So, you think you can fire Kansiime...


Mwanasheria Fulgence Massawe, John Mnyika wazungumzia hukumu ya Mramba, Yona, Mgonja


Ndani mwa ukumbi mpya wa CCM Dodoma


Mwonekano wa nje wa jengo jipya la ukumbi wa mikutano wa kisasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Dodoma. Ukumbi huu utaanza kutumika rasmi Julai 10, 2015 wakati wa Mkutano Mkuu wa CCM wa kupitisha jina la mgombea Urais atakayeipeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu. Ukumbi huu una uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 3,000 kwa wakati mmoja.Taarifa ya Habari ya kutwa nzima Channel TEN, Saba Saba, 2015


Taarifa ya Mkuu wa Mkoa kuhusu Ulinzi na Usalama Dodoma

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

Mkoa wa Dodoma
Anwani ya Simu REGCOM
Simu Nambari: 2324343/2324384
E-Mail No. [email protected]
Fax No. 255 026 2320046

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
S.L.P. 914,
DODOMA.

TAARIFA YA MKUU WA MKOA WA DODOMA MHE. CHIKU GALLAWA 
KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkoa wa Dodoma, kwa kipindi cha wiki moja kuanzia leo tarehe 7/7/2015 kutakua na mikutano mikubwa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ikitanguliwa na Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na kuhitimishwa na Mkutano Mkuu, ambapo agenda kuu ni kuchagua mgombea wa kiti cha Urais atakayeiwakilisha CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba.

Mikutano hii yote na shughuli nyingine mbalimbali zinazoendelea hapa Mkoani Dodoma zinajumuisha idadi kubwa ya watu wakiwemo Viongozi Wakuu wa Kitaifa, Viongozi mbalimbali, Wajumbe wa Mikutano hiyo yote na wageni waalikwa mbalimbali. Vilevile wananchi wa Mikoa mingine na hata Mataifa mbalimbali yatakuwa yakifuatilia kinachoendelea hapa Mkoani Dodoma.

Natumia fursa hii, kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma, kuwakaribisha wageni wote na Itifaki nzima inayokuja hapa Mkoani Dodoma Makao Makuu ya Nchi na Chama Tawala, kwa ajili ya Mikutano hiyo Mikubwa. Mkoa wa Dodoma una uzoefu wa kubeba matukio makubwa kama haya katika nchi yetu.

Mkoa wa Dodoma tumejiweka tayari kuwahudumia wageni wote kwa huduma muhimu zitakazohitajika kwa kipindi hiki, niwaombe wananchi wa Dodoma hasa wajasiriamali wa bidhaa na huduma mbalimbali kuchangamkia fursa hii kubwa iliyopo hapa Dodoma. Pia kuhakikisha usalama na ubora wa huduma.

Vilevile, kwa niaba ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dodoma, natumia fursa hii kuwataka wananchi wote hapa Mkoani Dodoma na Wageni wote kudumisha hali ya Utulivu, Amani, Ulinzi na Usalama ili mikutano hii yote na shughuli mbalimbali zifanyike kama zilivyopangwa kwa mafanikio. Kila mmoja awe balozi na mlinzi wa mwenzie na Wananchi tuwe wepesi kutoa ushirikiano kwa vyombo vyetu vya ulinzi pale inapohitajika.

Napenda kuwatoa hofu na Mashaka wageni wote na wananchi kwa ujumla hapa Mkoani Dodoma kwamba, vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana, vimejipanga na kujiimarisha ipasavyo ili kuhakikisha kwa namna yoyote ile kunakuwepo na Utuivu, Aman, Ulinzi na Usalama.

Niwatahadharishe wale wote wanaojipanga kwa namna moja ama nyingine kushiriki vitendo vya uvunjifu wa Amani, Utulivu, Ulinzi na Usalama kwamba tutawashughulikia kwa mujibu wa sheria za nchi. Asiye mjumbe wa Mikutano na wala siyo mwalikwa ni bora wasije kabisa Dodoma.

Kwa kuwa Mikutano hii itachangia ongezeko la idadi na muingiliano wa watu hapa Mkoani Dodoma, baadhi ya Wajumbe/Wageni watakuwa na vyombo vya Moto vya usafiri, hivyo, niwaombe madereva wote kuendesha kwa ustaarabu mkubwa na kuzingatia sheria za usalama barabarani na udereva wa kujihami, ili kuepusha ajali. Askari wa Usalama barabarani wasimamie kwa makini usalama barabarani.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza

Chiku A. S. Gallawa
MKUU WA MKOA WA DODOMA
Julai 07, 2015

Laptop ya BVR yaibwa


Kompyuta mpakato (laptop) inayotumika kwenye mashine ya ‘Biometric Voter Registration’ (BVR) imeibiwa na watu wasiojulikana katika Kata ya Nyugwa wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita.

Akisimulia tukio zima lilivyokuwa, Afisa mwandikishaji msaidizi wa uchaguzi wa halmashauri ya Nyang’hwale Slyvester Kabora, alisema kuwa mashine zote za BVR zilikaguliwa na kuonekana ziko salama ambapo zilipakiwa kwenye gari na hatimaye maafisa uandikishaji walikabidhiwa lakini cha kushangaza walipata taarifa mashine moja imenyofolewa laptop mpakato.

