Mtikila aandaa makabrasha ya kumburuza Lowasa, Magufuli kortini


MWENYEKITI wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, amesema chama chake kinaandaa taratibu za kwenda

mahakamani ili kumshtaki mgombea urais mteule wa CCM, Dkt. John Magufuli na mgombea urais wa CHADEMA, Bw. Edward Lowassa.

Alisema wagombea hao kwa nyakati tofauti, wameshiriki kuiingizia Serikali hasara ya mabilioni ya fedha ambapo wanasheria wa chama hicho wapo katika hatua za mwisho ili wafunguliwe mashtaka mahakamani.

Mchungaji Mtikila aliyasema hayo Dar es Salaam jana, alipozungumza na waandishi wa habari akisisitiza kuwa, wagombea hao wamepoteza sifa za kuwania nafasi hiyo akidai hawana vigezo kwa mujibu wa sheria.

Aliongeza kuwa, Bw. Lowassa, anahusishwa na sakata la kampuni ya kufua umeme ya Richmond na kuishangaa CHADEMA akidai chama hicho kilipata umaarufu wa kupinga vitendo vya ufisadi lakini wamempokea Bw. Lowassa na ana tuhuma kama hiyo.

"Kipindi cha nyuma, CHADEMA walianzisha operesheni nyingi ikiwemo ya Sangara na Movement for Change zikiwa na lengo la kupinga ufisadi, kwanini wamempokea Lowassa waliyemuita fisadi.
"Hii ina maana kuwa, ndani ya CHADEMA hakuna siasa, nawapongeza baadhi ya viongozi wa chama hicho na wanachama wao ambao kimsingi hawakubaliani na matakwa ya viongozi wa juu," 
Akimzungumzia Dkt. Magufuli, alimhusisha na tuhuma ya uuzwaji wa nyumba za Serikali akidai kitendo hicho kimeisababishia hasara Serikali lakini hakupelekwa mahakamani kwa kutumia madaraka yake vibaya kama ilivyokuwa kwa Basil Mramba, Daniel Yona ambao hivi sasa wanatumikia kifungo gerezani.

Alisema nyumba hizo zilikuwa makazi ya viongozi kama Majaji, Makatibu Wakuu na Watendaji waandamizi serikalini ambao wengi wao walilazimika kuishi hotelini kwa gharama za Serikali.
  • Imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la MAJIRA

Makongoro M. Mahanga "usituzeveze" - Katabazi

AGOSTI Mosi Mwaka huu ,Chama Cha Mapinduzi (CCM), kiliendesha kura za maoni kwa wagombea wake kwa ngazi za Ubunge na Udiwani kote nchini.

Kwa tuliofutilia harakati za kupatikana kwa wagombea hao kwa zaidi ya miezi mitatu sasa katika baadhi ya maeneo hapa nchini tumelishuhudia matumizi ya fedha kwa baadhi ya wapambe wa wagombea kuandaa mikutano ya wapiga kura wa CCM katika Matawi,Kata ambao walikuwa na Kadi za CCM.

Wiki iliyopita mimi mibanfsi nilikuwa nikishinda mitaani ,kwenye vijiwe,kuzungumza na baadhi ya wanaume na wanawake ambao wengine ni wake za watu ambao ilipokuwa ikifika saa nane mchana kutwa kiguu na njia kwenda kwenye vikao vilivyokuwa vinaandaliwa na wapambe wa wagombea na wanawake hao walikuwa wakienda haraka haraka kwenye vikao hivyo vya kukutanishwa na baadhi ya wagombea kwasababu mwisho wa vikao hivyo walikuwa wakihongwa Sh.5,000,10,0000 na Sh.3,000.

Tumesikia Madai ya tuhuma za Rushwa na uhuni wa kila aina Katika mchakato huo wa kura za maoni ndani ya CCM.

Baada ya baadhi ya wagombea walioshinda Katika kura za maoni wametuhumiwa na wapambe wa kambi za wagombea wenzao Kuwa wametumia Rushwa na figisufigisu.

Lakini hata Hao walioshindwa Katika kura hizo za maoni ambao wapambe wao wanalalamika Kuwa washindi walitumia Rushwa,nao pia walitumia Rushwa Katika kampeni zao kwa kuwahonga baadhi ya Wapiga kura,wajumbe wa nyumba Kumi ,mawakala wao na baadhi ya viongozi wa CCM ili wamsaidie washinde ila tu Fedha zao zimeliwa na ushindi hawajapata.

Naomba vikao Vya juu Vya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete na Timu yake vichunguze vizuri wale wote walioshinda kura za maoni Kama walishinda kwa njia chafu basi wahenguliwe.

Maana siyo Siri uchafu na matumizi ya Rushwa Kabla na wakati wa uchaguzi huo yalitawala katika baadhi ya majimbo na Kata vitendo ambavyo vimethibitisha Kuwa ni Ngumu sana kupata madaraka ndani ya CCM bila kumwaga Fedha na kufanya ghiriba maana Takukuru nikama walikuwa mbingu nyingine.

Turejee Katika mada Kuu ambayo ni Agosti Mosi Mwaka huu,
aliyekuwa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea kwa vipindi viwili mfululizo tangu mwaka 2000-2010 ambaye ni Naibu Waziri wa Wizara ya Kazi na Ajira, Dk.Makongoro Mahanga kwa tiketi ya CCM, alishindwa katika kura za maoni .

Agosti 2 Mwaka huu, yaani Jana Dk.Mahanga aliitisha mkutano wake na waandishi wa Habari na kutoa shutuma kuwa uchaguzi ulitawaliwa na Rushwa, hira, mizengwe na kwamba Kabla ya uchaguzi huo kufanyika Juzi .

Mara kwa Mara alikuwa akilalamika Kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Ilala Kuwa kuna baadhi ya wagombea wenzake wa Ubunge wanavunja Kanuni za chama lakini uongozi wa CCM Wilaya ya Ilala ulimpuuza.

Na kwasababu hiyo ametangaza rasmi kuhama CCM anakwenda zake kujiunga na Chadema.

Kwa mujibu wa Ibara ya 20 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, inatoa Haki ya Mtanzania yoyote kujiunga na Chama chochote cha siasa.Hivyo Kwenda kwako Chadema wala ujafuvunja Sheria za nchi.

