APTR-CDC fellowship program announces available position

APTR is pleased to offer recent health profession graduates an exciting opportunity to gain practical public health experience at the Centers for Disease Control and Prevention (CDC). Applications are currently being accepted for the 2016 APTR-CDC Public Health Fellowship Program.

Fellows gain leadership experience in public health practice and policy, access to state-of-the-art technology and national databases, and will train with leading experts in the field of preventive medicine and public health.

Available Position(s): Implementing Recommendations of the Advisory Committee on Integration of Immunization into Undergraduate Nursing Curriculum (ACIIUN)

Eligibility


1. Applicant must be either a U.S. Citizen, non-citizen national, or foreign national possessing a visa permitting permanent residence in the U.S. (Alien Registration or "Green Card"). Student visas and temporary work visas do not qualify.

2. Graduate-level academic background in nursing. You must complete all required graduate work by the fellowship start-date, including online courses or thesis work.

3. The fellowship program is designed to support the development of young professionals in the field of preventive medicine and population health. Candidates must be within 5 years of graduation.

4. There is no membership requirement to apply. If you are selected for the fellowship position then you must be either (1) a student or graduate of an institutional academic member program of APTR, or (2) be an individual member of APTR.

Deadline: September 18, 2015

More Information

APTR Training Programs
(202) 463-0550 ext. 137
toll-free (866) 520-APTR
[email protected]

source: www.aptrweb.org

Mama aliyevaa mavazi ya rangi manjano na kijani azomewa Kariakoo


Faida ya yoga - Sensei Fundi

Mwalimu wa Yoga wa kimataifa,Sensei Rumadha Fundi katika mazoezi tofauti ya sanaa ya Yoga, akielezea ni nini hasa maana ya kutafakari kwa njia ya sanaa ya Yoga.

Meditation & Mantra -- Mara nyingi neno "Meditation" au kutafakari huchanganywa na kufikiri ni kukaa kimya kufumba macho kiufanisi au kuwaza jambo fulani. Pia, wengine huchanganya hili neno na kuwa umekaa kimya na kujaribu kutofikiria lolote, ama pia kuivuta au kuisukuma akili yako na kutoku fikiria kitu cha iana yeyote ile muda wote wa kutafakari na kuamini kwamba hiyo ni “Meditation” au Tafakari. Kamwe, hamna hata moja ya mifano hii inaweza kuifikia maana yake halisi katika mfumo kisayansi na filosofia ya “Yogic”.

Kisayansi ya Yoga, “Meditation” inaitwa “Mtiririko wa akili”(Flow of the mind).” Kuiongoza akili au mawazo ya mtu kupia Meditation, inahitaji pointi au sehemu muhimu katika maungo yako unayo kuwa unatumia kama vile mfano wa mionzi ya akili kuirushia na kuelekeza katika sehemu moja tu. Hivyo kwa kutumia msaada wa sauti maalum itwayo “Mantra”, hiyo ndio chombo hutumika kupitia mkufunzi aliye hitimu Sanaa ya Yoga na kufundisha kutokana na mazingira tofauti kati ya tofauti za watu zilivyo.

Kama jinsi inavyoelezwa katika filosofia ya Yoga kwamba, akili ya mwana adam, kamwe haitulii, wakati wote ipo mbio na inatafuta cha kufikiri, hivyo basi huwa ni kazi ngumu sana kwa mtu hata kuanza tu somo la kwanza (First lesson), kwa mistuko ya mchanganyiko wa mawazo ya mwana adam. Hivyo huwa taabu sana kukusanya mawazo yako binafsi na kufanya meditation bila muongozo wa kiutaam.

