Mfanyabiashara maarufu Mwanza awapiga risasi wenzake

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia mfanyabiashara maarufu Jijini humo Juma Mahende, anayemiliki Mabasi ya J4 kwa tuhuma ya kuwapiga risasi watu wawili na kuwapotezea maisha, katika eneo la Boma lililopo kata ya Nyakato Jijini humo.

Ni nyumbani kwa Marehemu Cloud Skalwanda, eneo la Nyasaka kata ya Kiloleli wilayani Ilemela Jijini Mwanza, ambako ndugu, jamaa na marafiki wa Marehemu, wamekutana kuomboleza msiba huo.

Tukio hilo limetokea majira ya saa nne usiku wa kuamkia leo katika eneo la Boma lililopo kata ya Nyakato, baada ya mtuhumiwa Juma Mahende kumuita Marehemu Cloud Skalwanda, na mwenzake Ally Mohamed mkazi wa kata ya Igoma kuzungumza masuala ya kibiashara.

Baada ya tukio hilo nyumbani kwa Marehemu Ally Mohamed kata ya Igoma, simanzi na vilio pia vikatawala, huku chanzo cha mauaji hayo kikielezwa kuwa marehemu hao walikuwa wakimdai mtuhumiwa shilingi milioni 25/=.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Charles Mkumbo, amesema kuwa tayari Jeshi la Polisi mkoani hapa, linamshikilia mtuhumiwa Juma Mahende kwa uchunguzi zaidi.
  • via Channel TEN

Prof. Mbele leo anawashangaa CCM

Kwenye blogu yake, Prof. Mbele leo anaeleza kushangazwa kwake na baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, "wanaolalamikia mchakato wa chama chao wa kumpata mgombea urais."
Mwaka 2010 CHADEMA walilalamika sana kwamba wamefanyiwa rafu na CCM. Hakuna yeyote katika CCM aliyewasikiliza CHADEMA, wala kuwaonea huruma. CCM wote waliibeza CHADEMA, kwamba ingojee uchaguzi ujao. Sasa leo wanalalamika kuwa wamefanyiwa rafu huko huko CCM. Sio kwamba hao wanachukia rafu. Wanalalamika kwa sababu rafu wamefanyiwa wao. Mimi kama raia ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa naona kuwa hawana sababu ya kulalamika, kwani wanavuna walichopanda.

Labda watajifunza umuhimu wa kutetea haki wakati wote na kwa yeyote. 

Mgombea Urais Tanzania 2015 kutoka UKAWA...


Mgombea urais ndani ya UKAWA kuja kutangazwa kwa shamrashamra ni ndani ya siku saba.

Ni baada ya kikao (summit) kukamilisha maridhiano ambapo kilizungumzia jinsi gani ya kuachina majimbo yalibaki na swala la mgombe urais

Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa NCCR Mageuzi JAMES MBATIA aliwaeleza wanahabari kuwa taratibu zote zimekamilika ndani ya vyama vinavyounda UKAWA na kilichobaki ni jinsi gani ya kumtangaza mgombea urais ndani ya UKAWA kwa kushirikiana na vyama vyote vinavyounda umoja huo, ndani ya siku saba .

Huku akiwasisitiza watanzania kuwa wavumilivu na kuwataka wajitokeze kujiandikisha katika daftari la kudumula wapiga kura linalotegemewa kuanza punde katika mkoa wa Dar es Salaam huku wakitega maskio yao na kumpokea mgombea urais ambaye atatambulishwa kuipeperusha bendera kupitia UKAWA.

Akijibu swali la mwandishi wa habari aliyeuliza swali
Je, ni kweli kama ilivyotapaka katika mitandao ya jamii juu ya Lowassa Kujiunga na chama kimojawapo ndani vyama vinavyounga UKAWA?

