Kinachomchagua Rais...

MAANDALIZI ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka huu ni ya kipekee kutokana na kupambwa na mbwembwe nyingi ikiwamo misafara na maandamano makubwa ya wagombea urais. Ni jambo la kujivunia kuona kwamba wananchi wengi wameonyesha mwamko mkubwa wa ushabiki wa kisiasa.

Hadi sasa dalili za awali zinaonyesha kwamba ushindani mkubwa wa kinyang’anyiro cha urais utakuwa kati ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Misafara na maandamano makubwa ya wagombea urais hao vinazidi kuteka akili za wananchi wengi waliogawanyika katika makundi mawili yanayoelekea kulingana; kundi linalomshabikia Lowassa na jingine linalomuunga mkono Dk. Magufuli.

Kutokana na misukumo mikubwa ya hisia za kisiasa, kuna wananchi ambao ukiwambia kuwa Dk. Magufuli ndiye rais ajaye wanaweza kukutoa roho! Vivyo hivyo, wapo wengine ambao wakikusikia unasema njia ya Lowassa kuelekea Ikulu ni nyeupe wanaweza kukutenga katika jamii.

Ukiuliza sababu za wanaoamini kwamba Lowassa atashinda urais watakwambia ni misafara na maandamano makubwa ya watu wanaoonekana kumshabikia. Hata kwa upande wa Dk. Magufuli jibu ni hilo hilo!

Lakini kwa upande mwingine, wapambe wa Lowassa wanamuelezea kwamba ni mwajibikaji na mwenye uamuzi mgumu katika masuala ya umma, hivyo anafaa kukabidhiwa uongozi wa nchi kwa ajili ya kuboresha maisha ya Watanzania kiuchumi na kijamii.

Wengine wanaamini kwamba Dk. Magufuli ndiye anafaa kukabidhiwa mikoba ya Ikulu ya Tanzania baada ya Rais Jakaya Kikwete. Kwamba mgombea huyo ni msafi asiye na kashfa za ufisadi, lakini pia hayumbishwi katika kusimamia misingi ya uwajibikaji kwa umma na kutetea maslahi ya Taifa.

Kimsingi hakuna wa kuwalaumu mashabiki wa pande hizo mbili maana wanatekeleza haki yao ya kikatiba na kidemokrasia ilmradi hawavunji sheria za nchi.

Lakini pamoja na haki hiyo, mashabiki hawa wanapaswa kutafakari vizuri juu ya misimamo yao ya kuamini kwamba misafara ya kifahari na maandamano makubwa ya watu ni kielelezo tosha cha ushindi kwa mgombea urais.

Si sahihi kutumia takwimu za idadi kubwa ya watu katika misafara na maandamano kuwa ndiyo kigezo cha ushindi kwa mgombea, maana mbwembwe za aina hiyo hazimchagui rais. Kinachomchagua rais ni kura zinazopigwa kwa utaratibu uliowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), si vinginevyo.

Tukumbuke kwamba mtu yeyote ana uhuru wa kushiriki maandamano ya wagombea urais, ubunge na udiwani bila kuulizwa kitambulisho. Lakini haruhusiwi kupiga kura za kuchagua viongozi wa nafasi hizo kama hana kitambulisho husika na iwapo atakiuka maelekezo ya NEC.

Hii ni sawa na kusema kwamba katika Tanzania hii, kila mtu, yaani mwenye kitambulisho cha kupiga kura, asiye nacho, mtoto na hata mgonjwa wa akili, wote wana uhuru wa kushiriki maandamano ya wagombea, jambo ambalo ni tofauti na utaratibu wa kupiga kura za kuchagua viongozi wa kisiasa.

Ikumbukwe hata wakati wa ziara ya Rais Barack Obama wa Marekani hapa Tanzania Julai 2013 maelfu ya watu walijitokeza kumlaki, kumwona na kusikia anachosema, ingawa si kweli kwamba wote walikuwa wanampenda wala kumkubali na kumfurahia. Miongoni mwao walikuwapo wanafiki waliochukizwa na ziara hiyo wakiamini kimakosa kwamba alikuja kusaini mikataba ya kuuziwa nchi yetu!

