Katuni zilizochorwa kuhusu hali za wawania Urais kupitia CCM


kisha....

Utunzi wa Daniel "Danny" Mzena
Utunzi wa Daniel "Danni" Mzena

halafu...

Utunzi wa Daniel "Danny" Mzena
Utunzi wa Daniel "Danni" Mzena

Tanzania's economic performance weakens due to delays in donor support

The International Monetary Fund (IMF) says Tanzania’s macroeconomic performance remains strong with favourable medium-term prospects. The country has however seen a recent weakening in its economy due to delays in donor support.

The IMF through its Policy Support Instrument (PSI) supports the East Africa nation's medium-term objectives.

Some of the objectives include maintenance of macroeconomic stability, the preservation of debt sustainability, and the promotion of more inclusive growth and job creation.

IMF’s Min Zhu, deputy managing director and acting chair, said performance under the PSI was satisfactory through December 2014, but weakened in early 2015 due to a range of factors, including delays in mobilising external financing and donor support.

“Against this backdrop, the authority’s corrective measures aimed at achieving the 2014/15 budget deficit target are commendable, though earlier expenditure ceiling adjustments could have helped preserve development spending,” said Zhu.

The Fund said the fiscal target also puts Tanzania on a path to a 3-per cent deficit over the medium term, which is consistent with maintaining a low risk of debt distress.

“The authorities’ plan to address verified domestic supplier arrears transparently through the budget are welcome. Commitment controls on expenditures and related sanctions for breaching rules need to be strengthened to ensure new arrears do not accumulate. The strategy to address arrears to pension funds needs to be finalised quickly to allow for clearance of these arrears in 2015/16,” read the IMF statement.

“The current monetary policy stance is appropriate, delivering high growth and low and stable inflation. The use of foreign exchange intervention should be restricted to smoothing volatility in the foreign exchange market, with higher reliance on domestic-currency instruments to address excess liquidity situations.”

Vigezo vya uteuzi wagombea kupitia CHADEMA

Kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya CHADEMA

SIKU chache baada ya zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kugombea nafasi za ubunge na udiwani kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kukamilika katika majimbo yasiyo na wabunge sasa chama hicho kimetoa waraka mzito kuhusu namna ya kusimamia kikamilifu hatua zinazofuata kwa mujibu wa ‘katiba na kanuni za chama.’

Waraka huo namba tatu (3) wenye kumbukumbu namba C/HQ/ADM/CIR/15/48, umetolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbroad Slaa, ukiwataka watendaji wote wa Chama kujitenga na rushwa na kujiepusha na matumizi mabaya ya madaraka wakati wote wa mchakato wa “kura ya maoni” katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Vigezo vya kuwapata wagombea Ubunge Jimbo katika Chadema

Dk Slaa amevitaja vigezo muhimu vitakavyotumiwa na Chadema kuwapata wagombea katika ngazi za ubunge na udiwani.

“Licha ya wagombea kuwa na sifa zinazotakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi, Chama kitazingatia sifa” ambazo zimeainishwa katika Kanuni za Chama,” alifafanua Dk Slaa.

Kwa mujibu wa waraka huo, “sifa za kuzingatiwa katika kuteua wagombea katika uongozi wa Chama na Uwakilishi katika Vyombo vya Utawala” zimeainishwa katika Kanuni za Chama katika kifungu cha 7.6.

Dk. Slaa alizitaja sifa hizo kuwa ni pamoja na: uzoefu katika uongozi wa kisiasa ndani ya chama; mahusiano mazuri na viongozi wengine ndani ya chama; uadilifu katika uongozi wa nyuma kisiasa na kijamii; uwezo wa kutekeleza majukumu ya ngazi inayoombwa; uwezo wa kushirikisha na kushirikiana na watu wengine katika kutekeleza majukumu husika; ufahamu wa madhumuni, itikadi na falsafa ya Chama; uanachama hai katika msingi au tawi la chama katika eneo anamoishi au anakotoka mgombea; na ujuzi wa kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza.

“Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa wagombea wetu wanatimiza sifa hizo na nyinginezo kwa mujibu wa sheria za nchi zinazosimamia uchaguzi wa Rais, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani,” alisisitiza Dk Slaa.

Kwa upande wa wagombea ubunge, sifa “nyinginezo kwa mujibu wa sheria za nchi,” zinazoongelwa na Dk Slaa, zimetajwa katika ibara ya 67 ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977.

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania (1977) ibara za 67(1) (a), 67(1) (b) na 67(2)(b), mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo ni raia wa Tanzania, ametimiza umri wa miaka ishirini na moja, anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza, ni mwanachama wa chama cha siasa,ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa, na anazo akili timamu.

Aidha, kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania (1977) ibara ya 67(1)(c), mtu atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge ikiwa, katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi hajawahi kutiwa hatiani katika mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali.

Aidha, kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania (1977) ibara ya 67(2)(c), mtu atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge ikiwa mtu huyo hajawahi kuhukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.

Vile vile, kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania (1977) ibara ya 67(2)(d), mtu atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge ikiwa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya Uchaguzi Mkuu mtu huyo hajapata kuhukumiwa na kupewa adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Kuhusu wagombea wa Viti Maalum vya Ubunge na Udiwani, Dk Slaa alibainisha kuwa Baraza la wanawake Chadema (Bawacha) imeongeza sifa za vigezo vya ziada vyenye lengo la kuwapata wagombea wanaokubalika katika jamii.”

Vigezo vya kuwapata wagombea Ubunge Viti Maalum katika Chadema

Kwa mujibu wa Katibu wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) Taifa, Grace Tendega, kuna vigezo vya ziada vitano vilivyopitishwa rasmi na baraza hilo.

Kigezo cha kwanza ni kiwango cha uwajibikaji wa mgombea katika utekelezaji wa majukumu ya uanachama kupitia baraza la wanawake. Kiwango hiki kitatamkwa katika “fomu za siri” zitakazo jazwa na viongozi wa Chama katika ngazi za Wilaya, Mkoa, Kanda na ya Kitaifa.

