Umewasikia hawa "Kama siyo juhudi zako Kikwete, Lowasa tungem..."


Rafiki yangu Jakaya Kikwete ameuharibu uchumi wa nchi yetu - Lowasa
EDWARD Lowassa, mgombea urais wa Tanzania kupitia CHADEMA amesema, Rais Jakaya Kikwete ameharibu uchumi wa Tanzania.

Akizungumza na wafuasi wa Chadema pia UKAWA katika ofisi za Chadema mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho amesema, 
“rafiki yangu Jakaya Kikwete ameuharibu uchumi wa nchi yetu,”
“Wakati Rais Mkapa anaondoka madarakani kilo ya sukari ilikuwa Sh. 600 leo ni Sh. 2,300. Mchele ulikuwa Sh. 550 leo ni Sh. 2,300. Sembe ilikuwa Sh. 250 leo ni Sh. 1,200.”
Aidha Lowassa amesema, katika kipindi cha utawala wa Rais Kikwete ndipo wanyama wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya Tanzania.
“Katika utawala wa Rais Kikwete, tembo wameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia duniani kote.
“Kila aina ya mnyama ameuwawa kuliko kipindi chochote katika historia ya nchi yetu. Nitaijenga serikali yenye uchumi kwa speed (kasi), ambaye hawezi akae pembeni” 
amesema Lowassa.

Utafiti: Kahawa itakulinda na magonjwa ya moyo - Dk Ndosi & Mndeme


Imeandikwa na Dkt Mwidimi Ndosi & Bw Mathew Mndeme, Uingereza -- Utafiti uliofanywa nchini Korea na mtafiti Choi na wenzake na kuchapishwa mwezi Machi kwenye jarida la kisayansi liitwalo Heart, umechangia sana kuondoa utata uliokuwepo kwa muda mrefu kuhusu ubora au madhara ya kiafya yatokanayo na unywaji kahawa. Utafiti huo ambao ni mkubwa sana ulihusisha zaidi ya watu elfu ishirini na tano (25,000) umeonesha unywaji wa kahawa hadi vikombe 5 kwa siku husaidia kupunguza maradhi ya moyo.

Kahawa inajulikana kwa kuongeza kasi ya mapigo ya moyo kitu ambacho kinaweza kuchangia kuongeza shinikizo la damu, lakini pia kahawa husaidia kushusha shinikizo la damu kwa kupanua mishipa ya damu mwilini na kupunguza maji mwilini kwa kupitia mkojo. Wataalamu wengi wa afya kwa muda mrefu wameshauri kinyume na unywaji wa kahawa na kuonya kwamba inaweza kupelekea kuleta magonjwa ya moyo.

Shirika la kukinga na maradhi ya moyo nchini Marekani (American Heart Society) liliwahi kutoa mapendekezo yake mwaka 2008 na kushauri watu wasitumie kahawa ili kujikinga na madhara ya moyo. Utafiti wa sasa ni mkubwa sana na wenye ushahidi wa kisayansi usio na shaka kiasi kwamba imebidi mamlaka husika nchini Marekani mwaka huu warekebishe mapendekezo yake ya lishe na kusema watu wasiogope tena kunywa kahawa. Taarifa hii yenye ushauri mpya imechapishwa mwezi Februari mwaka huu.

Suala la kahawa limewachanganya sana wataalamu wa afya kwa sababu tafiti nyingi zilizofanyika hapo awali zilikuwa na matokea yenye kuchanganya. Nyingine zilionesha madhara ya kahawa na nyingine faida za kahawa. Katika taaluma ya utafiti, kuna utaalamu wa jinsi ya kuchanganya matokeo ya tafiti zote nzuri na kupata matokeo ya ujumla wake (utaalamu huo unaitwa meta-analysis). Hivyo ndivyo walivyofanya akina Mostofsky na wenzake mwaka 2012 Hawa watafiti baada ya kukusanya data zote kwa pamoja, (utafiti uliohusisha zaidi ya watu laki moja na arobaini) waligundua uhusiano kati ya kahawa na magonjwa ya moyo unapochorwa katika grafu unaleta uhusiano usio katika mstari ilionyooka, bali unakuwa wa umbo kama la herufi 'J' fulani. Hii ilimaanisha kwamba, jinsi unavyokunywa vikombe vya kahawa, unapata faida ya kupunguza magonjwa ya moyo. Faida hiyo inaongezeka na kuwa ya juu kabisa pale unapukunywa vikombe 4 kwa siku na unapozidisha vikombe 4 faida hiyo inaanza kushuka. Kwa wale wanaokunywa vikombe 10 kwa siku na zaidi, basi hawapati faida tena bali hasara maana uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo unaanza kuongezeka.

