[copy] BoT Statement: FBME is financially sound


THE Bank of Tanzania (BoT) said yesterday the USA's Financial Crime Enforcement Network (FinCEN) final ruling will have an effect for the future of FBME Bank.

The FinCEN recently ruled that FBME was linked to money laundering and that prohibits the US financial institution from opening or maintaining correspondent accounts or payable on behalf of the bank.

The BoT said in a public notice published in several newspapers that it was aware of the ruling and currently reviewing the situation with the view of determining an appropriate course of action to take including resolution options.

"At the moment FBME will continue with normal banking operations until such time when the Bank of Tanzania will determine its future," the central bank said.

BoT added: "nevertheless, in its financial position FBME remained liquid and solvent." The FinCEN ruling pertains to FBME's banking operations outside Tanzania where scores of its customers have been forced to seek services from other banks and financial institutions.

In another development, the FBME Statutory Manager, Mr Lawrence Mafuru said the final rule-making and the proposed measures issued at end of last week "do not have any new effects" to the bank's customers as are served locally.

"The management of the (FBME) will continue to ensure that all the depositors continue to access their money as much as possible without any need to panic," Mr Mafuru, who is also a Treasury Registrar, said.

The statutory manager said they will continue with their duty of discharging their obligations in line with the term of reference of statutory management mandate.

Since last July, the BoT took over the management of FBME and put it under statutory management with a view to ensure customer's deposits are safe. The move, however, causes no disruptions on the country banking system.

Rather deployed smooth investigations without causing any loss of damage of the bank's assets or panic. FBME is the largest bank in the Tanzania in terms of assets, despite of having all of its assets outside the country, mostly in Cyprus.
  • By Abduel Elinaza, THE DAILY NEWS via AllAfrica

"Dk Slaa ajiuzulu" na "nimestaafu siasa"
Mwanachama aliyejitolea kuendesha akaunti za CHADEMA 'aumizwa'

Miongoni mwa wafuasi, wapenzi na washabiki wa CHADEMA ambao kwao ilikuwa ni nguzo imara ya kutumainia katika ulingo wa siasa, wameeleza 'kuumizwa' na mabadiliko yanayotokea katika chama hicho na baadhi yao wamejikuta katika njia panda, ama kwa kukatishwa tamaa ama kwa kutokujua wapokee vipi yanayotokea, hata ikiwa hawakubaliani nayo.

Baadhi yao baada ya kutafakari kwa muda wameona mengi waliyovumilia na kukubaliana kwa ajili ya umoja na ustawi wa chama yametosha na mengine yanayotokea sasa ni makubwa kupita uwezo wa kuafiki na kukubaliana nayo.

Hivyo basi, katika kuzungumza na baadhi yao, wapo ambao wameamua kutokujishughulisha na masuala ya siasa kabisa hasa kwenye mitandao ya kijamii na hata makundi ya mawasiliano kwenye WhatsApp. Ni kama kwa wakati mmoja, ghafla wamepigwa na butwaa na kushikwa na soni pamo hapo.

Wapo wachache ambao wamechukua maamuzi ya kutangaza kuong'atuka...

Yaliyojiri Twitter, Facebook: Hawa nao wanajiunga CHADEMA?


