Magufuli ahimiza umoja na mshikamano kwa WanaCCM


Dkt John Pombe Magufuli kwa pamoja akicheza wimbo wa "Adinselema" uliokuwa ukiimbwa na wanachama hao mara baada ya kumpokea na kuamsha shamra shamra na shangwe za hapa na pale. Pichani kulia ni Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mama Salma Kikwete akishuhudia.


Mgombea Uraisi wa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa kwa shangwe na shamra shamra kutoka kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM waliokuwa wamekusanyika nje ya ofisi za CCM mkoa wa Lindi, alipofika kusaini vitabu, kuwashukuru na kujitamulisha kwao.


Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mama Salma Kikwete akizungumza jambo na Wanachama wa chama hicho nje ya Ofisi za CCM mkoa wa Lindi


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wanachama wa CCM na wafuasi wa chama hicho waliofika kumlaki alipowasili kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama hao mapema leo Agosti 8 2015.Dkt Magufuli amewataka wananchama hao kushikamanana kuwa wamoja katika kipindi hiki muhimu cha uchaguzi,ambacho anaamini kitaipatia ushindi chama CCM.


Dkt John Pombe Magufuli akitia sahihi vitabu ndani ya ofisi ya CCM mkoa wa Lindi,pichani kati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa,Ndugu Ali Mtopa pamoja na Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mama Salma Kikwet.


Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi,Ndugu Ali Mtopa,alipowasili kumkaribisha Mgombea Mteule wa chama cha Mapinduzi,Dkt John Magufuli aliyewasili kwenye ofis hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Lindi,Ndugu Ali Mtopa alipowasili kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM mkoani humo mapema leo Agosti 8 2015


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu, Mama Salma Kikwete. Dkt Magufuli aliwasili kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM mkoani humo mapema leo Agosti 8 2015


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanachama wa chama hicho waliofika kumlaki alipowasili kwenye ofisi hizo kwa ajili ya kusaini vitabu pamoja na kuwashukuru na kujitambulisha kwa wanachama na wafuasi wa chama cha CCM mkoani humo mapema leo Agosti 8 2015


"Karibu Bwana Magufuli... karibu sana Lindi" mmoja wa Wanachama akimkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mara baaada ya kuwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Lindi ambapo alisaini vitabu, aliwashukuru wanachama na wafuasi wa chama hicho pamoja na kujitambulisha kwao.


Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mmoja wa watoto waliofika kumlaki mgombea huyo.


"Karibu Bwana Magufuli... karibu sana Lindi" mmoja wa Wanachama akimkaribisha Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mara baaada ya kuwasili katika ofisi za CCM mkoa wa Lindi ambapo alisaini vitabu,aliwashukuru wanachama na wafuasi wa chama hicho pamoja na kujitambulisha kwao. 


Dkt John Magufuli akisalimiana na aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Mtama,kabla ya Mhe. Bernad Membe, Ndugu Kassim Abdallah.
  • Picha: Michuzi Jr, Lindi. 

CCM Viti Maalumu 2015: Walioshinda; Walioshindwa

UCHAGUZI wa Wabunge wa Viti Maalum umeleta sura nyingi mpya huku baadhi ya vigogo wakiwemo Maua Daftari, Alshaymaa Kweigy, Magreth Mkanga na Shyrose Bhanji wakishindwa katika uchaguzi uliofanyika jana.

Matokeo hayo yalitangazwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi huo, Zakhia Meghji ambaye pia ni Katibu wa uchumi na fedha. 

Nafasi ya uwakilishi Viti Maalum, walemavu nafasi mbili, walioshinda ni Stella Alex na Amina Mollel, Stella alipata kura 51 huku Amina Mollel akipata kura 44.

Wagombea wengine ambao walishindwa katika uchaguzi huo ni Alshamaa Kweygir alipata kura 38, Khadija Taya ‘Keisha’ alipata kura 37, Magreth Mkanga kura 27, Elizabeth Msaki kura 26, Bahati Hemed kura 17, Salma Ramadhani kura 15, Hidaya Juma kura 10, Halima Seif kura tano, Sitta Kelvin kura nne, Suzan Mushi kura nne.

