Michezo mingine hakuna?....


[video] Did you know sugar removes greaser? + 5 other uses of sugar you probably didn't know

HouseholdHacker put together a list of awesome other uses for sugar:
  1. Make flowers last longer
  2. Garden Booster
  3. Preserve Baked Goods
  4. Get rid of Grass Stains
  5. Remove Grease and Oil from Skin
  6. Get rid of Wasps
Watch the video below...FREE for download! Over 240 eBooks from Microsoft


Microsoft Senior Sales Excellence Manager Eric Ligman is giving Microsoft eBooks for free.

They include User Guides, Deployment Guides, Step-By-Steps, etc.

He says, people around the world use them and have been a huge success:
In fact, two years ago, there were over 3.5 MILLION free eBooks downloaded throughout the year. Then last year, we gave away over 1 MILLION FREE eBooks in just 2 days, and over 2 MILLION in less than a week! That was phenomenal! So how many MILLIONS of FREE Microsoft eBooks are you going to download this year?
Get them at: blogs.msdn.com

[video] Pochi ilivyoibwa katika eneo la starehe 'la kistaarabu'

Video iliyopachikwa hapo chini imepatikana kupitia WhatsApp, inaelezwa kuwa kilichotendeka kimetokea siku ya Ijumaa, Julai 17 mwaka huu huko Salt Restaurant, Oysterbay jijini Dar es aslaam.

Hii ni video iliyonaswa na camera za ulinzi (CCTV)

Mnaaswa kuchukua tahadhari "abiria chunga mzigo wako".


Lowasa atarajiwa "kumshitaki" Kikwete wiki hii

picha ya maktaba ikiwaonesha Lowasa (kushoto, aliyevaa miwani) na Kikwete miaka kadhaa iliyopita
picha ya maktaba ikiwaonesha Lowasa (kushoto, aliyevaa miwani) na Kikwete miaka kadhaa iliyopita

Kwenye gazeti tando la  MwanaHALISI Online, Saed Kubenea anasema kuwa mwasisi wa "Safari ya Matumaini", Edward Lowassa, amepanga wakati wowote kutoka sasa, kumkatia rufaa Rais Jakaya Kikwete kwa kuzungumza na waandishi wa habari, Jumatatu au Jumanne wiki hii.

Kwamba, mkutano huo malengo yake ni kumshitaki Mwenyekiti wa CCM Taifa, Kikwete kwa wananchi kwa “kukaidi matakwa ya wengi”kwa kulikata jina lake kwa maslahi binafsi.
“Ni kweli kwamba Edo (Edward Lowassa), amepanga kueleza kilichotokea Dodoma kwenye mikutano ya chama chake. Atafanya hivyo kupitia mkutano kati yake na waandishi wa habari” 
Amenukuu Kubenea taarifa hiyo aliyosema ameelezwa na mmoja wa watu waliokaribu na kiongozi huyo.

Hata hivyo, taarifa hiyo imehitimisha kwa kusema kuwa haijafahamika mara moja ikiwa Lowassa atautumia mkutano huo kueleza mustakabali wake wa baadaye wa kisiasa.

Waziri mlevi aliingizia Serikali hasara mil 11/= kwa kuchelewa ndege

Mahojiano aliyoyafanya mwandishi wa habari mzoefu, Saed Kubenea kwenye MlimaniTv katika video iliyopachikwa hapo chini, amegusia hilo wakati akizungumzia masuala ya dhana ya faragha kwa mtu ambaye ni kiongozi wa umma.

Pia amejibu swali kuhusu, je!, gazeti la Mawio ndiyo mbadala wa MwanaHalisi?Mahojiano na mtangazaji wa Azam aliyekuwa RTD, RadioOne, DW na BBC, Charles Hilary

Charles Hilary
Charles Hilary

Ilitokea, lakini haikuandikwa. Charles Hilary ndiye Mtanzania wa kwanza kutangaza kwa Kiswahili mechi za fainali za Kombe la Dunia akiwa uwanjani.

