Prof. Mbele akumbuka kitabu cha dada'ke Obama, Auma

Nilivyomwona dada huyu, nilikumbuka kuwa niliwahi kumtaja katika blogu hii baada ya kununua kitabu chake, And Then Life Happens: A Memoir. Niliingia mtandaoni nikaona mahojiano aliyofanyiwa na mtangazaji wa CNN. Halafu nilikitafuta kitabu chake katika maktaba yangu nikakipitia, kwa kuwa nilikuwa sijakisoma, bali nilikuwa nimekipitia juu juu tu.

Hakuna ubishi kwamba Auma Obama ni mama mwenye fikra za kusisimua na uwezo mkubwa wa kujieleza. Hilo linajitokeza wazi katika mahojiano yake. Masimulizi ya maisha yake, yaliyomo katika kitabu chake, yana mambo yanayoweza kuwahamasisha watoto wetu, hasa wasichana, wawe wanajiamini na kuwa watafuta elimu na maendeleo, wakijua kuwa wao wana uwezo sawa na mtu mwingine yeyote.

Kitu kingine kilichonivutia juu ya Auma Obama ni kwamba anakimudu sana ki-Jerumani, lugha ambayo alianza kujifunza alipokuwa Kenya na baadaye alipokuwa masomoni Ujerumani, ambako aliishi na kufanya kazi kwa miaka mingi. Kitabu chake alikiandika kwa lugha hiyo.
Soma zaidi na tizama picha nyingine katika blogu ya Pro. Mbele - Hapa Kwetu

Mwanamuziki 'Bongo Fleva' Khadija Shabani 'Keisha' ashinda CCM

MSANII wa Bongo Fleva, Khadija Shabani Taya 'Keisha' ameibuka mshindi kwenye kura za maoni za Ubunge wa viti maalum kundi la Walemavu MKoa wa Dodoma na kuwa mshindi wa kwanza.
Keisha amepata kura 340 huku Stella Fueda akiibuka na kura 112, Anna Fungo kura 100 na Graceana Kavishe kura 54.
Jumla ya kura 721 zilipigwa ambapo kura 75 ziliharibika na kura za halali zilikuwa 646.

Msanii huyo aliwahi kuhojiwa na vyombo vya habari na kubainisha kuwa japo ni mlemavu wa ngozi lakini anajikubali anajipenda kujiamini na amekuwa akipigania amani ambayo wanastahili kuipata kutoka nchini.

Alisema alipoanza kuweka picha zake za siasa kwenye mtandao kuna baadhi ya watu walimpongeza na wapo waliosema kuwa hana uchungu na wenzake kwani waliamini anaingia kwenye siasa kwa nia ya kujinufaisha “Wapo wanaohisi nimeingia huku kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe mimi
ni mpiganaji na ndomana siku zote nimekuwa nikiwaza kuhusu amani yetu” alisema.

Alisema fimbo ya mbali haiui nyoka na kidole kimoja hakivunji chawa akimaanisha kuwa lazuima kusimamia sheria ambazo zitatusaidia kuendeleza amani hivyo basi lazima kuwe na wawakilishi wa kutosha ndani ya bunge ili sauti zisikike ili sheria kutungwa na kutekelezwa pia.
  • Taarifa ya Sifa Lubasi, Dodoma
Habari za asubuhi ndugu zangu rafiki zangu mashabiki zangu na media zote nchini.najua wengi mnajiuliza maswali mengi sana juu yangu kwanini nimeamua kuingia kwenye siasa lakini leo naomba nifunguke na kuwaambia kitu.

Mimi kama mlemavu wa ngozi najikubali najipenda na ninajiamini lakini yote tisa napigana kwa uhuru na amani ambayo tunastahili kuipata kutoka nchini kwetu.