Misafara na maandamano ya wagombea ni sawa na kokoro ambalo wakati mwingine hubeba viumbe wasiohitajika. Kuna watu wanashiriki misafara na maandamano ya aina hiyo wakiwa na dhmira ya kweli ya kuwaunga mkono wagombea, lakini wengine wanakwenda kufanya kazi zisizo za kisiasa kama vile kulinda usalama, kupiga picha, kurekodi video na sauti.

Kwa hiyo, kuamini au kujitumainisha kwamba idadi kubwa ya watu kwenye misafara na maandamano ya wagombea ndiyo kigezo cha ushindi, ni sawa na ndoto za mchana kweupe ambazo daima hazitimii.

Itakuwa jambo la maana kama mashabiki na wapambe wa kisiasa watazingatia umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kupiga kuza za kuwachagua wagombea wanaowataka kuliko kujiridhisha na wingi wa watu katika maandamano ambayo hayana nafasi ya kuchagua viongozi.

Kuamini kwamba idadi kubwa ya watu kwenye misafara na maandamano ya wagombea ndiyo kigezo cha ushindi ni dhana potofu na matokeo yake mwisho wa siku upande unaoshindwa katika uchaguzi hudhani umeibiwa kura, na wakati mwingine hugeuka kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani usiyo wa lazima.

Jambo la msingi zaidi kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu ni kuongeza juhudi za kuhamasishana (kwa wenye vitambulisho waliojiandikisha kwenye dafrari la kudumu la wapigakura) kujitokeza kwa wingi kupiga kura za kuchagua viongozi tunaowataka siku ya Jumapili Oktoba 25, mwaka huu.

Sambamba na hilo, wananchi wote tunapaswa kushiriki mikutano ya kampeni za wagombea kutoka vyama mbalimbali vya siasa ili kuwachuja na kubaini wanaofaa kutuongoza baada kusikia sera na ilani za vyama vyao.

Ingawa baadhi ya wananchi imani zao zimejikita kwenye vyama, lakini ni vizuri zaidi kuchagua mtu kwanza, chama baadaye kwa sababu maendeleo na mabadiliko tunayoyataka yataletwa na viongozi watu, siyo vyama ambavyo daima haviwezi kufanya chochote.

Lakini pia, tushirikiane kuuombea Uchaguzi Mkuu ujao baraka za Mungu ili ufanyike kwa uhuru na haki. Tuombe tukitambua kwamba mshindi wa uchaguzi huo atakuwa ni yule aliyepigiwa kura nyingi kwa utaratibu halali, si vinginevyo. Mungu ubariki Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015.

Imeandikwa na CHRISTOPHER GAMAINA

Katuni Ijumaa Agosti 14, 2015Nakala ya waraka wa makubaliano ya UKAWA
Polisi yasitisha maandamano wakati wa kurejesha fomu NECJeshi la Polisi nchini limetangaza kusitisha maandamano ya aina yoyote wakati wote wa zoezi la kuchukua fomu za kuwania urais, kutafuta wadhamini mikoani na hata wakati wa kurejesha fomu kwenye tume ya taifa ya uchaguzi.

Uamuzi huo umetokana na kile polisi ilichosema ni sababu za kiusalama, hasa baada ya kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa wa sheria za usalama barabarani kutokana na misafara mirefu iliyohusisha watu waliokuwa wakitembea kwa miguu, magari, pikipiki na baiskeli wakati wakiwasindikiza wagombea wa vyama vya Chadema na CCM.

Naibu inspekta Jenerali wa Polisi D/IGP Abdulrahman Kaniki akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam amesema manung'uniko na usumbufu uliojitokeza wakati za zoezi la wagombea urais wa CCM na Chadema kuchukua fomu tume ya taifa ya uchaguzi ni miongoni mwa sababu zilizosababisha kusitishwa maandamano hayo.

