Nje ya Bunge: Tundu Lissu alipozungumzia Waliofukuzwa Bungeni


Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Julai 5, 2015

Job opportunity for a Video Journalist/Broadcaster

Contractor Position available for Video Journalist/Broadcaster at an International Broadcasting Organization

Standard: The Video Journalist/Broadcaster shall have at least three (3) years of current experience.
 1. The Video Journalist/Broadcaster shall perform a combination of services that will include researching, interviewing, writing and voicing original news stories and reports, as well as services related to acquiring news video content, including, researching, photographing, lighting, editing, and producing. 

 2. The Video Journalist/Broadcaster shall have the ability to adapt material for radio, television and/or internet in Kiswahili language about events in the target region (East and Central Africa), the U.S. and other countries. 

 3. The individual shall produce and edit reports using compatible digital technology and shall be able to record and process interviews by phone, live face-to-face or in the field. 

 4. He or she shall provide video photography and editing services which go beyond standard camera operation. The Video Journalist/Broadcaster shall be well versed in video photographic styles and techniques while being able to tell a story with pictures. 

 5. The Video Journalist/Broadcaster shall, when required, serve as a producer for television news and feature stories, and, when required, serve as the video editor with a script timed to video shots, natural sound emerges and actualities, and complete with suggested visual, audio and graphic efforts and/or perform desktop video editing as practical. 

 6. The individual shall have extensive knowledge of the target region, its people, culture, institutions and political situation, and the ability to adapt English material to the target language. 

 7. Kiswahili language is a MUST. 
Send resumes to: [email protected]

Taarifa ya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu mpya wa TCRA

Ally Yahaya Simba
Ally Yahaya Simba

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria Na. 12 ya mwaka 2003 ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania Kifungu cha 13 (1) amemteua Dkt. Ally Yahaya Simba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia tarehe 6 Julai 2015.

Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Ally Yahaya Simba alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Imetolewa na:

Selina Lyimo
KAIMU KATIBU MKUU
Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Aliyeko nyuma ya kampeni za Dogo Jembe na #IkuluSioLeo nimelazimika kuandika makala hii baada ya kufanya maongezi na jamaa yangu mmoja huko Tanzania ambaye katika nafasi yake kikazi, anafahamu mambo mengi yanayojiri 'nyuma ya pazia.'

Alichoniambia kimenishtua sana. Ni kuhusu kampeni zinazoendelea mtandaoni zinazomhusisha mtoto mdogo anayejiita DOGO JEMBE. Pia kampeni hizo zinatumia hastag #IkuluSio.

Huyo jamaa yangu, pengine kutokana na majukumu yake kikazi au ufuatiliaji tu, amenionyesha ushahidi unaothibitisha kuwa kampeni hiyo inaendeshwa na mtangaza nia mmoja wa CCM. Kwahiyo tofauti na picha inayojengwa na DOGO JEMBE kuwa yupo upande wa maslahi ya Watanzania, kimsingi mtoto huyo anatumiwa tu na mwanasiasa huyo anayetaka urais.

Kwa mujibu wa jamaa yangu huyo anayefanya kazi katika taasisi moja 'nyeti' huko nyumbani, kosa la msingi lililofanywa na waandaaji wa kampeni hiyo ni kwenye kitu kinachofahamika kama IP,Address ambayo kwa lugha nyepesi ni anwani ya mlolongo wa namba zinazotenganishwa na nukta ambao unaitambua kompyuta katika mtandao. 'Mtaalam' huyo amefanikiwa kubaini kuwa posts za kampeni hiyo zinatoka kwa IP address ya mdogo wa mwania nia fulani. Amenitumia screenshots zenye uthibitisho kuhusu suala hilo.

Amenijulisha pia kuwa taasisi anayoitumikia inafahamu bayana kuhusu 'uhuni' huo, na hii unaisoma hapa kwa mara ya kwanza, usishangae ukikutana na breaking news hii katika vyombo vya habari katika siku chache zijazo. Inaelekea kuna 'wakubwa' hawajapendezwa na mbinu hiyo ya kuwahadaa Watanzania kwa kisingizio cha kumsaka Rais bora.