Kigezo cha pili ni umri wa mgombea ndani ya chama, ambapo mgawanyo wa pointi utakuwa kama ifuatavyo: umri wa mwaka 1 hadi 5 pointi 2, umri wa miaka 5 hadi 10 pointi 4, umri wa miaka 10 hadi 15 pointi 6, umri wa miaka 15 hadi 20 pointi 8, na umri wa miaka 20 hadi 25 pointi 10.

Kigezo cha tatu ni ngazi ya uongozi alio nao mgombea ndani ya chama, ambapo mgawanyo wa pointi utakuwa kama ifuatavyo: ngazi ya msingi au tawi pointi 2, ngazi ya kata pointi 4, ngazi ya wilaya au jimbo pointi 6, ngazi ya mkoa pointi 8, na ngazi ya taifa pointi 10.

Kigezo cha nne ni kiwango cha elimu ya mgombea, ambapo mgawanyo wa pointi utakuwa kama ifuatavyo: elimu ya darasa la saba pointi 2, elimu ya cheti pointi 4, elimu ya diploma pointi 6, elimu ya shahada ya kwanza pointi 8, na elimu ya uzamili au uzamivu pointi 10.

Na kigezo cha tano ni uzoefu wa uongozi katika taasisi mbalimbali, ambapo mgawanyo wa pointi utakuwa kama ifuatavyo: uongozi katika ngazi ya kijiji au mtaa pointi 2, uongozi katika ngazi ya kata au shehiya pointi 4, uongozi katika ngazi ya wilaya pointi 6, uongozi katika ngazi ya mkoa pointi 8, na uongozi katika ngazi ya kitaifa pointi 10.

Tendega aliliambia gazeti hili kuwa, vigezo hivi vilipitishwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bawacha Taifa kilichofanyika mjini Dodoma mnamo 06-07 Februari 2015.

Kwa mujibu wa Tendega, kikao hicho kiliamua kwamba, mwanachama wa Chadema atakuwa amepoteza fursa ya kuwa mgombea wa Ubunge Viti Maalum ikiwa anayo sifa yoyote kati ya sifa zifuatazo: amekuwa na mahusiano mabaya na viongozi, wanachama na jamii; amekuwa mkwepaji wa majukumu na wajibu wake kwa chama, baraza la wanawake na jamii; au amekuwa na mwenendo wa kutiliwa mashaka katika uaminifu wake kwa chama.

Pia, mwanachama wa Chadema atakuwa amepoteza fursa ya kuwa mgombea wa Ubunge Viti Maalum ikiwa amekuwa msaliti, mpika majungu na dhihaka kwa viongozi; amekuwa akishiriki siasa za makundi, majungu, fitina na ubaguzi dhidi ya jamii, viongozi na wanachama wenzake; au amekuwa akitoa au kupokea rushwa.

Marufuku dhidi ya rushwa

Mbali na kutaja vigezo vya uteuzi wa wagombea katika nafasi mbalimbali, waraka wa Dk Slaa umepiga marufuku “vitendo ambavyo vinakiuka Katiba na Kanuni za Chama wakati huu wa kuelekea kwenye zoezi la kura ya maoni.”

Dk Slaa amevitaja vitendo hivyo kuwa ni pamoja na “rushwa, matumizi mabaya ya madaraka, makundi na upendeleo kwa baadhi ya wagombea, vitendo ambavyo vinafanywa na baadhi ya viongozi na wagombea wa nafasi mbalimbali za ubunge na udiwani.”

Vitendo hivyo ni pamoja na “kutoa fedha, vyakula, vinywaji, kusafirisha wajumbe kwa lengo la kuwahonga, kutoa au kushinikiza rushwa ya ngono, kutumia mamlaka ya kiongozi kupendelea upande mmojawapo na kuitisha vikao ambavyo sio halali kwa lengo la kukutana na wapiga kura.”

Hivyo, Dk Slaa amewataka viongozi wa chama, wanachama na wagombea wote kuusoma tena na kuzingatia kwa ukamilifu “Mwongozo wa Chama dhidi ya Rushwa toleo la mwaka 2012″ katika wakati huu tunapoelekea kwenye zoezi la kura ya maoni ndani ya Chama.

Marufuku dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka

Matumizi mabaya ya madaraka ndani ya Chadema ni jambo jingine lililopigwa marufuku kupitia waraka huu. “Ni kosa kwa mujibu wa katiba yetu kwa kiongozi kutumia madaraka yake kwa lengo la kujinufaisha yeye binafsi kinyume na kanuni na taratibu za Chama, ” alisema Dk Slaa.

Kwa mujibu wa Dk Slaa, wapo viongozi wa chama “ambao wanatumia hata vitendo vya ukabila, udini na ukanda katika kuwapendelea baadhi ya wagombea.” Lakini pia, alisema kuwa wapo viongozi wanaofanya “vitendo vya kuwachafua wagombea wengine kinyume kabisa na mwongozo wa kutangaza kusudio la kuwania nafasi za uongozi kwenye Chama, Mabaraza na Serikali vifungu vya 1(d), 1 (e) na 1 (f).”

Dk Slaa amekemea vikali tabia hii mbovu akitishia kuwachukulia hatua wote watakaothibitika kutumia vibaya madaraka yao.

Butiku auliza: "mmeshaamua, Dodoma mnakwenda kufanya nini?"

Watanzania wametakiwa kuhakisha kuwa katika kipindi hiki ambacho taifa linafanya Uchaguzi Mkuu wanahakikisha kuwa hawawachagui viongozi ambao wana aina yoyote ya doa la rushwa na wenye uchu wa madaraka kwani kwa kufanya hivyo kuna uwezekano mkubwa wa nchi kuingia katika machafuko makubwa kwani watu hao watakapoingia madarakani wataendesha nchi kwa manufaa ya kikundi kidogo cha mafisadi ambacho kitakuwa kikiwazunguka.


