Taarifa ya Ikulu kuhusu habari iliyochapishwa Mwananchi 27.7.2015

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: [email protected]
Website : www.ikulu.go.tz   
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Gazeti la Mwananchi la leo, Jumatatu, Julai 27, 2015, kwenye ukurasa wake wa 26 limechapisha habari yenye kichwa cha habari, “Marais watano wanaotajwa kuongoza kwa mishahara minono barani Afrika ni hawa hapa”.

Katika habari hiyo ambayo gazeti hilo linadai chanzo chake ni “uchambuzi wa mtandao wa African Review” inadaiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, anashilikia nafasi ya tano miongoni mwa viongozi 38 wa nchi za Afrika wanaolipwa mshahara mnono zaidi.

Gazeti hilo linadai kuwa Rais Kikwete analipwa Dola za Marekani 192,000 kwa mwaka, ikiwa ni malipo ya Dola za Marekani 16,000 kwa mwezi.

Habari hizi siyo za kweli. Ni uongo na uzandiki. Ni uzushi mtupu na ni uzushi wa hatari.

Mshahara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwezi ama kwa mwaka haufikii na hata wala kukaribia kabisa kiwango kinachotajwa na Gazeti la Mwananchi.

Tangu Uhuru, mwaka 1961, Rais wa Tanganyika na baadaye tangu mwaka 1964 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa miongoni mwa viongozi wanaolipwa mishahara ya chini kabisa duniani.

Mshahara wa Rais wa Tanzania kwa mwezi ni wa chini kiasi cha kwamba mshahara wake unazidiwa, tena kwa mbali, na mishahara wanayolipwa baadhi ya watendaji wakuu wa baadhi ya taasisi za umma nchini.

Aidha, ni jambo la kushangaza kwamba Gazeti la Mwananchi, linalochapishwa hapa nchini, linaweza kupata kiasi cha uongo anacholipwa Rais wa Tanzania katika mitandao ya nje badala ya kuuliza rasmi na kupewa majibu sahihi.

Kwa kujiingiza katika uzushi wa kupindua kiasi hiki, Gazeti la Mwananchi haliwezi kuwa na nia nyingine yoyote isipokuwa nia ya kuwachochea wananchi na kuwajengea chuki dhidi ya Serikali yao na Kiongozi wao Mkuu.

Ni matarajio yetu, kuwa Gazeti la Mwananchi litafanya jitihada za makusudi, kama taaluma ya uandishi wa habari inavyoelekeza, kutafuta usahihi wa jambo hili na kuwaambia Watanzania ukweli.

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
27 Julai, 2015

Vyama 21 vyasaini Maadili ya Uchaguzi Mkuu 2015 Tanzania

Vyama vya Siasa 21 vinavyotarajiwa kushiriki katika uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani baadaye mwaka huu vimesaini "Maadili ya Uchaguzi" yatakayotumika wakati wa kampeni, kupiga kura na wakati wa kutangaza matokeo.

Maadili hayo yanayohusisha Serikali, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Vyama vya Siasa yalisainiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dk. Florence Turuka, Mwenyekiti wa NEC Jaji Damian Lubuva na Wawakilishi wa vyama vya Siasa 21 nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume hiyo amesema Chama cha Wananchi (CUF) hakikusaini Maadili hayo kutokana na kuwa na kazi nyingine lakini akasisitiza kuwa chama hicho kitasaini Maadili hayo wakati wowote.

Akifafanua kuhusu Maadili hayo, Jaji Lubuva alisema Maadili yanapaswa kuanza kutumika rasmi Agosti 22 mwaka huu wakati kampeni za uchaguzi zitakapoanza, katika kipindi cha kupiga kura na wakati wa kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo. 

Lubuva alisema Maadili hayo pia yatahusu wajibu wa vyama vya siasa na wagombea na mambo yasiyotakiwa kufanywa na vyama vya siasa na wagombea. 