Kilichomkera, kinachonikera, na ambacho pengine nawe Mtanzania kitakukera ni kitendo cha mwania huyo kuwafanya Watanzania wapumbavu. Kwanini nasema hivyo? Kwanza ni 'kosa' la kumtumia mtoto mdogo kuvuta hisia za watu, kuwaaminisha kuwa lengo ni kupigania maslahi ya taifa kwa kuamsha tafakuri ya nani hasa anatufaa kuwa Rais wetu ajaye, ilhali ukweli ni kwamba kampeni hiyo ina lengo la kumpigia debe mwania nia huyo.

Kwa mujibu wa jamaa yangu huyo ambaye kwa ninavyomfahamu hana kambi yoyote hasa kwa vile majukumu yake kikazi yanamzuwia kujihusisha na siasa, kuna data nyingine ambazo zinaihusisha moja kwa moja kampeni hiyo na mwania nia huyo.

Japo nipo katika wakati mgumu kutokana na kuzorota kwa afya ya Mzee Chahali lakini afya ya Tanzania yetu ni muhimu pia kama afya ya mzazi wangu, na nimeshindwa kukaa kimya baada ya kuletewa ushahidi kuhusu 'uhuni' huu.

Amenieleza kuwa kauli ya Dogo Jembe kuwa 'Ikulu sio ya baba yako' ilimlenga Makongoro Nyerere kwa vile yeye ni mtoto wa Nyerere, na kauli kuwa 'Ikulu sio hospitali' illimlenga Lowassa kwa vile mwania nia huyo amedaiwa kuwa afya yake sio nzuri japo haijathibitishwa.

Lakini pengine hata bila kupata 'ufunuo' huu, ilipaswa tujiulize NANI ANAYEFADHILI KAMPENI HII YA KISASA KABISA?

Kwa mtizamo wa jamaa yangu huyo, kosa jingine la kampeni hiyo ni kwamba imejitengenezea 'ufupi wa maisha' kwa maana kwamba ipo siku Dogo Jembe atalazimika kuwashawishi tena Watanzania kuwa 'mtaka nia flani ana sifa za dogo jembe, na ndio anafaa kuwa Rais,' na hapo all hell will break loose kwa sababu kila mwenye akili timamu atabaini nani alikuwa behind kampeni hiyo.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete afungua kikao cha kuipitia Ilani ya Uchaguzi 2015


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionyesha kitabu ya Rasimu ya Ilani ya CCM kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, wakati wa Kikao cha Kamati Kuu cha kuijadili na kuipitisha Ilani hiyo kinachofanyika, leo Julai 4, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wakipitia Rasimu ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, wakati wa Kikao cha Kamati Kuu cha kuijadili na kuipitisha Ilani hiyo kinachofanyika, leo Julai 4, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma.


Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndg. Abdulrahman Kinana akizungumza wakati akimuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua Kikao cha Kamati Kuu cha kuijadili na kuipitisha Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kinachofanyika, leo Julai 4, 2015 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa CCM Makao Makuu, Mjini Dodoma. Wengine pichani ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Ndg. Phillip Mangula.


Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa kwenye Kikao hicho.

Ofisa Mtendaji Mkuu akiri "Kampuni ya TTCL ni mufilisi" yapata hasara ya bilioni 300/=


KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL), ambalo ni shirika kongwe la umma, sasa imefilisika kibiashara kutokana na ubia tata kati ya serikali na wawekezaji wenye mgongano wa kimaslahi katika sekta ya mawasiliano.  

Aidha, ubovu wa menejimenti, ubadhirifu wa fedha za umma, wafanyakazi waliokatishwa tamaa, ukosefu wa mtaji, madeni sugu, na mitambo iliyopitwa na wakati ndivyo vinavyochangia kuliua.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura, kampuni hii inachungulia kaburi kwa sababu imekuwa ikipata hasara mwaka hata mwaka kiasi cha kufikia hadhi ya “kutokopesheka.”

Dk. Kazaura ameiambia MwanahalisiOnline kwamba kampuni ya TTCL imepata “hasara kubwa ya kiasi cha Sh. 335 bilioni mpaka kufikia mwaka 2013″ jambo ambalo limeifanya “kushindwa kukopesheka huku ikibaki na mtaji hasi wa Sh. 88 bilioni.”

