga kura saa tatu usiku nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa wa Nyakato wilayani humo Mayunga Alphonce (CHADEMA), huku wakiwalipa shilingi 5,000/= kila mmoja.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 3 usiku katika mtaa wa Nyakato ambapo mashine hiyo ilikutwa ikiwa inafanya kazi ya kuandikisha wapiga kura.

Mpesya amesema kuwa vyombo vya usalama wilayani humo vilipata taarifa kutoka kwa raia wema ambazo zimewezesha kukamatwa kwa mashine hiyo pamoja na vitambulisho vitano ambavyo tayari vilikuwa vimeshakamilika kuandikishwa.

Ameongeza katika harakati za kukamata mashine hiyo pia wameweza kumkamata mhamiaji haramu mmoja raia wa Burundi ambaye tayari alikuwa ameshaandikishwa na mashine hiyo akiwa ndani ya nyumba ya mwenyekiti huyo.

Mpesya amesema jeshi la Polisi wilayani humo linamshikilia Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Nyasubi, Lugina Misango ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia mashine hizo kwa kosa la kuruhusu mashine hiyo kutumika nyumbani kwa Mwenyekiti wa Mtaa.

Katika hatua nyingine, Mpesya amewataka waandishi wa habari wanaotumiwa kukanusha taarifa hiyo, kutambua kuwa ofisi yake ina mamlaka kamili ya serikali na kwamba wasubiri hatua za kisheria kwani ushahidi wa kukamatwa kwa mashine hiyo upo katika kituo cha polisi.
 • Taarifa hii imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Malunde1

Ngeleja: Kuwania Urais kumenipa fundisho

Ngeleja akibadilisha mawazo na wabunge wenzake, Ezekiel Maige (Msalala) na Dk. Dalaly Peter Kafumu (Igunga), wakati aliporejesha fomu kwenye ofisi za Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma.

MBUNGE wa Sengerema, William Ngeleja, amesema amepata fundisho kubwa katika harakati zake za kuwaomba udhamini ili ateuliwe kuwania urais na kwamba, limemuongezea shauku kubwa ya uongozi.

Ngeleja, ambaye amepata kuwa Waziri wa Nishati na Madini katika serikali ya Awamu ya Nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, amesema yuko tayari kuwatumikia watanzania iwapo CCM kitampa ridhaa ya kupeperusha bendera.

Akizungumza wakati akirejesha fomu za kuomba kuwania urais kwenye uchaguzi mkuu ujao, Ngeleja alisema anatambua nafasi anayoimba ni nyeti na kwamba, amejipima na anatosha kubeba mikoba ya JK.

Alisema kazi ya kutafuta wadhamini katika mikoa mbalimbali nchini, Ngeleja alisema wakati wa zoezi hilo amejifunza mambo mengi na ambayo yamemfanya kuendelea kuifahamu nchi kijiografia na changamoto zake.
“Nipo tayari na shauku yangu ya kuliongoza taifa imezidi kupamba moto wakati wa zoezi la kuzunguka kuomba udhamini kwenye mikoa yote nchini.
“Nimeona na kujifunza mengi na nimepata fursa ya ya kuona maendeleo makubwa yaliyofanywa na serikali yetu katika nyanja zote na changamoto ambazo bado zinatukabili kama taifa,”
alisema Ngeleja.

Alisema watanzania wana shauku kubwa ya kupambana na umasikini na kwamba, nimejionea mwenyewe namna ambavyo watu wana shauku kubwa ya kupambana na umasikini.
"Unajua sisi wabunge mara nyingi tumekuwa na majukumu makubwa ya majimboni na mara nyingi tathmini tunayoifanya ya maendeleo kwa nchi yetu inatokana na kile kinachofanyika majimboni kwetu, lakini zoezi hili la udhamini limenipa fursa ya kuona kinachoendelea nchi nzima.
“Kila tulikopita tuliwakuta wananchi wanashiriki kwenye miradi ya ujenzi wa maabara za shule, madarasa ya shule, zahanati, watoto wanakwenda ama kutoka shuleni,” 
alisema Ngeleja.