Utafiti huu mpya wa Choi na wenzake uliofanyika mwaka huu umetoa majibu yanayokubaliana na utafiti wa akina Mostofsky na wenzake wa mwaka 2012. Ushauri wao ni kwamba watu wanywe kahawa kwa furaha ila wasizidishe vikombe 4 au 5 kwa siku.

Matokeo ya utafiti huu yanaleta habari njema sana, kwanza kwa wanywaji wa kahawa ambao kwa muda mrefu walidhani wanadhurika kwa kunywa kahawa; pili furaha kubwa inakuja kwa wakulima wa kahawa nchini maana watajua kwamba zao la kahawa wanalojishughulisha nalo sio tu linawapa mapato bali pia linaleta faida mwilini. Habari hii njema itawatia moyo waendelee kulima kahawa kwa wingi na ubora zaidi maana kinywaji hiki kitaendelea kuhitajika sana duniani.

Pamoja na habari hizo njema zitokanazo na utafiti huu, angalizo mbili zinatakiwa kuzingatiwa: kwanza, inabidi wanywaji kahawa wasizidishe kiwango kilichoshauriwa na wanasayansi. Pili, pamoja na kwamba utafiti umeonesha kahawa inaweza kukinga magonjwa ya moyo, haimaanishi kwamba kahawa ni dawa ya kuponya magonjwa hayo. Kwa hiyo wale ambao tayari wana magonjwa ya moyo, inabidi wafuate ushauri wa madaktari wao na wasiache kuzingatia kumeza dawa zao na kufuata maelekezo mengine waliyopewa.

Mwishoni tunawashauri wataalamu wa afya wasome utafiti huu mpya kwa undani ili waweze kutoa maelezo sahihi kwa wananchi ili kuondoa hofu zisiyo za msingi kisayansi.

Unaweza kupata undani wa utafiti huu mpya kuhusu kahawa kwa kusoma machapisho tuliyoorodhesha hapa chini.
 1. Yuni Choi, Yosoo Chang, Seungho Ryu, et al. (2015) Coffee consumption and coronary artery calcium in young and middle-aged asymptomatic adults. Heart. Published Online First 2 March 2015. http://heart.bmj.com/content/early/2015/02/06/heartjnl-2014-306663
 2. Elizabeth Mostofsky, Megan Rice, Emily Levitan, et al. (2012). Habitual Coffee Consumption and Risk of Heart Failure A Dose-Response Meta-Analysis. Circulation: Heart Failure, 5(4), 401-405. http://circheartfailure.ahajournals.org/content/5/4/401.long
 3. The 2015 Dietary Guidelines Advisory Committee (2015). Scientific Report of the 2015 Dietary Guidelines Advisory Committee. http://www.health.gov/dietaryguidelines/2015-scientific-report/
 4. Douglas Schocken, Emelia Benjamin, Gregg Fonarow, et al. (2008). Prevention of heart failure A scientific statement from the American Heart Association councils on epidemiology and prevention, clinical cardiology, cardiovascular nursing, and high blood pressure research; Quality of care and outcomes research interdisciplinary working group; and functional genomics and translational biology interdisciplinary working group. Circulation, 117(19), 2544-2565. http://circ.ahajournals.org/content/117/19/2544.long
Waandishi wa makala hii.
 • Dkt Mwidimi Ndosi ni Mtafiti wa huduma za afya na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Leeds Uingereza. 
 • Bw Mathew Mndeme ni Mtafiti wa matumizi ya mifumo ya TEHAMA katika huduma za afya na pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kura za maoni CCM: Ahukumiwa jela miaka 3 kwa kujeruhi

MKAZI wa Kijiji cha Ishunju, wilayani Missenyi, Sikitu Filemoni (27), amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kutiwa hatiani kwa kumsababishia mwenzake ulemavu wa kudumu.

Hukumu hiyo ilitolewa Ijumaa iliyopita na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Gera, Allen Ifunya, ili iwe fundisho kwa mshitakiwa na watu wengine wanaoshindwa kutawala hasira zao.

Ilielezwa mshitakiwa alimrukia Dafroza Severian (41), mkazi wa kijiji hicho na kumng’ata mdomo, kitendo kilichosababisha kuondoa kipande cha mdomo wa chini, hivyo kupata ulemavu wa kudumu.