Ziko redio nyingi zilizowahi kutangaza fainali hizo kwa Kiswahili, lakini zote zilifanya hivyo kwa kuangalia mechi hizo kwenye runinga na si kutokea uwanjani.

Hilo ndilo linalomtofautisha mtangazaji huyo mkongwe wa zamani wa Redio Tanzania na watu wengine wote kwenye fani hiyo. Charles alikuwa ameshikilia microphone akiwa viwanjani.

Rekodi yake inanogeshwa na ukweli kwamba hata fainali hizo za Kombe la Dunia zilikuwa za kwanza kufanyika barani Afrika baada ya taifa la Afrika Kusini kupewa uenyeji wa michuano hiyo mikubwa katika mchezo wa soka duniani.

“Ilikuwa ni furaha zaidi kwangu,” anasema Hilary akikumbuka fainali hizo ambazo hushirikisha timu za taifa za wawakilishi wa mabara yote duniani.

“Mwaka 2010 ndiyo fainali za Kombe la Dunia zilifanyika kwa mara ya kwanza Afrika. Mimi nilikuwa Mtanzania pekee niliyepata nafasi ya kutangaza ‘live’ kwa Kiswahili. Sikutarajia. Hiki ni kitu cha furaha sana kwangu.

“Hakuna Mtanzania mwingine aliyewahi kutangaza ‘live’ na sijui kama itatokea tena hivi karibuni. Kwa kuweka kumbukumbu ya furaha hiyo nilinunua na kurejea na vitu mbalimbali ikiwamo mavuvuzela, nembo za timu za taifa ambazo manahodha wa timu hubadilishana na vitu vingine vingi.”

Hilary anaweza kutangaza vipindi vingine vingi, lakini anajulikana zaidi kutokana na umahiri wake wa kutangaza mpira, kuelezea mwenendo wa mchezo, kueleza haiba za wachezaji, lakini zaidi ana msamiati mkubwa, sitiari na misemo inaomtofautisha na watangazaji wengi wa enzi zake, akiwaacha mbali zaidi watangazaji vijana wa sasa.

Lakini gwiji huyo, ambaye baada ya kufanya kazi Ujerumani na Uingereza amerejea na kujiunga na Azam Media, sasa anasema wakati wake wa kuonyesha umahiri wake kwenye utangazaji mpira, umeisha.

“Mie tena, wakati wa mpira umefika ukingoni. Nimestaafu kutangaza soka, ila sasa nataka kufundisha vijana kutangaza,” anasema Hilary.

“Nilipokuwa Uingereza nilikuwa nawafuatilia (watangazaji mpira wa sasa). Wengi hawatangazi vizuri na sasa nimerudi jukumu langu ni kuwafundisha, sifa nilizopata kwa utangazaji kwa miaka 33 zinatosha,” anasema Hilary, mmoja wa watangazaji wa kwanza wa kituo cha Radio One Stereo alichojiunga nacho mwaka 1994.

“Tatizo katika utangazaji ni radio binafsi kutaa faida ya haraka. Hata hao wanaotangaza mpira ni juhudi zao, hawana A, B, C (mafunzo) za utangazaji; ni vurugu mechi. Wanazungumza sana, wanataka kuwa wachambuzi zaidi badala ya kutangaza.

“Lakini si kosa lao, kosa la wamiliki hawakuwatafuta watangazaji wakongwe kuomba ushauri ili kutoa maelekezo. Lakini sasa nipo Azam, ingawa kazi zinanibana, mtu akinitafuta nipo tayari. Ninawakaribisha, hata wakinipigia simu nitawaeleza cha kufanya.”

Hilary anaona kuwa wamiliki wa vyombo vya habari, hasa radio, wana wajibu wa kukuza ujuzi wa vijana angalu kwa kuwapeleka kwenye mafunzo kila baada ya miezi sita au mwaka, ndani hata nje ya nchi badala ya kujali faida.

