Call for entries: First ever Pan African prize - Etisalat Prize for Literature 2015


PRESS RELEASE

The first ever Pan African prize celebrating debut African writers of published fiction


Nigeria’s fastest growing and most innovative telecommunications company, Etisalat has announced the call for entries for the 2015 Etisalat Prize for Literature which is in its third year. The prize is the first ever Pan African prize celebrating debut African writers of published fiction.

According to Matthew Willsher, the Chief Executive Officer, Etisalat Nigeria, “Etisalat Prize for Literature serves as a platform for the discovery of new creative writing talents out of the African continent.”

The CEO highlighted that following the success of the second edition, the literary community is eagerly awaiting the third edition. NoViolet Bulawayo won the maiden edition with her highly celebrated debut novel, We Need New Names, while Songeziwe Mahlangu emerged winner of the second year of the prize with his novel, Penumbra.

The Judging panel for the 2015 edition will be chaired by Professor Ato Quayson, a Professor of English and inaugural Director of the Centre for Diaspora Studies at the University of Toronto; alongside Molara Wood, writer, blogger, journalist, critic and editor and Zukiswa Wanner, author of The Madams and Men of the South.

The Judges will develop a list of nine novels and shortlist three novels before finally selecting a winner. Submission of entries are ongoing, having opened June 18, 2015 and would close August 27, 2015.

The winner receives a cash prize of £15,000 in addition to a fellowship at the prestigious University of East Anglia under the mentorship of award-winning author, Professor Giles Foden. The winner will also receive a sponsored three-city book tour while the two other shortlisted writers will receive a sponsored two-city book tour to promote their books. The Etisalat Prize for Literature also supports publishers by purchasing 1000 copies of the shortlisted books for distribution within the continent.

Entries must be a writer’s first work of fiction of over 30,000 words, and published within the last 24 months. The Etisalat Prize will also launch the online-based flash fiction prize later in the year to engage the rising stars of fiction.

On how to enter, visit: http://prize.etisalat.com.ng/how-to-enter

For rules and guidelines visit http://prize.etisalat.com.ng

Kipanya: "waacheni majeruhi waje kwangu" kwa maana...


Kwa wale wasomaji wa Biblia, kuna mstari karibuni na mwisho wa barua ya 11 ya Mathayo usemao, "Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha." ndicho kilichonijia kichwani nilipoiona katuni ya Masoud "Kipanya" hapo...

Marando ang'aka! CHADEMA itawaburuza Magufuli, TFF kortini

Ndege ya serikali, Fokker F28, aliyoitumia Magufuli alipokwenda Mwanza
 • CCM yasema walikodi
 • Wakala asema sheria haijavunjwa
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiko mbioni kufungua mashauri mawili mahakamani dhidi ya John Pombe Magufuli, mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mabere Marando, mwanasheria mkuu wa chama hicho, ameliambia MwanaHALISI Online, kesi dhidi ya Magufuli itafunguliwa mahakama kuu, haraka iwezekanavyo.
“Tutamshitaki Magufuli haraka iwezekanavyo. Huyu mtu ana sifa ya kutoheshimu utawala wa sheria, hivyo tunataka kumuonyesha kuwa nchi hii inatawaliwa kwa sheria,”
kwa sauti ya ukali, amesema Marando.

Amesema chama chake kitafungua mashauri mawili. Shauri la kwanza litahusu mwanasiasa huyo kuanza kampeni kabla ya wakati na jingine, ni juu ya matumizi ya vyombo vya serikali kwenye kampeni za kisiasa.
“Yote haya yatamhusu Magufuli na mawakala wake. Hatuwezi kuruhusu mtu mmoja au chama kimoja, kinatumia madaraka yake binafsi na sisi tunanyamaza,” 
Marando anasema, katika shauri la kwanza, chama chake kitawaunganisha shirikisho la soka nchini (TFF); Baraza la Soka la Afrika Mashariki (CECAFA); CCM na wakala wa ndege za serikali.

Anasema, TFF itaunganishwa katika shauri hilo kutokana na hatua yake ya kumualika Magufuli kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano yanayoandaliwa na CECAFA.

