Katuni tulizopata Agosti 11, 2015


2016/2017 Chevening Scholarships now open

Applications for 2016/2017 Chevening Scholarships are now open. Please read the information on this page carefully prior to applying. Applications close on 3 November at 12:00 GMT (midday UK time)

Applications for Chevening Scholarships can only be submitted using the Chevening online application system, available through the 'apply' button on this page.

Prior to starting your application for a Chevening Scholarship please ensure you have the following ready:

Essential:
  • Two references to be provided in a letter format and written in English
  • Valid passport/national ID card
  • University transcripts (undergraduate, postgraduate)
  • Three different UK Master's course choices
Please note that only documents in PDF format can be uploaded and documents cannot be over 5MB in size.

Optional:
  • English language (if already met the requirements) 
  • UK Master's university offer (if already met the requirements)
You can submit your initial application without these optional documents and upload them to your application at any point up to 14 July 2016.

Please note that if you are eventually conditionally selected for a Chevening Scholarship, it is essential that you provide evidence that you meet the Chevening English language requirements and that you have at least one offer from an eligible course before 14 July 2016 in order to remain in the process.

Application guidance
It is recommended that you read the guidance below to help you submit an eligible application.
Source for more info: www.chevening.org/apply

Taarifa ya kuibwa kwa stakabadhi za malipo ya Serikali

Ofisi ya Madini, Kanda ya Mashariki Dar es Salaam inautangazia Umma kwamba, usiku wa Jumapili ya kuamkia tarehe 03-08-2015 wezi walivunja Ofisi ya Madini Kanda ya Mashariki iliyopo Upanga, Dar es Salaam na kuiba vitu mbalimbali vya Ofisi vikiwemo vitabu vya Stakabadhi za malipo ya Serikali.

Katika tukio hilo, stakabadhi namba ERV 6361601-6361800, na ERV 6361201, 6361202, 6361203, 6361204 ziliibwa.

Aidha, vitabu vipya vinane (8) vyenye Stakabadhi namba 6360201-6360400, 6360401-6360600, 6360601-6360800, 6360801-6361000, 6361001-6361200, 6361205-6361400, 6361401-6361600 na 6361801-6362000 viliibwa, kuharibiwa na kutupwa nje ya ofisi ya madini.

Kwa taarifa hii, tunautangazia Umma kwamba stakabadhi zote zilizoibwa na kuharibiwa hazitumiki na malipo yote yatakayofanyika kupitia stakabadhi tajwa hapo juu yatakuwa ni batili.

Tunaomba yeyote mwenye taarifa sahihi zitakazoweza kusaidia kukamatwa kwa wezi husika kutoa taarifa katika Ofisi ya Madini au kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu.


Imetolewa na:
Kamishna Msaidizi wa MadiniKanda ya Mashariki – Dar es Salaam

TBS notice to all motor vehicle importers


Taarifa ya TBS kwa waagizaji wa magari kutoka nje


SUA - Bean Project job opportunity: Lab Tech


Kalulunga: Hawajui wanachokitaka zaidi ya Lowassa na Magufuli

Kizazi...Nini kipimo chake? Wakati? Mazingira ama Nyenzo?

Labda wapo wanaoshangaa kuwa mtu na mzazi wake wanahesabika kuwa watu wa vizazi tofauti licha ya kwamba wote wako hai.

Wengine wanakubali kuwa wao na wazazi na wazazi wa wazazi wao ni vizazi tofauti licha ya kwamba wote wako hai.

Lakini wapo ambao pengine bila kufikiria wanaamini kuwa kila uzao ni
kizazi. Naamini wote wapo sawa bali hisia za tafsiri ndizo tofauti.

Na pia wapo ambao wanaamini kuwa yachukua miaka mingi kutoweka kwa kizazi kimoja kwenda kingine kwani kila siku si tunasikia muziki huu wa "bongo flava" ukiitwa muziki wa kizazi kipya?