Akijibu swali hilo kwa kulitolea mifano ya mitandao ya jamii inayotumika na watu fulani kwa maswai yao binafsi na sio kuelimisha jamii, Mh Jamse Mbatia ilizungumzia moja ya account ya twitter iliyofunguliwa kwa jina mtandao mkubwa duniani BBC ikieleza kuwa Lowassa tayari ameshajiunga katika chama cha ACT na kusisitiza habari hizo sio za kweli huku akiwashauri watanzania kupima uzito wa habri na chombo kinachokiwasilisha na kuwataka wananchu wafatilie habari za vyama kupitia mitandao ya vyama.
  • via CHADEMA blog
Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA vimetangaza rasmi kufikia makubaliano ya kusimamisha mgombea mmoja wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Akitangaza makubaliano hayo mara baada ya kumalizika kwa kikao kirefu kilichokuwa kikijadili mustakabali wa kumpata mgombea urais pamoja na ugawanaji wa majimbo mapya, mwenyekiti mweza wa UKAWA James Mbatia amesema kuwa umoja huo umemteua mgombea ambaye ni chaguo la watanzania.
“Mgombea tutakayemtaja ndiye chaguo la watanzania” 
Amesema Mbatia

Mbatia amegoma kutaja jina la mgombea aliyepitishwa na umoja huo na kusema kuwa atatangazwa siku chache zijazo kwa madai kuwa anaandaliwa utambulisho maalum utakaoambatana na shamra shamra.
“Tayari jina tunalo lakini tutaliweka hadharani baada ya siku mbili tatu hivi, na tutamtoa kwa kimasomaso”

Katika kikao hicho kilichomalizika majira ya saa 3:30 usiku kikihusisha wenyeviti wa vyama hivyo pamoja na kamati ya ufundi ya UKAWA, mwenyekiti mwenza wa UKAWA kutoka chama cha wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba hakuweza kuhudhuria.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka CUF, chama hicho kilimuagiza Naibu Katibu Mkuu wa CUF Magdalena Sakaya kuiwakilisha, lakini baadaye Sakaya aliondoka katika kikao hicho bila maelezo yoyote.

Mkurugenzi wa mawasisliano wa chama hicho bwana Abdul Kambaya alipoulizwa kuhusiana na hilo akasema kuwa hakuna mwakilishi yeyote wa CUF aliyekuwepo kikaoni hapo hadi kikao hicho kinamalizika.

Mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk Mohammed alipoulizwa kuhusiana na kukosekana kwa Prof Lipumba kikaoni hapo amedai kuwa Prof Lipumba ni mgonjwa, na hali yake ya kiafya haimruhusu kuhudhuria kikao hicho.

“Mwenyekiti wetu ni mgonjwa, alikuwa safarini kutoka Kigoma, amerejea lakini hali yake si nzuri, ameshikwa na Malaria kali sana na miguu pia inamsumbua” Amesema Rajab Mbarouk.

Viongozi waliokuwepo wakati wa mazungumzo na waandishi wa habari ni James Mbatia, Freeman Mbowe, Tundu Lissu, John Mnyika, Emmanuel Makaidi, Dkt Wilbroad Slaa, Dkt George Kahangwa (mgombea urais kupitia NCCR) na mtu anayetajwa kuwa mwakilishi kutoka chama cha CUF. 

[via EATv]Afisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Tumaini Makene akizungumza na waandishi habari hivi punde juu kinachoendelea katika mkutano wa kutafuta mgombea wa Urais kwa tiketi ya UKAWA, uliofanyika katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam.

Makene amesema majadiliano yao siyo ya urais tu bali kuna mipaka ya majimbo mapya jinsi watavyojipanga katika kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. 

Makene amewataka waandishi wa habari wawe na subira kwa ajili ya maamuzi yatakayotoka katika kikao hicho ambacho kimeanza tangu asubuhi ya leo.

Baada ya kusubiri kwa muda mrefu tangu mchana, waandishi wa habari waliopiga kambi wakisubiri kupata jina la mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA katika hoteli ya Colosseum Masaki leo jijini Dar es Salaam wakajikuta wanaacha stendi za kamera zao na kukaa pembeni kama zionekanavyo pichani usiku huu, wakisubiri lolote litakalojiri.Waandishi wa Habari wakiwa wameweka kambi tangu saa saba mchana wakisubiri kupata jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA katika Hoteli ya Colosseum Masaki leo jijini Dar es Salaam, hiyo inatokana na taarifa zilizotolewa na UKAWA kuwa leo ndiyo siku rasmi ya kutangaza jina hilo, lakini saa zinazidi kwenda huku kikao chao kikiwa kinaendelea.