Akizungumzia kuhusiana na uamuzi huo huenda ukatafsiriwa kuwanyima haki wananchi ya kuamua kushiriki kwenye shughuli za kisiasa, Naibu inspekta Jenerali wa Polisi anafafanua zaidi.

Hivi karibu wagombea wa nafasi ya urais wa vyama vya CCM na Chadema wakiambatana na wafuasi wao walisababisha baadhi ya shughuli kwenye maeneo kadhaa jijini Dar es salaam kusimama kwa saa kadhaaa kutokana na maandamano yaliyokuwa yakielekea kwenye ofisi za tume ya taifa ya uchaguzi kwa ajili ya kuchukua fomu.
 • video: ITV, maaandishi: ChannelTEN

First-ever Investment Plan for Tanzanian Diaspora - Jubilee and R&R
Press Release
Jubilee InsuranceTanzania  and R&R Insurance Brokers introduce the first-ever Investment Plan for Tanzanians living in the Diaspora


Dar es Salaam – 12th , August, 2015…R&R Insurance Brokers Limited (R&R) in partnership with Jubilee Insurance companies in Tanzania announced the first-ever Investment Plan cover that combines both Life Insurance and Repatriation (Funeral) cover for Tanzanians living in the diaspora.

OMCTP ni neema kwa waombaji leseni za madini nchini

Afisa Madini Mkazi- Njombe, Samwel Ayubu (kulia) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo kwa wachimbaji Madini wa Mkoani Njombe kuhusu Huduma za Leseni kwa njia ya Mtandao (OMCTP) mjini Njombe. Wengine ni Maafisa kutoka Kitengo cha Leseni Mjiolojia Mwandamizi, Idd Mganga (kushoto) na Mhandisi Edward Mumba (katikati).
Na Mohamed Saif

Imeelezwa kwamba huduma ya leseni za madini kwa njia ya mtandao itampunguzia gharama na adha za usafiri mmiliki wa leseni za madini kwa kumuwezesha kulipia ada za leseni yake pale alipo.

Hayo yameelezwa hivi karibuni na Afisa Madini Mkazi-Njombe, Samwel Ayubu alipokuwa akifungua mafunzo ya matumizi kuhusu huduma za leseni kwa njia ya mtandao yaani Online Mining Cadastre Portal (OMCTP) kwa wachimbaji wa madini mkoani Njombe.

Ayubu alisema kupitia mfumo wa zamani, wakati mwingine mmiliki wa leseni analazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia ghrama kubwa na vilevile kupata usumbufu usio wa lazima pindi anapohitaji kuhuisha leseni yake ama pale anapokuwa na maombi ya leseni.
“Kwa kupitia huduma hii ya kielektroniki, mmiliki wa leseni ataweza kuepuka changamoto mbalimbali alizokuwa akikutana nazo wakati wa mfumo wa zamani wa uombaji leseni,”
 alisema Ayubu na kytaja manufaa mengine ambayo yanatokana na huduma hiyo kuwa ni kuongeza uwazi na kasi ya utoaji wa leseni za madini kwakuwa waombaji wa leseni wataingiza maombi ya leseni wao wenyewe na hivyo kupunguza tatizo la mlundikano wa maombi kwenye ofisi za madini.