Pia anaona watangazaji wengi vijana wanabweteka badala yake kujitahidi kujifunza kwa wengine ambao ni wakongwe kwa kuwa wana safari ndefu.

Hilary, ambaye pia aliasisi kipindi cha Charanga Time kilichomzidishia umaarufu akiwa Radio One Stereo, alizaliwa Zanzibar miaka 56 iliyopita eneo la Jang’ombe. Aliwahi kunusurika kuuawa kwa risasi mwaka 1964, siku moja baada ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyoundoa utawala wa Sultan na kuiweka Serikali ya Watu wa Zanzibar.

Charles alikutwa na tukio hilo Januari 13 wakati akiwa na umri wa miaka mitano.

Mwaka 1968 alihamia jijini Dar es Salaam na kujiunga na Shule ya Msingi ya Ilala Mchikichini. Alijiunga na Redio Tanzania mwaka 1981 na kukitumikia chombo hicho cha umma hadi mwaka 1994 alipojiunga na kituo binafsi cha Radio One Stereo kinachomilikiwa na IPP.

Mwaka 2003 aliondoka nchini na kujiunga na Radio Deutsche Welle na miaka mitatu baadaye alijiunga na Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC akiwa Idhaa ya Kiswahili.

Akieleza sababu za kuondoka BBC kurejea nchini, Hilary anasema ni umakini wa wamiliki wazawa wa vyombo vya habari.

“Kilichonisukuma kuja hapa ni umakini wa wamiliki na jinsi Watanzania wenzetu walivyojitoa kuwekeza fedha nyingi kwenye mradi huu. Mimi nimekuja kusaidiana nao ili kuipa hadhi kubwa Azam katika habari za televisheni na redio itakayoanza Julai mwishoni na mimi ndiye mkurugenzi wake,” alisema mkongwe huyo.

“Wamiliki ni wazalendo, wapo serious (makini), hiyo imenivuta. Hebu fikiria nimekaa mika 15 nje ya Tanzania, miaka mitatu nilikaa Ujerumani Redio Deutsche Welle na miaka tisa BBC, sasa nimevutika kwa Azam.”

Wakati mgumu michezoni

Miaka zaidi ya 30 kwenye tasnia ya habari haiwezi kupita bila ya matatizo, na Hilary alikumbana na hali ngumu kwenye kazi yake ya utangazaji.

“Kuna mengi lakini hasa siku ambayo Arsenal ilifungwa magoli 8-2 na Manchester United (katika Ligi Kuu ya Soka ya Uingereza). Mechi hiyo nilitangaza miye, ulikuwa wakati mgumu sana, sana, sana,” anakumbuka.

“Ingawa niliumia, sikuonyesha katika utangazaji wangu. Hiyo ni moja ya sifa anazotakiwa kuwa nazo mtangazaji wa mpira, hata kama unapenda timu fulani, ikifungwa hupaswi kujionyesha.”

Ni mpenzi wa Arsenal, lakini Hilary anasema hapa nchini hakupenda kuingia kwenye ushabiki wa Yanga na Simba.

“Kwa hapa Tanzania nilikuwa naipenda klabu ya Mlandege ya Zanzibar. Sikupenda mambo ya usimba na uyanga. Niliipenda klabu hiyo pia kwa sababu kuna mdogo wangu alikuwa akiichezea anaitwa Shem Frank, alikuwa nahodha.

“Lakini nje ya Tanzania, mimi ni mshabiki wa Arsenal, tena sana sana, tena sana.”

Kuanzisha Radio One Stereo

Moja ya kazi ngumu alizokumbana nazo ni kuanzisha kituo cha redio cha Radio One Stereo.

“Nakumbuka tulipewa jukumu la kuanzisha Radio One, wakati huo nikiwa na Brother Mikidadi Mahmoud na Julius Nyaisanga (marehemu). Hilo ndilo jambo gumu zaidi nililokutana nalo,” anasimulia.