Hatua ya Chadema kuamua kufungua shauri dhidi ya mwanasiasa huyo imekuja baada ya Magufuli Dar kutumia ndege ya Serikali katika anachoita, 
“kampeni yake ya kichama ya kujitambulisha.”
 wakisema hatua hiyo ni matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa.

Katika hatua nyingine, Marando amesema, mbali na kufungulia mashitaka mahakamani dhidi ya Magufuli, CCM na mawakala wake, chama chake kitawasilisha pingamizi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuomba kumzuia Magufuli kuwa mgombea urais.
“tutamuwekea pingamizi kwa kuanza kampeni kabla ya wakati. Tunataka tupate rais anayefuata sheria, siyo rais anayevunja sheria.” [via MwanaHALISI]

Upinzani waja juu Magufuli kutumia ndege ya Serikali

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA), Kapteni Keenan Mhaiki alisema kitendo cha CCM kutumia ndege ya Serikali hakivunji sheria na taratibu zozote kwa kuwa mbali na kusafirisha viongozi wa Serikali, pia wanaruhusiwa kufanya biashara kwa kuhudumia umma.

Kuhusu suala hilo la gharama, Kapteni Mhaiki alisema gharama ya kukodi ndege hizo zipo tofauti kutokana na aina inayohitajika akisema aliyoitumia Dk Magufuli inagharimu Dola za Marekani 4,000 sawa na Sh milioni 8.4 kwa saa moja.
Katika ufafanuzi wake, Kapteni Mhaiki alisema hakuna haja ya suala hilo kuchukuliwa kisiasa... “Jukumu la kwanza ni kubeba viongozi wa Serikali lakini kama kuna muda wa ziada tunawahudumia watu wengine kibiashara na huwa tunasafirisha hata timu za mpira na wageni kutoka nje ya nchi wanapotembelea nchini. “Mtu yeyote anaruhusiwa kuomba kuikodi, atapatiwa ankara yake… hata awe CUF, CHADEMA au chama chochote kile kama kuna nafasi anapata,” 
Alipoulizwa juu ya tuhuma za upendeleo kwa chama tawala hivyo kutoleta uwanja sawa wa ushindani, alijibu: 
“Upendeleo upi unaozungumza au unautaka? Hata wewe mwandishi ukitaka tupigie simu ndege ikiwapo utapata.”
TGFA kwa sasa ina ndege nne ambazo ni Fokker F28 ya mwaka 1978 yenye usajili wa 5H-CCM, Piper PA-31 Navajo (1980, 5H-ILS), Fokker 50 (1992, 5H-TFG) na Gulfstream 550 ya mwaka 2004 iliyosajiliwa kwa namba 5H-ONE.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema walifuata taratibu zote kuikodi ndege hiyo na kwamba chama chake ni kikubwa na hakiwezi kushindwa kukodi usafiri huo.
“Ile ni ndege ya Serikali, yeyote anayetaka kuitumia aende kulipia tu, atapewa. Sisi tumekwenda kama wateja wa kawaida tukalipia, ukitaka kujua ni kiasi gani kawaulize wahusika watakueleza” 
alisema Nape. [via MWANANCHI]


Jobs available: World Bank Group Recruitment Drive for African Nationals


The World Bank Group is launching a recruitment drive aimed at increasing the number of Sub Saharan Africans in its work force. This commitment to hire Sub Saharan Africans reflects the Bank Group’s senior leadership commitment for a diverse workforce in which African nationals can play a key role in fighting poverty and increasing shared prosperity. Employment opportunities will be in various technical areas and professional streams for talented and diverse young professionals and mid-career level professionals to contribute and grow their skills in a career in international development.

A career with the World Bank Group offers a unique opportunity for exceptionally talented individuals with a passion for international development to contribute to solving some of the world’s most pressing problems. Bank staff work with governments, civil society groups, the private sector, and others in developing countries around the world, assisting people in all areas of development, from policy and strategic advice to the identification, preparation, appraisal, and supervision of development projects.

Below are the areas that we are currently recruiting for. Positions may be based in Washington, D.C. or in a regional office.