Nape aelezea kutokufanyika kikao cha CCM


Wananchi walinganisha ukumbi wa CCM na "St Kayumba"

Picha via WhatsApp

Mnada wa hadhara wa vifaa vya Ubalozi wa Marekani


UBALOZI WA MAREKANI

DAR ES SALAAM 

MNADA WA HADHARA:

UNIVERSAL AUCTION CENTRE Kwa idhini waliyopewa na Ubalozi wa Marekani watauza kwa mnada wa hadhara gari, generator, fanicha za ofisi na nyumbani, makontena na mashine za gym tarehe 11 Julai, 2015 Jumamosi saa 3:00 asubuhi. Mnada utafanyika Golden Resort Sinza, Lion Street.

MALI ZITAKAZOUZWA: sofa sets, chest drawer, recliner, dressers, coffee table, book shelve, meza za ofisi/viti, dining table/chairs, carpet, hoover, vitanda, magodoro, fridges, freezer, cookers, TV set, washer, dryer, computer set, photocopy m/c, A/c split units, portable toilets, Gym equipments:Stairmaster Eliptical, Comber, Kettler Butterfly,Treadmill, na vingine vingi

Gari, Genereta & Makontena yatakayouzwa:

Idadi
Aina
Model
Mwaka
Ushuru
1
Ford Everest  S/ Wagon
WL  Diesel Engine
2007
Bado
2
Generator
60 & 81 KVA  Silent

Bado
   3
Empty Container
40 & 20 Fts
2012, 2011,1995
Bado

Mali zote zinaweza kukaguliwa Golden Resort Sinza, Lion Street tarehe 9 na 10 Julai, 2015 kuanzia saa 4.00. asubuhi mpaka saa 10.00 jioni.

MASHARTI YA MNADA:
Mnunuzi wa furniture na genereta atatakiwa kulipa malipo yote kwa keshia (cashier). Na mnunuzi wa gari atatakiwa kulipa 25% pale pale na salio lilipwe ndani ya siku 5 za kazi, ukishindwa kulipa kwa muda huo gari litauzwa kwa mshindi mwingine aliyefwata na dhamana haitarudishwa.

Mali zote zitauzwa kama zilivyo bila dhamana.

Mnunuzi atawajibika kulipa ushuru na kodi zingine zote.

Mali yote iliyouzwa itatakiwa kuondolewa baada ya kulipa malipo yote pamoja na kodi .

Kwa maelezo zaidi waone:
UNIVERSAL AUCTION CENTRE
NKRUMAH STREET, MKABALA NA CO-CABS
SIMU NA: 0754-284 926, 0757 284 926 
Email : [email protected]
DAR ES SALAAMVituo vya runinga vilivyoadhibiwa na TCRA na kutozwa faini

Vituo vya runinga vya TBC1, Channel TEN na StarTv vimepewa onyo na kuadhibiwa kwa kutakiwa kulipa faini kwa makosa waliyokiri.

Video ya Mwananchi hapo chini ina maelezo zaidi.Maneno mapya matatu ya Kiswahili niliyojifunza leo: Msadi, Kitamizi, Makavazi

Lugha yoyote iliyo hai hukua kwa kuongezeka maneno na msamiati.

Leo katika jukwaa la Wanazuoni nimejifunza taafsiri ya Kiingereza - Kiswahili kwa maneno haya matatu:
  • ...hivi majuzi nilikuwa kwenye warsha nikasikia mshiriki mmoja akitumia neno 'Msadi' kama Kiswahili cha 'Consultant'. Mimi pia nilikuwa natumia 'Mtaalamu Mshauri'. Kiswahili kinakua kila siku. Sina uhakika kama hilo la 'Msadi' limepitishwa. TUKI wanatumia neno 'Mshauri' au 'Mwelekezi' lakini tafsiri hiyo imo katika juzuu (version) ya Kamusi yao ya zamani. [BJ]
  • nimekutana na maneno ya kiswahili kama hayo kwenye maonyesho ya sabasaba 2015. Moja ni kitamizi (incubator) kwa wale jamaa wa VETA, wana vijana wa utindio wa ubongo, lakini wako kwenye kitamizi, wakitengeza bidhaa mbalimbali za kuvutia, samahani sikupiga picha. Kukata kona, nikakuta banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salam, nikamkuta Mtalaam Ndugu, Lenard Bakize. Nikawa namuuliza kama naweza kupata vitabu vya Kiswahili, nilichosoma darasa la kwanza.. huyu ni Juma, Juma ana dada. Dada yake Juma ni Roza. Akaniambia niangalie kwenye makavazi yao. (archives) Yaani huyu mtalaam alikuwa anatumia kiswahili tupu bila kuchanganya kiengereza. [LR]
Taarifa ya michango ya mawazo kuhusu maneno haya mageni kwa baadhi yetu...
Wanazuoni,
Istilahi ya consultancy iliyokita mizizi hadi sasa ipo nayo ni ujasiriamali. Kwa hivyo consultant ni mjasiriamali.
Katika incubator- vitabu vilivyochapishwa na makamusi ya kuanzia mwaka jana yanalo neno- kitotoa na kiangulio- hata kamusi ya Kiswahili-Kiingereza toleo la majuzi zaidi la TATAKI-UDSM na makamusi mengineyo hapa Nairobi.
Kuna pia hili la green-house kuwa na kivungulio . Nalo limekita na kuna vitabu vya bunilizi vimeanza kulibugia tayari. [GH]
Mchango wa Bw. Aldin kwa mchangiaji CH hapo juu
Bwana H
Ninadhani dhana ya ujasiriamali ni muhimu ifafanuliwe.
Dhana hiyo inalenga shughuli inayozalisha zaidi ya kile mtu alichokuwa nacho awali. Ni tafsiri ya entrepreneurship. Inahusu biashara, au uanzishwaji wa kampuni. Mtaji mdogo unazalisha na kupata zaidi. Ndipo humo inapoibukia dhana ya "mali". Katika neno ujasiriamali.
Lakini hii ni tofauti na Consultant: mtu anayefanya kazi (sio lazima biashara, au mali).
Hivyo, neno (au istilahi) Msadi, ni dhana ambayo mimi binafsi ningeliimakinikia kwa umakini na kuikubali kuwa ina mashiko.
Pili, kuhusu "makavazi"
Istilahi hii imekuwa ikitumika tangu zamani na TUKI. Wale waliotembelea jengo la Kiswahili hapa Chuo Kikuu cha Dar, wanalijua jina hilo kuwa lina zaidi ya miaka 10. Jina la "kavazi" lilibuniwa kutoka Makavazi ili kuleta upekee wa Kituo cha Nyerere. Kufupisha kutoka MAkavazi na kuwa KAVAZI kulimaanisha ule umahususi wa Kituo hicho cha Nyaraka. Kwa hiyo, kimsingi maneno yote mawili: MAkavazi na Kavazi, yana maana moja ya msingi yakimaanisha archive. Kavazi lina kuwa mahususi, (particular) na Makavazi ni ya jumla.
Aldin
Lakini bwana Chambi alikuwa na swali

Mwalimu Aldin, ujasili-amali au ujasilia-mali i.e. maana imejikita kwenye neni amali au mali?

