Wachoma moto sanduku la kura


Wanachama 401 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), tawi la Gidamula, Kata ya Gidehababieg, wilayani Hanang, wamevamia kituo cha kupiga kura na kuchoma moto kura zilizokuwa kwenye boksi baada ya kuelezwa wasingeweza kupiga kura kwa vile namba za kadi zao hazimo kwenye daftari la wanachama.

Wakati wanachama hao wakichoma moto kura hizo, baadhi ya wanachama katika tawi la Orbesh lililopo Kata ya Ideti, walikuja juu na kulazimisha uchaguzi huo kusitishwa baada ya majina yao kutokuwepo kwenye daftari la wanachama licha ya kuwa na kadi za CCM.

Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang, Kajoro Vyohoroka, alithibitisha kuchomwa kwa kura katika tawi la Gidamula na kusitishwa upigaji kura tawi la Orbesh juzi.

Alisema baada ya kushauriana na Katibu wa CCM Mkoa wa Manyara, walikubaliana zoezi la kura lifanyike upya kwa siku ya jana.

Akifafanua zaidi kuhusu vurugu hizo, alisema, awali upigaji kura tawi la Gidamula ulianza vizuri asubuhi, lakini ilipofika majira ya saa 9 alasiri, liliibuka kundi kubwa la wanachama waliounga foleni wakitaka watumie haki yao ya kupiga kura licha ya namba za kadi zao kutokuwa katika daftari.

“Walikuwa na kadi halali, lakini wakati wakifanyiwa uhakiki kwenye daftari la wanachama katika tawi halikuonyesha namba za kadi hizo.

“Hali hiyo ilisababisha wanachama, wasimamizi na viongozi wa tawi na wagombea kugawanyika huku wakitaka waruhusiwe kupiga kura huku wengine wakipinga.

“Sasa wanachama hao wakaona haki yao ya kupiga kura itapotea…wakajiunga kwenye foleni huku wakisema kura haiwezi kuendelea kupigwa vinginevyo na wao waruhusiwe kupiga.

Hata hivyo, vurugu hizo zilisababisha wanachama hao kuvamia chumba cha kupigia kura na kubeba boksi la kuwekea kura na kutoka nalo nje na kuchoma moto kura zote kuharibu ushahidi.

“Mwanzoni walichukua boksi la kura huku wakidai haziwezi kuhesabiwa bila ya wao kuruhusiwa kupiga kura, lakini baadaye wakatoka nazo na kuzichoma moto ili kupoteza ushahidi kabisa.

Alisema walikuwa wakisema wanafanya hivyo kwa sababu wameona haki yao ya kupiga kura inapotea.
Walisema kosa lililotokea la kutoandikwa namba zao katika daftari hilo sio la kwao hivyo hawapaswi kuzuiwa kupiga kura.

“Niliwasiliana na Katibu wa Mkoa kuhusu suala hilo naye akaunga mkono kura zipigwe upya leo (jana)… baada ya kwenda kuwasikiliza na kutatua sintofahamu hiyo.

“Nimeitisha kikao cha halmashauri ya tawi, mabalozi wote katika tawi hilo na kamati ya siasa ya kata pamoja na wagombea,” alisema na kuongeza, kikao kimefanyika vizuri na zinarudiwa kupigwa. Akizungumzia tukio la pili katika tawi la Orbesh, Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Vyohoroka alisema, baadhi ya wanachama katika tawi hilo waliokuwa na kadi hawakukuta majina yao yameorodheshwa katika daftari la wanachama.

Alisema majira ya asubuhi wanachama ambao hawakukuta majina yao walipoelezwa kuwa hawawezi kupiga kura waliondoka bila matatizo, lakini ilipofika saa 9:45 wachache ambao hawakukuta majina yao walikataa kuondoka.

Alisema wanachama hao walitaka waruhusiwe kupiga kura hivyo wakalazimisha zoezi la kupiga kura lisitishwe.

Alisema katika hatua hiyo kulikuwa na mgawanyiko kati ya wasimamizi, viongozi wa tawi na wagombea ambapo baadhi yao walitaka waruhusiwe na wengine wakipinga.

Alisema waliopinga walitaka wale waliozuiwa majira ya asubuhi nao waitwe ili kupiga kura.
Alisema mtafaruku huo ukasababishe zoezi hilo liahirishwa hadi jana.

Alisema aliwenda kukutana na uongozi wa ngazi ya tawi hilo pamoja na wagombea ili kutatua tatizo hilo na kura zilipigwa upya kwa kuwaruhusu wale ambao majina yao hayakuwamo kwa sababu tatizo lililotokea lilikuwa la kifundi lililosababishwa na kati ya tawi kushindwa kuandika majina katika daftari hilo.

“Tatizo la Orbesh ni la taratibu za kiufundi…hili ni tawi jipya toka Ideti, hivyo wanachama hao walikuwa bado hawajahamishwa kutoka upande mmoja wa tawi kwenda tawi lingine.

“Taratibu za kiufundi tu…aliyehamisha majina kwenda Orbesh hakuhamisha majina yote na kuyapeleka kila upande.