“Tulikesha ili kufikiri namna bora ya kuendesha redio hiyo iliyokuwa ya kwanza binafsi nchini. Sote tulitoka Radio Tanzania, hivyo ugeni wa jukumu ulitufanya kulala wakati mwingine saa 8:00 usiku tukijaribu kupanga kipindi hiki kiende wapi, kile kitoke saa ngapi.

“Nakumbuka tulifanya kazi kwa ushirikiano sana pia na Taji Liundi, Rankim Ramadhan na Flora Nducha. Hakika ilikuwa ni kipindi kigumu.”

Historia ya utangazaji

Mbali na yote hayo Charles anakumbuka kwamba akiwa RTD, kwa mara ya kwanza alisoma taarifa ya habari ya saa 7:00 mchana mwaka 1981, ingawa hakumbuki siku wala mwezi.

“Nakumbuka pia mechi yangu ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara wakati huo kutangaza ilikuwa kati ya Yanga na Coastal Union, hiyo ilikuwa mwaka 1982. Nilikuwa na walimu wangu Salim Mbonde na Ahmed Kipozi,” anasema.

Ilikuwaje?


Charles anaeleza kuwa siku hiyo akiwa bado kijana mdogo alikwenda uwanjani na wakongwe hao na kwa kawaida wanafunzi walipewa dakika tano za kujifunzia.

“Kipozi akanipa ‘mic’ nikaanza kutangaza, nilipokamilisha dakika zangu tano, nikataka kurudisha kipaza sauti, lakini Kipozi akaninong’oneza akisema; “endelea”. Hiyo iliashiria naweza na tangu siku hiyo nikawa natangaza mpira,” anasema Charles.

[video] How to prevent cut apples and potatoes from browning

Add two table spoons of honey to a cup of water, then soak your fruit or vegetable (potatoes).

Watch the video below..Waliochukua fomu za Ubunge katika majimbo ya mkoa wa Kagera

Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Sued Kagasheki anaemaliza muda wake

August 20 mwaka huu, leo amerudisha fomu za kugombea ubunge katika jimbo la Bukoba mjini kupitia CCM. 

Akiongea na wanachama waliomsindikiza amewahakikishia kuwa wasiwe na wasiwasi jimbo litabaki mikononi mwa CCm.

Amewakumbusha kipindi cha nyuma wakati jimbo lilipo kuwa mikononi mwa upinzani adha kubwa walizokutano nazo. Lakini pia amesema katika kipindi cha ubunge wake yapo mambo mengi sana yamefanyika, japo wapo watu wanatumia kila njia kusambaza propoganda za kupotosha, lakini akasema uwezi kuzuia mtu kusema kile anachokiamini.

Akasema kuna watu katika dunia hii hawaamini kama Mungu yupo:
sasa mimi Kagasheki ni nani nipendwe na wote? Kuna watu walimkataa Yesu na wengine Mtume, lakini si kitu hao waache, walio wengi wanatambua kazi tulizofanya na tutazieleza wakati ukifika. 
Wengine waliorudisha fomu ni Bw George PhilbR ubaiyuka, Eliet Projestus, Philbert Katabazi,Anatory Aman na Mujuni Kataraiya aliepoteza jimbo mwaka 2000 na kuchukuriwa na Wilfred Rwakatare na kuchukuliwa na Balozi Kagasheki 2005 na 2010.

Wanachama wakimpungia Balozi Kagasheki.Balozi Kagasheki akiongea na wanachama.

WanaCCM waliojitokeza kumsindikiza Balozi Kagasheki kurudisha fomu.


Mwenyekiti wa kata ya Bilele Taofiq sharifu akitoa msimamo wa bilele.

Katibu wa kata ya hamugembe bw Hamza akieleze msimamo wa kata ya Hamugembe.
Balozi Kagasheki akisaini kitabu cha uthibitisho wa kurudisha fomu.


Balozi Kagasheki akizungumza na wanachama wa ccm na wapenzi waliomsindikiza kurudisha fomu.

