One thing you should never say about yourself

That, “I need recognition for my actions to be worthwhile!

Do what you know is right. Integrity is doing the right thing, no matter what, even when nobody’s going to know whether you did it or not. Life always finds its balance. Don’t expect to get back everything you give. 

Don’t expect recognition for every effort you make. And don’t expect your kindness to be instantly recognized or your love to be understood by everyone you encounter. What seems like the right thing to do could also be the hardest thing you have ever done. Do it anyway. 

There is no greatness or peace of mind where there is betrayal of your own goodwill. Always aim at complete sincerity of your thoughts, words and deeds. If it is wrong, don’t do it. If it is untrue, don’t repeat it. Do what you do because you believe it’s the right thing to do. Do the right thing even when nobody is looking. Be one of the people who make a true difference in the world by leaving it a little better and more wholesome than you found it.

- Angel Chernoff

Utalii katika mwambao wa ziwa Nyasa

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa 
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa amesema ili kuimarisha uchumi wa Mwambao wa Ziwa Nyasa Serikali imeamua kujenga karakana ya kisasa ambayo itakuwa na uwezo wa kutengeneza boti kubwa na ndogo.

Wilaya ya Nyasa ina vitega uchumi vingi ikiwemo maliasili kama milima ya Livingstone, ufukwe wa ziwa Nyasa, samaki wa mapambo, pamoja na visiwa ambavyo vinaweza kuwa vyanzo vya utalii.

Pamoja na utengenezaji wa zana za kisasa wananchi wa kijiji cha Chiulu wameiomba Serikali kutazama upya samaki waliopo katika Ziwa Nyasa, wapo samaki ambao hawakui ambao ni pamoja na Vituhi, Unjukwa, ambao hata ukiwapasua utawakuta wakiwa na mayai, hali hiyo ni kuonyesha kuwa hawezi kukua tena, kukataza kuwavua ni kurudisha nyuma uchumi wa wananachi wanaoishi kando kando ya ziwa Nyasa.


Mtumbwi unanesa kwa nyuma huku maji yakiingia; Hilo ni jambo la kawaida kwa wavuvi


Moja ya samaki wanao patikana katika ziwa Nyasa hao ni mbufu na kambale


Hii nimoja ya karakana ya kutengenezea boti za kisasa ambazo zimegharimiwa na Serikali ya Tanzania


Bio Camp Lodge


Wavuvi katika mwambao wa ziwa Nyasa wamesema pamoja na kukosa samaki lakini changamoto nyingine ni pamoja na kukabili kuchomewa nyavu mara kwa mara na Afisa uvuvi wakidai kuwa ni nyavu ndogo jambo linalosababisha kuwaacha wavuvi katika hali ya umaskini.


Karakana ya kutengeneza boti za kisasa imejianda kwa kuweza kununua jenereta za kuweza kusaidia endapo umeme utakatika


Hiyo ni gharama ya vitu utakavyotaka kuvitumia uwapo Bio Camp Lodge


Hali halisi ya Bio Camo Mbambabay. Vitega uchumi kwa ajili ya watalii. Nyumba unazoziona hapo ni za kulala wageni ambazo zinajulikana kwa jina la Bio Camp Lodge Mbamba Bay yenye vyumba zaidi ya 40 na maeneo mengi ya kupumzika na kuburudika na michezo mbalimbali ikiwemo ngoma za asili.

Uezekaji wa Nyumba hizi umetumika zaidi nyasi hivyo pamoja Wilaya ya Nyasa kuna joto lakini eneo hili ni baridi

Mwandishi wa Habari, Judith Lugoye akiwa Bio Camp Lodge


Nyumba vilivyopo vinajitegemea. Kila nyumba ni chumba kimoja


Bio Camp inajali afya za wateja wake. Chandarua unayoiona huzuia mbu ili kulinda afya ya mteja.

Mambo haya tulizoea kuyaona Ulaya lakini kitanda unachokiona kipo Mbambabay kwenye Bio Camp.


Umeme unaotumika hapa unategemea kinyesi cha wanyama (biogas) hivyo umeme haukatiki muda wowote

Sehemu ya II: Maoni ya Mndeme kuhusu aliyosema Polepole

Maoni yangu juu ya Kauli na Misimamo ya Ndugu Humphrey Polepole katika Kipindi cha Mada Moto Channel Ten: Sehemu ya Pili