Ilielezwa mahakamani kuwa, Agosti 4 mwaka huu, wanawake hao walikuwa wakibishana kuhusu matokeo ya kura ya maoni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyofanyika Agosti Mosi, ikuhusu udiwani katika Kata ya Ishunju, ambapo mgombea aliyekuwa akipendwa na mshitakiwa alishindwa, hivyo kujihisi kuwa anazomewa na mwenzake, ndipo alipomrukia na kumng’ata.

Baada ya kusomewa mashitaka, mshitakiwa alikiri kutenda kosa hilo.

Hakimu alimhukumu kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela, adhabu itakayoanza kutumikiwa baada ya kuthibitishwa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya.

Katika matokeo ya kura ya maoni ya udiwani kwenye kata hiyo, Msafiri Nyema maarufu Matelefoni, aliibuka mshindi kwa kupata kura 477, akiwabwaga Murshid Ibrahim (388) na Vincent Kamugisha (190).

Rais Kikwete awasili Dodoma kuongoza vikao vya Kamati


Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa, baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma, ambapo ataongoza vikao vya Kamati ya Maadili na Kamati kuu ya CCM vitakavyofanyika katika ukumbi wa White House Makao Makuu Dodoma. Kushoto ni Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, alipowasili leo Uwanja wa Ndege mjini Dodoma. Katikati ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa.


Mwenyekiti wa CM, Rais Jakaya Kikwete akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mwenyekiti wa CCm mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa alipowasili leo mjini Dodoma.

Watanzania 7 wateuliwa kuwa Wajumbe wa Kamati CAF

Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la mpira barani Afrika (CAF ) kilichokutana mwishoni mwa wiki jijini Cairo nchini Misri, kimewateua watanzania saba kuwa wajumbe wa kamati zake mbali mbali kwa kwa kipindi cha miaka miwili 2015-2017.

Walioteuliwa pamoja na kamati zao katika mabano ni:
 1. Leodeger Tenga - (Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya fainali za Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa Kamati ya Ushauri na Vyama Wanachama).
 2. Jamal Malinzi - (Mjumbe kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20)
 3. Mwesigwa Selestine - (Mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya Miaka 17).
 4. Richard Sinamtwa - (Mjumbe Kamati ya Rufaa)
 5. Dk Paul Marealle - (Mjumbe Kamati ya Tiba)
 6. Lina Kessy - (Mjumbe ya Soka la Wanawake)
 7. Crescentius Magori - (Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la Ndani)
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania - TFF linawapongeza wajumbe wote walioteuliwa kuingia katika kamati mbali mbali na linawatakia kila la kheri wanapoiwakilisha nchi yetu.

Waliowahi kuwa viongozi CCM Mbeya na Bukoba wahamia CHADEMA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM katika Manispaa ya mji wa Bukoba,  Diwani wa Kata Kahororo, Chief Kalumuna amejiunga rasmi na CHADEMA, Agosti 10, 2015.

Mkoani Mbeya, aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoani humo Regnald Msomba pamoja na aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Kyela, George Mwakalinga, wametoa kadi za CCM kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya Joseph Mwachembe maarufu kwa jina la China, na kuhamia CHADEMA.

Taarifa ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuhusu 'uzushi'

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasikitika kuwepo kwa taarifa za uzushi ambazo zimesambaaa kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ataongea na vyombo vya habari kuhusu msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.

Habari hizi si za kweli na tunaomba kuueleza umma wa Watanzania kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais, hausiki na taarifa hizo zilizoenea kwenye mitandao ya Kijamii na wala hajapanga tukio lolote la kukutana na waandishi wa habari na wala hana mpango wa kuzungumzia msimamo wake ndani ya Serikali na Chama Cha Mapinduzi.

Aidha tunatumia nafasi hii kuwataka wale wote wenye tabia ya kuvumisha taarifa zisizo sahihi kwa maslahi yao waache kufanya hivyo kwa kuwa ni kosa kisheria. Tunawaomba waandishi wa habari kufuata taratibu za kazi na kutafuta taarifa sahihi kwenye vyombo vinavyohusika na kutambulika.

Boniphace Makene
Mwandishi wa Habari wa
Makamu wa Rais
10/8/2015


Lowasa achukua fomu NEC za Urais wa Tanzania 2015


Hakuna alietaka kupigwa na tukio hili.