“Nimeenda na kuyapitia madaftari ya pande zote na kuhakiki majina na hatimaye wamepiga kura,” alisema.

Katika uchaguzi huo, Katibu wa CCM Wilaya, alisema mbunge aliyemaliza muda wake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uratibu na Mahusiano), Dk Mary Nagu, alikuwa anaongoza kwa kupata kura 21,837 katika matawi 148 kati ya matawi 150 yaliyopo jimboni humo.

Alisema matokeo ya kata mbili yalikuwa yakisubiriwa baada ya wananchi kurudia kupiga kura.

Wagombea wengine wa nafasi ya ubunge jimboni humo na kura zao katika mabano ni Peter Nyalandu (5,558), Wakili Duncan Mayomba (4,412) na Dk Eliamani Sedoyeka.
Kata mbili ambazo zilikuwa na vurugu zimerudia uchaguzi.

Madereva watangaza mgomo nchi nzima wiki ijayo


Magazetini Agosti 3, 2015


Asubuhi Njema ya ChannelTEN Agosti 3, 2013


Amama Mbabazi ajitoa chama tawala; Atajitegemea kuwania Urais

 Amama Mbabazi
 Amama Mbabazi

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi, ametangaza kwamba atawania kiti cha urais wa nchi hiyo kama mgombea wa kujitegemea katika uchaguzi utakaofanyika mwaka 2016 nchini humo.

Mbabazi ambaye alifutwa kazi mwezi Septemba mwaka jana, alitoa maelezo kwa waandishi wa habari na kufahamisha kujiondoa kwake katika kinyang’anyiro cha kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama tawala cha NRM kinachoongozwa na rais Yoweri Museveni.
‘‘Nimeamua kutowania nafasi ya kubeba bendera ya chama tawala cha NRM. Badala yake, nitasajiliwa kama mgombea wa kujitegemea na tume ya uchaguzi ya kitaifa.’’
Mbabazi amekuwa akishutumu malipo ya chama na kusema kwamba yanalenga kuwapa nafasi wanachama matajiri na kuwakandamiza masikini.

Mnamo tarehe 15 mwezi Juni mwaka huu, Mbabazi alitangaza kwamba atagombea urais kwa tiketi ya chama tawala. [via Radio Uturuki Swahili]

Mkuu wa ujasusi (mstaafu) Burundi auawa


Luteni jenerali Adolphe Nshimirimana, mkuu wa zamani wa majeshi kutoka kundi la zamani la waasi la CNDD-FDD na mmoja wa wababe wa utawala wa Pierre Nkurunziza ameuawa Jumapili asubuhi Agosti 2 mjini Bujumbura katika shambulio la roketi.

Wakati hu huo, mwandishi wa Idhaa ya Kifaransa ya RFI mjini Bujumbura, Esdras Ndikumana amekamatwa na afisaa wa Idara ya Ujasusi wakati alipokua akiendesha kazi yake ya kutafuta habari katika eneo la tukio. Esdras Ndikumana amepigwa vikali katika ofisi za Idara ya Ujasusi kabla ya kuachiliwa huru.

Kwa mujibu wa mashahidi, gari la luteni jenerali Adolphe Nshimirimana lililengwa kwa mashambulizi ya roketi mbili, kisha kufyatuliwa risasi nyingi asubuhi ya Jumapili mwishoni mwa juma hili. Tukio hilo limetokea karibu na hospitali ya Mfalme Khaled katika mji mkuu, Bujumbura. Vikosi vya usalama vimearifu kuwa vimewakamata watu saba wanaoshukiwa kuendesha shambulio hilo, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Muda mfupi kabla ya saa sita mchana, mshauri mkuu wa rais anaye husika na maswala ya mawasiliano, Willy Nyamitwe, amethibitisha kifo cha afisa huyo mwandamizi katika jesi. " Nimempoteza ndugu, jamaa. Ninasikitika kwa kweli na kifo cha Adolphe Nshimirimana, ambaye hayupo tena katika ulimwengu huu ", Willy Nyamitwe ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter.

Adolphe Nshimirimana
Adolphe Nshimirimana (picha: isanganiro.org)

Mkuu wa zamani wa majeshi kutoka kundi la zamani la waasi la CNDD-FDD na mkuu wa zamani wa Idara ya Ujasusi, kabla ya nafasi yake kuchukuliwa mwezi Novemba mwaka 2014 na jenerali mwenye msimamo wa wastani Godefroid Niyombare.

Adolphe Nshimirimana alikua mmoja wa wababe wa utawala wa Pierre Nkurunziza, ambaye alionekana kuwa karibu na rais huyo kwa kipindi kirefu cha utawala wake. Luteni jenerali Adolphe Nshimirimana alikua aliteuliwa afisaa anayehusika na safari za rais, lakini, kwa ukweli, aliendelea kujishughulisha na uongozi wa jeshi na kazi zingine za kumlindia usalama rais Pierre Nkurunziza, huku akiwa na ushawishi mkubwa katika chama tawala cha Cndd-Fdd.