Napenda kuongelea vitu vichache hapa. Kuna vitu, au pointi tano tofauti zilizo muhimu na utumika katika mbinu za kutafakari kwa jina la “Sense withdrawal”, ambayo huitajika ili uweze kushawishi akili yako na mawazo kwamba utaweza kutafakari bila vikwazo vya mawzo yoyote au kuwa na utata katika mfomo mzima wa kutafakari. Ufuatao ni muktasari tu wa jinsi gani wana-Yoga wana tafakari kwa masaa mengi bila mgongano au (interruption) kupitia njia hii:
  1. Asana (Mkao wa mazoezi ya Yoga): “Lotus posture” kukunja miguu. Faida zake; kuweza kumiliki viungo vya mwili wakati wa kutafakari. Ndipo jinsi unaweza kumiliki viungo vya mwili wako vinavyokuwezasha kuona vitu “Sensory organs”. Kufumba macho, kutokuona kinachoendelea nje ya upeo wa macho ili kuweza kuelekeza mionzi ya fikra zako (Focus) sehemu moja tu. Kukunja ulimi zidi ya dari ya mdomo “Roof of the mouth” (Palate) wako ili kuweza miliki hamu ya kuonja radha au haja ya chakula chochote kile (Control taste). Kukunja mikono na vidole kuweza kumiliki hamu ya kushika kitu (Control sense of touch). Kitu kisicho wezekana kukimiliki ni harufu (Sense of smell), na ndio maana “Meditation” hufanywa katika mazingira safi bila moshi wala harufu mbaya kuepuka mkatiko wa mtiririko wa mawazo waka wa kutafakari.

  2. Kutoka katika mazingira ya mzumguuko wako wa kila siku (Withdrawal from external world) “Bhuta Shuddhi”. Kujitoa kimawazo kiuwoga wa matatizo ya kila siku kimaisha, kuwa umetulia mwili wako wakati wa kutafakari (Relaxation).

  3. Kujitoa kimawazo katika mwili wako mwenyewe (Withdrawal from the body) “Asana Shuddhi”. Kutowaza lolote kuhusu mwili wako na hali yake nzima au kutokuambatanisha fikra zako katika maumbile ya mwili wako (Withdrawal from each parts of your body; concentrate in one singular point) “Ista Chakra”.

  4. Kujitoa kabisa kimawazo (Withdrawal from thoughts of interruption) “Citta Shuddhi”, hapa katika hatua hii, mraba wa akili unakuwa unaelea kimawazo sambamba katika anga za ulimwengu (Total suspension of mind in cosmic space; Consciousness)

  5. Mtiririko wa mawazo na Mantra (Flow of mind) “Dhyana” hii ndio njia nzima ya utaratibu wa kufanya Meditation, au kwa namna nyingine ni mwanzo wa Kutafakari (Process to start meditating). Hapa ndipo sasa mkufunzi wa taaluma ya Yoga anakuwa anarudia kimoyo moyo Mantra aliyoisoma, sasa hapa ndipo mwanzo wa kile tunaita “Tafakari”. (Meditation).
Zipo njia nyingi zaidi za kufanya “Meditation” au kutafakari ngazi ya juu zaidi kupitia njia ya pumzi au “Prana Yama”(Vital Breathing). Hivyo, huu hapa ni muktasari tu wa jinsi na namna gani tunaitafsiri “Meditation ” au kutafakari kupitia mafunzo ya Yoga. Hayo pia ni machache naona vizuri kushirikiana na kumulika mwanga kidogo kwa wale wasio fahamu nini hasa maana ya Meditation kupitia Sanaa yaYoga.


  • Imeandikwa na mkufunzi wa Sanaa ya Yoga, Rumadha Fundi, mwenye uzoefu mkubwa na diploma ya somo la Yoga toka “ College of Neo-humanists Studies, Gullringen, Vimmerby, Sweden, aliyopa mwaka 1986 na hatimae baadae mwaka 1987 kwenda Tiljala, Culcutta, India, na kupata shahada ya juu kabisa ya Yoga duniani ijulikanayo kwa jina la “Avadhuta”.

FFU Ughaibuni wafanya kweli Liga Summer Festival 2015


Liga, Latvia

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya, Ngoma Africa band maarufu kama
FFU ughaibuni ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki Alien juzi wikiendi walifanikiwa kuwadatisha washabiki wa muziki nchini Latvia katika maonyesho ya Summer Festival, yaliyofanyika Liga. 