Aidha, Afisa Madini Mkazi huyo aliwataka wachimbaji waliohudhuria mafunzo hayo kuwa mabalozi kwa wale ambao hawakupata fursa ya kuhudhuria mafunzo hayo.
“Kwa mafunzo mtakayoyapata hapa, nawaomba mkawe walimu kwa wenzenu ambao hawakufanikiwa kuhudhuria semina hii,” 
Alimalizia kwa kuwaasa wachimbaji hao kuhakikisha wanatembelea Ofisi ya Madini-Njombe kwa lengo la kupatiwa elimu zaidi kuhusu mfumo huo na vilevile kufika hapo kwa ajili ya kusajiliwa kwenye huduma hiyo.
Watumishi wa Wizara ya Nishati wakiwa katika picha ya pamoja kwenye Ofisi za Madini-Njombe baada ya Mafunzo kwa wachimbaji madini mkoani humo. Watatu kutoka kushoto ni Afisa Madini Mkazi-Njombe, Samwel Ayubu kushoto kwake ni Idd Mganga na kulia kwake ni Mhandisi Edward Mumba.

First in Africa: New Masters degree in public policy


NAIROBI, Kenya, August 13, 2015/African Press Organization (APO)/ -- Public policy practitioners and students in Africa now have a chance to study a specialised masters course offered in twelve universities, and uniquely designed to meet the continent’s needs, which was launched in Nairobi, Kenya today.

See PASGR-MRRP brochure: http://www.apo-mail.org/PASGR-MRPP-brochure.pdf

The course, the first of its kind in Africa, prepares students for careers in diverse fields, including: Government, universities, think tanks, research organisations, civil society organisations, media and development agencies.

The course content was developed by academics from the partner universities, with input from scholars from respected European public policy institutions.

It equips students to identify and address national developmental challenges and issues that affect people in their daily lives, such as security, management of natural resources, hunger, HIV/AIDS and women’s empowerment.

Students taking up the two-year full time course have a choice of two career pathways: Research and Policy Practice.

“The Research option familiarises students with the use of data to undertake policy research or pursue advanced scholarship, while Policy Practice equips students to use research to influence, inform or shape public policy,” said Prof Tade Akin Aina, the Executive Director of PASGR. “MRPP is one of the key pillars of our community of practice and thought working together to build excellence in research, training and higher education for public policy in Africa".

The launch event in Nairobi was presided over by Kenya’s Cabinet Secretary for the National Treasury, Mr Henry Rotich, and the Chief Justice, Dr Willy Mutunga. Other dignitaries at the event were: The deputy chair of the Education Committee in the Kenyan Parliament, Hon Julius Kibiwott Melly, vice chancellors and academics, and PASGR Board member Amb Prof Judith Bahemuka. It was also attended by students already enrolled in the programme, researchers and policy practitioners from NGOs, development partners and PASGR staff.

Speaking before officially launching the programme, Mr Rotich noted that effective public policy could only be a reality if the people in charge possessed a deep understanding of the challenges that face Africa, based on solid and credible research.

“Having seen the course content of this new programme, I have no doubt the MRPP will contribute towards efficient, effective and transparent public policy,” he said. Drawing from his personal experience while beginning his postgraduate studies, Mr Rotich expressed his intent to lead a public service fellowships initiative through which students could seek funding to undertake the MRPP.

The programme has already been rolled out in eight universities where 150 have enrolled, with the first cohort set to graduate next year. It is being offered in Egerton and Maseno universities in Kenya; University of Dar es Salaam and Mzumbe in Tanzania; Jos, and Ibadan universities in Nigeria; and Ugandan Christian and Ugandan Martyrs universities.

Hon Melly challenged governments in Africa to enrol their staff for the new programme and offer opportunities to those students seeking work experience.

“I strongly commend the attention paid to relevance of this course as well as the innovative learning approaches. These are valuable learning lessons for us as we grapple with the dilemma of the mismatch between education and the labour market, and the diminishing quality of education,” he added.

As he launched the programme, Kenyan Chief Justice Dr Willy Mutunga stated that research was key to identifying African interests, and that the continent’s interests should in turn inform Africa’s relations with the West.

Prof Aina thanked the partnering universities for their diligence and contribution to the realisation of the programme.

“The MRPP is working, thanks to the efforts of everybody who has been there throughout the journey — my predecessor, the Steering Committee and PASGR colleagues,” he said. "For us at PASGR, the MRPP is special as one of the key pathways to building the next generation of public policy leaders and researchers in Africa".