Aliongeza kuwa jambo lingine ambalo amejifunza wakati wa kazi ya kusaka wadhamini ni kuwa Tanzania bado ni ya wakulima na wafanyakazi, ingawa makundi ya wavuvi, wafugaji, wajasiriamali, wafanyabiashara, wana michezo na wasanii nayo ni makundi makubwa katika jamii.

Ngeleja aliwaahidi wanachama wenzake wa CCM kuwa ili nchi ifanikiwe kupunguza umasikini na kufikia hadhi ya uchumi wa kati ifikapo au kabla ya mwaka 2025, ni lazima uwekezaji mkubwa ufanywe kwenye sekta za kilimo, uvuvi, ufugaji, viwanda, michezo na tasnia ya sanaa, ambazo zinaongoza kutoa ajira kwa zaidi ya asilimia 75 ya watanzania.

Kuhusu kilimo, Ngeleja alisisitiza kuwa ni muhimu kurejeshwa kwa hadhi ya kilimo kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo, uchumi wa nchi ulibebwa na sekta hiyo hususan mazao ya biashara kama pamba, mkonge, korosho, karafuu, kahawa na michikichi.

Mgombea huyo kijana ambaye anatajwa kuwa ni miongoni mwa wachapakazi mahiri, ameendelea kujinadi kupitia kauli mbiu yake ya Maono Sahihi, Mikakati Thabiti, Matokeo Halisi (MMM).
“Kauli mbiu hii inabeba vipaumbele vinne ambavyo ni ujenzi wa uchumi imara, uimarishaji wa utawala bora, huduma za jamii na miundo mbinu,” 
alisema.

Aidha, amejinadi kuwa na weledi wa hali ya juu kuhusu sekta binafsi ambayo ndiyo injini ya maendeleo ya uchumi wa taifa lolote duniani.

Kuhusu uimarishaji wa CCM, Ngeleja ameendelea kuwaahidi wana CCM wenzake kwamba akifanikiwa kuwa akifanikiwa kupeperusha bendera na kushinda, ataendeleza maboresho yanayofanywa sasa na chama chake ili kulingana na kile cha African National Congress (ANC) cha Afrika Kusini, ambacho kina miradi ndani na nje ya nchi.
MBUNGE wa Sengerema mkoani Mwanza, William Ngeleja, akirejesha fomu za kuomba kuteuliwa kuwania urais kupitia CCM kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rajab Luhwavi, kwenye Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho mjini Dodoma, jana.


Rais Kikwete ashuhudia kusimikwa Kiongozi Mpya wa Waluguru

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia kusimikwa kwa Kiongozi mpya wa kabila la Waluguru Chifu Kingalu wa 15 katika kijijini Kinole mkoani Morogoro Alhamisi Julai 3, 2015 kufuatia kifo cha Chifu Kingalu wa 14 aliyefariki jana Jumatano jijini Dar es salaam na kuzikwa leo kijijini hapo.

Kiongozi mpya wa kabila la Waluguru Chifu Kingalu wa 15 akitolewa nje baada ya kusimikwa rasmi kuwa kiongozi wa kabla hilo kijijini Kinole mkoani Morogoro Alhamisi Julai 3, 2015 kufuatia kifo cha Chifu Kingalu wa 14 aliyefariki jana Jumatano jijini Dar es salaam na kuzikwa leo kijijini hapo.

Kiongozi mpya wa kabila la Waluguru Chifu Kingalu wa 15 akichomeka fimbo yake ya Uchifu kabla ya kuketi meza Kuu na Rais Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kusimikwa rasmi kuwa kiongozi wa kabla hilo kijijini Kinole mkoani Morogoro Alhamisi Julai 3, 2015 kufuatia kifo cha Chifu Kingalu wa 14 aliyefariki jana Jumatano jijini Dar es salaam na kuzikwa leo kijijini hapo.
Picha kutoka Ikulu