Siyo Siri baada ya kumsikia Dk.Makongoro Kwenye Redio na kumshuhudia Kwenye Televisheni akizungumza maneno hayo na uamuzi huo, niliishia Kusema kweli 'Mungu wa siku hizi ni kijana analipa hapa hapa Duniani' na Kwamba Muosha uwoshwa tena wakati wa kuoshwa ulipuliwa.

Leo Dk.Mahanga analalamika Rushwa hira zimesababisha ashindwe?.Lini we Makongoro na wewe na genge Lako mliacha kucheza Michezo hiyo unayowatuhumu wenzio wamejifanya ?

Mahanga huyu huyu ninae mfahamu Mimi anadiriki Kusema hayo?Nimecheka sana.Kweli Dk.Mahanga safari hii umempata Kiboko yako mwanamke wa Shoka Bonna Kalua ambae amekuangusha Katika kura za maoni nafasi ya Ubunge.Kalua umetoa kamasi Makongoro hadi ameamua CCM ,safi sana Kalua ,wanawake tunaweza Kuwa wabunge majimboni sio siku zote Kuwa wabunge wa viti Maalum.

Minamuuliza huyu Bwana Makongoro huo ujasiri wa kukemea figisufisu na Rushwa Katika uchaguzi Katika Jimbo la Segerea ameupata wapi?

Ina maana ujasiri huu wa kuona Rushwa ,figisufigisu Katika uchaguzi CCM, Dk.Mahanga ameupata baada ya kubwagwa na aliyekuwa mgombea mwenzake ambaye ni binti Mdogo Juzi?

Kweli Mtenda akitendewa uisi kaonewa na Yale yote aliyoyatenda uwa yanamrudia alijiimbiaga Mwanamuziki Ally Choki.

We Dk.Makongoro Mahanga kweli Leo hii unapata ujasiri wa kutoa malalamiko hayo tena hadharani Wewe Huyo?

Minimuulize Mtani wangu Dk.Mahanga Ina maana wewe na genge Lako lililokuwa likikupigia kampeni hamkutoa hata Sh.100 kwa Wapiga kura ili kuwashawishi wakipigie kura za ndiyo?

Maana wakati mwingine Nyie wanasiasa muwe mnamuogopa Mungu na muwe wa kweli. Sema Dk. Makongoro Kama kweli hukutoa hata senti Moja kwa baadhi ya Wapiga kura ili wakuchague?

Minakufahamu vizuri sana na wewe tangu Enzi zile nakuja kuandika Habari za jimbo Lako na waandishi wenzangu ambao hivi sasa ni marehemu Jackline Mwingira(Nipashe), Agnes Yamo ( Tanzania Damia) na Veronica Charles ( Majira).

Au Katika uchaguzi wa kura za maoni Mwaka 2015 ulishampokea Bwana Yesu ,umeokoka unampenda Yesu hivyo Figisufisu 'ghiriba' za uchaguzi wewe na kambi yako hamkuzifanya Mwaka huu?

Lakini Mtani wangu wakati wewe ukiwatuhumu waliokushinda na mchakato huo Kuwa ulighubikwa na Rushwa, pia kuna Wapiga kura wa jimbo la Segerea baadhi Yao na wanakutuhumu Kuwa nawewe na kambi yako mlishiriki kucheza Michezo hiyo haramu ' Figisufisu' Katika uchaguzi huo uliomalizika Juzi.

Ila tu uchaguzi 2010 , wana CCM Jimbo la Segerea wamekuchoka waliamua kutafuna Fedha zako kwa makusudi na Kisha KUIBWAGA na kweli wamekubwagwa kama zigo hadi umeonekana kukumbwa na kiwewe?

Watu wamechoka za Fedha zako sasa uende nazo uko Chadema,na Chadema wameishafanya uchaguzi wa kura za maoni za Ubunge na Udiwani, sasa sijui utaweza kuvumilia Kuwa Mwanachadema wakati Huna Cheo cha Ubunge wala Udiwani?

Maana siyo Siri kilichokuamisha CCM ni baada ya kushindwa Katika kura za maoni ya Ubunge yaani ni kukosa madaraka ndani ya CCM ndiko kulikosababisha uame CCM .

Sasa ndiyo Sultani wenu Mkuu mnayemfuata huko Chadema ambaye aliamia Chadema kwa kishindo Jumanne iliyopita kwa kile alichodai aliamua kuhama CCM baada ya jina lake kuenguliwa Katika Hatua za awali za mchakato wa kumpata mgombea Urais CCM.

Sasa Kama Chanzo cha kuhama CCM ni baada ya wewe kushindwa kura za maoni Jimbo la Segerea, umeamua kuhamia Chadema, sasa kwakuwa wewe mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa mmeonyesha Kuwa Shida yenu Kuu ni Kupata madaraka tu .

Ikitokea Chadema wakakunyima madaraka siutaihama Chadema kwa Kigezo Kuwa hawajakupa madaraka?

Tamaa na Kupenda madaraka itakuja kuwadhuru siku Moja.Yaani mjue mnawashangaza sana watu wanaofikiri sawa sawa.

Dk.Mahanga ,waziri mzima umekaa Katika baraza la Mawaziri Katika serikali ya awamu ya nne yote Kama Niabu Waziri eti umeshindwa kura za maoni basi bila haya wala hujui vibaya unasema Rushwa ilitawala Katika uchaguzi na kwamba unahama CCM. Unamdanganya nani na unamkomoa nani?

Mimi nimekuwa nikikufuatilia nyendo zako muda mrefu kisiasa wewe Makongoro ulikuwa Team Lowassa na siyo dhambi.Na ni mbunge ambaye Wapiga Kuwa wa Jimbo la Segerea walikuwa wameishakukinai na Ndio maana wamekubwaga.

Mpango wenu wa kitoto wa kuhama CCM Kama aliyekuwa mgombea wenu wa urais jina lake lisipopitishwa na CCM Kuwa mgombea urais, ule hajulikani NA watu wenye akili timamu .

