US Wins FIFA Women's World Cup in style


In the first five minutes, captain Carli Lloyd scored two swift goals — the fastest two goals in FIFA history, according to the FIFA Women's World Cup twitter account.Just a few minutes later, Lauren Holiday brought the score up to 3-0.

Lloyd again —from midfield — netted the ball to raise the score to an astounding 4-0, just 15 minutes into the game. It was the first hat trick in a Women's World Cup final and the fastest hat trick in any World Cup game.Japan hadn't given up. They scored an elegant goal in the 27th minute.

In the second half, Julie Johnston scored an own goal that Hope Solo couldn't block, bringing Japan's score to 2. A few minutes later, Tobin Heath scored again for the U.S., bringing America back to another dominant lead: 5-2 which they held through game's end.

The game was a rematch of the 2011 World Cup final, which Japan won in a dramatic penalty kick shoot-out. That game was tense: 1-1 at the end of regulation and 2-2 at the end of overtime, before Japan won the shootout 3-1.

Madabida akana kumfananisha mgombea Urais na Mtume - Taarifa ya Habari ChannelTEN, Julai 5, 2015


Anna Ponera ana sh laki 3 anaomba umchangie atimize 1,600,000/= afanyiwe operesheni

Anna Joseph Ponera (48) ni mzaliwa wa Kijiji cha Mtyangimbole Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma, yeye ni Mama wa watoto wawili anayeishi peke yake huku akitegemea misaada ya wasamaria mbalimbali kutoka katika kijiji anachoishi na maeneo mbalimbali nchini ili walau aweze kuiona siku inayofuata.

Kati ya watoto wote aliofanikiwa kuwapata, Ponera, aliwazaa kwa njia ya upasuaji ambapo mmoja kati yao alikufa mwaka 2011 kutokana na matatizo ya kiafya.

Mwaka 1993 alifanyiwa oparesheni ya pili ya uzazi na kufanikiwa kupata mtoto wa pili wa kike ambaye kwa sasa analelewa na Watawa wa Kanisa Katoliki mkoani humo chini ya Shirika la St. Agnes Chipole la mkoani humo kutokana na kukosa uwezo wa kumtunza.

Akizungumzia maisha yake kwa ujumla na FikraPevu iliyomtembelea nyumbani kwake katika Kijiji hicho, amesema baada ya kuendelea kupata maumivu ya tumbo kwa muda mrefu alishangaa kuona uvimbe mdogo uliojitokeza sehemu ya chini ya kitovu ambao anasema ulimsababishia maumivu makali sana hadi leo.

Mara baada ya kuona maumivu yanazidi alikwenda katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma ambako wataalamu wa afya walimfanyia uchunguzi na kugundulika kwamba anatakiwa kufanyiwa upasuaji ili kuondoa uvimbe huo. Alifanyiwa upasuaji na mara tu baada ya upasuaji huo aliweza kukaa miezi mitatu tu na kuanza tena kusikia maumivu makali ya tumbo hali liyimfanya aripoti tena hospitalini kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake.Anna Joseph Ponera anayesumbuliwa na tatizo la uvimbe tomboni kwa zaidi ya miaka 10

Hata hivyo, kuanzia mwaka huo hadi sasa hivi, anaeleza kwamba aliendelea kuishi na maumivu yale kwa muda wa miaka miwili akidhani ni maumivu ya kidonda cha upausji aliofanyiwa, lakini baadaye hali hiyo iliendelea kuwa mbaya hadi alipoamua kwenda katika Hospitali ya Misheni ya Peramiho ambako alifanyiwa vipimo na kuambiwa ana uvimbe mwingine tumboni hivyo alitakiwa kufanyiwa upasuaji mwingine.

Mnamo mwaka 1999 alifanyiwa operesheni hiyo na baada ya upasuaji tumbo lake lilianza kutulia kwa muda, kabla ya mwaka mmoja toka alipofanyiwa upasuaji wa mwisho, maumivu yalianza tena sehemu ya chini ya kitovu na uvimbe wenye asili ya kitu kigumu sana.

Ilipofika mwaka 2001 alifanyiwa tena oparesheni kwa mara ya nne ili kuondoa uvimbe huo ambao ulikuwa umejitokeza, wakati huo wote hali yake iliendelea kuwa mbaya na uvimbe mwingine ulijitokeza tena sehemu ile ile yenye mshono, uvimbe huo ulijitokeza nje kama chungwa au ukubwa wa embe dodo

“Mwaka 2004 anilikwenda tena Hospitali ya mkoa wa Ruvuma iliyopo Songea safari hii nayo walinipima na kuamua kunifanyia oparesheni nyingine ya tano wakaondoa ule uvimbe” alieleza Ponera.

Tangu afanyiwe upasuaji huo pamoja na mambo mengine, anaeleza kwamba afya yake ilianza kutengemaa licha ya kwamba afya yake ilikuwa inamsumbua mara kadhaa hali iliyomfanya awe na utaratibu wa kufuata huduma ya dawa za kutuliza maumivu mara kadhaa hospitalini. Anasimulia kwamba amekuwa akiishi hivyo kwa muda mrefu hadi ilipofika mwaka 2014 alipokwenda tena katika Hospitali ya Mkoa huo na kufanyiwa tena vipimo ambapo wataalamu wa afya walimuambia anatakiwa kufanyiwa tena oparesheni kubwa ambayo inatakiwa kufanywa katika Hospitali Taifa ya Muhimbili.