Leo ni siku inayofuatia jana, siku ambayo Ndugu yangu Edward Ngoyai Lowassa aliacha rasmi uanachama wa CCM na kupewa kadi ya uanachama wa Chadema.Si yeye tu bali alisindikizwa na mke wake mpendwa Mama Regina Lowassa. Nilidhani leo mitandao yote ingesheni habari hiyo kubwa. Kumbe nami nimekuwa " staa " katika mitandao ya kijamii. Kuanzia asubuhi nimekuwa nikipokea na kujibu simu mbalimbali nikiulizwa maoni yangu kuhusu tukio la jana, kuhusu mchakato wa Dodoma uliomalizika hivi karibuni, na " habari " kubwa imekuwa Mwandosya, Mwapachu na ole Medeye wahamia Chadema ! Kuhusu Ndugu Lowassa kuhamia Chadema nionavyo mimi ni jambo la kawaida sana katika demokrasia ya vyama vingi. Wanachama hutoka na kuingia karibu kila siku.Hivyo basi tukio la jana lisingegonga vichwa vya habari kama isingekuwa kwa umaarufu wa mhusika. Jambo la msingi kwa CCM ni kutafakari, bila ghadhabu, na kwa utulivu, ni sababu zipi za msingi zilizofanya hili jambo litokee? Je tunaweza kujifunza lolote katika hili ili kukiimarisha Chama? Tunaweza kuboresha nini katika taratibu na kanuni zetu?

Nimeulizwa pia kitendo cha Ndugu Lowassa kuhamia Chadema kina athari gani kwa CCM? Pamoja na kutotokuwa msemaji rasmi wa Chama, tukio hili lina maslahi ya umma kwa ujumla hivyo kukwepa kujibu hakusaidii. Siasa ni takwimu, hasa tunapoelekea Oktoba. Kwa mantiki hiyo mtu mmoja kukihama Chama kuna maana kura moja iliyopungua. Kwa kuwa haiwezekani kuirudisha, basi changamoto ni kuwa na mkakati wa kutafuta kura ya kufidia, kuzuia kupotea kwa kura nyingine,na kuongeza idadi ya wanaoingia ili iwe kubwa kuliko ile ya wanaotoka. Msaafu wa dini unasema mchungaji bora ni yule anayeweza kuwaacha kondoo wake tisini na tisa walio salama ili amtafute yule mmoja aliyepotea! Suala la kujiuliza katika mazingira ya yaliyotokea ni je tulikuwa wachungaji bora? Nadhani moja ya mambo ya msingi CCM itabidi tulitafakari kuhusiana na mchakato wa kumpata mgombea wetu kwa nafasi ya urais ni je tunamtafuta mwanachama ambaye atakuwa Rais? Je tunamtafuta mtu ambaye atakuwa Rais wa nchi na Mwenyekiti wa Chama? Au tunamtafuta mtu atakayekuwa Rais na Waziri Mkuu? Vigezo vya kumtafuta mtu huyo vinapishana kama ambavyo orodha wa wenye nia au mifumo ya kumpata itapishana. Naamini tungelitafakari haya yote huenda, huenda tusingefika hapa tulipo. Lakini Taifa ni kubwa kuliko sisi watu na uhai wake ni mpaka " kiama cha wafu ". Tujadili masuala haya na mengine muhimu, kwa ujasiri, uwazi na ukweli.

Nahitimisha kwa kujibu taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii na watu wengi ikiwa ni pamoja na waandishi wa habari kuhusu Mwandosya kuhama kwenda Chadema. Misingi iliyojengwa na waasisi wa Chama, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume naendelea kuamini bado ni sahihi. Ndiyo iliyotuletea heshima kubwa kama Taifa. Kama tumeyumba turudi katika misingi. Itikadi ya Chama inajengwa juu ya misingi hiyo. Hivyo basi kwangu mimi Ilihali misingi ipo,na imara, nitaendelea kuwa mwanachama wa CCM ili kwa pamoja na wanachama wenzangu tuendelee kulijenga Taifa juu ya misingi hiyo, kila wakati tukikumbuka kile alichotuasa Baba wa Taifa, Tujisahihishe!

Mwandosya (via Facebook)

Mwaustralia aimba "Tanzania, Tanzania Nakupenda.." Rais Kikwete alipotukiwa


Mrs Bernadette Mathias akiimba Wimbo wa Tanzania Nakupenda Kwa kiswahili akimpongeza Mhe. Dr Jakaya Mrisho kikwete Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa Kutunukiwa Shahada ya heshima ya Udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Chuo Kikuu cha Newcastle cha nchini Australia.

