Taarifa ya NEC ya mabadiliko ya zoezi la BVR kwa wakazi wa Dar es Salaam
Hizi katuni na vibonzo vya siasa mwaka huu... Utacheka tu!


UKAWA kumtaja mgombea Urais Tanzania 2015 leo kama...

Baada ya vikao mfululizo wiki hii, hatimaye Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) unatarajia kumtangaza mgombea urais wake kesho.

Taarifa zilizopatikana jana zimeeleza kuwa baada ya kikao cha viongozi wa ngazi za juu wa UKAWA, umoja unaoundwa na NLD, CHADEMA, CUF na NCCR – Mageuzi kilichofanyika juzi, mambo kadhaa yameafikiwa na kama hakutokuwa na mabadiliko yoyote, mteule wa urais kupitia umoja huo atabainishwa.

Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Dk Emmanuel Makaidi alithibitisha kuwa tayari makubaliano ya kugawana kata na majimbo kwa nafasi za udiwani na ubunge yamekamilika na kilichobaki ni utekelezaji.
“Tumeshakubaliana namna ya kugawana kata na majimbo 13 yaliyobaki na Jumamosi tutaweka wazi kwa wananchi. Pamoja na hilo pia tutamtangaza mgombea urais na chama anachotoka,” 
alisema Dk Makaidi.

Siku chache baada ya baadhi ya wabunge kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya Bunge na Spika Anne Makinda, Jumanne ya wiki hii CHADEMA ilifanya mkutano wa dharura kujadili mambo kadhaa ya kitaifa.

Siku moja baada ya kikao hicho, viongozi wa waandamizi wa UKAWA walikutana na kujadili mambo yanayohusu umoja huo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.

Hata baada ya vikao hivyo, mpaka jana CHADEMA iliendelea na vikao vyake vya ndani kujadili mambo kadhaa kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya UKAWA kinachotarajiwa kufanyika leo kupitisha jina la mgombea urais.

Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, John Mnyika alithibitisha kuendelea kwa vikao vya ndani vya chama hicho na kueleza kuwa hawezi kusema chochote kwa sababu ajenda bado zinajadiliwa na kwamba kesho taarifa za uhakika zitatolewa kwa vyombo vya habari.
“Kwa kifupi ni kwamba kikao bado kinaendelea. Nimetoka mara moja tu kupokea simu yako. Mazungumzo yatakapokamilika tutawajulisha (vyombo vya habari),” 
alisema Mnyika.

Mvutano

Wakati hilo likisubiriwa, zipo taarifa kuwa kuna mvutano baina ya vyama ndani ya umoja huo hasa katika nafasi ya mgombea urais baada ya kuwapo kwa watia nia zaidi ya mmoja.

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya umoja huo kilisema kuwa Kamati Kuu ya Ukawa ina kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa maridhiano yanafikiwa ili kumpata mgombea atakayeungwa mkono na vyama vyote katika jitihada za kuiondoa CCM madarakani.
“Licha ya kutangaza kugawana kata na majimbo yaliyobaki jina la mgombea urais litatangazwa pia. Hilo litafanyika endapo mwafaka utapatikana katika kikao cha Kamati Kuu kitakachofanyika kesho (Julai 10, 2015) Kikao kikiridhia chama gani kitoe mgombea, basi Watanzania watamjua hiyo Jumamosi,” 
kilisema chanzo hicho.

CHADEMA na CUF bado viliendelea na vikao vyake vya ndani jana. Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Shaweji Mketo alisema hakuna taarifa ambayo ingeweza kutolewa jana.

Alipoulizwa juu ya makubaliano yaliyopitishwa katika kikao cha UKAWA alijibu: “Hakuna maazimio yaliyofikiwa, bado tupo katika mjadala.”

Kuhusu kuungwa mkono miongoni mwa vyama vingine vya UKAWA kwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba aliyetangaza nia, Mketo alisema hana taarifa.

Wenyeviti wenza wengine wa vyama hivyo hawakupatikana kuzungumzia suala hilo. Hata walipopigiwa simu zao za mkononi, ziliita pasi na kupokewa.

Kuhusu wagombea 5 waliopitishwa CCM


Moja ya mabango yanayozunguka WhatsApp lililopo pia  kwenye akaunti ya Twitter ya CCM_Tanzania ambalo wavuti.com imepata nakala (bila kuthibitisha hivyo inabakia kuwa tetesi tu!) ni hilo lililopachikwa hapo juu.

Tweet1 na Tweet2

Kwingineko kwenye blogu ya Michuzi kuna taarifa mpya isemayo kuwa,
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari usiku huu nje ya ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma, mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichokaa kupitisha majina matano ya wagombea Urais yatakayopelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM kujadiliawa hapo saa nne asubuhi, hakutaja majina ya wagomea hao waliopita kwenye tano bora, kwa kusema kuwa atataja asuhuhi.
Muda mfupi baada ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kumaliza kuzungumza na waandishi wa habari, walitoka wajumbe watatu wa Kamati Kuu ambao ni Dkt. Emmanuel Nchimbi, Mhe. Sophia Simba na Mhe. Adam Kimbisa ambao walizungumza na waandishi wa habari juu ya walichokizungumza kwenye kikao hicho, ambapo wao walisema wamegomea makubaliano ya majina yaliyopitishwa kwenye kikao hicho kwa madai kwamba Kikao kimekiuka tararibu za uchujaji wa majina hayo, kwani yalijadiliwa majina machache tu na kupitishwa kwenda tano bora, nao hawakuyataja majina hayo.

