Mkutano wa majadiliano kati ya Tanzania, Japan kuhusu miradi ya 2015/16

Mhandisi Happiness Mgalulla, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango (aliyesimama) akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa mkutano huo. Kushoto kwake ni Bw. Maduka Kessy, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango. Wengine ni Bibi Florence Mwanri, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango (wa kwanza kulia), Bw. Paul Sangawe, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais Tume ya Mipango (wa tatu kulia)
Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, pamoja na majukumu mengine, inajukumu pia la kuratibu miradi ya maendeleo kwa ajili ya ufadhili wa serikali ya Japan kila mwaka. Maandalizi ya mwaka huu yameshakamilika na mkutano wa majadiliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muuungano ya Tanzania na Serikali ya Japan ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hotel ya Hyatt Regeny, The Kilimanjaro, Dar es Salaam. Majadiliano hayo kwa upande wa Serikali ya Japan yaliongozwa na Bw. Masaharu Yoshinda, Balozi wa Japan nchini Tanzania, kwa upande wa Tanzania yaliongozwa na Mhandisi Happiness Mgalulla, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.

Malengo ya mkutano huo ni kujua hatua iliyofikiwa katika maombi ya ufadhili wa miradi ya maendeleo kutoka Serikali ya Japan kwa mwaka 2014/15, kuwasilisha miradi ya maendeleo kwa ajili ya ufadhili kwa mwaka 2015/16, kujadiliana changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi na kupendekeza hatua za kuchukuliwa ili kuboresha ushirikiano baina ya Serikali hizi mbili. Pia Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, iliwasilisha mawazo ya awali ya Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP II).

Wizara zilizoshiriki katika Mkutano huo ni pamoja na Ofisi Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, na Wizara ya Fedha.

Wizara zingine ni pamoja na Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Chakula na Ushirika, Wizara ya Mifugo na Mendeleo ya Uvuvi, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, na Tume ya Mipango – Zanzibar.

Kwa upande wa Serikali ya Japani taasisi zilizohudhuria ni pamoja na Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, JICA – Tanzania, Makao Makuu ya JICA- Japan na Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan.

Ujumbe kutoka Serikali ya Japan ambao unajumuisha Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, JICA – Tanzania, Makao Makuu ya JICA- Japan na Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan wakifuatilia mjadala kwa makini

Ujumbe kutoka Serikali ya Tanzania wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa kiongozi wa ujumbe huo Mhandisi Happiness Mgalulla, Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango

Bw. Masaharu Yoshinda, Balozi wa Japan nchini Tanzania (wa pili kushoto) akisistiza jambo wakati wa mkutano huo. Wengine pamoja nae ni wajumbe kutoka Serikali ya Japan

Wajumbe wakifuatilia majadiliano hayo kwa umakini yatari kwa kutoa michango yao juu ya mada iliyoko mezani

Nyumbani na Diaspora: Wazazi, Watoto na Matumizi ya mitandao


Viroja vya uchaguzi: Mbuzi, ?HelikoptaMakulilo: A Letter to Myself

Ernest Boniface Makulilo
Ernest Boniface Makulilo
Dear Ernest Boniface Makulilo,

Today is 16th August 2015. It is one of the most important date in my life. On this date, seven years ago (16th August, 2008) I arrived in the United States of America. My dream was a reality. I very much remember when I was in grade school fifth grade to be specific when I “decided” one day I will come and make life in this great nation and live the dream.

Fast-forwarding seven years later, we are not talking of the dream anymore. I have reached all my dreams as a child. All I wanted was to get great education, have a wonderful family and most important to live in USA. I have achieved all of these by being here for seven years. But all these would be of no value, as Bishop Desmond Tutu in Ubuntu says, “a person is a person through other people’s eyes”, if I do not help others, if I do not use my education and exposure to be in the USA help others to reach their dreams too.

I am very much happy myself to be an inspirational to many people in many Developing Countries. I have used all my resources and knowledge to help thousand of students to know procedures on how to apply for scholarships and other opportunities. I have managed to be in touch with many immigrants here sharing our stories and give them some insights to make our lives easy here in USA. When one person achieves something he has dreamed of makes me happy. You cannot succeed in this life alone. Find very close people who can help you, give you a hand when in need to climb the ladder. Use the golden rule in this life. I want other people to help me too.

Special thank you to the Makulilos to be the role model and all support you have given me. I was able to have a dream and went through it. I saw it possible because you knew nothing was impossible under the sun, as long as you work hard and ask God for his blessings.

