Mwenyekiti wa walemavu achukua fomu za Ubunge Kawe

Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Anastaz Mpanju ambaye pia alikuwa Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba Mpya amejitokeza hii leo sambamba na wana CCM wengine katika safari ya kuwania Ubunge katika Jimbo la Kawe Wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza katika ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, Mpanju amesema huu ni wakati muafa kwake kuwatumiakia wana Kawe.

Mpanju ambaye kitaaluma ni Mwanasheria, amesema wanakawe wananafasi sasa ya kuandika historia ya aina yake si tu kumchagua mtu mlemavu bali kumchagua, kijana na mchapakazi mwenye uwezo wa kutetea na kuwasilisha hoja za kuleta maslahi kwa kawe na taifa.
“Huu ni wakati wa wananchi wa Kawe kuandika historia ya aina yake, sit u kwa kumchagua mtu mwenye ulemavu kuwaongoza bali kijana mwenye uwezo wa kutetea hoja na maslahi yua wananchi na taifa kwa ujumla,”
alisema Mpanju.

Mpanju amekuwa ni mwananchi wa 16 kujitokeza kugombea jimbo la Kawe na ni mwana CCM wa 39 kujitokeza kuomba ridhaa ya chama kuteuliwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya chama hicho.
“Mimi nitoe wito kwa watu wote wenye ulemavu nchini ambao wanasifa na vigezo vinavyotakikana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi nchini wajitokeze na kufanya hivyo na watatendewa sawa sawa na wengine bila ubaguzi au unyanyapaa,”
alisema Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe.


Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Mpanju akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe.


Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe akimsaidia kutia saini ya dole gumba Mpanji.


Mwenyekiti wa wa Shirikisho la vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Amon Mpanju akipokea fomu kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe, kwaajili ya kuomba ridhaa ya wana CCM Kinondoni kumteua kugombea Ubunge Jimbo la Uchaguzi la Kawe katika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.


Nae Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athumani Sheshe (pichani), amempongeza Mpanju kwa uamuzi wake huo na kusema kuwa anatekeleza moja ya kanuzi na sheria za Chama kuwa watu wote ni sawa na walemavu wanahaki ya kuchagua na kuchaguliwa kuwa vipongozi.
  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Mroki Mroki/Father Kidevu blog

Fomu za Ubunge, Udiwani sasa zauzwa shilingi milioni 5

FOMU ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika majimbo mbalimbali nchini likiwemo Jimbo la Songea Mjini, mkoani Ruvuma na Babati mkoani Manyara, kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imepandishwa kutoka kiwango cha Sh 100,000 kilichowekwa na chama hicho Taifa hadi kufikia Sh 5,000,000 kwa kila anayetaka kugombea nafasi hiyo katika jimbo.

Aidha, katika maeneo mbalimbali nchini, fomu za nafasi za madiwani zinazotakiwa kulipiwa sh. 10,000 hivi sasa wanaotaka kuteuliwa na chama hicho wanalipia kati ya shilingi 10,000 na 30,000.

Habari zaidi kutoka ndani ya CCM zinaeleza kuwa, fomu ya ubunge katika maeneo yote nchini zinatakiwa kulipiwa Sh. 100,000 na fomu ya udiwani ni Sh. 10,000 hali ambayo ni tofauti katika majimbo na kata hizo nchini.

Taarifa kutoka wilayani Babati mkoani Manyara, zinaeleza kuwa CCM inatoza wanachama wake kati ya shilingi milioni 2 na milioni 5 kwa watu wanaotaka kuteuliwa kugombea nafasi hiyo.

Kuchukua fomu ya ubunge Jimbo la Dk Nchimbi sasa ni Sh. milioni 3.1 badala ya 100,000

Uchunguzi wa FikraPevu katika Jimbo la Songea mkoani Ruvuma imebaini kuwa fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea ubunge katika Jimbo la Songea Mjini, mkoani Ruvuma, kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imepanda kutoka kiwango cha Sh 100,000 kilichowekwa na chama hicho Taifa hadi kufikia Sh 3,100,000 kwa kila anayetaka kugombea nafasi hiyo katika jimbo hilo.

Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Mjini, Juma Mperi, amethibitisha chama chake wilayani humo kuweka kiwango hicho cha gharama cha Sh milioni 3.1 kwa ajili ya kuchukulia fomu.