Nilipoanza kupost picha zangu za siasa kuna ambao walinipongeza na kuna ambao walinisema kwamba sina uchungu na wenzangu kwakuwa wanahisi nimeingia huku kwa ajili ya kujinufaisha mwenyewe mimi ni mpiganaji na ndomana siku zote nimekuwa nikiwaza kuhusu amani yetu.fimbo ya mbali haiui nyoka na kidole kimoja hakivunji chawa nikimaanisha kwamba lazima tusimamie sheria ambazo zitatusaidia kuendeleza amani hivyo basi lazima tuwe na wawakilishi wa kutosha ndani ya bunge ili sauti zetu zisikike ili sheria kutungwa na kutekelezwa pia.hivyo mimi kama mtanzania mwenzenu nahitaji support yenu ili niweze kufikia malengo yetu kwa yeyote ambaye anaupendo nasi na mimi na harakati zangu anisaidie kwa chochote ambacho kitanifikisha nnapoataka.

this is my tigo no 0718785045 na hii ni account number yangu ya crdb 011 2022295800 jina ni hadija shabani Taya unaweza kuchangia humo na kwa upendo kabisa naomba u repost hii post kadri muwezavyo ahsanteni shukrani.

Picha za kuapishwa kwa Mkurugenzi Mpya wa Uchaguzi


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ikulu jijini Dar es Salaam jioni ya Julai 25, 2015.


Ndugu Kombwey akiweka sahihi kwenye hati baada ya kuapishwa.


Rais Kikwete akiweka sahihi baada ya kumwapisha Ndugu Kombwey.


Rais Kikwete akikabidhi vitendea kazi.


Rais Kikwete akipeana mikono na Ndugu Kombwey.


Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Ndugu Kombwey. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Florens Turuka, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Hamid Mohamoud Hamid, Rais Kikwete, Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi.


Rais Kikwete akipeana mkono na Mkurugenzi wa Uchaguzi mpya Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey.


Rais Kikwete akisalimiana na mtoto wa Ndugu Kombwey, Msemakweli (2)w akati wa hafla hiyo fupi. 
  • Picha: Ikula

Taarifa: Rais Kikwete afanyia mabadiliko Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Mkurugenzi wa Uchaguzi mpya Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey.
Mkurugenzi wa Uchaguzi mpya Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mabadiliko ya Utendaji katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kumteua Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi.

Aidha, Rais Kikwete amemteua Jaji Richard Mziray kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Vile vile, Rais Kikwete amewateua majaji wapya 13 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumamosi, Julai 25, 2015 na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa teuzi hizo zote zimeanza leo hii.

Kwa mujibu wa taarifa ya Balozi Sefue, Ndugu Kombwey ambaye anaapishwa baadaye leo jioni, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndugu Julius Benedicto Mallaba.

Badala yake, Rais Kikwete amemteua Bwana Mallaba kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kombwey alikuwa Mkurugenzi wa Utawala, Tume ya Uchaguzi.

Taarifa hiyo pia imesema kuwa Jaji Mziray ambaye anateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam.

Majaji wa Mahakama Kuu ambao wameteuliwa na Rais Kikwete, kwa mujibu wa taarifa hiyo, Ndugu Ignas Pius Kitusi ambaye ni Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Ndugu Wilfred Peter Dyansobera ambaye ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu; Ndugu Lameck Michael Mlacha ambaye ni Naibu Msajili na Mwenyekiti wa Baraza la Rufani la Kodi; Ndugu Salima Mussa Chikoyo ambaye ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi; Ndugu Isaya Arufani ambaye ni Naibu Msajili na Katibu wa Jaji Mkuu wa Tanzania na Ndugu  Julius Benedicto Mallaba.

Wengine ni Ndugu Adam Juma Mambi ambaye ni Katibu Msaidizi, Tume ya Kurekebisha Sheria; Ndugu Sirilius Betran Matupa ambaye kwa sasa ni Msaidizi wa Rais, Sheria, Ofisi ya Rais, Ikulu; Ndugu Issa Maige ambaye ni wakili wa kujitegemea, Ndugu Licia Gamunya Kairo ambaye ni wakili wa kujitegemea; Dkt. Masoud Shaaban Benhaji wakili wa kujitegemea na Mhadhiri Mwadamizi, Chuo Kikuu Huria, Dar es Salaam, Ndugu Victoria Makani ambaye ni wakili wa kujitegemea na Ndugu Rehema Joseph Kerefu ambaye ni mwanasheria wa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Taarifa hiyo imesema kuwa wakati Ndugu Kombwey anaapishwa leo, majaji wataapishwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

25 Julai, 2015


10 Pasta cooking tips

10. FOR EACH POUND OF PASTA, USE 6 QUARTS WATER AND 3 TABLESPOONS KOSHER SALT. DON’T SALT THE WATER BEFORE IT HAS COME TO A BOIL, OR IT WILL TAKE LONGER TO BOIL.