To my hero in heaven, Mr. Boniface Makulilo, my beloved Baba I have nothing to say. You created one strong family, which has been helping many people in Tanzania and other parts of the world through education. You made your legacy. It’s our responsibility to carry your legacy to the next generation. Rest in peace…we’ll meet in heaven and enjoy life after with Jesus and Angels.

Seven years from now, August 16, 2022: I am very much optimist and motivated. I currently live my dream life. What next? I have to dream further and make all plans to execute them. In years to come, my EBM WHOLESALE, LLC will be one of the strong and successful company in clothing business. Become a millionaire in US Dollars. Owning the mansion…extremely big home for my family. Have a TV Show for scholarship opportunities to help more people to get scholarships overseas and reach their dreams through education. Possess PhD. And most importantly, Family First in all aspects of my life.

Special thanks to: the U.S. Department of State for giving me Fulbright Scholarship, University of San Diego for Joan B. Kroc Scholarship, and Rotary International for Rotary Ambassadorial Scholarship. These scholarships worth more than $100,000 made my path and life in America very smooth.

To my lovely wife, Marie Anna and my crazy little monster Benedikt Fulbright…thank you so much for being part of my life. We have been together in both ups and downs. You have trusted me and loved me so much. I am paying for being the best husband and father. I am with you and promise to love you and support the family no matter what.

Lastly, thank you United States of America. You have been welcoming to almost everybody and that what makes this great nation on Earth.

GOD: Nothing can be achieved without your blessings. You have guided me all these years despite my weaknesses and sins as human being. I promise to be closer and closer to you everyday. Thank you so much. I really appreciate you LOVE. Amen.

Best of luck Ernest Boniface Makulilo in the next coming 7 years (August 16, 2022).

Sincerely,

Ernest Boniface Makulilo
CEO – EBM WHOLESALE, LLC
www.ebmwholesale.com


Maoni ya Mndeme kuhusu aliyosema Polepole katika "Mada Moto" Channel TEN

Maoni yangu juu ya Kauli na Misimamo ya Ndugu Humphrey Polepole katika Kipindi cha Mada Moto Channel Ten


Ndani ya siku kadhaa zilizopita, watanzania wanaofuatilia kipindi ya MADA MOTO cha Channel Ten, wamemshuhudia Mtanzania mwenzetu mzalendo aitwaye Humphrey Polepole (a.k.a HP) akitoa mchango wake wa mawazo kuhusu siasa za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu. HP alinza mjadala huu alipoitwa akiwa mwenyewe kwenye kipindi hicho; kisha kipindi kilichofuata alikua yeye na Mch Msigwa, na juzi alikuwa yeye na Ndugu Julius Mtatiro ambaye kwa mwanachama wa chama cha CUF na mtafiti wa mambo mbalimbali ya kijamii. Mijadala au maoni haya ya Ndugu HP yameleta mijadala mingi na mipana katika mitandao ya kijamii, makundi ya watu na baadhi ya mambo aliyoyaongea yamezagaa kupitia "video clips" kwenye Whatsapp. Binafsi nimeshiriki mjadala kwenye moja ya mawasiliano ya kundi fulani ambalo halipatikani kwa kila mtu na nikaona ni vema mawazo yangu juu ya mjadala huu niyaweka kwenye uwanja mpana zaidi ili yasomwe na wengine ikiwa ni pamoja na Ndugu HP.


https://pbs.twimg.com/profile_images/567230623031377920/NDKZiJyO.jpeg


Nianze kwa kukiri kwamba HP kapata "neema" ya kukubalika na kusikilizwa kwenye jamii kupitia ushiriki wake kama mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Warioba. Katika mchakato huo, HP alijijengea heshima na umaarufu kwa kusimamia hoja na ukweli hata pale kulipokua na kila sababu ya kuupindisha. Hii ni tunu na jambo la kuthaminiwa sana katika ulimwengu wa sasa hasa kwa vijana kama yeye. Pili, nikiri kwamba HP ana uwezo mkubwa sana wa kushawishi, kuhamasisha, kuambukiza hisia kwa hadhira inayomsikiliza na kujenga hoja zenye mshawasha na hivyo ni vigumu sana kutokukubaliana naye katika yale anayoyasema. Ukimruhusu aingie kwenye 18 zake, huna namna nyingine zaidi ya kumsikiliza na mara nyingine kukubaliana naye. Kipaji hiki ni kizuri na nadra kwani wanacho watu wachache.
Hata hivyo niseme kwamba, moja ya kasoro (weakness) ambazo zaweza kujitokeza kwa wazi kwa mtu wa aina ya HP, ni pale ambapo kipaji kilekile chenye manufaa makubwa kinapoweza kutumika kuinyume na hivyo kuweza kupotosha pia badala ya kujenga. Hii yaweza kutokea ama kwa makusudi au kwa kutokukusudia kwa vile pamoja na vipaji vyake bado yeye ni mwanadamu na hana ukamilifu katika mambo mengi hata katika yale anayoyasimamia. Hiki ndicho nilichokiona kwenye mijadala ya Ndugu HP katika vipindi hivi vya Mada Moto. Sina hakika kama nilichokiona kimetokana na umakusudi au ubahati mbaya, lakini kuna namna ambavyo HP katumia nafasi yake isivyo na hivyo kuharibu dhana nzima ya hoja zake na mimi kama Mtanzania mzalendo kama yeye ninashawishika kutoa maoni angu juu ya maoni na mtazamo wake.