Job opportunity at SUA for an Administrative Officer III

Mapokezi ya Magufuli nyumbani kwake Chato
Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.


Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake waliokuwa wamekusanyika kwenye kituo cha mabasi wilayani humo wakishangilia kwa furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao.


Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumlaki Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo na shamra shamra za mapokezi kurindima kila kona wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli,huku wengine wakiwa wamebeba mabango kama hivyo pichani.


Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.


Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Luhavi akiwasalimia wachama wa CCM pamoja na Wananchi waliofika kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo katika kituo cha mabasi cha zamani ndani ya wilaya hiyo.Ilikuwa ni shangwe tu jioni ya leo ndani ya Wilaya ya Chato ambako ndiko nyumbani kwa Mbunge na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM, Dkt John Pombe Magufuli. 


Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji wa Katoro mkoani Geita alipokuwa akipita njiani kuelekea wilayani Chato.Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli mkoani humo wananchi walijitokeza kwa wingi kila baada ya kilometa kadhaa na kuziba barabara wakita kumuona Dkt Magufuli na kumpongeza kwa kuchaguliwa kwake na chama cha CCM.


Mwananchi akiwa amekumbwa na joto la furaha mara baada ya kumuona Dkt Jonh Magufuli akiwa na msafara mzima wakielekea jimboni kwake Chato mkoani Geita.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mh. Magesse Mulongo akiwasalimia wananchi wa Chato jioni ya leo,kabla ya kumkaribisha Dkt John Magufuli aliyewasili mjini humo jioni ya leo akitokea mkoani Mwanza akijitambulisha kwa wananchi na kuwashukuru.


Dkt Magufuli akizungumza jambo kwa maelfu ya wakazi wa mji wa Chato jioni ya leo


Dkt Magufuli akifurahia jambo mbele ya umati wa watu,mara baada ya kujitambulisha kwao.


Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru wakazi wa mji huo kwa kujitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi. Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa CCM kwa Dkt Magufuli.


Maelfu ya Watu walijitokeza kumlaki Dkt Magufuli jioni ya leo mjini Chato


Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi CCM ,Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga Wananchi wa Chato waliojitokeza kwa wingi kumlaki, mara baada ya kumaliza kujitambulisha na kuwashukuru kwa kiasi kikubwa kwa kuchaguliwa kwake katika nafasi ya kupeperusha bendera ya chama chake kuwania nafasi ya Urais .PICHA NA MICHUZI JR-CHATO-GEITA.

"Rais wa Ludewa" Filikunjombe apelekewa nyumbani fomu ya Ubunge


Wazee wakimpoelekea fomu ya ubunge Deo Filikunjombe nyumbani kwake kwa maandamano 

WAZEE Ludewa wamemchukulia fomu ya kugombea Ubunge, mbunge aliyemaliza muda wake hivi karibuni, Deo Filikunjombe wakimwomba kuendelea kuongoza jimbo hilo kwa miaka 20 zaidi huku wakidai kuwa kama usingekuwa ni utaratibu wa chama cha mapinduzi (CCM) na ule wa tume ya uchaguzi (NEC) wa kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano, basi wao wangempitisha mbunge huyo bila kupingwa na uchaguzi kwa wilaya ya Ludewa ungekuwa wa madiwani pekee na sio kwa urais Dk John Magufuli wala mbunge wao huyo.

Filikunjombe amewaunga mkono kwa kusema anajivunia uchapakazi wa Rais Dk Jakaya Kikwete kwani ni Rais pekee aliyesaidia kuiwezesha Ludewa kusonga mbele na zawadi ambayo wananchi wa Ludewa  wanaitoa kwa CCM ni kuhakikisha mgombea urais wa CCM, Dk Magufuli anapata kura nyingi zaidi ukilinganisha na wilaya yoyote hapa nchini kwani pia amehusika kuwakomboa wananchi wa Ludewa kwa kutengeneza barabara za wilaya hiyo.

