Mwaliko wa ibada ya kumuaga Balozi Mulamula

[update #4] CHADEMA: Matokeo ya kura kwa walioomba kuwania UbungeBaadhi ya wabunge wa CHADEMA wanaotetea viti vyao wameibuka kidedea katika kura za maoni zilizofanyika katika majimbo mbalimbali nchini jana.

Hao ni pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ aliyejizolea ushindi mnono wa kura 356 akiwaacha kwa mbali wapinzani wake, Joyce Mashine aliyepata kura43 na Tito Mwanjale kura 18. Wengine waliokuwa wakiwania kuteuliwa na chama hicho ni Lazaro Mwankemwa aliyepata kura 15, Christopher Nyenyembe (12) na Sishe Simbeye (6).

Mbunge mwingine, aliyepata ushindi wa kishindo ni Highness Kiwia wa Ilemela aliyejizolea kura 134 na aliyemfuatia alikuwa Gasper Mwanaliela ambaye alipata kura 28.

Wabunge wengine, Joshua Nassari hakuwa na mpinzani katika Jimbo la Arumeru Mashariki kama ilivyokuwa kwa David Silinde katika Jimbo la Momba.

Tafrani Mbarali


Awali, kulizuka tafrani iliyotokana na mgombea, Meshack Kapange kuenguliwa. Mgombea huyo alipinga akidai kuwa hakutendewa haki na kwamba kilichofanyika ni kumkingia kifua Sugu.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema Mbeya Mjini, John Mwambigita alisema Kapange alikwishavuliwa uanachama na suala la kuchukua fomu za kuomba ubunge ilikuwa ni haki ya kila mmoja.

Kapange alisema atakata rufaa kwa kuwa hakutendewa haki na wasimamizi wa mchakato huo... “Nimempigia Katibu Mkuu wa Chadema (Dk Willibrod Slaa), akaniambia yuko kwenye mkutano Mwanza, nitampigia kesho (leo) kumweleza kunyang’anywa haki yangu,” alisema. 

Tafrani Mbarali

Mzozo mwingine uliibuka Mjini Mbarali baada ya Jidawaya Kazamoyo aliyepata kura 109 kulalamika kuwa ndiye mshindi na kuzuka vurugu zilizosababisha Liberatus Mwang’ombe aliyeshinda kwa tofauti ya kura moja kutolewa nje ya ukumbi akiwa chini ya ulinzi mkali.

Matokeo ya kura ya maoni CHADEMA

Segerea: Anatropia Theonest (49), Kisheli Mchele 26 Masato Wasira (24), Baraka Sawema (15), Habron Mwakagenda (6), Bakari Yusuph (2), Loyce Gibona (2), Amos Maziku (0), Dominic Orembe (0), George Martin (0).

Lupa: Miraji Hussein amepata kura (65) na kuwashinda wenzake Njelu Kasaka (45) na Fillipo Mwakibinga (32).

Korogwe Mjini: Amani Kimea amewashinda kwa mbali wenzake watano kwa kupata kura 56. Aliyefuata ni Mwakolo Wynjones (26), Calistus Shekibaha (8), Steven Kimea (4), Benson Mramba (1) na Grayson Kibwana (0).

Busega: David Nicad (116), Buluba Mabelele (67), Revocatus Madundo (55), Modest Masunga (4), Sajda Dotto (3), Mapambano Ochalo (2), Keneddy Lufulondama (1), Adam Komanya (0), Lutandula Mabimbi (0) na Mhere Mwita (0).

Sikonge: Godfrey Ndaki (16), Moses Kaombwe (17), Dk Mmeta Yongolo (19), Mtemi Zombwe (70) na Hija Ramadhani 83.

Manyoni: Alute Emmanuel (171) na Thedey Meremeta (47)

Vwawa:
Fanuel Mkisi (136), Stephen Mwamengo (42), Solomon Kibona (22), Andrea Bukuku (9), Fadhil Shombe (8), Bob Mwampashe (5) na Jonathan Mwashilindi (5).

Ilemela: Highness Kiwia (134), Gasper Mwanaliela (28), Bugumba Nsumba (20), Wema Dilala (17), Deus Ng’hanyanga (15), Edwin Sarungi (13), Telexphone Masalu (8), Kageshiza Mwendesha (7), Mayalo Kasili (3), Thobias Mogole (7), Magesa Masinde (6), Damas Kimenyi (5), Habath Matalu (5), Greyson Wanzagi (13), Darius Ngocho (5), Humphrey Mmanda (3), Malehe Sweta (3) na Frederick Mataja (2).

Mbozi: Paschal Haonga (82), Fredy Haonga (34), Sophia Mwabenga (18), Ambukusye Kabango (4), Eliud Kibona (3), Anastazia Nzowa (2), Eliud Msongole (1), Seule Nzowa (1) na Zabron Nzunda (1).

Ileje:
Emmanuel Mbuba (98), Gwamaka Mbughi (66) na Emmanuel Msyani (37).

Tunduma: Frank Mwajoka (130), Victor Nkonjela (20) na Clemence Nyondo (15).

Momba: David Silinde hakuwa na mpinzani.

Babati Vijijini:
Daniel Karenga (14), Esther Sarwatt (17), Herman Sanka (5), Leonard Mao (3), Salum Shawishi (8) na Lawrence Tara (288).

Arumeru Mashariki:
Joshua Nassari amepita bila kupingwa.

Makambako: Olaph Mhema (72), Fred Kalonga (57) na Kheri Kisingile (0).

Kibaha Mjini: Michael Mtali (62), Henry Msokwa (38), Ishaka Mnembwe (31), Joachim Mahega (13), Bosco Mfundo (4) na Frank Mzoho (3).

Mbeya Mjini: Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (356) Christopher Nyenyembe (12), Joyce Mashine (43), Lazaro Mwankemwa 15, Tito Mwanjale (18) na Sishe Simbeye (6).

Mbarali: Liberatus Mwang’ombe (110), Jidawaya Kazamoyo (109), Tazan Ndingo (25), Grace Mboka (14) na Dickson Baragasi (9).
Kura za maoni ndani ya CHADEMA zimeanza kuwa chungu kwa baadhi ya wabunge.

Mbunge wa Mbulu, Mustapha Akoonay na mwingine wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (Kinondoni) jana waliangukia pua, huku mwenzao wa Karatu, Mchungaji Israel Natse akitangaza kuachana na ubunge na kurejea katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Lyimo alianguka baada ya kupata kura 32 nyuma ya Mustafa Muro aliyepata kura 47. Wengine ni Rose Moshi (8), Agrey Mkwama (6), Gemeral Kaduma (4) na Francis Nyerere (0).

Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema tayari uchaguzi umefanyika katika majimbo matano.

Alisema Mbulu Mjini, kulikuwa na wagombea wawili, Akoonay alipata kura 108 dhidi ya 132 alizopata Diwani wa Mbulu, Michael Sulle.

Golugwa alisema, Joseph Selasini ametetea nafasi yake katika Jimbo la Rombo baada ya kupata kura 313 akiwaacha mbali wapinzani wake Ben Sanane aliyepata kura 26 na wengine kura mojamoja.