CLICK THE IMAGE TO MAKE HOMEMADE MEZZALUNE!

9. USE WELL-CRAFTED EXTRA VIRGIN OLIVE OIL. CONSIDER THE REGION, NUANCE, CLARITY AND WEIGHT OF THE OIL WHEN CHOOSING ONE FOR A PASTA DISH.


oliveOil
CLICK THE IMAGE TO LEARN!

8. NEVER ALLOW THE OIL TO SMOKE. IF NECESSARY, REMOVE THE PAN FROM THE HEAT BRIEFLY.


ahiPbISD7bGaBUI4csnMkIl1TtcdS8jzfXT9YkLMI2oFmNVaDLrEgq4HSrb5fxOeGo-oIsEQ6inFktKxQRaxiU
FRESH TAGLIATELLE WITH GARLIC, RUCOLA & SUNDRIED TOMATOES

7. NEVER BOIL A SAUCE UNTIL YOU’VE ADDED THE PASTA.


Postimage_Bucatini-with-Crayfish
BUCATINI WITH CRAYFISH, JALAPEƑOS AND BASIL

6. THE SAUCE SHOULD ALWAYS BE WELL INTEGRATED WITH THE PASTA, UNCTUOUS, AS SUPPLE AS SILK AND HOMOGENOUS.


promo209772397
CLICK FOR MARIO’S BASIC TOMATO SAUCE RECIPE

5. WHEN FINISHING A PASTA WITH A BUTTER SAUCE, USE COLD BUTTER FOR A BETTER EMULSION.


RAMP SPAGHETTI
SPAGHETTI WITH RAMPS

4. FOR DEPTH, FRESHNESS AND CONTRAST, ADD FRESH HERBS OR RAW TOMATOES AFTER TOSSING THE PASTA WITH THE SAUCE, THEN FINISH WITH OLIVE OIL.


IMG_1094_amatriciana1-610x408
BUCATINI ALL’ AMATRICIANA

3. REMOVE THE PAN OF PASTA AND SAUCE FROM THE HEAT BEFORE ADDING THE CHEESE.


pennette_post image
PENNETTE WITH CAULIFLOWER RAGU

2. LESS IS ALWAYS MORE. IT’S MORE IMPORTANT FOR THE SAUCE AND PASTA TO BE ONE, A SUM GREATER THAN ITS PARTS. FAT AND CHEESE ARE NOT AS IMPORTANT AS WATER AND BALANCE.


post_linguine with lemon
LINGUINE WITH LEMON

1. ALWAYS PLATE PASTA WITH THE THOUGHT OF ITS PERFORMANCE ON THE TABLE IN A FEW MINUTES.

IMG_11432-700x440

SPAGHETTI ALLA CARBONARA

[full video] Pres. Obama & Kenyatta address in Nairobi, Kenya


[video] Rais Obama asalimia Wakenya, "Ni aje Wasee"


Mwaka huu wananchi watapigiwa magoti sana!

Iliripotiwa Mbeya siku chache zilizopita... safari hii ni kutoka huko kusini.

Mwandishi wa habari wa kituo cha Clouds Tv, Kijakazi Yunusu akipiga magoti kuomba kura kutoka kwa wajumbe ubunge viti maalumu, kupitia jumuiya ya wananwake CCM, katika ukumbi wa Kaagwa.

Jumuiya ya Wanawake wa CCM mkoani Lindi imefanya uchaguzi wake na kuchagua wabunge wa viti maalumu, wawili kati ya wagombea 13, waliomba nafasi hiyo.

Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Lindi Mantumu Mahiza alitangaza walioshinda nafasi, Hamida Abdallah, aliyepata kura 281 na Tekla Uongere aliyejipatia kura 231, katika ukumbi wa Kaagwa mjini hapa.

Alisema kuwa wajumbe waliopiga kura 541 kati ya hizo 18 ziliharibika kura za halali 523.

Mahiza alisema washindi hao wawili majina yao yatapelekwa umoja wa wanawake CCM, makao makuu na hatimaye kuwasilishwa katika ofisi ya tume ya uchaguzi, mwaka huu.

