Mwigamba kuwania Ubunge Ubungo apambane na Kubenea, Masaburi

Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba (pichani), amechukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Ubungo ambako atapambana na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Didas Masaburi wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Said Kubenea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mwigamba ameahidi kuwa endapo atapata nafasi ya kuwa mbunge, atahakikisha sheria inayowabana wabunge wasio watendaji inapitishwa bungeni ikiwa ni pamoja na wananchi kuwa na mamlaka ya kumtengua mbunge kabla ya kipindi chake kumalizika.

Mwigamba alichukua fomu hiyo jana jijini Dar es Salaam, katika Ofisi za jimbo zilizopo Ubungo External na kusema kuwa azma yake ya kuwania nafasi hiyo ni kuwapatia wananchi wa jimbo hilo maendeleo waliyoyakosa kwa muda mrefu.

Alisema moja ya changamoto kubwa iliyopo katika jimbo hilo ni tatizo la maji ambalo Mbunge aliyepita alishindwa kulitatua, John Mnyika (Chadema), pamoja na tatizo la foleni katika eneo la Ubungo ambako ni kitovu cha jijini hili.

“Naamini kupitia ACT-Wazalendo tunaweza kuwapatia maendeleo wananchi wa jimbo la Ubungo ambayo wameyakosa kwa vipindi vyote walivyokuwapo wabunge waliotangulia pamoja na kutatua kero mbalimbali,” alisema Mwigamba.

Pia, alisema kuwa kupitia ilani ya chama chake, hawawezi kukiuka taratibu na kanuni za katiba hiyo, hivyo watawatumikia vyema Watanzania kwa kuzingatia hayo bila kubadilisha misimamo waliyojiwekea kama vyama vingine.

Kwa mujibu wa Katibu wa Jimbo hilo, Patrick Malya, waliochukua fomu hadi jana ni 11 na waliorudisha ni wagombea nane na kwamba kura za maoni zinatarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii.

Pia waliorudisha fomu katika Ofisi hizo jana kwa ajili ya kuwania ubunge katika jimbo la Kibamba ni mwandishi wa habari wa gazeti la The Guardian, Dickson Ng’ili na Eliya Msope ambaye ni mwenye ulemavu wa macho. [NIPASHE]

Mnyika ashinda kura za maoni Kibamba

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (Chadema), ameshinda katika kura za maoni za kugombea ubunge katika Jimbo la Kibamba kwa kupata kura 65 kati ya kura 80 zilizopigwa (asilimia 65).

Katibu wa Jimbo la Ubungo wa Chadema, Justine Malel, alilieleza NIPASHE jana kuwa nafasi hiyo iliwaniwa na wagombea nane ambao waliambulia asilimia 15 huku Mnyika akiongoza.

“Uchaguzi ulifanyika jana (juzi), Mnyika ameshinda kwa kishindo dhidi ya wagombea wenzake nane, pia katika kura za ndani ya chama ameshinda bila ya kupingwa kwa asilimia 100, kwa maana hiyo Chadema tumemsimamisha Mnyika kugombea jimbo la Kibamba,” alisema Malel.

Mnyika atachuana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenela Mukangara, mgombea wa nafasi hiyo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku mgombea wa nafasi hiyo kupitia Chama Cha ACT-Wazalendo akitarajiwa kujulikana Jumamosi. [NIPASHE]

Magazetini Agosti 7, 2015
Four suspected criminals from Zambian shot dead in Tanzania

Four suspected criminals believed to be Zambians have been gunned down at Tuduma in Tanzania by the Tanzanian police during an exchange of heavy gun fire.

Both Tanzanian police and Muchinga Deputy Commissioner of Police Peter Bubenshi have confirmed the incident in an interview with ZANIS at Tuduma today.

Mr. Bubenshi said the four suspected criminals were gunned down at about 11:00 hours yesterday when they staged a day-light robbery at beer depot located at Songea about 6 km inside Tuduma town from the Zambian border town of Nakonde.

Mr. Bubenshi said Tanzanian police have since recovered 400,000 cash Tanzanian Shillings equivalent to K1.6 million, an AK 47 Rifle and a Semi Automatic Machine Gun (SMG).