Maadili pia yatahusu masuala yanayotakiwa kufanywa na yasiyotakiwa kufanywa wakati wa kupiga kura.

Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa maadili yaliyosainiwa pia yatahusu maadili kwa Tume ya Uchaguzi yaani mambo yanayotakiwa na yasiyotakiwa kufanywa na Tume hiyo. 

Aidha, maadili hayo yatahusu mambo yanayotakiwa na yasiyotakiwa kufanywa na watendaji wa serikali katika kipindi chote cha uchaguzi.

Major flaw in Android: Hackers use text to take control of your phone


And, according to mobile security experts at the firm Zimperium, there's a gaping hole in the [Android] software — one that would let hackers break into someone's phone and take over, just by knowing the phone's number.

In this attack, the malicious code would take over instantly, the moment you receive a text message (the target would not need to goof up — open an attachment or download a file that's corrupt).

Joshua Drake, security researcher with Zimperium and co-author of Android Hacker's Handbook tells the NPR that:
"This happens even before the sound that you've received a message has even occurred," "That's what makes it so dangerous. [It] could be absolutely silent. You may not even see anything."
There is an audio below with details...

Dada mchuuza dagaa ashinda uchaguzi CCM


Mchuuzi wa dagaa kwenye mwalo wa Mwigobero uliopo Manispaa ya Musoma, Agnes Methew, ameibuka mshindi wa kwanza kwenye kura za maoni za kutafuta Mbunge wa viti maalumu (CCM) mkoa wa Mara.

Akitoa shukrani kwa wajumbe wa mkutano wa uchaguzi mara baada ya kutangazwa mshindi na msimamizi wa uchaguzi huo,Samwer Kiboye ambaye ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Rorya,alisema wajumbe wameonyesha namna ambavyo hata mtu wa chini anaweza kushinda tofauti na inavyozungumzwa.

Alisema wao watu ambao wamekuwa wakizungumza pembeni ukiwa Chama cha Mapinduzi huwezi kupata nafasi ya uongozi kama hauna fedha jambo ambalo sio kweli kwa kuwa yeye amechaguliwa bila kujali kipato chake na kuwashinda walioonekana na kipato cha juu na majina makubwa.
“Niwashukuru sana wajumbe kwa kunipigia kura za kishindo na kunifanya niibuke mshindi kati ya wagombea wengine 9 wanachma wenzangu ambao nilikuwa nikishindana nao ndani ya uchaguzi huu.
“2010 nilikuja kwa mara ya kwanza kuwaomba nafasi hii lakini kura hazikutosha lakini safari hii mmeamua kunichagua mimi muuza dagaa na kuudhilihisha umma ndani ya CCM hata mtu wa hali ya chini anaweza kupewa uongozi. Kwa jinsi mlivyoniamini naomba niwahakikishie sitawaangusha na kikubwa naomba tupeane ushirikiano na pale nitakapofanikiwa kuingia bungeni nitakuwa mstari wa mbele kuzungumzia masula yanayowahusu wanawake katika kufanikisha chachu ya maendeleo,”alisema Agnes.
Wakati akiomba kura kabla ya kuchaguliwa, mgombea huyo aliwatoa chozi wajumbe baada ya kuomba kura huku akilia akiomba kuchaguliwa muuza dagaa kwa kuwa kwa kipindi chote amekuwa yupo na wajumbe katika kiangazi na mvua.

Katika uchaguzi huo, Agnes Methew alichaguliwa kwa kupata kura 418 kati ya kura 641 zilizopigwa na kufuatiwa na Chrstina Samo aliyepata kura 226 huku Mwenyekiti wa (UWT) mkoa wa Mara, Nancy Msafiri akipata kura 208 na kushika nafasi ya tatu.

Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano huo,msimamizi wa uchaguzi,Samwer Kiboye, aliwahasa wagombea wote kukubalina na matokeo kwa kuwa uchaguzi ni wa haki ili kuweza kushirikiana kwa pamoja kutafuta kura za CCM katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.  • via Shommi Binda, blog

Jukwaa Langu: Sikiliza kila Jumatatu kuhusu Uchaguzi Mkuu 2015JUKWAA LANGU ni kipindi ambacho kitakuwa kikikujia kila Jumatatu, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka huu.

Rais Kikwete ziarani nchini AustraliaTHE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: [email protected]
Website : www.ikulu.go.tz   
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye aliondoka nchini usiku wa Jumamosi, Julai 25, 2015, amewasili nchini Australia na kuanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku nne kesho, Jumatatu, Julai 27, 2015.

Rais Kikwete anafanya ziara hiyo rasmi ya Kiserikali katika Jumuia ya Madola ya Australia (The Commonwealth of Australia) kwa mwaliko wa Mheshimiwa Jenerali Sir Peter Cosgrove AK MC (Mstaafu), Gavana Jenerali wa Jumuia ya Madola ya Australia.

Wakati wa ziara yake, Rais Kikwete ambaye mara ya mwisho alitembelea Australia kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Serikali wa Nchi za Jumuia ya Madola mjini Perth mwaka 2011, atatembelea mji mkuu wa Australia wa Canberra na miji ya Newcastle na Sydney.

Mara baada ya kuwasili mjini Canberra kesho, Rais Kikwete atapanda Mti wa Kumbukumbu katika Bustani ya Taifa ya Miti ya Australia na kutembelea Makumbusho ya Taifa ya Vita ya nchi hiyo kabla ya kukutana na Watanzania wanaoishi katika Australia.

Kesho kutwa, Jumanne, Julai 28, 2015, Rais Kikwete atafanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali na Waziri Mkuu wa Australia, Mheshimiwa Tony Abbot (MB) na pia kukutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake Gavana Jenerali Sir Peter Cosgrove ambaye alipata pia kuwa Mkuu wa Majeshi ya Australia.

Aidha, Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na Mheshimiwa GaiBrodtmann (MB), Waziri Kivuli wa Ulinzi wa Australia.

Maeneo makuu ambako mazungumzo kati ya Rais Kikwete na viongozi hao wa Australia yanatarajiwa kujikita ni katika eneo la madini na uchimbaji wake, fursa za elimu ya juu na mafunzo ya ufundi, masuala yanayohusu Bahari ya Hindi (The Indian Ocean Rim) na usalama wa Bahari hiyo, ugaidi na masuala ya usalama wa nchi za Afrika Mashariki.

Rais Kikwete pia atatumia nafasi hiyo kuwashukuru na kuagana na viongozi wa Australia, nchi ambayo kwa miongoni mitano iliyopita imekuwa na uhusiano wa karibu na Tanzania katika maeneo ya uchumi, ulinzi, siasa, jamii na masuala ya usalama.

Jioni ya siku hiyo, Rais Kikwete atahudhuria dhifa ya kitaifa ambayo itaandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake, Gavana Jenerali Sir Peter Cosgrove na baada ya dhifa hiyo, Rais Kikwete na ujumbe wake wataondoka mjini Canberra kwenda Sydney, mji mkuu wa kibiashara wa Australia.

Jumatano, Julai 29, 2015, Rais Kikwete atakwenda mjini Newcastle ambako atatunukiwa Digriii ya Uzamivu ya Heshima ya Sheria (Degree of Doctors of Laws Honoriscausa – honorary LLD) na Chuo Kikuu cha Newcastle. Rais atatunukiwa digrii hiyo ya heshima kwa kutambua uongozi wake uliotukuka na mchango wake katika maendeleo ya Tanzania na Afrika na jitihada zake za kuleta amani.

Chuo Kikuu cha Newcastle ni moja ya vyuo ambavyo vimekuwa vinatoa nafasi za masomo kwa wanafunzi wa Tanzania, chini ya sera ya miaka mingi ya Australia kusaidia elimu katika Tanzania.