Hata kama anayeuimba amevutiwa na muziki miaka michache iliyopita baada ya kumsikiliza "mkongwe" ambaye (kwa tafsiri "yao") si mtu wa kizazi chao?

Hujasikia wasanii wakirudia nyimbo za miaka kadhaa iliyopita na kusema wamezirudia katika muziki wa kizazi kipya katika harakati za kutenga kizazi cha "remix" na muziki halisi? Achana na hayo...

Napenda kuanza rasmi maana ni siku nyingi hamjasikia michapo ya
tafakuri kutoka huku nyikani. Nianze kwa kusema kuwa katika uchaguzi wa mwezi Otoba 25 mwaka huu, kutakuwa na changamoto kubwa sana haijalishi nani atashinda.

Unapoangalia mwelekeo wa siasa za Tanzania unagundua kuwa zinaendeshwa kwa hisa zaidi badala ya uhalisia.

Kwa sasa zimebakia siku si chini ya 75, watanzania wengi wameendelea kujadili majina ya watu badala ya kujadili sera ama wakitakacho katika serikali ya awamu ya tano.

Wanajadili kuhusu Prof. Ibrahim Lipumba, Dkt. Wilbroad Slaa, Dkt. John Magufuli na Edward Lowassa na viongozi wengine, hali ihii inaonyesha ni jinsi gani ukionacho nje hakiko ndani hata kama unashangiliwa ama kuzomewa.

Kwanini nasema siasa za Tanzania zinaendeshwa kwa hisia badala ya uhalisia? Jibu lake ni kwamba kuna mifano hai. Mmoja wapo ni kule jimbo la Muleba mkoani Kagera, Prof. Anna Tibaijuka alijiuzulu uwaziri na akazomewa jimboni kwake lakini kwenye kura za maoni amepigiwa kura na kushida.

Hali hiyo inatuonyesha kuwa watanzania bado tunaendesha siasa kwa hisia ambazo mwangwi wake auakisi uhalisia, yaani kilichopo nje sicho kilichomo ndani mwetu kutokana na kutojua tukitakacho.

Tukitazama suala la aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kuhamia Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni suala ambalo utagundua kuwa kuna tatizo la jamii nzima ambalo linaongozwa na hisia.

Hisia hizo ni zile ambazo zinahusisha njia za (short cut) ili angalau
kuweza kufikia kwenye mafanikio ya kushika nchi na zinaonyesha ni jinsi gani ambavyo vyama vya upinzania havijajipanga vema kushika dola.

Licha ya kuonyesha kuwa wapinzani hawajajipanga, wanapaswa kupongezwa kwa kuchukua njia ya Short cut kwa kumpata Lowassa na Jusa ingawa ni (risk) kubwa sana kwao ingawa mtu yeyote anayeogopa risk huwa hafanikiwi.

Nasema wamechukua risk kwasababu wao chini ya Dkt. Slaa ndiyo walikuwa wa kwanza kumchafua Lowassa kuwa ni fisadi na wameendelea kumtaja hadharani kuwa ni mmoja kati ya viongozi wa CCM ambao si wasafi, lakini leo wameamua kumchukua na wameahidi kumsafisha chini ya kauli ya kisiasa kuwa katika siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu.

Nilipata shida kidogo baada ya Lowassa kuingia Chadema na viongozi wa chama hicho kipya kwa mwanachama mpya Lowassa waliposema CCM ndiyo tatizo wala si Lowassa.

Lakini wakasahau papo hapo kuwa Lowassa ameutangazia ulimwengu kuwa yupo ndani ya CCM tangu mwaka 1977 akimaanisha malezi na makuzi ya kisiasa anayaishi ya mfumo wa CCM.

Hapo inaleta shida kuhusu uelewa wao wa kufikiri na kuaminika maana hatujui kesho watasema nini na ninakumbuka maneno ya zamani kuwa kuna watu walifundishwa uongo kutoka katika matumbo ya mama zao.