[video] Kingunge: Kama Nape hajui historia ya rufaa za wagombea, aulize


Kada mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi mzee Kingunge Ngombale Mwiru amekihadharisha chama hicho kuhusiana na matamko ya kutatanisha ambayo yametolewa hivi karibuni kuwa CCM haihitajali shinikizo la mtu, kikundi ama watu na kwamba kutokana na muda kutokutosha, hakuna mgombea atakayeruhusiwa kukata rufaa kutoka vikao vya chini kwenda juu.

Mahojiano kwa kina (dakika 20) yapo katika video ifuatayoKanusho la CCM kuhusu akaunti ya Facebook yenye jina la Nape


Kitengo cha Mawasiliano na Umma katika Idara ya Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi, kinapenda kuujulisha uuma kwamba Akaunti yenye maneno hayo hayo hapo juu siyo ya Katibu wa NEC, Itikadi na Unezi, Nape Nnauye, bali akaunti hiyo imetengenezwa na watu ambao tunaweza kuwaita kuwa ni wahuni kwa lengo la kutaka kukata kiu ya wanachohitaji.

Mtakaoisoma taarifa hiyo eleweni kuwa si maneno ya Nape. 

Tabia hiyo siyo ya kiungwana na ya kimaadili katika matumizi ya mitandao ya kijamii. Ni vyema wanaopenda tabia hii waiache kwa manufaa ya Tanzania.

Wazanzibari wakusanya ushahidi wa kumshitaki Dk Shein huko ICC


KUNA nyakati ambapo watawala wetu lazima waambiwe ukweli. Huu ni wakati mmojawao. Na wa kuwaambia ukweli ni sisi wenyewe. Haitokuwa mara ya kwanza katika historia kwa umma kuwaambia ukweli watawala wao. Wala sisi hatutokuwa wa mwisho kuwaambia ukweli watawala.

Kila pale watawala wanapopandwa na kiburi cha kuamini kwamba wao ndio wenye uwezo wa kuamua nini kiwe na nini kisiwe, nani awe na sauti ya kusema na nani asiwe na sauti inatupasa tusimame pamoja tuwaambie ukweli wasiotaka kuusikia.
Ukweli wenyewe ni rahisi kuufahamu kama wana masikio yenye kusikia. Ni rahisi zaidi kuuelewa kama wana akili na wanaweza kufikiri.

Ukweli wa mwanzo wanaohitaji kuambiwa ni kuwa udhalimu haudumu daima dawamu. Ukweli wa pili wanaolazimika kuambiwa ni kwamba ijapokuwa wanajidai kuwa wao ni wababe wa kisiasa kwa sababu vyombo vya dola vimo mikononi mwao, kwa hakika ya mambo hawana ubabe unaoweza kuushinda ubabe wa nguvu za umma.

Vitendo vya mashambulizi ya kisiasa ya hivi karibuni yanayozidi kuihatarisha hali ya utulivu na amani visiwani Zanzibar, ni vitendo watavyokuja kuvijutia wenyewe.
Vitendo hivyo ni nyongeza nyingine katika kumbukumbu ya msururu wa unyama wa kisiasa unaofanywa visiwani humo.

Mashambulizi hayo yamekwishaipaka matope Zanzibar, yanawaaibisha viongozi wa serikali ya huko pamoja na wa Serikali ya Muungano. Pamoja na yote, mashambulizi hayo yanathibitisha kukosekana utawala bora na udhaifu wa demokrasia nchini Tanzania.

Katika hali hizi, ni taabu kuamini kwamba uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 utafanywa kwa njia za kistaarabu au kwamba utakuwa na uhalali unaostahiki uwe nao, licha ya kuwa huo utakuwa uchaguzi wa sita nchini tangu urejeshwe mfumo wa siasa za vyama vingi.
Watawala wetu hawawezi kujiweka mbali na yanayotokea sasa wala hawawezi kusema kwamba hawakuyatarajia.

Walikwishaonywa mara kadha wa kadha kwamba kuna njama za kuirejesha Zanzibar pabaya. Ishara zikionekana alfajiri na mapema..

Zilianzia kwa uhuni wa kisiasa kwa njia ya matusi ya nguoni dhidi ya wapinzani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Waliokuwa wakitukana wakiwa juu ya majukwaa ya CCM walikuwa baadhi ya viongozi wa chama hicho.

Wengine wakiandika na kusambaza vipeperushi vya matusi dhidi ya hata kiongozi mwenzao, Rais mstaafu Amani Abeid Karume.

Wakati hayo yakiendelea, kuna viongozi wengine wa CCM walikuwa wakisema wazi kwamba watatumia nguvu kuzuia chama chao kisishindwe katika uchaguzi mkuu ujao wa Oktoba 25. Majina ya wachochezi wote hao yanajulikana na kanda za video zenye kuthibitisha shutuma dhidi yao zipo.

Kwa bahati mbaya, wakuu wa polisi wamenyamaza kimya na hawakuwachukulia hatua yoyote viongozi hao. Hawakuthubutu hata kutoa taarifa ya kuwaonya kuhusu vitimbi vyao. Wakuu wengine wa serikali, Bara na Zanzibar, nao pia wamekaa kimya.
Lililozidi kusikitisha ni kuwaona baadhi ya vigogo vya CCM kutoka Bara wakihutubia mikutano ya hadhara Zanzibar huku wakiushadidia uovu wa wahafidhina wa chama chao wa Visiwani.