Wengine ni Lupui Mwaswaya kura nne, Edith Kagomba kura tatu Mary Kalumuna kura tatu, Rwehema Joshua kura tatu, Sarah Mkumbo kura tatu na Riziki Lulida kura moja.

Nafasi za uwakilishi wa wanawake kundi la NGO, nafasi mbili walioshinda ni Dk Gertrude Rwakatare na Rita Mlaki.

Rwakarate alipata kura 82 na Mlaki kura 59.
Walioshindwa katika kundi hilo ni Khadija Aboud kura 36, Maua Daftari kura 29, Zainabu Gama kura 10, Angela Mwangoza kura 10, Saum Abdallah kura tisa, Grace Mahumbuka kura tisa, Chiku Mugo kura tisa, Sitti Ally kura nane, Diana Lenatus kura saba.

Wengine ni Nebro Mwina kura saba, Angela Bayo kura nne, Renatha Kapinga kura nne, Devotha Mtonyole kura nne, Hawa Isengwa kura tatu, Christina Kulunge kura tatu, Said Sharifu kura tatu na Mickness Mahella kura moja.

Nafasi ya uwakilishi wa wanawake vyuo vikuu nafasi mbili walioshinda ni Dk Jasmine Tiisekwa na Ester Mmasi.

Dk Tiisekwa alipata kura 61 na Mmasi alipata kura 46.

Walioshindwa katika nafasi hiyo ni Dk. Alice Kaijage alikuwa mshindi wa tatu kwa kupata kura 39, Lucy Saleko kura 25, Theo Ntara kura 24, Maurine Castico kura 20, Juliana Manyerere kura 16, Mariam Khamis kura 12, Mary Lubeleje kura 11, Kuluthumu Makame kura 10, Godliver Kaijage kura nane.

Wengine ni Mwadawa makame Ame kura saba, Furaha Mramba kura tano, Zainabu Zonzo kura tano na Tumwangile Mwakyusa kura nne.
Kwa upande wa nafasi ubunge wanawake wafanyakazi nahasi mbili walioshinda ni Angellah Kairuki na Hawa Chakoma. Kairuki alipata kura 47 na Chakoma alipata kura 47.

Wagombea wengine katika nafasi hiyo walikuwa Shyrose Bhanji alipata kura 30, Asmayah Ally kura 29, Lamela Malya kura nane, Vedate Ligalama kura saba, Amina Mweta kura sita, Bijuma Hamad kura tano, Meck Gushaha kura nne, Janeth kabeho kura nne, Flora Masakilija kura nne.

Wengine ni Zeleikha Salim kura nne, Esther Kimwei kura tatu, Mwanamwanga Mwadunga kura mbili na Mwantumu Othuman kura mbili.

Katika nafasi ya wagombea Ubunge Viti Maalum CCM Kundi la vijana Zanzibar nafasi nne walioshinda ni Khadija Nasri Ally alishika nafasi
ya kwanza kwa kupata kura 117, Munira Mustafa Khatibu kura 105, Nadra Juma Mohamed kura 103, Time Bakari Sharifu kura 91.

Walioshindwa ni Salma Seif Ally alipata kura 87 na Mwanaenzi Hassan Suluhu kura 66. 
  • Taarifa ya Sifa Lubasi akiliripotia gazeti la Habarileo
TWEETVISIT WEBSITE

Katuni tulizozipata leo 08.08.2015 kuhusu saisa za Tanzania

 

   

Tangazo: Ratiba ya kuhakiki taarifa kwa waliojiandikisha BVR


Orodha ya vyama vya siasa vitakavyoshiriki Uchaguzi Mkuu 2015

Orodha ya vyama vya siasa vitakavyoshiriki Uchaguzi Mkuu 25.10.2015

[video] Nikki wa Pili: Tunahitaji utafiti kwenye muziki


Taarifa ya habari "Asubuhi Njema" ChannelTEN Nane Nane


Magazetini, Nane Nane 2015

Matukio katika ulimwengu wa kisiasa wa Juma Duni Haji

Juma Duni Haji
Juma Duni Haji
Mwanasiasa machachari wa upinzani kutoka Zanzibar, Juma Duni Haji aliteuliwa kuwa mgombea mwenza wa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Lowassa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA); Uteuzi uliofanyika mara tu baada ya mwanasiasa huyo kukihama Chama cha Wananchi (CUF) ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA - vyama vingine vilivyomo kwenye Ukawa ni NCCR-Mageuzi na National League for Democracy (NLD)).