Alisema Kifaa hicho kiliibiwa mnamo Julai 6 mwaka huu, ambapo maafisa uandikishaji waliofika katika kituo zilipokuwa zimehifadhiwa mashine hizo saa 12:00 asubuhi, waligundua mashine moja ina kasoro.
“Mashine zile zilifikishwa katika kata ya Nyugwa zikawekwa katika ofisi za kata hiyo, ila cha ajabu asubuhi maafisa wakiwa katika harakati za kuzisambaza mashine hizo kwenye vituo ndipo moja iligundulika haina laptop... lakini mazingira ya kuibiwa laptop hiyo ni ya kutatamisha kwa sababu mlango ulikuwa haujavunjwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Fortunata Mallya alikanusha madai ya kuwa mashine moja ya BVR imeibiwa kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyo ripoti.

Akizungumza jana na waandishi wa habari ofisini kwake Fortunata Mallya alisema kuwa kuna redio moja nchini (jina tunalo), ilitangaza kuibiwa kwa mashine hiyo taarifa ambazo ni za uongo na kwamba kitu kilichoibiwa kwenye mashine hiyo ni laptop na siyo mashine ya BVR.
“Nimesikitishwa sana na baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari pasipo kujiridhisha kama taarifa hizo ni za kweli ama la. Kwanza nawashukuru sana nyinyi waandishi mliofunga safari kutoka Geita kuja huku kufuatilia suala hili, ni kwamba nina mashine BVR 49 moja ndiyo waliyoitolea laptop,’’
alisema Mkurugenzi.

Watu watatu wanashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo ambao ni Aloyce Kata mkazi wa eneo hilo, wengine wawili majina yao hayakuweza kufahamika mara moja.

TPA yafungua ofisi ndogo nchini Zambia

Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma (katikati) akifurahia baada ya uzinduzi rasmi wa ofisi ndogo ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mjini Lusaka hivi karibuni. Ofisi hiyo ilizinduliwa na Waziri wa Usafirishaji, Kazi na Mawasiliano wa Zambia, Bw. Yamfwa Mukanga (kushoto); kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Awadh Massawe.

Mhe. Nassari apata ajali ya helikopta


Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki (CHADEMA), Joshua Nassari amepata ajali ya helikopta aliyokuwa akiitumia kufanya ziara jimboni kwake hii leo.

Habari kutoka Arumeru zinasema kuwa helikopta hiyo ilipoteza mwelekeo na kwenda kugonga mti na kunasa juu ya mti huo.

Aidha taarifa hizo zinaeleza kuwa Mbunge huyo na rubani wake walitoka wakiwa wazima na wapo katika Hospitali ya Kanisa la Kilutheri ya Selian ya jijini Arusha. Abiria wawili, mmoja anajulikana kwa jina la Eve ambaye ni mmoja wa viongozi wa BAWACHA jimboni, ameumia mbavu na mwingine kuvunjika mguu.


  • Taarifa via Father Kidevu Blog.Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe ametuma salaamu za pole na kuwatakia uponaji wa haraka majeruhi wa ajali mbili zilizotokea maeneo tofauti leo, moja ikihusisha helkopta nyingine ikitokana na ajali ya basi.

Katika salaamu hizo, Mwenyekiti Mbowe ametoa pole kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari, Mjumbe wa Baraza la Wanawake (BAWACHA) Wilaya Eva Kaaya, Katibu wa Mbunge Elisa Mungure pamoja na rubani William Silaa kutokana na ajali ya chopa iliyotokea eneo la Leguruki wakati mbunge na viongozi hao walipokuwa kwenye ziara jimboni humo.

“Wakati tukiwa kikaoni hapa tumepokea taarifa mbaya zinazohusu ajali mbili, ajali moja imewahusisha Mbunge Nassari pamoja na viongozi wengine wawili wa chama ambapo chopa waliyokuwa wakitumia kufanya ziara jimboni kwake ime-crash.

“Taarifa za awali zimetuhakikishia kuwa wamenusurika katika ajali hiyo na wamekimbizwa Hospitali ya Serian mjini Arusha ambako wanaendelea kupata matibabu kutokana na majeraha waliyopata...hali zao zimeelezwa kuwa si mbaya sana.

Tunaendelea kufuatilia kwa karibu hali za majeruhi hao ambao wamepata ajali wakiwa kwenye mapambano.
“Mbunge wetu Mwanamrisho Abama naye amenusurika kwenye ajali iliyotokana na basi alilokuwa amepanda akiwahi kuja kwenye kikao hiki…basi hilo limepinduka wakati likitoka Dodoma kuja Dar es Salaam. Mheshimiwa Abama naye pia anaendelea vizuri.

Tuwatakie uponaji wa haraka wote waliopatwa na ajali hizo zote mbili na Mwenyezi Mungu awapatie wepesi katika hali hiyo,” amesema Mbowe.

Imetolewa 7 Julai 2015 na;
Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA

4 Tips for Finding the Right Rental Property


If you like the idea of investing in something you can touch and feel, buying a rental property can be an attractive option. The key, experts say, is purchasing the right place up front. Here are some tips on locating a good rental and sizing it up.