Nalo gazeti la MwanaHALISI Online lina habari ifuatayo:

Wagombea watano wa CCM hawa, CC yapasukaDk. Emmanuel Nchimbi akitoa malalamiko yake mbele ya vyombo vya habari mara baada ya kutoka kwenye kikao cha CC. Kulia kwake ni Adam Kimbisa
Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa malalamiko yake mbele ya vyombo vya habari mara baada ya kutoka kwenye kikao cha CC. Kulia kwake ni Adam Kimbisa
KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC-NEC) imetoa orodha ya wagombea watano bila ya jina la Edward Lowassa kuwemo ndani. Lakini katika hali inayoonesha mpasuko, baadhi ya wajumbe wa kamati kuu wamepinga uamuzi huo. 

Majina yaliyopatikana, ambayo hata hivyo hayajatangazwa rasmi na chama, ni ya Bernard Membe, Dk. John Magufuli, Dk. Asha Rose-Migiro, January Makamba na Balozi Amina Salum Ali.

Membe ni mbunge wa Mtama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Magufuli ni mbunge wa Chato na Waziri wa Ujenzi, Dk. Migiro ni mbunge wa kuteuliwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Makamba ni mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, na Balozi Amina ni Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Tume ya Umoja wa Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, Marekani.

Maamuzi hayo hayakuwaridhisha baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu hasahasa wanaojulikana kuwa ni waungaji mkono wa Lowassa, na wametokeza hadharani kuyapinga huku wakilalamika kuwa kanuni zimevunjwa.

Dk. Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa wamefika mbele ya vyombo vya habari mara tu kamati kuu ilipomaliza kikao chake usiku huu, na kusema hawakubaliani na kilichotendwa.

Wajumbe hao wakizungumza kwa kupokezana huku wakitoa kauli kali, wamesema kanuni za utendaji katika vikao vilivyotangulia Kamati Kuu zimekiukwa. Kamati Kuu ina wajumbe 32.

Wamesema ukiukaji umekuja pale Kamati Kuu ilipopatiwa majina matano, badala ya kupokea majina yote ya wanachama walioomba kuteuliwa, ili yenyewe ndiyo itoke na majina matano baada ya kuyafanyia uchambuzi.
“Kanuni zinasema Kamati Kuu itapokea majina ya waombaji wote na ikishafanya uchambuzi wa kila muombaji, yakiwemo maoni ya kamati ya usalama na maadili, ndiyo huchagua majina matano yanayofikishwa mbele ya Halmashauri Kuu,” 
alisema Dk. Nchimbi ambaye alitokea kama kiongozi wa hao wajumbe watatu.

Kimbisa ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, amesema hawakubaliani na maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu kwa sababu hawakutarajia Kamati Kuu itakiukwa na kupokea majina ya baadhi tu ya waombaji.
“Haijawahi kutokea tangu nilipoingia katika Kamati Kuu kushuhudia ukiukaji wa kanuni kama ilivyotokea leo (jana) hii. Tumejitahidi kuuliza kwa mwenyekiti imekuaje kanuni inakiukwa lakini tumekosa maelezo ya kuridhisha,” 
amesema Simba, waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.

Wakati wajumbe wa Kamati Kuu walipokuwa wanatoka nje ya ukumbi wa kikao, Nape Nnauye, Katibu wa Itikadi na Uenezi, aliwaambia waandishi wa habari kikao kimemaliza kazi, tayari anayo majina matano ya waombaji walioteuliwa kupelekwa NEC, lakini “nitayatangaza kesho (leo) saa 4 asubuhi.”

Muda huo ni muda ambao kwa mujibu wa ratiba aliyoitoa mapema jana, kikao cha NEC kimepangwa kuanza. NEC yenye wajumbe wapatao 378 huwa inajadili majina hayo na kupiga kura ili kuchagua majina matatu ambayo hupelekwa mbele ya Mkutano Mkuu kwa uamuzi wa kupata mgombea.

Mgombea wa CCM anatarajiwa kutangazwa mara tu mkutano mkuu ambao utaanza mchana, utakapomaliza kupiga kura. Mkutano Mkuu una wajumbe zaidi ya 2,000.

Kabla ya hapo, itakuwa yametolewa matokeo ya kura alizopigiwa Dk. Ali Mohamed Shein aliyepitishwa kugombea tena nafasi ya urais wa Zanzibar.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari asubuhi hii nje ya Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM Mjini Dodoma, akithibitisha taarifa iliyokuwa ikizagaa mitandaoni ya Wagombea Urais walioingia katika hatua ya tano bora, ambao aliwataja kuwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Mh. Bernard Membe, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. January Makamba pamoja na Balozi Amina Salum Ali. Majina hayo yanapelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kujadiliwa na kupatikana matatu yatakayopelekwa kwenye Mkutano Mkuu na kupatikana moja ambaye ndie atakuwa Mgombea Urais.
Mikoba yenye makabrasha ya Mkutano Maalum CCM tayari...

Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM wakipakia mikoba yenye makabrasha ya mkutano maalum wa CCM Taifa 2015 unaotarajiwa kuanza kesho Mjini Dodoma katika ukumbi mpya wa uliozinduliwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete [picha: Ikulu.]