Viongozi wa UKAWAwalipokutana kupitia majina ya wanasiasa wenye sifa ya kuwa wagombea wenza, walikubaliana kumteua mwanasiasa huyo ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CUF na Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inayofanya kazi chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).

Mwanasiasa huyo amekuwa na historia ndefu na mara tatu amewahi kuteuliwa na CUF kuwa mgombea mwenza wa urais wa Jamhuri ya Muungano, akiwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba. Amekuwa mgombea mwenza wa Profesa Lipumba katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, mwaka 2005 na mwaka 2010. Duni amewahi kunukuliwa akieleza kuwa yeye ni mtumishi wa watu na kila mara alikotumwa alikwenda. Hivyo, hata leo akiteuliwa kwenda kuongoza kijiji au kitongoji ilimradi Watanzania wametaka hivyo, ataitikia wito.

Juma Duni alianza safari ya kisiasa kwa “kulazimishwa” mwaka 1984, baada ya Serikali ya Muungano kutoa Waraka wa Serikali (White Paper) na kutakiwa wananchi watoe maoni yao juu ya hali na matatizo ya Muungano.

Wakati huo, makatibu wakuu wa Serikali ya Zanzibar akiwamo yeye walitoa maoni dhidi ya muungano. Uhuru huo wa kitaalamu uligeuzwa kuwa mchungu kwani walisingiziwa kwamba wamefanya kinyume na walivyoagizwa na baadhi yao wakapewa onyo kali na wengine wakateremshwa vyeo.

Juma Duni aliteremshwa cheo kutoka wadhifa wa Katibu Mkuu hadi mwalimu wa kawaida kwa Tangazo la Rais. Huko nako pia hakubaki salama kwani alituhumiwa kuwajaza wanafunzi kasumba, hivyo alirudishwa Wizara ya Elimu kama Ofisa Mipango ambako pia alituhumiwa kujihusisha na siasa za upinzani. Duni alipoona amechoka kuhamishwahamishwa na kushutumiwa, aliomba likizo ya bila malipo kwenda kusoma, ombi ambalo pia lilikataliwa.

Hapo ndipo alipoamua mwenyewe kuondoka na kwenda kujisomesha kwa fedha zake Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza na kuhitimu stashahada ya Juu ya Biashara kati ya mwaka 1993-1994. Alipofika Uingereza, akatumiwa barua ya kuachishwa kazi na kupoteza haki zake zote za miaka 18 ya utumishi serikalini.

Mwaka 1994 akiwa bado nchini Uingereza, akaunganisha masomo na kusomea Shahada ya Uzamili akibobea kwenye usimamizi wa Rasilimali Watu na kabla hajahitimu akarejea nchini ili kusaidia upinzani kujipanga kiuchaguzi. Moja kwa moja akajiunga na vuguvugu la uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi akajiunga na CUF na akateuliwa kuwa mgombea mwenza wa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama hicho, Profesa Lipumba wakati bado hajakamilisha shahada yake ya pili ya uongozi na utawala.

Tangu ajiunge CUF, Juma Duni ameshika nyadhifa mbalimbali kwa nyakati tofauti. Amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu, Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha, pia amekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi. Amekuwa Makamu Mwenyekiti wa CUF nafasi aliyoishika hadi wiki hii alipojiuzulu kimkakati na kujiunga na Chadema.

Juma Duni si mgeni katika masuala ya kibunge au ya kiuwakilishi. Mwaka 1997 aligombea nafasi ya ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Jimbo la Mkunazini, akashinda na kuwa mwakilishi kuanzia mwaka 1997-2000.