Hadi sasa ni kiongozi mmoja tu wa taifa hili anayeonekana kufanya juhudi za kuwatahadharisha viongozi wa serikali na kuujulisha ulimwengu kuhusu njama ovu za baadhi ya viongozi wa CCM/Zanzibar zinazoweza kusababisha umwagaji wa damu. Naye ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.

Mfano mmoja wa jitihada zake ni mkutano aliokuwa nao na waandishi wa habari katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, Mei 10, mwaka huu. Kwenye mkutano huo, Hamad alizilaumu Tume za Uchaguzi nchini yaani Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuwa zinatumiwa na CCM dhidi ya wananchi.

Alieleza kwa ufasaha kuhusu njama zinazofanywa na taasisi mbalimbali za serikali, zikiwa pamoja na vikosi vya Ulinzi na Usalama, katika zoezi zima la uandikishaji wa watu katika Daftari la Kudumu la Wapigajikura.

Taksiri zilizojitokeza katika zoezi hilo ni taksiri zilizosababishwa kwa makusudi kuiridhisha CCM, alidai Hamad. Hamna shaka kwamba yanayojiri sasa ni matokeo ya hayo aliyokuwa akiyalalamikia Hamad.

Tangu zoezi hilo la uandikishaji wapigajikura lianze kumetokea rabsha na vurugu katika vituo kadhaa vya uandikishaji wapigakura kisiwani Unguja.

Isitoshe, kumetokea na mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari kwa lengo la kutaka kuwanyamazisha wasiuseme uovu unaotendwa na vyombo vya dola. Kwanza kulikuwako na taarifa za kutekwa nyara na kupigwa mwandishi habari wa kujitegemea aitwaye Ali Omar.

Waliompiga walikuwa wamejifunika nyuso zao ki-“Ninja” na walimshutumu kuwa alikwenda kutafuta habari kwenye kituo cha kujiandikisha wapigakura huku akiwa mwandishi habari wa Upinzani.

Siku mbili baadaye, Juni 29, 2015 ilikuwa nyongeza nyingine katika orodha ya tarehe za unyama wa kisiasa unaofanywa Zanzibar.

Siku hiyo, kwa mujibu wa mashuhuda, genge la watu wasiojulikana waliokuwa pia wamejifunika nyuso na wanaokisiwa kufikia 20 walivamia kituo cha redio binafsi iitwayo “Coconut FM,” iliyo katika eneo la Kilimani, Unguja Mjini.

Dhamira ya washambulizi hao ilikuwa ni “kumshughulikia” mwandishi habari wa redio hiyo aitwaye Ali Mohamed, aliyeandaa kipindi maalumu kilichojadili hali ya vitisho katika vituo vya kuwaandikisha wapigajikura.

Chama cha Wananchi (CUF) katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Ismail Jussa, Kaimu Mkurugenzi Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, kilidai kwamba hao “watu wasiojulikana” walikuwa ni watu “wanaosadikiwa” kuwa ni askari wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

Aidha, Jussa alidai kwamba watu hao walikuwa wakitumia magari yenye namba za vikosi vya polisi vya Zanzibar. Hizi ni shutuma nzito na hazistahili kupuuzwa hata kidogo.

Ikiwa shutuma hizo ni za kweli basi wahalifu katika kadhia hiyo si hao askari peke yao waliovaa “Ninja” wakiwa na silaha za namna kwa namna zikiwa pamoja na bunduki za rashasha, mapanga, marungu na msumeno.

Wanaowajibika katika kadhia hiyo ni pamoja na wakubwa wa hao askari polisi, waziri wao, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Wakuu wa polisi wananukuliwa wakikana kama wanahusika na mashambulizi hayo lakini inashangaza kwamba wao wala wakubwa zao serikalini hawakuyalaani mashambulizi hayo seuze kuwachukulia hatua za kuwatia nguvuni wahusika.

Vikosi hivyo vimekuwa vikionekana katika vituo vya uandikishaji wa wapigakura vikiwa na silaha na vikiwa vimejifunika nyuso. Wamewajeruhi watu kadhaa katika vituo mbalimbali vya uandikishaji wa wapigakura.

Ikiwa vikosi hivyo vya washambulizi hao si vikosi vya polisi ya Serikali ya Zanzibar, vilivyo chini ya Waziri Haji Omar Kheri, basi nani mwenye kuviratibu na kuviongoza vikosi hivyo? Nani mwenye kuvimiliki?

Haya ni maswali yanayohitaji kujibiwa na viongozi wa ngazi za juu kabisa wa serikali mbili.

Tunajua kwamba mitaani vimepewa jina la “Janjaweed” vikifananishwa na wanamgambo wa Janjaweed wanaodaiwa kutumiwa na Serikali ya Sudan kufanya mauaji na vitendo vingine vya ugandamizi dhidi ya raia wa kawaida katika eneo la Darfur, magharibi mwa Sudan, na pia mashariki mwa Chad.

Mashambulizi ya Janjaweed wa Darfur ndiyo yaliyosababisha Mahakama ya Kimataifa Jinai (ICC) kutoa waranti za kutaka akamatwe Rais wa Sudan, Hassan Ahmed al Bashir, waziri wake Ahmad Harun pamoja na Ali Kushayb, anayedaiwa kuwa mmoja wa viongozi wa Janjaweed.

Ugaidi ni ugaidi. Hauna hili wala lile. Lakini nadhani hakuna ugaidi ulio wa hatari zaidi ya ule unaotekelezwa na vyombo vya dola kwa niaba ya viongozi wasiostahiki kuongoza.

Hatari nyingine ni kwamba hivi vyombo vya dola vikishaota meno na kuanza kutafuna, baadaye vikishazoea huwa havichagui tena nani wa kumtafuna, huwa mpata, mpatae.