Kwa mujibu wa Mperi, kiasi hicho cha fedha, kinajumuisha gharama ya kuchukua fomu ambayo ni Sh 100,000 kama ilivyotangazwa na CCM Taifa, lakini kwa yeyote anayetaka kugombea jimbo hilo atalazimika kutoa kiasi kingine cha Sh 3,000,000 kwa ajili kulipia gharama za uchaguzi.

Ingawa Katibu huyo wa CCM hakuweza kufafanua gharama hizo za uchaguzi ni zipi, inaeleweka kwamba gharama hizo zinahusiana na mchakato wa kura za maoni, ambapo wajumbe wote wa mkutano mkuu wa jimbo hutakiwa kugharamiwa na chama katika jimbo husika, zikiwemo gharama za usafiri kutoka majumbani kwao hadi kwenye kituo cha kupigia kura za maoni kama zoezi hilo litafanyika katika kituo kimoja.
  • Kumbukumbu zinaonyesha kwamba siku chache zilizopita Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walitangaza kuwa fomu kwa wagombea urais zitatolewa kwa Sh1 milioni, ubunge Sh250,000 na udiwani Sh50,000.
  • Kwa upande wa Chama cha NCCR-Mageuzi kupitia kwa Naibu Katibu Mkuu-Bara, John Nyambabe kimesema mgombea wa urais, atalazimika kulipa Sh1 milioni kwa nafasi hiyo na gharama za fomu za ubunge ni Sh50,000 na udiwani Sh20,000 huku kikieleza kuwa fedha zitakazopatikana kwa gharama za fomu zitatumika kusaidia shughuli za chama.
  • Ofisa Uchaguzi wa CUF, Lugoni Abdulrahaman,amesema mgombea urais atalazimika kulipia fomu Sh 500, 000 na tayari wabunge wamesharejesha fomu na kura za maoni zilianza Mei 20, 2015 ambapo wagombea hao walichukua fomu kwa Sh50,000, huku za udiwani zikiwa ni Sh20,000.
Taarifa hii imenukuliwa kutoka FikraPevu.com

Chikulupi Njelu Kasaka achukua fomu ya Ubunge Mbeya


*Anaitwa Chikulupi Njelu Kasaka.

*Ni Mwanasheria (wakili) kitaaluma.

*Ni mfanyakazi wa Bunge la JMT

*Sasa anawania Ubunge wa Viti-maalum (vijana).

*WASIFU WA MGOMBEA: BI. CHIKULUPI KASAKA

ELIMU:
Chikulupi Kasaka ni mzaliwa wa Chunya na babu na Bibi ni wakazi wa Kijiji cha Mtanila katika Wilaya ya Chunya.

Chikulupi alizaliwa mwaka 1986 na kuanza elimu ya msingi mwaka 1994 katika shule ya Chunya Kati. Chikulupi alimaliza elimu ya msingi Mkoani Tabora na kuchaguliwa kwenda shule ya Serikali ya Sekondari ya Wasichana Msalato iliyopo Dodoma ambapo alisoma kidato cha kwanza mpaka cha nne mwaka 2000-2004. Mwaka 2005-2007 alijiunga na Shule ya Serikali ya Sekondari ya Wasichana Loleza iliyopo Mkoani Mbeya. Alishaguliwa kijunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2007 kusomea Shahada ya Kwanza ya Sheria na kumaliza mwaka 2011. Mwaka 2013 alijiendeleza kwa kujiunga na mafunzo ya uanasheria kwa vitendo na kumaliza mwaka 2014 katika chuo kiitwacho Law School of Tanzania ambapo baadaye niliapishwa kuwa wakili.

UZOEFU KATIKA UONGOZI:
Chikulupi aliwahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi akiwa anasoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alikuwa Mbunge katika Serikali ya wanafunzi - DARUSO.

Chikulupi alichaguliwa mwaka 2009 kuwa Makamu wa Rais wa Umoja wa Wanafunzi wa Afrika Mashariki uitwao East Africa Community Students Union -EACSU.

Pia alikuwa Afisa Mahusiano ya Umma katika Taasisi ya wanafunzi wa Sheria iitwayo University of Dar es Salaam Human Rights Association –UDHRA. Mwaka 2010 alishiriki mafunzo ya Uongozi kwa Vijana yaliyofadhiliwa na Shirika la Kijeruman liitwalo Friedrich Ebert Stiftung –FES.