Nitatoa maoni au mtazamo (reflection) wangu kuhusu maeneo matatu niliyoyaona yanahitaji ama mjadala au ufafanuzi mbadala wa ule uliotolewa na Bwana HP. Maeneo hayo ni Maadili; Ukweli na Haki; pamoja na dhana ya Mabadiliko na Mageuzi (change and transformation). Leo nitaanza na Maadili.


Katika uwasilishaji wake HP amejitambulisha kama mzalendo, mtetea haki za wanyonge, mkweli, muungwana na mchukia maovu ya aina zote. Hizi ni tunu na sifa njema kwa raia yeyote anayeitakia nchi yake mema. Hata hivyo kujitambulisha kwa sifa hizi na kuziishi kwa vitendo ni mambo mawili tofauti. Katika kumsikiliza na kuchanganua kauli za HP, nimeona kuna utata juu ya kile anachojitambulisha nacho na kile anachokisimamia kupitia kauli na hisia zake. Kwa nini nimesema haya?
 1. HP anatumia vibaya kukubalika kwake mbele ya hadhira ya watanzania kupitia ushiriki wake katika mchakato wa mapendekezo ya katiba. Kwa kuwa kajitambulisha katika misingi ya maadili, kwa maadili hayohayo, sidhani kama ni sahihi kwake kwenda kwenye runinga na kuanza kuchambua uovu wa mtu mwingine kwa nguvu kubwa ya ushawishi wake. Nadhani tafsiri halisi ya maadili, aliyonayo inamlazimisha kutomuhukumu mtu mwingine (raia wa Tanzania) bila vielelezo na kwa habari za kusikia, kuambiwa, na shutuma za kisiasa. Maadili anayoyasimamia, yanamlazimisha kuheshimu na kustahi watu wengine huku akitambua wana haki, uhuru na wanalindwa na sheria kama ilivyo kwake. Kwa kwenda kutangazia dunia ubaya/uovu wa mtu mwingine kwa kigezo cha uzalendo, kupenda maadili, na uanaharakati wake ni kinyume na misingi ya sheria na kimaadili anayoisimamia yeye mweyewe. Nina hakika kabisa kwa uelewa wake HP anajua misingi ya "natural justice" na imani ya dini yake haimpi kibali cha kukalia "kiti cha enzi cha hukumu" kuwahukumu watenda dhambi kwa majina yao. Kama jamii itaanza kuruhusu mambo ya mambo kama haya basi nchi haitakalika maana kwa namna moja au nyingine kila mmoja anajua uovu/ubaya/mapungufu ya wengine. Kama maadili anayosimamia HP ndio haya, basi tutegemee kesho ataibuka na kuanza kumchambua mwingine na mwingine. HP anajua hii ilivyo mbana na inavyoweka kumuumiza mwingine kwani pale Mch Msigwa alipoamua kumtajia shutuma zake, alikua mkali na kutaka kujibu hapohapo kila kitu ingawa haikua sehemu ya mada. HP anafikiri ni watu wangapi watapata nafasi kama yake kwamba wanapohutumiwa ovyo kwenye runinga nao watapata "airtime" kama yake ya kwenda kujibu?