Luteni Jenerali Nshimirimana alionekana kama mwaandaaji na mpangiliaji wa ukandamizaji ulioshuhudiwa katika miezi ya hivi karibuni, na pia alikua mmoja wa maafisa wa jeshi waliozima jaribio la mapinduzi lililotokea mwishoni mwa mwezi Mei.

Kifo cha jenerali adolphe Nshimirimana kinakuja wiki moja baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa urais, ushindi unaompelekea rais huyo kuanza awamu ya tatu, ambayo imezua utata nchini Burundi.

Mwandishi wa RFI akamatwa na kupigwa


Muda mfupi baada ya shambulio hilo, mwandishi wetu nchini Burundi, Esdras Ndikumana, alijielekeza katika eneo la shambulio, na wakati alipokuwa akipiga picha, alikamatwa na kupelekwa kwenye makao makuu ya Idara ya Ujasusi. Huko, alipigwa na kuitwa " mwandishi wa habari adui ". Baadae aliachiliwa na kupelekwa hospitalini kwa matibabu ya kidole chake kilichovunjwa.

RFI inatolea wito Ofisi ya rais wa Burundi kupinga kitendo hicho cha ukatili alichofanyiwa mwandishi wetu.

Adolphe Nshimirimana, alikua miongoni mwa wanaomuunga mkono Pierre Nkurunziza

Adolphe Nshimirimana alikuwa mwaminifu kati ya waaminifu wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, mkono wake wa kulia, mtu muhimu kwa usalama wake. Alikuwa mmoja wa wale ambao rais alijua angeweza kutegemea. Luteni jenerali Adolphe Nshimirimana kama rais Pierre Nkurunziza, walifanya vita vya maguguni kutoka kundi la waasi wa kihutu la Cndd-Fdd, ambacho kwa sasa ni chama tawala. Luteni jenerali Nshimirimana aliwahi kuwa mkuu wa majeshi ya Burundi katika miaka ya 2005 hadi 2007.

Tanzania to host origins of humankind talks

Panoramic view of Olduvai Gorge.jpg
"Panoramic view of Olduvai Gorge" by רנדום - Own work. Licensed under CC BY-SA 3.0 via Wikimedia Commons.

ARUSHA, Tanzania - International scientists and researchers of the origin of humankind are set to meet in Dar es Salaam this week to discuss and review scientific findings of the history of the first human being.

The East African Association for Paleoanthropology and Paleontology (EAAPP), the four-day scientific conference is expected to attract scientists and historians to review their work on the discovery of early man in East Africa.

According to a statement from EAAPP offices in Tanzania and Kenya said the researchers will hold their fifth biannual conference in Dar es Salaam from3rd to 6th August.

EAAPP is currently commemorating the height of the 50th anniversary of the milestone discovery of the remains of early man on earth in which the specimens are preserved at the National Museum of Tanzania and the Olduvai Museum in Ngorongoro Conservation Area in northern Tanzania.

Named “Zinjanthropus” or Homo habilis (OH7), the discovery of this humanoid skull with huge teeth allowed scientists to date the beginnings of mankind between two and 3.5 million years ago, and to confirm that, in deed, human evolution began in Africa.

The milestone discovery of the remains of early man on earth was made by the famous British archeologist, Dr. Louis and his wife Mary, at Olduvai Gorge inside the Ngorongoro Conservation Area in 1959 after years of archaeological research and excavation.

EAAPP conference has invited East Africans, international researchers and cultural heritage managers in a forum to share current research findings and knowledge on the status of human origins fifty years after the discovery of Zinjathropus (Homo habilis) at Olduvai Gorge.

The forum will also provide unique opportunity of discussions among scientists, curators and experts on pre-history to review their research development, conservation, and curatorial management.

Excavation sites in Tanzania and Kenya are part of tourist attractive sites where tourists across the world visit to learn about the early man and pre-historic discoveries.
  • By Elisha Mayallah, Saturday, August 01st, 2015 via BusinessWeek

Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA: Mnyika ahudhuria; Dk Slaa "nope"

Pichani kutoka kushoto Naibu katibu mkuu Bara Mh John Mnyika, Naibu katibu mkuu Zanzibar Mh Salum Mwalim, Mwenyekiti Mh Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Mh Issa Mohamed na Makamu Mwenyekiti Bara Prof Abdalla Safari.

MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika, amehudhuria kikao cha Kamati Kuu (CC) ya chama chake jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka ndani ya kikao cha CC kinachofanyika katika hoteli ya Bahari Beach zinasema Mnyika amehudhuria mkutano huo na kueleza kuwa kutoonekana kwake kumetokana na matatizo ya familia.

Mnyika ambaye ni Naibu Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amekuwa haonekani tangu Edward Lowassa alipojiunga na chama hicho, Jumapili iliyopita.

Mwanasheria mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu amethibitisha Mnyika kuhudhuria mkutano huo:
“…Mnyika yupo ndani ya ukumbi wa mkutano. Anashiriki kikao cha kamati kuu. Waliokuwa wanadhani chama chetu kimepata mpasuko kutokana na ujio wa Lowassa, walikuwa wanajidanganya.”
Lissu amesema, ndani ya CHADEMA wako wamoja, yote yaliyotokea yalikuwa mapambano yanayotokana na ukomavu wa kidemokrasia uliyopo.