Ikiwa na makao yake nchini Ujerumani ikiongozwa na mwanamuziki mahiri Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja, imejizolea umaarufu wa Kimataifa kwa kutumia mdundo wake wa "Bongo Dansi" uliochanganywa na rumba la kukata na shoka mdundo huo umefanikiwa kuwazoa na kuwadatisha akili washabiki wengi wa kimataifa.

Ngoma Africa Band kwa sasa wanatamba na single CD yao mpya 'La Mgambo" yenye mbili za kumuaga rais JK.
Unaweza kuwasikiliza kupitia reverbnation.com/ngomaafricaband au kuungana nao facebook.com/ngomaafricaband 

CCM jiandaeni kushangilia! Tumejiandaa; Uwezo tunao, Maarifa tunayo, Tutashinda - Kikwete

Rais Kikwete, akajiunga kucheza muziki wa TOT kabla ya kuwashusha jukwaani Dk. Magufuli na mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan

MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli ambaye aliambatana na mgombea mwenza, Samia Suluhu leo amechukua fomu ya kuwania nafasi hiyo katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Msafara wa Magufuli na Suluhu ulifika katika ofisi za NEC saa 5.43 asubuhi huku ukisindikizwa na makada wa chama hicho wakiwemo: Katibu Mkuu, Abrahaman Kinana, Katibu Mwenezi, Nape Nnauye, Waziri wa Katiba na Sheria, Asha Rose Migiro; Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiq.

Aidha, ulinzi uliimalishwa huku askari polisi waliokuwa na silaha za moto wakizunguka jirani na ofisi za NEC.

Baada ya kuwasili katika ofisi hizo, wagombea hao walitumia muda wa dakika 27 kukamilisha zoezi la kuchukua fomu kisha kurejea katika viwanja vya ofisi za CCM makao makuu Lumumba kuungana na Rais Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM aliyeongozana na mkewe Salma Kikwete, kuhutubia mamia ya wanachama wa chama hicho waliojitokeza kuwasindikiza wagombea kuchukua fomu.

Akizungumza baada ya kukaribishwa na Kinana, Rais Kikwete alinzakuzungumza huku akivirushia dongo vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kwamba wamechukua “makapi ya CCM” huku akisema, "Wale wanaodhani CCM ni ya mchezo watakiona cha mtema kuni."

Huku akiongeza kuwa watu wenye tama kupitiliza "Tumejiandaa vya kutosha na tutashinda. Uwezo tunao, maarifa tunayo, tutashinda. Tujipange kwa hoja za kuzungumzia uzuri wa CCM."

Kwa upande wake Magufuli amesema, “leo tumechukua fomu, tutaizungusha kuweza kupata wadhamini. Nimepokea kijiti hiki kwa mikono miwili. Mategemeo ya watanzania ninayajua. Uongozi wa awamu ya nne uliweka msingi mzuri. Nitaipeperusha vizuri CCM kwa maslahi ya watanzania wote bila kujali chama,” amesema Magufuli.“CCM jiandaeni kushangilia ushindi….Utawala bora upo, demokrasia ipo, uhuru wa habari upo, watu wanajiunga na vyama vya siasa kwa uhuru, uchumi unakuwa na maendeleo yanaendelea kupatikana,” amesema Rais Kikwete.

SUA call for applications: MSc Scholarships on Health of Aquatic Resources

 TRAHESA NORHED NORAD PROJECT 2014 – 2018

Sokoine University of Agriculture (SUA), in collaboration with the Norwegian University of Life Sciences (NMBU), Makerere University (MU), University of Nairobi (UoN), University of Zambia (UNZA) and the University of Dar es Salaam’s - Institute of Marine Sciences (IMS) in Zanzibar is undertaking a collaborative research project entitled “Capacity Building for Training and Research in Aquatic and Environmental Health in Eastern and Southern Africa (TRAHESA)”.

Click here to read.