Mwalimu agusia Slaa, Lissu, Mnyika kutokuwepo Lowasa akijiunga CHADEMA

L-R: Mnyika, Slaa, Mwalimu
L-R: Mnyika, Slaa, Mwalimu

Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao Makuu ya Chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam amezungumzia minong’ono inayodai kwamba Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, Naibu Katibu Mkuu - Bara, John Mnyika na Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria wa chama hicho kwamba walisusia tukio la Lowassa kujiunga na chama hicho.
“Jana ilipita minong’ono mingi tu, katibu mkuu wetu yupo kwenye majukumu mengi. Katika kipindi hiki cha uchaguzi tuna mambo mengi. Hatuwezi wote kuwa pamoja. Tunagawanyika kulingana na programu tulizonazo” Lissu azungumzia wanaotaka kuhama baada ya Lowasa kupokelewa CHADEMA


Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu, amesema chama chao kinatarajia kupata wanachama wengi baada Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.

Lissu ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba wapo wanachama wa CHADEMA ambao watakihama chama hicho kutokana na kutokubaliana na ujio wa Lowassa ndani ya CHADEMA.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Lissu amesema,
“Kama wapo watakao jiondoa CHADEMA, wengi zaidi watakuja. Tupo katika kipindi ambacho hatujawahi kuwepo tangu mfumo wa vyama vingi uanze. Mfumo tawala unabomoka vipande vipande. Unapobomoka, dalili zake ni watu ambao wamekuwa katika mfumo huo kuondoka kama alivyofanya Lowassa.”

“Mabadiliko katika nchi yanatokea pale mfumo tawala unapo pasuka. Lowassa ni mfano mzuri.

Tunamkaribisha kwetu siyo kwa sababu ni mwanasiasa msafi. Tumempokea kwa sababu tunaongeza nguvu kubwa kwa wale wanaotaka mabadiliko. Imetokea Zambia Mawawi, Nigeria na Kenya” 
Akizungumza kuhusu CHADEMA kumtuhumu Lowassa kwamba “ni fisadi” kabla ya kujiunga na chama hicho Lissu amesema 
“…hatukuwa na makosa hata kido kumweka Lowassa katika kundi la watuhumiwa wa Richmond. Mambo yalizungumzwa bungeni. Aliwajibika na amesema mwenyewe aliwajibika.”

“Alijiuzulu Uwaziri Mkuu kwa sababu ya Richmond. Tulimweka katika orodha ya mafisadi kwa sababu ya Richmond. Na jana alisema alimwambia rais “tuvunje mkataba” rais akaataa. Angefanyeje? Hilo ni vumbi, litakapotulia Chama Cha Mapinduzi na mfumo tawala utakuwa umeanguka, tutajenga nchini. Bila kuvunja mfumo tawala hakuna kusonga mbele,” 
ameeleza Lissu.

Rais Kikwete atunukiwa shahada ya heshima ya Chuo Kikuu cha Newcastle Ausralia

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans Chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitunukiwa shahada ya heshima ya udaktari wa Sheria (Doctor of Laws honorific causa) na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Newcastle Bwana Paul Jeans Chuoni hapo nchini Australia leo tarehe 29.7.2015 katika ukumbi wa chuo hicho.

Mazingira walimokamatwa "wawekezaji" wakiweka maji ya kunywa kwenye chupa


Uingereza na TAKUKURU watoa mafunzo kwa maafisa wa ofisi 27 za mikoa

Phill Jones na Dk Hoseah

Wachunguzi kutoka ofisi 27 za mikoa za TAKUKURU wanapata ujuzi kupitia mafunzo yenye kugusa masuala ya utakatishaji wa fedha, kupata taarifa na mlolongo wa uhalifu kwa kutumia sheria za sasa za Tanzania.

Mafunzo haya yamefadhiliwa na DFID kama sehemu ya Mpango wa Kuimarisha Mapambano dhidi ya Rushwa Tanzania (STACA) na inasimamiwa na Afisa wa Uingereza toka kitengo cha NCA, Bwana Phill Jones.