Siasa zetu nazidi kusisitiza kuwa zimejawa na hisia kwasababu watu hawayatazami yote hayo bali kushabikia na kubeza.

Jambo hilo nalifananisha na mpira unapochezwa kisha timu moja wapo ikashinda watu wakashangilia basi mtu ambaye alikuwa hajui kuwa hata mchezo ulichezwaje naye anainuka kushangilia na hata kufikia kubishana na wengine kupigana kwa ushabiki wa michezo ambayo hata hawahusiki moja kwa moja.

Lililotokea kwa Lowassa nafananisha na hali ya maisha ya kawaida ya jamii zetu ambapo yule aliyezoea kuitwa mhalifu kisha siku moja akaamua kwenda kanisani na kuwaambia waumini akiwemo Mchungaji kuwa ameokoka na siku hiyo anahitaji kuhubiri injili hakika sina uhakika kuwa atakataliwa bali anapewa nafasi ya kuhubiri.

Ikumbukwe kuwa, Lowassa siyo wa kubezwa kama ambavyo baadhi ya wana CCM wanavyombeza.

Nasema hivyo kwasababu licha ya wanaoonekana kutoka CCM na kujiunga na Chadema kuwa wamemfuata yeye, lakini ikumbukwe bado wafia dini iitwayo Lowassa ndani ya CCM wamebaki na ni wengi.

Baadhi ni wale wanaojiita Friends of Lowassa, wapo. Wanaendeleza harakati za ushindi wa Lowassa ndani ya CCM. Kuna wengine walimpenda na wanaendelea kumpenda bure. Wengine wapo serikalini na mashambani.

Wote hao kura zao sina imani kuwa zitaenda kwa Magufuli wa CCM, bali wengi watampigia Lowassa bila kujali itikadi za siasa.

Ni wakati sasa wa watanzania kuanza kujiuliza kuwa tunataka nini badala ya akili zetu kuzielekeza kuwa tutampata nani.

Ninaamini kuwa, endapo wazo la kwanza kwa kila mtanzania litakuwa ni tunataka nini, basi wazo la pili litakuwa tumpate nani ili asimamie kufikia malengo tuyatakayo.
  • Imeandikwa na GORDON KALULUNGA via blog

Taarifa muhimu kutoka TFF Agosti 11, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI - RELEASE NO. 142

TAREHE 11 AGOSTI 2015

KIKOSI cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kimeanza mazoezi katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

Wachezaji wa Taifa Stars chini ya kocha wake mkuu Charles Mkwasa watakua wakijifua mara mbili kwa siku asubuhi na jioni katika uwanja wa Karume katika kujiweka fit na maandalizi ya mchezo huo.

Kufuatia baadhi ya wachezaji kuwa na majukumu na timu zao kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Hisani utakaochezwa Agosti 22, Mkwasa amewaongeza wachezji wengine kumi (10) kutoka katika orodha yake ya akiba.

Lengo la kambi hii ya awali ya siku tano, ni kocha mkuu pamoja na benchi lake la ufundi kupata nafasi ya kuwaona wachezaji katika mazoezi hayo kabla ya safari ya kuelekea nchini Uturuki Agosti 23 mwaka huu kwa kambi ya siku kumi.

Wachezaji walioitwa na kuanza mazoezi leo ni Said Mohamed, Vicent Andrew (Mtibwa Sugar), Mohamed Hussein, Ibrajim Hajibu (Simba SC), Hamis Ali, Juma Mbwana (KMKM), Tumba Sued (Coastal Unioni), Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Ibrahim Hilka (Zimamoto– Zanzibar) na Mohamed Yusuf (Prisons).

Wachezaji wengine waliopo kambini ni Said Ndemla, Hassan Isihaka, Abdi Banda(Simba SC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Orgeness Mollel (Aspire Academy) na Abdulhaman Mbambi (Mafunzo).

TWIGA STARS KUIVAA HARAMBEE STARLETS

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) iliyopo kambini kisiwani Zanzibar, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Wanawake kutoka Kenya (Harambee Starlets) Agosti 23, 2015.

