Mgombea Urais wa Tanzania 2015 kupitia CCM


Matokeo ya kura za wagombea kutoka Mkutano Mkuu ni:
  1. Dk John Magufuli 87.1%
  2. Balozi Amina Salum Ali 10.5%
  3. Dk Asha-Rose Migiro 2.4%

Kura zilizopigwa zilikuwa 2422.
Kura zilizoharibika zilikuwa 6. 
Kura halali ni jumla ya 2416. 

Mgawanyo wa kura ukawa kama ifuatavyo:-
Dk. Asha-Rose Migiro alipata jumla ya kura 59.
Balozi Amina Ali alipata jumla ya kura 253.
Dk John Magufuli alipata jumla ya kura 2,104.

John Magufuli
John Magufuli 

Nukuu za Mhe. Magufuli alipozungumza baada ya kuteuliwa:
"Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kunifanya niwe salama...Nafasi mliyonipa ni kubwa sana. Jana wakati naomba kura niliwaambia nitumeni nami nitawatumikia... nitawatumikia kwa nguvu zangu zote, kwa moyo wangu wote kwa kutumia vipaji vyangu vyote nilivyopewa na Mwenyezi Mungu. Wingi wa kura hizi nilizopata ni uthibitisho kuwa CCM ni wamoja. Naamini tutashirikiana ili kuutafsri ushindi huu katika uchaguzi mkuu ujao."
"Kinachotakiwa ni ushirikiano kwa wanachama, wote, tuungane kwa pamoja ili kuhakikisha kuwa chama chetu kinapata ushindi ulio mnono sana kwenye uchaguzi mkuu ujao. Nafurahi kuwa napeperusha chama imara, chenye watu wenye hamasa ya juu, chama kilichoipatia sifa nzuri nchi yetu, chama kilichokomaa."
"Waheshimiwa wanachama wenzangu wa CCM naomba kuwahakikishia kuwa nitakuwa nanyi kweli kweli, nitakuwa mtumishi wenu. Hapa ni Chama kwanza."
Na taarifa kuhusu yaliyojiri huko kikaoni, kutoka kwenye blogu ya Habari na Matukio inasema...
WAZIRI wa Ujenzi na Mbunge wa Chato, Mh.Dkt. John Pombe Magufuli, ameteuliwa na Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, kuwa Mgombea wake wa Kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Habari za mkutano huo uliofanyika kwenye kituo cha mikutano cha Dodoma, kinachomilikiwa na CCM, zimeeleza kuwa, Mh. Dkt. Magufuli amepata jumla ya kura 2, 104, na kuwashinda wapinzani wake, Dkt. Asha-Rose Migiro, aliyepata kura 59, na Mh. Amina Salum Ali, amenyakua kura 253.
Awali kabla ya kufikia kilele cha mchakato huo wa kumpata mgombea wa CCM palizuka mvutano mkali kwenye vikao vya mchujo, ambapo manung’uniko na mifarakano ilianza pale Kamati Kuu ya chama hicho, kutojadili majina yote ya wagombea na badala yake kujadili majina machache huku yale yua makada waliopuwa wakipigiwa upatu, kuachwa.
Haata baada ya kikao nhicho cha kamati kuu, hali ilikuwa mbaya zaidi wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC), ambapo baadhi ya wajumbe walionyesha wazi wazi upinzani wao dhidi ya maamuzi ya kamati kuu, hali iliyopelekea jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama kuongeza nguvu ya ulinzi ikiwa ni tahadhari endapo patatokea jambo baya.
Majina yaliyofikishwa ili kujadiliwa na Halmashauri kuu ni pamoja na lile la Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe, Waziri wa Sheria na Katiba, Mh. Dkt. Asha Rose Migiro, Naibu Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano, Mh. January Makamba, na Waziri wa Ujenzi, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, na Mh. Balozi Amina Salum Ali.
Halmashauri Kuu ikapitisha majina matatu ya watakaoingia kwenye uamuzi wa msiho wa Mkutano Mkuu wa CCM ambapo hatimaye umemchagua Mh. Dkt. John Magufuli kuwa ndiye atakayepeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu.

Julai 12, 2015 mwendo wa saa sita u nusu usiku (majira ya Tanzania), Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, ameahirisha kikao kilichokuwa kinaendelea ili kumpata mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia chama hicho. Amesema kwa kuwa shughuli ya kuhesabu kura ni ya kukesha, wanalazimika kuondoka sasa na watarejea hapo kesho saa nne asubuhi ili kukamilisha kikao hicho.