One of the deceased suspects was also found with a ticket for a Zambian bus operating between Lusaka and Nakonde which showed that he arrived in Nakonde in the morning yesterday and allegedly took part in staging the robbery.

The bodies of the four suspects are lying at Tuduma mortuary awaiting further investigations.

Meanwhile, a team of Zambia Police officers from Chinsali has arrived at Tuduma Tanzania for further investigations.

Mr. Bubenshi said the team will be in Tuduma working with the Tanzanian police to ensure that the case is fully investigated and the source of fire arms traced.

Mgombea Urais kupitia UKAWA kuungwa mkono na SAU, APPT-Maendeleo

Wakati vyama vinne vinavyounda UKAWA, vimempitisha Edward Lowassa kugombea urais, vyama vingine vya SAU na APPT-Maendeleo vimetangaza kumuunga mkono mgombea huyo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa SAU, Ali Kaniki alisema chama hicho kimefikia uamuzi wa kuunga mkono umoja huo kutokana na nafasi kubwa iliyopo ya kushika dola. Kaniki alisema kwa sasa wana wanachama zaidi ya 500,000 nchi nzima, hivyo wanaamini kuwa na mchango katika harakati hizo.

Mwenyekiti wa APPT-Maendeleo, Peter Mziray alisema chama hicho kinaamini mabadiliko kupitia kambi ya upinzani, hivyo wameamua kuunga mkono UKAWA.
“Uchaguzi wa mwaka 2010, nilishika nafasi ya nne kwa kupata kura 96,000, lakini pia tuna madiwani watatu na wanachama wameongezeka kwa hivyo ninaamini mchango wetu utakuwa na nafasi kubwa UKAWA,” 
Mwenyekiti wa UDP, Mkoa wa Dar es Salaam, Joackim Mwakitinga alisema chama hicho kitakuwa tayari kuunga mkono mgombea mmoja kutoka CCM au UKAWA.
“Nafasi ya urais hatutasimamisha mgombea ila tutaunga mkono kati ya vyama hivyo wakati wa kampeni.”
via gazeti la Mwananchi

Maimam 6 kutoka Tanzania watekwa DRC

Taarifa iliotolewa na Katibu Mkuu wa shirika la Waislam mkoni Kivu imefahamisha kuwa maimamu sita kutoka Tanzania wameshikwa kama mateka na watu ambao wanashukiwa kuwa waasi wa Rwanda katika kitongoji cha Katwiguru Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Imam Hashim Musa aliliambia shirika la habari la Anadolu kuwa Maimamu hao walikuwa wakihubiri Rutshuru tangu Agosti 2 na baadaye kujielekeza Katwiguru ambapo walitekwa pamoja na dereva wao na watu ambao wanashukiwa kuwa waasi wa FDLR.

Imam Hashim Musa amefahamisha kuwa, waasi hao walitoa taarifa kuwa wanahitaji kitita cha pesa elfu 40 sarafu za Marekani ili kuwaacha huru mateka hao.

Asasi za kiraia Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimelaani vikali kutio hilo.

Takwimu rasmi nchini DRC zinafahamisha kuwa idadi ya waislam inakadiriwa kufikia watu milioni 10 kati raia milioni 65.7 hivi. [via Idhaa ya Kiswahili ya TRT]

[video] Huku Magufuli anapiga tumba, kule Nape anacharaza gitaa, hapa kati Rais Kikwete anaserabuka


Msaada tafadhali kwa ajili ya tiba ya Selemani Rashidi

Selemani Rashidi, naomba msaada kwa yeyote anisaidie niweze kufanyiwa matibabu kwa kinyama kilichojitokeza kichwani mwangu toka nilipozaliwa.

Selemani Rashidi (kushoto), akiwa na mama yake mzazi pichani, ambaye alisimulia mkasa mzima wa mwanaye, alizaliwa akiwa mzima na baada ya kuzaliwa alipatwa na matatizo ya ugonjwa wa degedege na alimpeleka kwa mganga wa kienyeji na kupona matatizo hayo na ndipo kikaota kipele kichwani cheusi na kikawa kinakuwa na kushikana na sikio. Kwa kutokuwa na uwezo wa kipesa hakuweza mpeleka popote. Baba yake yapata miaka kumi na tano toka afariki. 