Wanafunzi 26 wa Tanzania tayari wamemaliza masomo katika chuo hicho na kurejea nyumbani katika maeneo ya madini, elimu ya juu, vyombo vya habari, masuala ya fedha na masuala ya serikali. Wanafunzi 45 bado wanaendelea na masomo yao katika chuo hicho.

Rais Kikwete na ujumbe wake wataondoka Australia asubuhi ya Alhamisi, Julai 30, 2015 kurejea nyumbani.

Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kijeshi wa Fairbairn mjini Canberra katika siku ya mwanzo ya ziara yake Rasmi ya siku nne ya Kiserikali nchini Australia
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitembezwa katika jumba la Makumbusho ya Taifa ya vita - Australian War Memorial - mjini Canberra zilikohifadhiwa kumbukumbu mbalimbali ambayo zinazoonesha jinsi Australia ilishiriki kwenye vita mbalimbali katika siku ya mwanzo ya ziara yake ya Kiserikali nchini Australia
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua na kutoa heshima katika kaburi la askari wa Australia wakati alipotembelea jumba la Makumbusho ya Taifa ya vita - Australian War Memorial - mjini Canberra zilikohifadhiwa kumbukumbu mbalimbali ambayo zinazoonesha jinsi Australia ilishiriki kwenye vita mbalimbali katika siku ya mwanzo ya ziara yake ya Kiserikali nchini Australia
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na \atanzania waishio Australia alipkutana nao na kuongea nao katika siku ya mwanzo ya ziara yake ya Kiserikali nchini Australia.

Job opportunity: Director of Administration and Finance


The Council for the Development of Social Science Research in Africa (CODESRIA) invites applications from suitably qualified nationals of African countries to fill the vacant position of Director of Administration and Finance in its pan-African Secretariat located in Dakar, Senegal. This position is categorised as one of the senior posts in the Council and the successful candidate will join a team of staff members functioning under the direct supervision of the Executive Secretary of the Council.

Recognised as the premier centre on the continent for the generation and dissemination of multidisciplinary social science knowledge, CODESRIA has undergone an exponential growth in programmes, finances and membership over the last decade. The Administration, and Finance department has, as its primary responsibility, the day-to-day management of the administrative and financial affairs of the Council, covering banking and accounting services, the preparation of financial reports for submission to the funders of the Council, budget monitoring and control, human resources (staff recruitment, training, evaluation, discipline and welfare), protocol services, the maintenance of the headquarters building, the monitoring of the physical assets of the Council, the internal and external audits of the financial statements and other accounts of the Council, and all aspects of the procurement of goods and services for the use of the Council.

The Department is also involved in the implementation of a long-term strategy for the financial stability and sustainability of the Council, including the CODESRIA Endowment Fund.

Furthermore, the Director of Administration and Finance (DAF) is responsible for preparing the annual workplan of activities and budgets of the Council, and for monitoring expenses and programme implementation. The successful candidate will also be called upon to initiate, develop and apply new human resource management tools, lend support in the implementation of an IT plan, contribute to the organisation of donor conferences, and manage aspects of the Council’s relations with the public administration services of the host country as may be entrusted to him/her. In all, the candidate who will be chosen will be expected to work towards the efficient and result-oriented administration of all aspects of the mandate of the Council.

Key responsibilities of the DAF also include the following: provides strategic leadership and guidance in administrative and financial management; leads a team of staff in delivering CODESRIA’s administrative and financial obligations; remains up-to-date with the latest methodologies and best-practices, and donor requirements; ensures improved service to Secretariat and community; works with other departments to execute programmes and projects within agreed calendar and timelines; develops suitable and sustainable strategies in administrative and financial management; plans and manages budgets.

More information about CODESRIA and its programmes can be obtained from the Council’s website: www.codesria.org.