Kwa mujibu wa Dk. Kazaura, “kwa sasa Kampuni ya TTCL ni mufilisi,” hatua ambayo inatokana na “mbia mwenye hisa za asilimia 35, kutofanya uwekezaji mkubwa tangu aingie katika ubia na serikali mwaka 2001.”

Dk. Kazaura aliyasema hayo mjini Dodoma mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi.

Nae Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, amesema mchakato wa kuondoka kwa Kampuni ya Airtel kutoka TTCL “uko katika hatua za mwisho.” Ameeleza kuwa tayari “makubaliano ya bei” ya hisa zinazodaiwa kumilikiwa na Airtel katika TTCL yamefikiwa “katika kikao cha majadiliano kilichofanyika tarehe 20 Novemba 2014.“

Akielezea majadiliano yalivyokuwa, Profesa. Mbarawa amesema Kampuni ya Airtel “iliafiki kuachia hisa inazomiliki ndani ya TTCL” na kisha Serikali kukubali “kuzinunua hisa hizo kwa Sh. bilioni 14.9″ za Tanzania.

Tayari “Baraza la Mawaziri liliidhinisha Serikali kununua hisa hizo” kwa mashrati kwamba malipo hayo yafanywe “baada ya taratibu za kisheria kukamilika” ili hatimaye “Serikali iweze kuimiliki TTCL kwa asilimia 100,” aliongeza Profesa Mbarawa.

Profesa Mbarawa aliyatamka hayo wakati akiwasilisha hotuba ya makadirio ya matumizi ya bajeti ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha wa 2015/16, bungeni Dodoma hivi karibuni.

Kufuatia kuibuka kwa taarifa za malipo haya, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kupitia kwa msemaji wake wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, (CUF) Mohamed Habib Mnyaa, imehoji umakini wa serikali na kuitaka itekeleze mambo kadhaa.
 • Kwanza, serikali imetakiwa kufafanua matakwa ya mkataba wa awali kati ya Serikali na Kampuni ya MSI na hatua za utekelezaji wa makubaliano ya mkataba huo mpaka sasa.
 • Kueleza iwapo mkataba huo ulikuwa unairuhusu kampuni ya MSI kuuza hisa zake kwa makampuni mengine yaliyofuata kama vile Celtel, Zain na sasa Airtel.
 • Kutoa ufafanuzi kuhusu uhalali wa maamuzi yake ya kuilipa kampuni ya Airtel Sh. 14 bilioni. 

Wadau wapinga malipo ya bilioni 14 kwa Airtel

Wakati mvutano huo ukiendelea kushika kasi wadau mbalimbali wamepinga hatua ya serikali kulipa mabilioni ya shilingi hayo kwa kampuni ya Airtel.

Kwa mfano, kati ya tarehe 16-18 Juni mwaka huu, wadau mbalimbali walikutana mjini Dodoma na Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na mgogoro huu wa TTCL.

Pia, wadau kadhaa waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa majina walisema ni makosa kwa serikali kuilipa Airtel wakati haijawahi kuwekeza hata senti moja katika TTCL.

Kwa mfano, mdau mmoja ambaye ni mhandisi wa muda mrefu ndani ya TTCL, aliyejieleza kwa kirefu, lakini kwa masharti ya kutotajwa, akisema:
“Ndani ya TTCL kuna tabaka la ngazi za mishahara ya watawala (TTCL1 hadi TTCL3), kwa upande mmoja, na tabaka la ngazi za mishahara ya makabwela (TTCL4 hadi TTCL10), kwa upande mwingine.
“Wafanyakazi wengi tulirundikwa katika tabaka la makabwela na tukapewa cheo cha ‘Team member’ lakini bila kuzingatia elimu, weledi, wala uzoefu wetu.
“Katika zoezi la mabadiliko hayo, Menejimenti iliongeza mishahara na kuboresha maslahi ya wafanyakazi wote walio katika tabaka la mishahara ya watawala lakini ikatutelekeza sisi wafanyakazi tulio katika tabaka la mishahara ya makabwela.
“Hata hivyo, sisi wafanyakazi wa ngazi za kawaida ambao hatukuboreshewa malipo ndio wazalishaji wakuu ndani ya TTCL.
“Kwa hiyo, sasa tunashangaa kuona kwamba sisi watu ambao tulisahaulika siku nyingi hatukumbukwi lakini wakati huo kampui ya Airtel ambayo haijawahi kuwekeza hata shilingi inatengewa mabilioni.
“Hivyo basi, kama serikali wanazo fedha za kichezea kiasi hicho waanza na maboresho ya maslahi ya wafanyakazi kabla ya jambo jingine lolote.”