Latest highlights from International Energy Agency: Oil price could fall

Highlights (10 July 2015)
  1. Crude oil prices fell to their lowest in nearly three months in early July, pressured by ever rising supply while financial turmoil in Greece and China unsettled world markets. At the time of writing, Brent was around $59/bbl and US WTI at $53.10/bbl.
  2. Global oil demand growth is forecast to slow to 1.2 mb/d in 2016, from an average 1.4 mb/d this year, with strong consumption expected in non-OECD Asia. World oil demand growth appears to have peaked in 1Q15 at 1.8 mb/d and will continue to ease throughout the rest of this year and into next as temporary support fades.
  3. Global oil supply surged by 550 kb/d in June, on higher output from OPEC and non-OPEC. At 96.6 mb/d, world oil production gained an impressive 3.1 mb/d on 2014, of which OPEC crude and NGLs accounted for 60%. Non-OPEC supply growth is expected to grind to a halt in 2016, as lower oil prices and spending cuts take a toll.
  4. OPEC crude supply rose by 340 kb/d in June to 31.7 mb/d, a three-year high, led by record high output from Iraq, Saudi Arabia and the UAE. OPEC output stood 1.5 mb/d above the previous year. The 'call on OPEC crude and stock change' for 2016 is forecast to rise by 1 mb/d, to 30.3 mb/d.
  5. OECD industry inventories hit a record 2 876 mb in May, up by a steep 38.0 mb. Product holdings led the build and by end-month covered 30.7 days of forward demand. Global supply and demand balances suggest that the rate of global stock builds quickened rapidly to an astonishing 3.3 mb/d during 2Q15.
  6. Robust margins spurred stronger-than-expected OECD refinery runs, lifting 2Q15 global throughput estimates to 78.7 mb/d. Global refinery throughputs are forecast to increase by a further 0.7 mb/d in 3Q15, with annual gains shifting to the non-OECD. New capacity start-ups in 2015 and 2016 will put margins under pressure.
*Please note that these Highlights are from the latest Oil Market Report, which is released in full to subscribers only - according to this schedule each month. Non subscribers get free access to the latest Highlights on this schedule, however the full Oil Market Report is released to the public two weeks after the report is released to subscribers. If you would like to receive the full report with accompanying charts and graphs on the day of publication please subscribe or contact the subscription manager.

Mwandishi wa habari, blogger Kalulunga atangaza kuwania Ubunge


Mwandishi wa Habari, Gordon Kalulunga akizungumza katika viwanja vya mahubiri alipokuwa akitangaza nia ya kugombea Ubunge jimbo la Mbeya vijijini.

MWANDISHI wa habari wa gazeti la Mtanzania kutoka Mbeya, Gordon Kalulunga (mwenye blogu ya Kalulunga Media) amejitosa kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo la Mbeya Vijijini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kalulunga alitangaza kuingia kwenye mchakato wa kugombea kuteuliwa na Chama ili aweze kupeperusha bendara katika uchaguzi mkuu ujao katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jana kwenye viwanja vya mahubiri Mbalizi mkoani Mbeya.

Mtia nia huyo alisema endapo Chama chake kitampitisha na hatimaye kushinda Ubunge katika Jimbo hilo atahakikisha wananchi wote wanajiunga na mfuko wa bima ya afya kwa ajili ya matibabu kwa kila kaya kuchangia ili kupunguza adha na gharama kubwa za matibabu.

Aliongeza kuwa akifaniiwa kuukwaa Ubunge pia atasimamia kuhakikisha Jimbo hilo linapata Chuo cha aina yoyote kikiwemo Chuo cha ufundi kwa ajili ya vijana kupata elimu jambo lilatalopunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana.

Kalulunga alisema kipaumbele kingine atakachoshughulikia ni pamoja na kupigania ujenzi wa ofisi za makao makuu ya Wilaya hiyo katika eneo husika ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi tofauti na ilivyosasa ambapo Ofisi za Wilaya ya Mbeya zipo katikati ya Jiji la Mbeya.

Awali Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Mbeya vijijini, Japheti Siulanga aliwataka vijana wote kuungana ili kumuunga mkono kijana mwenzao aliyejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kuongoza akiwa Mbunge wa jimbo hilo.

Aidha katika mkutano huo vijana zaidi ya 26 walijiunga na Chama cha mapinduzi na kukabidhiwa kadi za umoja wa Vijana.


Kalulunga akitaja vipaumbele vyake


Katibu wa Umoja wa Vijana Wilaya ya Mbeya vijijini, Siulanga akiwaasa Vijana kumuunga mkono kijana mwenzao.


Kalulunga akisalimiana na mmoja wa wazee waliojitokeza kumsikiliza alipokua akitangaza nia


Vijana wakiserebuka


Burudani zikiendelea


Wananchi wakimsikiliza Kalulunga

  • via MbeyaYetu blog


Kubenea: Lowasa aenguliwa

Kibonzo kimetungwa na Daniel "Danny" Mzena

JINA la Edward Lowassa, mmoja wa wasaka urais kwa udi na uvumba, limeenguliwa katika hatua za awali za kinyang’anyiro hicho.

Taarifa kutoka kwa watu waliokaribu na mmoja wa viongozi wakuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mjini Dodoma zinasema, jina la mwanasiasa huyo machahari limeondolewa kutokana na shinikizo la baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho.
“Ni kweli jina la Lowassa limeondolewa katika kinyang’anyiro hiki. Baadhi ya wakubwa wamekuja na msimamo na wameapa kutosikia mtu anayeitwa Lowassa akikatiza na kuingia NEC,” 
ameeleza mtoa taarifa wa gazeti hili.

Vikao vya uteuzi vya chama hicho – Kamati ya Maadili, Kamati Kuu (CC) na Halamashauri Kuu – tayari vimeanza mjini Dodoma mchana huu. Mkutano wa NEC umepagwa kuanza kesho saa nne asubuhi.

Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema, ikiwa jina la Lowassa limeondolewa katika kainyang’anyiro hiki katika hatua za awali, basi ndoto za mwanasiasa huyo kushika madaraka ya juu katika nchi, zitakuwa zimezimwa.

Lowassa amekuwa akihaha kutaka kuwa Rais wa Jamhuri tangu mwaka 1995, ambako alijitosa kugombea nafasi hiyo.

Hata hivyo, jina lake liliondolewa katika hatua ya awali baada ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere “kumng’ang’ania” na kushinikiza kuondolewa kwa jina lake.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Lowassa hakujitosa katika kinyang’anyiro hicho; badala yake alimuunga mkono Kikwete kwa makubaliano ya kufanywa kuwa Waziri Mkuu na baadaye kuwa Rais.