Amewaaga wajumbe wote kwa kuwafahamisha kuwa siku moja zaidi imeongezwa kwa ajili ya kukamilisha shughuli za mkutano huo.

Kura ndiyo zinapigwa sasa ili kumpata mshindi...


Watatu waliopita CCM katika mchujo wa kuwania Urais Tanzania 2015

Chama cha Mapinduzi kimetangaza majina matatu, ambayo usiku huu yanapelekwa katika Mkutano Mkuu ili kupata jina moja la mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama hicho. Watatu hao ni:

  1. JOHN POMBE MAGUFULI

  2. ASHA-ROSE MIGIRO

  3. AMINA SALUM ALI

Akamatwa na sanduku lenye maburungutu ya fedha Dodoma

Taarifa mpya kwa mujibu wa gazeti la NIPASHE JUMAPILIMtu mmoja amekamatwa mkoani dodoma na maburungutu ya fedha hotelini, inasemekana alikuwa na lengo la kuwahonga wajumbe wampitishe mmoja wa gombea uteuzi... nani kamtuma?

Ilikuwa kama sinema wakati mabegi matatu yaliyokuwa yamesheni mamilioni ya fedha yalipokamatwa katika hoteli ya St. Gaspar mjini hapa, fedha zinazodaiwa kuwa zimetolewa na Mfanyabiashara Yusufu Manji, kwa nia ya kuhonga wajumbe wa vikao vya maamuzi vya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Fedha hizo zilikamatwa jana katika hoteli hiyo iliyopo eneo la Kisasa, zikiwa mikononi mwa mfanyakazi wa Kampuni ya Quality Group (T), Amit Kevaramani, akiwa na hati ya kusafiria M1470774 ya nchini India.

Quality Group (T) inamilikiwa na Yusuf Manji.

Kiasi cha fedha kilichokamatwa hakijaweza kuthibitika mara moja, ila waliohusika katika kamata hiyo na baadaye kushuhudia polisi waliofika eneo la tukio baada ya kuitwa kuhesabu, walisema zinafikia Sh. 725,2050,000.

Mbali na polisi, maofisa wengine wa vyombo vya usalama walioshuhudia rundo hilo la fedha za noti za Sh. 5,000 na 10,000 zikiwa zimefungwa kwa mabunda ya Sh. milioni 10 kila moja, ni maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Usalama wa Taifa.

Waliomkamata na fedha hizo walishtukia mwenendo wa mfanyakazi huyo, aliyeonekana akihamisha mabegi makubwa moja baada ya jingine kupeleka kwenye gari lililokuwa limeegeshwa nje ya hoteli hiyo likiwa na namba za usajili T687 ANQ Toyota Land Cruiser.

Katika hoteli hiyo ambayo kulikuwa na wajumbe wengi wa Mkutano Mkuu, na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM inadaiwa kuwa mamilioni hayo yalikuwa yanapelekwa kwa kambi ya mmoja wa wagombea watano waliopitishwa na Kamati Kuu, juzi usiku.

Katika simu ya mkononi ya mtuhumiwa huyo, ilipokaguliwa na waliomkamata zilikutwa jumbe fupi za maandishi (SMS) zilizotumwa kwake kutoka kwa mfanyabiashara (Manji) zikimueleza watu wa kuwapeleka fedha hizo.

Mfanyakazi huyo akizungumza kwa Kiingereza na Kiswahili cha kubabaisha, alipogundua kuwa amekamatwa, alijaribu kumhonga mwanamke mmoja begi moja lenye fedha, lakini alikataa na kuwaita watu wengine kushuhudia tukio hilo.

Katika simu yake, miongoni mwa waliotakiwa kupewa fedha ni Mbunge mmoja wa jimbo lililopo Dar es Salam ambaye alitakiwa kupewa milioni 10 kama mkopo na alitakiwa asaini vocha ya malipo.

Wengine walionufaika na mgawo huo, ni manaibu waziri wawili, mmoja milioni 15 na mwingine milioni 10.

Aidha, kwenye simu hiyo kulikuwa na orodha ndefu ya watu waliotakiwa kupewa fedha hizo.

Mbali na mfanyabiashara huyo kukamatwa na polisi, dereva kutoka kampuni ya Ngatuni Traders, Rashid Nkungu, ambaye alikodishwa na mfanyakazi wa Manji, aliwaambia waandishi wa habari kuwa alitumwa kwenda kuwapokea katika uwanja wa ndege wa Dodoma juzi asubuhi majira ya saa 1:30.

Alisema mfanyakazi huyo alikuwa amefuatana na wenzake watatu, wote wenye asilia ya Asia.