Lowasa kuchukua fomu CHADEMA za kuwania Urais Tanzania 2015


Edward Lowasa anatarajiwa kuchukua fomu kutoka chama alichojiunga nacho, CHADEMA, za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania Urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Ikiwa atafanikisha lengo hilo, anatarajiwa kuwa mwakilishi wa vyama vinne vinavyojiita "UKAWA" vilivyokubaliana kumsimamisha mgombea mmoja kwa kila kiti cha uongozi katika Uchaguzi huo.

Taarifa ya Lowassa kuchukua fomu hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Zanzibar, Salum Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika Makao Makuu ya Chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam.
“Kesho saa 5 asubuhi hapa makao makuu ya chama, Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa atachukua fomu ya kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA. Kutakuwa na shamrashara nyingi sana. Na kutakuwa na matokeo mengi baada ya kesho” 


Akamatwa 'stationery' akidurufu shahada 43 za wapiga kura


KIJANA mmoja aliyetambulika kwa jina la Buhula Ngassa (46) mkazi wa kijiji cha Chikobekatika Kata ya Nyachiluluma Wilayani Geita, amekamtwa na viongzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoani humo, akiwa na shahada 43 za kupigia kura.

Tukio la kukamatwa kijana huyo limetokea jana majira ya saa kumi jioni wakati kijana huyo alipokuwa katika duka moja la vifaa vya elimu "stationery" akiwa anatoa nakala ya vitambulisho hivyo.

Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Busanda, George Kwacha pamoja na Mwenyekiti wa tawi la Bugambelele,  Daniel Musa wameeleza jinsi walivyomkamta na kumfikisha katika kituo cha polisi Katoro.

Hata hivyo, mtuhumiwa amedai kuwa shahada hizo zilikuwa za wateja wake waliofika kusajili simu zao.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo akikiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa alikutwa na shahada zilizopita muda wake 7 na nyingine mpya 36 zilizotengenezwa kwa BVR. Uchunguzi zaidi unafanyika ili kufahamu malengo ya kijana huyo.


[video] Mwandishi wa habari akerwa na mkutano wa CCM leo


[update] Naibu Spika lawamani kwa kumpiga mtu "hadi kuzimia"

Update: 31.07.2015 -- Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amekanusha kumshushia kipigo Dk. Joseph Chilongani, ambaye ni mgombea mwenzake katika mchakato wa Chama Cha mapinduzi (CCM), kupata mgombea ubunge Jimbo la Kongwa.

Awali ilidaiwa kuwa Jumatatu jioni Ndugai, alitumia fimbo kumpiga Dk. Chilongani, ambaye alipoteza fahamu kabla ya kupelekwa hospitali ya wilaya hiyo, ambako aliendelea na matibabu mpaka jana aliporuhusiwa.
Mganga Mkuu wa Wilaya, Festo Mapunda, alilieleza NIPASHE jana kuwa walimruhusu kutokana na hali yake kiafya kuwa nzuri.

Naye Naibu Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, hakuwa tayari kueleza ikiwa mpaka jana alikuwa amepokea taarifa rasmi ya tukio hilo kutoka kwa walalamikaji badala yake alisema Dk. Chilongani, jana aliendelea na kufanya kampeni kama kawaida.

Madai dhidi ya Ndugai yalielezwa na Dk. Chilongani, kuwa sababu ya mtafaruku huo ilikuwa mzozo uliyoibuka kati ya Ndugai na mgombea mwingine, Simon Ngatunga, na baadaye Ndugai kumtuhumu Dk.