Babati Mjini, Mbunge wa Viti Maalumu, Paulina Gekur ameibuka kidedea kwa kura 88 akiwatupa nje wapinzani wake, akiwamo mkuu wa wilaya wa zamani, Gabriel Kimolo na wenzake.

Mbulu Vijijini, Aman Gaseri alishinda kwa kura 76 huku Michael Aweda akipata 75.

Jimbo la Same Magharibi:
Jonas Kadeghe alishinda kwa kura 68 akifuatiwa na Christ Mbanjo aliyepata kura 49 na Gervas Mgonja kura 30.

Muleba Kaskazini: Najim Kasange alipata kura 247 na kumshinda mwandishi wa habari mkongwe, Ansbert Ngurumo aliyepata kura 55. Mgombea mwingine, Christina Mwainunu alijitoa.

Jimbo la Ukonga, Nickson Tugara alishinda kwa kura 59 hivyo kuwaacha kwa mbali wagombea wenzake 14. Alifuatiwa na Waitara Mwikwabe aliyepata kura 49, Elly Dallas (15), Deogratias Munishi (8), Lucas Otieno (6), Asia Msangi na Deogratias Mramba waliopata kura tano kila mmoja na Gasto Makwetta (1). Wengine saba hawakuambulia kura hata moja.

Butiama: Yusuf Kazi aliibuka kifua mbele baada ya kujikusanyia kura 202 na kuwapiku Adam Taya (39) na Issa Yusuf (31), Daniel Obeiya (3), Annicent Marwa (2) na Lucas Ossoo na Marto Yohana waliopata kura moja kila mmoja.
Nyamagana: Wenje aliibuka kidedea kwa kupata kura 194 na Patrick Masagati (32).

Msalala: Paulo Ndundi alishinda kwa kura 113 akiwashinda Peter Machanga (49) na Ezekiel Kazimoto (48). Wengine ni Emmanuel Mbise (43), Francis Makune (15), Vincent Manoni Mhagwa (10) na Richard Mabilika aliyepata kura moja na Stephen Bundala (0).

Sumbawanga: Shadrack Malila aliibuka na ushindi wa kura 277 dhidi ya Kassian Kaegele (28), Musa Ndile (9) na Matokeo Lyimo (1), Eliud Mwasenga na James Kusula (0).

Nkasi Kusini: Alfred Sotoka aliongoza kwa kupata kura 70 akifuatiwa na Kaminga Hyporito (39), Emmanuel Sungura (9), Edson Ndasi (4) na Joseph Kitakwa (2).

Nkasi Kaskazini: Keissy Sudi alishinda kwa kura 158 na kufuatiwa na Triphone Simba (70) na Stanley Khamsini (5).

Kwela: Daniel Ngogo aliwabwaga wenzake kwa kura 151 akifuatiwa na James Mwamlyela (117), Ameri Nkulu (27), Alstidi Maufi (13) na Michael Moka (4).

Mlalo: Kelvin Shemboko alipata kura 56 akifuatiwa na Lewis Kopwe (31), Jumanne Pazia (15) na Mkazeni Mkazeni (0).[update] Hackers take control of Jeep Cherokee and crash it into a ditch

After narrowly averting death by semi-trailer, I managed to roll the lame Jeep down an exit ramp, re-engaged the transmission by turning the ignition off and on, and found an empty lot where I could safely continue the experiment. -  ANDY GREENBERG

Hackers took control of a car and crashed it into a ditch by remotely breaking into its systems from 10 miles away whilst sitting on their sofa.

In the first such breach of its kind, security experts cut out the engine and applied the brakes on the Jeep Cherokee - sending it into a spin.

The US hackers said they used just a laptop and mobile phone to access the Jeep’ s on-board systems via its wireless Internet connection. [The DailyMail]

The original story is at WIRED: Hackers Remotely Kill a Jeep on the Highway—With Me in It

See the video below...

Cheka kidogo: Usajili katika klabu za siasa kwa fainali ya Oktoba


Baada ya dirisha la usajili kufunguliwa nchini TZ baadhi ya klabu zimekwisha kukamilisha uhamisho wa wachezaji.

-Klabu ya ACT imefanikiwa kunasa saini ya mshambuliaji hatari wa NCCR Moses Machali, nayo

-Klabu ya CHADEMA inafikiria kumsajili mlinda mlango wa (CCM) aliyekosa namba kwenye kikosi cha kwanza cha CCM Eduwad Lowassa huku dau lake likitarajiwa kuvunja rekodi ya duniani.

-Na klabu ya CUF nayo iko mbioni kumsajili mlizi wa (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru ambaye kwasasa hana furaha klabuni hapo.

-Wakati klabu ya NCCR Mageuzi ikihaha kupata mbadala wa nyota wake aliyetimkia ACT Machali taarifa zinasema klabu hiyo imeanza mazungumzo na winga wa (CCM) Makongoro Nyerere aliyesumbuliwa na majeruhi kwa msimu mzima juu ya kujiunga na miamba hiyo ya NCCR Mageuzi.

-Naye winga wa (CCM) James Lembeli amezungumzia hatma yake klabuni hapo na amesema yuko tayari kuondoka endapo wachezaji wenzake wataendelea kumchezea rafu kwa kipindi cha kujianda na msimu wa ligi, zipo klabu nyingi zinawania saini mchezaji huyo ila yeye anatamani kujiunga na Chadema.

-Baada ya ACT kuikosa saini ya mchezaj wa (CCM) (Shibuda) aliyekuwa kwa mkopo Chadema, ACT wameelekeza nguvu zao kwa mchezaji nguli wa CCM Emanuel Nchimbi ambaye amevurugana na timu yake.

-CCM imempeleka tena kwa mkopo - TADEA mchezaji Shibuda kwa mkataba wa miaka 4 hadi 201.

Wakati huo huo mchezaji wa CCM mwenye machachali mengi, Ester Bulaya nae ametangaza kuikacha Klabu yake hiyo zamani na kutimkia Chadema baada ya kutangaziwa donge nono.

-Said Arfi, amerejea kwenye timu yake ya zamani CCM baada kumaliza mkataba wake wa miaka 10 akiwa chadema

Kwa tetesi zingine ni kesho tukijaaliwa...

Waziri ateua Mkurugenzi Mkuu mpya TCRA

Dk. Ally Y. Simba
Dk. Ally Y. Simba

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa hivi karibuni alimteua Dk. Ally Yahaya Simba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, (TCRA) kufuatia mchakato wa kumpata Mkurugenzi Mkuu kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mawasiliano ya 2003 kifungu cha 9 na kifungu cha 13. (TCRA Act, 2003)

Dk. Simba aliteuliwa rasmi kushika wadhifa huo mnamo tarehe 6 Jula1 2015 kwa kipindi cha miaka mitano. Kabla ya uteuzi huo, Dk. Simba alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia tangu Agosti 2013. Dk. Simba ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 katika Sekta ya Mawasiliano ambapo amefanya kazi kwa watoa huduma, Taaluma ya Utafiti, Udhibiti pamoja na Serikali Kuu.
Dk. Simba ana Shahada ya B.Sc. (Hons.) Shahada ya Sayansi ya Elektroniki na Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania, aliyopata mwaka 1998. Pia ana Shahada ya Uzamili ya Uhandisi aliyoipata mwaka 2003 na Shahada ya Uzamivu (Ph.D) ya Uhandisi wa Kielektroniki kutoka Chuo Kikuu Cha Hokkaido, Sapporo, nchini Japan, aliyoipata mwaka 2006. Kuanzia mwaka 2006 mpaka 2011, Alikuwa Mtaalamu Mtafiti katika Taasisi ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, huko Tokyo, Japan, ambako alihusika katika kufanya utafiti wa madhara ya ya kiafya kwa mwanadamu kwa kutumia simu za mikononi na kwa kuwa karibu na minara ya mawasiliano.