Hayo yalisemwa na mama yake mzazi ambaye anaitwa Zamda Kibosha, wakiwa wamekaa kwao maeneo ya kitongoji cha Lugongoni, (A) Kata ya Nguruka Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma.

Mama yake anasema mwanaye baada ya kuota kinyama hicho, kauli kutoka ni kwa shida, akijibu mara moja harudii tena kuongea. Anakwenda mwenyewe chooni, anakula kama kawaida. 

Mama anaomba kwa mtu yeyote mwenye kuona na kusikia amsaidie wa hali na mali ili mwanaye apate matibabu. Kwa mawasiliano mwenye chochote kitumwe kwenye namba 0687946492, Mariam Hamza Thabiti, Nguruka, Kigoma. 
Selemani Rashidi, anapoishi na mama yake mzazi

Picha, maelezo: KHAMIS MUSSA

Waziri awasimamisha kazi maafisa waliojimilikisha viwanja[video] Mikutano ya CHADEMA/UKAWA 2015
Taarifa ya Wizara kuhusu habari za kunyanyaswa ofisini kwa kuvaa hijab

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

Gazeti la kila wiki la Imaan la Agosti 3-9, 2015 Toleo Na.022, lilichapisha habari katika ukurasa wake wa pili yenye kichwa cha habari: “Watatu wasimulia walivyonyanyaswa kwa hijab Serikalini.”
Katika habari hiyo mwandishi alieleza kuwa baadhi ya watumishi wa umma ambao wanavaa mavazi kulingana na imani za kidini wananyanyapaliwa na kunyimwa safari. Ilieleza kuwa baadhi ya taasisi za Serikali (alizitaja) ikiwemo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo zinawanyanyapaa wafanyakazi wa kike wanaovaa mavazi aina ya hijab ambayo ni maarufu zaidi kuvaliwa na wanawake waumini wa dini ya Kiislamu.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina dini hivyo siyo kweli kwamba Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imekuwa ikiwakataza wanawake wa Kiislamu kuvaa hijab kama ambavyo mwandishi alieleza katika habari hiyo.

Kimsingi habari hiyo ni ya kizusha na yenye lengo la kupandikiza chuki baina ya jamii yenye imani ya dini ya Kiislam dhidi ya Serikali yao. Hata hivyo, mwandishi ameandika habari hiyo bila kupata maoni au maelezo upande wa pili unaotuhumiwa kwa maana ya uongozi wa taasisi alizozitaja kwamba zinawazuia wanawake kuvaa hijab badala yake ametumia maelezo ya upande mmoja unaolalamika.

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inafuata mwongozo wa Waraka wa Utumishi wa Umma Na. 3 wa mwaka 2007 kuhusu mavazi kwa watumishi wa Umma. Waraka huo umeainisha mavazi ambayo hayafai kuvaliwa katika ofisi za umma kwa wanawake na wanaume; aidha umeelekeza aina za mitindo ya nywele isiyofaa pamoja na aina za viatu visivyofaa.

Mifano ya mavazi yasiyokubalika kwa watumishi wa umma wanawake ni kama vile nguo zinazobana, nguo fupi ambazo zinaacha magoti wazi, nguo ambazo zinaacha sehemu ya mwili wazi kama vile kitovu na kifua, nguo ambazo zina picha, michoro, na maandishi ambayo hayaendani na shughuli za Serikali, kaptura aina yoyote ile kama vile pedo na pensi, nguo zinazoonyesha maungo ya mwili (transparent), suruali za ‘Jeans’, na nguo zingine zote zenye kukinzana na maadili ya utumishi wa umma na jamii kwa ujumla.