Watu wakawa wanawatazama nakuwaacha mjazane Ujinga, matumaini makubwa ya kupeana madaraka na mtekeketeze fedha zenu sasa mgombea wenu alipokatwa jina na vikao Vya juu vya CCM Dodoma ndiyo kambi yenu mkaanza kupata wazimu Msijue pakukamata maana mkijiamini sana na Fedha nyingi mkateketeza na mlilolitaka hamkulipata.

Sisi wajuzi wa mambo ulipotangaza Jana unahama CCM ,tuliishia kucheka na kukuonea huruma tu Manaa Miaka yote mlivyoenda Timu Lowassa mlifikiri mmejificha Kwenye Giza Kumbe mlijificha Kwenye Mawingu mnaonekana,watu wana Wachora wanajua wanawakona wapi.Na ndiyo basi Mtani wangu Ubunge na unaibu waziri umeutema.

Waswahili wanamsemo wao usemao " Aliyejamba atakunya tu". Siku zote ulijidai ni CCM Damu na upo na CCM Katika Shida na raha lakini Juzi baada ya kushindwa Katika kura za maoni ( Ndio wakati wa Shida), umeamua kuitosa CCM na kwenda Chadema mchana kweupe .Balaa.

Licha ni Haki yako ya Kikatiba kuamia Chama chochote unachotaka.
lla Mimi Kama Mtani wako nakwambia hivi uamuzi wako wa kuamia Chadema hautakuwa na faida kwako zaidi ya Majuto muda Si mrefu,tusubiri Tuone na hili litatokea usije kulia na Mtu.

Leo Dk.Mahanga Unaiona Chadema ni nzuri na umeamua kujiunga nayo wakati mi nakumbuka ni hawa hawa Chadema ndiyo walikuwa wakikutukana matusi usiku kucha Katika mitandao na magazeti Kuwa wewe ni "Fisadi wa Elimu" , umeghushi Vyeti Vya elimu .

Na kwamba Katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010 hukushinda, ulimuibia kura aliyekuwa Mgombea Ubunge (Fredy Mpendazoe)?

Na kila ulipopita walikuwa wanakuchafua hasa na hadi siku ile Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara,Dar Es Salaam,ulioposhinda Kesi ya kupinga Bunge wako iliyokuwa imefunguliwa na Mpendazoe dhidi yako na wenzako?Kesi ya kupinga Ubunge wako na zile Kesi zote za kudhalilishwa na Kaineruba.

Lini Chadema wamekusafisha wewe? Mtani wangu Mahanga sio kila siku lazima uwe Mbunge ,Naibu waziri.

Siku nyingine Unatakiwa uwe Mwananchi wa kawaida na wewe watu wakuongoze.Mahanga acha kutuzeveza.

Tamaa ya madaraka itakuja kuwawaisha Kuzimu maana unaweza kujikuta unaanguka ghafla na kufariki kwa BP baada ya kupata taarifa umeshindwa Katika uchaguzi uliokuwa ukigombea.

Nakushauri wewe na wenzio ambao ni wazi mna onyesha mnapenda sana kupata madaraka nendeni katika makanisa ya Kiroho mkakemewe hili hiyo roho ya Kupenda madaraka iwatoke.

Maana hiyo roho ya Kupenda madaraka inawasumbua ,kuwatesa na kuwadhalilisha sana .Na Kwa Mungu hakuna linashindikana.

Mtani wangu Hupaswi Kulalamika Katika uchaguzi huu ulioshindwa eti uligubikwa
Na figisufigisu, inakupasa ukae chini ujiulize ni kwanini hizo figisufigisu unazodai zilikuwepo zikasababisha ushindwe ni kwanini zimetokea na ni kwanini wewe kambi yako na mawakala wako ,mamlaka husika mlishindwa kuthibiti figisufigisu hizo unazodai zilishamiri?

Uoni figisufigisu hizo ni malipo kwako kutokana na figisufigisu ulizotuhumiwa kumfanyia aliyekuwa mgombea Ubunge (Chadema) Mwaka 2010 ?

Watoto wa mjini tunasema " Malipo ni Dunia akhera kuhesabiwa usijigeuze nyani kucheka uliyoumbiwa". Sasa basi figisufigisu zilizokupaa Katika kura za maoni CCM Juzi ni malipo ya figisufigisu zile.

Minawashauri watu walionizidi umri,na viongozi wetu Nyie msipende kuchukua maamuzi wakati mnahasira na machungu moyoni Kwani mwisho wa siku mtajikuta mnajutia maamuzi hayo mliyoyachukua wakati mnahasira na uchungu moyoni.

Mtani wangu Mahanga Nakutakia kila lakheri katika makazi mapya ya siasa huko ulikosema anaenda kuamia Chadema, Mungu akutangulie.Ila tabia ya kuama Chama na kutoa kashfa dhidi ya CCM baada ya kushindwa kura za maoni uache haitokufikisha Kokote Kwani hata huko uendako Kama kuna viongozi wenye akili timamu na wenye busara wana Haki ya kukataa usijiunge na Chama chao kwasababu kupitia maelezo yako ni wazi unaamia Chadema siyo kwasababu unaipenda Chadema kutoka moyoni.

Unahama Chadema baada ya kushindwa Katika kura za maoni za Ubunge CCM Juzi, na Jana ukatangaza unahama CCM unaenda Chadema.

Hivi nikikuuliza wewe Dk.Mahanga lini ulijipa muda ukaisoma Katiba ya Chadema na Kanuni zake ukazielewa vyema na zikakuvutia ndani ya saa 24 ukaamua kujiunga na Chadema?

Chadema muwe makini sana na hili Wimbo la makada wa CCM waliokosa fursa za uongozi ndani ya CCM wanaamua kujiunga na Chadema.

Kuweni nao makini sana, Wengi wao wana uchu na tamaa ya madaraka na viongozi wa aina hii mnavyozidi kuwakaribisha misiwakatazi msiwakatibishe ila Mkae mkijua hipo siku watawasumbua.

Mwenye Kilema abadili Mwendo. Lowassa,Dk.Mahanga tayari wameisha jidhihirisha ni aina ya binadamu wanaopenda madaraka kupita kiasi.Hivyo licha wamekuja Chadema Lowassa mmempa nafasi Adimu ya Kuwa mgombea urais ambayo nafasi hiyo Ina malizika Oktoba 25 Mwaka huu .