Habari zinasema, kuzimwa kwa ndoto za Lowassa, kunafuatia taarifa kuwa mchakato wa uchujaji majina ya wasaka urais kupitia CCM, kuendeshwa na baadhi ya vigogo kutoka idara ya usalama ambayo imesheheni “wabaya” wake.

Lowassa, mwanasiasa machachari katika siasa za CCM, ni miongoni mwa makada 38 wa chama hicho waliochukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa na chama chao kugombea wa urais wa Jamhuri.

Inaelezwa kuwa vita ya kisiasa anayopigana Lowassa kwa sasa, siyo tena kati yake na chama chake, bali ni kati yake na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).

Mgogoro wa Lowassa na TISS unatokana na ukaribu wa mwanasiasa huyo na aliyewahi kupata kuwa Mkurugenzi mkuu wa idara hiyo, Apson Mwang’onda.
“Lowassa akiteuliwa kugombea nafasi hiyo, atakuwa amewashinda watu wa usalama waliopo sasa; jambo ambalo haliwezi kukubarika,” 
kimeeleza chanzo kimoja cha taarifa mjini Dodoma.

Anaongeza,
“…ikiwa hivyo, maana yake ni kuwa TISS iliyoko kwenye uongozi wa sasa itakuwa imeonyesha udhaifu mkubwa mbele ya Apson anayeratibu mbinu na mikakati ya Lowassa.”

Mkurugenzi wa Usalama wa sasa, Othuman Rashid anadaiwa kumuunga mkono Bernard Membe, mmoja wa wasaka urais anayetajwa kuwa chaguo la Kikwete.

Katika hatua nyingine, taarifa zinamnukuu mmoja wa viongozi wa kamati kuu akisema, chombo hicho muhimu katika uteuzi wa wagombea urais, imegawanyika.
“Mgawanyiko unatokana na baadhi ya watu kutaka Lowassa asikatwe, huku wengine wakisema, sharti aondolewe,” 
anasema mmoja wa watoa taarifa wa gazeti hili.
Picha via WhatsApp (wavuti.com)

10 cool things you can do with a hanger


If you need more hanger hacks, head on to YouTube (click here) and learn some.

Some antidepressants pose increased risk of birth defects - Study

The study, published Wednesday in The BMJ, found no association between the most commonly used antidepressant, sertraline (Zoloft), and birth defects.

[...] also found no increased risk of birth defects with the antidepressants citalopram (Celexa) and escitalopram (Lexapro).

But the analysis did find an association between birth defects and the antidepressants fluoxetine (Prozac) or paroxetine (Paxil). That included heart defects, abdominal wall defects, and missing brain and skull defects with paroxetine, and heart wall defects and irregular skull shape with fluoxetine. The relative risk increased 2 to 3.5 times, depending on the defect and the medication. [NPR]

Mkutano wa Mkuu CCM kuoneshwa LIVE mtandaoni

Mhadhiri Chuo Kikuu achukua fomu CCK za kuwania Urais Tanzania 2015


Vyama vya siasa Zanzibar vyakataa kusaini maadili ya uchaguzi

Wadau wa vyama vya siasa wamekataa kusaini maadili ya uchaguzi mpaka kiingizwe kipengele cha jeshi la polisi

Wadau wa vyama vya Siasa wamekataa kwa sauti moja kusaini maadili ya vyama vya siasa mbele ya uongozi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Kikao hicho kilichohuduriwa na wajumbe wa vyama vyote vya siasa kilifanyika jana katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace na kushuhudiwa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jecha Salum Jecha, Mkurugenzi Salum Kassim Ali na maafisa wengine wakiwemo Makamishna wa tume hiyo pamoja na maafisa wa Shirika la UNDP.

Maadili hayo yalipangwa kutumika wakati wote wa uchaguzi mkuu ambapo wadau hao walitakiwa kuyazingatia na kuyafuata ili kuweka mazingira mazuri ya uchaguzi ya kufanyika kwa haki na uhuru.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe Ismail Jussa alisema hawatasaini waraka wa maadili hayo hadi kitakapoingizwa kipengele kitakachoeleza wazi majukumu ya jeshi la polisi na vikosi vya Serikali ya Zanzibar ambavyo vimeonesha ishara mbaya hivi karibuni.

Jussa alisema licha ya kuwa vikosi vya SMZ havitakiwi kisheria kusimamia uchaguzi lakini vimeshuhudiwa vikiingilia uandikishaji wazi wazi na kufanya ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu, kukiuka sheria, kanuni na taratibu za uandikishaji jambo ambalo limezusha malalamiko makubwa kwa wananchi na wadau hao.

Alisema bila ya kuwekewa kipengele mahsusi jeshi la polisi na vikosi vya SMZ maadili hayo yatakuwa hayana maana yoyote kwa kuwa hivi karibuni wazanzibari wameshuhudia vikosi vya SMZ vilivyopita njiani na kuvaa soksi usoni huku vikiwa vimebeba silaha nzito nzito pamoja na silaha za kienyeji kama mapanga, nodno na misumeni ya kukatia miti wakiwatisha wananchi na kuwatishia maisha waandishi wa habari.
“Mwenyekiti mimi na chama changu hatukubaliani na kusaini maadili haya na ninawashawishi wenzangu wakatae hadi hapo kitakapoingizwa kipengele ambacho kitaeleza bayana majukumu ya jeshi la polisi, majukumu ya vikosi vya SMZ kwa sababu hivi juzi tu vimeonesha mfano mabaya sana kwa vikosi hivi kuvaa masoksi usoni kuwavamia na kuwapiga watu kuvamia vituo vya radio na kufanya uhuni mkubwa kwa hivyo kama hawajaingizwa hawa kwenye muongozo huu wa maadili hatuwezi kutia saini kikao kivunjike mkaingize tena kisha tuitane tena kuja kusaini” 
alisema.