Qualifications for the entry level is a Master's degree plus 5 years of relevant professional experience. For mid-career professionals, the requirements are a Master's degree plus 8 years of relevant professional experience. Ideal candidates for these positions must have a demonstrated capacity for strategic thinking, the ability to conduct dialogue on relevant development policies and priorities, and be fluent in English with very good writing and communication skills.

All applications must be received by August 31, 2015. Qualified candidates will be interviewed at the beginning of September 2015 in locations in Africa and Europe. Applications received after the closing date will not be considered.

To submit your application, please click the area(s) listed below.

CUF yamsafisha na kumkaribisha Lowasa

Ibrahim Lipumba (kijivu) na Edward Lowassa
Ibrahim Lipumba na Edward Lowassa

Chama cha Wananchi (CUF), kimeibuka na kumtetea aliyekuwa Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM), kilimuonea kwa kukata jina katika ngazi ya Kamati ya Maadili na kushindwa kulifikisha Kamati Kuu ya CCM (CC).

Lowassa alikatwa jina lake akiwa ni miongoni mwa wagombea 38 wa urais kupitia CCM, lakini inadaiwa kwamba aliondolewa katika hatua za awali kwenye Kamati ya Maadili.

Kadhalika, CUF kimesema kipo tayari kumpokea Lowassa ndani ya chama hicho kwa kuwa ni msafi na hajawahi kufikishwa hata mahakamani kwa ajili ya kushitakiwa kutokana na madai ya rushwa.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Abdul Kambaya, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Pilikapilika za uchaguzi nchini kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Star Tv.

Kambaya alirejea ripoti ya Kamati teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe mwaka 2008 kuchunguza kashfa ya Richmond ambayo ilimng'oa Lowassa katika nafasi ya Waziri Mkuu.

Alisema katika kamati hiyo, Dk. Mwakyembe aliweka bayana kwamba kila mtu aliyehusishwa ama kutajwa katika kashfa ya Richmond angefikishwa mahakamani kujibu mashtaka.

Kambaya alisema mpaka sasa Lowassa hajawahi kufikishwa mahali popote kushitakiwa na kwamba hatua hiyo inaoonyesha kwamba kiongozi huyo hakuwa na kashfa yoyote.

Alisema lengo la CUF ni kuing'oa CCM na kwamba ukiona kuna mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuitikisa chama hicho na kukipasua wapo tayari kumkaribisha ili washirikiane naye.

Alifafanua kuwa mtu ambaye siyo msafi hawezi kukaribishwa CUF na kwamba Lowassa kama angekuwa mchafu angekuwa ameshitakiwa mahakamani tangu alipojiuzuru mwaka 2008. Katika mjadala huo washirki walijadili matumizi makubwa ya fedha yaliyojionyesha ndani ya CCM tangu mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu ulipoanza.

Mwenyekiti CCM-Monduli 'abariki' madiwani wake kuhamia CHADEMA

Hali bado si shwari ndani ya CCM Wilaya ya Monduli baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Edward Sapunyo, Kupigilia msumari wa mwisho na kubariki hatua ya madiwani wake 20 kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Akizungumza mjini hapa jana, Sapunyo ambaye alikuwa Diwani wa kata ya Moita, alisema madiwani wake hawawezi kusubiri hadi Mbunge wa Jimbo la Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, atoe kauli kuhusu hatma yake ya kisiasa ndani ya CCM.

Kauli ya Sapunyo ambaye hatagombea udiwani uchaguzi wa mwaka huu, imekuja siku moja baada ya madiwani 20 wa jimbo hilo kutangaza rasmi kukihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
“Hatuwezi kuona baba yetu anapigwa na kuanguka chini halafu tusubiri kauli yake, ni lazima tuchukue hatua mara moja…hii haivumiliki, kitendo alichofanyiwa (Lowassa) na vikao vya CCM mjini Dodoma hivi karibuni kwa kukata jina lake pasipo kumpa haki ya kumsikiliza siyo cha kidemokrasia”
“Tumepigwa, tumesambaratika (CCM) Monduli, hatuwezi kuchukua fomu za kuomba kugombea au kutetea nafasi zetu ndani ya chama hiki, tumehamia CHADEMA”
Akizungumzia hali ilivyo, Katibu wa CCM Wilaya ya Monduli, Elisante Kimaro, alidai kuwa siyo kweli kwamba madiwani wote wamekihama chama chao.