  • Taarifa mpya zikipatikana zitawekwa kwenye chapisho hili kama 'updates/taarifa mpya'

Mwandishi wa habari DIMBA atangaza kuwania Ubunge Same

Ahadi Kakore
Ahadi KakoreMwandishi wa gazeti la DIMBA, Ahadi Kakore ametangaza nia yake ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Same Magharibi, Kilimanjaro, kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kakore alisema kuwa baada ya kujipima na kutafakari juu ya matatizo yaliyopo kwenye Jimbo la Same Magharibi ameamua kuwania nafasi hiyo ili kupeleka mbele maendeleo yaliyokwama kwa miaka mingi.

Alisema kuwa Jimbo la Same Magharibi ni miongoni mwa majimbo yenye matatizo mengi ikilinganishwa na maeneo mengine katika mkoa wa Kilimanjaro jambo alilodai kuwa kwa wakati huu anahitaji mtu makini, anayefahamu matizo ya Wanasame lakini mwenye uwezo wa kuyashughulikia kwa uhakika.
“Nimetafakari kwa kina nikajipima nikaona kuwa wakati wa kuwatumikia Wanasame Magharibi umefika na kwa muda mrefu wamekuwa wakihitaji mtu makini na mwenye uwezo wa kuwasaidia wananchi kulingana na matatizo waliyonayo.
“Naelewa Same tangu Uhuru tuna matatizo ya Barabara, Maji, Afya, Mazingira na Michezo mambo ambayo yamekuwa ni kero kwa miaka mingi hivyo zinahitaji mtu makini na kijana ambaye anaweza kusaidia kuyatatua kwa haraka na wakati unaofaa,” 
alisema Kakore.

Kakore ni mwandishi mkongwe wa habari za michezo kazi ambayo ameifanya kwa zaidi ya miaka 15 ambapo alishafanya kwenye vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya Tanzania.

Jimbo la Same Magharibi kwa sasa linashikiliwa na David Mathayo David ambaye amekaa kwenye kiti hicho kwa miaka 10 tangu mwaka 2005 hadi sasa. Mionggoni mwa watu wa kwanza kuwa wabunge kwenye Jimbo hilo ni aliyewahi kuwa waziri katika katika serikali ya awali ya kwanza, Marehemu Chediel Mgonja.

Hasara kwa kulifanyia mtaji wa biashara jina la Lowasa


Hiyo ni moja ya picha nilizozipata huko WhatsApp na kwenye 'social media', inawezekana kabisa kuwa biashara nyingi zilipangwa kwa kutumia jina la Lowasa kama mtaji kwa imani kuwa angekuwa Rais wa Tanzania mwaka huu.

Hata hivyo walisema wahenga kuwa huwezi kufanikiwa usipojaribu na katika biashara kuna kupata na kukosa. Hivyo, pamoja na hasara, isiwe ndiyo mwisho wa kujaribu baada ya kujifunza.


Ni vyema kuifanyia biashara siasa katika uimla wake. Badala ya kujikita kwenye kufanya biashara ya mgombea fulani, ni afadhali kuwekeza kwenye chama kwa sababu wataendelea kubakia wanachama katika chama hicho licha ya kuwepo tofauti za wagombea au hata wanachama wake.

Njia ya mkato ya kutafuta kujipatia kipato kikubwa kwa haraka katika muda mfupi ni sawa na kucheza kamari kwa imani kuwa mzunguko unaokuja ndiyo nafasi yako ya kuvuna mamilioni, ukasahau kuwa mnaotarajia hivyo mpo wengi zaidi ya nafasi.