Fedha na mali wanazo lakini wanachokisaka kwa kwa udi na uvumba ni madaraka.Watu wenye akili timamu na tunaofikiri sawa sawa tu nawaogopa sana sana.

Mimi binafsi naamini Lowassa hawezi Kuwa rais kupitia Chadema.Huo ndiyo ukweli mchungu nafahamu itawakera sana Chadema na baadhi ya watu wa Kanda ya Kaskazini ambao huku mitaani hivi sasa wanasema wanaeneza siasa za ukanda wa Kaskazini lakini vumilieni.

Swali Je, Cheo hicho cha ugombea urais wa Chadema ambacho anacho Lowassa kwa sasa kikimalizika Oktoba 25 Mwaka huu.

Je Mzee wangu Lowassa atavumulia kuishi Chadema bila kupewa Cheo chochote kikubwa ?

Kweli nimeamini wanasiasa Wengi ni walafi wa madaraka,hawajui kukosa ,wanajua kupata tu siku zote. CCM Kwao uwa ni nzuri pale inapowapa madaraka lakini CCM hiyo ugeuka Kuwa Mbaya Kwao pindi anapokosa madaraka au Kama wanapoona kuna Dalili za kushindwa Katika uchaguzi wa CCM.

Ndiyo Lowassa na Mahanga,Ester Bulaya, James Lembeli CCM ni Mbaya kwasababu wamekosa madaraka ila Kipindi kile wana madaraka ndani ya CCM , walikuwa wakitamba majukwani kuwa CCM ni Chama bora na Hakuna Kama CCM na hawatahama CCM .

Mei Mwaka huu, Lowassa Katika mikutano yake na waandishi wa Habari ambayo imerekodiwa alijiapiza kuwa Katu hawezi kuhama CCM hata kidogo.

Miuwa nawasikitikiaga sana watu wa aina hii na kuwaombea kwa Mungu awatengeneze upya kiroho.

Itakumbukwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ,Julai 28 Mwaka huu, wakati akihutubia umma Katika mkutano wa kumkabidhi rasmi Kadi ya Chadema, Lowassa,pamoja na mambo mengine Mbowe alinukuliwa akisema Kuwa alitumia Miezi mitatu kufanya mawasiliano na Lowassa ya kumshawishi Lowassaa ajiunge na Chadema.

Wenye akili timamu tumeitafakari hiyo Kauli ya Mbowe Kuwa alitumia Miezi mitatu kufanyamawasiliano na Lowassa ajiunge na Chadema na kweli Chadema umefanyikiwa kumnasa mgombea Lowassa.

Julai 10 Mwaka huu, CCM ndiyo ilichuja Majina ya wagombea urais ikiwemo jina la Lowassa kwa kuyakata na kupata tano bora ambapo Lowassa akufika tano Bora.

Ndani ya Miezi hiyo mitatu aliyotueleza Mbowe, Lowassa alikuwa ni miongoni mwa wagombea urais kwa CCM na ni wazi CCM ilikuwa ikiwafuatilia nyendo za wagombea wake wote kwa karibu.

Ikiwa Hali ndiyo ilikuwa baina ya Lowassa aliyekuwa mgombea urais CCM alikuwa na mawasiliano Mwenyekiti wa Chadema ,Mbowe ili Lowassa aame CCM.Mnafikiri wanausalama wa CCM walikuwa hawajabaini Njama hiyo chafu ya Lowassa ya kusaliti CCM kwa Chadema?

Kama CCM walibaini mawasiliano hayo ya Lowassa na Mbowe ya kuhama CCM hatuoni nayo hiyo ni miongoni mwa Sababu uenda zilizotumiwa na Kikao CCM kumuhuengua Lowassa mapema Katika kinyang'anyiro cha ugombea urais CCM?

Minafananisha hiyo alilolisema Mbowe Kuwa alikuwa akimtongoza Lowassa ili aamie Chadema, ni sawa Mke wa Mtu Aliyepo ndani ya ndoa ila kwakuwa tu ni Malaya Akaamua Kuwa anasaliti ndoa yake kwa bwana mwingine.Maana huwezi Kuwa Mke wa Mtu au mume wa Mtu halafu ukaanza kutongozwa Mara kwa Mara na bwana mwingine ukakubari wakati ukijua una ndoa yako,ukifanya hivyo ukae ukijua jina unalostahili kupachikwa ni mwanamke au mwanaume Malaya.

Maana haiwezekani uwe mgombea urais CCM mwenye hadhi ya madaraka aliyowahi kushika Lowassa ambaye hadi sasa analindwa na walinzi waliokula kiapo cha kutii serikali iliyopo madarakani na Amir Jeshi Mkuu ,halafu uwe unafanya mipango ya kuhamia Chama cha upinzani halafu vyombo Vya Ulinzi na Usalama visibaini Usaliti huu.

Vilibaini Njama yake hiyo mapema vikawa vinamtazama kwasababu Tayari walikuwa wanajua wakati wanaoutaka wao utafika na watamtia adabu, na kweli adabu waliomshikisha kwa Kulikata jina lake mapema bila kuogopa Kuwa anaungwa mkono na baadhi ya watu.

Chadema Mnapaswa mjiulize Lowassa huyu ambaye ndiye mgombea wenu wa urais wa sasa Enzi zile alipokuwa mgombea wa CCM aliweza kurubuniwa na Mbowe ili aamie Chadema na kweli amerubunika baada ya CCM kuchinja jina lake Kahamia Chadema, hamuoni huyu mgombea wenu wa urais Lowassa akitokea Mtu mwingine amshawishi aihame Chadema anaweza kuhama?

Mungu Ibariki Tanzania

Happiness Katabazi
0716 774494
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook: Happy Katabazi
3/8/2015.

Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM Taifa, Mgana Msindai aonekana CHADEMA

Mgana Msinda
Mgana Msinda
Mwenyekiti wa wenyeviti ccm Taifa i na mwenyekiti wa mkoa wa singida Mhe Mgana Msinda ndani ya gwanda.
Mhe . Edward Lowassa, Laiguanani wa Malaigwanani Afrika Mashariki, ndani ya Baraza Kuu la CHADEMA TAIFA.
Hakuna kulala, mpaka walale wao!!