Naye Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni chini ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia, Habib Mnyaa alipinga malipo hayo.

Amesema kampuni ya Airtel hawapaswi kulipwa chochote kwa kuwa, mwekezaji huyu pamoja na watangulizi wake waliahidi kujenga 
“njia 800,100 za simu lakini wakashindwa, na badala yake hata njia 270,000 walizozikuta zimepungua kufikia njia 158,000 tu.”
“Kwa vile Airtel ilianzishwa kwa fedha, leseni na raslimali za TTCL, na mpaka sasa inatumia miundombinu ya TTCL kama vile jenereta, majengo, na viwanja, basi haipaswi kulipwa hata senti,” alisisitiza Mnyaa ambaye ni mbunge wa jimbo la Mkanyageni, Kusini Pemba.
“Tukumbuke kwamba mwaka 1998 Kampuni ya Simu ilikuwa na mawasiliano ya simu katika makao makuu ya takribani wilaya zote nchini. Hivyo, tulitarajia kwamba kwa mwaka 2015 kampuni hii ingekuwa imefikisha mawasiliano hayo katika kila Kata ya Tanzania, lakini wapi. Huu ni udhalilishaji kwa Watanzania.”amesema.
“Tofauti na Taarifa ya Wizara inavyopendekeza, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Hazina kusitisha makubaliano ya utoaji wa fedha hizo. Badala yake, turudi kwenye mkataba wa mwekezaji wa asili, MSI, ambaye amehamisha hisa zake kwa Bharti Airtel. Ufanyike uchunguzi kubainisha makubaliano katika mkataba na kuona kwa kiwango gani mwekezaji alitekeleza masharti ya mkataba.”

Mnyaa anamalizia kwa kusema tunapaswa 
“kuchunguza (MSI) alitakiwa kufanya nini, amefanya nini mpaka sasa, na kwa hisa 35% alizopaswa kulipia alitoa fedha kiasi gani. Kama matakwa ya mkataba yametekelezwa ndio mambo mengine yaendelee. Vinginevyo Airtel alipwe dola moja tu na kufunga virago haraka.”

Ubovu wa Menejimenti ya TTCL
Kwa upande mwingine, tayari Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Profesa Mussa Asad, amemfikishia Rais Kikwete taarifa mbaya kuhusu TTCL.

Taarifa hizo zimemfikia Rais kupitia “Ripoti ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.”

Profesa Asad na ujumbe wake walikutana na Rais Kikwete 26 Machi 2015 Ikulu na kukabidhi ripoti hiyo.

Ripoti inabainisha mambo kadhaa yanayoashiria ulegevu wa Menejimenti ya TTCL kama yalivyogunduliwa na CAG.

Kwanza, ilibainika Menejimenti ya TTCL imeshindwa kuimarisha mifumo ya udhibiti wa ndani ili kukabiliana na vihatarishi vya usalama wa kampuni.

Pili, Menejimenti imeshindwa kusimamia ipasavyo mfumo wa mishahara jambo ambalo lilitoa mwanya kwa mtumishi mmoja kutumia mfumo huo kuiibia kampuni kwa kujizidishia mshahara wake kwa kiasi cha Sh. 72 milioni.

Tatu, Menejimenti imefanya manunuzi ya bajaji 30 zenye thamani ya Sh. 156 milioni bila ya kuzingatia vyema Sheria ya Ununuzi wa Umma ya 2004. Hapa, Bodi ya Zabuni ya TTCL ilitumia utaratibu wa zabuni zuifu (restricted tendering) kinyume na maamuzi yaliyofanywa na Bodi ya Wakurugenzi walioidhinisha mchakato wa manunuzi wa ushindani wa kimataifa.