Mwaka 2009 aliteuliwa na Rais Amani Abeid Karume kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa mara ya pili, akakaa katika wadhifa huo hadi uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ulipofanyika na kuundwa kwa SUK.

Katika SUK, Juma Duni aliteuliwa na Rais wa Zanzibar kuwa mwakilishi na kisha akateuliwa kuwa Waziri wa Afya wa Zanzibar, wadhifa ambao ameushikilia hadi Rais Dk Mohamed Shein alipovunja Baraza la Wawakilishi.

Sifa kubwa ya Duni ni ucheshi na kuchangamana na watu, ni rafiki wa wakubwa na wadogo kiasi cha kwamba kwa wengi wanaomfahamu humwita ‘Babu Duni.’

Maswali 7 kuhusu "dinner" wasanii na Rais Kikwete

Rais Kikwete akisakata muziki katikati ya wasanii
HAFLA inayotajwa kuandaliwa na “Umoja wa Wasanii Tanzania” ya kumuaga Rais Jakaya Kikwete anayestaafu baada ya uchaguzi wa Okotoba mwaka huu, imezua mjadala mkubwa nchini.

Mjadala wenyewe unatokana na kile ambacho wengi wa wasanii wanasema kwamba hawajapata kujua kwamba kuna umoja wa wasanii Tanzania.

Mingi ya mijadala inayoendelea kwenye kota mbalimbali za jiiji la Dar es Salaam pamoja na mitandao ya kijamii yanajadili kwamba kama ni umoja wa wasanii kumuaga Rais kikwete, imekuaje ukumbi umejaa makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwepo mgombea Urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu huo, John Magufuli.

Hoja kuu hapa ni, Je, umoja huo wa wasanii umeundwa ndani ya mfumo wa CCM? au wasanii waliokuwa mbele katika hafla hiyo walitumika tu kujenga picha kwamba umma wa wasanii Tanzania unamsapoti Magufuli?

Ukweli ni kwamba, katika miongoni mwa wasanii wenye majina makubwa katika tasnia ya filamu na muziki, ukiwemo wa bongo fleva, taarabu, muziki wa injili na dansi, wapo wengi siyo tu ni viongozi katika vyama vya upinzani, pia ni wagombea nafasi za ubunge kupitia vyama hivyo vya upinzani.

Baadhi wa wasanii ambao ni wagombea ni Seleman Msindi ‘Afande Sele’ na Joseph Haule ‘Prof. Jay’. Wasanii waliokuwa meza kuu katika hafla hiyo sambamba na Kikwete ni Jacob Steven ‘JB’ na Nikii wa Pili.

Yafuatavyo ni maswali yanayouliwa katika mijadala iliyopo katika mitandao ya kijamii:-
  1. Umoja huo umeanzishwa lini na viongozi wao kina nani?
  2. Wasanii wanatambua kua kuna umoja wa wasanii tena usiokua na jina rasmi?
  3. Kama wasanii wameungana ili kumuaga rais wa nchi, kwanini kulikuwa na lundo la viongozi wa chama kimoja cha siasa?
  4. Magufuli kupewa nafasi ya kipekee, alienda kama mgombea wa chama, kama waziri au kama mpiga ngoma mtarajiwa wa Twanga?
  5. Nani aligharamia gharama za sherehe?
  6. Wasanii walizipataje hizo pesa za sherehe wakati wenzao wakiumwa hadi waandae matamasha ya kuchangia kwa njia ya kiingilio na hawapati zaidi ya Sh. milioni mbili.
  7. Kwanini wasanii ambao ndio wanaodaiwa kuwa waandaaji waliandaliwa kadi za mwaliko badala ya wao kumuandalia mheshimiwa rais kadi ya mwaliko?