Mchezo huo wa kirafiki utachezwa katika uwanja wa Aman Kisiwani Zanzibar, ikiwa ni sehmu ya maandalizi ya kikosi hicho kujiandaa na fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofayika nchini Congo-Brazzavile kuanzia Septemba 4 – 19, 2015.


Twiga Stars inaendelea na mazoezi kutwa mara mbili katika viwanja vya Aman na Fuoni chini ya kocha wake mkuu Rogasian Kaijage kujiandaa na fainali hizo za michezo ya afrika, wachezaji wote waliopo kambini wapo katika hali nzuri wakiendelea kujifua na michezo ya Afrika.

USAJILI Dirisha la usajili limeongezwa toka tarehe 06 Agosti hadi tarehe 20 Septemba, baada ya muda huo klabu itakayochelewesha kuleta usajili wake itatozwa kiasi cha shilingi laki tano (Tsh 500,000) kwa kila mchezaji itakayemsajili mpaka siku ya tarehe 30 Agosti.
Mwisho wa kufanya uhamisho wa kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao TMS ni tarehe 6 Septemba.

Kikao cha kamati ya sheria kitakaa tarehe 28 kwa ajili ya kuupitisha usajili na kitakaa tena tarehe 8/9/2015 kwa ajili ya kupitisha usajili.

Kuanzia tarehe 21 hadi 27 itakuwa ni wiki ya pingamizi, ambapo majina yatabandikwa TFF Karume na kuwekwa kwenye mtandao ili kuwezesha vilabu vyenye pingamizi kuwawekea wachezaji mapingamizi.
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza tarehe 12 Septemba 2015, Daraja la kwanza (FDL) ikitarajiwa kuanza Septemba 17 na Ligi Daraja la pili inatarajiwa kuanza Oktoba 16 mwaka huu.

MICHUANO YA COPA COCA-COLA 2015

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) bado linaendelea na mazungumzo na wadhamini wa michuano hiyo (Coca-Cola). Kutokana na mazungumzo hayo, ratiba ya michuano hiyo itachelewa kutoka.

Hivyo, tunawaomba kuwa na uvumilivu wakati mchakato wa mazungumzo hayo yanayokaribia ukingoni ukiendelea.

UAMUZI WA KAMATI YA RUFAA YA TFF JUU YA RUFAA YA DR. DEVOTA JOHN MARWA,YA MAAMUZI YA KAMATI YA UCHAGUZI WA SOKA LA WANAWAKE (TFF)

Mwomba rufani, Dr. Devota John Marwa, (Mrufani) ni msomi mbobezi katika taaluma ya michezo, akiwa ni mhadhiri katika kitengo kinachojihusisha na taaluma ya michezo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Akiamini kwamba anakidhi vigezo vilivyowekwa kwa nafasi ya mgombea uenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake(TWFA), alichukua fomu ya kuomba kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama hicho.

Maombi hayo yalikumbana na pingamizi zilizoletwa na wakereketwa wawili wa soka la Wanawake, Bi. Chichi Mwidege na Bi. Mwajuma Noty, ambao kwa pamoja walimwekea pingamizi Mrufani, kwamba hakidhi matakwa ya kanuni za ugombea wa nafasi ya Mwenyekiti.

Waleta mapingamizi walidai kuwa Mrufani hakuwa na sifa zilizoainishwa katika Kanuni za Uchaguzi za T.F.F. (TFF Electoral Code) Ibara ya 9 (tisa) kipengele cha 3 (tatu), kinachomtaka mgombea awe amejihusisha na uongozi wa mpira wa miguu kwa muda usiopungua miaka mitano.