  1. Buy in a desirable location. Good schools, low crime rates and nearby amenities like parks and shopping all matter in a real estate search. Some experts suggest limiting your search to properties near your home (say, a 20-minute drive) so you can keep ties with tenants and respond quickly in case of emergencies. Wherever you search, look into local vacancy rates and rental prices for comparable properties, and ask whether any new apartment buildings are in the works.

  2. Consider landlord laws. Being a landlord means being up to speed on all applicable laws, from federal fair housing laws to local ordinances that may dictate regulations like minimum square footage or ceiling height for bedrooms. If you're buying into an association, consider those rules as well. Many condos, for instance, cap the number of units that can be rented at any given time.

  3. Total your expenses. Think beyond the mortgage. Tally up real estate taxes, association fees, the cost of finding tenants, and your insurance and maintenance outlays. Save about one to three percent of the value of your rental property for upkeep each year. The goal, of course, is finding a property where the rent exceeds your costs, but you'll still need a plan for carrying the expenses yourself in the event of a vacancy.

  4. Inspect the property. If you're the DIY type, then by all means, consider a fixer-upper. Otherwise, look for a newer or recently renovated property that won't take too much effort to maintain. A home inspector can help identify structural or safety issues and may help you assess the condition of related factors too -- for instance, when the condo unit is in great shape, but the building roof needs repair. A detailed inspection can save you an extra outlay of cash down the road.
Tips by Ben Allred
Sr. Loan Officer
Phone: (480) 635-3084
Mobile: (480) 495-3197

Here as some US Universities in trouble and under Gov investigation


Well intentioned or not, the unfettered rise of for-profit colleges since the 1990s is costing taxpayers. For-profit schools consistently take in more federal loan money than nonprofit schools, despite enrolling a smaller number of students. Yet, for-profit students also account for 47 percent of all federal student loan defaults, according to a 2012 Senate investigation.

In addition to loan defaults, state and federal investigations have turned up widespread allegations of fraud and deceptive business practices, particularly in the case of the now-defunct for-profit chain Corinthian Colleges. The findings have been so startling that last month the Education Department launched a major consumer bailout program and appointed a "special master" to oversee debt relief for students.

Certain Corinthian-related programs, including those at Heald College, were deemed so unfair and predatory that the Education Department set up a website to make the process of debt relief easier for those students. Officials estimate bad debt resulting from Heald College at about $542 million. The total could climb. The Education Department estimates it loaned some $3.6 billion in the past five years to Corinthian students before the government forced it to sell or close its campuses.

Other for-profits too are showing signs of trouble: ITT Educational Services, Education Management Corp., University of Phoenix, Career Education Corp., Kaplan and DeVry University are among those that have disclosed to shareholders that they are or have been subjects of investigations by state or federal authorities.

Gumzo la leo WhatsApp ni hizi picha za viongozi wakipelekwa jela

Kamati Kuu ya CHADEMA yakutana kwa dharura

Kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya CHADEMA

KAMATI Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), leo wamekutana Jijini Dar es Salaam kwa dharura kwa ajili ya kujipanga ili kukabiliana na changamoto za kisiasa wanazokabiliana nazo kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Wakizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu amesema kwamba kikao hicho ni kwa ajili ya kupokea, kujadili na kutolea mamuzi taarifa kadhaa.

Amesema kuna Taarifa ya Utekelezaji wa Mkakati wa CHADEMA kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 mpaka sasa, Taarifa ya Zoezi la Uandikishaji Wapiga Kura kwa kutumia mfumo mpya wa BVR nchini, Hali ya Kisiasa huko Zanzibar, Taarifa ya Wabunge Kuhusu Yaliyojiri Bungeni kuhusiana na miswada tata ya gesi na mafuta, na Taarifa nyingine kuhusiana na utendaji wa kazi za kila siku za chama.

Mwalimu amesema Zanzibar watu wanapigwa hovyo wakiwa katika vituo vya kujiandikisha. Serikali ya Mapinduzi ikiulizwa amesema vitendo hivyo vinafanywa na genge wahuni wanaomiliki silaha

Kuhusu zoezi la Kuandikisha wapiga kura nchi nzima, Mwalimu amesema kwamba, kuna taarifa za vurugu kutoka sehemu mbalimbali nchini kote; kwamba magari ya serikali yanasemekana kukosa mafuta na hivyo kushindwa kubeba mashine za BVR katika baadhi ya maeneo.
“Mambo haya yanatokea katika maeneo ambako ni ngome ya UKAWA kisiasa. hivyo kuwa kikao cha leo kitapokea taarifa kamili kutoka kila mkoa na hatimaye kufanya maamuzi stahiki kuhusu zoezi hili.”
amesema.

Nae Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, John Mnyika, amesema katika mkutano alipinga vikali taarifa zilizochapishwa na gazeti moja la serikali ya CCM likidai kwamba wabunge wa ukawa wanakwepa kujadili miswada ya gesi na mafuta kwa kuwa ni vibaraka wa makampuni ya kigeni yaliyowekeza katika sekta hii.

Kwa mujibu wa Mnyika, 
“wabunge wa CCM wanaoshirikiana na Spika Makinda kupitisha miswada husika kinyemelea ndio wanapaswa kuhesabiwa vibaraka wa wawekezaji hao.” 
Mnyika aliwaomba waandishi wa habari kutafuta habari za kiuchunguzi kuhusu jambo hili kusudi hatimaye walisaidie taifa kuujua ukweli wote kuhusu ukibaraka huu wa wabunge wa CCM na serikali yao.