Pia mwaka 2014 alishiriki mafunzo ya Viongozi Vijana toka barani Afrika nchini Marekani ambao alisomea masomo ya Public Management katika chuo cha Howard kilichopo Washington. Pia nilipata fursa ya kukutana na Rais Barack Obama ambae ni mwanzilishi wa mafunzo haya.

UZOEFU NDANI YA CHAMA/UVCCM:
Chikulupi Kasaka alijiunga na CCM hasa katika jumuiya ya UVCCM mara tu baada ya kumaliza elimu ya sekondari 2006.
Alipokuwa anasomea Shahada ya Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alijikita katika shughuli mbalimbali za kuimarisha chama na mwaka 2010 alichaguliwa Mwenyekiti wa UVCCM tawi ya Abiyan-Chuo Kikuu. Na mjumbe wa Shirikisho la Vyuo Vikuu wanaCCM, Mkoa wa Dar es Salaam.

Mgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Mbeya Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto) akikabidhiwa Fomu ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana Mbeya na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu

KAZI:
Mara baada ya kumaliza chuo kikuu Julai 2011 Chikulupi alifanya kazi katika Shirika la Wakimbizi katika Mradi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam uitwao International Migration Management Program (IMMP).

Mwaka 2012 aliajiriwa na Serikali kama Hakimu Mkazi daraja 2, katika Mahakama ya Mwanzo Makongorosi-Chunya, Mbeya. Mwishoni mwa mwaka 2012 nilijiunga na utumishi wa Chama Makao Makuu ya CCM Dodoma.

Nilipangiwa kufanya kazi za Chama katika Upande wa Bunge hasa za kisheria. Tangu kipindi hicho mpaka sasa Chikulupi anafanya kazi kama Msaidizi wa Katibu wa Wabunge wote wa CCM, Bungeni Dodoma.

VIPAUMBELE:
Chikulupi Kasaka anaomba ridhaa yako ili aweze kuwawakilisha vijana wa Mkoa wa Mbeya katika nafasi ya Uongozi wa Kitaifa kupitia ngazi ya Ubunge wa Viti Maalum-Vijana.

Kama mkazi wa Mbeya naamini vijana wa Mbeya wanauwezo, nguvu, bidii na jitihada katika shughuli zao za kila siku. Lakini mimi nitapigania kuwapatia vijana wa Mbeya fursa nyingi zaidi katika vipaumbele vifuatavyo:

ELIMU, AJIRA, MICHEZO, UTALII na AFYA.
ANAOMBA UMUUNGE MKONO KWA FURSA ZAIDI KWA VIJANA WA MKOA WETU WA MBEYA.


Kushoto ni Bw. Moses Mwakibinga Katibu wa Hamasa na Chipukizi Wilaya ya Chunya, Bi. Chikulupi Njelu Kasaka (Kushoto) na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mbeya Bi. Aida Mamu Baada ya kukabidhiwa Fomu

via Blogu ya Habari Mseto

Taarifa ya kutwa nzima ChannelTEN Julai 17, 2015
Orodha ya sasa ya waliochukua fomu za Ubunge

Mbunge Machali na aliyekuwa mlinzi wa Dk Slaa wahamia ACT-Wazalendo

Baada ya tetesi za muda mrefu, hatimaye Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi ), Moses Machali amejiunga na Chama cha ACT - Wazalendo.

Naibu Katibu Mkuu wa ACT - Wazalendo, Msafiri Mtemelwa alisema hayo jana.

Machali alithibitisha kwa simu jana kujiunga na chama hicho kipya na kusema atatoa ya moyoni Julai 21 katika mkutano utakaofanyika kwenye Uwanja wa Kiganamo, Kasulu Mjini.
“Nitakuwa na Zitto na wabunge wengine ambao siwataji kwa sasa,” 
alisema Machali. 

Mtemelwa alisema Machali amejiunga na chama hicho na kwamba kinachosubiriwa ni utaratibu maalumu wa kumtambulisha kwa wananchi.
“Siyo Machali pekee ambaye amekuwa akihusishwa kuhamia katika chama hiki, bado kuna wabunge kama wanne, nao wakati wowote watatambulishwa kwa wananchi. Staili yetu kwa hawa wabunge ni kuwapokea na kuwatambulisha katika majimbo yao, mbele ya wapigakura,” 
alisema Mtemelwa.

