Rais Kikwete ateua Wenyeviti wa Bodi: RAHCO na KADCO


Ilani ya CCM yakamilika, Hakuna ahadi ya laptop, fedha

Ilani ya CCM 2015
Ndugu Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akielekea kwenye ukumbi wa mkutano kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari, huku akiwa ameshikilia kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 iliyopitishwa jana na Halmashauri Kuu ya CCM mjini Dodoma.

Ilani hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa tarehe 25 Agosti ndiyo itakayotumika kwa kipindi cha miaka 5 ijayo iwapo Chama cha Mapinduzi CCM kitapewa ridhaa na wananchi kuongoza nchi kupitia mgombea wake wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, katika uchaguzi mkuu ujao wa rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu kote nchini Tanzania.

Nape Nnauye amelaani na kuzikanusha taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya magazeti kuandika kwamba Dk. John Pombe Magufuli alinukuliwa akisema atagawa kwa kila mwalimu kompyuta moja na kila kijiji shilingi milioni 50 
"Jambo hili ni uzushi mkubwa kwani Ilani ya Uchaguzi ilikuwa haijakuwa tayari ndiyo imekamilika jana, Mambo hayo hakuna kwenye ilani ya Uchaguzi ya CCM ".
“Hizi ni njama za kufanya CCM ionekane imeanza kampeni mapema wakati hatuwezi kufanya hivyo na tunajua sheria na taratibu za uchaguzi”.
Mkutano huo umefanyika katika Makao makuu ya CCM Ofisi ndogo Lumumba, Ijumaa ya Agosti 14, 2015.
Rais Kikwete katika hafla ya Kongamano II la Diaspora


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mama wa Mitindo Asia Idarous-Khamsin wakati alipowasili hoteli ya Serena jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo kuhudhuria hafla ya Kongamano la pili la Diaspora. Kushoto mwenye kanzu ni Mhe Ali Mzee Ali, Mjumbe wa Bodi ya AICC

Lowasa atambulishwa Mbeya jana, leo kutambulishwa Arusha


Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mapokezi ya mgombea Urais Edward Lowassa kupitia CHADEMA yamekamilika kwa asilimia miamoja na tukio hilo kuliita la kiistoria ambalo litafanyika katika viwanja vya tindigani kata ya kimandolu jijini Arusha siku ya Jumamosi (kesho tarehe 15) (habari, picha na Pamela Mollel wa JamiiBlog)
Edward Lowassa anatarajiwa kupokelewa kwa mapokezi makubwa katika Uwanja wa Ndege wa KIA hadi viwanja vya Tindigani katika Kata ya Kimandolu jijini Arusha siku ya Jumamosi (tarehe 15) ambapo atahutubia wananchi katika mkutano ulioandaliwa na chama hicho.

KKKT yapata Askofu mpya

Askofu Shoo
Askofu Shoo
MAASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamemchagua Askofu Dk. FREDERICK SHOO kua mkuu mpya wa Kanisa hilo.

Uchaguzi huo uliofanyika jana kufuatia kumalizika kwa muda wa uongozi wa wa Askofu Mkuu wa KKKT Dk. Alex Malasusa.

Kabla ya uteuzi huo, Dk. Shoo alikua ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Kaskazini.

Askofu Mkuu Mteule, Dk. Shoo alizaliwa mwaka 1959 na kabla ya uchaguzi huo, alikuwa Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi hiyo kwa miaka 10 kuanzia mwaka 2004.

Alibarikiwa kuwa Mchungaji Desemba 14 mwaka 1986 katika Usharika wa Lyamungo Kati. Kuanzia mwaka 1986 hadi 1988, alikuwa Mchungaji Kiongozi katika Usharika wa Mwika.

Alipata shahada ya uzamili na uzamivu nchini Ujerumani. Alikuwa Mkuu wa Chuo cha Biblia Mwika, mwaka 1995 hadi 2003.

NEC yataja idadi ya wafuasi siku ya kurudisha fomu za Urais, MakamuRais Kikwete azindua Hati za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi, Watumishi


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini Hati za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi, Watumishi wa Umma na Sekta binafsi akishuhudiwa na viongozi wa taasisi na sekta hizo Agosti 14, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiikabidhi baada ya kuweka saini Hati za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi, Watumishi wa Umma na Sekta binafsi akishuhudiwa na viongozi wa taasisi na sekta hizo leo Agosti 14, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam

Hati za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi, Watumishi wa Umma na Sekta binafsi zikioneshwa huku zikishuhudiwa na viongozi wa taasisi na sekta hizo Agosti 14, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam

Mwenyekiti wa Business Round Table, Ali Mufuruki na Mkuu wa BRELA wakisaini kwa niaba ya sekta binafsi na za umma Hati za Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi, Watumishi wa Umma na Sekta binafsi akishuhudiwa na viongozi wa taasisi na sekta hizo Agosti 14, 2015 Ikulu jijini Dar es salaam.
  • Picha:IKULU

Prof. Lipumba arejea

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Rwanda jana. Picha na Said Khami
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba alirejea nchini juzi jioni akitokea Kigali, Rwanda alikokwenda mara tu baada ya kujiuzulu wadhifa huo siku nane zilizopita.

Profesa Lipumba aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) saa 10.10 jioni kwa ndege ya Rwanda Air.