Mnamo mwaka 2011 hadi mwaka 2013, alifanya kazi Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kama Meneja Mipango na Utafiti wa Mamlaka.

Dk. Simba ametoa machapisho kadhaa yaliyosambazwa kote duniani katika majarida ya kimataifa na amewasilisha matokeo ya tafiti zake katika zaidi ya mikutano 30 ya kimataifa ndani na nje ya Tanzania. Aidha Dk. Simba alikuwa Kiongozi wa timu ya wataalamu wa Kitanzania iliyoandaa Sheria za Uhalifu wa Mitandao nchini iliyopitishwa na Bunge hivi karibuni.

Dk. Simba ni Mhandishi Mahiri (Chartered Engineer), aliyesajiliwa nchini Uingereza katika Baraza la Uhandisi nchini humo na ni “Fellow” wa Taasisi ya Uhandisi na Teknolojia ya nchini Uingereza, ambako alifanya kazi kama Mshauri wa Kimataifa wa Usajili wa Wanataaluma Wahandisi kutoka Aprili 2011 mpaka Machi 2014. Pia Dk. Simba ni Mwanachama wa “Institute of Electrical and Electronics Engineers” (IEEE). Hali kadhalika Dk. Simba amechapishwa katika jarida la “Marquis Who's Who in Science and Engineering” katika toleo la 11, la mwaka 2011–2012.

Dk. Simba ni miongoni waliopata Udhamini wa Serikali ya Japan (Monbukagakusho Scholarship) kutoka mwaka 2000 mpaka 2006.

Gia za kuombea "kula": Mgombea asema, "Magufuli rafiki yangu sana, ananipenda sana, nimesoma naye"

Mwania ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Dodoma Mjini, Dk. David Malole amenukuliwa akisema kuwa:
“Magufuli ni rafiki yangu sana na ananipenda sana kwa sababu nimesoma naye shule moja ya seminari, naimani kwa kushirikiana naye tutawaletea maendeleo,” 
Dk. Mallole alitoa kauli hiyo jana mjini hapa wakati alipokuwa akijinadi mbele ya wanachama wa CCM na wananchi wa Kata ya Nala iliyopo wilaya ya Dodoma Mjini.

Mbali na hilo aliwatumainisha wananchi wa jimbo la Dodoma mjini kuwa iwapo atachaguliwa tena kuna uwezekano mkubwa wa kupatiwa nafasi mbalimbali ya uongozi ndani ya serikali jambo ambalo litachochea maendeleo katika jimbo hilo.

"Mchungaji" akamatwa kwa 'kuwalisha' waumini nyoka hai, mijusi, panya, makaratasi, vitambaa


Mchungaji mmoja wa Kanisa mwenye umri wa miaka 24 amekamatwa na Polisi mwishoni mwa juma lililopita huko nchini Afrika Kusini akituhumiwa kuwalisha waumini wake nyoka walio hai Kanisani.

Mchungaji huyo mwenye msimamo mkali aliwambia waumini wake kuwa nyoka hai wana ladha ya chokoleti na yeyote atakula akiwa na imani thabiti.

Mchungaji huyo, Penuel Mnguni alikamatwa baada ya kuonekana kwa picha katika mtandao wa kijamii akiendesha tukio hilo.

Kiongozi katika shirika la kutunza wanyama Afrika limemshataki mchungaji huyo kwa kusema kuwa nyoka hailiwi akiwa nzima na kuwa kitendo hicho kimewaathiri watoto walikuwa katika Kanisa hilo.

Shirika la SPCA linamshtumu pia Mchungaji huyo kuwalisha "kondoo" wake panya na mijusi.

Mwaka 2014, mchungaji mwingine nchini humo aliwalisha waumni wake majani mabichi na ukoka kwa kuwaamuru kuketi ama kuinana na kuyala kwa midomo yao. Imeelezwa kuwa mchungaji Penuel ni mmoja miongoni mwa wafuasi wa Mchungaji huyo.


EATv: Weusi - Zamu Yako 2015

Huu ni wimbo maalum ulioimbwa na kundi la "Weusi" kwa ajili ya kampeni ya "Zamu Yako 2015" iliyoanzishwa na kituo cha East Africa Television na East Africa Radio ikiwa na lengo la kumhamasisha kijana kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na pia kupiga kura katika uchaguzi mkuu ifikapo mwezi Oktoba.Kubenea achukua fomu kuwania Ubunge Ubungo


SAED Kubenea, ameamua kuvunja ukimya baada ya uvumi kuenea kuwa alikuwa na nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Mafia mkoa wa Pwani baada ya kuchukua fomu rasmi kugombea ubunge Jimbo la Ubungo, Dar es Salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari leo mchana makao makuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amesema 
“Nimeamua kugombea jimbo la Ubungo ninaamini ni demokrasia na ni haki yangu kufanya hivyo kama mtanzania” huku akizungumza kwa kujiamini kwa kurejea kauli ya baba wa Taifa, Mwl. Nyerere aliyesema “wananchi wanahitaji mabadiliko, wasipoyapata ndani CCM watayatafuta nje ya CCM”.
Kwa vile wananchi wameshindwa kupata mabadiliko ndani ya CCM , Kubenea amesema ameamua kugombea nafasi hiyo kupitia tiketi ya CHADEMA, chama makini, ili aweze kuwa sehemu ya Bunge ya kutunga sheria na kuisimamia serikali kwa maslahi mapana ya watanzania na ustawi wa nchi kwa ujumla.

Alipoulizwa kuwa haoni kuwa kutakuwa na mgongano kati yake na John mnyika (MB), kwa kugombania jimbo hilo, na kama alishaomba ushauri kutoka kwa Mnyika, Kubenea amesema haoni tatizo kwani demokrasia inaruhusu yeyote mwenye sifa kugombea, zaidi ya hayo alisema sio vizuri kuongea naye kwani yeye ni Naibu Katibu Mkuu (Bara), ana nafasi kubwa ndani ya chama na yeye ni kiongozi wa wagombea wengine wote, kujadiliana naye ni kufanya ‘lobbying’, akimaanisha kufanya ushawishi kitu ambacho sio utawala bora na ni kunyima haki kwa wengine.

Hata hivyo Kubenea alisema akipata fursa atamshauri Mnyika kwenda kugombea jimbo jipya la Kibamba. Alipoulizwa endapo hataafiki kwenda Kibamba amesema ataamua kumuachia.