Winners of first-ever Nelson Rolihlahla Mandela Prize

Laureates of the 2015 UN Nelson Rolihlahla Mandela Prize Helena Ndume (left) and Jorge Fernando Branco Sampaio. UN Photo/Rick Bajornas

Helena Ndume of Namibia and Jorge Sampaio of Portugal received the first-ever Nelson Rolihlahla Mandela Prize at the UN Headquarters in New York on Friday.

The prize was established in June 2014 by the UN General Assembly (UNGA) to recognize the achievements of those who dedicate their lives to the service of humanity by promoting the UN purposes and principles.

Ndume, a female ophthalmologist, has been treating blindness and eye-related illnesses in Namibia and throughout the developing world. Sampaio, the former president of Portugal from 1996 to 2006 and also the former mayor of Lisbon from 1989 to 1995, has been awarded for his contribution to his country.

Tamko la Mahakama kuhusu habari iliyochapishwa kwenye Mwananchi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAHAKAMA

TAARIFA KWA UMMA

MAKALA YA GAZETI LA MWANANCHI YA TAREHE 21-07-2015 YENYE KICHWA CHA HABARI “MTANDAO WA RUSHWA MAHAKAMANI HUU HAPA”

1.0      UTANGULIZI
1.1        NAFASI YA VYOMBO VYA HABARI MAKALA MAALUM YA GAZETI LA MWANANCHI LA TAREHE 21/07/2015  UK. 25 - 26
Mahakama ya Tanzania inatambua nafasi ya vyombo vya habari katika kuwafikishia wananchi habari na kuwaelimisha. Vile vile tunatambua nafasi ya kipekee ya vyombo vya habari katika kukosoa utendaji wa taasisi za umma na binafsi. Kwa kutambua hilo Mahakama imeunda jukwaa la mahakama na vyombo vya habari (Judiciary- Media forum)
1.2        USHIRIKIANO WA MAHAKAMA NA VYOMBO VYA HABARI
Katika kudhihirisha dhamira yake ya kushirikiana na vyombo vya habari ili kuboresha huduma na utoaji habari, tarehe 3/12/2014 Mahakama iliandaa kongamano la kujadili changamoto zinazoikabili pamoja na nafasi ya vyombo vya habari. Kongamano hili lilihusisha wahariri wa vyombo vyote vya habari. Katika kongamano hilo, pamoja na mambo mengine, tulikubaliana yafuatayo:-
·        Kuimarisha ushirikiano kwa kupeana taarifa muhimu
·        Mahakama kutoa ufafanuzi wa masuala yasiyoeleweka kwa waandishi wa habari ili kuepusha upotoshaji

·        Kushirikiana katika kujengeana uwezo wa kuandika habari za mahakama.

1.3        UTEKELEZAJI WA MAKUBALIANO
Mahakama inatekeleza makubaliano haya kwa kutoa taarifa na maelezo ya kina kuhusu masuala mbalimbali hasa ya kesi zinazoendelea mahakamani. Mahakama inafanya hivyo kwa ufanisi zaidi pale ambapo mtaka taarifa anataja namba ya kesi na mahakama ilipo kesi au mtumishi anayelalamikiwa. Bila kutolewa kwa taarifa hizi ni vigumu kwa mahakama kuchukua hatua.
2.0        UMUHIMU WA TAARIFA HII
Katika gazeti la Mwanachi la tarehe 21/07/2015 ukurasa wa 25 na 26 kulikuwa na habari yenye maneno “Mtandao wa rushwa Mahakamani huu hapa.” Katika habari hiyo Mwandishi ametoa tuhuma kwamba kuna rushwa Mahakamani kwa kutolea mifano kama ifuatavyo:-
2.1   Bw. Muhidini Ngulumwa, anashitakiwa kwa jinai  
     Katika Mahakama ya Mwanzo Magomeni lakini 
     mlalamiko hafiki Mahakamani kwa miaka mitatu sasa   
     ambapo pia  aliombwa rushwa ya shilingi laki tano.

2.2.      Bi. Kuruthum Majjid, alitoa rushwa ya laki moja ili Polisi wamkamate mtuhumiwa. Mtuhumiwa alifikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Mogomeni ambapo amepewa dhamana lakini haudhurii Mahakamani kwa muda wa miezi kumi na tatu sasa.