 1. HP angetusaidia watanzania wengi kama mimi ambao kwa miaka mingi tunasumbuliwa na utata wa Edward Lowasa (the question of Edward Lowasa...aka EL). Kwa miaka mingi tumekua tukisikia habari za Mzee Lowasa kwamba ni mtu mchafu, tajiri mwenye pesa nyingi za kununua watu na mengine mengi. Jambo hili limeongolewa kiasi kwamba limeingia ndani mwa masikio ya wengi kiasi kwamba kuna watoto wamezaliwa na leo wana miaka 8 ukiwauliza tafisiri ya neno Fisadi wanasema ni Lowasa. Mimi kama mtu ninayependa kujiaminisha vitu kwa vielelezo (hata kama sio kwa 100%) nimekua nikitamani sana kukubaliana na shutuma na dhana hii dhidi ya mtazania huyu mwenyeji wa Monduli lakini kwa ushahidi/vielelezo.  HP angetusaidia na kututendea haki watu kama mimi kama angekuja na ushahidi unaonesha mambo yafuatayo:
  1. Atutajie sheria ambazo EL amevunja na kumfanya kuwa mtu asiyekubalika kwenye jamii
  2. Maadili ya uongozi aliyokiuka katika nafasi alizopewa
  3. Wizi wa mali ya umma na za wengine alizohusika
  4. Ufisadi alioshiriki na yanayofanana na jinsi alivyoshiriki
  5. Atuambie EL ana mali zisizokua na maelezo (labda mwizi, halipi kodi, kapora mahali, nk)
  6. Atuambie hizo mali ni zipi, ni kiasi gani na ziko wapi
  7. Kisha atuambie hizo njia ovu ambayo Mzee huyo kazitumia


 1. HP kuja tu na shutuma za jumla huku akitumia kipaji na uwezo mkubwa wa kuongea na kushawishi kumpaka raia mwingine matope usoni na kumvua nguo mbele ya familia yake, ndugu zake na watanzania kwa ujumla, ni kinyume kabisa na misingi ya kisheria, haki na kimaadili anayoisimamia HP


 1. Pamoja na namba 2 na 3, HP angetutendea haki sisi wenye udadisi wa kutaka kuujua "ukweli wote" kwa kuziweka shutuma za Mzee EL katika muktadha wa kitaasisi na kisheria (justifications of the stated accusations in the context of intuitional  and legal perspective). Mzee EL ni raia wa nchi hii na yuko chini ya mifumo ya kisheria na kiutawala inayongoza nchi yetu. Nilitegemea Ndugu HP:
  1. Atuambie ni kwa nini huyu mtu anayemwelezea kama mchafu na gwiji ya ufisadi hajawahi chukuliwa hatua za kisheria
  2. Atuambie ni kwa nini serikali na vyombo vyake vimeamua kumfumbia macho mtu mmoja aishi kama vile yuko kisiwani ndani ya taifa linaloongozwa na serikali inayojinasifu kwa utendaji wake na misingi ya sheria
  3. Atuambie ni kwa nini serikali ambayo kiaina inaonekana anaitetea, imehifadhi tu kumbukumbu za uovu wa Mzee EL lakini haimchukulii hatua stahiki ili kuleta usawa na haki mbele ya sheria
  4. Atuambia ni adhabu gani anaipa serikali ambayo inaficha waovu na nani anatakiwa kuwajibisha kwa uovu huu mkubwa wa kuhifadhi waovu
  5. HP haoni kwamba wa kuhojiwa zaidi kuhusu anachokiita uovu na ufisadi wa Mzee EL ni serikali na vyombo vyake ambavyo tumevipa mamlaka ya kisheria kutulidha dhidi ya maovu na waovu?


 1. HP anatumia vibaya nafasi aliyopewa na Rais kwa niaba ya watanzania kuchafua majina ya wengine kwenye jamii. Nadhani nafasi yake kama mjumbe na kamishna wa tume ilikua chini ya kiapo ambapo pamoja na mambo mengine ni kutunza siri na mambo binafsi. Sidhani kama ni sahihi kwake kuja leo na kusema Mwalimu MM alipokuja kwenye mazungumzo ya faragha na tume kwa nafasi yake kama kiongozi alisema muungano uvunjwe au tuhamishie visiwa vya Zanzibar kwenda ziwa Victoria au tupeleke Kisiwa cha Ukerewe karibu na Pemba ili kuimarisha muungano.  Kutumia nafasi yake ya ujumbe wa tume kumsulubisha raia waliyempa nafasi kama kiongozi mstaafu kutoa maoni yake, ni ukiukwaji wa maadili kwa nafasi aliyopewa. Kwa hili namfananisha HP na kasisi anayeletewa kesi za ndoa na mambo mengine binafsi na kisha kwenda kuyatumia baadaye kunapokua na sababu ya kutofautiana na hao aliowasaidia kama mshauri wao. HP amekwenda mbali kudai kwamba sio tu alipata huo muda wa kuongea na EL na kuijua dhamira yake mbaya, bali kwa kuwa alikua serikalini aliona mengi yanayomuhusu EL. Sidhani kama hii ndio misingi ya maadili anayoisimamia na kama ni hivyo kwa nini asiwaulize huko serikali sababu inayowafanya watunze maovu ya EL badala ya kumwajibisha? Je HP kaona maovu ya watanzania wangapi "huko serikalini" alikokua  na kapanga kwenda kuyatumia wapi na wakati gani? Haya ni maadili gani?