Academics and students who spoke during the launch gave accolades to the new programme, observing that it was already transforming teaching and learning at the universities.

They were full of praise for the innovative pedagogy, which embraces interactive teaching approaches, such as simulations, debates, role-plays and project-based learning, field experience and case studies.

“My students are more eager to attend my lectures…” said a lecturer.

Another lecturer reported that lecturers from other faculties were interested in adopting the MRPP teaching method (using e-cases).

For more information and to arrange interviews, please contact:

Wanja Njogah
Email: [email protected]
Tel: +254 729 111 031
+254 731 000 065

Visit www.pasgr.org

Founder universities

The 12 founder universities are: University of Dar es Salaam, University of Ghana, University of Ibadan, University of Lagos, University ofJos, Egerton University, Maseno University, Mzumbe University, Uganda Christian University, Uganda Martyrs University, University ofSierra Leone and University of Botswana.

Feedback on the programme by students and lecturers indicates that the innovative teaching techniques are contributing to improved learning.

Course structure and delivery

The MRPP is a full-time two-year programme covered in four semesters, including field experience and thesis preparation.

The programme entails five courses in each of the two semesters during the first year. This is followed by a long break for field experience in a policy or research institution during which students refine research ideas and start data collection. In the second year, three courses are offered, while the rest of the time is devoted to thesis development.


About PASGR

The Partnership for African Social and Governance Research (PASGR) is an independent, non-partisan pan-African not-for-profit organisation established in 2011 and located in Nairobi, Kenya. Currently engaged in more than 12 African countries, PASGR works to enhance research excellence in governance and public policy that contributes to the overall wellbeing of the citizens.

In partnership with individual academics and researchers, higher education institutions, research think tanks, civil society organisations, business and policy communities both in the region and internationally, PASGR supports the production and dissemination of policy relevant research; designs and delivers suites of short professional development courses for researchers and policy actors; and facilitates the development of collaborative higher education programmes.

Our vision is ‘a vibrant African social science community addressing the continent’s public policy issues’. PASGR’s three core programmes (Research, Higher Education, and Professional Development & Training) bring together the right mix of universities, research institutions, government, policy actors, researchers and academics to:
Establish and sustain partnerships at national/regional and international levels for advancing research, higher education and training;
Facilitate the creation of policy and research communities;
Enhance the institutionalisation of a research culture in Africa’s universities and research organisations; and,
Coordinate a collaborative Master of Research and Public Policy with universities in Africa.

Madhara ya vipodozi vyenye viambato sumu


1. Moja kati a viambato vilivyopigwa marufuku kutumika kama kipodozi ni aina ya “steroids” ambazo kimsingi ni dawa, mfano wa viambato hivi ni pamoja na “Clobetasol” na “Betamethosone” zinazopatikana katika dawa aina ya MOVATE, BETACIRT-N, DIPROSON, GENTRISONE, n.k

2. Bidhaa hizi zinaendelea kutumika kama dawa za cheti (prescription only medicine) na lazima zitolewe kwa wagonjwa wa ngozi kwa kufuata maelekezo ya kidaktari na mfamasia. Hata hivyo, haziruhusiwi kutumika kama vipodozi.

3. Dawa nyingine zilizopigwa marufuku kutumika kama vipodozi nizile za kuongeza makalio na maziwa. Hii ni kutokana na kusadikiwa kuwa huleta madhara kwa watumiaji ikiwa ni pamoja na kuhatarisha kupata ugonjwa wa kansa.

4. Kutokana na madhara hayo ya kiafya na kiuchumi yanayoweza kusababishwa na matumizi ya mikorogo na vipodozi vyenye viambato sumu, TFDA imeweka mifumo ya kiuthibiti wa vipodozi ili kuhakikisha kuwa vipodozi vinatumiwa na wananchi ni bora na salama. Hii ni kwa kuhakikisha kuwa vipodozi hivi havina viambato vyenye sumu vinavyoweza kudhuru afya ya mtumiaji.