Kauli ya Jussa iliungwa mkono na wadau wengine huku wakipiga makofi kuonesha kuunga mono hoja hiyo wajumbe hao wamesema ni kweli kuna kila sababu ya jeshi la polisi na vikosi vya SMZ kuwekewa utaratibu wa maadili kwa kuwa wao ndio hawaribifu wa uchaguzi namba moja hivyo sio vyema maadili yakawaacha nyuma.

Suleiman Mohammed Abdallah kutoka chama cha NRA ambaye amesema anashangazwa kuona serikali ikikaa kimya licha ya kelele zote zilizopigwa za ukiukwaji mkubwa wa sheria na haki wa kuingilia uandikishaji huku jeshi la polisi likiwakana watu wao na kusema hawawajui wenye kuendesha vitendo hivyo.
“Mimi nashangaa ikiwa serikali inaona vitendo vilivyokuwa vikifanyika njiani watu wamebeba silaha za moto, wamebeba mapanga, wamebeba misumeni ya kukatia miti wanatumia magari ya polisi na wengine wamevaa sare sasa hawa kama hawajawekewa utaratibu maalumu au hawajaingizwa kwenye haya maadili watakuja kutuletea maafa baadae” 
alisema Mohammed.

Akitaja kipengele cha kuongeza katika maadili hayo Jussa alisema kifungu cha 15 kwenye wajibu wa serikali na wajibu wa tume ya uchaguzi kuongezwe wajibu wa jeshi la polisi na wajibu wa vikosi vya SMZ mbapo iwe wajibu wa jeshi la polisi ni kuhakikisha wanalinda usalama wa raia na mali zao, wanalinda wapiga kura maafisa wa tume lakini pia kuhakikisha wanalinda Amani na usalama na hawaingiliwi na taasisi nyengine ya ulinzi kwa kuwa wao ndio wenye mamlaka ya ulinzi.

Aidha katika kipengele hicho jeshi la polisi lihakikishe linafuata sheria na katiba na kwenye idara maalumu za SMZ zina sheria na jukumu na sheria iliyoanzishwa idara hizo na zijikubalishe kuwa hazitaingilia kwa hali yoyote katika uchaguzi.

Juma Said Sanani kutoka Chama cha ACT Wazalendo, amesema kuwekwa maadili ya uchaguzi ni vizuri kwa kuwa yatakuwa ni muongozo wa kuipelekea nchi kwenye amani na kufanyika uchaguzihuru na wa haki.
“Maadili haya tunayokuja kuyaweka basi yawe yanafuatwa ili tuvuke katika uchaguzi kwa salama bila ya hivyo tutakuwa na uchaguzi usio huru wala haki na matokeo yake tutashuhudia machafuko kama nchi nyengine kwa hivyo mimi nashauri maadili haya yatupeleke kwenye ukweli atakayeshinda apewe ushindi wake na alokuwa hajashinda akubaliane na matokeo” 
alihimiza Sanani.

Makamo mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema, Zeudi Mavamo Abdillahi alisema matumizi ya nguvu ya vikosi vya SMZ yaliotumika ni makubwa hivyo haiwezekani vikosi kuwekwa nyuma kutokana na kuonesha mfano mbaya hivi karibuni.
“Hatuwezi kusaini bila ya vikosi na wao kuingizwa humu kwa sababu wao wanajulikana namna gani wanavyoingilia chaguzi zetu na kwa kuwa tumeshatafunwa mara moja hatukubali kutafunwa tena juzi tu hapa wamefanya uhuni mkubwa kwa kuingilia watu na kuwapiga ovyo vipi tukubali tu hilo haliwezekani” 
alisema Zeudi.

Mohammed Noor kutoka CUF naye alipendekeza kwenye kifungu cha 13 kuongezwa kifungu chengine kidogo kushughulikia kwa wepesi malalamiko yanayotolewa kwani kumeonekana malalamiko yanapotolewa tume huchukua muda kuyashughulikia.

Aidha amesema katika kifungu cha 18 badala ya vyama vya siasa kuahidi kuyakubali matokeo ya uchaguzi bali kuwepo neno halali
“Mimi hapo kwenye neno kuyakubali matokeo kuongezwe neno halali hivyo isomeke vyama vya siasa tunaahidi kutakubali matokeo halali ya uchaguzi kwa mujibu wa fomu za uchaguzi yaliosainiwa kwenye vituo vya upigaji kura” 
alisema Noor.

Peter Magwira wa UDP amesema kuna kila sababu ya kuwekwa maadili ya vyama vya siasa ili yaweze kuwaongoza wakati wote wa uchaguzi na baada ya kutoka matokeo ya uchaguzi ili nchi iwe salama na uchaguzi ufanyike kwa Amani.
“Watu wengine hawapendi kuyaheshimu haya maadili wakati sisi wenyewe ndio tunaoyatengeza lakini mimi nawashauri wanasiasa wenzangu tuyaheshimu haya maadili tunayoyatengeneza” 
alisisitiza Peter.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya vyama vya siasa, Kamishna Nassor Khamis Mohammed kutoka ZEC alikubaliana na wadau hao kwamba maadili hayo yasisainiwe lakini akawaomba wafanye marekebisho ya vifungu ambavyo wanataka kuviongeza ili waende sambamba na dhana ya kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki.