Chilongani kuwa alikuwa akitumia simu yake ya kiganjani, kumrekodi video ili kusambaza mitandaoni. Hata hivyo Ndugai alisema jana kuwa miongoni mwa wagombea tisa wanaowania nafasi hiyo, baadhi wamepandikizwa kwa lengo la kufanyia fujo.
“Tangu tuanze kampeni, wagombea mapandikizi wanafanya kazi ya kunitukana na kunidhalilisha kila tunakokwenda, mmoja ananiporomoshea matuzi ikitokea nikajibu, wanakuwa wameshapanga mmoja wao wa kunirekodi ili wazidi kunidhalilisha mitandaoni,” 
alieleza Ndugai

Alisema tukio la Jumatatu, wakiwa kwenye mkutano wa hadhara Ngatunga, alimtukana matusi ya nguoni na kusababisha mzozo kati yao, wakati watu wakiendelea kumsihi ampuuze yule kijana huyo akagundua Dk. Chilongani akitumia simu yake kumrekodi.
“Nilishamuonya mara kadhaa aache kujifanya mwandishi wa habari, kwa kuachukua video tena akinilenga mimi tu, lakini hakusikia nilichofanya niliigonga ile simu aliyokuwa akiitumia kuchukua video,”
“Nikaigonga nikimwambia hebu usiendelee kunichukua video na kikamera chako hicho simu ikaanguka chini, nikashangaa kuona na yeye akijiangusha chini kama wachezaji wa mpira wa miguu, ambao hujiangusha kwa lengo la kusingizia wamefanyiwa fujo ili wenzao wapewe kadi nyekundu.”
Ndugai alisema.

Kwa mujibu wa Ndugai, hakumpiga Dk. Chilongani wala hakujaribu kumpiga Ngatunga [NIPASHE]

(wavuti.com imepata picha hii kupitia WhatsApp)

Mbunge wa Kongwa aliyemaliza muda wake ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amempiga mgombea mwenzie kwa nafasi ya ubunge, Dk. Joseph Chilongani kwa madai ya kumpiga picha wakati anafanya fujo kwenye mkutano wa kampeni wa kura za maoni.

Tukio hilo limetokea jana jioni wakati wagombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM wakiwa kwenye mkutano na wanachama wa CCM kwa ajili ya kujinadi kwenye kata ya Ugogoni iliyopo Wilayani Kongwa, Mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo ambaye pia ni mdogo wa Dk. Chilongani, Michael Chilongani, Ndugai alichukua uamuzi huo baada ya mmoja wa wagombea anayeitwa Simon Ngatunga kusema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuwa na ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma na kuahidi kuwa kama atakuwa mbunge atahakikisha kuwa anaziba mianya yote ya ubadhirifu kauli iliyomkera Job Ndugai.

Ilipofika zamu ya Ndugai kujinadi kwa wanachama wa CCM alimtuhumu Ngatunga kwa kusema uongo na kwamba hakuna ubadhirifu wa aina yoyote ndani ya Halmashauri hiyo.

Amesema Ndugai aliposhuka jukwaani alianza kumtafuta Ngatunga ili ampige kwa fimbo ambayo huwa anatembea nayo kwenye kampeni hizo.

Wakati akifanya fujo za kumpiga mgombea huyo, Dk. Chilongani alikuwa anampiga picha kwa kutumia simu yake ya mkononi ambapo Ndugai alipomwona alianza kumshambulia kwa fimbo katika maeneo ya tumboni na kichwani hali iliyomfanya mgombea huyo kupoteza fahamu papo hapo.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, David Misime alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alisema kuwa hana taarifa kuhusiana na tukio hilo ambapo Job Ndugai simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani. [Taarifa ya maandishi imenukutliwa kutoka EATv]


Dk. Joseph Chilongani akiwa hospitali mjini Kongwa

Mnamo tarehe 28.7.2015 majira ya jioni JOSEPH ELIAZA CHILONGANI alifika katika kituo cha Polisi Kibaigwa akilalalmika kuwa wakati wakiwa kwenye kampeni za kujinadi kwa wanachama kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea ubunge kupitia CCM alishambuliwa kwa fimbo sehemu za kichwani na tumboni na JOBU YUSTOO NDUGAI (MB).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamiz wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema mtu huyo aliyejeruhiwa alipewa PF3 na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa uchaguzi wa madaktari na matibabu. Amelazwa na anaendelea na matibabu hadi sasa, hali yake anaendelea vizuri.

Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa malalamiko hayo unafanyiwa kazi kwa kupata maelezo ya watu walio kuwa kwenye mkutano huo wa kampeni na ukikamilishwa jalada litapelekwa kwa Wakili wa Serikali kwa hatua zaidi za kisheria. [Lakia Ndwellah wa Jeshi la Polisi Dodoma.][update] Imekanushwa! Yatokanayo na mkutano: CCM yaeleza sababu 7 za jina la Lowasa kukatwa

Taarifa iliyochapishwa awali yenye sababu 7 za kukatwa kaw jina la Loasa ni ya kupuuzwa kwa kuwa imekanushwa ifuatavyo:-

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Siku za hivi karibuni kumeibuka baadhi ya watu ambao wamekuwa kwa makusudi na kwa malengo maalum wakitunga na kujiandikia taarifa, za uongo, kujenga hofu na au kupotosha na kisha kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa malengo mahsusi dhidi ya Chama Cha Mapinduzi.
Watu hao katika nyakati tofauti wamekuwa wakitengeneza uzushi na uongo huo na kuusambaza kwenye mitandao pamoja na baadhi ya vyombo vya habari kwa lengo lisilo wazi.
Baadhi ya uzushi na uongo uliotungwa na kusambazwa na watu au kikundi hicho ni pamoja na hii ya leo inayoeleza mambo mbalimbali juu ya Ndugu Edward Lowasa na ambayo watunzi wake wameandika kuwa imetolewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Moses Nnauye.
Ifahamike kuwa uzushi huo na mwingine uliofanywa na watu au kikundi hicho umekusudia kujenga msukumo ambao haupo ili kuujengea umma hofu ya huruma dhidi yao ili kusukuma na kushinikiza agenda zao.
Jambo hilo ni uzushi mtupu kwa sababu kwanza Ndugu Nape na wajumbe wote wa Sekretarieti hawapo jijini Dar es Salaam badala yake wapo mikoani kushiriki katika zoezi la kura ya maoni kwa ajili ya uteuzi wa wagombea Udiwani na Ubunge zoezi ambalo litakamilika Agosti Mosi, 2015.
CCM inasisitiza kuwa habari hizo si za kweli, zimeandikwa na watu kwa malengo binafsi ya kugombanisha, kujenga chuki na uhasama baina ya Ndugu Nape, Chama, Wajumbe wa Sekretarieti na wananchi kwa ujumla bila sababu.
Viongozi, wana-CCM na wananchi kwa ujumla hawana budi kupuuza uzushi wowote ule unaotolewa na kusambazwa na watu au vikundi vya hovyo vinavyotumiwa na watu kwa maslahi binafsi, badala yake CCM itakuwa inatoa taarifa sahihi kwa wakati ili kutoruhusu uwepo au kuibuka kwa ombwe la mawasiliano baina ya umma na Chama.

Imetolewa na:-

Kitengo cha Mawasiliano na Umma
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM
Lumumba, Dar es Salaam.
29/07/2015 

-------------

Ndugu wananchama wa Chama cha Mapinduzi-CCM ni wiki mbili tangu tulipo maliza mchakato ndani ya chama kumpata mgombea wa Urais hapo Octoba 25, 2015. 

Kwa mara ya kwanza wananchama 41 waliomba kuteuliwa na chama. Hii inaonyesha kwamba demokrasia imekuwa ndani ya chama. Kati ya wanachama wa CCM waliochukua fomu alikuwa ni mheshimiwa waziri mkuu mstaafu Ndugu Edward Lowasa. Utaratibu wa chama ulifuatwa ili kumpata mgombea ikiwa ni pamoja kamati ya maadili, kamati kuu na halmashauri kuu ya taifa na mkutano mkuu. Katika mchakato pia chama kilitumia idara mbalimbali kama usalama wa taifa, takukuru na tume ya maadili ya umma kupata taarifa mbalimbali kuhusu wagombea hasa za uadirifu, usalama wan nchi na kadhalika.