5. Mifumo ya uthibiti wa vipodozi inajumuisha usajiri wa vipodozi, udhibiti katika uingizaji, ukaguzi na ufuatiliaji na utoaji wa vibali vya biashara ya vipodozi kama ilivyoainishwa.

MADHARA YATOKANAYO NA MATUMIZI YA VIPODOZI VYENYE VIAMBATO VYENYE SUMU


1. BITHIONOL
Kupata mzio wa ngozi/allergic na athari kwenye ngozi ikiwa itapata mwanga wa jua.

2. HEXACHLOROPHENE
 • Inapenya kwenye ngozi na kuingia kwenye ishipa ya fahamu na kusababisha ugonjwa wa mishipa ya fahamu hasa kichwani.
 • Pia inasababisha ugonjwa wa ngozi na kuathirika kwa ngozi pindi unapokuwa kwenye mwanga wa jua.
 • Kwa watoto wachanga husababisha uhalibifu kwenye ubongo
 • Vile vile ngozi inakuwa laini na kusababisha kupata ugonjwa kama fangasi kwenye ngozi au maambukizi ya vimelea vya maradhi.
3. ZEBAKI (MERCURY)
 • Husababisha madhara ya ngozi, ubongo, figo na viungo, mbalimbali vya mwili
 • Zebaki inapopakwa kwenye ngozi kuweza kupenya taratibu ndani ya mwili na kusababisha sumu yake kuingia kwenye damu na kusababisha madhara mwengi mwilini.
 • Mama mjamzito akitumia vipodozi vyenye zebaki mtoto huathirika akiwa akiwa bado tumboni na huzaliwa akiwa na mtindio wa ubongo.
 • Husababisha ngozi kwa laini na kuwa na mabaka meusi na meupe
 • Husababisha mzio/ allergic wa ngozi na muwasho
 • Sumu iingiapo kwenye mishipa ya fahamu husababisha ugonjwa wa mishipa ya fahamu.
 • Sumu ya zebaki ikiingia mwilini kwa kiwango kikubwa husababisha madhara maka upofu, uziwi, upotevu wa fahamu wa madhara mara kwa mara.
4. VINYI CHLORIDE
 • Inasababisha kansa ya maini, ubongo, mapafu na mfumo wa damu
 • Sumu pia husababisha kuumwa kichwa, ksikia kizunguzungu na kupoteza fahamu
5. ZIRCONIUM
Husababisha kansa ya mapafu na ngozi