“Mimi hawa Wahindi wamekodisha gari katika ofisi yetu, mimi ni dereva nimewapokea uwanja wa ndege nikawaleta hapa St. Gaspar, walikuwa na mabegi yao kutoka uwanja wa ndege mpaka hapa walikuwa wanne,” alisema Nkungu.

Aidha, alisema kati ya abiria hao wanne, aliweza kumtambua mmoja wao ambaye ni Yusuph Manji na baadaye aliwatoa hotelini hapo na kuelekea Benki ya CRDB tawi la Dodoma.

Alisema aliwapeleka benki watatu na baadaye akawarudia wawili mmoja wao akabaki benki.

Walipofika hotelini abiria hao walimchukua mwenzao mmoja kisha wakaelekea uwanja wa ndege Dodoma.

“Hakuna Mswahili hata mmoja aliyekuja kuwapokea wote walikuwa Wahindi na hakuna mtu aliyekuja kuwapokea zaidi yangu mimi, kuna mmoja nilimtambua ambaye ni Manji,” alisema Nkungu.

Alisema baada ya kuwapeleka uwanja wa ndege, Nkungu alisema kuwa alipita benki kumchukua aliyebaki huko, alitakiwa aingize gari kwenye uzio wa benki, kisha alitoka mfanyakazi huo akiwa na begi.

“Baada ya kuwarudisha hapa nikalipwa hela kiasi cha Shilingi laki tatu nikaondoka, kurudi zangu nyumbani na tukaagana vizuri na leo asubuhi (jana) akanipigia tena nimfuate nimpeleke airport namba yake sikuwa nakumbuka inaishia namba 24,” alisema Nkungu.

Hata hivyo, alisema baada ya kufika na kumsubiri nje mfanyakazi huyo alitoka na kupakia kwenye gari begi la kwanza na kumtaka dereva huyo asikae ndani ya gari na pia akarudi kupakia begi la pili na kumwambia aendelee kusubiri nje, lakini baadaye akaona mtu anakuja na kupiga picha gari mbele na kuchukua ufunguo na kuzima gari.

Kwa upande wake, Meneja wa Hoteli hiyo, Denis Johannes, alisema mgeni huyo alipokelewa juzi katika hoteli hiyo akidai kuwa alitumwa na ubalozi wa India na kulazimika kumpatia chumba kimoja.

“Sisi kama hoteli mgeni tunamsikiliza na tuna uhusiano mzuri sana balozi zote Tanzania, Balozi yeyote yule akikosa nafasi tunampa kipaumbele, na walipoingia walisema wao wametumwa na balozi ya India, na kuangalia alivyo walisema wamekosa vyumba katika hoteli ya Moreno wakasema kwa hiyo wamekuja hapa,” alisema Meneja huyo.

Alisema awali aliwajibu kuwa hana taarifa za kuwapo kwa chumba kwa ajili yao, lakini kwa kuzingatia ushirikiano na balozi zilizopo wakaamua kumpatia chumba kimoja.

Hata hivyo, baada ya kukagua nyaraka za kujisajili kulala hotelini hapo, aligundua kuwa maelezo binafsi ya mteja huyo ni tofauti na alivyojieleza awali.

*Imeandikwa na Godfrey Mushi, Editha Majura, Jacqueline Massano na Agusta Njonji, Dodoma
via NIPASHE JUMAPILI

—————––—

Taarifa mpya kwa mujibu wa kituo cha runinga, ChannelTENMtu mmoja akamatwa fedha nyingi Dodoma


Katika hali ya kutatanisha raia mmoja mwenye asili ya Asia, Amit Kejalraman amekutwa na kiasi kikubwa cha pesa, bastola na risasi saba leo asubuhi katika hoteli ya Saint Gasper iliyopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.

Mtu huyo alishindwa kutolea maelezo fedha hizo jambo lililozua maswali mengi kwa mashuhuda na wakazi wa mjini Dodoma hasa wakati huu ambapo vikao vya juu vya CCM vinaendelea kuchuja majina ya kumpata mgombea urais kupitia chama hicho.

Taarifa za kukamatwa raia huyo aliyefahamika kwa jina la Amit Kejalraman mwajiriwa wa kampuni ya Quality Group ya Dar es Salaam, zimepatikana baada ya marafiki wa Edward Lowasa na baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM waliokuwa wakijiandaa na vikao vinavyoendelea mjini humo kuona raia huyo akiwa na mabegi matatu,  ambayo waliyatilia shaka na ndipo walipoamua kumuhoji.