NCCR-Mageuzi yaanza kushambulia Vunjo


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha NCCR-Mageuzi Taifa, Hemed Msabaha akizungumza wakati wa mikutano wa kutamburisha wagombea wa nafasi ya udiwani inayofanyika katika jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro.

New video: Fred Swagg ft Baraka da Prince - Kikomo


Mwigulu Nchemba ataja "Kikosi cha Ushindi CCM"


Kilele cha maadhimisho ya 23 ya Wiki ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama Kitafifa


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akitoa hotuba ya kuhitimisha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa kwenye viwanja vya Nane Nane Nzuguni Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki.Picha na John Banda wa Pamoja Blog.


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Margreth Mussa wa shule ya msingi Maria de Matias baada ya kushinda shindano la kuandika insha ya lishe na unyonyeshaji wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nane Nzuguni Mkoani Dodoma


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akimkabidhi zawadi Bi. Lilian Simon mmoja ya wakina mama walionyonyesha watoto wao kwa kufuata maelekezo ya wataalamu na kuwezesha watoto wao kuwa na afya bora na kukua vizuri.


Kikundi cha ngoma za asili ya kigogo cha zepisa Hombolo kikitumbuiza wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nanne Nzuguni Mkoani Dodoma.


Vijana wa bendi ya muziki ya Winners ya Mjini Dodoma wakionesha ufundi wa kusakata muziki wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nanne Nzuguni Mkoani Dodoma.


Bi. Lilian Simon akiwa amembeba Mwanae Dorcas David (3) akipongezwa na Vijana wa bendi ya muziki ya Winners alipotoa ushuhuda wa faida ya kumnyonyesha mtoto wake maziwa ya mama pekee hadi alipofikisha umri wa miezi sita na baadae kuendelea hadi miaka miwili wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nanne Nzuguni Mkoani Dodoma


Bi. Judina Deus Malya akiwa na watoto wake mapacha Noel na Nance Malya (4) mara baada ya kutoa ushuhuda wa faida ya kuwanyonyesha watoto wake maziwa ya mama pekee hadi walipofikisha umri wa miezi sita na baadae kuendelea hadi miaka miwili wakati wa sherehe za kilele cha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nanne Nzuguni Mkoani Dodoma


Baadhi ya Wananchi wa Dodoma waliofika kwenye viwanja vya Nane Nane Nzuguni wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Chiku Gallawa (hayupo pichani) wakati akitoa hotuba ya kuhitimisha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa mwishoni mwa wiki.


Picha ya pamoja baina ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa (katikati), viongozi wa Mkoa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na wamama walionyonyesha watoto wao kwa kufuata masharti ya wataalamu na watoto wao wenye afya bora baada ya kumalizika kwa Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa mwishoni mwa wiki kwennye viwanja vya Nane Nane Nzuguni Mkoani humo.


Picha ya pamoja baina ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma, viongozi wa Mkoa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambao kwa pamoja wameshirikiana katika maandalizi na kufanikisha Maadhimisho ya 23 ya wiki ya unyonyeshaji maziwa ya mama kitaifa yaliyohitimishwa mwishoni mwa wiki kwenye viwanja vya Nane Nane Nzuguni Mkoani humo.

Bandio: Maisha ya sasa, ni kukimbiza 'deathday' kuliko kuikimbia 'birthday'

Mubelwa T Bandio
Mubelwa T Bandio
Na Mubelwa T Bandio

MAISHA. Nimejifunza kuwa hayako sawa. Na naamini huo ndio usawa wake, kwani humu tuishimo hakuko sawa.

Hivyo, haitakuwa sawa kwa maisha kuwa sawa katika "uwanja" usio sawa kwa waishimo.

Na...

Najua nililoanza nalo na nitakaloendeleza halitaeleweka sawa, na huo ni udhihirisho wa usawa wetu, ambao nao hauko sawa.

Leo, Agosti 10, ninapoadhimisha mwaka mwingine katika maisha yangu, naitumia siku hii KUAKISI maisha yangu kuliko kusherehekea.

UKWELI ni huu...

Unasoma hapa kwa kuwa "umekua" na kufikia umri wa kusoma na kuelewa. Huu ni umri wa kusherehekea ama kuadhimisha siku kadhaa za kuzaliwa kwako.

Na, kama unasoma hapa, jambo moja ninaloweza kukuhakikishia ni kuwa UTAKUFA.

Kwa hiyo, kama wanadamu, haya mawili yanakuwa ya lazima. Ukizaliwa, utakufa. Tofauti ya maisha yetu ipo katikati ya haya mawili.