Baada ya mchakato kumalizika baadhi ya wagombea na wanachama hawakuridhika na matokea, katika chama kikubwa kama CCM haizekani wanachama wote wakaridhika na maamzi. Ndugu wanachama na watanzania tunaomba kuelewa kuwa kumpata kiongozi mkubwa wa nchi kama Rais siyo kazi rahisi. Baadhi ya wanachama ambao hawakuridhika na maamzi ya chama ni Ndugu Edward Lowasa, amekuwa akizungumza nje ya chama kuhusu kutotendewa haki na baade kuhama chama na kujiunga na chamacha demokrasia na maendeleo-CHADEMA.

Kwa nini Ndugu Lowasa hakuteuliwa kuwa mgombea wa CCM?

Ndugu wanachama na watanzania, Mheshimiwa Lowasa alijenga hisia na kuamini kuwa ndani ya CCM wagombea wote walistahili kuenguliwa isipokuwa yeye. Hii siyo demokrasia, baada ya kupitia repoti mbalimbali Ndugu LOWASA alienguliwa kwa sababu zifuatazo:-
  1. Kukiuka taratibu za chama kwaani alionekana kufanya kampeni badala ya kutafuta wadhamini
  2. Kutoa rushwa kwa wanachama mbalimbali hivyo kukigawa chama na kama angepishwa kuwa mgombea CCM ilikuwa katika hatari ya kuwekewa pingamizi mahakamani lakini pia angeweka watu wake kwenye utawala kuwalipa fadhira.
  3. Edward Lowasa aliwahonga wajumbe katika uchaguzi wa wajumbe NEC uliofanyika miaka iliyopita ili kupata watu wake ndani ya NEC.
  4. Kuanza kampeni kabla ya wakati, alikuwa akisafirisha watu mbalimbali na kuwalipa fedha nyingi kisha kutoa taarifa kuwa walikuwa wakimtaka kugombea Urais, hii ni hadaa na hatari kwa chama.
  5. Kuwa na kashfa nyingi za ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi ya umma akiwa waziri.
  6. Kusemwa semwa kuhusika kuhusika na tuhuma za kutumia watu kudhuru baadhi ya watanzania na viongozi, hili lipo kwenye vyombo vya dola kwa uchunguzi, uchunguzi ukikamilika sheria itachukua mkondo wake.
  7. Utajiri na mali usiokuwa na maelezo alizipataje kama vile kumiliki majumba nje ya nchi kama uingereza, singapole na nk.
Mwisho chama kimesikitishwa sana na kauli kuwa amekuwa akionewa na kusingiziwa kuwa alihusika na kashfa ya RICHMOND, ndugu wanachama kashfa ya RICHMOND ilianzia bungeni, CCM haikuhusika na kumwondoa kwenye uwaziri mkuu, lakini kwa kuwa imekuwa inajengeka kuwa alionewa tunaviomba vyombo vya sheria kulipeleka jambo hili mahakamani ili kuondoa dhana inayojengeka kuwa serikalia ya CCM inaonea wanachama wake. Doa linalotakwa kujengeka litapatiwa ufumbuzi na iwapo inathibitika kulikuwa na njama binafsi wote waliohusika kulidanganya bunge watachukuliwa hatua na chama lakini pia sheria itachukua mkondo wake.

Imetolewa na :-
Nape M.Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI

Taarifa ya habari ya kutwa nzima ya Jumanne, ChannelTEN
Taarifa ya Asubuhi Njema ya ChannelTEN 29.7.2015


Magazetini Jumatano, Julai 29, 2015