Tarehe mpya za BVR kwa wakazi wa Dar na Pwani

Tume ya Uchaguzi imearifu kuwa tarehe mpya za kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Mpiga kura kwa njia ya Biometric (BVR) litafanyika kuanzia tarehe 7 hadi 20 Julai 2015 kwa mkoa wa Pwani na kuanzia tarehe 16 hadi 25 Julai 2015 kwa wakazi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Qatar Airways flight schedules Doha - Kilimanjaro - Zanzibar
Qatar Airways launched its second new destination of the year, touching down in the Spice Island of Zanzibar yesterday. Zanzibar is the airline’s third route in Tanzania, following Dar-es-Salaam and Kilimanjaro. Qatar Airways Chief Commercial Officer Marwan Koleilat said, “This latest route marks yet another significant milestone for the airline that has spread its international wings to its 20th gateway in Africa and 148th destination globally.”
Qatar Airways will initially operate five weekly flights to Zanzibar via Kilimanjaro, and commencing 1st October 2015, the airline will offer an additional two weekly flights making it a daily operation. Out of the daily flights from October, passengers will be able to fly non-stop to Zanzibar three-times-a-week and on a linked flight via Kilimanjaro four-times-a-week.

“By providing a reliable, convenient and award-winning travel experience from Zanzibar, Qatar Airways will provide passengers with the opportunity to travel to Doha and connect onwards to more than 140 worldwide destinations through our new state-of-the-art Hamad International Airport.”
Qatar Airways is operating an Airbus A320 in a two-class configuration on the Zanzibar-Doha route, with 12 seats in Business Class and up to 132 seats in Economy. Each seat on selected flights offers an interactive audio and video entertainment system featuring up to 1,000 options of movies, TV programmes and music channels.

The current Doha-Kilimanjaro-Zanzibar schedule:

Mondays, Wednesdays, Fridays, Saturdays and Sundays
Depart Doha QR1355 at 08:50, arrive Kilimanjaro at 14:20
Depart Kilimanjaro QR1355 at 15:20, arrive Zanzibar at 16:20
Depart Zanzibar QR1355 at 17:20, arrive Doha at 22:35

Daily flight schedules from October:

Mondays, Wednesdays, Fridays and Saturdays
Depart Doha QR1355 at 08:50, arrive Kilimanjaro at 14:20
Depart Kilimanjaro QR1355 at 15:20, arrive Zanzibar at 16:20
Depart Zanzibar QR1355 at 17:20, arrive Doha at 22:35

Tuesdays, Thursdays and Sundays
Depart Doha QR1357 at 08:50, arrive Zanzibar at 14:40
Depart Zanzibar QR1357 at 15:40, arrive Kilimanjaro at 16:40
Depart Kilimanjaro QR1357 at 17:40, arrive Doha at 22:35


 • Photos: ZaniNews blog

Tahadhari ya Wizara kuhusu wanaojitambulisha kama viongozi wa kielimu

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

Tanzanian Government National Emblem Logo ngao uhuru na umoja

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MATAPELI WANAOOMBA RUSHWA KWA KUJITAMBULISHA KAMA VIONGOZI WA ELIMU

Kumejitokeza kundi la watu ambao ni matapeli wanaoomba rushwa kwa kujitambulisha kama viongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kutumia namba za simu zilizoandikishwa kwa kutumia majina ya viongozi hao. Namba hizo hutumika kwa muda na baada ya kufanikisha lengo lao, watu hao huzifunga na hivyo kutokupatikana tena hewani.

Majina ya viongozi yanayotumika katika utapeli huo ni ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katibu Mkuu, Kamishna wa Elimu na ya baadhi ya Wakurugenzi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Namba hizo za simu hutumika na matapeli hao kwa kuwapigia watu wanaohitaji huduma katika ofisi za elimu na kuwaomba wawatumie fedha kupitia namba hizo ili kufanikisha upatikanaji wa huduma wanazozihitaji kutoka katika ofisi hizo. Huduma zinazotajwa ni pamoja na kufanikisha usajili wa shule na vyuo.

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inawatahadharisha wananchi kujiepusha na kundi hili la matapeli na ifahamike kuwa huduma zote zinazotolewa katika ofisi za elimu zikiwemo za usajili wa shule hazitolewi kwa rushwa au malipo ya aina yoyote.