Rais Kikwete azindua barabara ya Ndundu - Somanga


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa kilomita 60, hafla hiyo imefanyika jana Agosti 7 2015 mkoani Lindi.Wengine pichani ni Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najem, Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait, Abrahman Al- Hashim,Mkuu wa Mkoa wa Pwan, Eng. Evarist Ndikilo, wengine kushoto ni Waziri wa ujenzi Mhe. John Pombe Magufuli, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Mwantumu Mahiza.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazia Dkt. Jakaya Kikwete akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbali mbali mara baada ya kufunguarasmi barabara ya Ndundu - Somanga.


Rais Kikwete akimshukuru Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim mara baada kuweka jiwe la msingi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika kwenye kijiji cha Marendego,wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.


Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa pamoja na mkewe Salma Kikwete akimwagia maji mti wa kumbukumbu alioupanda baada ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga mkoani Lindi.


Wafadhili wa ujenzi wa barabara ya Ndundu-Somanga, Balozi wa Kuwait Jassem Ibrahim Al Najim na Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwait ,Abrahman Al Hashim mara kwa pamoja wakishiriki kupanda mti wakati wa sherehe fupi zilizofanyika kwenye kijiji cha Marendego ,wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.


Rais Kikwete akiwasalimia na kuwaaga wananchi wa kijij cha Nangurukulu na kumtambulisha Mgomea Urais kwa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akielekea mkoani Lindi.


Mgombea Urais wa chama cha Mapinduzi Dkt John Pombe Magufuli akijitambulisha kwa wakazi wa mji wa Nangukurulu,mara baada ya sherehe fupi za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga kukamilika mkoani Lindi.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ujenzi ambaye pia ni Mgombea mteule wa Urais wa chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili katika kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kufungua barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo imejengwa na Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa Kuwait pamoja na mfuko wa OPEC .


Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akipokelewa na Mkuu wa mkoa wa Lindi, Mh. Mwantumu Mahiza mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa mkoani Lindi kushiriki ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 6.Barabara hiyo imejengwa na Serili ya Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa Mfuko wa Kuwait pamoja na mfuko wa OPEC .
Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa,Mh.Bernad Membe mara baada ya kuwasilia katika kijiji hicho Marendengo,ambapo sherehe za uzinduzi wa barabara ya Ndundu-Somanga zilifanyika na mgeni Rasmi alikuwa ni Rais Dkt Jakaya Kikwete.


Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam,Mh Said Meck Sadick akiwa sambama na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mh.Mwantumu Mahiza.


Wananchi kutoka kijiji cha Marendego na vijiji vyake wakishangilia jambo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Ndundu –Somanga yenye urefu wa kilometa 6,inayojengwa na Tanzania kwa kushirikiana na Ufadhili wa mfuk wa Kuwait pamoja na Opec.Katika unziduzi huo viongozi mbalimbali wa chama na serikal,viongozi wa dini pamoja na watu wengine walishiriki kushuhudia tukio hilo adhimu hapa nchini.


Wananchi wakifuatilia tukio hilo


Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakati wa ufunguzi wa barabara hiyo ya Ndundu -Somanga yenye urefu wa kilometa 60


Wananchi wakifurahia ufunguzi wa barabara hiyo iliyokuwa kero kubwa kwa wananchi wa Mtwara na Lindi


Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa sherehe fupi za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga iliyojengwa kwa kiwango cha lami na yenye urefu wa kilometa 60 ,Somanga mkoani Lindi.


Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa,Mh Bernad Membe


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa Kilomita 60 mkoani Lindi.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa Kilomita 60 mkoani Lindi.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimu wananchi waliojitokeza kushuhudia ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga yenye urefu wa Kilomita 60 mkoani Lindi.


Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe fupi zilizofanyika kwenye kijiji cha Marendego kata ya Somanga za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.


Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wananchi wakati wa sherehe fupi ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga mkoani Lindi yenye urefu wa kilomita 60 na imejengwa kwa kiwango cha lami.
  • Picha: Ikulu

Lowasa kuchukua fomu NEC za kuwania Urais wa Tanzania 2015

Haji, Lowasa, Seif
L-R: Haji, Lowasa, Seif
AGOSTI 10 mwaka huu, Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) umekusudia kufanya msafara mkubwa wa kumsindikiza Edward Lowassa kuchukua fomu ya kugombea urais katika Ofisi za Tume ya Uchaguzi (NEC), Jijini Dar es Salaam.