Aidha, kwa upande wa wanaume mavazi yasiyokubalika ni pamoja na nguo ambazo ni za kazi maalum kama vile michezo (hizi zivaliwe wakati wa shughuli hiyo tu), nguo ambazo zina michoro, maandishi na picha ambazo haziendani na shughuli za Serikali, nguo zinazobana, kaptura ya aina yoyote, suruali yoyote inayoachwa bila kupindwa, suruali za “Jeans” na Fulana “T-shirts” (Hizi zivaliwe tu wakati wa shughuli maalum inayotambulika), Kikoi au msuli, nguo zenye maandishi ya chama chochote cha siasa na yenye kuonyesha ushabiki wa kitu fulani.

Pamoja na kuwepo kwa miongozo ya mavazi yanayostahili kwa watumishi wa umma, tafsiri ya mavazi ya heshima hutegemea mila na desturi ya jamii husika. Katika utumishi wa umma mavazi ya heshima kwa mtumishi wa umma ni yale ambayo yanazingatia mila na desturi za taifa letu.

Kwa kutambua kuwa kila mmoja wetu ana imani yake na anao uhuru wa kuamini katika dini yoyote ni vyema sisi wenye dhamana ya kuhabarisha umma tukaepuka kueneza habari za chuki dhidi ya imani nyingine au Serikali kwani kufanya hivyo kutasababisha utengano miongoni mwa jamii, badala ya kuleta umoja na mshikamano kwa ustawi wa Taifa letu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Watatu washikiliwa kwa mauaji ya ASP Palangyo

Elibariki Palangyo
Elibariki Palangyo
Jeshi la Polisi Kanda Maaluma ya Dar es Salaam linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya ofisa wake Marehemu ASP Elibariki Palangyo huko Yombo Kilakala Dar es Salaam. 

Mkuu wa Oparesheni wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Sirro alise tukio hilo la mauaji lilitokea Agosti 4, mwaka huu nyumbani kwa marehemu.

Kamanda Sirro, amesema kua Polisi Mkoa wa Temeke ilifanya msako mkali dhidi ya watuhumiwa wa tukio hilo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wa tatu wanaosadikiwa kuhusika na mauaji hayo.

Amewataja watuhumiwa waliokamatwa kua ni Salim Khatib (32) dereva bodaboda Mkazibwa Tabata Luis aliyekamatiwa maeneo ya Kiwalani akiwa mafichoni. Mtuhumiwa mwingine ni Ismail Said (36) dereva bodaboda na mkazi wa Yombo Makangarawe, pamoja na Pirimini Haulemi (25), dereva bodaboda mkazi wa Yombo Makangarawe.

Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali ilibkuweza kubaini watuhumiwa wote waliohusika katika mauaji hayo.

Aidha Kamanda Simon Sorro ametoa wito kwa raia wema kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kutoa taarifa sahihi na za uhakika zitakazosaidia kupatikana kwa watuhumiwa wa tukio hilo la mauaji pamoja na matukio mengine ya uhalifu.

Rais Kikwete atuzwa alipoiaga rasmi Idara ya Mahakama


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo maalumu kutokana na mambo makubwa liyoifanyia idara hiyo kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi. 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionesha tuzo maalumu aliyoipokea kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Sehemu ya wastaafu na viongozi wa taasisi wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


MC wa shughuli katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Meza Kuu katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Rais Kikwete akisalimiana na watumishi wa Mahakama jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Rais Kikwete akisalimiana na Majaji wa Mahakama Kuu jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Rais Kikwete katika picha ya pamoja Majaji wa Mahakama Kuu ya Rufani jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.


Rais Kikwete katika picha ya Mwanasheria Mkuu, Mtendaji Mkuu wa Mahahama, Rais wa Tanganyika Law Society jijini Dar es salaam leo Agosti 6, 2015 katika sherehe fupi iliyoandaliwa na Mahakama na wadau wa Sheria kumuaga rasmi Mhe Kikwete kama Rais wa nchi.  • Picha kutoka Ikulu

Wajasiriamali wa uwakala wa forodha hawastahili kuwezeshwa?

JE WAJASIRIAMALI KATIKA SEKTA YA BIASHARA YA UWAKALA WA HUDUMA ZA FORODHA NCHINI TANZANIA HAWASTAHILI KUWEZESHWA?