Mnyika alitumia nafasi hiyo kutoa msimamo wa CHADEMA kuhusu hukumu iliyotolewa na Mahakama dhidi ya Aliyekuwa Waziri wa Fedha Basil Mramba na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Daniel Yona amesema adhabu ya miaka mitatu waliyopewa ni ndogo ikilinganishwa na ukubwa wa hasara waliyolisababishia taifa.

Hata hivyo, Mnyika ameipongeza hukumu hiyo kwani imethibitisha tuhuma zilizotolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbroad Slaa, mnamo 15 Septemba 2007 huko Mwembeyanga jijini Dar es Salaam, alipowataja mafisadi wakuu 11, wakiwemo Yona na Mramba.

Mnyika alitumia nafasi hiyo kuikumbusha serikali kuendeleza zoezi hili la kuwaburuza mafisadi wote mahakamani bila kujali sura zao. Kwa upekee aliiomba serikali kuwaburuza mahakamani watuhumiwa wote katika sakata la EPA, Escrow, na kashfa nyingine kubwa zilizolikumba taifa hili mpaka sasa.

Hata hivyo viongozi hao wamesema wataweka wazi kwa waandishi wa habari yale yote yatakayojadiliwa katika kikao na maazimio waliyoyaweka baada kumalizika.

Kulikoni? Kaburi la marehemu latupiwa vitu vyake, viti, meza, godoro...


Katika tukio lisilokuwa la kawaida ambalo limevuta umati mkubwa wa watu katika mji wa Bariadi mkoani Simiyu katika eneo la makaburi ya Kidinda ni wananchi kukuta kwenye kaburi mojawapo kukiwa na vitu mbalimbali ikiwemo godoro, mabegi, viti, kutanda, meza, vyombo na vitu vingine

Mashuhuda waliobaini kuwepo kwa tukio hilo wamesema inawezekana linatokana na imani za kishirikina.

Wamesema walifika katika makaburi hayo kwa ajili ya kumsitiri ndugu yao aliyefariki lakini cha kushangaza wakaona juu ya moja ya makaburi kukiwa na vitu hivyo na kudai kuwa huenda marehemu alizikwa navyo.
"Sisi tulikuwa na msiba... tukaja hapa makaburini kuzika, ghafla tukaona juu ya kaburi kuna vitu hivyo..inaonekana huyu marehemu alizikwa na vitu vyake vikaletwa hapa makaburini na kuwekwa juu ya kaburi lake", 
alieleza mmoja wa mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Stanslaus Rweyemamu.

Kufuatia taarifa hizo waandishi wa habari bila kupoteza muda walifika katika eneo la tukio na kukuta vitu hivyo vikiwa juu ya kaburi la marehemu, huku wahusika waliofanya hivyo wakiwa hawajulikani kutokana na wahusika wa msiba kutokujulikana.


Hata hivyo baada ya askari hao kufika eneo la tukio walivichukua vitu hivyo na kuondoka navyo kituo cha polisi Bariadi .

Kamanda wa polisi Mkoani Simiyu Gemini Mushy amethibitisha kuwepo kwa tukio hilo na kwamba wanaendeela kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.


Baadhi ya vitu vilivyokutwa juu ya kaburi la Marehemu


Baadhi ya wananchi wakishuhudia tukio hilo


Wakazi wa eneo hilo wakishangaa mizigo hiyo
  • Imenukuliwa kutoka Malunde 1 blog

Mch. Mtikila kuwafungulia kesi wawania Urais 6 kupitia CCM


MWENYEKITI wa Democratic Party, (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, anatarajia kutinga mahamani kukifungulia mashtaka Chama Cha Mapinduzi (CCM), pamoja na makada wake sita, akidai wameanza kampeni za uchaguzi mkuu mapema.

Makada hao ni Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, na Waziri mstaafu Frederick Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe.

Wengine ni William Ngeleja, Waziri wa Chakula na Kilimo Stephen Wasira na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia January Makamba, ambao wote hao waliwahi kupewa adhabu Februari 18 mwaka jana, kwa kosa la kuanza harakati za kuwania nafasi ya urais.

Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mchungaji Mtikila, alisema kuwa suala la makada hao sio la kuliacha hivi, hivi, kwani linagusa maslahi ya nchi.

Alisema, amefikia hatu hiyo baada ya kujiridhisha kuwa wanaushahidi wa kutosha juu ya vitendo vya makada hao kwenda kinyume na sheria za uchaguzi.

Mchungaji Mtikila, alisema makada hao wamejiingiza kwenye vitendo vya matumizi makubwa ya fedha kwa kusafirisha watu kwenda maeneo mbalimbali huku watu hao wakilewa na kulala bure.
“Wanasheria wetu hivi sasa wanapinda migongo katika kukamilisha mchakato wa shauri hili n kwamba litakapokamilika wakati wowote kuanzia sasa tutawaita kuwaeleza kwamba linakwenda mahakamani.
“Baadhi ya watu wanatafuta utawala kwa sababu ni meno ya kumung’unya rasilimali za nchi hii,”
alisema Mchungaji Mtikila.