Kwenye msafara huo Lowassa ataongozana na mgombea mwenza wake Juma Duni Haji. Lowassa alijiunga na Chadema Julai 28 mwaka huu akitokea Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) huku Duni alijiunga Agosti 4 akitokea CUF.

Msafara huo utaanzia kwenye Ofisi Kuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam saa 3:00 asubuhi ambapo wanachama wa vyama vinavyounda umoja huo (Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF) watakutana na kuanza safari ya kwenda NEC.

Baada ya Lowassa kuchukua fomu NEC, msafara huo utaelekea Makao Makuu ya Chadema yaliyopo Mtaa wa Ufipa, Kinondoni ambapo wateule hao watafanyiwa sherehe ya kupongezwa kwa hatua waliyofikia.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara, Salim Mwalimu akiwa kwenye Ofisi za NCCR-Mageuzi walipofanyia mkutano amesema, wagombea hao wapo tayari.

Akifafanua kuhusu msafara huo amesema, wagombea hao watasindikizwa na viongozi wa UKAWA, wanachama wa umoja huo pamoja na wananchi watakaojitokeza kumsindikiza Lowassa.

Kuhusu suala la ugawanywaji wa majimbo baina ya umoja huo Mwalim amesema
“tumeshamaliza kila kitu na tumeshagawana ila bado kutangaza tu muda ukifika tutawatangazia wananchi”.
Mbali na hilo Mwalimu ameongelea kuhusu mbinu za wizi zinazofanywa na NEC kwa kushirikiana na Chama tawala (CCM) ambapo amedai kuwa kumekuwa na malalamiko mengi toka kwa wananchi ambao wanafanyiwa udanganyifu.
“Kumekuwa na wizi wa waziwazi unaofanywa na CCM na tunasikitika kuwa tume ipo kimya ikionesha kuridhia na matendo hayo. Vijijini watu wanaombwa namba zao za vitambulisho vya kura na watu wanaodai wametumwa na serikali, sisi tumegundua tayari.
“Namba ya kitambulisho ni mali ya mwananchi na sio ya serikali wala tume. Tumegundua mbinu zote zinazofanywa na CCM ili waendelee kubaki madarakani ila wakae wakijua mawimbi haya hayawezi kuzuilika kwani Ukawa ni chaguo la wananchi.”
Kuhusu kuachia ngazi kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amesema, kuondoka kwake hakuwezi kubomoa Ukawa wala kusambaratisha CUF.
“Ukawa bado tupo hai wala hatutapoteza muda wetu kukaa kumlilia aliyejitoa kwani yawezekana mwezetu hana ndoto ya matumaini ya kushika dola, anapenda tubaki chini,”
“Nawapongeza sana CUF kwa kuweza kulichukulia wepesi hilo na kutomjali kwa kujiuzulu kwake kwani hakujaharibu chochote. Sisi bado tunasonga mbele na Jumatatu tutawasha moto Ofisi Kuu ya CUF.”
Naye Tozzy Matwanga ambaye ni Katibu Mkuu wa NLD amewataka wanachama wa chama hicho wote wajitokeze kwa wingi siku hiyo katika msafara wa kwenda NEC.
“Pia tunaomba serikali kuimarisha ulinzi pale unapohitajika. Hivyo hivyo kwa NEC wasimamie haki na misingi ya kazi yao kwani damu ya wananchi ikimwagika wao ndio kitakuwa chanzo.”
via MwanaHALISI Online 

Maalim Seif azungumzia uamuzi wa Prof. Lipumba
Katibu Mkuu wa CUF na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad amesema ameshangazwa na sababu zilizotolewa na Profesa Ibrahim Lipumba aliyejivua uenyekiti wa chama hicho, kuwa amechukizwa na kitendo cha kukaribishwa kwa makada wa CCM ndani ya Ukawa.