Maelezo kamili kuhusu usajili wa shule yanapatikana katika ofisi za Ukaguzi wa Shule za Wilaya na Kanda na ofisi za Makao Makuu ya Wizara, au chumba namba 21 na 36 hapa wizarani. Tafadhali wasiliana na Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu au Kamishna wa Elimu endapo utapigiwa simu na mtu usiyemfahamu atakayejitambulisha kwako na kudai fedha ili afanikishe usajili wa shule au kupata huduma zingine wizarani. Usikubali kudanganywa na kutoa fedha kwa huduma inayopatikana bure.
Imetolewa na:

Katibu Mkuu,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
02 Julai, 2015

Magereza yajivunia vifaa vyake bora katika maonesho ya Sabasaba


Meza ya Chakula iliyotengenezwa kwa Ustadi mahiri katika Kiwanda cha Userelemala kilichopo Gereza Kuu Ukonga, Dar es Salaam. Meza hiyo ina viti vinane imetengenezwa kwa kutumia mbao ya Mninga inauzwa kwa Tsh. 2500,000/=


"Sofa set" yenye uwezo wa kukaliwa na watu saba, sofa hii imetengenezwa pia na Mafundi waliobobea kutoka Kiwanda cha Uselemala kilichopo Gereza Kuu Ukonga, Dar es Salaam kwa kutumia mbao aina ya mninga ambapo inauzwa kwa Tsh. 4,500,000/=


Meza Maalum ya Ofisi iliyotengenezwa kwa kutumia mbao ya mninga inapatikana katika Banda la Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam. Meza hiyo kwa pembeni ina meza ndogo kwa matumizi ya kiofisi kama ambavyo inaonekana. Aliyeketi ni Afisa Habari wa Jeshi la Magereza nchini, Mrakibu Msaidizi wa Magereza Lucas Mboje akiendelea na majukumu kama anavyoonekana katika picha.


Seti mbalimbali za kapeti za mlangoni ambazo zimetengenezwa kwa kutumia malighafi za mkonge na nazi kama zinavyoonekana katika picha. Kapeti hizo zenye ubora zinauzwa Tsh. 7000/= hadi 15,000/=


Vikoi kutoka Kiwanda cha Ushonaji cha Gereza Kuu Butimba, Mwanzaj vikiwa katika Banda la Jeshi la Magereza katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa, kikoi kimoja kinauzwa kwa Tsh. 10,000/= tu


Bidhaa za mianzi zinazotengenezwa kutoka Gereza Njombe, Mkoani Njombe. Stafu Sajin wa Magereza, Shukrani wa Gereza Njombe akielezea namna bidhaa hizo zinavyotengenezwa pia namna Wafungwa wanavyonufaika kupitia Stadi hiyo ya utengenezaji wa bidhaa za mianzi Mkoani Njombe.


Vinyago vya aina mbalimbali kama vinavyoonekana katika picha ambapo vimechongwa kwa kutumia Mti wa Mpingo. Vinyago hivyo imetengenezwa katika Kiwanda cha Gereza Kuu Lilungu, Mkoani Mtwara. Wafungwa wa Gereza Kuu Lilungu wananufaika sana na Stadi hiyo ya uchongaji Vinyago hivyo kujipatia ujuzi na ajira mara wamalizapo vifungo vyao magerezani. Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.

Bungeni: Yaliyotokea baada ya Mnyika "kumtibua" Spika akaahirisha Kikao


BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeahirishwa ghafla leo baada ya wabunge wa upinzani kusimama na kukataa kutoka nje ili kuzuia miswada mitatu muhimu ya gesi, petroli na uziduaji kusomwa kwa Hati ya Dharura.

Hali hiyo imetokea baada ya Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika kuomba mwongozo juu ya uvunjaji wa kanuni za bunge kwa kuwekwa miswada mitatu sambamba.

Spika wa Bunge, Anne Makinda aliwataka wabunge hao kutoka nje kama hawataki kuendelea na kikao ila baada ya kugoma kufanya hivyo na kusimama kisha kuanza kupiga kelele, Spika aliamua kuahirisha bunge.