Katibu mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa ambaye alishiriki vikao vyote muhimu na majadiliano vilivyomkaribisha Lowassa ndani ya CHADEMA, hajaonekana katika ofisi za chama hicho tangu Lowassa ajiunge na CHADEMA; jambo ambalo limezua taharuki kwamba huenda amejiuzulu wadhifa wake.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (pichani) amezungumzia kukosekana kwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa katika vikao vya chama hicho vinavyoendelea jijini, akisema: “Nitazungumzia suala hilo muda muafaka ukifika.”

Mbowe alisema hayo jana katika Hoteli ya Ledger Plaza Bahari Beach kilipokuwa kinafanyika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema jana.

“Siwezi kusema zaidi ya hapo,” alisema Mbowe alipoulizwa sababu za kutokuwapo Dk Slaa katika vikao hivyo muhimu na kuongeza atatoa baadaye, mrejesho wa kikao hicho.

Kauli hiyo ya Mbowe haikuondoa wingu zito lililotanda Chadema baada ya kutoonekana hadharani kwa kiongozi huyo katika matukio manne muhimu ya chama hicho kikuu cha upinzani, tangu waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ajiunge nacho.

Tofauti na Dk Slaa, Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika alionekana jana kwa mara ya kwanza katika kikao hicho na kufuta uvumi uliokuwa umesambaa kuwa alikuwa na mpango wa kuachana na Chadema kama inavyodaiwa kwa Dk Slaa.

Viongozi hao walianza kutoonekana katika shughuli za chama tangu Lowassa alipojiunga na Chadema Julai 28 na kukabidhiwa fomu ya kugombea urais Julai 30 na juzi Agosti Mosi alipozirejesha.

Hata hivyo, viongozi waandamizi wa Chadema wamesema suala la kutokuwapo kwa Dk Slaa halipaswi kukuzwa kwa kuwa ‘anafanya kazi nyingine za chama.’

Alipoulizwa jana, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu alisema: “Suala la kutokuwapo Dk Slaa ni kitu cha kawaida, anafanya kazi nyingine huko, lakini pia kuna wasaidizi wake hapa ambao ni sisi manaibu. Mlikuwa mnazungumzia Mnyika naye haonekani, si huyo. Hatuwezi kuendelea kujibu ‘rumors’ (uzushi) wa kwenye mitandao… nyie subirini si tupo mtaona kama yupo au la.”

Mnyika atinga kikaoni

Jana, Mnyika alionekana katika viwanja vya hoteli hiyo lakini alikataa kuzungumzia kwa undani suala hizo.

“Siwezi kuzungumza chochote,” alisema Mnyika na hata alipoulizwa ni lini atawaeleza Watanzania juu ya kutoonekana kwake alisisitiza mara tatu kuwa “Siwezi kuzungumza chochote.”

Chama hicho kinaendelea na mfululizo wa vikao vya vyombo vya juu ambapo leo kinatarajia kutafanya kikao cha Baraza Kuu kabla ya Mkutano Mkuu kesho kumpitisha mgombea wa urais kesho.
  • Imeandikwa na  Kelvin Matandiko na Bakari Kiango via Mwananchi

ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, ambaye tayari amekwishakujivua uanachama wa chama hicho, amesema maisha yake binafsi pamoja na ya familia yake sasa yapo hatarini.

Hatua hiyo ya Dk. Slaa kufichua hatari hiyo inayomkabili dhidi ya maisha yake aliiweka bayana mwishoni mwa wiki katika mawasiliano yake na chumba cha habari cha Kampuni ya Raia Mwema Ltd, inayochapisha gazeti la kila wiki la Raia Mwema na gazeti hili la Raia Tanzania, linalochapishwa kila siku.

Slaa alilieleza Raia Tanzania kwamba kuna juhudi kubwa zinazofanywa na watu ambao hakuwa tayari kuwataja, akisema juhudi hizo zinalenga kutengeneza mizengwe ya kila aina na kisha kumdhuru, lakini hata hivyo, akisema haogopi chochote na kama ni “Mapenzi ya Mungu yatimizwe.”

“Ni dhahiri ninatengenezewa mizengwe ya kila aina. Inaonekana maisha yangu na ya familia yangu sasa yako hatarini. Nimekuambia (mwandishi wa gazeti hili) ili ikitokea chochote ujue siyo bahati mbaya. Sijawahi kuogopa na wala sitaogopa. Mtetezi wangu ni Mungu aliyehai na nina hakika atanilinda kama yanayopangwa siyo mapenzi yake. Kama ni mapenzi yake yatimie na isiwe kama ninavyotaka mimi,” alisema Dk. Slaa.