Hali iliyopo sasa Zanzibar ni hali ya kutisha na inaashiria hatari kubwa inayovikabili visiwa hivyo tunapoukaribia uchaguzi mkuu.

Toka lianze zoezi la uandikishaji wa wapigakura, watu kadhaa wamejeruhiwa na hivyo vikosi vya watu wenye silaha za kila aina, wasiovaa nguo rasmi za polisi lakini wenye kutumia magari ya polisi na wanaoziba nyuso zao wasionekane. Watu kadhaa wamejeruhiwa na vikosi hivyo Unguja Kaskazini, Wilaya ya Magharibi, Wilaya ya Mjini na Makunduchi, Mkoa wa Kusini.

Huko Makunduchi, watu watano walijeruhiwa, wawili kwa kupigwa risasi Julai 4, wakati wa uandikishaji wa wapigakura katika Daftari la Kudumu. Mmoja wa majeruhi ni mzee wa miaka 70, aliyepigwa kwa magongo na nondo. Hili ni tukio la karibuni kabisa wakati naandika makala haya.

Vurugu lilianza watu walipokusanyika kujadili namna wasivyofurahishwa na zoezi hilo lilivyokuwa likiendeshwa kwa vile walidai kwamba mamluki walikuwa wakiandikishwa katika Daftari hilo. Ndipo walipovamiwa na kundi la askari wasiovaa sare lakini waliojifunika vinyago usoni na waliokuwa na silaha za moto.

Kamanda wa Mkoa wa Kusini, Unguja, Juma Saadi, alisema kwamba polisi walipiga risasi hewani na hakujeruhiwa mtu. La kushangaza hapa ni kwamba majeruhi walipelekwa hospitali ambako madaktari walithibitisha kwamba baadhi ya majaraha yao yalisababishwa na kupigwa risasi.

Moja ya picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii za majeruhi hao zinaonyesha risasi iliyotolewa kutoka kwenye mwili wa majeruhi mmoja.

Angalau Kamanda Saadi amekiri kwamba washambulizi walikuwa askari polisi. Ya kuulizwa hapa ni kwanini askari hao wakawa wanafunika nyuso zao wasijulikane? Kwa nini wanakwenda kwenye vituo vya uandikishaji wapigakura wakiwa na silaha nzito? Kwa nini wanalazimisha watu fulani waandikishwe kwenye Daftari la Wapigakura na wengine wasiandikishwe?

Swali lililo muhimu zaidi ya yote ni: Nani aliyewapa amri ya kutenda wayatendayo?

Hakuna lolote linaloweza kuhalalisha unyama huu. Na ndio maana kuna Wazanzibari ambao tayari wamekwishaanza kukusanya ushahidi wa hotuba, picha na video za viongozi na wakuu wa serikali waliochochea mashambulizi hayo au wenye kuhusika nayo moja kwa moja.

Nia yao ni kuuwasilisha ushahidi huo mbele ya Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC), huko Hague.

Kwa hili, ni muhali kwa Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, na hata mwenzake wa Muungano, Jakaya Kikwete, kuliepuka kwa vile ndio wakuu wa juu kabisa wenye dhamana ya kusimamia amani nchini na kuyalinda maisha ya wananchi wao.

Matamshi ya mara kwa mara ya Shein kuwa atahakikisha amani inalindwa na kuwa hatomvumilia yeyote atayevuruga amani hayatamsaidia kitu endapo ataendelea kushindwa kutekeleza ahadi hiyo.

Imeandikwa na:
Ahmed Rajab 
8 Julai 2015

Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje kujenga jengo jipya

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Hassan Simba Yahya kulia na Mwakilishi wa Kampuni itakayojenga jengo la Wizara ya Mambo ya Nje wakiweka saini Makubaliano ya mchoro wa jengo hilo.
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, imeidhinisha michoro ya Jengo jipya la wizara hiyo, litakalojengwa jirani na Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Makubaliano kuhusu michoro hiyo ya jengo la ghorofa sita, litakalogharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, yametiwa saini jana baina ya wizara na mwakilishi wa mkandarasi wa ujenzi.

Akiongea baada ya kutia saini makubaliano hayo kwa niaba ya wizara, Naibu Katibu Mkuu, Balozi Hassan Simba Yahya, alisema hatua hiyo inatoa fursa kwa matayarisho ya ujenzi kuanza, na kuwa kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza kabla ya mwisho wa muhula wa Serikali ya Awamu ya Nne.
"Tumekamilisha hatua muhimu katika matayarisho ya ujenzi wa Jengo la Wizara," 
alisema, na kuongeza kuwa mradi huu ulianzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete.

Utiaji saini wa makubaliano ya michoro hiyo ulishuhudiwa na wawakilishi wa Wakala wa Majengo (TBA).

Balozi Yahya akibadilishana nyaraka za makubaliano ya michoro ya jengo la Wizara na Mwakilishi wa Kampuni itakayojenga jengo hilo.

via blog ya Wizara ya Mambo ya Nje

Greece situation forces Tanzania to delay loan; Its shilling is Africa’s worst-performing currency


Tanzania’s central bank shelved plans to raise $600 million through a private placement managed by Rand Merchant Bank of South Africa, citing fallout from the Greek debt crisis.

“We have postponed,” Joseph Masawe, head of economic research and policy at the Bank of Tanzania, said in a telephone interview from Dar es Salaam, Tanzania’s commercial capital, on Wednesday. “Because of the Greece default, conditions attached to the loan are going to be more stringent. We are waiting for when market conditions are better.”

Rand Merchant Bank referred questions to First National Bank Tanzania Ltd. Both are units of FirstRand Ltd., the Johannesburg-based lender. FNB Tanzania Chief Executive Officer Dave Aitken declined to comment, citing a non-disclosure agreement.

The central bank said last month it agreed to raise $800 million of loans from Rand Merchant and China Development Bank Corp. to bolster its foreign-exchange reserves and plug a budget deficit. The Tanzanian shilling weakened 22 percent against the dollar this year and is Africa’s worst-performing currency in that period, according to data compiled by Bloomberg.

The government received $200 million from China Development Bank, in addition to $100 million from the World Bank and $77 million from African Development Bank, Masawe said. The loans will be used to support the budget and boost foreign-currency reserves, he said.