Qualifications

Applicants must:


• Have a sound university education in the field of business/financial administration, accounting and/or human resource management (an MBA will be an advantage) with at least five years post-graduation experience in a similar position;

• Hold a post-graduate technical qualification in accountancy or in a related field, and have a demonstrable knowledge of International Financial Reporting Standards (IFRS) in their current application;

• Have experience in fund management, preferably in a not-for-profit organisation;

• Be familiar with accounting and budgetary systems and software employed by international non-governmental organisations;

• Have a demonstrable capacity to initiate and supervise internal and external audit processes;

• Be conversant with the international research funding environment and the requirements of various funding agencies especially in terms of reporting;

• Be knowledgeable and skilled in the management of all aspects of personnel matters, bearing in mind that CODESRIA is a multi-cultural pan-African environment and is committed to the promotion of gender equality;

• Demonstrate a sound knowledge of procedures linked to the diplomatic immunities enjoyed by international organisations;

• Have a demonstrable knowledge of labour laws in an African context;

• Have a capacity to be innovative and forward-looking in the management of the administrative processes and procedures of an organisation like CODESRIA;

• Have good organizational and time management skills highly desirable.

• Personal attributes should also include strong analytical skills and ability to formulate unique solutions based on knowledge and understanding of the challenges; Be strategic, innovative and creative thinker; planning and problem-solving in both short-term and long-term; results-driven; team player; inclusive, flexible, and sensitive to multi-culturalism;

• Have strong communication skills; be self-motivated; possess the ability to lead and motivate a team is crucial; be a professional with high integrity and good stewardship of resources; and

• Be fluent in French or English and have a good working knowledge of the other language.

Working Conditions

The salary level that will be offered will depend on the successful applicant’s experience and qualifications, and will be comparable to those of similar posts in other international organisations.

How to Apply


Applicants must supply the following documents:

1. A written application;

2. A detailed CV describing the contents of their training and professional experience;

3. Three reference letters, two of which must be professional references.

The reference letters in support of candidates must be sealed and sent under separate cover and marked ‘Confidential Reference’, or emailed directly by the referees. The application letters and other supporting documents of candidates should be sent in a sealed envelope marked ‘Application Documents’, or emailed to the address below. Reference letters and applications sent by email should have ‘APPLICATION’ written in the subject line. Both the applications and the reference letters should be sent to:

The Executive Secretary
CODESRIA
Avenue Cheikh Anta Diop x Canal IV
B.P. 3304, CP 18524,
Dakar/SENEGAL
Email: [email protected]

Closing Date

All applications must be received by 15th. September 2015. Any application received after this date will not be considered.

Magazetini Jumatatu, 27.7.2015Aliyekuwa Mbunge CUF na kuhamia ADC achukua fomu ya UraisNa Abdi Suleiman na Abdi Shamnnah,PEMBA.

Aliyekuwa mwanachama wa chama cha siasa cha CUF na Mbunge wa jimbo la Wawi kisiwani Pemba, ambaye kwa sasa amehamia chama cha ADC, Hamad Rashid Mohamed, Leo amechukuwa fomu ya kugombea urais wa Zanzibar kupitia chama chake hicho kipya.

Fomu hiyo alikabidhiwa leo na kamishna wa ADC Kanda ya Pemba, Said Seif huko katika ofisi za chama hicho Wawi kibegi Wilaya ya Chake Chake Pemba.

Akitoa nasaha zake mara baada ya kuchukuwa fomu hiyo, mgombea huyo Hamad Rashid, alisema hatua ya kuchukuwa kwake fomu inalenga kuleta mabadiliko makubwa ya kisiasa Zanzibar.
Alisema kuwepo kwa chama hicho ni kuondosha dhana iliyojengeka miongoni mwa wananchi wa Zanzibar, pamoja na viongozi wa vyama vya upinzani, kwamba vyama vya CCM na CUF ndio vyama vyenye uhalali wa kuongoza nchi.