Magazetini 04.08.2015


Wanachama wawafungia ofisini viongozi wa CCM Buguruni


Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wamejikuta wakifungiwa ndani ya ofisi na wanachama wa chama hicho kwa madai ya kushindwa kutangaza matokeo ya kura za maoni katika nafasi ya udiwani, hali iliyozua vurugu za kurushiana viti na kulazimu viongozi hao kuanza kuhesabu kura upya ili kutenda haki.

Balozi Mulamula ajibu maswali katika studio za Kilimanjaro, Marekani
Balozi Liberata Mulamula akiwasili nje ya jengo lenye studio ya Kilimanjaro tayari kuongea LIVE katika kipindi cha Jukwaa langu kinachorushwa kila siku ya Jumatatu kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 2 usiku saa za Mashariki za Marekanui. anayemfungulia mlango ni Abdul Malik.
Balozi Liberata Mulamula akiingia ndani ya studio akiwa amesindikizwa Harriet Shangarai (kushoto) ambaye pia ni Mkurugenzi wa studio hiyo, kulia ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme na Abdul Malik.


Balozi Liberata Mulamula akipata maelezo kutoka kwa studio meneja ambaye pia ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha Jukwaa langu, Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani) Kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akifuatilia maelezo hayo.


Mhe. Liberata Mulamula akiendelea kusikiliza maelezo kutoka kwa meneja wa studio Mubelwa Bandio ambaye ni mtangazaji na mtayarishaji wa kipindi cha jukwaa lako. Kati ni matangazaji maarufu wa Radio ya Times FM na aliyewahi kutangaza Radio One Bi. Rose Chitalah ambaye pia anamsaidia Mubelwa Bandio katika utangazaji na kuchangia hoja mbalimbali katika kipindi cha Jukwaa langu.


Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Mubelwa Bandio (kulia) na Rose Chitalah (hayupo pichani ) na wasikilizaji waliokua na shahuku ya kumuuliza maswali.


Balozi Liberata Mulamula akiendelea kujibu maswali ya watangazaji mahiri Bwn. Mubelwa Bandio (hayupo pichani ) na Rose Chitalah (kushoto)


Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme akisikiliza mahojiano na kunakili baadhi ya vipengele katika mahojiano hayo.


Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Swahiba Mdeme, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakiwa katika picha ya pamoja.


Kutoka kushoto ni Dj Luke Joe, Meneja wa studio ya Kilimanjaro, Mubelwa Bandio, Mhe. Balozi Liberata Mulamula na mtangazaji mahiri Rose Chitalah wakipata picha ya kumbu kumbu na Balozi Liberata Mulamula anayemaliza muda wake kama Balozi wa Tanzania nchini Marejkani na Canada na sasa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Maalim Seif azungumzia taarifa za kuhama Pror. Lipumba


Na Hassan Hamad OMKR

Dar  es Salaam, AM. 04/08/2015

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amekanusha taarifa za kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa Ibrahim Haruna Lipumba.

Amesema akiwa Katibu Mkuu wa Chama hicho, hajapokea taarifa zozote za kujiuzulu kwa Prof. Lipumba, na kwamba hadi saa nne za usiku wa jana Jumatatu ya tarehe 03/08/2015, alikuwa na mazungumzo ya faragha na Prof. Lipumba na wala hajamzungumzia juu ya jambo hilo.

Maalim Seif ametoa taarifa hiyo katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, wakati akihutubia kwenye mkutano Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, ambao umewajumuisha pia viongozi wakuu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA.

Amesema kwa mujibu wa Katiba ya CUF, kiongozi yeyote wa Kitaifa wa Chama hicho iwapo ataamua kujiuzulu, anatakiwa kuiandikia barua mamlaka iliyomchagua ambayo ni Mkutano Mkuu wa Chama hicho, lakini akiwa katibu wa Mkutano huo, bado hajapokea taarifa hizo.

Amefahamisha kuwa gazeti lililochapisha taarifa hizo katika toleo lake la leo tarehe 4/8/2015 lilikuwa na malengo maalum ya kuvuruga Muungano wa vyama vinavyounda UKAWA, na kwamba malengo hayo hayatofanikiwa.