Miswada iliyowasilishwa ni:
 1. Muswada juu ya Petroli, 2015 (The Petroleum Act, 2015)
 2. Muswada juu ya Usimamizi wa Mafuta na Gesi, 2015 (The Oil and Gas Revenues Management Act, 2015)
 3. Muswada juu ya tasnia ya Uziduaji Tanzania (The Tanzania Extractive Industries Act, 2015): The Tanzania Extractive Industries Act, 2015.Watuhumiwa wa wizi wa fedha za EPA waachiwa huru

Rajabu Maranda
Rajabu Maranda

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaachia huru Kada wa CCM, Rajabu Maranda na wenzake waliokuwa wanakabiliwa na kesi wizi wa Sh milioni 207 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Jopo la mahakimu watatu likiongozwa na Hakimu John Utamwa, Ignas Kitusi na Eva Nkya liliwaachia washitakiwa hao baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa hao.

Mbali na Maranda washitakiwa wengine walioachiwa huru ni Farijala Hussein na waliokuwa wafanyakazi wa BoT, Ester Komu, Bosco Kimera na Imani Mwakosya.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Utamwa alisema washitakiwa waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka manne kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo BoT na wiziwa Sh milioni 207.2 wako huru kutokana na upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka hayo bila kuacha shaka kama inavyotakiwa kisheria.

Alisema upande wa Jamhuri umeshindwa kuithibitishia mahakama jinsi Maranda na Farijala walighushi makubaliano ya kukusanya deni kati ya Kampuni ya General Marketing ya India kwenda Kampuni ya Rashas (T) ya Tanzania.

Katika hukumu hiyo iliyosomwa bila Mwakosya kuwepo mahakamani, Hakimu Utamwa alisema upande wa Jamhuri wameshindwa kumleta mpelelezi wa kesi hiyo ili aweze kuithibitishia Mahakama saini ambazo zinadaiwa kuwepo katika makubaliano hayo hivyo udhaifu huo hauwezi kuwatia washitakiwa hatiani.

Aliongeza kuwa, upande wa Jamhuri ulishindwa kuthibitisha shitaka la kughushi, kwa hiyo shitaka la kuwasilisha nyaraka za uongo litakuwa limekufa,kwa sababu wameshindwa kuonesha kweli nyaraka ni za kughushi.

Aidha alisemwa wameshindwa kuonesha ni jinsi gani fedha hizo zilihamishwa kama wanavyodai kuwa mchakato huo ulifanikiwa kwa sababu Maranda na Farijala walitumia nyaraka za kughushi.
“Hakuna shahidi aliyeweza kutoa ushahidi ukaenda sawa na hati ya mashitaka iliyofunguliwa mahakamani hapo dhidi ya washitakiwa,” 
alisema Hakimu Utamwa.

Nyaraka zinazodaiwa kughushiwa ni hati za makubaliano ya kuhamishiwa deni kutoka Kampuni ya General Marketing ya India kwenda Kampuni ya Rashas (T) ya nchini Tanzania, ambazo walizutumia na kuiba fedha hizo.

Baada ya Hukumu hiyo, Farijala alirudishwa rumande kwa sababu anatumikia kifungo cha miaka miwili jela alichohukumiwa katika kesi nyingine na Maranda aliachiwa lakini bado ataendelea kwenda mahakamani kwa kuwa anakabiliwa na kesi nyingine.

Ndugu na marafiki waliokuwepo katika eneo hilo la mahakama walishukuru mahakama kutoa uamuzi wa haki na kusema kweli Mungu ametenda miujiza.

Kenya wamezindua, Ghana wamezindua, Uganda wamezindua, Tanzania...


Re-advertised: Job opportunity at Sikika for a District CoordinatorJoin us in advocating for quality health services for all Tanzanians 

Introduction

Sikika is a non-governmental organization that advocates for quality health services for all Tanzanians. For more information on our work please visit us at www.sikika.or.tz.

Title: District Coordinator

Work Station
: Iramba District

Reports to
: Head of Field Office

Objective: To contribute to the realization of the organizations objectives by coordinating and facilitating implementation of Sikika’s AWP activities in the district”.