Ilivyokuwa kujivua uanachama

Maisha ya Dk. Slaa yapo hatarini ikiwa ni takriban wiki moja tangu ajiuzulu wadhifa wake wa Katibu Mkuu Chadema na kisha kujivua uanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Katika uamuzi wake wa kujiuzulu na kisha kujivua uanachama, Dk. Slaa pia aliweka bayana kwamba anastaafu shughuli za kisiasa, akifanya hivyo kutokana na uongozi wa juu wa Chadema kumkaribisha “kwa mizengwe” ndani ya chama hicho aliyekuwa kada wa CCM, Edward Lowassa, ambaye sasa ndiye mgombea wao pekee wa urais.

Dk. Slaa hakubaliani na namna Lowassa alivyokaribishwa Chadema bila kufuata utaratibu waliokubaliana ndani ya vikao vya chama hicho.

Taarifa ambazo gazeti hili lilizipata wiki iliyopita zinasema, miongoni mwa mali za Chadema ambazo Dk. Slaa alizirejesha baada ya uamuzi wake wa kujiuzulu na kujivua uanachama, ni pamoja na gari alilokuwa akitumia kwa nafasi yake ya Katibu Mkuu. Mbali na gari hilo, alirejesha pia nyaraka nyingine za chama hicho.

Raia Tanzania lilipata taarifa za kurejeshwa kwa mali hizo za Chadema na kupiga kambi Ijumaa iliyopita, maeneo ya Ofisi za Makao Makuu ya Chadema, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam hadi liliposhuhudia tukio hilo la kihistoria.

Majira ya saa 3.15 hivi, gari aina ya Noah lenye namba za usajili T 217 BUZ liliingia katika Ofisi za Chadema likiwa na watu wawili na gazeti hili liliwashuhudia wakiteremka na mkoba mwekundu na kisha kuingia ofisini.

Wakati huo nje ya ofisi, kulikuwapo pikipiki moja iliyokuwa ikizunguka Mtaa wa Ufipa kana kwamba inafanya doria.

Baada ya muda mfupi, saa 3:20 hivi, watu hao walitoka nje ya Ofisi ya Chadema wakiwa mikono mitupu, wakaingia kwenye gari lao na kuondoka eneo la Ufipa. Raia Tanzania lilishuhudia pikipiki hiyo iliyokuwa ikifanya doria ikiingizwa ofisini humo muda mfupi baadaye.

Kuhusu kurudisha kadi yake ya uanachama wa Chadema Ijumaa usiku, Dk. Slaa aliliambia Raia Tanzania akisema: “Sikuwahi kurudisha kadi ya CCM, kwa nini nirudishe kadi ya Chadema? Kadi ni mali yangu na hili nimekuwa nikilieleza mara kwa mara.”

Mbali na kauli hiyo ya Slaa, moja ya vyanzo vyetu vya habari kutoka Makao Makuu Chadema kilieleza; “Hilo sasa ni suala ambalo confirmed (ni rasmi). Dk. Slaa amejivua nafasi yake ya Ukatibu Mkuu na kujivua pia uanachama wa Chadema. Amekerwa na namna mambo yalivyofanyika hovyo, bila kujali misingi ya utawala na maadili katika chama.”

Dk. Slaa aliacha uanachama wa CCM na kuingia Chadema mwaka 1995 baada ya kutoridhishwa na mchakato wa kusaka wabunge ndani ya chama hicho.

Mwaka huo 1995 alishinda ubunge kupitia Chadema na kudumu bungeni hadi mwaka 2010 alipogombea urais na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais Jakaya Kikwete, huku matokeo ya kura za urais yakigubikwa na tuhuma za uchakachuaji.

Tangu gazeti hili lilipoweka hadharani wiki iliyopita ukweli kwamba mwanasiasa huyo anayekubalika zaidi nchini ameacha nafasi ya Katibu Mkuu wa Chadema, kumekuwa na uzushi mwingi katika mitandao ya kijamii nchini.

Uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wake Chadema kwa kutoridhishwa na kupokewa kwa Lowassa kwenye chama hicho bila masharti, umefuatiwa na juhudi kubwa kutoka kwa watu mbalimbali kukanusha taarifa hizo kwa malengo ambayo hayajaeleweka wazi, lakini Ijumaa Dk. Slaa aliliambia Raia Tanzania kwamba ameamua kukaa kimya na kutojibizana na watu hao, asije akawa kama wao.

“Nimezoea kusimamia maadili ninayoyaamini. Nimeheshimu na kutii dhamira yangu daima kwa kuwa naamini Mungu huzungumza nasi kupitia dhamira zetu ndiyo maana binadamu tuko tofauti na viumbe wengine. Watasema mengi, propaganda daima hazijengi,” alisema Dk. Slaa na kuongeza:

“Wanaotumia propaganda kuhalalisha uamuzi mbovu, hawajui madhara wanayoyasababisha.

“Nitakuwa sina tofauti na wao nikipoteza muda kujibu kila kinachoandikwa kwenye mitandao. Nakuhakikishia sitakwenda chama kingine, bali nimestaafu siasa ili nitumikie taifa langu kwa njia nyingine,” alimwambia mwandishi wetu.