Nne, Menejimenti imefanya manunuzi ya magari 10 yenye thamani ya Sh. 1.25 bilioni pasipo kuzingatia vyema Sheria ya Ununuzi wa Umma. Kamati ya Tathimini ya Zabuni ilipendekeza zabuni hiyo itolewe kwa Toyota Tanzania pamoja na kwamba mzabuni huyu hakukidhi vigezo vingi vilivyoainishwa katika zabuni hiyo.

Tano, Menejimenti imeshindwa kudhibiti matumizi ya mafuta ya magari jambo ambalo liliingizia kampuni hasara ya Sh. 73.7.

Sita, Menejimenti imeruhusu manunuzi ya kiasi cha Sh. 45.7 bilioni nje ya mpango wa ununuzi wa mwaka. Hatua hii ni kinyume na matakwa ya kif. 45 cha Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2004 na Kanuni ya 25(3) ya Kanuni za Sheria ya Ununuzi ya Umma ya Tangazo la Serikali Na.97 la mwaka 2005. Kanuni hii inazitaka taasisi za umma kuandaa mpango wa ununuzi kwa kuzingatia mahitaji yaliyopo ndani ya mpango mkakati.

Saba, Menejimenti imefanya manunuzi yenye thamani ya Sh. 3.442 bilioni pasina kuzingatia viwango vya ukomo vilivyoainishwa kwenye jedwali la pili la Kanuni za Sheria ya Ununuzi Tangazo la Serikali Na.97 na 98 la mwaka 2005. Kiwango kilichozidishwa ni Sh. 1.742 bilioni.

Ukiukwaji wa matakwa haya ya kisheria unapaswa kupata idhini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi (PPRA) kama inavyoelekezwa na kifungu cha 31(3) cha Sheria ya Ununuzi ya Umma ya mwaka 2004. Lakini hakuna kibali kilichoombwa wala kutolewa na PPRA kwa ajili hiyo.

Kutokana na kasoro hizo, Mdhibiti na Mkaguzi ametoa mapendekezo makuu matatu:-

Kwanza, Menejimenti ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ifikirie “kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wote ambao ripoti hii imeainisha kuwa wamehusika katika kuisababishia kampuni hasara ya upotevu wa fedha.”

Pili, “Wakurugenzi wa Bodi ya TTCL watoe mwongozo wa uadilifu na kutekeleza sheria za kukomesha udanganyifu.”

Tatu, “TTCL ihakikishe inafanya ukaguzi endelevu na usimamizi mzuri wa miamala inayofanyika katika mfumo wa hesabu wa Sunsystem, ili kudhibiti wizi kama uliofanyika kwenye mfumo wa uandaaji wa Mishahara.”

Ubia wenye utata kati ya serikali na wawekezaji

Taarifa kwamba kampuni ya TTCL sasa inashikilia mkia wa kibisahara katika sekta ya mawasilianonchini Tanzania kutokana na serikali kuwakaribisha wawekezaji wenye mgongano wa kimaslahi katika sekta hii zinayo historia ndefu sasa.

TTCL ilianzishwa kwa mujibu wa sheria Na.20 ya 1993 na kupata leseni ya kuendesha biashara ya mawasiliano ya simu za mezani. Mwaka 1999 tayari TTCL ilikuwa imefanikiwa kutafuta leseni ya kuendesha biashara ya simu za mkononi pia kupitia kampuni tanzu iliyoiita Celnet Tanzania Limited.

Ofisi za Celnet Tanzania Limited zilikuwa Kijitonyama, Dar es Salaam, mkabala na jengo la Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTEC).

Uanzishwaji wa Celnet Tanzania Limited ilikuwa ni moja ya mbinu za menejimenti kujiimarisha kibiashara ndani ya ushindani zikiwepo kampuni mbili tu – Tigo na Tritel. Kumbukumbu zinaonesha mtaji wa Celnet Tanzania Limited ulikuwa ni Sh. 500 milioni.