Khamis alisema maadili hayo ni yao wao kwa pamoja na sio ZEC peke yao hivyo wana kila sababu ya kuwasikiliza wadau hao hadi hapo watakapowafikiana kwani mwisho wa siku muongozo huo ndio utakaotumika kwa wote wakati wa uchaguzi hivyo sio busara wao kama ZEC kushikilia wanavyotaka wao tu bila ya kuridhiwa na wadau wote.

Hata hivyo Chama Cha Mapinduzi hakikuhudhuria katika kikao hicho, akiomba radhi kwa kutoshirikia Mwenyekiti wa maadili hayo alisema kwamba aliwasiliana nao wamesema hawakuhudhuria kutokana na viongozi ambao walipaswa kuwepo kwenye kikao hicho wamekwenda Dodoma kwenye shughuli za kumtafuta mgombea urais lakini wanakubaliana na mabadiliko na maamuzi yeyote yatakayofanyika katika kikao hicho.

Orodha ya vyama vilivyopewa siku 14 kujieleza la sivyo vifutwe

VYAMA VINAVYOKUSUDIWA KUFUTWA VYAPEWA SIKU 14 ZA KUJIELEZA

Orodha ya vyama vyenye madeni vilivyo hatarini kufutwa na Serikali

ORODHA YA VYAMA VYENYE MADENI YA ADA YA MWAKA NA WASIOLETA TAARIFA YA FEDHA YA KILA MWAKA. VYAMA HIVI VINAPEWA KUSUDIO LA KUFUTWA CHINI YA KIFUNGU CHA 17 CHA SHERIA YA VYAMA VYA KIJAMII SURA 337

Vurugu Bagamoyo: Kituo cha Polisi Bunju chachomwa motoJengo la kituo cha Polisi likiteketea kwa moto

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kuchoma kituo kidogo cha Polisi kilichopo Bunju ‘A’ jijini Dar es Salam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni Camillus Wambura alisema tukio hilo lilitokea saa 3:00 asubuhi wakati Tanroads pamoja na Jeshi la Polisi walipokuwa katika mazungumzo ya kuweka matuta katika barabara hiyo.

Alisema kabla ya kuchomwa kituo hicho dereva aliyetambulika kwa jina la Yohana John aliyekuwa akiendesha gari aina ya Coaster alisababisha ajali katika eneo hilo na kumgonga mwanafunzi mmoja wa shule ya Bunjua ‘A’ Radhia Omary na kusababisha kifo chake.

Alisema baada ya mwanafunzi huyo kupoteza maisha wanafunzi wa shule hiyo pamoja na wananchi wa eneo hilo walikusanyika na kulala barabarani hali iliyosababaisha magari kutoendelea na safari zake.

Alisema wananchi hao pamoja na wanafunzi walifunga barabara hiyo kwa muda wa saa tatu wakidai kuwa wanataka matuta yawekwe katika eneo hilo lililopo karibu na shule hiyo ili liweze kuwasaidia wanafunzi wakati wa kuvuka barabara.

Hali hiyo ilileta usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo kwa kufungwa na kushindwa kuendelea na shughuli zao hali iliyosababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya watu.
“Baada ya tukio hilo polisi na Tanroads tulikaa kikao cha dharura kilichokuwa kikielekeza utengenezwaji wa matuta ya haraka katika eneo hilo.
“Wakati tukiendelea na mazungumzo hayo wananchi walipata mwanya wa kukivamia kituo hicho na kukichoma moto.
“Sababu ya wananchi hao kuchoma kituo hicho hakuna, na wamefanya jambo ambalo si la busara na wamesahau kuwa kituo hicho kinawasaidia watu wote wa eneo hilo,” 
alisema Kamanda Wambura.

Alisema mbali na kuchoma kituo hicho pia wamechoma magari mamne ya watu binafsi yaliyokuwa yameegeshwa pembezoni mwa kituo hicho.

Pia alisema wanamshikilia dereva wa Coaster aliyesababisha ajali pamoja na gari hilo.
“Kwa sasa tupo katika zoezi la kuwasaka na kuwakamata watu wote waliosababisha vurugu hizo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake,” 
alisema Kamanda Wambura.

Shuhuda wa tukio hilo, Moshi Sultan, alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 3:00 asubuhi baada ya gari kumgonga mwanafunzi huyo aliyekuwa anakwenda shule.

Alisema baada ya tukio hilo wananchi wa eneo hilo walikusanyika na kufunga barabara hali iliyosababisha polisi kuingilia kati na kuanza mvutano kati yao na hatimaye wananchi hao kuvamia kituo hicho na kukichoma moto.

Alisema wananchi hao waliwasha moto kituoni hapo pamoja na tairi za gari na kudai kuwa askari waliopo hawafanyi kazi kwa umakini.
“Kutokuwapo kwa askari wa kutosha katika kituo hicho kumechangia wananchi hao kuvamia kwa urahisi na kuchoma moto kituo hicho,”
alisema.

Katika tukio jingine, moto mkubwa umezuka na kuteketeza nyumba yote inayomilikiwa na Hamisi Katori iliyopo katika mtaa wa Mabanda Marefu Ukonga Mombasa jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Lucas Mkondya, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme.

Alisema wakati moto huo ukiendelea kuwaka alikuwepo mtoto mdogo mwenye umri wa miaka miwili aliyetambulika kwa jina la Mohamed Shabani ambaye alikuwa amelala ndani lakini msamaria mwema alifanikiwa kumuokoa.

Mkondya alisema moto huo uliteketeza nyumba yote, mali na thamani zilizoteketea kwa moto bado hazijafahamika.

Alisema hakuna madhara kwa binadamu, moto ulizimwa na kikosi cha Zimamoto Uokoaji cha Jiji kwa kushirikiana na wananchi wa eneo hilo.