Mbali na mwanachama huyo, pia aliyewahi kuwa mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Khalid Kagenzi naye alionekana katika ofisi hizo.

Alipoulizwa na waandishi wa habari kama amehamia alijibu: 
“Ni haki ya kila Mtanzania kujiunga na chama chochote cha siasa anachokitaka. Bado sijachukua kadi yangu ya uanachama,”
alisema Kagenzi.

Imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la MWANANCHI

Ajali yaua 4 Kwa Sadala, Hai. Kilimanjaro


WATU wanne wamekufa papo hapo na wengine 11 kujeruhiwa , baada ya gari walilokuwa wakisafiria lenye namba za usajili T 196 AAW aina ya Toyota Hiace, kugongwa kwa nyuma na gari lenye namba

za usajili T 430 AQQ aina ya Fuso.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani, alisema tukio hilo limetokea leo asubuhi saa 12:40 katika daraja la mto Kikavu, lililopo wilaya ya Hai.

Kamanda Ngonyani alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari la fuso, kukosa umakini wakati wa kushuka kwenye mlima Kikavu ambao una kona kali pamoja na mto mkubwa.

Alisema dereva wa Fuso alikosa umakini wa kupunguza mwenbdo, baada ya kufika kwenye daraja la mto Kikavu, na kusababisha kugonga kwa nyuma Hiace iliyokuwa mbele yake.

Majeruhi wamelazwa katika hosptali ya mkoa wa Mawenzi, huku majeruhi watatu wakikimbizwa katika hosptali ya rufaa ya KCMC kwa matibabu zaidi.

Mtoto wa Rais staafu Zanzibar, Salmin awania Ubunge Mkwajuni


Mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar "Komando" Dk Salmin Amour Juma, Amini Salmin achukua Fomu kogombea Jimbo la Mkwajuni Zanzibar akiwasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kaskazini A Gamba kwa ajili ya kuchukua Fomu kogombea Jimbo hilo, akisalimiana na Wananchi waliopo hapo.


Mama wa Amini Salimi Bi Khadija Kasimi akisalimiana na Katibu Msaidi wa Ofisi ya CCM Wilaya Kaskazini A Unguja alipofika katika Ofisi hizo kumshindikiza Mtoto wake kuchukua Fomu ya Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Zanzibar.Katibu Msaidizi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Kaskazini Unguja Ndg Shafi Hamad akitowa maelezo kwa Mgombea kabla ya kumkabidhi fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Jimbo la Mkwajuni


Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Amini Salimini akihesabu fedha kwa ajili ya kulipia Fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge kupitia CCM katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kaskazini Unguja Gamba.


Katibu Msaidi Ofisi ya CCM Wilaya ya Kaskazini a Unguja Ndg Shafi Hamad akimkabidhi Fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Mkwajuni Amini Salimini, baada ya kukamilisha taratibu zote za malipo na kutimiza masharti ya Chama cha Mapinduzi.


Katibu Msaidi wa CCM Wilaya ya Kaskazini A Unguja akitowa maelezo kwa mgombea baada ya kumkabidhi fomu hiyo Ndg Amini Salimini.


Mgombea wa Jimbo la Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Unguja Amini Salimini akiwa katika picha ya kumbukumbu na familia yake baada ya kuchukua Fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni kwa tiketi ya CCM, akiwa katika Ofisi za CCM Gamba.


Amini Salimini akiwa katika picha ya pamoja na familia yake baada ya kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mkwajuni Zanzibar.Akionesha fomu yake baada ya kukabidhiwa kwa hutua za ujazaji


Amini Salimini akitoka katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kaskazini A Unguja baada ya kuchukua fomu hiyo akionesha kwa wananchi walioko katika eneo hilo.


Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Unguja Amini Salimini akiwa na Mtoto wake wa Kwanza wakishikilia fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuiwakilisha CCM katika Jimbo la Mkwajuni Zanzibar.


Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Amani Salimini akiomba dua katika makaburi ya Wazee wake huko Kidombo baada ya kuchukua Fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Zanzibar


Amini Salimini akipata dua kutoka kwa Wazee wa Kijiji cha Kidombo Mkwajuni baada ya kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge wa Jimbu la Mkwajuni Zanzibar kupitia CCM