Kimaro alidai kuwa baadhi ya madiwani waliotangaza kukihama chama hicho wameanza kusalitiana.

Alisema madiwani hao ambao anawaita ni makada baada ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Monduli kuvunjwa, walifanya mkutano kwa kushawishiwa na mmoja wao.

Alisema ushawishi huo unatokana na uchu wa madaraka alionao kwa kuwa tayari wananchi wa Jimbo la Monduli, wanapenda aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM, Namelok Sokoine, kuchukua fomu za ubunge wa jimbo hilo.

Alisema kutokana na ugumu huo, diwani huyo wa zamani ametumia mbinu ya kuwarubuni wenzake wakihame chama hicho ili agombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA.
“Huo ni uchu wa madaraka aliyo nayo,”
“Diwani huyo hakubaliki na wananchi wa kata yake."

Alidai kabla ya kutangaza kukihakama chama hicho, madiwani hao walikuwa wameshafanya kikao na kuweka azimio la pamoja la kuondoka CCM, lakini juzi walipotangaza uamuzi wao, walijikuta wapo madiwani watatu.

Alisema baadhi ya madiwani walimfuata ofisini kwa lengo la kumuomba radhi lakini yeye aliwaambia waende kuwaomba radhi wananchi katika kata zao.
“Madiwani wachache walikuja hapa ofisini kuomba radhi kwa Katibu wa CCM Wilaya, nikawaambia waende kuwaomba radhi wananchi” 
Akimzungumzia Lowassa, alisema anachoelewa ni kwamba hajatoa tamko lolote kama anakihama chama hicho kama inavyodaiwa na baadhi ya watu na mitandao ya kijamii.
“Bado tuna imani na Lowassa kuwa ni CCM, mpaka sasa hajatoa tamko lolote kukihama chama, lakini ikiwa vinginevyo itakuwa hatari kubwa,”
 alisema.

Bulaya kama Lembeli: Agoma kugombea Ubunge kupitia CCM

UPDATE/Taarifa Mpya Julai 21, 2015

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya amesema ndani ya saa 48 (kuanzia jana), atatangaza chama ambacho atahamia na kugombea ubunge.
“Ni kweli sigombei kupitia CCM, ila ndani ya siku mbili nitawaambieni chama ambacho nitatumia kugombea ubunge. Haya mambo ya vyama yapo tu na ni njia tu ya kupita, lakini lengo letu ni kuhakikisha tunaleta maendeleo kwa wananchi bungeni.
“Nilipokuwa CCM nilijitahidi kuleta maendeleo, lakini imefika wakati ambao nadhani nitaleta maendeleo zaidi kupitia chama kingine ambacho ndani ya siku mbili mtakijua,” 

Halima Mdee, Shy-Rose Bhanji, Ester Bulaya
Halima Mdee, Shy-Rose Bhanji, Ester Bulaya

Hali imeendelea kuwa tete ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Mara, Ester Bulaya, kutangaza kukitosa kwa kutangaza uamuzi wake wa kutogombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho.

Bulaya ambaye alikuwa mbunge machachari kabla ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvunjwa na Rais Jakaya Kikwete, hivi karibuni , ametangaza kutogombea ubunge kupitia CCM wakati akizungumza na NIPASHE baada ya kazi ya kuchukua fomu ndani ya chama hicho na kurejesha kuhitimishwa rasmi nchini jana.

Tangu mwanzo mwa mwaka huu, Bulaya alitangaza kugombea ubunge katika Jimbo la Bunda kupambana na Mbunge aliyemaliza muda wake ambaye ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira.

Bulaya amekuwa kada wa pili ambaye alikuwa mbunge kutangaza kutogombea ubunge kwa tiketi ya CCM, mbunge wa kwanza kutangaza kutogombea ubunge kupitia CCM baada ya James Lembeli, ambaye alikuwa Mbunge wa Kahama.