Mchungaji Mtikila alisema kuwa hatua hiyo ya kukifikisha chama hicho pamoja na makada wake hazitaishia hapo bali watafanya hivyo hata katika vyama vingine pindi watakapobaini vimeingia kwenye vitendo vya matumizi ya fedha chafu katika upataji wa wagombea wake.
“Kumekuwa na umwagwaji kubwa wa mabilioni ya fedha chafu kwa ajili ya kusaka madaraka jambo ni sawa na uhalifu na uhani,”
alisema Mchungaji Mtikila.


KATIKA UCHAGUZI MKUU HUU TUSIRUHUSU MAFISADI WALICHEZEE TAIFA


Edward Lowasa ni balaa kwa Taifa!

Democratic Party (DP) inatarajia kufikisha Mahakamani chama cha CCM pamoja na wanachama wake sita, Edward Lowasa na wengine, kwa mujibu wa Ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, kwa kosa kubwa sana la kuvunja Katiba na Sheria za Nchi kwa kuanza kampeni ya Uchaguzi kabla ya wakati unaopasa kwa mujibu wa Sheria.

1. Tunao ushahidi mzito unaothibitisha kwamba Edward Lowasa na wenzake walianza kampeni ya urais ndani ya chama chao kabla ya wakati, na kwamba chama chao kiliwapa adhabu ya kutofanya siasa kwa miezi 12. Lakini safari hii Lowasa ameanza kampeni ya urais Arusha kwa mkutano mkubwa sana wa hadhara wa kampeni haramu na kumwaga rushwa ya kutisha!

2. Kama ni wadhamini alipaswa kuwapata katika ofisi za chama chake, katika mikoa nane (8) tu Tanganyika na mikoa miwili tu Unguja na Pemba, wadhamini 45 tu katika kila mkoa. Lakini Edward Lowasa amefanya mikutano nchi nzima, ya kuwaahidi maelfu ya wananchi katika kila mkutano wa hadhara, mambo atakayofanya kama wakimpa kura zao awe Rais! Hii ndiyo kampeni halisi, ambayo ni ukiukaji wa Katiba na Sheria za Nchi! Uchaguzi Mkuu unaendeshwa na Sheria, hivyo ni lazima Sheria ichukue mkondo wake dhidi yake kwa kuivunja.

3. Edward Lowasa amevunja Katiba ya Nchi na Sheria ya kiwango cha fedha kinachoruhusiwa kutumika katika shughuli halali za Uchaguzi, kiasi kwamba CCM na Taasisi zote za uchunguzi wa kifedha nchini, upelelezi wa Jinai na Usalama wa Taifa ni mlazima wanayo kazi muhimu sana ya kupata ukweli kuhusu haya mabilioni ya fedha yanayomwagwa nchini na fisadi Edward Lowasa, ameyapata wapi na kwa namna gani, kumehusika ‘’Money laundering’ au la, kama mapato ya mapesa hayo yote ni halali, na kama mapato hayo yote yalilipiwa kodi inayopasa kwa ajili ya Taifa.

Ni marufuku kabisa tena ni makufuru Edward Lowasa kuruhusiwa kugombea urais, kwa sababu amevunja Katiba ya Nchi na Sheria na Kanuni za Uchaguzi. Sifa mojawapo ya kustahili kugombea uongozi wa nchi yoyote ni maadili mema na uzingatiaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za Utawala wa Sheria.

4. Edward Lowasa, kwa kujimilikisha maeneo nchi nzima kwa kutumia kifisadi Uwaziri wake wa Ardhi, ameliweka Taifa katika hatari kubwa ya mmwagiko wa damu baina ya wakulima na wafugaji, baada ya kueneza nchi nzima makundi ya ng’ombe wake, na kusababisha mapigano makali ya mara kwa mara kila mahali nchini kati ya wafugaji wake na wakulima. Kwa sababu ya uovu huu hata katika kampeni yake haramu Lowasa ameshindwa kusema lolote juu ya kilimo, ingawa ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi yetu na ndiyo shughuli inayotunza uhai wa asilimia 95 ya wananchi!

Kwa kuwaingilia wakulima katika ardhi yao, kuwaua ovyo, kuwaonea kiasi cha kufisha matumaini yao katika kilimo, kumeifanya kauli mbiu ya “Kilimo kwanza” kuwa porojo tu ya kisanii!

5. Edward Lowasa ni mwiko kabisa kupewa kugombea urais, kwa sababu siyo tu aliutumia kifisadi Uwaziri wa Ardhi akajitajirisha na kujipatia maeneo makubwa ya ardhi nchini kote, bali alitumia kifisadi zaidi uwaziri wa nchi katika ofisi ya Waziri Mkuu, katika uagizaji wa mashangingi ya Wabunge, mawaziri, wakuu wa Mikoa na Wilaya.

6. Edward Lowasa alikemewa mnamo mwaka 1995 na Mwalimu Nyerere anayeenziwa na CCM lama “Baba” yao, alipotaka kugombea urais, kwa sababu alikuwa fisadi papa, wala hakuweza kujitetea kwavile utapeli wote aliojitajirishia ulikuwa mezani. Leo baada ya mabiashara haramu mengi na kulipora sana Taifa kukiwa ni pamoja na utapeli wa “kununua mvua Thailand” na kuliibia Taifa mabilioni ya fedha kwa kutumia kampuni hewa ya RICHMOND, huyu ni fisadi-nyangumi. Ni mlemavu wa rushwa tu wa kununuliwa na mapesa machafu anayomwaga Lowasa, anayeweza kumruhusu fisadi Edward Lowasa agombee urais.