Katikati ya harakati hizo, 21 Februari 2001, serikali iliamua kuibinafsisha TTCL kwa kuuza sehemu ya hisa. Serikali iliuza 35 kwa Dola 120 milioni kwa kampuni ya Mobile System International (MSI) ya Uholanzi.

Hata hivyo, kampuni ya MSI ililipa dola 60 milioni tu (nusu ya kiwango halisi) kwa madai kuwa wangelipa kiasi kilichobaki baada ya mahesabu kukaguliwa upya na mkaguzi huru. Hivyo, malipo waliyoyafanya yalikuwa ni sawa na bei ya hisa asilimia 17.5 pekee. Serikali ilikabidhi menejimenti ya TTCL kwa MSI pamoja na kasoro hiyo ya kutekeleza mkataba.

Baada tu ya MSI kushika mamlaka ya TTCL, ilibadilisha leseni na jina la kampuni ya Celnet Tanzania Limited kuwa Celtel Tanzania Limited, ambayo Novemba 2001 ilipewa leseni ya kuendesha simu za mkononi.

Kampuni ya TTCL ilipewa asilimia 40 ya hisa za Celtel Tanzania Limited, ambazo baadaye zilihamishwa na Serikali na kupelekwa Hazina. Profesa Mark Mwandosya alikuwa ni Waziri mwenye dhamana na TTCL wakati huo, na Mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa Andrew Chenge.

Nyaraka mbalimbali zinaonesha kwamba MSI hawakuwekeza hata senti moja katika kampuni ya Celtel Tanzania Limited. Kinachoonekana ni kwamba, kabla ya kampuni ya MSI kuondoka TTCL mwaka 2005, walikuwa wamelipa ziada ya dola za Kimarekani 8 kati ya dola za Kimarekani 55 walizopaswa kulipa kama sehemu ya pili ya malipo ya hisa walizonunua katika TTCL.

Kwa ufupi, tangu kubinafsishwa kwa TTCL mwaka 2001, hisa zake zipatazo 35% zimekuwa zikiuzwa kwa mkopo kupitia utaratibu wa “mpokezano” kwa makampuni tofauti, yote yakiwa yanajitambulisha kama “wawekezaji” katika TTCL.

Mpokezano huo ni kama ifuatavyo: kutoka MSI kwenda Celtel International (2005), kutoka Celtel International kwenda Zain ya Kuwait (2008) na kutoka Zain ya Kuwait kwenda Bharti Airtel ya India (2010). Kampuni ya Bharti Airtel Ltd ya India ndio mmiliki wa Airtel Tanzania Ltd kwa sasa. Kumbukumbu zinaonesha kuwa wawekezaji hawa wote hawajawahi kuwekeza fedha yoyote ili kuimarisha TTCL.

Utafiti zaidi unaonesha MSI, Celtel International, Zain ya Kuwait na Bharti Airtel ya India wamekuwa “wawekezaji” na wakati huohuo “washindani” wa TTCL kibiashara katika sekta ya mawasiliano.

Kwa hivyo, haya ni makampuni yaliyokuwa na mgongano wa maslahi. Kwa sababu hii, wachunguzi wa mambo wanasema mgongano huu wa kimaslahi uliwasukuma “wawekezaji” hawa “kuihujumu TTCL kisayansi.”

Kwa mfano, utafiti wa Mwanahalisionline ndani ya TTCL umebaini kuwa mpaka leo hii, bado kampuni hii inatumia teknolojia ya mawasiliano duni kuliko teknolojia inayotumiwa na makampuni mengine ya mawasiliano hapa nchini.

Wakati Tigo, Airtel na Vodacom wamekuwa wanatumia teknolojia ya kisasa ya “Global System for Mobile Communication” (GSM), TTCL wamekuwa wanatumia teknolojia kongwe ya “Code Division Multiple Access” (CDMA).

Simu zinazotumia “simukadi” za teknolojia ya CDMA haziwezi kupokea “simukadi” za teknolojia ya GSM. Hivyo, wateja wenye “simukadi” za mitandao ya Tigo, Vodacom na Airtel hawaoni sababu ya kununua “simukadi” za mtandao wa TTCL kwani “simukadi” hizi hazingiliani na simu za mikononi zinazotumiwa na wateja hawa wa mitandao ya Tigo, Vodacom na Airtel.