Katika hatua nyengine Mkutano Mkuu wa Chadema umempitisha kwa kauli moja Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Edward Lowassa kuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho, na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CUF Mhe. Juma Duni Haji kuwa mgombea mwenza kupitia Chadema.

Mkutano huo pia umeridhia Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kuwa mgombea pekee wa urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi CUF, kwa kuwakilisha vyama vinavyounda UKAWA ambavyo ni CUF, CHADEMA, NCCR MAGEUZI na NLD.

Ole Medeye, Msindai, Makongoro wachukua kadi CHADEMA ikimtangaza Lowassa na Duni Haji kugombea Urais Tanzania 2015WANACHAMA wapya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa na Juma Duni Haji wamepitishwa katika Mkutano Mkuu wa chama hicho kugombea ngazi ya urais na umakamu wa rais kwa asilimia 99.3.

Rais Kikwete atuma salamu za rambirambi kwa msiba wa Mzee Kisumo

Peter Kisumo
Peter Kisumo
Muasisi wa Tanu na baadaye CCM, Mzee Peter Kisumo (pichani) amefariki dunia. Mwanasiasa huyo mkongwe nchini ambaye aliwahi kushika nyadhifa kadhaa katika Serikali ya Awamu ya Kwanza, alifariki Dunia jana saa moja usiku katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Mtoto wa marehemu, Michael Kisumo alilithibitishia juu ya kifo cha baba yake akisema kilitokana na maradhi ya figo ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
“Tulikuja hapa Muhimbili kwa ajili ya mzee kufanyiwa dialysis (usafishaji damu katika figo) sasa ikajitokeza complication (utata) akaanza kuharisha damu,”
alisema.

Michael alisema baba yake alilazwa wodi ya kawaida juzi ili jana apatiwe tiba hiyo kabla ya hali yake kubadilika ghafla.
“Daktari wake alipokuja leo (jana) na kumwangalia aliagiza atolewe wodi ya kawaida ahamishiwe ICU lakini ilipofika saa moja usiku akatutoka” 
alisema Michael.

Kifo cha mwanasiasa huyo kimekuja takribani mwezi mmoja tangu arejee kutoka India ambako amekuwa akienda mara kwa mara kuchunguzwa afya yake. Hali ya ugonjwa wake huo ilifikia katika kiwango cha juu na kulazimika kufanyiwa uchujaji wa figo mara tatu kwa wiki kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.

Kisumo aliwahi kuwa mmoja wa mameneja wa kampeni wa Rais Jakaya Kikwete mwaka 2005 akisimamia kanda ya kaskazini iliyojumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga. Mbali ya kuwa waziri, aliwahi pia kuwa mkuu wa mkoa na mdhamini wa CCM.

---

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesikitishwa na kuhuzunishwa na kifo cha mmoja wa wanasiasa wa kongwe nchini, Mzee Peter Kisumo ambaye alipata kuwa Mzee wa Chama cha TANU, Muasisi na mdhaminiwa Chama cha CCM naaliyeshikilia nafasi nyingi za uongozi ndani ya Serikali na utumishi wa umma ukiwemo uwaziri.

“Nimepokea kwamasikitiko makubwa na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mzee Peter Kisumo ambaye nimejulishwa aliaga dunia jana, Jumatatu, Agosti 3, 2015, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, ambako alikuwa anapatiwa matibabu ya figo,”amesema Rais Kikwete katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya MzeeKisumo.

Amesema RaisKikwete: “Kwahakika, kama taifa letu limeondokewa na kiongozi wa kupigwa mfano katika utumishi uliotukuka wa umma na Chama chetu cha Mapinduzi, na kabla ya hapo Chama cha TANU,ni MzeePeter Kisumo.

Alikuwa mzalendo wa kweli. Alikuwa Mtanzania halisi ambaye hakusita kutetea maslahi ya taifa lake. Katika nafasi zote za uongozi wa taifa letu alizozishikilia – Ubunge, UkuuwaMkoa, Uwaziri, Udhaminiwa Chama Chetu – daimaalionyeshauongoziwakiwango cha juu.