Picha na maandishi vimenukuliwa "as is" kutoka kwenye ukurasa wa Joshua Nassari

[video] Prof. Kitila Mkumbo 'anaswa' akielezea 'strategy' ya upinzani kumtaka Lowasa


[update] Matokeo ya kura za maoni CCM: Kigoma

WAGOMBEA wa Kura za Maoni kupitia CCM Jimbo la Kigoma Kusini walikuwa 13.

1.Hasna Mwilima kura 6,063

2.Eng: Salum Sasilo kura 5,501

3.Nashon Bidyanguze kura 3,867

4.Ali Kalufya kura 3,792

5.Manju Salum Msambya kura 3,233

6.Kifu Gulam Husein Shabani kura 2,410

7.Jumanne Husein Mhitila Kalimanzila kura 1,973

8.Norbet Nshemetse kura 1,843

9.Idd Ndabhona kura 1,397

10.January Kizito kura 1,331

11.Waziri Mourice kura 613

12.Dismas Malele kura 443

13.Thomas Sangai kura 79

------

ZOEZI la upigaji kura ya maoni ili kupata wagombea wa ubunge ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM, kwa majimbo ya Mkoa wa Kigoma umekamilika na yafuatayo ni matokeo ya majimbo matatu kati ya nane ambayo yemetolewa hii leo.

JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI WILAYA YA KIGOMA:

Peter Serujamba ameongoza kwa kupata kura 19,424, akifuatiwa Robinson Lembo kura 2,236, Omary Nkwalulo kura 1,291, Mahwago Kayandabila kura 1,268, Hamisi Betese kura 724, Halimenshi Kahena kura 261, Juma Matete kura 169, Robert Yohana kura 124, Ernest Rugiga kura 121, Emile Kamulenga kura 74 na Musa Mayeye kura 63.

Kulingana na Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma, Mobutu Malima, Kura zilizopigwa zilikuwa 26,904, kura zilizoharibika ni 1,149 na kura halali zilikuwa 25,755.

JIMBO LA KIGOMA MJINI:

Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma, Norbet Kibaji ametangaza matokeo ya Jimbo la Kigoma Mjini kuwa Dkt. Amani Warid Kabourou amepata kura 8,551, Zuberi Mabie kura 2,640, Elisha Zilikana kura 1,793 na Sospeter Kabangutse kura 978.

JIMBO LA MUHAMBWE WILAYA YA KIBONDO:

Katibu wa CCM Wilaya ya Kibondo ametangaza matokeo ya kura za maoni jimbo la Muhambwe ambapo Jamal Tamim kura 9,592, Emmanuel Gwegenyeza kura 2,910, Batashaka Julius kura 1,937, Edgar Mkosmali kura ,1,072, Richard Kigaraba kura 877, Anderson Kabuko kura 413, Moshi Mganga kura 361, Joseph Tutuba kura 304 na Regia Kayabu kura 148.

JIMBO LA BUYUNGU WILAYA YA KAKONKO:

Katibu wa CCM Wilaya ya Kakonko, Julius Mbwiga, ametangaza matokeo ya kura za maoni jimbo la Buyungu ambapo Christopher Chiza amepata kura 10,249, akifuatiwa na Nsakila Kabende kura 3,689, Modest Apolinary kura 848, Carlos Gwamagobe kura 426, Ernest Basaya kura 107 na Liberia Ndabita kura 89.

Matokeo ya jimbo majimbo ya Kigoma Kusini, Kasulu Vijijini, Kasulu Mjini na Manyovu bado hayajatangazwa.

Mbowe: Kamati Kuu CHADEMA imempumzisha Dk Slaa

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe (kulshoto) akiwa na Katibu Mkuu, Wilbrod Slaa

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimempumzisha Katibu Mkuu wake Dk. Wilbroad Slaa.

Aidha, wanachama wake wametakiwa kuacha kuwa hofu kutokana na ujio wa Lowassa kwa kuogopa kunyanganywa vyeo vyao na wafuasi wake.

Mbowe amesema,
“inawezekana Slaa naye anahofu juu ya ujio wa Lowassa kama ilivyo kwa wanachama wengine, wakidhani kuwa nafasi zao zitachukuliwa na wananchama wapya”. 
Hayo yanabainishwa leo Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho Freeman Mbowe alipokuwa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
“Katika hatua zote hizo tulikuwa sambamba na Slaa lakini baadae alibadilika ghafla na kutofautiana na Kamati kuu. Na mimi mwenyewe binafsi jana nimekaa nae zaidi ya masaa mawili nikijaribu kuongea nae lakini hatukufikia muafaka” 
amesema Mbowe.

Amesema maamuzi hayo ya kumpumzisha Slaa yameamuliwa na Kamati kuu ya Chadema baada ya kuwa katika mazungumzo ya muda mrefu bila kupata muafaka wa hatima ya ukimya wake.

Akizungumza na waandishi kabla ya kuanza Mkutano wa Baraza Kuu Chadema Mbowe amesisitiza kuwa Slaa alibadilika ghafla baada ya Kikao Cha Kamati Kuu.

Mbowe ameeleza kuwa, awali Chama kilikaa vikao vingi kujadili juu ya ujio wa Waziri mstaafu Edward Lowassa kujiunga na Chadema na kufikia makubaliano yaliyowahusisha viongozi wote wa Chama akiwemo Slaa.

Mbowe amesema, chama hakiwezi kusimama kufaya shughuli zake kikisubiri maamuzi ya mtu mmoja hivyo kitaendelea na kazi zake hususani katika kipindi hiki kigumu cha uchaguzi.