Waliojitokeza CCM hadi sasa na majimbo wanayowania Ubunge


Sengerema: William Ngeleja, Lawrence Masha, Anna Shija, George Rweyemamu, Philemon Tano, Dk Omari Sukari, Dk Angelina Samike, Jumanne Mabawa, Mussa Malima, Baraka Malebele, Joshua Shimiyu na Zablon Bugingo

Nsimbo, Katavi: Said Arfi, Shabir Hasanari “Dallah’, Richard Mbogo, Manamba David na Mapesa Frank.

Katavi, Katavi: Isaack Kamwelwe, Shafi Mpenda, Maganga Kampala na Oscar Albano.

Kavuu, Katavi: Zumba Emmanuel, Mselem Said na Prudenciana Kikwembe.

Mpanda Mjini, Katavi: Sebastian Kapufi, Galus Mgawe na Gabriel Mnyele na katika Jimbo la Mpanda Vijijini ni Moshi Kakoso, Abdallah Sumry, Willy Makufe, Elizabeth Sultan, Godfrey Nkuba, Rock Mgeju na Chifu Charles Malaki.

Bagamoyo: Dk Shukuru Kawambwa, Abdul Zahoro, Muharami Mkenge, Salim Abed, Mbonde Mbonde, Mathew Yungwe, Maulid Mtulya, Fabian Said, Lekesani Mvule na Chacha Wambura.

Chalinze: Ridhiwan Kikwete, Iman Madega, Mbaraka Tamimu, Changwa Mkwezu, Omar Kabanga na Hamis Devile.

Kibaha Mjini: Silvestry Koka, Rugemalira Rutatina, Idd Majuto, Rashid Bagdela na Abdulaziz Jadi.

Kibaha Vijijini: Dk Ibrahim Msabaha, Hamoud Jumaa, Bureta Allen, Hussein Chuma, Janeth Munguatosha na Shomary Sangali.

Kahama Mjini: Jumanne Kishimba, Wilbert Nkuba, Deogratius Sazia, Deogratius Mpagama, Adam Ngalawa, Michael Bundala, John Nyenye, Andrew Masanje, Masubo Julius, Luhende Shija na Godwin Kitonka.

Ushetu: Elias Kwandikwa, Isaya Bukakie na Erhard Mlyasi.

Msalala: Ezekiel Maige, John Sukili, Emmanuel Kipole, Nicholaus Magangila, John Lufunga na Wakilala Mashara.

Geita Mjini: Ngara Kanyasu, Daffa Daffa, Dk Samweli Opulukwa, Jacob Mtalitinya, Paschal Malugu, Mathayo Melikiory, Dk Leonard Mugema, Regina Mikenzi, Evarist Nyororo, Juma Malunga na Chacha Mwita.

Geita Vijijini: Jivitius Sabatho, Ernest Mabina, Thoma Ntogwakulya, John Marco, Emmanuel Sherembi na Joseph Msukuma.

Busanda: Tumaini Magesa, Lolesia Bukwimba, Luchenche Mbatilo, Francis Kiganga, John Mhonzu, Sostenes Kulwa na Marko Malembeka.

Buchosa: Dk Charles Tizeba na Eston Malima.

Mbeya Mjini: Christopher Nyenyembe, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Lazaro Mwankemwa.

Kyela: Bernard John, Babylon Mwakyambila, Lusekelo Mwasasumbe, Godfrey Mwakalukwa, Dickson Mwaipopo, Denis Maria, Claud Fungo, Bruno Lupondo, Michael Mwasanga, Clemency Kyando, Alinanuswe Mwalwange na Abraham Mwanyamaki.

Busokelo: Dk Stephen Kimondo, Ambakisye Mwakifwange, Asifiwe Mwakalobo, Isack Mwambona, Boniface Mwabukusi, Elias Mwakapimba, Simon Mwamaso na Elisha Mwambapa.

Rungwe: Deogratius Mwailenge, Ayubu Mwakasole, Nicodemas Ngwala, Ahobokile Mwaitenda, Sophia Mwakagenda, John Mwambigija, Barnaba Pomboma, Brown Mwaipasi, Yassin Mwakisole, Festo Mwaipaja, Christopher Kitweka, Richard Mbalase, Wilfredy Mwaipyana, Bertha Mwakasege, Daud Mwasanga na Yusuph Asukile.

Mbarali: Jidawaya Kazamoyo, Dickson Baragasi, Grace Mboka, Tazan Ndingo, Rajab Msingo, Liberatus Mwang’ombe na Ronilick Chami.

Lupa: Victor Kinyonga, Ernest Mwamengo, Philipo Mwakibingo, Enock Mageta, Emil Mwangwa, Sande Sanga, Moses Mwaifunga, Mohamed Hussein, Jamson Mwiligumo, Njelu Kasaka, George Mwaipungu na Peter Noah.

Mbozi: Eliud Msongole, Abraham Msyete, Solomon Kibona, Eliud Kibona, Zablon Nzunda, Abdul Nindi, Anastazia Nzowa, Happiness Kwilabya, Fannuel Mkisi, Furaha Mwazembe, Gift Kalinga, Pascal Haonga, Andrew Bukuku, Ambakisye Kabango, Stephen Mwakingili, Jerald Silwimba, Fadhil Shombe, Jonathan Mwashilindi, Fredy Haonga, Bob Mwampashe, Ostern Meru, Sophia Mwabenga, Mochael Mtafya, Mchungaji Wilhelm Mwakavanga, Seule Nzowa na Dickson Kibona.

Mbeya Vijijini: Moses Mwaigaga, Chance Mwaikambo, Franco Mwalutende, William Msokwa, Stephano Mwandiga, Frank Mwaisumbe, Elias Kwimba, Antony Mwaselela, Wila Jacob, John Mwamengo, Jeremiah Mwaweza, Adson Sheyo, Emmanuel Shonyela, Alimu Mwasile, Adam Zella, Nhungo Jisandu, Daud Mponzi na Cyprian Magulu.

Ileje: Nicolaus Mtindya, Emmanuel Mbuba, Emmanuel Msyani, Gwamaka Mbughi, Cosmas Sikinga, Leornad Fumbo, Joel Kajinga na Riziki Mbembela.

Songwe: Mpoki Mwankusye, Michael Nyilawila, John Mwaniwasa, Ofugan Wanga na Frank Mwakitalima.

Babati Vijijini: Omary Kwaang’, Damas Nakey, Vrajlal Jituson, Hassan Kaniki, Vencent Naano, Faustine George, Mary Geai, Charles Ingi, Jamal Mukta, Valerian Margwe, Atanas Kijuu, Stephano Manda, Daniel Sulle, Laurent Tara, Ester Sarwat, Leonard Mao, Daniel Marko, Herman Sanka, Salum Shawishi. Christina Kembe, Ester Sarwat na Respikia Muna (viti maalumu).

Babati Mjini: Kisyeri Chambiri, Haines Darebe, Ally Msuya, Ally Sumary, Sulei Doita, Samo Samo, Cosmas Masauda, Ramadhan Slaa, Paulina Gekul na Gabriel Kimolo.