Taarifa ya Polisi Dodoma ya kukamatwa kwa "Daktari feki"

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 14.08.2015

Tarehe 12.08.2015 majira ya 15:00 mchana huko kijiji cha Nyerere Kata ya Hogoro, Tarafa ya Zoissa Wilaya ya Kongwa, mtu aliyefahamika kwa jina na MOHAMED ABDALLAH, Miaka 35, Mkazi wa Katesh Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara alikutwa akitoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa zaidi ya 20 akiwa hana kibali wala leseni ya kutoa huduma hiyo.

Baada ya taarifa za siri kulifikia Jeshi la Polisi, mtuhumiwa alikamatwa katika nyumba ambayo haistahili kufanyiwa shughuli za matibabu ambayo ni mali ya SIKITU MAGOMBA aliko panga katika kijiji cha Nyerere alipopekuliwa alikutwa na dawa za aina mbalimbali zenye nembo ya MSD, Drip 500mls chupa tisa ambazo haziruhusiwi kuuzwa, sindano na baadhi ya vifaa tiba vidhaniwavyo vilipatikana kwa njia isiyo halali.

Aidha baada ya kuhojiwa mtuhumiwa alikiri kutenda kosa hilo na kwamba hana taaluma yoyote ya utabibu na elimu yake ni darasa la saba. Uchunguzi zaidi unaendelea na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Nitoe wito kwa wananchi kuwa makini na kuhakikisha wanatibiwa kwenye Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali zinazofahamika ili kuepuka madhara dhidi ya tiba bandia. Pia wawafichue madaktari feki ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwani unapotibiwa na mtu ambaye hana Utaalam kama Daktari mbali ya kuumwa kwanza hutapona na pili utapata madhara ambayo yanaweza kukuletea madhara ya kudumu na pengine kupoteza maisha.

Imetolea na
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma 
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi - Misime D.A (SACP).


Mtuhumiwa Mohamed Abdallah
Baadhi ya vifaa tiba na dawa

[video] Watch: Kenya blows up heroin-smuggling yachtNAIROBI, Kenya, Aug 14 – Kenya on Friday blew up a yacht seized while smuggling heroin across the Indian Ocean, the Interior Ministry said, as the East African nation tries to crack down on a rise in drug trafficking.

Kenyan police seized the yacht in April after 6.7 kilogrammes of heroin was found onboard, Interior Minister Joseph Nkaissery said in a statement.

“Any vessel, vehicle or plane found ferrying drugs or ivory under my watch will be destroyed,” Nkaissery said, after the boat was sunk off the Indian Ocean coast.

“Kenya will not be used as a transit country nor will it be used as a drug trafficking base.”

Police said the small yacht – called “Baby Iris” – was used to ship drugs from between the Seychelles, Tanzania and Kenya.

It was seized while at anchor in Kilifi, a sleepy Kenyan port, some 70 kilometres north of Mombasa.

It is the second time Kenya has sunk a drug smuggling boat, after President Uhuru Kenyatta watched the scuttling of a merchant vessel found with 377 kilogrammes of heroin in August 2014.

East Africa has become a new route for drug smugglers.

The so-called Smack Track – that leads from Afghanistan to the Makran Coast of Iran and Pakistan and across the Indian Ocean to East Africa – is an alternative to the traditional opium trail via Central Asia and the Balkans.

The path was first revealed in 2010 when police busted four Tanzanians and two Iranians with 95 kilogrammes of heroin in Tanga, northern Tanzania.

Since then seizures have grown exponentially. Last year, nearly four tonnes of heroin was seized by piracy-patrolling warships of the east African coast, almost double the amount found in 2013.

JWTZ yazungumzia taarifa za kuwanyang'anya shahada askari wake

Kanali Ngemela Lubinga (katikati). Kulia ni Msaidizi wa Kanali Lubinga, Meja Joseph Masanja na kushoto ni Kapteni Swaleh Omari.
 Kanali Ngemela Lubinga (katikati). Kulia ni Msaidizi wa Kanali Lubinga, Meja Joseph Masanja na kushoto ni Kapteni Swaleh Omari.
Na Dotto Mwaibale

JESHI la Wananchi Tanzania (JWTZ), limekanusha kuwanyang'anya kadi za kupigia kura maofisa na askari wake kama ilivyodaiwa na mmoja wa viongozi wa chama kimoja cha siasa na kutolewa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Ngemela Lubinga alisema madai hayo siyo ya kweli na kuwa jeshi hilo halijafanya hivyo na wala haliwezi kufanya hivyo.
"Wanajeshi hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama chochote cha kisiasa na kuwa mwanajeshi haruhusiwi kuwa shabiki wa chama chochote cha kisiasa."
Lubinga alisema Jeshi la Wananchi Tanzania linafanya kazi zake kama 'professional state organ duniani na kuwa mwanajeshi anayekiuka huchukuliwa hatua za kinidhamu za kijeshi wala si za kiraia.

Alisema Jeshi la Wananchi Tanzania limesikitishwa na kauli hiyo iliyotolewa na kiongozi huyo.
"Wananchi na viongozi wa kisiasa mnaombwa mfanye kazi zenu za kisiasa na zisianzishwe hoja nje ya maeneo hayo ya kisiasa kwani lugha hizo za upotoshaji zinaweza kuleta hofu, ukakasi na wasiwasi kwa wananchi" 
alisema Kanali Lubinga.

Kanali Lubinga alisema jeshi hilo linaendelea na shughuli zake kama kawaida halipendi litolewe kauli za upotoshaji, kusikoeleweka ufuatwe utaratibu wa kuuliza kupata majibu ya uhakika kwani wananchi wanaimani na jeshi lao.