Mbali na hilo, amesema,
“Chama kipo tayari kumpokea wakati wowote atakapokuwa tayari kurudi katika nafasi yake na sisi bado tunampenda na kumheshimu kama kiongozi”
“Leo nimeamua kuweka wazi suala hili baada ya kusikia na kuona vyombo vya habari mbalimbali vikiripoti habari zisizo za kweli ya kwamba Slaa amejiuzu na kwamba Chama kimempora mali zake na kumtishia habari hizo sizakweli na wala chama hakina ugomvi nae”.
Amesema, wanachama hawatakiwi kuhofia chochote juu ya ujio wa Lowassa na wafuasi wake kwani Chadema ni chama cha wananchi kwa yoyote atakae hitaji kujiunga anakaribishwa.
“Lakini hofu hii haipo kwetu tu ipo hata kwao Chama cha mapinduzi (CCM) kwani hawajawahi kupata hofu na viboko kama hivi vya kuondokewa na wafuasi wengi tena kwa wakati mmoja kama mwaka huu”.
Amesema CCM hadi sasa bado hawajielewi kutokana na mapigo mengi yaliyowapata kutokana na kuondokewa na kada wao mkubwa, na wengine bado wanakuja na hii ndio furaha ya chadema ili kuweza kuimaliza CCM Oktoba Mwaka huu.
“Ni lazma tuitumie fursa hii tuliyoipata na hatuwezi kuiacha. Lengo letu ni kuwa na wafuasi wengi zaidi haswa kutoka CCM ili tuzidi kuwamaliza kabisa tumeshawapokea wengi na tutazidi kuwapata wengi zaidi”.
Akizungumzia mkutano mkuu utakaofanyika kesho katika ukumbi wa Mlimani city Dar, ambapo amesema utamtangaza rasmi mgombea urais kwa tiketi ya Chadema pamoja na kumtangaza mgombea mwenza wa chama hicho.
  • Imeandikwa na Anaandika Sarafina Lidwino via MwanaHALISI Online

Irene Uwoya ashinda kura dhidi ya Zahara M. Michuzi

Wagombea wakiwasalimia wajumbe wa mkutano maalumu leo mapema.
Leo hii mchana Zahara (binti ya mpiga picha na mwanablogu maarufu nchini anayeambatana na rais Kikwete katika ziara zake, Muhidin Issa Michuzi) alishindwa kupata kura za kutosha kumwezesha kushinda nafasi ya ubunge wa vijana kupitia tiketi ya CCM mkoa wa Tabora baada ya msanii wa filamu Bi Irene Uwoya kupata kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.

Zahara ambaye ni mhitimu wa shahada ya uchumi toka chuo kikuu cha UDOM aliyakubali matokeo hayo bila kinyongo na kusema "Napenda kuwashukuru wagombea wenzangu na wajumbe wote, pamoja na kura mlizonipigia hazikutosha leo lakini nitabaki na azma yangu ya kuwatumikia wana Tabora" wajumbe walimshangilia sana na kumpongeza kwa ukomavu wa kisiasa aliouonesha ambapo mwenzie Mariam Shamte alisusia na kuondoka ukumbini. Mariam alimteua nduguye Hapsa kumwakilisha ktk uhesabuji kura hizo ambazo yeye Mariam alipata kura 3. Hakuingia ukumbini katika usomwaji wa matokeo.

Awali mgeni rasmi wa mkutano huo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora Bw Hassan Wakasuvi aliwaeleza wajumbe kuwa Obama alizaliwa na baba raia wa Kenya na mama Mmarekani lakini leo hii anaiongoza Marekani, hivyo wasione ajabu kama pana mgombea asiyetokea Tabora kiasilia. Bila shaka alikuwa akimzungumzia Irene Uwoya ambaye kabla ya uchaguzi wakazi wengi wa Tabora walielekea kutomkubali kwa kusema kwa nini CCM ituletee mgombea toka Arusha, Moshi au Dar es Salaam, na kwa nini Irene asigombee Dar anapoishi au Kwao kaskazini? kwani Tabora hakuna vijana wenye uwezo wa kugombea?

Waliendelea kuhoji kuwa ni vipi Irene atayajua matatizo ya vijana wa Tabora ambao hawajui wala hana uelewa na mkoa huo? Lakini hayawi hayawi hatimaye yamekuwa kwa Irene ameibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho. Kama maneno ya Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Tabora yalifanya kazi kusababisha Irene Uwoya achaguliwe kwa kishindo mimi na wewe hatujui.

Irene Uwoya mcheza sinema maarufu nchini alishinda uchaguzi huo kwa kura 34 kati ya 39 zilizopigwa.

Mariam Shamte alishika nafasi ya pili kwa kupata kura 3

Zahara Muhidin Michuzi alishika nafasi ya 3 kwa kupata kura 2 katika kura 39 zilizopigwa.

Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo maalum.

Team Irene wakifuatilia mchakato

Matokeo ya kata 3 yaliyompa "kufuru" ya ushindi Prof. Msola yafutwa

Mbunge wa Kilolo anayemaliza muda wake Prof Peter Msolla (katikati) akiwa na wabunge wa zamani, Steven Mwabuma (kulia) ambae alikuwa mbunge wa kwanza wa jimbo la Kilolo na Venance Mwamoto aliyeongoza jimbo hilo mwaka 2000-2005
CHAMA Cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimefuta matokeo ya kata tatu za jimbo la Kilolo, matokeo yaliyokuwa yakimpa ushindi mkubwa mbunge anayemaliza muda wake, Prof Peter Msola na kuagiza uchaguzi huo kurudiwa kesho.

Matokeo hayo ambayo yamekataliwa na wagombea wote yanadaiwa kupachikwa katika vituo vya kata hizo tatu japo hata hivyo hayana uhalisia ukilinganisha na idadi ya wanachama wa maeneo husika.

Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Bw Hassan Mtenga alisema kuwa kutokana na dosari mbalimbali ambazo zilijitokeza katika kata hiyo ambazo ni Nyalumbu, Lugalo na Uhambingeto alisema kilichoonyeshwa ni matokeo hayo kuwa tofauti na matokeo halisi ambayo mawakala wa wagombea walikuwa nayo na katika kata hiyo makatibu matawi na kata wa CCM hahakuweza kupeleka matokeo kwa wakati kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi hadi alipoyafuata na kuona kasoro hiyo.

Katibu huyo alisema karatasi zilizoonyesha ushindi wa mgombea mmoja Prof Msola zilikuwa ni tofauti na karatasi halisi zilizotolewa na chama hivyo kutokana na utofauti huo wagombea wengine waliweza kugomea matokeo hayo.