Amesema gharama zinazohitajika kwa ajili ya upasuaji huo ni Sh. 1,500,000, huku akieleza kuwa hana fedha za kugharamia usafiri wa kwenda na kurudi kutoka Songea hadi Muhimbili kwa watu 2 ambaye ni mtu wa kumhudumia ambapo kila mmoja nauli yake ni Sh. 100,000 pamoja na fedha za kujikimu wakiwa Muhimbili.

Mpaka sasa kutokana na mahangaiko ya matibabu ameuza vitu vya ndani vingina sasa anaishi katika nyumba ya kupanga huku kiwanja alichokuwa akikimiliki akiwa amekiuza ili kupata fedha ya kujitibu. kia Baada ya kukosa msaada wa fedha alijitahidi na kujishughulisha na bishara ndogo ndogo ikiwemo kuuza mboga mboga ambapo hadi kufikia mwezi wa pili mwaka huu alishindwa kufanya kazi hiyo kutokana na maumivu makali na sasa anategemea misaada kutoka kwa wasamaria.Mazingira ya ndani kwenye nyumba anayoishi, Anna Joseph Ponera,

Baadhi ya watu wanaomsaidia hadi sasa kwa karibu ni Wakristu wenzake wa Jumuiya ya Mtakatifu Joseph Mjimwema Manispaa ya Songea ambako anaishi kwa sasa pamoja na majirani wenye huruma na mapenzi mema ambao humsaidia chakula.

Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Songea imempatia msaada wa kumpa kibali cha muda wa miezi mitatu ili aweze kuomba msaada kwa wasamaria wema (Hajafanikiwa kuzunguka kwa watu ili kupewa msaada wa fedha). katika kuendelea kuomba fedha ya matibabu alikwenda tena Kanisa katoliki la Mji Mwema Manispaa ya Songea kuomba Msaada ambako walimchangia kiasi cha Sh. 140,000 hivyo mpaka sasa kiasi alichonacho mkononi ni Sh. 300,000 tu.

“Ninawaomba ndugu zangu Watanzania wanisaidie kunichangia fedha ili niweze kupatiwa matibabu kwamaana ninapata mateso na maumivu makali, wakiniona tumbo langu jinsi lilivyokubwa watanionea huruma. Ninatokwa na manundu makubwa matatu. Mungu awabariki wote mtakaojaliwa kutoa msaada kwangu na wale wenye lengo la kutoa lakini hawana uwezo Mwenyzi Mungu awazidishie” alieleza Ponera.

Amesema kwa yeyote mwenye mapenzi mema anaomba amchangie fedha kwa ajili ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupitia namba yake ambayo ni 0756 603 148. Atakapopata kiasi hicho cha fedha ndipo atakapopewa barua na Hospitali ya Mkoa huo kwenda Muhimbili kwa ajili ya matibabu.

Anna Ponera, hana uwezo kabisa wa kujihudumia na anaishi kwa msaada wa wasamaria wema wanaojitolea kumhudumia. Hana ndugu wala rafiki wa karibu anayemfariji kwani mumewe alifariki mwaka 2008.

Taarifa ya TFF kuhusu mechi ya Uganda vs Tanzania

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager imetoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya wenyeji Uganda (The Cranes) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za CHAN mwaka 2017 nchini Rwanda uliofanyika uwanja wa Nakivubo.

Stars ambayo leo imeonekana kabadilika katika mchezo wa leo, ilicheza soka la kuvutia tangu mwanzo mpaka mwisho wa mchezo hali iliyowaduwaza wenyeji Uganda.

Mpaka dakika 45 za mchezo za kipindi cha kwanza zinamalizika, Uganda 0 - 0 Tanzania. Kipindi cha pili kilianza kwa Stars kufanya mashambulizi mfululizo kupitia kwa washambuliaji wake John bocco na Rashid Mandawa.

Dakika ya 58, John Bocco aliipatia Tanznaia bao la kwanza kwa mkwaju wa penayi kufuatia mlinzi wa Uganda Bakaki Shafik kuunawa mpira wa ndani ya eneo la hatari.

Mara baada ya bao hilo Uganda walifanya mashambulizi mfululizo langoni mwa Stars na kufanikiwa kupata bao la kusawzisha dakika ya 82, kupitia kwa mchezaji Kizito Hezron.

Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Uganda 1 - 1 Tanzania. Kwa matokeo hayo Uganda wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 4 - 1 na sasa watakutana na Sudan.

Mara baada ya mchezo huo kochaa mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema anashukuru vijana wake wamejitahidi kucheza vizuri, mchezo ulikua mzuri timu ilitengeneza nafasi chache na kuweza kutumia nafasi moja iliyopatikana.

Mkwasa amewaomba watanzania kuendelea kuwapa sapoti, wamekaa na timu kwa muda mfupi wa wiki moja tu lakini katika mchezo wa leo mabadiliko yameonekana, hivyo wanahitaji muda kidogo kuweza kukaa na vijana kwa muda mrefu ili kujenga timu bora.

Stars inatarajiwa kurejea Tanzania siku ya jumatatu mchana kwa usafiri wa shirika la ndege la Rwanda Air.

Taifa Stars: Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Haji Mngwali, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Frank Domayo,/Said Ndemla John Bocco, Rashid Mandawa/Salum Telela, Saimon Msuva/Ramadhan Singano.

The Cranes: James Alitho, Muzamiru Mutyaba, Brian Ochwo, Hassan Waswa, Denis Oola, Faruk Miya, John Shemazi/Robert Sentongo, Bakaki Shafik, Tekkwo Derick/Kizito Hezron/Kalanda Frank.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)