Polisi wa wakijaribu kuwatawanya watu katika eneo la kituo cha Polisi Bunju baada ya wanachi kukichoma moto baada ya mwanafunzi wa shule kugongwa na gari na kufa papo hapo.Moja ya Gari iliyokuwepo kituoni hapo ikiwa imenyofolewa vifaa vyake wakati wa vurugu hizo


Kituo cha Polisi cha Bunju kinavyoonekana baada ya kuchomwa moto.

Kituo cha Polisi cha Bunju A kikiteketea kwa moto.

Polisi akikagua uharibu katika moja ya gari lililokuwa kituoni hapo.
Imevunjwa kioo chote cha nyuma

Baadhi ya polisi wakiangalia uharibifu uliofaywa na baadhi ya watu waliovamia kituo hicho cha polisi Bunju,kufuatia tukio la kudaiwa kugongwa na gari mwanafunzi mmoja na kufa papo hapo.


Baadhi ya Polisi wakiwatawanya watu (hawapo pichani) kwa mabomu ya machozi mara baada ya tukio la kuchomwa moto kituo cha polisi Bunju, tukio hilo limetokea.Kituo cha polisi Bunju kilichopo nje kidogo ya jiji la Dar kimechomwa moto na baadhi ya Wananchi kufuatia tukio la kudaiwa kwa Mwanafunzi mmoja kugongwa na gari na kufa papo hapo.

Dakika mbili za Tundu Lissu "Kikaangoni" EATv


Tanzania yasaini mkopo wa shilingi bilioni 223 kutoka Ufaransa

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano mara baada ya kusaini ambapo hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi Ufaransa nchini Malika Berak.

Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) imesaini makubaliano ya mkopo nafuu wenye thamani ya Sh. bilioni 223 za Kitanzania ambazo ni sawa Euro milioni 93 kwa ajili ya uboreshaji wa sekta ya maji na umeme nchini.

Makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam ambapo kwa upande wa Tanzania Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua amesaini kwa niaba ya Serikali na kwa upande wa Serikali ya Ufaransa imewakilishwa na Balozi wake nchini Malika Berak na Mwakilishi wa AFD Yves Boudot.

Dkt. Mwinyimvua amesema kuwa fedha hizo kutoka Shirika la Maendeleo la Ufaransa zimetolewa kwa ajili ya kutiasaini mikataba mitatu ili boresha upatikanaji wa huduma za jamii.

Mkataba wa kwanza unahusisha sekta ya maji ambao wenye thamani ya Euro milioni 40 utakaosaidia kuboresha huduma ya uzalishaji maji, utunzaji maji safi na salama pamoja na kuboresha huduma ya maji taka nchini katika maeneo ya mijini na vijijini.

Dkt. Mwinyimvua alisisitiza kuwa mkataba wa pili una thamani ya Euro milioni 53 kwa lengo la uboreshaji wa sekta ya umeme nchini ambapo vituo 10 vilivyo chini ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na vitanufaika na mkopo huo ili kutakarabati mtandao wa miundo mbinu ya umeme na kukabiliana na upotevu wa umeme nchini.

Vituo hivyo vitakavyokarabatiwa ni Chalinze, Mlandizi, Same, Tabora, Mbeya, Mufindi, Dodoma, Mwanza na Bukoba pamoja na Mkongo wa Taifa.

Na mkataba wa tatu unahusisha mkataba wa Tanzania na Ufaransa wa mwaka 1998 ambao ni umekuwa wa muda mrefu ili kuendana na hali ya sasa ambapo yametokea mabadiliko mengi ambayo yanapaswa kuendana na wakati.

Kwa upande wake Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kudumisha ushrikiano uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Ushirikiano wa Tanzania na Ufaransa katika miradi ya maji na umeme umekuwa na tija kwa wananchi kijamii na kiuchumi tangu miaka ya 2009 ambapo Shirika la AFD lilitoa zaidi ya sh. bilioni 628/=.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Hamisi Mwinyimvua (kushoto) akisaini mkataba wa mkopo wa sh. Biloni 223 kwa niaba ya Serikali Tanzania ambapo makubaliano hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi Ufaransanchini Malika Berak.

Ratiba ya CCM ya vikao vya leo Julai 10, 2015


Ratiba ya vikao vya CCM kwa siku ya leo tarehe 10/7/2015:

Saa 4 - 7 mchana.
Kikao cha Usalama na Maadili chini ya M/kiti wake Rais Jakaya Kikwete.

Saa 8-12 Jioni.
Kikao cha Kamati Kuu kitakachopitisha majina ya wagombea watano.

Baada ya Futari, Saa 2 Usiku:
Kikao cha Halmashauri Kuu kupitisha majina matatu ili Mkutano Mkuu utakaoanza kesho asubuhi upokee majina hayo matatu na kumchagua mmoja wapo atakayepeperusha bendera ya Chama.

SABABU YA KUCHELEWA VIKAO:

Ratiba ya vikao ambayo ilikuwa imetolewa awali haikufuatwa kwa sababu ya Shughuli zilizojitikeza za Mhe Rais za Kichama na Serikali ambazo amekuwa akizifanya tangu alipowasili Dodoma juzi.

Sababu nyingine ni kuwepo kwa Vikao vya mashauriano, ili kuhakikisha kuwa vikao vya mchujo vinaisha kwa salama na hatimae Mgombea wa CCM apatikane kwa Amani


KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, Nape Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo asubuhi amesema majina matano ya makada wa chama hicho kati ya 38 walioomba kuteuliwa na CCM kuwania kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yatajulikana, na kufuatia majina matatu ya makada hao ambayo yatapelekwa mbele ya Mkutano Mkuu utakaofanyika kesho Jumamosi Julai 11, 2015.