Responsibilities:

1. Coordinating Social Accountability Monitoring (SAM) activities at District, ward and facility level

 • Working closely with office of the District Commissioner and District Council to ensure smooth implementation of SAM activities in the district.
 • Coordinating and supervising activities of SAM team in the district especially those related to Health and HIV/AIDS at district and facility level.
 • Organize / attend periodic meetings at community level to mobilize citizens and raise their awareness on accountability issues
 • Attend all Full Council meetings to track commitments and decisions made for monitoring of SAM district action plan
 • Promptly share with respective departments issues that come up during the implementation / monitoring of activities in the district
 • Conduct official and informal meetings with Ward Executive Officers (WEOs), Community Development Officers (CDOs), Village Executive Officers (VEOs) and Facility management committees and Multi-sectoral HIV & AIDS committees on accountability in the health sector
 • Encourage dialogue on health related issues between citizens and their leaders at village and ward level
 • Encourage participation of religious leaders, political leaders, opinion leaders, disadvantaged groups such as people with disability, people living with HIV/AIDS in all activities aimed at promoting accountability at local level
 • Drafting and sharing progress made to head of Field Office on weekly, monthly and quarterly basis
 • Prepares Singida rural reports with a clear alignment to our work plans and strategic plan.


2. Implement Sikika departments’ specific activities in your district. These will include:


 • Making follow up on reported cases of misconducts / unethical behaviors of health workers at facility level
 • Promoting community monitoring of health and HIV&AIDS services with focus on availability of medicines and supplies (including CD4 count machine), budget information and the importance of using existing complaint mechanisms
 • Distribute Sikika publications and track how such publications support citizens in understanding critical issues and how such information enables them to take actions
 • Contribute to Sikika’s quarterly newsletter by sending stories, best experiences and lessons from the field


3. Joint Advocacy and relationship with other actors
 • Foster a good working relationship with Office of the District Commissioner (DC) and LGA (DED, DMO, DACC, CHAC) and head of health facilities by having periodic consultations and feedback meetings
 • Coordinate with other CSOs in the district in organizing experience sharing sessions on health at district level with the purpose of drawing lessons for advocacy work
 • Under guidance and in consultation with Head of Field Office in Dodoma, represent Sikika in all stakeholders meetings at district level

Required Qualifications

Education

A Bachelor Degree or higher degree in any Social science discipline.

Work Experience

A minimum of 2 years working experience in rural areas (Kiteto & Manyara areas preferred).

Key Skills and Abilities

The Jobholder must be fluent in both oral and written Swahili & English, possess reasonable skills in coordination, research, experience in analyzing written works

Remuneration

An attractive remuneration package will be offered to successful candidates.

Send your application papers by e-mail to: [email protected]. Attn: The Human Resources and Administration Manager, Sikika. Ladies are highly encouraged to apply

Application Deadline: June 12, 2015

[audio song]: Tuwaonee huruma - Lake Zone All Stars

Ombi la msaada wa hali na mali kwa kijana Abel Machanga atibiwe

Abel Machanga

Kijana Abel Machanga mwenye umri wa miaka 24 amelazwa Hospital ya Taifa Muhimbili Wodi ya Sewahaji,chumba namba 19,Kitanda namba 28 kwa tatizo la uvimbe kwenye ubongo ambalo limesababisha macho yake kutoka nje.

Familia inaomba msaada wa wasamaria wema ili kugharamia matibabu ya Abel kutokana kuwa gharama za matibabu ni kubwa kuliko uwezo wa familia.

Kwa yeyote atakayetakayeguswa na taarifa hii, anakaribishwa kumtembelea Abel Hospitalini ili kukutana naye na kusikia kilio chake Kwa mlio mbali, tunaomba misaada yenu kupitia kwa kaka wa Abel Bw.Christopher Machanga kwa namba

Tigo 0655 54 56 67
Airtel 0784 54 56 67
Voda 0755 54 56 67

SHIME WATANZANIA TUJITOE KWA MOYO KUOKOA MAISHA YA MWENZETU NA KUPUNGUZIA MATESO MAKALI ANAYOKABILIANA NAYO KWA SASA. TUNATANGULIZA SHUKRANI.