Akizungumza na wanachama wa CUF makao makuu ya chama hicho Buguruni, Dar es Salaam juzi usiku, Maalim Seif alimtakia kila la kheri profesa huyo mtaalamu wa masuala ya uchumi na kusisitiza kuwa chama hicho kitaendeleza malengo ya kuanzishwa kwake, ikiwa ni pamoja na kushika dola.

Profesa Lipumba, mmoja wa waasisi wanne wa Ukawa-Umoja wa Katiba ya Wananchi unaoundwa na vyama vinne vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi alichukua uamuzi huo juzi na kwamba amejitahidi kuvumilia ujio wa makada wa CCM ndani ya Ukawa, lakini ameshindwa.

Wengine walioongoza harakati za kuasisi Ukawa ni Freeman Mbowe, ambaye ni mwenyekiti wa Chadema, James Mbatia wa NCCR-Mageuzi na Emmanuel Makaidi wa NLD.

Profesa Lipumba, mmoja wa wenyeviti wanne wa Ukawa na mwenyekiti wa wenyeviti hao, aliyeeleza sababu za kumkaribisha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenye umoja huo takribani siku 10 zilizopita, amejivua wadhifa huo kutokana na vyama hivyo kukubali kupokea watu walioshiriki kukataa Rasimu ya Katiba iliyopendekezwa na wananchi, kitu ambacho kilikuwa msingi wa kuundwa kwa Ukawa.
“CUF kipo imara na katika mikono salama kabisa. Mimi na viongozi wenzangu tuliobaki tutahakikisha chama hiki kinafikia malengo ya kuundwa kwake, hakuna jingine isipokuwa kukamata hatamu ya dola,” 
alisema Maalim Seif na kushangiliwa na kundi kubwa la wanachama wa chama hicho waliofika makao makuu ya chama hicho usiku kujua hatma ya uongozi na viongozi wao.

Mbali na kumshukuru, alisema Profesa Lipumba ndiye mwasisi wa Ukawa na alikuwa mwenyekiti wa wenyeviti wa Ukawa, kusisitiza kuwa alikaa na wenzake (wenyeviti wenza wa Ukawa) na kukubaliana kumkaribisha Lowassa ndani ya Ukawa.
“Na yeye ndiye aliyeanza kumsafisha mzee Lowassa. Nasema kwamba Ukawa ipo na imeimarika. Kwa kumuingiza Lowassa na nguvu za pamoja za vyama vinavyounda Ukawa ikiungwa mkono na wananchi wote wa Tanzania, Magufuli (John) hataiona Ikulu ya Kigamboni,” 
Wakati akitangaza kujivua uenyekiti, Profesa Lipumba alipoulizwa sababu za kugeuka wakati yeye alikuwa ni miongoni mwa wenyeviti wa Ukawa waliomkaribisha Lowassa, alikiri akisema kuwa suala la rushwa na ufisadi ni mfumo ambao lazima uondolewe lakini kwa sasa “dhamira yangu na nafsi yangu vinanisuta.”

Katika maelezo yake ya juzi usiku, Maalim Seif alisema ana uhakika Ukawa itachukua dola kwa maelezo kuwa haitarudi nyuma na si dhamira yake kurudi nyuma.
“Lowassa ana msamiati wake kuwa kushindwa kwake mwiko, lengo letu ni moja tu, vyovyote itakavyokuwa tushike hatamu ya dola,”
 alisisitiza Maalim Seif.
Kikao cha Dharura

Wakati hali ya sintofahamu ikiwakumba makada wa chama hicho, uongozi wa CUF umeitisha kikao cha dharura cha Kamati ya Utendaji ya Taifa na Baraza Kuu la Uongozi ili kutafuta mwanachama atakayekaimu nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Lipumba kitakachofanyika kesho.

Tamko hilo limetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Ismail Jussa Ladhu, na kuwahahakikishia wanachama, wapenzi wa CUF na wananchi wa Tanzania kwamba chama hicho hakitayumba.

Alisema katika historia yake, CUF imepita katika dhoruba na misukosuko mingi, lakini mara zote imeonyesha uwezo mkubwa wa kuhimili na kukabiliana na athari zake.

via gazeti la Mwananchi