Hanang’: Dk Mary Nagu, Dk Eliamani Sedoyeka, Peter Nyalandu, Deusdedit Mayomba, Derick Magoma, Nada Shauri, Cyiril Ako, Leonard Guti, Whilhelem Gidabudai, Dk Haite Samo na Rose Kamili anayegombea viti maalumu.

Mbulu Mjini: Zacharia Isaay, Peter Pareso, Andrew Aqweso na Juma Marmo.

Mbulu Vijijini: Fratley Gregory, Martha Umbulla, Malkiani Nari, Dk Isack Maleyeki na Simon Daffi.

Simanjiro: Christopher Ole Sendeka, Peter Toima, Simon Ndwala na James Ole Millya.

Kiteto: Benedict Ole Nangoro, Emmanuel Papien, Amina Mrisho, Joseph Mwaseba na Ally Lugendo.

Ukerewe: Sumbuko Chipanda, Osward Mwizalubi, Christopher Nyandiga, Deogratias Lyato, Dk Elias Misana, John Mkungu, Magesa Boniphace, Hezron Tungaraza, Dk Deusdedit Makalius, Marick Marupu, Laurent Munyu, Bigambo Mahendeka, Bandoma Kabulile, Gerald Robert na Emerciana Mkumbulo.

Bariadi: Andrew Chenge, Masanja Kadogosa, Cosmas Chenya na Joram Masanja.

Meatu: Donald Masanga, Oscar Paul, Romana Kitija na Salum Mbuzi.

Itilima: Daud Njalu, Masanja Ngangani, Dani Makanga, Kulwa Njanja na Hilu Kibilu.

Kisesa: Ruhaga Mpina

Maswa Mashariki: Michael Jilala, Mashimba Ndaki, Benjamin Tungu, Aron Mboje na Henry Nditi.

Maswa Magharibi: Jonathan Ngela, Stanslaus Nyongo, Ally Mtegwa, George Lugomelo, Edward Bunyongoli na George Nangale.

Busega: Dk Titus Kamani, Dk Rafael Chegeni, Bernard Kibese, Igo Shing’ombe, Dismas Shwea, Robert Nyanda, Nyangi Msemakweli na Josephat Mkwabi.

Njombe Kusini: Edward Mwalongo, Alfred Luvanda, Arnold Mtewele, Vitalis Konga, Mariano Mwanyigu, Romanus Mayemba, Deiniol Msemwa na Hassan Mkwawa.

Njombe Kaskazini: Laula Malekela, Emmanuel Nyagawa, Joram Hongoli, Lemah Hongoli, Osmund Malekela, Mussa Mgata, Gaston Kaduma, Avike Kyenga na Oscar Msigwa.

Ludewa: Deo Filikunjombe, Zephania Chaula na Kapteni Mstaafu Jacob Mpangala.

Makete: Dk Binilith Mahenge, Dk Noman Sigala, Lufunyo Kinda, Bonic Mhami na Fabian Mkingwa.

Wanging’ombe: Gerson Lwenge, Thomas Nyimbo, Yono Kevela, Kenned Mpumilwa, Malumbo Mangula, Abraham Chaula, Richard Magenge, Petro Dudange, Hoseana Lunogelo, Nobchard Msigwa, Eston Ngilangwa na Abel Badi.

Makambako: Deo Sanga na Alimwimike Sahwi.

Viti Maalumu Njombe: Pindi Chana, Neema Mgaya, Nebo Mwina, Rosemary Staki, Suzan Kolimba, Margaret Kyando na Erica Sanga.

Kilombero: Kanali mstaafu Harun Kondo, Vitus Lipagila na Abdullah Lyana, Oscar Mazengo, Japhet Mswaki, Paul Mfungahema, Abubakari Asenga na Abdul Mteketa.Cheyo/UDP kuchagua wa kumuunga mkono mgombea Urais Tanzania 2015


Godwin Gondwe awania Ubunge Ilemela


Masha aenda Sengerema awaachia Nyamagana wapambane na WenjeWaziri wa zamani wa Mambo ya Ndani ya nchi, Lawrence Masha amemkwepa hasimu wake kisiasa, Ezekia Wenje katika Jimbo la Nyamagana, Mwanza na kwenda kugombea ubunge Sengerema ambako atavaana na mbunge anayemaliza muda wake, William Ngeleja.

Aidha, aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Said Arfi ambaye hivi karibuni alitangaza kujivua uanachama wa chama hicho, amejiunga na CCM na amechukua fomu za kuwania ubunge katika Jimbo la Nsimbo, Katavi.

Katika uchaguzi uliopita mwaka 2010, Masha aligombea kipindi cha pili katika Jimbo la Nyamagana (CCM), katika mpambano uliokuwa na ushindani mkali na kuangushwa na Wenje wa CHADEMA.

Awali, kabla ya uchaguzi huo, Masha akiwa waziri mwenye dhamana na mambo ya ndani, alimwekea pingamizi Wenje akidai hakuwa raia, lakini hoja hiyo haikumzuia mshindani wake, badala yake ilimwongezea kura za huruma hadi akaibuka mshindi.

Safari hii Masha amepima maji na kuamua kumvaa waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Ngeleja ambaye hivi karibuni alikuwa miongoni mwa wanaCCM 38 walioomba kuwania urais, lakini akaondolewa katika hatua za awali.

Alipoulizwa jana, Masha alisema amechukua fomu Sengerema kwa sababu ni nyumbani kwao, ndipo alikozaliwa na kukulia, hivyo ameamua kushirikiana nao kusukuma gurudumu la maendeleo.
“Nyamagana pia ni nyumbani, hivyo tutaendelea kushirikiana ili kuleta maendeleo kwa kila jimbo. Sijafanya maridhiano yoyote ya kuachiana jimbo, lakini natumia haki yangu ya kugombea popote,” 
alisema.

Hata hivyo, hata katika jimbo la Sengerema alikoomba kugombea hayuko salama kutokana na nguvu ya upinzani iliyopo kupitia Chadema ambacho nguvu yake ilidhihirika katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Desemba mwaka jana pale ilipochukua viti vyote katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Sengerema na maeneo mengine ya vijijini.

Mbali na Masha na Ngeleja, wengine waliojitokeza katika jimbo hilo kupitia CCM ni Anna Shija, George Rweyemamu, Philemon Tano, Dk Omari Sukari, Dk Angelina Samike, Jumanne Mabawa, Mussa Malima, Baraka Malebele, Joshua Shimiyu na Zablon Bugingo. 

[via MWANANCHI].

Lowasa "akaribishwa" CHADEMA; Turejee [video] alichosema Dk Slaa 2012
Baadhi ya wabunge wa Chadema wamezungumzia taarifa zinazosambaa zikieleza kuwapo mkakati wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhamia katika chama hicho, wengi wao wakimkaribisha.

Wakati wabunge hao wakikubali kumpokea, Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa amesema wananchi wasubiri mambo yatakapokuwa tayari badala ya kutegemea mitandao ya kijamii.

“Nitazungumza pale mambo yatakapokuwa sawa, siwezi kuzungumza sasa, subirini… sasa hivi mambo mengi yanazungumzwa kwenye mitandao,” alisema Dk Slaa ambaye pia anatajwa kuwa mgombea wa chama hicho ndani ya Ukawa.