Corruption Scandal

Tanzania is raising money for its budget after foreign donors, including the World Bank and the U.K., withheld $558 million of aid because of a corruption scandal in the energy ministry.

The budget deficit of East Africa’s largest economy after Kenya will widen to 4.2 percent of gross domestic product this year from 4 percent last year, Finance Minister Saada Mkuya said last month.

The central bank spent $410 million between January and May trying to stabilize the Tanzanian shilling, Masawe said. The currency strengthened 1.1 percent to 2,220.40 per dollar by 8:33 a.m. in Dar es Salaam on Thursday.

Mbunge (1995 - 2005) aaga dunia


Mwanasiasa mkongwe n aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM mwaka 1995 hadi 2005 Leonard Derefa amefariki dunia leo asubuhi kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu muda mfupi baada ya kutoka uwani kujisaidia.

Leonard Derefa (Mwanaderefa) alizaliwa mwaka 1942 katika kijiji cha Bulima wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na hadi umauti unamfika alikuwa anaishi katika mtaa wa Mbuyuni kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Mmoja wa watoto wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Newe Derefa amesema baba yake alifikwa na umauti leo asubuhi saa 12.30 muda mfupi baada ya kutoka uwani kujisaidia.

Newe amesema kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na mama yake, Thereza Derefa mara baada ya mumewe kutoka uwani aliingia chumbani na badala ya kurejea kitandani alipiga magoti pembezoni mwa kitandani na kuanza kusali huku akitoka jasho jingi mwilini kiasi cha kulowana na aliamua kumgusa na kumsemesha ili kujua kitu gani kilichokuwa kikimsumbua lakini hakujibu kitu.
"Nilimchukua na kumpeleka katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, madaktari walimpima ili kuelewa tatizo lakini walibaini tayari ameishafariki”,
amesema Newe.

Jina la Leonard Derefa siyo geni katika ulimwengu wa siasa nchini Tanzania ambapo kwa wafuatiliaji wa masuala ya siasa, hasa tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, watamkumbuka mwanasiasa huyo mkongwe kutokana na lafudhi yake ya Kisukuma iliyomfanya wakati mwingine apate ugumu kutamka baadhi ya maneno.

Tangu Tanzania ipate uhuru, Jimbo la Shinyanga Mjini limeongozwa na wabunge tisa ambao ni John Rupia, Bakari Msonde, Anna Tito Kachima, Ntemi Nyanda, Haninghton Mfaume, Paul Makune, Leonard Derefa, Dk Charles Mlingwa na sasa Stephen Masele.

[update] Hotuba ya Rais Kikwete katika maandishi akilihutubia Bunge kwa mara ya mwisho

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilihutubia Bunge la Tanzania na hatimae kulifunga. Kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anna Makinda. (Picha: Joseph Senga)

HOTUBA YA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WAKATI WA KUAGANA NA BUNGE NA KULIVUNJA BUNGE LA KUMI LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, UKUMBI WA BUNGE, DODOMA TAREHE 9 JULAI, 2015

Waandishi wa habari wachanga milioni 31 kuwasaidia wenzao

Mwenyekiti wa Kampeni iliyolenga kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari wanaougua magonjwa sugu yakiwepo ya saratani, (MEDIA CAR WASH FOR CANCER) , Benjamin Thompson akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kiasi cha fedha kilichopatikana katika harambee ya jijini Dar es Salaam ambapo kiasi cha shilingi Milioni 31 zilipatikan ikiwa ni ahadi na taslimu. Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi Kawawa. Harambee nyingine kama hiyo inataraji kufanyika Jijini Mwanza mwezi Agosti mwaka huu.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Dar es Salaam Julai 9, 2015

JUMLA ya shilingi milioni 31 zimepatikana katika harambee ya kuosha magari iliyofanywa na waandishi wa habari Julai 4, 2015 katika viwanja vya Leaders Club, Jijini Dar es Salaam. Kati ya fedha hizo, taslimu ni Milioni 12 na zingine ni ahadi.

Harambee hiyo inajulikana kwa jina la Media Car Wash for Cancer. Lengo la changizo hilo lilikuwa kupata Shilinngi Milioni 100, ili kuwahudumia waandishi wenye matatizo mbalimbali ya kiafya pamoja na kuwaingiza waandishi wa habari kwenye mfumo rasmi Bima ya Afya.

Kama tulivyotanzaga awali, wagonjwa ambao ni walengwa Adolf Simon Kivamo, Dastan Bahai na Athumani Hamisi.

Ili kutimiza lengo la changizo, Kamati ya Media Car Wash for Cancer inatarajia kuendelea na zoezi la kutafuta pesa mpaka kiwango hicho kitakapofanikiwa.

Mpaka sasa Kamati imeweza kuunda kamati ndogondogo zitakazosimamia zoezi la ufuatiliaji na ukusanyaji fedha kulingana na ahadi mbalimbali na wataifanya kazi hiyo kwa muda wa wiki moja.

Kisha, wajumbe wa kamati hii ambayo jumla yao ni 75 watatoa maamuzi wa mgao huo mara moja.

Kamati hizo pia zitafanya kazi ya kuwatambua idadi ya kamili ya waandishi wengine wanaosumbuliwa na magonjwa mbalimbali na hawana msaada unaoeleweka.

Aidha, hali kadhalika, kamati hiyo pia inafanya tathimini ili kujua idadi ya wanahabari ambao hawana Bima ya Afya ili utaratibu wa kuwaingiza kwenye mpango huo uandaliwe.

Katika awamu hii ya kwanza tunatarajia kuanza na wanahabari 50 ambao sio waajiriwa, lakini wanafanya kazi katika vyombo vya habari nchini yaani correspondents.

Uteuzi wa majina ya waandishi utakwenda kwa kufuatana, yaani kutoka na chombo kimoja hadi kingine.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Tanzania kwa waandishi wa Habari kuwa na mfuko huu ambao lengo lake ni kwasaidia katika masuala ya matibabu.