Sifa za mtu wa kukugombea Urais zimeelezwa bayana na Mwenyezi Mungu katika Kumbukumbu la Torati 17:15-20, ambazo Edward Lowasa hana hata mojawapo! Lowasa awali alikemewa na Mwalimu Nyerere ambaye CCM wanamuenzi kama “Baba” yao, kuwa hafai kabisa kuwania urais, kwa sababu alikuwafisadi papa, kama alivyomtangaza hata Reginald Mengi pale alipolazimika kujiuzulu Uwaziri Mkuu kwa ajili ya wizi kwa kampuni hewa ya Richmond, lakini leo akiwa fisadi la kutisha zaidi kuliko papa eti anataka urais!

Si ajabu kwamba magabacholi yalioipora vibaya sana Nchi hii kama Sigh Setti na hata Nazir Karamagi wote wamo katika genge la Edward Lowasa! Si ajabu hata fisadi Reginald Mengi leo kuungana na fisadi Lowasa yakizingatiwa machafu yake yeye mwenyewe, na kuhusika kwa Mengi na mauaji ya Chacha Wangwe, pamoja na mpango wa Chadema wa kumwua Mchungaji Mtikila, waraka feki wa kujaribu kuupotosha ukweli ukatangazwa kwa ITV yake.

Katika uwaziri wake katika ofisi ya Waziri Mkuu, na katika Uwaziri wakewa Ardhi na Uwaziri Mkuu, Lowasa alifanya ufisadi ambao katika nchi kama China zenye uchungu na maslahi ya mataifa yao angekuwa wa kupigwa risasi hadharani, lakini katika nchi yetu anatafuta urais!

7. Edward Lowasa AFYA yake imempiga marufuku kugombea Urais!
Kwa ajili ya kila ajira duniasni kote, moja ya mashart makuu ni lazima mwombaji awe na afya iliyo bora,ndiyo sababu ni lazima ajira ya kila mwombaji itegemee taarifa ya kitaalamu ya madaktari, inayothibitisha kwamba hana dosari kiafya. Sharti hili ni la lazima kwa sababu:

a. Majukumu yote atakayopewa mwajiriwa atayatekeleza kikamilifu kwa kutumia viungo vya mwili wake, kwahiyo viungo vyake vyote ni lazima viwe katika hali iliyo imara kwa ajili ya kazi.

b. Hata kama kwa uthibitisho wa kitaalamu wa madaktari mwajiriwa anazo akili nzuri kichwani mwake, akiwa na hitilafu katika viungo vingine vya mwili wake huathiri afya ya akili zake na uwezo wa utendaji wa akili zake.

c. Kazi ya Rais ni ngumu sana, kwa sababu ni pamoja na kusimamia shughuli zote za maendeleo ya nchi nzima, na matatizo yote yanayowatokea wananchi wote kila walipo, na kusimamia
utekelezaji wa majukumu yote ya watendaji wote katika Taifa, hivyo kwamba maamuzi sahihi yanatokana na afya bora yenye kuhakikisha uwezo unaopasa wa kiakili wakati wote

d. Hitilafu katika afya hudhoofisha uwezo wa kifikira na kusababisha maamuzi mabovu, ambayo huleta athari mbaya sana kwa Taifa. Na udhaifu huo huathiri mpaka maadili na hata uzalendo wa huyo kiongozi mdhaifu. Kwa mfano akipatikana Rais anayeishi kwa matumaini, kwa hofu ya kupoteza uhai kabla hajaweka sawa mambo yake na ya familia na jamii yake atatumikia maslahi yake
zaidi kuliko Taifa, tatizo hilo la afya likawa limelikosesha Taifa kipaumbele, na kuliangamiza kimaendeleo!

e. Wanaowania kugombea urais ni lazima wachunguzwe kwa makini sana afya zao, kwa sababu kukifanyika makosa akatawazwa mwenye hitilafu za kiafya, atakwenda kuwa mzigo mzito sana kwa
Taifa, hususan ugharamiaji wa utunzaji wa uhai wake ndani na nje ya nchi, kukosekana na umakini anaopasa kuwa nao kwa ajili ya dhamana kubwa aliyopewa n.k.

Kutokana na AFYA yake kuwa dhaifu sana hata kwa kumwona kwa macho tu, kabla ya uchunguzi wa kitaalamu ni kwamba Edward Lowasa hawezi kabisa kugombea Urais. Kwani amekosa sifa muhimu sana yaafya bora, ambayo ni ya lazima kwa mtu yeyote anayestahili kupewadhamana kubwa sana ya kuliongoza Taifa. Pengine hata kugombea urais kwenyewe anatafuta kutokana na hitilafu ya kiafya, iliyosababisha udhaifu katika kufanya maamuzi, hivyo amejikuta kwa bahati mbayaanagombea asichokiweza kabisa.