Msemaji wa Lowassa, Aboubakary Liongo alipoulizwa kuhusu kuwapo kwa mpango huo alisema hawezi kulizungumzia hilo kwa kuwa ni suala la mtu binafsi. Hata hivyo, jitihada za kumpata Lowassa jana hazikufanikiwa kwani simu yake iliita pasi na kupokewa.

Hivi karibuni, idadi kubwa ya madiwani wa CCM walirudisha kadi zao na kujiunga na Chadema wakisema sababu ni kutoridhishwa na kukatwa kwa jina Lowassa kati ya wagombea urais wa CCM.

Kadhalika, mtandao wa kijamii uliokuwa ukimuunga mkono mbunge huyo wa Monduli unajulikana kwa jina la 4U Movement ulitangaza kuhamia Chadema hali inayoashiria kuwa kuna dalili ya Lowassa pia kujiunga nao.

Wakiandika katika akaunti ya Twitter ya 4U Movement, wafuasi hao walisema: “Ukimya ni hekima na ukimya ni busara. Ukimya wa Edward Lowassa ni kutafakari Safari ya Matumaini... Tuungane kuyapata mabadiliko nje CCM.”

Akizungumzia taarifa hizo, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alikifananisha chama hicho na kanisa ambalo kwa kawaida halikatai mtu, bali linawapokea wenye dhambi na kuwaongoza kufanya toba.

“Chadema ni kama kanisa, hakataliwi mtu, tunahubiri habari njema ya wokovu, ukija hapa unatubu unaendelea kufanya kazi,” alisema.

Kuhusu viongozi wa CCM kuhamia Chadema, Msigwa alisema inawezekana kasi hiyo inachagizwa na Lowassa kukosa nafasi aliyoitaka ndani ya chama hicho.

“Unapokuwa mwanasiasa unakuwa na wafuasi, inawezekana wengine wanaohamia Chadema ni watu wake ambao wameona mtu wao amekosa nafasi aliyoitaka ndiyo maana wanakihama chama,” alisema.

Msigwa alisema Chadema ilikuwa inakusanya wanachama wapya kwa muda mrefu hata kabla ya vuguvugu la Lowassa na chama chake kuibuka na ushindi na wanaohamia wanafanya hivyo kwa sababu wanakipenda chama na wameichoka CCM.

Akizungumzia ujio wa Lowassa kwenye chama hicho, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisema iwapo Lowassa atahamia Chadema anakaribishwa na huenda akaitimiza safari yake ya matumaini.

“Namkaribisha Lowassa Chadema, huenda safari yake ya matumaini ikaishia huku, akawa mwanachama au hata kiongozi,” alisema.

Alisema hakuna shaka kuwa mbunge huyo wa Monduli ana nguvu ndani ya CCM ndiyo maana viongozi wengi wa chama hicho wanakihama wakati huu.

“Hiyo ilijionyesha kuanzia kwenye Kamati Kuu ya CCM, Halmashauri Kuu, Lowasa amekamata wajumbe kwa asilimia 80 na hiyo ni ishara kuwa ameishika CCM,” alisema.

Lema aliongeza kuwa wanaoihama CCM hawaihami kwa bahati mbaya, bali wameona mtu wao waliyemtarajia ameondoka.

“Ni wengi wanaohamia Chadema, kwa sasa kadi zimetuishia na hiyo ni ishara kuwa CCM inakufa, ripoti za mikoa yote tunazo,” alisema.

Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Owenya alisema wanaoihama CCM kwa sasa wamegundua kuwa chama pekee kinachoweza kutetea wananchi ni Chadema.

“Sisi tunawakaribisha kwa mikono miwili, waje tuchape kazi, ilimradi wanafuata kanuni na taratibu za chama, basi. Wamejionea wenyewe kuwa CCM hakuna chochote,” alisema.

Alisema CCM waliamua kupitisha katiba bila kuwapo kwa Ukawa, lakini sasa wameona kuwa walichokifanya ni makosa na wameanza kurudi Chadema ambako wanaamini kuna demokrasia ya kweli.

Mbunge wa Viti Maalumu, Cecilia Paresso alisema: “Tunamkaribisha kwa mikono miwili. Tumekinyooshea CCM vidole kwa muda mrefu kuwa kuna rushwa na makundi na hilo linajidhihirisha sasa. Lakini wale wote wanaokuja Chadema, tunawakaribisha ili mradi wafuate kanuni na taratibu zetu.”

Paresso alisema hana tathmini ya kina kuhusu wafuasi wa Lowassa wanaoihama CCM, bali wanaokihama chama hicho wameona kina matatizo.

Licha ya kuonyesha kumkaribisha, katika chama hicho, baadhi ya wabunge walimtaka Lowassa afuate kanuni ili awe mwanachama mwenye sifa.

Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde alisema anakaribishwa lakini hana budi kufuata sheria na kanuni za chama... “Anatakiwa afuate taratibu za chama, milango ipo huru, lakini afuate kanuni… asije akafikiri ataleta taratibu zake hapa, sitakubali.”

Silinde alisema wanaohamia Chadema hawajapendezwa na mwenendo mzima wa uteuzi wa mgombea wa urais na hivyo wameifuata demokrasia ya kweli ndani ya chama hicho.

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee hakutaka kuzungumzia kwa undani suala hilo lakini alisema endapo atajiunga, chama hicho kitampokea kulingana na vigezo na taratibu.

“Akihamia Chadema nitatoa maoni yangu lakini ninachoweza kusema ni kuwa kila mtu ana haki ya kwenda chama chochote ili mradi ana tija,” alisema.

Mdee alisema wanaCCM wanaohamia Chadema wamesoma alama za nyakati na kuona kuwa CCM haiendani na ahadi zake.

Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo alisema, Lowassa ni binadamu wa kawaida kwa hiyo kuhamia kwake Chadema si kitu cha ajabu ilimradi afuate kanuni... “Cha muhimu afuate masharti ya chama, kanuni na taratibu, kama watu wanahama vyama vingine yeye ni nani asihame CCM?”

Lyimo alisema wanaCCM wengine wanakaribishwa kujiunga kwa sababu kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu.

Mbunge wa Viti Maalumu, Pauline Gekul, aliwataka wana CCM na Lowasa kuhamia zaidi Chadema ili kuunganisha nguvu na kuichukua nchi.

“Mfikishie salamu Lowassa mwambie karibu kwenye jeshi la ukombozi,” alisema.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Ofisi za CCM Mkoa wa Dodoma, Katibu wa CCM mkoa huo, Albert Mgumba alisema ingawa kuhama chama ni hiari ya mtu, Lowassa hapaswi kuchukua uamuzi wa hasira kiasi hicho badala yake awe mstari wa mbele kuhamasisha umoja ndani ya chama.

Alimtaka kutothubutu kuihama CCM na endapo afanya uamuzi huo atambue kuwa hawezi kukisababishia pengo lolote zaidi ya kujipunguzia hadhi yake ya kisiasa.