Kamati itaanza na waandishi wa habari walioko kwenye vyombo vya habari vya Jijini Dar es Salaam na baadaye kuendelea katika mikoa mingine nchini.

Aidha, Kamati ya Maandalizi ya Harambee hii imeitisha mkutano mkuu wa wadau wa habari nchini utakaofanyika alhamisi Julai 16, 2015 kwa ajili ya kuanzisha mchakato wa usajili wa chombo hiki muhimu.

Wahariri wenu watakujulisheni muda na mahali utakapofanyika mkutano huu.

Pia, kamati hii inakusudia kufanya harambee nyingine katikati ya mwezi Agosti mwaka huu, itakayofanyika Jijini Mwanza.
Hatua za awali za harambee hiyo kwa kushirikiana na wenzetu wa Jiji hilo zimeanza,ikiwa ni pamoja na kutafuta eneo la kufanyia shughuli hiyo pamoja na wadhamini mbalimbali.

Mwisho tungependa kutoa shukrani zetu za dhati kwa wadhamini na wadau wote walioshirikiana nasi katika harambee hii ambao ni BOT, TPB, NHIF, TANAPA, NSSF, JUBILEE INSURANCE, ANSAF, ASTE INSURANCE, MOIL,TAGCO,TEA, Wizara Ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Bw. Reginald Mengi, Mh.Hamis Kagasheki, Mh. Ridhiwani kikwete, Mh.Shabiby, Clouds FM, Radio Five,New Habari. The Guardian Ltd, pamoja na Wanakamati,

Benjamin Andongolile Thompson
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi
Media Campaign for Cancer Campaign


Mwenyekiti wa Kampeni iliyolenga kupata fedha kwa ajili ya kuwasaidia wanahabari wanaougua magonjwa sugu yakiwepo ya saratani, (MEDIA CAR WASH FOR CANCER) , Benjamin Thompson akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza kiasi cha fedha kilichopatikana katika harambee ya jijini Dar es Salaam leo, ambapo kiasi cha shilingi Milioni 31 zilipatikan ikiwa ni ahadi na taslimu. Pamoja nao ni Wajumbe wa Kamati hiyo Mkurugenzi Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi Kawawa (kulia) na Judicate Shoo.Harambee nyingine kama hiyo inataraji kufanyika Jijini Mwanza mwezi Agosti mwaka huu.


Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa katika mkutano huo hii leo. Kutoka kushoto ni Mroki Mroki, Leah Samike, Judicate Shoo, Mwenyekiti Benjamin Thomson, Zamaradi Kawawa, Angela Michael Msangi, Grace Nakson na Somoe Ng'itu. Harambee nyingine kama hiyo inataraji kufanyika Jijini Mwanza mwezi Agosti mwaka huu.

Picha za uzinduzi wa CCM "Dodoma Convention Center"


Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya viongozi alipowasili kwenye uzinduzi wa ukumbi mpya wa CCM ambao ni wa kisasa uliopo nje kidogo ya mji wa Dodoma, leo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiongoza sherehe fupi za uzinduzi wa jengo jipya la mikutano la CCM mjini DodomaMkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya CRJE Ndugu Hu Bo akihutubia kwenye sherehe za uzinduzi wa Jengo la kisasa la mikutano la CCM mjini Dodoma.Viongozi wakifurahia hotuba ya Mkurugenzi wa CRJE


Balozi wa China Nchi Mhe. LU Youqing akizungumza wakazi wa uzinduzi wa Jengo jipya la Ukumbi wa mikutano la CCM mjini Dodoma.


Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa sherehe fupi za uzinduzi wa jengo la ukumbi wa kisasa wa mikutano wa CCM mjini Dodoma.


Bendera za CCM zikipepea nje ya ukumbi wa jengo jipya la kisasa la mikutano Dodoma Convention Center.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa salaam za kumkaribisha Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuja kutoa hotuba ya ufunguzi wa Ukumbi mpya wa kisasa wa mikutano wa CCM mjini Dodoma.


Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi wa ukumbi wa kisasa wa mikutano wa CCM mjini Dodoma


Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza tufe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa jengo jipya la ukumbi wa kisasa wa mikutano la CCM mjini Dodoma.


Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ufunguo kutoka kwa Mkurugenzi wa kampunzi ya ujenzi ya CRJE kutoka China Ndugu Hu Bo kama ishara ya kukabidhiwa jengo la ukumbi wa kisasa la mkutano la Dodoma Convention Centre.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akimkabidhi mfano wa ufunguo wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, Katibu Mkuu wa CCM , Abrahman Kinana, baada ya kuzindua rasmi ukumbi huo leo, mjini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu,Balozi wa China Nchini Mhe. LU Youqing na Viongozi wa CCM mkoa wa Dodoma


Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete na viongozi wengine wa ngazi ya juu CCM wakiwa wamekaa kwenye meza kuu ndani ya ukumbi mpya wa kisasa wa mikutano mjini Dodoma.


Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Fredrick Sumaye kwenye ukumbi mpya wa mikutano wa CCM mjini Dodoma.


Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Kikwete(wa nne toka kushoto),Makamu Mwenyekiti wa CCM(Zanzibar) Dk.Ali Mohamed Shein (wa tatu kutoka kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya ukaguzi wa jengo.na Balozi Seif Idd (kushoto) Makamu wa Rais Dk.Mohamed Bilal,Katibu wa NEC Oganaizesheni Dk.Mohamed Seif Khatib,Balozi wa China Nchini Mhe. LU Youqing,Mama Salma Kikwete, Mhe. Anna Abdala na Mzee Pius Msekwa. (Picha zote na Adam Mzee)

MoDewji aaga jimbo la Singida Mjini


Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akiwapungia wapiga kura wake kama ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kutangaza kutogombea tena ubunge wa jimboni humo wakati wa mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

MBUNGE wa Singida mjini na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji amesema hatagombea ubunge wa jimbo hilo tena baada ya kulitumikia kwa miaka 10 na kuwezesha maendeleo makubwa katika sekta ya elimu na afya.

Taarifa ya kutwa nzima Channel TEN, Julai 8, 2015


Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Julai 9, 2015