Akizungumzia taarifa zilizozagaa kwamba angezungumza na waandishi wa habari, Dk. Slaa aliliambia Raia Tanzania kwa kifupi: “Sina mpango huo, sina papara, najua kuna mengi yatasemwa. Wakati ukifika nitayazungumzia.”

Kutokana na uamuzi huo wa Dk. Slaa ni dhahiri sasa Chadema kinakabiliwa na wakati mgumu wa kusaka mrithi wa Katibu Mkuu huyo wa zamani aliyekuwa amekifikisha chama hicho katika kilele cha siasa Tanzania, na tayari watu wa karibu na Lowassa wameanza kujipanga kwa ajili ya kuinasa nafasi hiyo ya Katibu Mkuu.

Makongoro Nyerere ashangaa
Katika hatua nyingine, mmoja kati ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyekuwa akiwania kuteuliwa na chama hicho kupeperusha bendera kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu, Makongoro Nyerere, amesema Chadema kitapata wakati mgumu kumsafisha mgombea wao wa urais, Edward Lowassa.

Makongoro na Lowassa ni miongoni mwa makada 32 wa CCM waliokatwa majina yao na Kamati Kuu ya chama hicho mjini Dodoma mwezi uliopita.

Akizungumza na Raia Tanzania jana, Makongoro alisema uamuzi wa Lowassa kuhamia Chadema ni wa kidemokrasia na haki ya kila Mtanzania.

“Huo ni uamuzi binafsi, uheshimike. Lakini chama chake kipya kitapata wakati mgumu sana kumsafisha kutokana na tuhuma za ufisadi anazoandamwa nazo.

“Chadema walikubalika mioyoni mwa wananchi kutokana na hoja ya ufisadi dhidi ya Lowassa. Hiyo sabuni au brashi ya kumsafisha haipo hata Nakumatt,” alisema Makongoro, mmoja kati ya wanaCCM wachache waliokuwa wakimnyooshea kidole Lowassa wakati wa kusaka wadhamini ndani ya chama hicho.

Kuhusu uamuzi wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa kuachana na siasa, Makongoro alisema hilo si jambo jema hata kidogo.

“Tuna muhitaji. Taifa linamuhitaji. Wanasiasa wa aina yake wanatakiwa kuendelea kutoa mchango kwa mustakabali mwema wa taifa letu. Ninamshauri asiache siasa, aje CCM tujenge taifa,” alsema.
  • via Raia Tanzania

Tizama AzamTv LIVE online

Bofya hapa

Masista wa Italia wafanikisha ujenzi wa zahanati Vikawe

Mkuu wa Masista Waabuduo Damu ya Kristo, Euphrasia Julius akimtambulisha mgeni rasmi na meza kuu kwa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe (hawapo pichani) katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa Maria De Mathias (MDM) Vikawe, Kibaha.

Na Mwandishi wetu, Kibaha

MGANGA Mkuu wa halmashauri ya Mji Kibaha, Dk. Happniness Ndosi amepongeza shirika la Masista wa Waabuduo damu ya Kristo kwa kufanikisha ujenzi wa zahanati ya kisasa katika kijiji cha Vikawe wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Mganga huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa zahanati hiyo,pamoja na kuwapongeza amesema serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yote kwa lengo la kuwezesha kila kijiji kiwe na zahanati na kila kata kituo na kila wilaya kuwa na hospitali.

Aliwapongeza masista hao kwa kuonesha upendo na huruma kama Biblia inavyomsimulia msamaria mwema ambaye alikuta mtu aliyepigwa na majambazi na kumsaidia.

Aliahidi ushirikiano wa serikali katika kufanikisha usajili wa zahanati hiyo na kuendelea kuisaidia hatua kwa hatua hadi inakuwa kituo mpaka watakapofanikisha safari yao ya kuwa hospitali kubwa ya kisasa.

Mganga huyo pamoja na kutoa ahadi hiyo aliwataka wananchi wa Vikawe kutumia huduma hiyo na kwamba zahanati hiyo itakapohitaji msaada wa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) wataletewa kuchukua mgonjwa na kumfikisha panapohusika.

Zahanati hiyo ya DA.MA Africa imejengwa kwa ufadhili wa wakristo wa Italia chini ya usimamizi wa Muitalia, Germano Frioni.

Akitoa salamu zake Muitalia huyo amesema kwamba anawashukuru wakazi wa Vikawe kwa kumpa nguvu ya kusonga mbele hasa kwa kutambua kwamba yeye na marafiki zake wamefanyakazi usiku na mchana kutafuta fedha kwa ajili ya kusaidia marafiki wa Afrika.

Alisema atajitahidi kufanya kila linalowezekana kuhakikisha changamoto za zahanati hiyo zinafanyiwa kazi.

Aliwaomba wananchi wa Tanzania kuendelea kumuombea yeye na wenzake kama Papa Francis anavyoagiza ili malengo ya safari ya kuwapo duniani yafanikiwe.

Alisema kwamba watoto wake Daniel na Marco (kwa sasa wote ni marehemu) ambao ndio kifupi cha zahanati hiyo DA.MA wamemfanya kujitambua na kusaidia wengine katika kuonesha upendo.