Akizungumza na Channel TEN meneja wa hoteli ya Saint Gasper, Gasper Denis Johannes amesema alianza kumtilia shaka Amit kuanzia kwenye usajili wake hotelini hapo kwani maelezo yake yalikuwa yakitofautiana na taarifa alizotumia katika usajili.

Mtu huyo bado anaendelea kuhojiwa na TAKUKURU na jeshi la polisi kuhusiana na kukutwa na fedha hizo zaidi ya shilingi milioni mia sita.Zaidi ya picha zinazoonekana hapo ambazo wavuti.com imezipata kupitia mitandao ya kijamii, hakuna taarifa yoyote ya uhakika au iliyotolewa rasmi na vyombo vya usalama, kuhusu ni nani aliyekamatwa na makusudio ya kubeba kiasi hicho kikubwa cha fedha na uhusiano wake na vikao vya CCM vinavyoendelea huko Dodoma.

Hadi sasa zipo 'tetesi' tu katika blogu mbili ambazo zote zinaripoti taarifa zinazokinzana.

Blogu ya KajunaSon inasema:
Katika hali ya kushangaza mtu mmoja mwenye asili ya Kuburushi ambaye jina lake halikuweza kupatikana leo amekamatwa na marundo ya hela kwenye begi ikiwa amefika nazo kwa ajili ya kuzigawa kwa wajumbe wa NEC ili wasusie kikao cha leo hadi pale jina la Mhe. Edward Lowassa litakaporudishwa na kama ikishindikana achaguliwe Mhe. Magufuli.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na makachero wenu waliopo maeneo mbali mbali ya mji wa Dodoma zinasema kuwa watu hao walikamatwa katika hoteli ya St. Gasper iliyopo nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Mpaka sasa hali si shwari kwa mji wa Dodoma maana vijana wengi wamezagaa kila kona huku ulinzi ukiwa umeimalishwa.
Mhindi huyo alishukia kwenye hoteli ya St. Gasper ambayo wapambe wengi wa Lowassa wakiwamo mzee Kingunge ambaye wamepiga kambi.
Huyo Mburushi ni mtumishi wa Caspian ya Rostam Aziz. Wengine walioonekana pichani wamo Fadhili Ngajiro; Ole Porokwa; Omar Ng'wanang'wala.
Blogu ya Malunde1 inasema:
Kuhusu taarifa za kijana aliyenaswa na masanduku ya fedha upekuzi bado unaendelea kwenye eneo la tukio ambo taarifa zisiso rasmi zinadai kuwa kijana huyo alikamatwa na wafuasi wa Mh.LOWASSA ambao waliweza kuripoti Polisi na Takukuru na inadaiwa kuwa fedha hizo zilipelekwa kwa ajili ya kugawia wajumbe waweze kumchagua mmoja wa wagombea.
Aliyekamatwa kageuka, anasema katumwa na MembeTaarifa zaidi tutawafahamisha kadiri zitakavyo thibitishwa na mamlaka zinazoendelea na Uchunguzi.

Tony Elumelu Entrepreneurship Programme to transform Tanzanian Emerging Entrepreneurs
The Managing Director of UBA Tanzania Mr. Demola Ogunfeyimi addresses the Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship Programme (TEEP) Entrepreneurs heading for the training in Ota Nigeria from Tanzania during the send off dinner in Dar es Salaam organized by United Bank for Africa Tanzania.


The Managing Director of UBA Tanzania Mr. Demola Ogunfeyimi addresses the Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship Programme (TEEP) Entrepreneurs heading for the training in Ota Nigeria from Tanzania during the send off dinner in Dar es Salaam organized by United Bank for Africa Tanzania.


Head Marketing & Corporate Communications UBA Tanzania M/s. Josephine Lukoma addresses the Tony Elumelu Foundation Entrepreneurship Programme selected emerging entrepreneurs and media not in picture during the send off dinner in Dar es Salaam organized by United Bank for Africa Tanzania.


UBA Tanzania Staff having a light moment with their Managing Director Mr. Demola Ogunfeyimi during the send off dinner organized by United Bank for Africa Tanzania for the selected TEEP emerging Entrepreneurs from Tanzania heading for the training in Ota Nigeria held in Dar es Salaam.


Mercy Kitomari one of the selected emerging entrepreneurs shows her joy as UBA staff escort her and the other entreprenueurs, at the extreme left Nsajigwa Mwasege all happy to head for the training in Ota Nigeria.


The selected TEEP emerging Entrepreneurs from Tanzania heading for the training in Ota Nigeria, enjoying the dinner organized for them by United Bank for Africa Tanzania in Dar es Salaam.