Hata hivyo, Bulaya hakuweka wazi kama ana mpango wa kuhamia chama kingine cha siasa na kutimiza azma yake ya kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Ingawa Bulaya hajaweka wazi, vyama ambavyo vimekuwa vikitajwa kusubiri makada kutoka CCM kujiunga navyo ili wawanie ubunge ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ACT-Wazalendo na Chama cha Wananchi (CUF).

Wizara ikishirikiana na "Diaspora" yawapokea Madaktari kutoka MarekaniPichani juu ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi RoseMary Jairo akiwakaribisha nchini Timu ya Madaktari kutoka Marekani mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam hivi karibuni. 

Madaktari hao wapo nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu kwa magonjwa mbalimbali katika Hospitali za Mwananyamala ya Jijini Dar es Salaam na Mnazi Mmoja, Zanzibar. 

Ziara ya Madaktari hao ambao wametoka Majimbo ya Washington DC, Maryland na Virginia imeratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania waishio Marekani (Diaspora).


Rais wa Jumuiya ya Watanzania waishio Marekani, Bw. Iddi Sandaly ambaye amefuatana na Madaktari hao kutoka Marekani akielezea jambo mara baada ya kuwasili nchini.


Bibi Jairo akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu dhumuni la ziara ya madaktari hao hapa nchini.


Mmoja wa Madaktari kutoka Marekani akizungumza na Waandishi kuhusu ziara yao hapa nchini


Bw. Sandaly akifafanua jambo kwa waandishi kuhusu ziara ya madaktari hao kutoka Marekani.
 • Imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje

Waliovamia Polisi Sitaki Shari wakamatwa na sh milioni 170/-, silaha

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova akionyesha picha za amajambazi sugu wanaotafutwa na jeshi la polisi katika hafla ya kutuoa taarifa za kukamatwa kwa askari wa waliovamia kituo cha stakishari leo jijini Dar es Salaam 

Watuhumiwa wa ujamabazi waliovamia Kituo cha Polisi cha Staki Shari jijini Dar es Salaam, wawili kati yao wametiwa mbaroni huku watatu wakiuawa wakati wakitupiana risasi katika eneo la Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea Julai 17 mwaka huu huko maeneo ya Toangoma, Kigamboni jijini Dar es Salaam katika msako wa majambazi wa tukio la kinyama la kuuwawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Sitaki Shari wanakadiriwa kuwa kati ya 16 hadi 18.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova amesema kukamatwa kwa majambazi hao inatokana na kikosi kazi kilichoundwa na kanda maalumu kwa kushirikia na Mkoa Pwani.

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa ujambazi kulitokana na taarifa pamoja na mtego wa kiintelejensia katika eneo la Toangoma ndipo majambazi wakapita na pikipiki mbili walipowasimamisha askari majambazi hao walikaidi amri nakisha kuanza kurusha risasi na polisi wakajibu na majambazi watatu kuuwawa.

Majambazi waliouawa ni Abbas Hashimu Mkazi wa Mbagala, Yassin alitambulika kwa jina moja mkazi wa Kitunda Kivule, pamoja Saidi aliyetambulika kwa jina moja mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga.

Kamanda Kova amesema wanaowashikiria ni Ramadhan Ulatule (15), Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga, Omary Amour (24) Mkazi Mkazi wa Mbagala Kimbangulile.

Kova amesema baada ya kuwabana watuhumiwa wa ujambazi walikwenda kuonyesha bunduki 14 na risasi 28 walizopora katika kituo cha Sitaki Shari ambazo walikuwa wamehifadhi chini ya ardhi kuweka kinyesi juu.

Amesema katika shimo walilohifadhi walikuta bunduki aina Norinko ambayo wanatafuta ilipoibwa, SMG 7, bunduki za SAR 7  pamoja na fedha taslimu shilingi milioni 170 za Kitanzania.

Aidha amesema jeshi la polisi limejizatiti katika matukio na kutaka watu waachane na biashara hiyo ya ujambazi kuwa halipi.

Amesema fedha hizo wanazichunguza kujua zimeibiwa wapi,na pikipiki mbili aina ya boxer nazo wanazishiria na kutaka wauza pikipiki kuuzia watu ambao wanataarifa nazo.