Aidha Ibara ya 28 (ishirini na nane) kipengele cha 3 (tatu), kinamtaka mgombea awe amejihusisha japo miaka 2 (miwili) katika shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu nchini. Kamati ya Uchaguzi iliridhia mapingamizi hayo na kuliondoa jina la Mrufani katika orodha ya wagombea wa nafasi hiyo ya Mwenyekiti. Rufani hii ni matokeo ya uamuzi huo wa Kamati ya Uchaguzi uliotolewa taraehe 22 Julai, 2015.

Kwa ujumla, sababu za kupinga maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi zinaweza kuhesabiwa kuwa ni mbili. Moja ni iliyojikita juu ya hitilafu katika kuamua kwamba Mrufani hakuwa na uzoefu katika uongozi wa soka kwa muda ulioainishwa. Sabau nyingine ni kwamba Kamati ya Uchaguzi illibua sababu ambayo haikuwa katika Hati ya pingamizi iliyoletwa na Mleta pingamizi.

Wakati ambapo Mleta pingamizi alijikita katika kipengele cha 28(3), Kamati iliibua kipengele cha 28(8), cha Katiba ya TWFA kinachomtaka mgombea awe ametimiza uzoefu wa uongozi wa miaka mitano, ambacho hakikuwemo katika hoja za pingamizi zilizowasilishwa na mleta pingamizi.

Katika kufikia uamuzi wake, Kamati ya Rufani ilizipitia sababu za Mrufani kama zilivyoletwa, na baada ya kusikiliza maelezo ya Mrufani na hoja za Mwakilishi wa TFF, Wakili Msomi Edward Augustino, na imeamua kama ifuatavyo. Tutaanza na hoja ya mwisho.


Je, Kamati ilikuwa sahihi kuibua kipengele ambacho hakikuletwa katika hati ya mapingamizi? Kamati inaweza kuibua kipengele hicho endapo kwa kufanya hivyo, itakuwa imejielekeza katika nia njema ya maslahi ya suala linalozungumziwa.

Sharti jingine ni kwamba hoja hiyo inyoibuliwa isiwe na athari hasi(prejudicial) kwa mhusika. Kaika suala hili hata hivyo, hoja iliyoletwa na Mleta pingamizi, yaani hoja chini ya kifungu cha 28 (3), imeainisha kipindi kifupi cha uzoefu (miaka 2), na hoja iliyoibuliwa na Kamati inahitaji uzoefu wa miaka 5.

Endapo Mrufani angekuwa na uzoefu wa miaka 3 hadi 4, bado angekwama kutokana na hoja iliyoibuliwa na Kamati. Hii kwa vyovyote ingekuwa ni athari hasi (negative impact) katika harakati za Mrufani. Ni vema Kamati zinazosikiliza malalamiko zikajikita kwenye malalamiko yaliyoletwa na wahusika wenyewe. Kama pigamizi lingekuwa liko juu ya kipengele hicho tu, tusingesita kukubaliana na sehemu hii ya rufani. Hata hivyo, takwa la uzoefu wa miaka 5 limeainishwa pia katika Ibara ya 9 (3), ambayo ilikuwa ni sehemu ya mapingamizi yaliyokuwepo kwenye hati ya mapingamizi.

Kwa sababu hiyo, Kamati ya Rufani haioni kama hoja hiyo ina mashiko. Haitaitilia maanani. Hoja kuu ndani ya rufaa hii ni je, Kamati ya Uchaguzi ilijielekeza vema kuhusu suala la uzoefu wa uongozi ulioainishwa na Katiba?

Mrufani ameieleza Kamati ya Rufani mlolongo wa shughuli ambazo amekuwa akizifanya, nyingi zikiwa zimejikita zaidi katika taaluma. Miongoni mwa shughuli hizo ni kuandaa Mpango Mkakati wa kuendeleza soka la wanawake. Mpango huu uliridhiwa na kuwasilishwa Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira Duniani, yaani FIFA.

Maelezo mengine ni kushiriki katika kuongoza timu mbali mbali kule Chuo Kikuu, zingine zikiwa za watoto wadogo ambao baadhi ya matunda yake ni wachezaji walioibukia kwake kama vile Simon Msuva. Alisema zaidi kuwa alishiriki kuandaa warsha ilizoandaliwa kwa ushirikiano kati ya FIFA na TFF.