 1. HP angetutendea mema kama angetumia uzito wa maneno yaleyale aliyoyatumia kwa Mzee EL kuwasema wote waliopinga matakwa ya katiba ya wananchi. Kule bunge la katiba walikuwepo wajumbe zaidi ya mia nne nadhani ambao kwa mshikamano wao sio tu walipinga aliyoiita "katiba ya wananchi" bali wako waliosindikiza misimamo yao na kaauli za kutisha kidola, matusi na kejeli nyingi dhidi ya walioiunga mkono. HP kapanga na hawa kuja kwenye runinga na kuwachambua uovu wao lini ikiwa ni pamoja na ule aliouona "kule serikalini"?  Najiuliza tu kwamba kwani kazi ya tume ya Jaji Warioba ilikua ni nini? Ilikua ni kukusanya maoni yanayofanana kwa watanzania wote? Na kama ilikua ni hivyo wangeyajuaje na kwa nini walipoteza muda kuwasikiliza ambao walikua na mawazo ya tofauti? Kwani ilikua ni masharti ya Tume kwamba kila anayekwenda akaongee yale yalikubalika na wengi? Mbona Mh Rais wetu alipinga mambo kadhaa kwenye katiba ile hadharani na sijamuona HP akimchambua kwa ubaya na uovu wake kwa kupinga kauli za wananchi? Haya ndio maadili ya Ndugu HP?


 1. HP kajitangaza kama mfalme aliyejitawaza mwenyewe miongoni mwa watanzania (He has declared himself as a self-appointed king). Amejipa uhalali na mamlaka kwamba yeye anaweza kuwaambia/kuwashawishi kitu watanzania na wakamsikiliza. Kwamba watu wengine wafanye maamuzi kwa kuogopa kukosa "support" yake au "kulizwa" na maamuzi yake iwapo hamutamtii. Nani kamwambia kwamba yeye akiikubali CCM au UKAWA au wagombea wao basi watanzania watamsikiliza na kumtii? Yeye ni nani kuiambia timu yenye mapenzi makubwa na panga la "kukata" iliyokua imeketi Dodoma kwamba wafanye maamuzi katika uteuzi wa wagombea ubunge kwa kufuata matakwa yake? Pamoja na uwezo wake na mchango wake mzuri kwenye jamii, nadhani huu ni mtazamo usiyo sahihi kwa kujipa mamlaka na utisho wa kuwapa wengine masharti. Nadhani angetoa mchango mkubwa na wenye heshima zaidi kama mawazo yake yangejengwa kwa hoja na kutuaminisha juu ya yale anayoyasimamia bila vitisho iwapo watu hawatatii mtizamo wake. Kwa lugha ya kawaida mtu atajiuliza HP ni nani hata awe na sauti ya aina hii?