Kama nilivyowahi kuandika, kuwa UTAKUMBUKWA KWA DESHI YA MAISHA YAKO (rejea hapa)

Maishani, nimehudhuria BIRTHDAY(s) na MISIBA mingi tu, na kote nimejifunza mengi kuhusu maisha yetu ya sasa, tuyatakayo na namna tunavyojitahidi kuifikia TAMATI yetu.

Labda funzo kuu nililowahi kushiriki nanyi ni lile nililoliandika HAPA Agosti 22, 2011 baada ya kuhudhuria msiba wa Dada yetu hapa Washington DC.

Maisha yetu ya sasa yanaonekana kuwa ya mchakamchaka, twayakimbiza matumaini na (katika hali ya kushangaza) hata siku zaonekana kuwa fupi kuliko awali.

Kabla hujajipanga, ni kesho, ni juma lijalo, ni mwezi ujao na mwaka bila kukamilisha mengi uliyoamini ungependa kuyakamilisha katika muda uliojipangia.

Ninapoangalia miaka hii niliyoishi, naiona kuwa mingi sana. Si kwa kuwa nimeishi mingi kuzidi wote, bali kwa kuzingatia ni mara ngapi nimekuwa nikiamini nimefika mwisho wa uhai.

Nakumbuka kusoma makala ya Kaka Eric Shigongo, iliyosema kuuona mwaka mpya ni nafasi ya ziada. Na naamini katika hilo.

Mara kadhaa (na ni zaidi ya moja) nimekuwa kwenye nafasi ya kuona kama kesho ilikuwa mbali na isiyofikika kwangu nikiwa hai. Siku ambayo hunijia akilini zaidi juu ya hilo, ni HII

Lakini leo wasoma niandikalo.

NI NAFASI YA ZIADA katika kuikimbiza "siku ya mwisho"

Nikirejea kwenye kichwa cha bandiko hili,fikra kwamba maisha yetu ya sasa ni kama kuikimbiza kesho kuliko kuifikiria leo na hata jana, kunatufanya tuonekane kuyawaza yajayo kuliko tulikotoka.

Ni hili linalonifanya niamini kuwa, maisha yetu ya sasa yamewekeza katika yajayo. Na kama nilivyoeleza kabla, jambo pekee ambalo sote tuna hakika nalo, ni kifo.

Na ndio maana nikasema, MAISHA ya sasa. Ni kukimbiza DEATHDAY kuliko kuikimbia BIRTHDAY

Anyway!

Nisijesahau kujitakia EARTHday njema.

Najua fika kuwa hongera na shukrani za maisha yangu nazipokea kwa sababu ni Mungu aliyeniweka hai mpaka sasa.

Na ndiye aliyenipa WAZAZI wangu ambao sina ninanloweza kueleza kuhusu nafasi yao maishani ikalingana na walilotenda.

Labda jambo moja tu, kwamba walinibariki na NDUGU ambao uwepo wao umekuwa kama egemeo la kukua kwangu. Hawa ndugu wameniwezesha kuambatana na JAMAA ambao kwa muongozo wa ndugu, wameniwezesha kuwa nilivyo. Si unakumbuka kuwa Twachagua maongezi, maongezi yachagua mawazo na mawazo yatuchagulia jamii? (Isome hapa)

Nina maRAFIKI ambao wananisaidia katika kukua kwangu. Hawa nawajumusha na wale wanajiona kama maadui kwangu, ambao mara nyingi wamenifanya kujitahidi kukamilisha mambo ili wasipate la kusema.

Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa

Kipekee, namshukuru mke wangu mpenzi Esther na wanangu Paulina na Annalisa kwa kuwa wavumilivu kwenye harakati zangu (nyingine hazielewekagi yaani)

Hahahaaaaaaaaaaaaaa

Ni siku nyingine ya kukumbuka kuzaliwa kwangu. Nalikaribia hitimisho la maisha, na nikilijongelea, najitahidi kukamilisha dhumuni yangu ya kuwa humu duniani.

Mungu akubariki na kuonyeshe namna muafaka ya kutenda kila lililo jema, kadhi uikaribiavyo.

New audio: Dat ft Yunar - Kanulinuli

Vacancy:Challenge TB project in Tanzania

KNCV Tuberculosis Foundation

KNCV Tuberculosis Foundation is an international non-profit organization dedicated to the fight against tuberculosis (TB), still the second most deadly infectious disease in the world.