“Hatutafumbia macho kwa wale askari wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kuwachukulia hatua kali ikiwa hata kama wanajihusiha na ujambazi tutawashughulikia kwani risasi haichagui kuwa huyu raia au askari”amesema Kamishina Kova.

Tukio la kuawawa kwa askari wanne na raia watatu katika kituo cha Stakishari,lilitokea julai 12 majira ya saa nne.


Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Suleiman Kova akionyesha bunduki zilizoporwa katika uvamizi wa uliofanywa na majambazi katika kituo Sitaki Shari, TAZARA leo jijini Dar es Salaam.


Naibu wa Kamshina wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari juu operesheni iliyofanyika ya kuwakamata watuhumiwa wa ujambazi waliovyamia kituo cha Sitaki Shari ,Tazara, jijini Dar es Salaam.


Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Suleiman Kova akionyesha Fedha taslimu Sh. milioni 170 zilizkutwa katika Shimo na majambazi waliovyamia kituoa Sitaki Shari na kuua askari,leo jijiji Dar es Salaam.


Fedha za watuhumiwa ujambazi waliovamia kituo cha Polisi cha Staki Shari zikiwa katika sanduku zikionyeshwa kwa waandishi habari na wananchi leo jijini Dar es Salaam.


Pikipiki zilizokuwa zikitumiwa na majambazi waliovyamia Kituo cha Staki Shari zikiwa mbele ya Kamisha Kova wakati akitoa taarifa kukamtwa kwao leo jijini Dar es Salaam.
 • Imenukuliwa kutoka "Globu ya jamii" na gazeti la MWANANCHI

Taarifa ya habari "Asubuhi Njema" ChannelTEN Julai 20, 2015


Magazetini Julai 20, 2015

Job opportunity at Sikika for an HR & Admin. Manager (1 year Contract)

Join us in advocating for quality health services for all Tanzanians

Introduction

Sikika is a non-governmental organization that advocates for quality health services for all Tanzanians. For more information on our work please visit us at www.sikika.or.tz.

Title: Human Resources & Administration Manager (1 year Contract)

Work Station: Dar es Salaam

Reports to: Executive Director

Objective: To ensure that the organization has adequate, qualified human resources that are well equipped with suitable capacity to implement the Strategic Plan.

Responsibilities:
 • Be responsible for overall human resource management within the organization.
 • Be responsible for the maintaining the procedures and systems as outlined in the organisations human resources manual, which support human resource management for the organization and is available to answer any questions or provide clarification on any content of this manual. 
 • Process recruitment of new staff for Sikika
 • Ensure staffs performance appraisals are done on time
 • Be custodian of all official contracts between Sikika and other parties
 • Ensure documentation, filing and safe keeping of official Sikika documents
 • Organize and facilitate Management Team meetings
 • Be responsible for maintaining overall employment affairs of all the staff
 • Organise for socialization and job orientation to newly recruited staff
 • Ensure that the institution complies with the relevant laws and policies pertaining to employment.
Required Qualifications

Education

A Bachelor Degree or Masters degree in any Human resources Management or Business Administration or related discipline.

Work Experience

A minimum of 3 years working experience in the field preferably in NGO or CSO.

Key Skills, Knowledge and Abilities

The Jobholder must be fluent in written and spoken Swahili & English languages, and must have good coordination skills. The jobholder must also be well versed with the relevant laws and policies governing relationships between employers and employees.

Remuneration

An attractive remuneration package will be offered to the successful candidate.

Send your application papers by e-mail to: [email protected]. Attn: The Human Resources and Administration Manager, Sikika. Ladies are highly encouraged to apply

Application Deadline: July 25, 2015

Daudi Msungu achukua fomu za Ubunge


Kada mkereketwa wa CCM Ndugu Daudi Paulo Msungu mapema jana Julai 19, 2015 alifika makao ya CCM mjini Lindi kuchukua fomu kujaza na kuirudisha kwa ajili ya kuwania kiti cha ubunge wa jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya ridhaa ya chama cha Mapinduzi (CCM).