2.3.      Bw.Abdallaha Majata, kesi yake inazungushwa mahakama ya Mwanzo Mbagala kwa madai kuwa uchunguzi haujakamalika na kwamba kuna mshauri wa Mahakama anamwomba wamalize kesi nje ya Mahakama.

2.4.      Bi. Halima Abdan, ametoa fedha polisi na Mahakamani kuwezesha ndugu yake apewe dhamana bila mafanikio. Mwandishi hakutaja Mahakama ilipo kesi husika.

2.5.      Bw. Claudiana Mbazigwa, amepoteza milioni moja na laki nne katika jitihada ya kumdhamini ndugu yake katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo bila mafanikio.

2.6.      Bw. Abdallh Mpondela amepoteza laki tano akijaribu kumdhamini ndugu yake bila mafanikio Mwandishi hajataja Mahakama ilipo kesi husika.

2.7.      Bw. Laizer Kaanan ametoa shilingi laki sita katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo ili kumdhamini ndugu yake bila mafanikio.

3.0. UFUATILIAJI WA TUHUMA
Mahakama imeguswa na kusikitishwa na tuhuma hizi. Kwa vile kesi katika Mahakama husajiliwa kwa nambari za usajili kwa ajili ya utambulisho, na kwa vile katika Makala Mwandishi hataji namba za kesi na kwa kuzingatia uzito wa habari yenyewe, Mahakama imeanza uchunguzi juu ya tuhuma hizi kwa  hatua zichukuliwe na Idara ya Ukaguzi wa Huduma za Mahakama na Maadili kwenda ofisi za gazeti la Mwananchi (tarehe 22/7/2015) kupata taarifa zitakazowezesha kuchukuliwa hatua. Hadidu za rejea zifuatazo zilitumika:-
3.1.      Kufahamu iwapo mwandishi wa makala anafahamu anuani au namba za simu za walalamikaji ili wasaidie kutoa taarifa zaidi ikiwa ni pamoja na nambari za kesi kwa ajili ya uchunguzi na hatua zifaazo.

3.2.      Kufahamu iwapo mwandishi wa makala anafahamu nambari za kesi za matukio aliyoandika.

3.3.      Kufahamu iwapo mwandishi anawafahamu au ana anuani au namba za simu za wazee wa baraza aliohojiana nao.

3.4.      Kufahamu iwapo mwandishi alipata namba za simu ya askari aliyezungumza na Halima Abdan baada ya kuunganishwa na mzee wa baraza.

3.5.    Kupata maelezo ya aina ya uchunguzi aliofanya mwandishi ili kujiridhisha na ukweli wa habari.

4.0. MATOKEO YA UCHUNGUZI
Katika ofisi za gazeti la Mwananchi Ofisa wa ngazi za juu wa Mahakama alikutana na Bw. Joster Mwangulumbi ambaye ni Mhariri wa Habari za uchunguzi. Bw. Joster alimfahamisha Mkurungenzi Msaidizi mambo yafuatayo:-
4.1.      Mwandishi wa makala hayo (Bi. Kalunde Jamal ) yuko safarini na asingepatikana kwa mahojiano lakini alimpigia simu wakaongea kuthibitisha masuala kadhaa.

4.2.      Mwandishi wa makala ni mwandishi wa habari za Mahakama na katika kufanya kazi zake alipata malalamiko aliyoyatolea taarifa ofisini akatakiwa kufanya uchunguzi na matokeo ya uchunguzi ndiyo yaliyochapishwa.

4.3.      Katika ufuatiliaji Mahakimu Wafawidhi wa Mahakama za Mwanzo na Wilaya hawakuwa tayari kuzungumzia na kufafanua malalamiko hayo.

4.4.      Ofisi za gazeti na Mwananchi na mwandishi wa makala hawafahamu nambari za kesi zinazolalamikiwa, anuani na hata namba za simu za walalamikaji waliotajwa. Pia hawana namba za simu za wazee wa baraza au askari polisi aliyewasiliana na Halima Abdan na kwamba hawawezi kupata anuani au namba za simu hizo.