Ni lazima wagombea wote wa Urais, wa Ubunge na hata wa Udiwani wachunguzwe kwa makini afya zao kabla ya kupewa kugombea, na hata kuchunguzwa tena katikati ya muhula wa utumishi wao, kama kweli tunalithamini na kuliheshimu Taifa.

Sifa za urais ni wito au uhanga kwa ajili ya Nchi ambao ni zaidi ya maadili ya kizalendo, maono, vipawa na AFYA BORA. Ni dhana potofu sana kwamba sifa ya urais ni kushabikiwa na umati wa watu! Kwa sababu wengi hufuata mapesa na husombwa hata na magari ili umati wa kishabiki tu upatikane. Lakini kumpenda mtu huwa lazima kuwe na sababu, wakati ushabiki ni pepo mchafu au ‘psychological deficiency’.

Mchujo wa majina CCM: Kikao hakitoi sababu wala hakuna kukata rufaa - Nape


Mhasibu wa Kampuni ya Serikali atangaza kuwania jimbo la Waziri Mkuu, Mlele

 Shafi Mpenda
 Shafi Mpenda

MHASIBU wa Kampuni ya Serikali (TSN) inayochapia magazeti ya Daily News, Habari Leo, Habari Leo Jumapili na Spoti Leo, Shafi Mpenda (36) ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge katika Jimbo la Mlele mkoani Katavi kupitia CCM katika uchanguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2015.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye anashikilia Jimbo hilo la Mlele ameshatangaza rasmi kuwa hatagombea tena .

“Nikiwa mzawa wa jimbo hili, nilitafakari kwa makini sana, na kujiuliza maswali mengi sana...

Hatimaye nimepata majibu kwamba baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu kwenye taasisi yaSserikali, wakati umefika wa kurudi nyumbani na kuwa karibu zaidi na wananchi wenzangu wa jimbo hili ili niweze kuwatumikia na kutoa mchango wangu katika maendeleo ya jimbo letu na mkoa wa Katavi kwa ujumla wake.

Nawaomba wananchi wenzangu waniamini kwamba Kazi hii naiweza, naimudu, nimejipima na nimeona natosha katika kuwa sauti kwa wale wasio na sauti... Baada ya kuangalia changamoto tulizonazo, najua wapi tunataka kwenda ikizingatiwa kwamba Katavi bado tupo nyuma sana kimaendeleo” alieleza .

Akifafanua anaongeza kuwa Mbunge wa Jimbo hilo Pinda ambae pia ni Waziri Mkuu amefanya mambo makubwa sana ya kuanzishwa kwa mkoa mpya wa Katavi na wilaya mpya ya Mlele.

“Kwa maana nyingine ni kwamba, serikali sasa imesogea karibu na wananchi kwa ajili ya kuwahudumia vizuri zaidi…. Aidha, mzee Pinda ametoa mchango mkubwa katika kuendeleza sekta ya elimu, na sekta hii ni miongoni mwa mambo ambayo nakusudia kuyapa kipaumbele iwapo wana CCM wenzangu watanichagua kwenye kura ya maoni na kunipa ridhaa ili niweze kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba, 2015” alibainisha

Alitaja meneo mengine ya kipaumbele kuwa ni pamoja na kilimo ambacho kinajumuisha bei ya mazao ya biashara kwa mfano tumbaku,

“Kero zinazowakabili watu wa katavi ni nyingi na zinahitaji mtu imara kama Mzee pinda mwenye uwezo mkubwa wa kubuni miradi mbalimbali itakayoweza kuharakisha maendeleo ya katavi. Miongoni mwa kero kubwa ni pamoja na migogoro kati ya wakulima na wafugaji, Mawasiliano ya simu, barabara na Reli, maji, afya pamoja na elimu” alieleza

Aliongeza kuwa anachokiona yeye (Mpenda) ni fursa nyingi za kuleta mabadiliko katika mkoa wa Katavi ambazo zinahitaji mtu makini, mbunifu, mwenye uwezo mkubwa wa kushughulikia mabadiliko kwa kasi na kwa vitendo, aliye tayari kutumwa na akatumika, msikivu na mwenye hofu ya mungu, mwenye upendo na aliyekulia katika kupenda maendeleo.

Wengine ambao wamejitokeza kutaka kurithi mikoba ya Waziri Mkuu Pinda ni pamoja Kamwele Isaac Kilinda ambaye ni Meneja wa Tanroads mkoa wa Katavi, Lephy Gembe ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kilombero, Emmanuel Nzumba ambaye ni Mfanyakazi wa Tanapa-Simiyu.

Kadhalika wengine ni pamoja na , Maganga Kampala ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu (NEC) CCM, Richard Mbogo ambaye ni Kamanda wa Vijana CCM wilaya ya Mlele, Oscar Albano ambaye ni Mtaalamu wa kilimo, Pudenciana Kikwembe ambaye ni Mbunge wa viti maalumu jimbo la katavi.