Aidha alisema kwamba ataendelea kukumbuka Vikawe kwani alifika mara ya kwanza mwaka 2005 na kuona hali ilivyokuwa ambapo sasa lipo jengo la zahanati hiyo likiwa limekamilika.

Wazo la ujenzi wa zahanati hiyo , lilitolewa na wananchi wa Vikawe kwa Masisita Waabuduo Damu ya Kristo mwaka 2004 wakati wakiwa katika eneo hilo baada ya kununua ekari 40 kwa ajili ya kilimo mwaka 1994.

Alisema pamoja na maombi hayo na wao wenyewe kutambua kwamba kuna mahitaji makubwa ya huduma ya afya japokuwa kuna zahanati ya serikali, hawakuweza kutekeleza maombi ya wanavijiji hadi mwaka 2011 walipofanikiwa kupata ufadhili kutoka Italia na kuanza ujenzi mwaka 2013.

Katika risala yao walisema kwa ushirikiano kati yao na wafadhili hao wamefanikiwa kuwapo kwa zahanati hiyo yenye mahitaji yote ya msingi kwa mujibu wa taratibu za serikali na kuzidi.

Msoma risala alisema kwamba wataendelea kupanua miundombinu mpaka zahanati hiyo ifikie ngazi ya cha afya na baadae hospitali.

Pamoja na ujenzi wa zahanati hiyo ya kisasa masisita hao wameanzisha shule ya awali kuwaandaa wanafunzi wa darasa la kwanza.

Wamesema kwamba wanaamini kwamba wataendelea kushirikiana na wananchi na wadau wengine wa afya katika kuimarisha huduma za hospitali hiyo.

Zahanati hiyo pamoja na vifaa tiba pia ina raslimali ya visima vya maji ya mvua ujazo zenye ujazo wa lita laki moja na kingine lita 49 elfu, wanatumia umeme wa sola na jenereta .

Walisema kwamba wanachangamoto ya kukosa umeme wa Tanesco, barabara nzuri na nyumba za wafanyakazi.


Mwenyekiti wa kijiji cha Vikawe, Kibaha, Shabaan Mgini akiwasalimia wageni waalikwa wakati wa utambulisho.


Sr. Theresia Rogatus akisoma risala katika hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa DMD iliyopo Vikawe, Kibaha.


Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dk. Happiness Ndosi akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa -DMD kijiji cha Vikawe, Kibaha. Kutoka kushoto ni Mdau wa Zahanati hiyo, Dr. Zuberi Mzige wa Hospitali ya Mwananyamala,


Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dk Ndosi akimpa mkono wa shukrani Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Raia wa Italia, Germano Frioni kwa ujenzi wa Zahanati hiyo itakayohudumia wakazi wa kijiji cha Vikawe, Kibaha.


Masista Waabuduo Damu ya Kristo wakielekea meza kuu kwa mwendo wa madaha huku wakiwa wamebeba zawadi kwa ajili ya kumkabidhi mgeni rasmi na wafadhili waliojitolea kujenga Zahanati hiyo.


Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dk Ndosi (kulia) akimkabidhi zawadi Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Raia wa Italia, Germano Frioni. Anaye shuhudia tukio hilo ni Baba Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Kalmeri Bunju...


Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dk Ndosi akikabidhi zawadi kwa wadau waliombatana na Mfadhili aliyejitolea kujenga Zahanati hiyo Muitalia, Germano Frioni.
Mganga Mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dk Ndosi (wa pili kulia) pamoja na Mfadhili wa ujenzi wa Zahanati ya Da.Ma Africa ya kijiji cha Vikawe, Kibaha, Muitalia, Germano Frioni wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Zahanati hiyo inayosimamiwa na Masista Waabuduo Damu ya Kristo nchini.


Muonekano wa ndani ya Zahanati ya Da. Ma Africa-DMD iliyop Vikawe, Kibaha mkoa wa Pwani.


Mganga Mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha, Dk Ndosi akiangalia chumba cha dawa katika Zahanati hiyo mara baada ya kuzinduliwa.


Wageni waalikwa wakijadiliana jambo mara baada ya kufungiliwa rasmi Zahanati hiyo nje ya moja ya chumba cha upasuaji mdogo.


Baba Paroko wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Kalmeri Bunju akiendesha ibada takatifu ya misa maalum kabla ya ufunguzi rasmi wa Zahanati hiyo.
Wanakijiji wa Vikawe wakishiriki ibada maalum wakati wa uzinduzi wa Zahanati ya Da. Ma Africa.


Kwaya ikitoa burudani.


Wageni waalikwa na wanakijiji wakishiriki kuimba pamoja na kwaya.


Pichani juu na chini ni baadhi ya wanakijiji na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.


Umati wa wageni waalikwa na wanakijiji wa Vikawe.


Mgeni rasmi Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, Dr. Happiness Ndosi katika picha ya pamoja na wadau pamoja na wafadhili waliojenga Zahanati hiyo.


Masista Waabuduo Damu ya Kristo wakifurahia taswira za picha za mnato kutoka kwenye kamera.