Mapungufu haya yanaleta mashaka juu usahihi wa taarifa zilizoandikwa katika makala hayo. Licha ya upungufu wa dhahiri ambao hauiwezeshi Mahakama kuchukua hatua zozote, katika toleo la tarehe 22/07/2015 gazeti hili lilitoa tahariri yenye kusisitiza yaliyomo katika makala yenye utata ila yenye kuvutia.
5.0HARAKATI ZA MAHAKAMA KUBORESHA
5.1.    HATUA ZA KUBORESHA HUDUMA
Mahakama inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha huduma zake. Mahakama pia kama Taasisi ya Umma iko tayari na imekwisha toa fursa kwa wadau kutoa maoni yao kuhusu namna ya kuboresha huduma zake kupitia matangazo kwenye magazeti Mwananchi la tarehe 29/5/2015 na Mtanzania la tarehe 03/6/2015 ambapo maoni yanaendelea kupokelewa. Mahakama pia iko tayari kukosolewa kwa njia zote halali kwa lengo la kuboresha huduma, ili mradi taarifa hizo ziweze kusaidia kuchukua hatua kwa sasa na kuwa kama chachu ya mabadiliko/mageuzi yanayoendelea ndani ya Taasisi hii muhimu ya uendeshaji wa Nchi yetu.
5.2.   WITO KWA WANANCHI NA WADAU
Ili kuondoa kero zilizobainishwa na gazeti la Mwananchi, Mahakama inatoa rai kwa gazeti la Mwananchi au mtu yeyote mwenye taarifa sahihi kuipatia ushirikiano ili kupata nambari za kesi zilizolalamikiwa na mahakama zilikofunguliwa. Kwa lengo hilo la ushirikiano Mahakama inaomba wale wote waliotajwa katika makala iliyochapishwa tarehe 21/07/2015 kuhusu mtandao wa rushwa Mahakamani (Kama wapo) ambao ni Muhidini Ngulumwa, Kuruthum Majjid, Abdallah Majata, Halima Abdan, Claudiana Mbazigwa, Abdallah Mpondela na Laizer Kaanan wafike Makao Makuu ya Mahakama, Mahakama ya Rufani ya Tanzania, No 11409 Kivukoni Front, waonane na Mkurungenzi Msaidizi wa Malalamiko katika Idara ya Ukaguzi wa Huduma za Mahakama na Maadili ili  watatuliwe kero zao. Inasisitiza tena ili kuondoa rushwa, maadili yasiyofaa huduma suala la uwazi wa utoaji huduma na kuboresha mawasiliano ni muhimu kuanzia tarehe 6 Desemba, 2014. Mahakama imeweka namba ya simu Na. 0752- 500 400 ambayo inapokea malalamiko, maoni na mapendekezo ya wananchi na wadau mbalimbali kwa njia ujumbe mfupi na mitandao ya kijamii (WhatsApp, na barua pepe [email protected]judiciary.go.tz)
Matokeo ya utaratibu huu ni mafanikio makubwa ambayo Gazeti la Mwananchi ingeyatumia pia kwa manufaa ya Wananchi, kwa kutoa ushahidi na taarifa kamilifu.
PAMOJA TUNABORESHA HUDUMA”


IMETOLEWA NA:

MTENDAJI MKUU
MAHAKAMA YA TANZANIA

---------
PS: Makala inayozungumziwa unaweza kuirejea kwa kubofya hapa.

For easy clean up: Use tin foil to cover your cooker top


The photo above from davidlebovitz.com showing a technique of covering the surrounding surfaces with foil to protect your surfaces from splattered oil, soups and other cooking food particles.

Magazetini Jumamosi, Julai 25


Asubuhi Njema ya ChannelTEN Julai 25


Taarifa ya habari ya kutwa nzima ChannelTEN Julai 24
TBC1 video: Nyumbani na Diaspora w/ David Kyungu

David Kyungu ni mwana sanaa ya uchoraji
  • Amechora vikaragosi vya Karikenye
  • Alishiriki kuanzisha gazeti la SANI akishirikiana na Bawji
  • Alikuwa mmoja wa watu wa mwanzo kuchora stempu za Tanzania
  • Akiwa kwenye mahojiano studioni ameeleza kinachowawezesha kumchora mtu maarufu, ndipo Mjengwa alipompa kalamu na karatasi na kuomba amchore Magufuli papo hapo