Wakizungumza wakati wa kumkabidhi fomu nyumbani kwake Ibani mjini Ludewa wazee hao walisema wamelazimika kumchukulia fomu hiyo na kwenda kumkabidhi baada ya kuridhishwa na kazi kubwa aliyoifanya kwa kipindi cha miaka mitano ambayo amepata kuwa mbunge wa jimbo hilo na kuonyesha utendaji mkubwa zaidi ukilinganisha namaendeleo yaliyoonyeshwa na wabunge 7 waliotangulia katika jimbo hilo .

Hivyo walisema bado wanaimani kubwa na mbunge wao na kuwa imani na matumaini ya wananchi wa Ludewa ni kuona Filikunjombe anaendelea kuwatumikia wananchi hao kwa vipindi vingine 4 kwa maana ya miaka 20 ama kuendelea kuongoza jimbo hilo hadi pale atakapoamua kustaafu mwenyewe kwani utendaji kazi wake wa kazi ndio ambao umemfanya kupewa dhamana hiyo ya kuendelea kuongoza jimbo hilo.

"Tumekuamini na tumependezwa na utendaji kazi wako hivyo wewe tunakubariki kuendelea kuongoza tena na tena jimbo hilo kwani ulipokea likiwa katika hali mbaya na sasa wananchi wa Ludewa kupitia jopo la wazee tumekuamini zaidi na tumekuchukulia fomu hii ya ubunge kama ishara ya kukuamini zaidi ......tulikuita jembe na sasa wewe ni katapila letu Ludewa umeweza kupita pasipo pitika umetufanikishia maendeleo makubwa kwa kipindi kifupi zaidi "

Kwa upande wake mbunge Filikunjombe pamoja na kuwashukuru wazee hao na vijana wa boda boda  zaidi ya 300 katika wilaya ya Ludewa walioungana kumchukulia fomu hiyo alisema kuwa imani kubwa na ushirikiano mkubwa ambao wananchi wa Ludewa wameuonyesha wakati wa utumishi wake umemfariji na kuweza kufanya kazi kubwa zaidi ikiwa ni pamoja na kuwatumikia vema buneni pasipo kusinzia kama walivyofanywa baadhi ya wabunge wengine.

Filikunjombe alisema ili kuwa ni vigumu kwake kusinzia bungeni kutokana na aina ya makubaliano yake na wananchi waliomtuma kwenda kuwawakilisha na kuwa wananchi hao walimtuma kuwasemea bungeni hivyo kama nae angeungana na baadhi ya wabunge ambao uwakilishi wao bungeni ulikuwa ni kusinzia basi wilaya ya Ludewa isingekuwa na maendeleo kiasi hicho.

Alisema kuwa leo hata wale wananchi wa Ludewa ambao walikuwa wakikwepa kuitwa wana Ludewa kutokana na uduni wa maendeleo uliokuwepo katika wilaya hiyo hivi sasa wameanza kutembea kifua mbele kujivunia wilaya yao tofauti na zamani ambapo wengi wao walikuwa wakidanganya kuwa wanatoka mkoa wa Ruvuma.

"Kazi mlionituma bungeni Dodoma nimeifanya zaidi ya uwezo wangu na ndio maana leo wilaya yetu  imepiga hatua kubwa katika maendeleo na ukweli nimefanya yale mlionituma bungeni ombi langu kubwa kwenu wenzangu naomba mzidi kuniombea afya njema zaidi na kuniunga mkoni ili nikirudi bungeni tena kuweza kufanya mengine makubwa zaidi ya haya"

Alisema kuwa hawezi kusema wabunge waliotangulia hawakufanya chochote kabisa katika jimbo la Ludewa japo kila mmoja aliweza kufanya kulingana na uwezo wake ikiwa ni pamoja na mbunge wa kwanza kuleta meli ,mbunge mwingine alileta basi ,mwingine umeme Ludewa mjini lakini kwa upande wake amefanya zaidi ya hayo na kuifanya wilaya hiyo kuwa wilaya ya mfano katika wilaya za mkoa wa Njombe huku akisisitiza kuwa lengo yake ni kuona wilaya ya Ludewa inaendelea kuongoza kwa maendeleo ukilinganisha na wilaya zote za mkoa wa Njombe.