“Mgombea tuliyempata sasa ni makini kuliko, anapendwa, utendaji wake unajulikana kila mahali,” alisema Mgumba.

Mgumba alisisitiza kuwa badala ya Lowassa kuwa na mawazo ya kuihama CCM, anapaswa kutuliza fikra na kuonyesha ukomavu wake kisiasa kwa kuwa mstari wa mbele kuwaonya na kuwatuliza wote waliokuwa wakimuunga mkono ili wabaki kwa utulivu ndani ya chama na si vinginevyo.

“CCM siyo Mgumba, ni taasisi iliyosimama. Lowassa anapaswa kutambua hilo, atulie na awe mstari wa kwanza kuwaonya wanachama wachanga kisiasa, wasiokuwa na uzalendo ndani ya chama kwa kumfikiria mtu badala ya chama na masilahi ya Taifa” alisema Mgumba.

Taarifa kuhusu Kongamamo II la Diaspora Tanzania

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Rosemary Jairo akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa Habari juu ya Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (Tanzania Diaspora and SMEs partnership 2015) litakalofanyika kuanzia Tarehe 13 hadi 15 Agosti 2015, kauli mbiu ya Kongamano ni'Creating Linkages between Diaspora and local SMEs in Tanzania' katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. (picha: Reginald Philip)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: [email protected]
Barua pepe: [email protected]
Tovuti : www.foreign.go.tz
Nukushi: 255-22-2116600


20 KIVUKONI FRONT P.O. BOX 9000,
11466 DAR ES SALAAM, Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Uwekezaji cha Kimataifa (International Trade Centre UN-Agency) inafanya Maandalizi ya Kongamano la Diaspora (TanzaniaDiaspora & SMEs Partnership Conference 2015). Kongamano husika litafanyika hapa Dar es Salaam, kuanzia tarehe 13 hadi 15 Agosti 2015 katika Hoteli ya Serena. Kongamano hilo litakuwa la pili kufanyika hapa nchini na litahusisha Diaspora na Wadau wa hapa Tanzania.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Rais na Utawala Bora – Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu ndio Wadau Wakuu katika Maandalizi ya Kongamano hili.
Kongamano la mwaka huu lina Kauli Mbiu, ‘Creating Linkages between Diaspora and Local SMEs in Tanzania’na Dhumuni lake ni kuhamasisha Ushiriki wa Diaspora katika kukuza Biashara Ndogo na za Kati hapa nchini. Kongamano la mwaka huu pia litahusisha Mikoa ya Tanzania ambapo Mikoa itapata fursa ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Mikoani.
Kongamano hilo linatarajiwa kufunguliwa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kufungwa na Mhe. Dr. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Aidha, katika kuhitimisha kilele cha Kongamano hilo, Diaspora wanatarajiwa kufanya ziara Zanzibar tarehe 15 Agosti 2015, ikiwa ni sehemu ya mwaliko maalum kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Pamoja na Shughuli za Ufunguzi na Kilele, Matukio muhimu yatakuwa ni Maonesho ya Kibiashara, Majadiliano ya Mada kuhusu Ushirikishwaji wa Diaspora kwa Maendeleo ya Nchi hususan SMEs, uwekezaji Mikoani n.k.

Kongamano hilo litahudhuriwa na Watanzania Wanaoishi Ughaibuni (Diaspora) na wale waliorejea hapa nchini na Wadau wa Maendeleo kutoka hapa nchini.

Wizara ya Mambo ya Nje Usually integration involves one or more written agreements that describe the areas of cooperation in detail, as well as some coordinating bodies representing the countries involved.inawakaribisha kushiriki nasi katika Kongamano hilo. Tafadhali tembeleeni tovuti ya (www.tzdiaspora.com) kupata taarifa muhimu hususan kuhusu Ada za Ushiriki, fursa za Kufadhili na namna ya kujisajili.

Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
21 Julai, 2015


Arfi aliyehama CHADEMA ajiunga CCM na kuchukua fomu

Said Amour Arfi
Said Amour Arfi

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini, Said Amour Arfi (CHADEMA) amejiunga rasmi na CCM na amekuwa miongoni mwa makada 23 wa chama hicho waliochukua na kurejesha fomu za maombi ya kugombea ubunge mkoani humo kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Mwanasiasa huyo ambae aliwahi kuwa Makamamu Mwenyekiti CHADEMA Taifa alitangaza kujivua uanachama wake CHADEMA wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili mjini Mpanda.

Arfi alikuwa mbunge wa Mpanda Mjini kwa tiketi ya CHADEMA  kwa miongo miwili hadi hivi karibuni alipotangaza kujivua uanachama wa chama hicho na kutogombea katika Jimbo hilo la Mpanda Mjini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Mpanda, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Katavi, Averin Mushi amethibitisha kuwa Arfi alichukua na kurejesha fomu za maombi ya kugombea ubunge katika Jimbo jipya la uchaguzi la Nsimbo wilayani Mlele kwa tiketi ya CCM.

Hivi karibuni, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilitangaza majimbo mapya ya uchaguzi ambapo Jimbo la Katavi limegawanywa na kuanzishwa kwa majimbo mawili ya Uchaguzi ya Nsimbo na Kavuu.

Tanzia! Mbunge - Viti Maalum, CCM

Mariam Mfaki
Mariam Mfaki

Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Viti Maalum mkoani Dodoma, Mariam Mfaki amefariki dunia leo katika hospitali ya mkoa ya Dodoma, alikokuwa amekwenda juzi usiku kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya saratani ya utumbo na mapafu.

Marehemu amekuwa mbunge kwa vipindi vitatu, 2000 - 2005; 2005 - 2010 na 2010 - 2015.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, Mohammed Mfaki, mama yake alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani tangu mwaka 2012 ambamo alipatiwa matibabu nchini India katika hospitali ya Apollo.
“Awali kabla marehemu mama hajawa mbunge alikuwa Katibu tarafa kwa muda wa miaka 20 ambapo alistaafu mwaka 1987 na baadae aliingia kwenye siasa” 


Marehemu Mfaki amekuwa mbunge wa viti maalum kuanzia mwaka 2000 hadi 2015.

Kwa mujibu wa mtoto huyo maziko yatafanyika kesho maeneo ya Miyuji , Dodoma

Mbunge huyo alizaliwa Novemba 26, 1946 na kusoma shule mbalimbali.

Alianza shule ya msingi ya Pahi mwaka 1957 na kumaliza 1960 kabla ya kwenda shule ya kati Singida Girls 1961 na kumaliza 1964 .

Marehemu Mfaki alizaliwa mwaka 1947 na ameacha mume, watoto sita na wajukuu 10.

Mohamed amesema msiba upo nyumbani kwa marehemu Area E karibu na Summit hotel.

[update] Lembeli atangaza kujiunga rasmi CHADEMA

Mheshimiwa James Lembeli akifurahia jambo kwenye mkutano wa CHADEMA, Julai 22, 2015.

Aliyekuwa mbunge wa Kahama mjini James Lembeli, ametangaza rasmi kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na chama cha Demokrasia na maendeleo - CHADEMA.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , Lembeli amesema sababu kubwa zilizomfanya kuhama CCM ni pamoja na kufanyiwa hila na "mizengwe" na CCM wilayani Kahama pamoja na mbinu chafu zilizoambatana na vitendo vya rushwa.