The selected TEEP emerging Entrepreneurs from Tanzania heading for the training in Ota Nigeria, enjoying the dinner organized for them by United Bank for Africa Tanzania in Dar es Salaam.


The selected TEEP emerging Entrepreneurs from Tanzania heading for the training in Ota Nigeria, enjoying the dinner organized for them by United Bank for Africa Tanzania in Dar es Salaam.


Mercy Kitomari one of the selected emerging entrepreneurs, speaking to the media.


Picha mbalimbali kutoka kwenye vikao vya CCM, Dodoma


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wajumbe baada ya kuwasili ukumbini kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, leo katika Ukumbi wa jengo la White House mjini Dodoma. Kikao hicho ni cha kuchagua wagombea watatu kati ya watano waliopitishwa na Kikao Cha Kamati Kuu ya CCM kwa ajili ya kuwania kugombea Urais kwa tiketi ya CCM. Watatu watakaopatikana leo, watapelekwa kuigiwa kura katika Mkutano Mkuu wa CCM ili kupata mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi huo mkuu. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dk. Ali Mohamed Shein na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM, Rutaraka atanagza kuwania Ubunge Moshi Mjini


Mtangaza nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini, Edmund Rutaraka akiwasili katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, kwa ajili ya kikao na wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho wa wilaya chenye lengo la kutangaza azma yake ya kugombea Ubunge katika jimbo hilo.

Ndani ya Kikao cha CCM wakiimba, "Tuna imani na Lowasa"M-NEC Nazir Karamagi asema NEC ina madaraka ya kubadili mapendekezo


Kauli ya Ngeleja baada ya kuchujwa


Kauli ya Wasira baada ya kuchujwa


Masaburi ajeruhiwa ikihusishwa na masuala ya siasa

Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea, Steve Massaburi akiwa Hospitali ya Aga-khan leo akiendelea na matibabu.

WATU wasiojulikana wamejeruhi kwa mapanga Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea Steve Massaburi usiku wa kuamkia juzi nje ya nyumba yake alipokua akirejea kutoka matembezini.

Kwa mujibu wa Steve aliyelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, watu hao wapatao wanne wakiwa na Pikipiki, walimvamia majira ya saa tatu usiku nje ya geti la nyumba anayoishi na kuanza kumshambulia huku yeye akijaribu kupambana nao.

Steve ambaye ni mtoto wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam Dk. Didas Massaburi, alisema wakati watu hao wakimshambulia walikuwa wakisema wazi wazi kuwa lengo lao ni kumuona hagombei nafasi ya udiwani katika Kata hiyo ya Segerea baada ya yeye kuonyesha nia ya kutaka kugombea nafasi hiyo.
“Walikuwa wakiniambia kuwa wewe si unautaka udiwani sasa utaugombea ukiwa kitandani au kaburini, hapa hakuna na umaharufu wa mtu kwa kuwa kila mtu anaitaka nafasi hiyo” 
alisema Massaburi.

Alisema wakati akiendelea kupambana na watu hao alikuwa akipiga kelele jambo lililowafanya watu hao kumuacha na kasha kukimbia huku yeye akiwa amelala chini damu zikimtoka sehemu za shavuni kutokana na panga alilopigwa.

Pamoja na sehemu ya shavuni, watu hao pia wamemjeruhi sehemu mbalimbali za mkono wake wa kushoto alipokuwa akijaribu kuzuia panga kumdhuru sehemu za usoni.
“Kelele nilizopiga ndizo zilizonisaidia kwa kuwa ziliwafanya watu watoke katika majumba yao kuja kunisaidia wakati huo huo watu hao wakikimbia kwa kutumia pikipiki zao mbili walizokuwa wamekuja nao” 
aliongeza.

Alisema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri tangu alipofikishwa hospitalini hapo jana huku akishonwa nyuzi zaidi ya ishirini katika taya lilipigwa na panga na watu hao. 


Katibu wa Uchumi na Fedha Kata ya Segerea, Steve Massaburi akiwa Hospitali ya Aga-khan leo akiendelea kuuguza majeraha baada ya kujeruhiwa kwa mapanga nyumbani kwake Segerea jijini Dar es Salaam jana na watu wasiojulikana. Kushoto anayemuhudumia ni jamaa yake Martin Pemba.
Taarifa ya Na Dotto Mwaibale
Imeandaliwa na mtandao wa www.habarizajamii.com - simu namba 0712-727062

Taarifa ya asubuhi ChannelTEN, Julai11, 2015


Taarifa ya kutwa Channel TEN, Julai 10, 2015
Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Julai 11, 2015

Fuatilia LIVE mkutano mkuu wa CCM kupitia hapa