Mwania Urais kuishitaki CCM kortini isipomrejeshea milioni aliyochukulia fomu

Three ways to keep your retirement savings on track


Saving for retirement doesn't have to be hard or time-consuming. Once you've got the right investment strategy, three easy steps can keep you on track:

  1. Put your savings on autopilot.
  2. Resist the urge to tinker with your accounts.
  3. Check in on your accounts—occasionally.
Learn more about saving for retirement with the guidance and financial planning tools at investor.vanguard.com

Tangazo la kazi: Bodi ya mishahara na maslahi katika utumishi wa umma

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

BODI YA MISHAHARA NA MASILAHI KATIKA UTUMISHI WA UMMA

TANGAZO LA KAZI YA MUDA

WAKUSANYA TAARIFA ZA TATHMINI YA KAZI – (NAFASI 50)

Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma ambayo imeanzishwa kwa Hati Maalum iliyotolewa kwa Tangazo la Serikali Na. 162 la tarehe 3 Juni, 2011. Majukumu ya Bodi ni kufanya mapitio ya mara kwa mara ya viwango vya mishahara, posho na mafao mengine na kumshauri

Rais juu ya misingi ya miundo ya mishahara katika utumishi wa umma.

Katika mwaka wa fedha 2015/16, Bodi inatarajia kufanya Tathmini ya Kazi katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kuoanisha na kuwianisha mishahara. Bodi inahitaji watumishi 50 watakaomsaidia Mtaalam Mwelekezi kukusanya taarifa za awali:

a) Sifa za mwombaji

i) Mtumishi wa Umma;

ii) Elimu ni kuanzia shahada ya kwanza au stashahada ya juu na kuendelea;

iii) Uwezo wa kujieleza kwa ufasaha kwa Kiswahili na Kiingereza;

iv) Mwenye maadili, uwezo wa kufanya kazi inayozingatia matokeo, kujituma na kukamilisha malengo kwa wakati; na

v) Uelewa wa kutumia kompyuta.

b) Kazi za kufanya

i) Kuwahoji watumishi wa Umma na kujaza dodoso la kukusanyia taarifa;

ii) Kuingiza taarifa za madodoso kwenye mfumo wa kompyuta; na

iii) Kazi nyingine zinazohusiana na Tathmini ya Kazi kwa maelekezo ya msimamizi.

c) Mshahara

Waombaji watakaofanikiwa, kwa kuwa ni watumishi wa umma, wataendelea kulipwa mishahara yao kama ilivyo sasa. Aidha, Bodi itagharamia mafunzo na posho za safari za kikazi kwa viwango vya Serikali.

d) Muda wa Kazi

Kazi hii inatarajiwa kufanyika kwa jumla ya miezi 15. Hata hivyo, kazi ya mtumishi mmoja mmoja haitazidi siku 100.

e) Namna ya kuwasilisha maombi.

i) Maombi yote yaambatanishwe na Maelezo binafsi (CV), nakala za vyeti vya elimu ya juu na mafunzo ya kompyuta;

ii) Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya mtandao kwa kupitia anwani ya: [email protected]; na

iii) Maombi yote yapitishwe na waajiri wenyewe.

f) Mwisho wa kupokea maombi

Zoezi la kupokea maombi litafungwa tarehe 31/07/2015.

Tanbihi: Watumishi wanaofanyakazi katika Mamlaka za Serikali za Mtaa wanahimizwa kuleta maombi yao.

IMETOLEWA NA KATIBU MTENDAJI
BODI YA MISHAHARA NA MASILAHI KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Job opportunity at CRDB for a Bank Officer TraineeCRDB Bank PLC is urgently looking for suitable person to fill a vacant position of Bank Officer Trainee.

The ideal candidate will be candidate with Bachelors degree in business or related discipline from any recognized University.

How To Apply:

Interested candidates Apply through CRDB online Recruitment Portal - Recruitment.crdbbank.com

Or should submit an Application Letter accompanied with copies of academic transcript, certificates and with a detailed up to date CV with two work related referees addressed to;

Director of Human Resources
CRDB Bank PLc
P.O.Box 268,
DAR ES SALAAAM

Closing Date: 01-Aug-2015

Aliyekamatwa na masanduku yenye mabunda ya fedha arejeshewa milioni 700/= zake

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA


Napenda kutoa taarifa fupi kuhusu tukio lililotokea tarehe 11/07/2015 majira ya saa 10:00 hrs huko katika Hoteli ya St. Gasper hapa mjini Dodoma, kuwa wananchi walitoa taarifa majira ya saa 10:00 hrs kwamba kuna mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia amekamatwa na wananchi akiwa na fedha nyingi na kuna vurugu kubwa. Baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilifika eneo la tukio ili kuona kama taarifa hizo ni za kweli.