Kwani alisena nia, uwezo na nguvu ya kuifanya wilaya ya Ludewa kuongoza katika maendeleo bado anayo na kuwa kazi kubwa ya wananchi wa Ludewa kuendelea kutoa ushirikiano kwake tena .

Hata hivyo alisema mafanikio makubwa yaliyopatikana katika wilaya hiyo kamwe hataacha kumpongeza Rais Dk Kikwete ambae amekuwa sehemu ya mafanikio yake na mafanikio ya wananchi wa Ludewa katika maendeleo ila pia aliyekuwa waziri wa ujenzi Dr Magufuli ambae saa ndie Rais mtarajiwa wa awamu ya tano kwani kati ya mawaziri waliopambana kwa ajili ya Ludewa Dr Magufuli ni namba moja na kuwa zawadi yake ni kupata kura za kishindo katika wilaya hiyo ya Ludewa.

Alisema Rais Dk Kikwete kwa upande wake tayari amekwisha ahadi kufika kuwaaga wananchi wa Ludewa kabla ya kumaliza muda wake kwa kuzindua ujenzi wa viwanda vya chuma katika wilaya hiyo ila pia Dr Magufuli anataraji kufika katika wilaya hiyo ya Ludewa wakati wowote kuanzia sasa hivyo pamoja na kuwashukuru viongozi hao wakubwa kwa upendo wao kwa wana Ludewa bado alisema historia kubwa wameiandika katika wilaya hiyo.

Katika zoezi hilo la wazee kumkabidhi fomu ya ubunge Bw Filikunjombe zaidi ya Tsh 400,000 zikichangwa na wananchi mbali mbali yakiwemo makanisa na watu binafsi pamoja na mbuzi na zawadi nyingine kama sehemu ya kumuunga mkono mbunge huyo katika safari yake ya kugombea tena ubunge wa jimbo hilo la Ludewa.


Msafara wa vijana wa boda boda zaidi ya 300 waliowasindikiza wazee wa Ludewa kumchukulia fomu mbunge Deo Filikunjombe 


Safari ya kuelekea nyumbani kwa Filikunjombe kukabidhi fomu ya ubunge 


Wazee hao wakiwa nyumbani kwa mbunge Filikunjombe kumkabidhi fomu ya ubunge Ludewa


Hapa wakimkabidhi fomu Bw FilikunjombeMbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akipokea fomu kutoka kwa wazee na vijana waliomchukulia na kwenda kumkabidhi nyumbani kwake Ibani mjini Ludewa jana


Askari wa usalama barabarani akiongoza usalama

Filikunjombe akielekea kuwashukuru wananchi Ludewa kwa kumchukulia fomu ya ubunge


Ni zaidi ya furaha kwa mbunge Filikunjombe


Kikundi cha ngoma ya Mganda


Wananchi wakimsikiliza mbunge wao Filikunjombe


Wawakilishi wa wananchi wa jimbo jirani la spika Makinda wakimpongeza Filikunjombe


Filikunjombe akiwa amepokea zawadi ya mikuki kama zawadi kutoka kwa wananchi wa jimbo la Makinda ambao walifika kumpongeza pia


Hapa akikabidhiwa


Filikunjombe akiwashukuru kwa moyo wa upendo


Mkazi wa Ludewa akionyesha furaha yake kwa mbunge


Wadau mbali mbali wakimchangia pesa ya fomu Filikunjombe


Filikunjombe akikabidhiwa pesa za kampeni na fomu


Wananchi wakifurahia kuonyesha imani tena na Filikunjombe
Filikunjombe akizungumza na wananchi hao


Hotuba ya kipindi cha miaka mitano madarakani


Filikunjombe na familia yake wakifurahia upendo wa wana Ludewa
  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Francis Godwin/MatukiodaimaBLog