Alikuwa mwadilifu na mwaminifu na wala hakusita kuyasemea kwanguvu zake zote na kuyatetea yale aliyoyaamini na yale yaliyohusu ustawi wanchiyetu.” Ameongeza Rais Kikwete: “Mzee Kisumo ametuacha wakiwa.

Tumeondokewa na Mzee hodaria mbaye busara zake na ulezi wake vilikuwa bado vinahitajika sana katika taifa letu kwanyakati za sasa. Tutamkumbuka daima.”

Katika salamu hizo kwa familia, Rais Kikwete amesema: “Nawatumieni salamu za dhati ya moyo wangu kuomboleza kifo cha Mzee wetu.

Huyu alikuwa Mzee wenu kama alivyokuwa Mzee wangu na Mzee wa taifa letu na hivyo msiba huu ni wakwetu sote.

Naungana nanyi katika majonzi na maombolezo. Kwapa moja tuna mwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, atupe subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Aidha, tunamwomba Mungu aiwe kapeponi roho ya Marehemu Mzee Peter Kisumo. Amen”

Imetolewana: KurugenziyaMawasilianoyaRais, Ikulu,
DAR ES SALAAM. 4 Agosti, 2015

Dk Magufuli achukua fomu, aiwakilisha kwa Rais Kikwete kuithibitisha

UNDP PR: End of judges sensitization seminars on electoral dispute resolutionZahara azungumzia uzoefu alioupata katika kuwania Ubunge


Zahara Muhidin Michuzi
Zahara Muhidin Michuzi

Baada ya kura kutotosha kumfanya apite katika kura za maoni kugombea Ubunge kwa viti vya Vijana mkoani Tabora, Zahara Muhidin Issa Michuzi (pichani) amepokea matokeo kwa moyo mkunjufu na kumpongeza mshindi Irene Uwoya na kumuahidi ushirikiano katika mambo yote mema ya kuendeleza vijana mkoani humo.

Zahara ambaye sasa ataelekeza nguvu zake katika kusaka digrii ya pili ya uchumi, amesema kwamba anawashukuru wajumbe wa mkutano wa uchaguzi, baba yake, mama walezi, kaka Mkala Fundikira wa Tanzania Bloggers Network (TBN) kanda ya Magharibi na wana TBN wote wa ndani na nje ya nchi akiwemo kaka Jeff Msangi wa Canada na Mubelwa Bandio na DJ Luke wa Marekani, wanahabari wote wa makundi ya Whatsapp chini ya Francis Godwin na walimu wake pamoja na wananchi wote kwa ujumla kwa kumpa heshima ya kumuunga mkono kwa kujitokeza kujaribu kuomba nafasi hiyo.

Amesema kushindwa kwake hakumaanishi lolote zaidi ya kwamba demokrasia imechukua mkondo wake na aliyehitajika kuendeleza mapambano amepita na yeye hana kinyongo naye na ataendelea kuutumikia mkoa wa Tabora katika nafasi yake ya mtu ambaye si kiongozi.

Zahara ametoa mwito kwa wagombea wa nafasi zote kwamba kushindwa ni moja ya matokeo katika ushindani wowote hivyo ipo haja ya kujenga utamaduni wa kukubali matokeo bila ya hasira ama kinyongo kwani dunia i duara, na kwamba mlango mmoja ukifungwa kuna mwingine utafunguka.

Amesema hana mpango wa kuhama CCM ambayo anaiamini kuwa ni chama ambacho kitaenzi na kutunza hadhi na mustakabali wa Taifa la Tanzania kuliko chama chochote.

"Kushindwa kwangu kupata kura za kutosha sio mwisho wa dunia. Nina imani kwamba wapiga kura walijua wanachokifanya. Mimi ni nani kuwaoneshea kidole? Maisha yaendelee kama kawaida na Mola awajaalie wote kwa yote" alisema.