Hata hivyo mgombea Francis Mkokwa alisema kuwa walishangazwa kuona ghafla mbunge Prof Msola akiongoza katika vituo vya kata hizo ambazo hata matokeo yake hayakusainiwa na mawakala wa wagombea wengine na ndizo kata ambazo matokeo yake yalikuwa na utata na wakati wa kampeni mbunge huyo alikuwa hakubaliki katika maeneo ya kata hizo .

Walisema kimsingi matokeo halali ya kata zaidi ya 21, Mwamoto ndiye alikuwa akiongoza kwa kura nyingi zaidi kuliko za mgombea mwingine yeyote, huku mbunge anayemaliza muda wake akimfukuza kwa mbali na ajabu kushangazwa kuona udanganyifu mkubwa katika kura hizo.

Bila kutaja matokeo hayo, alisema walitegemea matokeo ya jumla mshindi kuwa Mwamoto ila ilitaka kuwa tofauti kwa ambaye hakuongoza katika vituo kutaka kuongoza kwa matokeo ya jumla hivyo kulazimika kuchunguza matokeo hayo na kubaini wizi huo.

Aligundua kuwa, katika vituo idadi ya kura ni nyingi kuliko ile ya wanachama na wakazi wa eneo husika hata kama wana kijiji wote hadi watoto wa mwaka mmoja wangepiga kura bado kura zilikuwa nyingi kuliko wakazi wa eneo husika kuwa kosa walilolifanya ni kuongeza idadi ya kura za mbunge Prof Msola bila kufuta idadi ya kura za Mwamoto ama idadi ya wapiga kura ya jumla:
"Ukitazama idadi halisi ya wapiga kura ,kura zilizopigwa na kura zilizoharibika bado ni vitu viwili tofauti na kufananisha wizi huo ni sawa na wizi bila mahesabu ....lazima chama kuchukua hatua kali kwa katibu wa chama wilaya na wote waliohusika "
Mgombea huyo alisema mbali ya kuwa yeye ni mgombea bado kwa sasa wameamua kuungana kupinga wizi huo na kuona mshindi wa kweli anapatikana na sio udanganyifu huo ambao umefanyika.

Kwa upande wake,  mgombea Ashraf Chusi pia alisema katika kata hizo kumefanyika udanganyifu mkubwa na kuwa kuna mazingira ya rushwa yalifanyika usiku wa kuamkia siku ya kupiga kura kwa eneo hilo la mji wa Ilula lenye shida kubwa ya maji watu kupewa rushwa na huduma ya maji kwa kufungulia bomba za maji kwa kituo kimoja baada ya kingine na katika vituo hivyo inasemekana walikuwa wakigawa pia kanga na pesa na pale mbinu hiyo inapobainika walikuwa wakifunga maji kituo husika na kufungua kituo cha pili.

Bw Chusi alisema jambo hilo wanaomba vyombo husika kuweza kuchunguza zaidi ili kuwachukulia hatua wahusika na kuwa hana shaka hata kidogo kuwa mshindi wao katika mchakato alikuwa ni Mwamoto.

Mwenyekiti wa CCM kata ya Nyalumbu Bw Bruan Mbululo alisema kuwa kimsingi wao walikamilisha kazi yao kwa kwenda kukabidhi matokeo kwa katibu wa CCM wilaya ya Kilolo na kama kuna dalili za udanganyifu wao hawahusiki japo alisema katika kata yake Prof Msola alishinda ila hakumbuki ni kwa kura ngapi.

Kamanda wa taasisi ya kuzuia na kuopambana na rushwa mkoa wa Iringa, Yunis Mmari akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alisema kuwa wanaendelea kuchunguza mchakato huo wa kura za maoni katika kata hizo tatu za jimbo la Kilolo.
  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Francis Godwin/MatukiodaimaBlog

Tanzania kivutio katika Maonyesho ya Afrika Mashariki


Ufunguzi wa maandamano ya maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yajulikanayo kama JAMFEST yaliyoanza leo katika Viunga vya Ukumbi wa Kimataifa wa Kenyata uliopo jijini Nairobi Kenya.


Muongozaji wa bendi ya polisi nchini Kenya akiongoza maandamano ya Ufunguzi wa Maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo nchi zote za Afrika Mashariki zimeshiriki maonyesho hayo yanayoanza leo katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyata.


Msafara wa uzinduzi wa maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiwa unatoka katika viwanja vya Uhuru Park uliopo ndani ya jiji la Nairobi kuelekea katika Viunga vya Ukumbi wa Kimataifa wa Kenyata ambapo baadhi ya wakazi wa nchi mbalimbali kutoka Afrika Mashariki wakionyesha bidhaa zao.


Watanzania wakiwa na bendera ya nchi kabla ya maandamano kuanza Katika viwanja vya Uhuru Park jijini Nairobi


Watanzania wakiwa na furaha ya kushiriki maonyesho ya jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoanza kufanyika katika Viwanja vya KICC Nairobi Kenya.




Watanzania wakitoa burudani katika viwanja vya Uhuru Park kabla ya Maandamo ya Ufunguzi wa Maonyesho ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayoanza leo katika viwanja vya KICC Nairobi Kenya.



Tanzania Kwanza mengine baadae..


Wadau wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Mkutano wa Injili Washington DC, Agosti 14 -16



Kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries linapenda kuwaalika katika siku tatu za mkutano wa uamsho utakaofanyika jijini Washington DC, Marekani Agosti 14 -16, 2015.



Mtumishi wa Mungu Emmanuel Mgaya ama Masanja Mkandamizaji alipohudumu kwa waumini wa jiji la Washington DC na vitongoji vyake siku ya Jumapili 07/07/2013 katika kanisa la THE WAY OF THE CROSS GOSPEL MINISTRIES


AIF call for applications: IPA 2016


PRESS RELEASE



Africa’s most prestigious innovation Awards celebrates its 5 year milestone in catalysing the innovation spirit in Africa!

ZURICH, Switzerland, August 3, 2015-- Are you an African ground breaker? Can you innovate for positive change? Do you want to be part of the growing innovation movement in Africa? Does your innovation boast the “Made in Africa” brand?