 1. HP kaonesha kwamba hana misingi na hana maadili katika ukamili anayotuaminisha kua nao. Katika tungo yake ya mwisho ya kumalizia kipindi siku alipokua na Mch Msigwa, anasema iwapo CCM watafanya yale aliyoyatamka yuko tayari kumuunga mkono mgombea wao na itakua kinyume chake wasipofanya hivyo. Hii inaonesha kuna shida katika misingi yake. Kwamba mgombea wa chama chetu kikuu anaweza kuwa msafi au mchafu mbele zake kutegemeana tu na iwapo "mamlaka yake ya kifalme aliyojipa" yatasikilizwa na kutekelezwa. Kwenye moja ya makala zake alizoandika kwenye blog yake mara baada ya uteuzi wa Dodoma, ameonesha kabisa kwamba anakubaliana na na uteuzi wa Dr. Magufuli na anamuunga mkono ikimanisha hatambui iwapo ana uchafu kama ambavyo amekua akichambua uchafu wa EL. (rejea hapa: http://hpolepole.blogspot.co.uk/2015/07/ukawa-ni-ama-mpite-katika-tanuru-na.html)
Siku EL apohamia CDM," Profesa wa Elimu aliyebobea na kujulikana na watanzania katika maswala ya kisiasa kuliko ya taaluma yake", yaani Prof. Kitila Mkumbo, alihojiwa na kituo cha BBC na alitakiwa kutoa uchambuzi wake wa tukio lile. Pamoja na mambo mengine, Profesa huyo alisema kitendo cha Chadema kumpokea na kumpa nafasi ya kuwa mgombea mtu ambaye waliwekeza kumchafua wao wenyewe kwa muda mrefu ina tafsi kuu mbili. Moja ni ushindi kwa EL kwamba walimchafua sasa wanamsafisha, na pili ni fundisho kwa Chadema na mwenendo mzima ya siasa za Tanzania zilizojikita katika shutuma za kuokota barabarani. Kwamba watu waache siasa za kuchafuana na kushutumiana ovyo kwa mambo yasiyo na ushahidi na wasiyo na uwezo wa kuyathibitisha pasipo shaka. Nasikitika kwamba tatizo hilo limemvaa HP. Ninaamini HP angeweza kuongelea dhana ya maadili katika uongozi na nafasi yake katika uchaguzi unaofuata bila kumdhalilisha EL au raia mwingine yeyote yule na ingekua na tija zaidi kuliko alivyofanya.


Bila kutazama kauli za kisiasa na mchakato wa uchaguzi ambao hamunyang'anyi mtu haki yake ya kikatiba, ninamtazama Mzee EL kama mtanzania mwingine yeyote yule mwenye haki ya kuheshimiwa, kuthaminiwa na kuhukumiwa anapofanya makosa  kwa misingi ya kitaasisi na kisheria tuliyojiwekea kama taifa. Tunapofurahi leo anachokifanya ndugu HP dhidi ya EL, kesho itakua ni kwa mwingine na mwingine na tunaelewa vema mambo kama haya yatatufikisha wapi. Kuna njia za kuonyesha machungu, mapenzi, na hofu zetu dhidi ya watu lakini nasita kama hii ya HP ni mojawapo tunayoweza kuikumbatia


Nitaendelea na sehemu ya pili.


Rejea:
 1. Siku ya 2 ya Mjadala wa HP na Mch Msigwa: sehemu ya kwanza: https://www.youtube.com/watch?v=-KvqAyxnWkU na sehemu ya pili: https://www.youtube.com/watch?v=fteTqyCOcrI


 1. Siku ya 3 ya mjadala wa HP na ndugu Mtatiro: sehemu ya kwanza: https://www.youtube.com/watch?v=GBhYacfvGuc na   sehemu ya pili: https://www.youtube.com/watch?v=8E-5WxBxzfQ

Mwalimu MM ni mhadhiri Katika kitengo cha Sayansi ya ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mtafiti wa mifumo ya TEHAMA (ICT) katika Huduma za Afya (Health Informatics). Unaweza kuwasiliana naye kupitia [email protected] Blog: http://mwalimumm.blogspot.com

Kingunge avuliwa Ukamanda Mkuu UVCCM

TAMKO LA BARAZA LA VIJANA WA CCM

Baraza kuu la Umoja wa Vijana wa CCM lililokutana tarehe 15.08.2015 katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre, pamoja na mambo mengine liliazimia mambo yafutauo:-
 1. Lilimvua Ukamanda Mkuu ndugu Kingunge Ngombale Mwiru. Maamuzi hayo yalitolewa kutokana na tabia na mwenendo wake wa hivi karibuni kuenda tofauti na maadili na taratibu za CCM. Aidha kikao kimetoa mapendekezo kwa vikao vya Chama Cha Mapinduzi kuuangangalia upya uanachama wake na kuchukua hatua kubwa zaidi.
 2. Kikao pia kiliunda timu ya kampeni ambayo itafanya kazi pamoja na kamati ya utekelezaji kuhakisha ushindi wa CCM kwa nafasi zote.
 3. Kikao kimemshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa hotuba nzuri ya ufunguzi wa Baraza na kikao kimeahidi kutekeleza maagizo na maelekezo ya hotuba hiyo kwa matendo.
Sixtus Raphael Mapunda
Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa

"I have respect for doctors that didn't want drug reps in their office"

The Vaccine Movie You've Been Hearing About! - Bought MovieNEC: Kuahirishwa kuwekwa wazi daftari la Wapiga Kura Dar