Na:Ray E.Njau (Mdau katika huduma za forodha nchini Tanzania)
----------------------

Kutokana na serikali na mamlaka zake kukosa uwezo wa kutoa ajira kwa wimbi kubwa na wananchi wengi wenye uhitaji imeonekana kuwa ni vema wananchi wajengewe mazingira rafiki yatakayowawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii,biashara na uchumi.

Wakati hayo yakiendelea sekta ya uwakala wa huduma za forodha ambayo inahusisha watoa huduma wa forodha,bandari,mawakala wa meli, reli, barabara, posta, simu na intaneti.

Makampuni ya uwakala wa huduma za forodha nchini Tanzania yanatekeleza shughuli zake chini ya mwamvuli wa chama cha mawakala wa huduma za forodha (Tanzania Freight Forwarders Association - TAFFA)

Utekelezaji wa kampuni husika katika sekta hii unawezekana tu pale vigezo na masharti husika kwa mujibu wa mamlaka zinazohusika.

Masharti hayo yanatia ndani usajili wa kampuni,leseni ya biashara,leseni ya forodha,usajili wa TAFFA, leseni ya SUMATRA, leseni ya bandari,vitambulisho kutoka sekta shirikishi ndani ya forodha na bandari kuu na bandari kavu.

Kutokana na madokezo yaliyopo hapo inaonekana ujasiriamali katika sekta unahitaji uwezeshaji wa serikali na mamlaka zake ili wananchi waweze kumudu utekelezaji wa shughuli zao za kila siku.

Uwezeshaji mwema kutoka serikali kuu na mamlaka zake siyo mikopo ya fedha bali kujenga mazingira rafiki yatayowawezesha wananchi wenye uchumi mdogo kukidhi vigezo na masharti ya kupata leseni na vibali halali kwa ajili ya kumiliki na kutekeleza biashara ya uwakala wa huduma za forodha nchini Tanzania.

Katika misemo mingi ya kiingereza leo napenda kuchagua msemo huu: "Cut your coat according to your cloth" (kata koti lako kulingana na kitambaa chako). Msemo huu unatausaidia kufanya yale mambo yaliyopo katika uwezo wetu na si vinginevyo.

Hili ni angalizo lenye ladha maridhawa kwa mamlaka zote zenye dhamana katika sekta hii ya biashara ya uwakala wa forodha nchini Tanzania kupitia upya vigezo, masharti na gharama zote husika ili kuona ikiwa kwa kweli ni kwa ajili kumwezesha mwananchi wa uchumi wa kawaida kujipatia riziki halali kupitia sekta hii au ni kwa ajili ya kupoteza kwa makusudi kile ambacho ni halali kwake kukipata.

Balozi Mulamula aondoka rasmi Marekani na kurejea Tanzania


Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC walipokwenda kumuaga nyumbani kwake Bethesda Maryland.


Safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Dulles ikianza.


Mhe Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Agnes Mutta Mke wa Mwambata wa Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC.


Mhe Balozi Liberata Mulamula pamoja na Mkuu wa Utawala Lily Munanka wakibadilishana mawazo pamoja na familia ya Mwambata wa Jeshi.


Mhe Balozi Liberata Mulamula akiwa pamoja na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta pamoja na Mkewe Agnes Mutta.


Mhe Balozi Liberata Mulamula akitoa pasi yake ya kusafiria kwaajili ya kujisajili tayari kwa kuondoka.


Mhe Balozi Liberata Mulamula akiwa katika hatua za mwisho za usajili.


Mhe Balozi Liberata Mulamula tayari usajili ulipokamilika


Mhe. Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi pamoja na familia zao.


Mhe. Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula akiwa tayari anajiandaa kwa ukaguzi wa mwisho na kuelekea kwenye ndege.


Kwa pamoja tunasema "Safari Njema na Ubarikiwe Sana, Balozi Mulamula daima tutakukumbuka".
  • Picha zote: Kamera ya Ubalozi
  • Tumeshirikishwa picha-taarifa hii na Kwanza Production