Jenereta la Zahanati ya Da.Ma Africa linalotumika kutoa umeme katika Zahanati hiyo.


Muonekano wa nje wa jengo la Zahanati ya Da.Ma Africa kabla ya kuzinduliwa rasmi.


Wanakijiji wa Vikawe na wageni waalikwa wakiingia kukagua Zahanati hiyo mara baada ya kuzinduliwa.

Uzinduzi wa filamu ya "AISHA" Pangani


Filamu iliyopewa jina la AISHA imezunduliwa rasmi siku ijumaa ya tarehe 31/7/2015 wilayani Pangani chini ya shirika lisilo la kiserikali la UZIKWASA.

Aisha ni filamu ya tatu katika mfululizo wa filamu za UZIKWASA zikiangazia aina mbali mbali za unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike. Filamu hizi ni ni sehemu mojawapo tu ya njia za mawasiliano katika kampeni shirikishi-jamii ya mabadiliko ya tabia inayofahamika kama 'BANJA BASI'!, Pangani, Tanga.

Kabla ya filamu ya Aisha iliyozinduliwa kwa kishindo hivi karibuni, shirika la UZIKWASA tayari limeshatengeneza filamu nyenigne mbili ambazo ni FIMBO YA BABA na CHUKUA PIPI, wengi wa waigizaji waliomo ni wasanii wa vijijini.

Pia filamu hizi zinatokana na maisha halisi na utafiti wa kina katika jamii. Kwa nji hii UZIKWASA inahakikisha filamu zake zinaeleweka na zinafanya kazi kama kioo wka jamii. Lengo ni tuone, tuguswe na hatimaye tuchukue hatua ili kuleta mabadiliko.

Filamu ya AISHA inamhusu mwanamke anayeishi mjini na kuamua kurudi kijijini kwao kuhudhuria harusi ya mdogo wake. Wakati anajikumbusha maisha yake ya zamani, na kukutana na familia yake pamoja na marafiki, kunatokea mkasa wenye athari kubwa katika maisha yake.

Watu wangefumbia macho mkasa huo, lakini Aisha anaamua kupambana nao vikali ili kupata haki yake.

Filamu hii inahusu unyanyaa, aibu na wahanga kulaumiwa, na namna gani inazuia wanawake na wasichana kusema wazi. Pia inahusu baadhi ya mamlaka na viongozi kusita kufatilia ukiukaji wa haki za binadamu.

AISHA imeongozwa na mtaalamu maarufu Chande Omar, imetayarishwa kwa ushirikiano na Kijiweni Production, imefadhiliwa na A. Schindler na Swiss Development Cooperation (SDC) na kusimamiwa na shirika la UZIKWASA.

Filamu ya aisha ni kwa heshima ya wanawake wote waliopitia mikasa ya namna hii.


Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Regina Chonjo ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, nae alipata nafasi ya kutoa hotuba yake.


Producer wa filamu ya Aisha Bwana Emil Shivji akizungumza na wananchi waliohudhuria viwanja vya Bomani.


Mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA Dokta Vera Piroth akitoa hotuba yake ya kipeke ambayo ilikuwa katika mtindo wa hadithi pamoja na maswali, Ilipendeza sana.


Shamra shamra za ngongoti zikikaribisha wageni waalikwa kwenye uwanja wa Bomani wilayani Pangani palipofanyika uzinduzi wa flamu ya Aisha.


Msanii maafuru wa mashairi Ndugu Mabwingo akitoa burudani jukwaani.


Wananchi wakiendelea kufatilia uzinduzi wa filamu ya Aisha.


Msanii mahiri katika uimbaji, Vitalis Maembe alikuwepo kwenye uzinduzi wa filamu ya Aisha, alitoa burudani ya kipekee.


Wasanii waliocheza filamu ya Aisha wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakipokea zawadi zao za ushiriki.


Washereheshaji katika uzinduzi wa filamu ya Aisha, Mohammed Hammie maarufu kama Anko Mo (kati kati), Nickson Lutenda aliyevaa koti la bluu pamoja na Pili Mlindwa.


Mkurugenzi wa shirika la UZIKWASA akiteta jambo na mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Regina Chonjo.


Msanii Godliver Gordian ambaye amecheza kama Aisha katika filamu hiyo, akifanya mahojino na kituo cha luninga cha TBC ambao walikuwepo katika uzinduzi huo.


Msanii Vitalis Maembe akiwa na Godliver Gordian (Aisha), wakati wa utambulisha wa wimbo uliotumika kama soundtrack katika filamu hiyo.


Godliver Gordian ama Aisha akiwa na mshumaa mara baada ya wananchi kuitazama filamu ya AISHA- lengo la mshumaa huo ni kumulika unyanyapaa, pamoja na aibu wanayoipata wanawake na wasichana wanapotendewa matendo maovu.


Wageni waalikuwa wakiongoza na mkuu wa wilaya Pangani Bi Regina Chonjo nao waliwasha mishumaa katika kumuunga mkono Aisha katika harakati za kufichua maovu.


Wananchi wengine pia waliwasha mishumaa kuashiria kuunga mkono harakati hizo.