Askari walithibitisha kuwa ni kweli walimkuta mtu mmoja mwenye asili ya Kiasia ambaye alijulikana kwa jina la AMIT KEVALRAMANI mwenye umri wa miaka 31, Mhindi, Mfanyabiashara, Mkazi wa Dar es Salaam akiwa na fedha kiasi cha Tshs. 722,500,000/= ambacho alipohojiwa alisema kuwa tarehe 10/07/2015 alifika Dodoma kwa ajili ya ununuzi wa mazao ya nafaka. Alipofika Dodoma tarehe 10/07/2015 majira ya asubuhi alifikia katika Hoteli ya St. Gasper na tarehe 11/07/2015 aliamua kurudisha fedha benki kutokana na kuona mkusanyiko wa watu wengi wasioeleweka na wenye viashiria vya vurugu.

Akiwa katika harakati ya kurejesha fedha hizo benki, ndipo kundi la watu waliokuwa katika eneo la Hoteli ya St. GASPER walimtilia mashaka na kumzuia asiondoke na ndipo taarifa zilitolewa polisi. Mashaka ya watu hao yalitokana na vuguvugu za kisiasa/mchakato wa uchaguzi kati ya makundi
mbalimbali kuwa kuna watu wanahonga wajumbe. Taarifa za aina hiyo ambazo hata Jeshi la Polisi lilikuwa limepokea bila uthibitisho.

Katika tukio hili na uchunguzi tulioufanya tumebaini kuwa hakuna kosa la jinai lililothibitika licha ya kukutwa na kiasi hicho cha fedha, tuhuma za rushwa ambazo ndiyo zilikuwa msingi wa ukamataji wa mtu huyo hazikuthibitika, kwa kuwa hakuna aliyeona akizigawa fedha hizo wala hakuna aliyedai kushawishiwa au kugawiwa fedha hizo.

Aidha imethibitika fedha hizo ni mali yake halali na kwa kuwa hakuna ushahidi mwingine uliyo thibitisha vinginevyo amerejeshewa fedha zake.

Mtangazaji wa RFA 'Kijukuu cha Bibi' atangaza kuwania Ubunge

Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi” akiwa amebebwa juu na wakazi wa Ushetu wakati wa mkutano wake wa kutangaza nia kuwania ubunge katika jimbo jipya la Ushetu wilayani Kahama
Siku moja tu baada ya Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania kutangaza majimbo mapya ya Uchaguzi, Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa (RFA) William Bundala maarufu kwa jina la “Kijukuu cha Bibi K” ametangaza rasmi kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania Ubunge katika Jimbo la jipya la Ushetu katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga, kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Bundala ametangaza kuingia kwenye mchakato wa kugombea kuteuliwa na chama ili aweze kupeperusha bendara ya CHADEMA/UKAWA katika uchaguzi mkuu ujao katika mkutano wake wa kutangaza nia uliofanyika katika Kijiji cha Bogomba “B” kata ya Ubagwe wilayani Kahama.

Mtia nia huyo alisema endapo chama chake kitampitisha na hatimaye kushinda Ubunge katika Jimbo hilo atahakikisha anasukuma kasi ya maendeleo katika jimbo hilo jipya lenye rasimali nyingi kupitia nafasi yake na wajibu kama anavyotakiwa Mbunge kufanya.

William Bundala
William Bundala 

Alisema kuwa dhamira yake imemsuta kwenda kuwatumikia wananchi wa wilaya hiyo ambayo yeye ni mzawa na kuwa atahakikisha anapigania maendeleo ya wananchi kwa kasi huku akiondoa uonevu kwa waandishi wa habari na watumishi wengine serikalini na katika halmashauri za wilaya.

Sambamba na hayo amesema kuwa sababu nyingine iliyomsukuma ni kuona wagombea wengine wanaolitaka jimbo hilo hawako kwa ajili ya ukombozi wa jimbo hilo bali wako kwa ajili ya maslahi binafsi kutokana na asilimia kubwa ya wagombea hao si wakazi wa eneo hilo na kwamba hawafahamu matatizo ya wana Ushetu kama anavyoyafahamu yeye.