Aidha. Alisema kuwa amekuwa kiongozi tangu akiwa bado kwenye vyuo vya ualimu, na baadaye alipohitimu na kufanya kazi kama Mwalimu, kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliko mpaka sasa. Akasema, hata alipokuwa Sweden kwa masomo ya juu pia lijihusisha na programu za maendeleo ya soka la wanawake.

Wakili msomi wa TFF akijibu hoja hizo, alikubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi kuwa Mrufani hajaonesha popote kwamba amewahi kuongoza soka, akasema Mrufani ni mtaalamu tu kama msomi, jambo linaloweza kufanywa na msomi yoyote. Akamalizia kwa kuiomba Kamati ya Rufani za Uchaguzi kuitupilia mbali rufaa ya Mrufani kwa kukosa mashiko.

Tofauti na Kamati ya Uchaguzi, Kamati ya Rufani imeona kuwa kwa maslahi mapana ya mchezo wa soka katika ujumla wake, ni vema kuweka tafsiri pana (wide interpretation) juu ya sifa zinazozungumzwa, badala ya kuweka tafsiri finyu (restricted/narrow interpretation) kama ilivyofanya Kamati ya Uchaguzi.

Baada ya kufanya hivyo, kuhusiana na Mrufani, Kamati imeona kuwa ana sifa zinazostahili. Kupitia sababu alizozitoa, na vielelezo vyake, Kamati ya Rufani haina wasiwasi kuwa Mrufani ana uzoefu mbali mbali sio katika soka tu, bali pamoja na michezo katika ujumla wake.

Tumeshuhudia katika maelezo yake kwetu kwamba ushiriki wake katika hatua mbali mbali, japo hakuwahi kuchaguliwa, sio ushiriki wa kitaaluma tu, kama msomi mwingine yeyote. Ni ushiriki wenye dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko/maendeleo katika soka la wanawake. Maelezo

yake kuwa aliaandaa programu ya maendeleo ya soka la wanawake, hayakupingwa. Kamati ya Uchaguzi ingeangalia namna ambavyo “visheni” iliyomo katika programu ile ambavyo ingeweza kutekelezwa na mtu aliyeaiandaa. Kwa hiyo, katika hoja hii, Kamati inakubaliana kuwa Mrufani anazo sifa stahiki, na kukatwa kwa sababu hii, Kamati ya Uchaguzi haikujielekeza vema. Kwa hiyo, Mrufani ameshinda rufaa yake? Kamati ya Rufani inachelea kujibu swali hili moja kwa moja. Utaratibu wa kuwasilisha rufani ulikiukwa, na hapa ndipo rufaa hii inapokwaa kisiki. Chini ya Ibara ya 13 (1) cha Kanuni ya Uchaguzi (Electoral Code), mgombea ambaye hakuridhika na maamuzi, atawasilisha rufaa yake ndani ya siku 3 (tatu) tangu uamuzi anaoupinga ulipotolewa.

Kipengele cha 3 (tatu) cha ibara hiyo kinasema kwamba Mrufani yoyote atakuwa na uhalali endapo rufaa yake imewasilishwa kwa mujibu wa kanuni hizo. Uamuzi unaolalamikiwa ulitolewa tarehe 22 Julai 2015, sababu za rufaa ziliandaliwa tarehe 27 Julai na sababu hizo za rufaa zililipiwa tarehe 28 Julai, 2015. Ni dhahiri kwamba rufaa ililetwa nje ya muda uliowekwa na kanuni, na kwa hiyo inakosa uhalali kisheria na kikanuni.

Japo katika mwenedo na maamuzi yake Kamati ya Rufani za Uchaguzi haifungwi na taratibu za kimahakama, suala la muda wa kuwasilisha rufani sio miongoni mwa mambo ambayo Kamati inaweza kutoyazingatia. Kwa sababu hiyo, Rufaa hii imetupwa, lakini kwa sababu tofauti na zile za Kamati ya Uchaguzi.