Alisema hatua ya wananchi wa Pemba kujitokeza na kumpokea kwa wingi ni thibitisho tosha kwa wananchi kuwa wamejenga imani nayeye na wamekubali mabadiliko ili kuelekeza nchi hiyo katika maendeleo ya kweli.

"Leo ni siku ya historia katika chama cha ADC tokea miaka tatu kuwepo kwao, kimeweza kutoa mabadiliko makubwa kufikia kupatikana mgombe wa urais wa Zanzibar" alisema Hamad Rashid.
Aidha aliwapongeza wananchi na viongozi wa ADC kwa ujasiri wao mkubwa wa kuanzisha chama hicho, huku baadhi ya watu na viongozi wa upinzani wakiona hatua hiyo kwamba ni dhambi.

Aliwataka wananchi kisiwani Pemba kuendeleza imani na chama hicho na kuondokana na dhana kwamba CUF ndio chama pekee chenye uwezo wa kuwapelekea maendeleo, huku akibeza kisiwa hicho kubaki nyuma kimaendeleo.

Mgombea huyo wa ADC anatarajiwa kurudisha fomu hiyo Julai 28 mwaka huu, Kwa katibu mkuu wa chama hicho Unguja, kabla ya kuchukuwa fomu ya Serikali ya kugombea urais wa Zanzibar.
Mapema kamishna wa ADC kanda ya Pemba Said Seif alimshukuru mgombea huyo kwa ujasiri na uamuzi wake wa kujitokeza kuchukuwa fomu ya kugombea urais wa Zanzibar kupitia ADC.

"Hiki ni kitendo cha kihistoria kwa mlezi wetu kujitokeza kuchukuwa fomu, sisi wananchi na wananchama wa ADC tuko pamoja na yeye"alisema.

Alisema mgombe huyo ni kiongozi shupavu na aliyekomaa kisiasa, huku wananchi wakiwa na matumaini makubwa kutoka kwake katika kupeperusha bendera ya chama hicho kwenye nafasi ya urais wa Zanzibar.
via ZanziNews blog

Aliyekuwa Mbunge CHADEMA arudi CCM

Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Leticia Nyerere akifafanua jambo kwa waandishi habari juu ya kuondoka katika chama hicho.

MBUNGE wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Mara, Leticia Nyerere amengatuka rasmi leo katika chama hicho na kudai kuwa anarudi nyumbani katika chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa idara ya habari maelezo jijini Dar es Salaam, Leticia amesema kuwa katika suala la kuhamia Chadema hakutafakari kwa kina labda angetafakari asingeweza kwenda huko.

Amesema mchango wake unatambulika sasa anaweza kutumikia CCM nje bila ya kuwa mbunge na kuweza kuleta maendeleo kutokana na uwezo wake katika masuala ya siasa.
“Moyo wangu umekuwa ukisoneneka kutokana na kukaa CHADEMA na kuacha kukaa katika chama kilichonilea na kunisomesha hadi nje ya nchi ,sasa nasema narudi nyumbani kutumikia”
amesema Leticia.

Leticia amesema kwenda CHADEMA alifanya ujinga bila kutafakari na hawezi kulaumu dhamira yake mpya kurudi katika chama kilichompa makuzi yote na atatumikia CCM kwa kasi mpya na kuleta maendeleo chanya kutokana na kile ambacho amekuwa akitoa katika michango ya bunge.

Amesema wapinzani wote wa zamani walikuwa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo katika maamuzi yake ya kwenda Chadema hayakuwa shahihi.


Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Leticia Nyerere akinyanyua mikono ikiwa ni sehemu ya ishara ya kuondoka katika chama hicho na kurejea Chama cha Mapinduzi (CCM) wakati alipokutana na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo leo jijini Dar es Salaam.