If your answer is yes to the above, then you’re invited to participate in the Innovation Prize for Africa (IPA) 2016 competition. The IPA is an initiative of the African Innovation Foundation (AIF) that was established in 2011. It aims to mobilize African innovators and entrepreneurs by providing US$ 150 000 for market-oriented solutions that support African-led development. Through the IPA, the AIF acknowledges and encourages the endeavours of African innovators and entrepreneurs, and works to raise their profiles on the development agenda.  Each nominee also receives a voucher of US$ 5000 to further develop their innovations.

After successful IPA editions in Addis Ababa (2012), Cape Town (2013), Abuja (2014), and more recently in Skhirat, Morocco (2015) AIF today announced the launch of its 5th edition of the IPA competition: “It’s all about Made in Africa now, “ says Pauline Mujawamariya, IPA Director, who has been at the helm of the IPA program since its inaugural launch in 2011, launched in collaboration with the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) and endorsed by Ministers attending the Africa Union (AU)/ECA conference. “Our dream is to see this competition grow, and with it, strengthen Africa’s innovation ecosystem. IPA 2016 marks bold new steps towards mobilizing all innovation enablers to join hands and ensure that African innovations make it to the markets,” she said.

© Link: IPA2016 APPLY NOW VIDEO http://bit.ly/1IrOaS5

The IPA 2016 edition, dubbed “Made in Africa” is in harmony with the AIF mission that seeks to catalyse the innovation spirit in Africa, living up to its credo: by Africans, for Africa. Now in its fifth year, IPA is the most celebrated innovation event on the African calendar, bringing together the best of African ingenuity in the rigours of science and technology, environment and energy, agri-business, health and well-being, the manufacturing and service industry, as well as the ICT sector.
Now in its fifth year running and a cash investment sum of $820 000, the IPA program has engaged, inspired and transformed more than 3000 movers and shakers across the continent, supporting more than 35 star innovators in 49 countries. The IPA achievements are illustrated by the fact that its social media community https://www.facebook.com/InnovationPrizeforAfrica?ref=hl has grown rapidly in the last quarter by 100%, with over 14 000 followers, a total reach of 1.1 million people and a total engaged user rate of 32 000!

The target for IPA 2016 is to attract applications from all 54 countries in Africa and the highest participation of women and young people. Once again, the grand share prize of US$150 000 will be split between the most impressive winners that can convince the AIF team of expert judges why their innovation must win. AIF is looking for unique, cutting-edge innovations (US$100 000) that reflect positive social impact (US$25 000) and have the potential to be transformed into a sustainable, commercial success (US$25 000).

But beyond the prestigious cash prize, IPA 2016 is set to break further ground, opening up new opportunities for innovation enthusiasts across Africa.  All nominees will receive additional post-prize support to the value of US$5 000 to take their innovations to a higher level. Thanks to increasing interest and buy-in from the African innovation pool, AIF will introduce further post-prize opportunities for 10 young Africans and 10 women whose innovations are addressing pressing challenges in Africa. Other incentives include training and pitching opportunities, association with the AIF brand, and local, regional and international media coverage, as well as networking opportunities with potential investors.

Says Jean-Claude Bastos de Morais, AIF Founding Board Member: “I am very excited about the Made in Africa theme for the 5th edition of IPA. It is a powerful message that captures the spirit, ingenuity and sophistication of African innovation today. Africans are beginning to see the value and merit in investing in home-grown innovation, and we are fiercely proud of African-made products and solutions. For the IPA 2016, the AIF is calling for innovators across the continent to bring forward innovations that will feed the demand and supply needs of African markets, stimulate local enterprise, and put African innovation on the world map”. 

You too can join the movement to change the face of Africa by helping us to build a strong African innovation ecosystems! All you need to do is submit to IPA your “Made in Africa” innovation no later than 31 October 2015. Check out our application guidelines, criteria for selection, the selection process and time-frame, and information on submission of entries on the IPA website, at www.innovation.prizeforafrica.org now, and you’re well on your way to being identified, rewarded and recognised as a top African innovator.

IPA 2016 promises to be bigger and better with the first ever Innovation Forum and a design “Do-Tank” workshop to be hosted by AIF, boasting the latest and smartest innovation fusions with opportunities for enhancing innovation design by Africans, for Africa. An extra special line up will showcase IPA achievements, and honour past and current nominees and winners. In addition, this will be a unique opportunity to interact with leading African innovation champions and thought leaders, topped by first class entertainment. This all, supported by the launch of a dynamic online platform for investors, innovators and innovation enablers driving the innovation frontier in Africa!
See you at IPA 2016 in June next year, and keep watching our social media channels for more details as they emerge, including information on our next host country, date and venue. Stay tuned with the IPA action by reading our happening blog at innovationprizeforafrica.org/blog

For more information, contact:
Aulora Stally
African Innovation Foundation
Communications Manager    
Strehlgasse 4
8001 Zurich
Switzerland
E-mail: [email protected]africaninnovation.org
Phone: +41 79 834 9163
Skype: amberstally

Find us on:

The Internet:www.africaninnovation.org
Innovation Prize for Africa
Facebook 
facebook.com/InnovationPrizeforAfrica
facebook.com/AfricanInnovationFoundation
Twitter @AfrinnovFdn @IPAPrize

About us

African Innovation Foundation (AIF) works to increase the prosperity of Africans by catalyzing the innovation spirit in Africa.
Innovation Prize for Africa (IPA) is a landmark initiative of the AIF and mobilizes African innovators to invest in African-led solutions to ensure a sustainable, prosperous Africa.

Singida Kaskazini yarindima kwa ushindi wa Nyalandu

Lazaro Nyalandu na mkewe Faraja wakisherehekea ushindi mara baada ya matokeo kutangazwa

Mamia ya wakazi wa Singida Kaskazini wameingia mtaani kusherehekea ushindi wa mbunge anaetetea kiti hicho Lazaro Nyalandu ambaye amefanikiwa kuibuka kidedea katika kura za maoni zilizopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Nyalandu ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 15 amepata ushindi wa kishindo wa jumla ya kura 13,496, huku anaemfuatia akiwa na kura 5822 hivyo kupata nafasi ya kukiwakilisha Chama Cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25.
 
Lazaro Nyalandu akiwa katika maandamano ya kusherehekea ushindi yakiongozwa na madereva wa bodaboda
Mheshimiwa Nyalandu akipongezwa na wananchi mara baada ya kutangazwa mshindi wa kura za maoni