Pamoja na uamuzi huu, Kamati ya Rufani za Uchaguzi inapenda kwa namna ya kipekee kumpongeza Mrufani kwa jitihada alizozionesha kutaka kuitumikia TWFA. Ni matumaini ya Kamati kuwa hatokata tama, na kwamba atakuwa tayari, akitakiwa kufanya hivyo, kupitia taalum yake, kushirikiana na wenzake katika jitihada za kuendeleza soka la akina mama lililo na changamoto lukuki.

Imetolewa na,
JULIUS M. LUGAZIYA
Mwenyekiti-Kamati ya Rufani za Uchaguzi
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Rais Kikwete ateua Mtendaji Mkuu TBS; Mabalozi 2, ahamisha 1

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Joseph B. Masikitiko kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kabla ya uteuzi huo Ndugu Masikitiko alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo (TBS).

Aidha, Rais Kikwete amefanya uteuzi wa Balozi mmoja na kuwabadilishia vituo vya kazi Mabalozi wawili kama ifuatavyo:

(i) Lt. Gen. Charles L. Makakala, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe. Kabla ya uteuzi huo Lt. Gen. Makakala alikuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defence College).

(ii) Balozi Wilson Masilingi aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi amehamishwa kwenda kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Liberata Mulamula aliyeteuliwa hivi karibuni kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa. Atakuwa pia anaiwakilisha Tanzania nchini Mexico.

(iii) Balozi Irene Kasyanju aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi kushika nafasi inayoachwa wazi na Balozi Wilson Masilingi.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Agosti 11, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Uteuzi na uhamisho huu unaanzia tarehe 07 Agosti, 2015.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
11 Agosti, 2015

Polepole ndani ya "Mada Moto" akijadili "Lowassa ndani ya UKAWA"Mazungumzo katika "Jukwaa Langu" kuhusu kung'atuka Prof. Lipumba na kukua ufuasi wa LowassaKatika kipindi cha "Jukwaa Langu" Jumatatu ya wiki hii, Agosti 10, 2015, tulijadili kuhusu kung'atuka uongozi kwa Prof Ibrahimu Lipumba na pia kukua kwa ufuasi kwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Edward Lowassa.

Pia, hotuba ya Zitto Kabwe huko Iringa, na mengine mengi.

Ungana na Dj Luke Joe (wa hapa), Rose Chitallah, Shamis Abdul (wa hapa) na Mubelwa Bandio (wa hapa) toka Kilimanjaro Studio, Beltsville Maryland na Jeff Msangi (msome hapa) kutoka Toronto Canada kujadili haya.

Pia, kulikuwa na simu za wasikilizaji kadhaa

KARIBU

Mbowe azungumzia afya yake baada ya kuugua ghafla jana
Habari iliyochapishwa leo kwenye gazeti la Mwananchi inasomeka ifuatavyo:

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana aliugua ghafla akiwa katika maandamano ya kumsindikiza mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho, Edward Lowassa baada ya kuchukua fomu za kugombea urais katika Tume ya Taifa Uchaguzi (NEC).

Mbowe alishiriki katika maandamano yaliyoanzia Makao Makuu ya CUF yaliyopo Buguruni wilayani Ilala kuelekea NEC na baada ya Lowassa kuchukua fomu, mwenyekiti huyo aliendelea na msafara kwenda Kinondoni yalipo makao makuu ya Chadema.

Wakiwa njiani Mbowe na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu walikuwa wamechomoza kwenye gari wakiwapungia wananchi waliojitokeza kwenye maandamano hayo.

Hali ya Mbowe ilibadilika ghafla na aliamua kushuka juu ya gari na kukaa katika kiti, ndipo Lissu na watu waliokuwamo kwenye gari hilo wakaanza kumpatia huduma ya kwanza kwa kumfungua vifungo vya shati lake katika eneo la Kinondoni kwa Manyanya.