6. HALOGENATED SALICYLANILIDE
 • Husababisha mzio wa ngozi mara inapopata mwanga wa jua
 • Husababisha ugonjwa wa ngozi
7. CHLOROQUINONE
 • Kundi zima la vipodozi vya CHLOROQUINONE hutumika kutengenezea vipodozi lakini kiambato ambacho kinachotumika ziaid ni kiambato cha Hydroquinone.
8. HYDROQUINONE
 • Husababisha muwasho wa ngozi, mzio wa ngozi, kansa, kuchubuka kwa ngozi na kusababisha mabaka meusi na meupe.
9. STEROIDS
 • Steroids ni kundi la homoni, homoni hizi hutenganezwa kwenye miili ya binadamy na wanyama. Pia zinaweza kutengenezwa nje ya mwili wa binadamu yaani bandia (artificial). Katika kundi hili, corticosteroids ndizo hutumika sana kama viambato kwenye vipodozi.
 • Steroids zikitumika kwa muda mrefu husababisha madhara mbalimbali kaam, ugonjwa wa ngozi na kutokwa na chunusi kubwa. Pia ngozi huwa nyembamba sana na laini na endapo ngozi itapata jeraha au kufanyiwa upasuaji kidonda hakitapona. Pia husababisha magonjwa ya moyo.
10. CHLOROFORM
 • Husababisha kansa ya utumbo mpana na kibofu cha mkojo
 • Husababisha ugonjwa wa akili na ugonjwa wa mishipa ya fahamu
 • Kwenye ngozi, chloroform husababisha ngozi kuungua, maumivu makali, ngozi kuwa nyekundu sana na kutokwa na vipele.
11. CHLOROFLUOROCARBON (HALOGENATED CHLOROFLUOROALKANES)
 • Husababisha madhara kwenye mishipa ya katikati ya fahamu na hivyo kusababisha mtu kutopumua vizuri
 • Husababisha kichefuchefu, kutapika, kuumwa na kichwa, kusikia usingizi na kusikia kizunguzungu.
12. METHYLENE CHLORIDE
 • Husababisha satarani/kansa (cancer)
 • Husababisha madhara kwenye mishipa ya kati ya fahamu, kwenye maini na kwenye mishipa ya moyo.
Pamoja na madhara ya kiafya yaliyotajwa hapo juu pia kuna madhara mengine ya kiuchumi yanayoweza kuambatana na matumizi ya vipodozi visivyo na ubora na usalama kwa mtumiaji.
 • Kwanza ni gharama za matibabu pale mtu anapopata madhara
 • Lishe kwa watoto na familia kwa ujumla hupungua kwa sababu pesa nyingi hutumiak kununua vipodozi au mikorogo.
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), inapenda kuwaasa watumiaji wa vipodozi na wananchi kwa ujumla kujiepusha na matumizi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kwani huleta madhara ya afya kwa mtumiaji.

Lowasa kutambulishwa Mbeya kesho

Mnamo tarehe 10/08/2015 Ofisi ya Mkuu wa polisi wilaya ya Mbeya ilipokea barua toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inayohusu taarifa ya mkutano wa hadhara utakaofanyika tarehe 14/08/2015 katika viwanja vya Ruanda Nzovwe. Lengo la mkutano huo ni mgombea wa raisi kuomba wadhamini.

Leo tarehe 13/08/2015 jeshi la polisi mkoa wa Mbeya lilikutana na Uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo akiwemo mbunge wa Mbeya Mjini na baadhi ya Madiwani katika eneo la Usalama wa Chama hicho katika ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya na kufanya mazungumzo kisha kufikia makubaliano kama walivyotoa taarifa yao kuwa hakutakuwa na maandamano bali ni mkutano. Hii inatokana na sababu za kiusalama pia kutozuia watumiaji wengine wa barabara hiyo ikizingatiwa barabara kuu itakayotumika ni moja. 

Hivyo basi kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya anatoa rai kwa wananchi kutofanya au kulazimisha maandamano yoyote yawe ya miguu au pikipiki. Hii ieleweke kwamba si maandamano bali ni mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja hivyo. Kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Imetolewa na:
Ahmed Z. Msangi – Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya.


Mgombea Urais wa Tanzania 2015 Edward Lowassa anatarajia kutambulishwa kesho kwa wanachama wa chama chake mkoani Mbeya.

Mwenyekiti wa CHADEMA mkoani Mbeya, Joseph Mwachembe maarufu kwa jina la China, amesema wanachama kutoka wilaya 10 za mkoa huo watafika Jijini Mbeya.

TCRA issues a strong warning to IPP's ITV, Radio One


In the picture above, the Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) Content Committee Chairperson Mrs Margaret Munyagi (left) signs a ruling against ITV and Radio One for allegedly airing ‘false breaking- news’ that the Police Force had forbidden a procession that was meant to escort the presidential candidate aspirant on CHADEMA ticket Mr Edward Lowassa who was to pick nomination forms on 10th August 2015.

Walioteuliwa CCM kugombea Ubunge, Uwakilishi, Viti Maalumu 2015

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akiendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, leo Agosti 13, 2015, katika ukumbi uliopo Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kupitisha majina ya walioomba kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM katika majimbo mbalimbali. Kulia kwake ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein. 