Lakini, kama TTCL wangetumia teknolojia ya GSM kwa muda wote huo, wangekuwa katika nafasi nzuri ya kushindana wakiwa na nguvu katika soko la biashara ya simu za mkononi nchini.

Hivyo, ni wazi kwamba kikwazo hiki cha kitekinolojia kimechangia kuidhoofisha kiuwezo TTCL na hivyo kubaki ikichechemea.

Takwimu za Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) zinathibitisha jambo hili. Mpaka Desemba 2012 Tanzania ilikuwa na watumiaji wa simu za meani na mkononi wapatao 28,024,611.

Wateja hawa waligawanyika kama ifuatavyo: Vodacom (44%), Airtel (27%), Tigo (20%), Zantel (8.4), TTCL (0.82%), Sasatel (0.18%) na Benson (0.0037%).

Mhandisi mmoja ndani ya TTCL, aliliambia Mwanahalisionline kwamba takwimu hizi ni ushahidi tosha kuonyesha kwamba “wawekezaji katika TTCL wameihujumu kampuni hii kwa sababu ya mgongano wa kimaslahi uliogubika dhamira na maamuzi yao.”

Hoja hii inaimarishwa na ukweli kwamba jitihada za TTCL kuingia katika soko la mawasiliano ya simu za mkononi zinazotumia teknolojia ya GSM mpaka sasa limekwama.

Historia inajieleza vizuri: Muda mfupi baada ya TTCL kupata hisa katika kampuni ya Celtlel Tanzania Ltd, ilinyang’anywa hisa zote na zikahamishiwa HAZINA mara moja, kwa sababu ya madai kwamba, kwa mujibu wa leseni yake, TTCL haikuruhusiwa kuanzisha biashara ya simu za mkononi.

Hata hivyo, baadaye mwaka 2005, serikali iliondoa masharti hayo ya leseni dhidi ya TTCL. Lakini Celtel international, ambaye tayari alikuwa ni mwanahisa katika TTCL na hivyo mbia wa serikali, alipinga wazo la TTCL kujiingiza kwenye biashara ya simu za mkononi. Sababu ni moja tu hapa: alikuwa ni mshindani wa TTCL katika biashara hiyo.

Baada ya kuona hivyo, wafanyakazi wazalendo ndani ya TTCL waliamua kuingiza biashara hiyo kwa siri kupitia teknolojia ya “CDMA” maarufu kama “TTCL Mobile.” Kwa namna fulani, wazalendo waliidanganya Bodi ya TTCL kuwa teknolojia ya “CDMA” ilikuwa ni kwa ajili ya “Fixed Wireless” au “Wireless Local Loop (WLL).”

Lakini, ukweli, kwa siri walikuwa wamebuni “Full Mobile Solution” ili kujitanua kibiashara. Bodi ya TTCL iliruhusu biashara hii kwa kuwa haikufahamu ukweli wote. Hata hivyo baadaye Bodi ilipogundua iliamua kuzuia uwekezaji zaidi katika mradi huo. Kwa hivyo, mradi wa “TTCL mobile” ukashindwa kufanyakazi kama lilivyokuwa lengo wakati wa kubuniwa.

Leo, miaka 15 baada ya TTCL kubinafsishwa, bado kampuni hii inashika mkia katika biashara ya mawasiliano ya simu.

Nyumbani na Diaspora: Mazungumzo na Haika Lawere


Beware of unaproved ear drops commonly given to children


The U.S. Food and Drug Administration this week announced its intention to take enforcement action against companies that manufacture and/or distribute certain unapproved prescription ear drop products (known as otic products) labeled to relieve ear pain, infection, and inflammation.

The unapproved prescription ear drops contain active ingredients such as benzocaine and hydrocortisone, and have not been evaluated by the FDA for safety, effectiveness and quality. The labels on these products do not disclose that they lack FDA approval, and health care professionals may not be aware of their unapproved status.