Wakati hali ya Mbowe ilipoanza kubadilika msafara wa Lowassa ulikuwa ukielekea katika Uwanja wa Biafra, Kinondoni na magari yalikuwa yakitembea mwendo mdogo kutokana na maelfu ya watu waliokuwa wakiandamana.

Wakati maandamano hayo yakiendelea, gari lililombeba Mbowe likiwa na walinzi wa Chadema walioning’inia milangoni, lilichomoka katika msafara huo ambao ulikuwa umeingia Barabara ya Kawawa na lilikunja kona katika barabara ya kuelekea Mahakama ya Kinondoni kwa ajili ya kumwahisha hospitali na taarifa zilizopatikana baadaye zilieleza kuwa lilielekea katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Akizungumzia hali hiyo, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, alisema kuwa Mbowe yuko salama na anaendelea vizuri.

“Ni uchovu, uchovu, uchovu tu but he is out of danger (hayuko katika hali ya hatari),” alisema Lissu.
Ofisa Uhusiano wa MNH, Aminiel Aligaesha alisema walimpokea Mbowe saa 11 jioni na alikuwa anaendelea na matibabu katika hospitali hiyo, hata hivyo hakutaka kuweka wazi ugonjwa uliokuwa unamsumbua.


Taarifa ya habari ChannelTEN Agosti 10, 2015
CCM yataja majimbo yatakayorudia kura za maoni
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanga nyaraka vizuri kwenye meza kuu, kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kuanza leo, katika Ukumbi uliopo jengo la White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma.

Baada ya kikao hicho kuanza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alitoka ukumbini na kuwaambia Waandishi wa Habari kwamba, moja ya maazimio ya Kikao hicho ni kwamba kura za maoni zitarudiwa keshokutwa Alhamisi, katika majimbo matano ya Ukonga, Kilolo, Busega, Rufiji na Makete ambako yamejitokeza malalamiko na kufika katika vikao vya Chama, kuhusiana na kura za maoni za awali
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili katika ukumbi uliopo jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kuendesha Kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti, 11, 2015 katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuzungua kikao hicho. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula


Kikao cha Kamati Kuu kikiendelea


Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Adam Kimbisa akisalimiana na Mkurugenzi wa Mawasiliano CCM, Daniel Chongolo, baada ya kuwasili kwenye jengo la White House kwa ajili ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo


Mjumbe wa Kamati Kuu, Adam Kimbisa akiwasalimia wajumbe wenzake ukumbini kabla ya kuanza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma. Kutoka kulia ni Shamsi Vuai Nahodha, Zakia Meghji na Dk. Salim Ahmed Salim


Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Huseein Mwinyi, Samia Sluhu Hassan ambaye pia ni Mgombea mwenza kwa tiketi ya CCM na Ameir Pandu Kificho wakiwa ukumbini kabla ya kikao hicho kuanza


Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akijadili jambo na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Mohammed Seif Khatib ukumbini. kushoto ni Katibu wa NEC, Ushirikiano wa Kimataifa, Dr. Asha-Rose Migiro


Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Zakiah Meghji na Dk. Asha-Rose Migiro wakibadilishana mawazo ukumbini


Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi akimsalimia mjumbe mwenzake Dk. Hussein Mwinyi ukumbini.


Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa ukumbini kabla ya kikao kuanzaWajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa na Mzee Steven Wassira wakibadilishana mawazo ukumbiniWajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa na Dk. Emmanuel Nchimbi wakibadilishana mawazo ukumbiniKatibu wa Sekretarieti ya CCM, Anamringi Macha, akiratibu mambo kabla ya kikao hicho kuanzaWajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk. Maua Daftari na Mgombea Mwenza wa CCM, Samia Suluhu wakijadiliana mambo ukumbiniWajumbe wa Kamati Kuu, Katibu w NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Megji walishauriana jambo kabla ya kikao hicho kuanza