Wenyeviti wa CCM Shinyanga, Dar wahamia CHADEMA
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja ametangaza rasmi kuachana na chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Pamoja naye katika kutangaza hayo ni kada maarufu wa chama hicho, John Guninita.

Mgeja ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, leo ametangaza rasmi kujiunga na CHADEMA mbele ya wanahabari jijini Dar es Salaam ambapo ametumia kauli ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aliyoitoa mwaka 1995 alipozungumzia haja ya chama hicho kujisahihisha kwamba, Watanzania wanahitaji mabadiliko na wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM.

Makada hao wamesema kuwa wamechoka kuona chama kinatumia ubabe na mabavu kuwasimika watu wasio na uwezo wa kuiongoza nchi na kuacha viongozi wenye uwezo jambo ambalo wamesema hawawezi kulivumilia milele.

Mgeja amesema kuwa hali iliyotokea Dodoma katika mkutano wa kufanya uteuzi hali ya Mwenyekiti kuingia na majina yake matano mfukoni na kukataa ushauri wa viongozi na wanachama ni jambo ambalo lilionyesha udhaifu mkubwa ndani ya chama hicho hasa pale walipoamua kutumia silaha na vyombo vya usalama kuwatawanya wanachama waliokuwa wanaihitaji haki itendeke.

Mgeja ni mmoja wa wanachama waliokuwa mstari wa mbele katika kumuunga mkono Edward Lowassa katika mbio za kuomba ridhaa ya CCM kugombea Urais wa Tanzanai 2015.

Akizungumzia mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, John Mgeja amesema kiongozi huyo ni sawa na "learner" anayejifunza kuongoza nchi kwani hajawahi hata kuwa balozi wa nyumba kumi kupitia chama hicho, hivyo watanzania hawako tayari kuwajaribu watu katika nafasi kubwa kama ya Urais.

Mgeja amesema kuwa kama viongozi wa CCM wanahitaji kukijenga chama lazima watengue maamuzi hayo na kuwaomba radhi wanachama wa chama hicho na kisha kuchagua mtu ambaye anaweza kukivusha chama hicho tofauti na hapo chama hicho kinakwenda kufa.

Mgeja amesema kuwa kama wana CCM watahitaji mambo mengine waite mdahalo na viongozi hao wakaseme yale yote yaliyotokea Dodoma.


Mgeja akitangaza kuhamia CHADEMA


Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani )juu ya kungatuka katika chama hicho na kujiunga na CHADEMA katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Kulia ni John Guninita.


Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita akitangaza kujiuzuru katika chama hicho na Kujiunga na Chadema leo majira ya saa tano katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo jijini Dar es Salaam. Kushoto Sheik Rajab Katimba na kulia ni aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja.


Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja akionesha kuwa yeye ni CHDEMA kwa sasa.

Lowasa azuiliwa kwa muda kijijini Maroro

Polisi mkoani Kilimanjaro wakiwa wameuzuia msafara wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea Urais kupitia Chadema na anaeungwa mkono na UKAWA, Edward Lowassa katika kijiji cha Maroro, Wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro, hii leo wakati anakwenda kuhudhuria mazishi ya Kada na Mwasisi wa Chama cha Mapinduzi CCM, mzee Peter Kisumo huko Usangi.


Viongozi wa upinzani waliokua katika msafara huo.

Msafara ukiwa umesimama
Polisi wakiwa wametanda.

Edward Lowassa akizungumza jambo.


Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia akijaribu kuzungumza na Polisi.

Mbatia akifafanua jambo kwa Wanahabari kuhusiana na zuio hilo la Polisi.

Lowassa akizungumza kwa simu huku akiwa na Mbunge wa Moshi Mjini Mzee Philemon Ndesamburo.

Edward Lowassa akizungumza na wanacham wa vyama mbalimbali waliojitokeza kumlaki na kumsimamisha katika eneo la Boma Ng'ombe.
 • Picha: Father Kidevu blog