Aliyekuwa Mbunge CHADEMA ahamia ACT-Wazalendo


Katibu wa Mipango na Mikakati wa Chama cha ACT-Wazalendo, Habibu Mchange (kushoto), akimkabidhi kadi ya chama hicho, aliyekuwa mbunge wa Viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Iringa mjini, Chiku Abwao baada ya kuhamia rasmi ACT-Wazalendo Dar es Salaam leo mchana.


Mbunge Chiku Abwao (kulia), akionesha kadi ya chama cha ACT-Wazalendo baada ya kukabidhiwa.


Mbunge Chiku Abwao (kulia), akizungumza na wanahabari baada ya kukabidhiwa kadi ya chama cha ACT-Wazalendo.


Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

  • Habari na Dotto Mwaibale

[update] Lowasa CHADEMA; Akaribishwa kujiunga UKAWAViongozi wa juu wa Umoja wa vyama vya Upinzania nchini Tanzania ujuliakanao kama UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi), umemkaribisha rasmi aliyekuwa Kada wa Chama cha Mapinduzi na aliyewahi kiuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli anayemaliza muda wake, Edward Lowasa kuwa mmoja wao. Haijafahamika bayana ikiwa Lowasa tayari amejiunga na chama kimojawapo kinachounda umoja huo ama la, kama inavyoonekana katika picha hapo juu akiwa na viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendelo, CHADEMA

Tukio hilo likiendelea katika Mako Makuu ya Chama cha Wananchi CUF.

Edward Lowassa anajiunga na CHADEMA na atakuwa mgombea urais wa CHADEMA na wa UKAWA. Lowassa is perhaps the most controversial and divisive political figure in the country right now. Na amekuwa hivyo kwa muda mrefu. Sisi CHADEMA tulimweka kwenye Orodha ya Mafisadi kutokana na kuhusika kwake na Kashfa ya Richmond mwaka 2007. Kwa hiyo swali halali kabisa ambalo lazima tulijibu kwa ufasaha ni hili: kwa nini tumekubali, sio tu kumpokea kama mwanachama, bali kumpa heshima ya kuwa mgombea wetu wa urais. Na kwa nini washirika wetu wa UKAWA nao wamemkubali kuwa mgombea wao wa urais??? Jibu ni kwamba tupo katika kipindi na mazingira ya kipekee ya kisiasa katika nchi yetu. Kwa mara ya kwanza katika historia yetu kama taifa, tunaona mfumo tawala ukipasuka vipande vipande. Kwa mara ya kwanza tunaona CCM ikipasuka katikati. Na mtu aliyeipasua CCM na mfumo tawala ni Edward Lowassa. Sisi CHADEMA tumefanya kazi kubwa ya kujenga chama tangu 2010. Tuna wagombea wengi na bora katika majimbo mengi ya uchaguzi na ngazi ya madiwani kuliko ambavyo tumewahi kuwa nao kwa miaka yote ya nyuma. Hata hivyo, ni ukweli pia kwamba kuna maeneo mengi ya nchi ambako tuko dhaifu sana. Kwa kuingia kwake CHADEMA na UKAWA, Lowassa anayaingiza maeneo hayo kwenye ulingo wa kisiasa and very much within our reach. Na Lowassa ataiporomosha CCM kwa sababu ana nguvu kubwa ndani ya chama hicho kuliko mwanasiasa mwingine yeyote. Katika mazingira ya sasa ya kipekee, tunahitaji kuamua nani ni adui mkubwa zaidi wa nchi yetu na ustawi wake: Edward Lowassa mtuhumiwa wa ufisadi au CCM na mfumo tawala ambao unajenga mazingira yanayostawisha na kulinda ufisadi. Sisi Chadema na UKAWA tumeamua kuwa adui yetu mkubwa wa sasa na siku zote ni CCM na mfumo tawala. Tumemkaribisha Edward Lowassa kwa sababu kuwepo kwake kutaharakisha kuiangamiza CCM na mfumo tawala. Tunaomba wananchi mtuelewe na kutuunga mkono.