Nape amesema vikao vyote vinaanza leo saa nne, na hakuna kikao chochote kilichokwisha fanyika ikiwa ni pamoja na kile kinachozungumzwa sana na vyombo vya habari yaani kikao cha kamati ya maadili ya chama hicho ambacho ndicho kinachokata majina na kutoa mapendekezo Kamati Kuu.

Alipoulizwa ucheleweshwaji huo umetokana na nini, Nape alisema "Nyote mmeshuhudia, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, amekuwa na kazi nyingi katika kipindi cha siku mbili hizi na hivyo asingeweza kusimamia vikao hivyo kama ilivyotarajiwa ingawa amedokeza kuwa "wakubwa" hao walikuwa wakikutana kwa majadiliano na wadau ingawa hakueleza ni wadau gani.

Mahasimu wa Museveni, Mbabazi na Besigye wakamatwa na kuachiwa

Viongozi wawili wa upinzani, mahasimu wakubwa wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni katika uchaguzi ujao wa Rais wameachiwa huru baada ya kukamatwa kwa saa kadhaa na polisi, kwa madai ya kutaka kuitisha kampeni za uchaguzi bila ya ruhusa. 

Waziri Mkuu wa zamani Amama Mbabazi na Kizza Besigye, mojawapo ya vigogo wa chama cha upinzani FDC, walikamatwa jana walipokuwa wanajiandaa kushiriki katika mikutano ya kisiasa. 

Viongozi hao wawili wametia saini waraka kwa hivyo wameachiwa huru bila ya masharti. 

Polisi nchini humo imeonya haitovumilia mikutano ya kisiasa itakayoitishwa bila ya ruhusa. Wahusika wanabidi kutuma ufafanuzi wa mikutano kwa polisi siku tatu kabla ya kuitishwa.

Wanachama CHADEMA wavua viongozi madaraka na kuunda kamati ya muda

NGUVU ya Umma ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Ruaha, Jimbo la Mikumi, Wilaya ya Kilosa, Morogoro, wamewavua uongozi waliokuwa viongozi wao na kuweka kamati ya muda (task force), kwa madai ya kuwa mamluki ndani ya Chama chao.

Waliovuliwa uongozi na kubaki na uanachama ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kata, George Banda, Katibu, Ally Mponda, Katibu Mwenezi, William Temu, Mweka Hazina, Aurelia Mnunga, na Mjumbe wa Kamati Tendaji, Mwalimu Myami.

Katika kikao cha ndani cha Julai 2 (ukumbi wa Linas), kilichosimamiwa na Mkurugenzi wa uchaguzi na mafunzo wa CHADEMA Taifa, Benson Kigaila; Baada ya kusikiliza ‘Tuhuma’ za Viongozi hao, aliwauliza wanachama wanataka nini, ambapo wote walipaza sauti; Wavuliwe uongozi na kubaki Wanachama!.

Aidha tuhuma zilizoelekezwa kwa viongozi hao, ni Kuwafukuza viongozi wenzao watatu wa CHADEMA, kwa kutumia Vifungu visivyokuwemo kwenye Katiba ya CHADEMA, ilihali wakijua ni kukinyang’anya Chadema Ushindi wake halali na kukifurahisha Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nyingine ni Viongozi hao kuhamisha vikao vya Chama, ambapo badala ya kufanyia kwenye Ofisi ya CHADEMA Kata, kwa miezi zaidi ya minne walihamishia vikao na Ofisi kwenye mgahawa wa mmoja wa Viongozi hao kinyume cha Katiba.

Kiongozi Mpya, Abasi Longa, alikiri kuchaguliwa Mwenyekiti wa muda kati ya viongozi waliochaguliwa na Wanachama; Hii ikiwa ni mara tu baada ya kumvua, Banda aliyekuwa Mwenyekiti, ambapo, Joram Zacharia, alithibitisha kuchukua ukatibu aliovuliwa, Mponda.

Mbali ya waliovuliwa nyadhifa kutotaka kuzungumza na Mwandishi hata walipopigiwa simu za Viganjani kuelezea walivypokea kuvuliwa Uongozi na kuwa Wananchama; Aliyekuwa Katibu, Mponda, pekee alikiri kuondolewa, akisema, “Siasa ni Kijiti, lazima tupokezana”.alisema

Hata hivyo, Longa alikiri kupokea fomu za viongozi watatu waliovuliwa uongozi na kubaki Wanachama wa CHADEMA, Banda, Mponda na Mnunga, ambao wametia nia ya Udiwani wa Kata hiyo.

Awali Mponda, alimthibitia Mwandishi wa habari, kuhusu azma yake kutia nia ya kugombea Udiwani wa Kata hiyo wakiwemo viongozi wenzake waliovulia madaraka, jambo ambalo limeendelea kuwawatia shaka wana CHADEMA kuwa, huenda kulikuwa na kitu nyuma ya pazia.
  • Imeandikwa na Bryceson Mathias, Kilosa, Morogoro

Taarifa ya kutwa nzima Channel TEN, Julai 9, 2015
Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Julai 10, 2015

Magavilla on UBISHI Episode 4 - Mwananchi/The Composition Challenge

The ‘composition’ challenge discussed on ‘UBISHI’

Released July 10, 2015

One of the great opportunities that we have in accelerating the fortunes of this great country is addressing, what I like to refer to as, our ‘composition’ challenge; what kind of people make up our populous, in particular our youth, in terms of skills, competencies and values.

If you are making strides in life and form part of the top echelons of society, the plight of the bottom of the food chain may not be of particular interest to you – think again!

Irrespective of its composition, the broad bottom will always carry the narrow top. The masses, at large, are either consumers of the products that keep our companies running and or are the ones casting the votes that inform who will lead our country.

Are you still not interested in the plight of broad bottom?

I reflect briefly on this in this week’s Ubishi Talk Show series, visit www.magavilla.com/videos where you can view my other videos.