Lembeli alisema amekuwa ndani ya CCM kwa miaka yake yote lakini kutokana na vitendo vinavyofanyika ndani ya chama hicho ameaona akae pembeni. Alisema, ili ufanikiwe CCM kupita michakato yote sahihi ni lazima utoe rushwa au kuiba kura jambo ambalo yeye analipiga vita hivyo kutofautiana na viongozi wa chama ngazi ya Wilaya.

"Ndani ya CCM rushwa imekuwa ibada inasumu kali kuliko ukimwi hivyo nimeshindwa kuvumilia naona Chadema wana viashiria vinavyofanana na mimi ngoja tukafanye kazi," alisema Lembeli.

Alisema katika harakati za kupata wagombea katika jimbo la Kahama kila mwaka ni lazima rushwa itumike lakini chama kimekuwa kimya na kuwabeba wale watoa rushwa.

Mbunge huyo alisema ushahidi wa watu kutoa rushwa hasa katika kipindi hiki umeonekana lakini wahusika wameendelea na hatua zingine bila kukemewa.

"Mimi mwaka 2010 nilikuwa nimekatwa lakini huruma ya Rais Jakaya Kikwete nilirejeshwa sasa nimeona hakuna sababu ya kuendelea kulazimisha kama viongozi hawakutaki," alisema.

Alisema iwapo angechukua fomu CCM mkakati ambao ulikuwepo ni kumkata kwa kile ambacho wanaamini kuwa amekuwa akisimamia misimamo ambayo ina madhara kwa Serikali.

Lembele alisema kutokana na dhana hiyo ni vema aende katika chama ambacho kinaonekana kuwa wabunge wake wanauchungu na nchi yao na sio kubebana kusiko na sababu.

"Kufanya kosa sio kosa lakini kurudia kosa ni kosa kubwa sana hivyo siwezi kurudia kosa la 2010 hivyo huku Chadema ndiko sahihi," alisema.

Alisema ukiona mwenzako ananyolewa ni vema kujiandaa kwa kutia maji nywele jambo ambalo ameliona na ameamua kufanya hivyo.

"Siwezi kutoa rushwa kwa sababu sijafunzwa hivyo na hata wananchi wa Kahama wanajua kuwa mimi sio mtoa rushwa hivyo ukiwa hutoi rushwa CCM ni ngumu kukubalika jambo ambalo linafanya kuwa rushwa iwe mbaya kuliko ukimwi," aliongezea.


Akizungumzia kugombea ubunge kupitia Chadema, alisema atafanya hivyo kwani ukweli ni kuwa anakubalika kwa wananchi wote kutokana na misingi yake ya utumishi.

Alisema mpaka anafanya uamuzi huo ameshafanya utafiti ambapo anaamini kuwa atashinda tena kwa kishindo kwani wananchi wa jimbo hilo wanamkubali.

Lembeli alisema kimsingi jimbo la Kahama wapinzani wapo tangu yeye akiwa Mbunge, hivyo anaamini kuwa iwapo atafanikiwa kushinda hatapata wakati mgumu kufanya kazi.

"CCM imefanya mambo mengi ambayo kimsingi hayana afya ndani ya chama ukiwa wa kwanza kwa kura ndani ya CCM unakuwa wa mwisho hali ambayo inakatisha tamaa na hilo lilitokea 2010 na Chadema wakapata ushindi," alisema

Pia alisema amepokea simu na meseji nyingi ambazo kutoka kwa wananchi zinamtaka agombee kupitia chama Chadema hivyo pamoja na ukweli kuwa ni uamuzi mgumu ila hawezi kula matapishi.

Alisema ilimchukua masaa 10 kumuelezea mama yake juu ya uamuzi huo lakini baadae alielewa hivyo kwa sasa ana baraka zote za mama na familia kwa ujumla.

Kuhusu uhusiano na 4U Movement

Akizungumzia kuhusu uamuzi huo kuhusishwa na kundi la 4u Movement, alisema kimsingi kundi hilo analiona kupitia mitandoa ya kijamii ila hana uhusiano nalo na hahitaji kuwa katika hao.

Lembeli alisema wananchi wa Kahama ni watu makini wanajua nini cha kufanya hivyo uamuzi ambao watafanya utakuwa ni kwa uelewa wao na sio kwa msukumo wa kundi hilo linalotajwa kuwa ni wafuasi wa Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa.

Kuhusu Katiba iliyopendekezwa Lembeli alisema yeye ni muumini wa Serikali tatu na alionesha hilo katika vikoa vyote vya bunge lile ambapo alikuwa katika kamati namba moja.

Alisema kutokana na ukweli huo ni dhahiri kuwa ameenda chama ambacho wanafanana kifra kwani bila Serikali tatu hatma ya Tanzania itakuwa mashakani.

"Kwa hili siwezi kubadilika mimi msimamo wangu hadi leo ni Serikali tatu ambapo pia ni msimamo wa Chadema hivyo wengi ndio walishinda lakini mimi sio mmojawapo," alisema.

Aidha Lembeli alitumia muda huo kufafanua ni kwanini alitoa hoja ya kutaka Lowassa na wengine ambao wamekutana na majanga ndani ya bunge wasafishwe ambapo alisema haki haikutendeka kusafisha watu baadhi na wengine kuachwa.

Lembeli alisema katika taarifa ya Operasheni Tokomeza haikusema mawaziri fulani wanamakosa ila iliweka bayana kuwa kulinga na nafasi zao wanapaswa kuwajibika kisiasa.

Alisema mfumo wa kusafisha watu fulani na wengine kuwaacha sio mzuri kwani hauendani na misingi ya haki za binadamu ni ubaguzi.

Kwa upande wa mtoto wake wa pili Wizilya James Lembeli alisema wanamuunga mkono baba yao kwa uamuzi huo na kuwa wako nyuma yake.

Alisema uamuzi ambao amechukua baba yake ni mgumu hasa ukilinganisha na kipindi husika lakini hakuwa na njia nyingine kwani ni mtu wa siasa.

Akizungumzia ujio huo Ofisa Habari wa Chadema ambaye ndiye alimpokea Lembeli alisema kimsingi mwanachama huyo mpya alikiwa ni mpinzani kiroho hivyo hawana shaka naye.

Makene alisema wanaamini kuwa wamepata mtu ambaye anapenda mabadiliko kwani alionekana ndani ya bunge na nje kwa kusimamia rasilimali za nchi bila uoga.

Alisema Chadema itaendelea kupokea wanachama wapya kutoa CCM na vyama vingine hadi Julai 25 kwani lengo lao ni kuhakikisha kuwa nchi inafikia kwenye mabadiliko chanya.

Lembeli amekuwa Mbunge wa jimbo la Kahama, tangu mwaka 2005 hadi 2015 ambapo awali alikuwa mwandishi na mtumishi katika shirika la Hifashi ya Taifa (Tanapa).
  • Imenukuliwa kutoka ChannelTEN na mtandao wa HabariZaJamii.com