In a federal register notice published today, the agency informed the companies that they must stop manufacturing these unapproved prescription otic products or be subject to enforcement actions, including seizure, injunction and/or criminal proceedings. Today’s action does not affect FDA-approved prescription otic products, or legally marketed otic products sold over-the-counter.

Unapproved prescription otic drug products containing the following ingredients are covered by this action:
 • benzocaine;
 • benzocaine and antipyrine;
 • benzocaine, antipyrine, and zinc acetate;
 • benzocaine, chloroxylenol, and hydrocortisone;
 • chloroxylenol and pramoxine; and
 • chloroxylenol, pramoxine, and hydrocortisone.
More info/source: www.fda.gov

Study proves for first time: Hotter temps change lizards gender

The AP reports that a scientist have, for the first time, been able to prove that hotter temperatures are messing with the gender of Australia's bearded dragon lizards.
"This is the first time we have proved that sex reversal happens in the wild in any reptile at all,"
said Clare Holleley of the University of Canberra, lead author of the study in the journal Nature Wednesday. 

She also said that the study "is showing that climate extremes can very rapidly fundamentally alter the biology of an organism.

It is noted in the article that, in the past, scientists showed in the lab that hot temperatures can switch that natural chromosome-based gender.

The AP article further discusses how dragons that are genetically male hatch as females and give birth to other lizards. And the way the lizards' gender is determined is getting changed so much that the female sex chromosome may eventually disappear entirely, the study authors say.

To understand what's happening, click the link above to read the whole article at the AP.

Bunge lazidi kupwaya: Spika atimua wengine

Taarifa ya BASATA kumhusu Ramadhan Masanja "Banza Stone"

Timu ya watendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ikiongozwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bi. Vivian Nsao Shalua mapema jana imemtembelea Msanii na mwimbaji wa muziki wa Bendi ndugu Ramadhan Masanja ‘Banza Stone ambaye kwa muda sasa amekuwa akiugua nyumbani kwao maeneo ya Sinza Jijini Dar es Salaam.

Lengo la ziara hii ilikuwa kumjulia hali Msanii huyu mahiri wa Bendi na kushauriana na familia yake juu ya namna bora ya kusaidia matibabu yake na kuhakikisha anapata huduma zote stahiki kulingana na maelekezo ya daktari wake.

Katika ziara hiyo, watendaji hao wakiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya African Stars Entertainment (ASET) Mama Asha Baraka walipata wasaa wa kufanya mazungumzo na familia ya mwanamuziki huyo ili kupata maendeleo ya afya yake, matibabu na mwenendo wake.

Wanafamilia hao wa Msanii Banza Stone wakiongozwa na Kaka yake Khamis Ally Masanja walieleza kwamba hali ya mgonjwa huyo imekuwa ikibadilika mara kwa mara na kwamba amekuwa akipata matibabu katika Hospitali ya Sinza iliyoko Sinza Palestina jijini Dar es Salaam. Aidha amekuwa akipelekwa hospitali mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam ikiwemo ya Mwananyamala ambayo anaendelea kutibiwa kwa sasa.

Baada ya kupata taarifa ya kina kuhusu afya ya msanii Banza Stone, watendaji wa BASATA kwa kushauriana na wanafamilia hao walifunga ziara kwenda hospitali ya Sinza ambayo pia amekuwa akitibiwa na kufanya utaratibu wa matibabu ili kuhakikisha anapewa huduma stahiki na kuhakikisha afya yake inaimarika.

Akizungumza hospitalini hapo Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA Bi. Shalua alitoa wito kwa wadau wa Sanaa na wasanii kwa ujumla kumwombea msanii Banza Stone na kujitolea kwa hali na mali katika kuhakikisha anarejea katika hali yake ya zamani na hatimaye kurudi kwenye Majukwaa ya maonesho.
“Wadau wa Sanaaa tumwombee na kumpa msaada stahiki msanii wetu. Msanii huyu ni muhimu kwenye tasnia ya muziki wa dansi. Amechangia sana katika kukuza muziki huu ndani na nje ya nchi. Tumwombee ili arudi katika hali yake ya awali” 
amesisitiza Bi. Shalua.

Imetolewa na Kitengo cha Habari cha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)