Aliongeza kuwa akifanikiwa kuukwaa Ubunge pia atasimamia kuhakikisha Jimbo hilo jipya linapata Chuo cha ufundi kwa ajili ya vijana wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne kupata elimu jambo lilatalopunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana.

Bundala alisema kipaumbele kingine atakachoshughulikia ni pamoja na kusimamia na kutoa elimu ya sheria kupitia wanasheria ambao watazunguka katika kata kutoa elimu hiyo hususan katika maswala ya umiliki wa ardhi, mirathi, haki za wakulima na wafugaji pamoja na haki za raia na mali zao kwa ujumla.

Akizungumzia kuhusu suala la michezo katika jimbo hilo, Bundala alisema kuwa kupitia Kijukuu Cup atahakikisha anashirikiana na halmashauri na wadau wa michezo kuhakikisha halmashauri ya ushetu inapata timu ya kucheza ligi kuu Tanzania Bara.

Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CHADEMA (BAVICHA) Halmashauri ya Ushetu Emmanuel Magema aliwataka vijana wote kuungana ili kumuunga mkono kijana mwenzao aliyejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kuongoza akiwa Mbunge wa jimbo hilo.

Wilaya ya Kahama kwa sasa ina halmashauri za wilaya tatu za Msalala, halmashauri ya mji wa Kahama na halmashauri mpya ya Ushetu na kufanya majimbo ya uchaguzi kuwa matatu.

Katika kinyang’anyiro cha Ubunge katika jimbo jipya la Ushetu kuna watu zaidi ya watano wanaotajwa kulimendea jimbo huku wagombea wa CHADEMA wakionekana kuungwa mkono na makundi mengi hususan vijana.Mwandishi wa habari na mtangazaji wa Radio Free Africa William Bundala maarufu kwa jina la “kijukuu cha bibi k” akizungumza na wakazi wa Ushetu wakati wa mkutano wake wa kutangaza nia kuwania ubunge katika jimbo jipya la Ushetu wilayani Kahama

  • Imenukuliwa kutoka Malunde1 blog, Ushetu

Mjue Daniel Mzena, mchora vibonzo/katuni za uchaguzi zinazovuma MwananchiRais Kikwete aelekea Geneva kwa ziara ya kikazi

Rais Jakaya Mrisho kikwete akiagana na makada wa CCM wakati akiondoka leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Dar es salaam kuelekea Geneva kwa ziara ya kikazi. Makada hao walikuwa uwanjani hapo kwa mapokezi ya mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli

Rais Jakaya Mrisho kikwete akiagana na makada wa CCM wakati akiondoka leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa 
wa Dar es salaam kuelekea Geneva kwa ziara ya kikazi. Makada hao walikuwa uwanjani hapo kwa mapokezi ya mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli

Rais Jakaya Mrisho kikwete akiagana na makada wa CCM wakati akiondoka leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa 
wa Dar es salaam kuelekea Geneva kwa ziara ya kikazi. Makada hao walikuwa uwanjani hapo kwa mapokezi ya mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli

Rais Jakaya Mrisho kikwete akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Said Meck Sadick wakati akiondoka leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kuelekea Geneva kwa ziara ya kikazi.

Rais Jakaya Mrisho kikwete akiagana na Mkuu wa Majeshi Jenerali davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshio la Polisi IGP Ernest Mangu wakati akiondoka leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kuelekea Geneva kwa ziara ya kikazi.

Mapitio ya magazeti kwenye Tv, Julai 14, 2015
British High Commission in Tanzania trains and hands aviation security equipment to TCAA

Acting High Commissioner, Ms Penny Smith giving her keynote address during closing of training course and handling of aviation security equipment along side are Vicky Hutchinson (RASLO) and TCAA Director General, Mr Charles Chacha and Director Safety Regulations, Mr Redemptus Bugomola (dressed in tie)

Acting High Commissioner, Ms Penny Smith hands over aviation security equipment to Director General of Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA), Mr. Charles Chacha

Acting High Commissioner, Ms. Penny Smith hands over a certificate to one of the participant of the training course.