Taarifa ya Nape: Ratiba na shughuli za Mikutano ya CCM Dodoma kuanzia leo


Leo tarehe 7 mwezi wa saba tunaanza vikao vya mchakato wa mkutano mkuu wa taifa wa Chama Cha Mapinduzi ambao unnategemewa pamoja na mambo mengine utapitisha ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 - 2020 lakini pia utateua mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, na pia kutakuwa na Kikao cha Halmashauri Kuu ambacho kitateua jina la mgombea wa urais kwa CCM kwa upande wa Zanzibar. Ratiba ya vikao, leo tarehe 7 kuanzia saa tano tutakuwa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ambacho kitaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana. Sekretarieti hiyo ina agenda moja kubwa kwa kupitia maandalizi ya Mkutano Mkuu na kuthibitisha. Yapo mambo mengi katika maandalizi kuna mambo ya ratiba, mambo ya malazi ya wajumbe, kuna mambo ya makabrasha mbalimbali na maandalizi ya documents mbalimbali zitakazotumika kwenye vikao vitakavyoendelea baada ya leo.

Kesho tarehe 8 kunategemewa kufanyika kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili cha chama, ambacho kitakuwa chini ya mwenyekiti wa Taifa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.

Tarehe 9 kichama kutakuwa na shughuli kuu mbili ya kwanza asubuhi, kutafanyika uzinduzi au ufunguzi wa ukumbi mpya wa CCM na ofisi zake ambao upo njia ya kwenda chuo kikuu cha Dodoma bila shaka baadhi yenu mtakuwa mmeona, Mwenyekiti wa chama, Rais Kikwete alipokwenda kutembelea kw ahiyo ufunguzi wake utafanyika tarehe 9, majira ya asubuhi kabla Mheshimiwa Rais hajaenda kuvunja Bunge, kama ratiba itabadilika tutawaambia lakini tarehe 9 tuna hiyo shughuli ya kwanza baadaye mchana kutakuwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM ambayo nayo ni muendelezo wa vikao vya awali kuelekea Mkutano Mkuu.

Tarehe 10 tunategemea kuwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ambacho kikao hiki kitafanya mambo makubwa matatu. Kwanza kitateuwa jina la mgombea Urais kwa upande wa Tanzania Zanzibar, halmashauri kuu ya taifa kwa mujibu wa katiba ndio inayoteua jina la mgombea urais wa Zanzibar kwahiyo hiyo itakuwa ni kazi mojawapo itakayofanywa na Halmashauri kuu ya Taifa na kazi ya pili, watapitia pia ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ambayo ndiyo itakayotumika kuombea kura na ndio itakayotumika kwa kipindi cha 2015 - 2020, na kutoka kwao hiyo ilani itapelekwa katika mkutano mkuu kwaajili ya kuhitimishwa.

Kazi ya tatu, halmashauri kuu hii itapokea majina matano kutoka kamati kuu ambayo yatakuwa yameteuliwa na kamati kuu, tarehe 9 na hapo watafanya kazi ya kupiga kura kupata majina matatu ya wanachama wa CCM walioomba kupitishwa na CCM kuwa wagombea wa nafasi ya urais kwa upande wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Majina matano haya yatapigiwa kura kupata matatu na tarehe 11 ndio siku ya mkutano mkuu wa Taifa wa chama cha mapinduzi ambao una kazi kubwa mbili, moja ni kupitisha hiyo ilani ambayo itakuwa imepitishwa na halmashauri kuu ya Taifa na maandalizi ya ilani hiyo yamekamilika, tuliunda timu kama mnakumbuka tumewahi kuitangaza ipo chini ya Wasira imefanya kazi nzuri ya kutengeneza ilani nadhani safari hii tutakuwa na ilani nzuri sana ambayo itaendeleza mafanikio yaliyopatikana katika awamu zote zilizopita lakini pia itatupeleka sasa kwenye hatua kubwa zaidi ya maendeleo ya nchi yetu.

Kazi ya pili, ni kupiga kura katika majina matatu yatakayowasilishwa katika mkutano mkuu ili kupata jina moja la mwanachama wa CCM ambaye ndiye atakuwa mgombea wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha mapinduzi, hivyo tarehe 11, itakuwa ni siku ya mkutano mkuu na mkutano mkuu huu utakuwa wa siku moja,lakini mkutano mkuu huu utaoneshwa moja kwa moja kupitia vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini, tv zote zitaonesha kuanzia ufunguzi ratiba ile mpaka wakati fulani halafu baadaye wakati wa matokeo na ufungaji wa mkutano karibia masaa sita au saba hivi tutauonesha moja kwa moja.

Ninachotaka tu ni kuwathibitishia watanzania tumejipanga vizuri chama chetu tupo wamoja tunaamini tutamaliza vikao hivi salama, na tutatoka tukiwa na ushindi, tutatoka tukiwa na nguvu, tutatoka tukiwa wamoja na bila shaka vikao hivi vitajenga msingi wa kushinda uchaguzi kwa kishindo sana mwaka huu.

Nataka pia nichukue nafasi hii kuwathibitishia wajumbe wa vikao vyote kuwa maandalizi yao yamekamilika na tunawatakia safari njema kutoka wanapotoka katika nchi yetu, tunawatakia afya njema na vikao vyema vya kamati ya maandalizi na tunawakaribisha sana Dodoma karibuni tukijenge chama chetu na demokrasia ya nchi yetu tuendelee kuimarisha demokrasia ya nchi yetu.
Nape Nnauye 
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM,

Taarifa iliyotolewa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti mjini Dodoma.


Taarifa ya Habari ya siku Channel TEN Julai 6, 2015
Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Saba, Saba 2015

Ndicho wanachosubiri UKAWA?