D&T Certified Trainer, Mr. Simon C. Bolt show-case the usage of one of the aviation security equipment . Looking are; Vicky Hutchinson, (RASLO), Acting High Commissioner, Ms. Penny Smith and Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA) Director General, Mr. Charles Chacha.

Capacity Africa, the only pan-African wholesale telecommunications event, to take place in Dar es Salaam


PRESS RELEASE

The international telecoms community regards Africa as an area of high value for new business

DAR ES SALAAM, Tanzania, July 14, 2015/ -- Africa’s telecoms industry forms a vital component to the country’s economic growth, affecting all aspects of the business and social sphere. Dramatic expansion in the telecoms sector has taken place over the past five years, with a 72% penetration on average in mobile subscriptions across the continent.

Consequently, a huge amount of investment is happening to improve Africa’s infrastructure to manage the rapid increase in data usage and the need for better connectivity, particularly in rural areas. For example, Millicom Ghana (Tigo) is to invest $24 million in the expansion of its 3G network in the country, according to local reports, with phase one of the expansion expected to include 114 cell sites installed in the Greater Accra, Ashanti and Western regions of Ghana over the next four months.

The international telecoms community regards Africa as an area of high value for new business. In East Africa for example, the construction of a fibre ring connecting five East African countries (Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda and Burundi) has just been completed by Liquid Telecom, to ensure reliable and continuous connectivity. Amb Dr Richard Sezibera, Secretary General of the East African Community (EAC), the regional intergovernmental organisation of the five countries, said of the deployment: "By providing our nations with a 21st-century broadband network that directly connects us to each other and the outside world, Liquid Telecom continues to help the economic development of our region."

Due to the size and scale of investment opportunities in African telecoms, wholesale telecoms carriers from across the globe meet annually at Capacity Africa, the largest pan-African wholesale conference to network, develop business and hear industry leaders deliver future commercial strategy. Taking place on 8 & 9 September in Dar es Salaam, 400+ senior telecoms executives from over 65 countries will take advantage of the entire African telecoms ecosystem being represented, all looking to secure new deals in the region’s lucrative telecoms market.

Discussing the event’s importance, Mike Last, Director, Marketing and International Business Development, WIOCC said: “Capacity Africa is without a doubt the best networking event for the African wholesale telecoms industry.” He added that it attracts “a very strong set of African and international carriers and creates a great environment for doing business”.

Expanding networks means increased demand for infrastructure and competition amongst operators. Regulators are playing a key role in providing stability to these operators active in the region ensuring a market driven industry. Capacity Africa recognises this, offering an agenda which brings together both the C-level executives of major telecoms organisations such as Seacom, Liquid Telecom and WIOCC, as well as the regulators such as the Nigeria Communications Commission to discuss the latest growth opportunities in front of an audience made up of the key decision makers in African telecoms.

To find out more information about Capacity Africa 2015, please visit www.capacityconferences.com/Capacity-Africa or contact Simon Murray on [email protected]

To read the latest reports on the critical business issues wholesale carriers face in this rapidly changing telecoms market, subscribe to Capacity Magazine for free today at www.capacitymagazine.com

Successful Tanzanian Women in the spotlight: Intereview with Dr MweleThe host of the show Fatema Dewji-Jaffer, during the interview with Doctor Mwele Malecela.

Educate, Empower and Inspire is a women’s empowerment show. The aim of this show is to put successful women in the spotlight and get a glimpse as to how they are making a difference to our society and how much hey can inspire others to do the same.

I interviewed a girl who dreamed about being a researcher, about a passionate woman who climbed the hills of Amani in search of that dream, and the woman who is living that dream doing research and contributing to the control of a disease she has worked on all her life!

Fatema Dewji-Jaffer conducted an interview with Doctor Mwele Malecela, Check out the full interview below:Kipindi cha "Jukwaa Langu" Julai 13, 2015Kipindi hiki ambacho kinakujia kila JUMATATU, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

Katika kipindi hiki utasikia mahojiano yetu na watu mbalimbali akiwemo Katibu Uenezi na Itikadi wa CCM Ndg. Nape Nnauye kuhusu DEMOKRASIA kuelekea uchaguzi nchini Tanzania

KARIBU