Nianze kwa kuwashukuru wale wote waliosoma makala niliyoandika jana juu ya mada hii na kuniandikia barua pepe.  Leo ninaendelea na sehemu ya pili ya maoni yangu dhidi ya kauli na misimamo ya Ndugu Humphrey Polepole (HP) aliyoitoa kwa siku tatu mfululizo katika kipindi cha MADA MOTO cha Channel Ten. Katika kipindi hicho, HP alitumia muda wake mwingi kuwashambulia vyama vinavyounda UKAWA na mgombea wao wa Urais Mh Edward Lowasa (EL) kwa hoja kwamba EL ni mchau, fisadi, mwizi, na alipinga katiba ya wananchi hivyo hastahili kuwaongoza watanzania na waliompokea wamepoteza mwelekeo na kukubalika (legitimacy). Katika makala jana, niliainisha kasoro ya kitendo cha ndugu HP, kauli zake na kujichanganya katika misingi ya maadili anayoitetea. Kwa kufanya hivyo, nilisema nitatoa maoni yangu kuhusu kauli zake kwakuchambua maeneo matatu ambayo ni Maadili, Ukweli na Haki, na dhana ya Mabadiliko na Mageuzi ambayo aliizungumzia kwa kirefu katika siku ya tatu alipokua studio na Ndugu Julius Mtatiro. Jana niliandika kwa undani kuhusu dhana ya Maadili ya ndugu HP na kama hukusoma nakushauri urejee kusoma makala ile kabla ya hii kwani nitairejea kama msingi wa nitakachoeleza leo. Inapatikana kwa kubofya hapa. Leo nitaendelea na kipengele kuhusu Ukweli na Haki kama vilivyojitokeza kwenye kauli za HP.
Kamusi ya Kiswahili Sanifu kama ilivyoandikwa na TUKI toleo la 3 la mwaka 2013 inatoa tafsiri au maana 2 ya neno HAKI (mkolezo ni wangu): (1) Jambo ambalo mtu anastahili au kitu anachostahiki kuwa nacho (mfano: mali) (2) Uendeshaji wa jambo kufuata sheria au kanuni zilizowekwa
Kama vile haitoshi, TUKI wameeleza maana ya neno UKWELI kama: (1) Uhakika wa jambo. (2) Maneno mengine yanayofafanua maana ya UKWELI ni Yakini, Ikhlasi,  Unyofu na Uaminifu
https://pbs.twimg.com/profile_images/567230623031377920/NDKZiJyO.jpeg
Nieleze Mambo Matatu:
MOJA:
Katika kumsikiliza Ndugu HP juu ya kile anachokisimamia, nilijiuliza maswali: HP ana HAKI kiasi gani katika hili analolifanya?  Je, anastahili kiasi gani kutumia nafasi yake kuchafua (au niseme kutukana) raia mwingine kwa kigezo cha yeye kutetea maadili? Je, jambo analolifanya analifanya kwa misingi ya kufuata sheria na kanuni za nchi? Ni sheria na kanuni gani ya utawala wa nchi yetu vinampa kibali na ujasiri wa kumchafua mtu mwingine kwa habari zisizo na uthibitisho au kwa nafasi alitopata kuwa karibu na "taarifa za serikalini"? Ni utaratibu gani wa kijamii na kimaadili unampa mamlaka, uhalali  na ujasiri huu?


Jana nilisema HP ana nguvu na uwezo mkubwa sana wa ushawishi na katika uwasilishaji wake anatoa tungo nzito kama vile zilikua zimeandikwa mahali na hivyo ni rahisi sana kukubali kwamba kila anachoongea ni cha kweli. Sina maana kwamba ndugu HP ni mwongo lakini jambo nililojiuliza katika vipindi vile na hasa kwa msimamo wake dhidi ya EL, ni je, HP ni MKWELI kiasi gani? Je, anayoyasema ni KWELI? Na kama ni kweli, tunauthibitishaje ukweli wake wakati kauli zake hazina tofauti na za kisiasa majukwaani (maana hatujawahi sikia za kisheria) kuhusu EL ambazo tumezikia tangu tunapata akili na hana kithibitisho chochote? Kama vile haitoshi, yeye mwenyewe ni mkweli kiasi gani kwa nafsi yake kwamba chuki aliyonayo na anayoipandikiza kwa wengine dhidi ya EL imetokana na mapenzi au misingi ya maadili anayoitetea? Ni kweli kwamba unaweza kutetea maslahi ya nchi kwa gharama ya kumchukia mtu mmoja na kumdhalilisha kinyume na sheria?
http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/10/Joseph-Butiku.jpg
Nimemsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (Mzee Joseph Butiku) katika uwasilishaji wa mada yake kwenye kongamano lililofanyika jana ambalo na ndugu HP alishiriki kama mzungumzaji.


Moja ya sentensi za Mzee Butiku ilikua hii na ninaomba nimnukuu: "Wakati umefika Watazania wawe huru kuzungumza lakini wajifunze kuzungumza kwa mujibu wa wa sheria"
Kuhusu dhana ya haki, sipati mahali panapompa HAKI ndugu HP kutumia vyombo vya habari na mikusanyiko anayopata nafasi kutoa mada au kushiriki midahalo kumchafua EL au raia mwingine yoyote ambaye kwa mtizamo wake hakubaliana naye kimaadili. HP ana haki na uhuru wa kutoa maoni yake juu ya mambo mbalimbali kama sheria na katiba ya nchi inavyomruhusu lakini anafungwa na sheria hiyohiyo kwamba afanye hivyo bila kungilia uhuru na haki za wengine. Sheria inamtaka atumie njia au kanuni tulizojiwekea katika kupambana na mtu au watu ambao kwa mtazamo au ushahidi aliona nao, ni wahalifu na wakosaji kama anavyomuelezea Mzee EL. Sina hakika kama HP alimsikia Mzee Butitu alipotaka kauli hii na kama hakuisikia anaweza kumsikiliza hapa: https://www.youtube.com/watch?v=C-mcSrJdoZI . Ni lazima kufuata sheria katika kuwahukumu watu na hukumu zetu juu yao zijikite katika makosa waliyoyatenda na sio katika UJUMLA WA CHUKI TULIZONAZO dhidi yao kama watu binafsi. Kitendo hiki cha kuchafua wengine hakina tofauti kabisa na wale wanaokamata vibaka na kuamua kuwachoma moto na kuwaua kwa kujichukulia sheria mikononi. Jamii zilizostaharabika kama Tanzania haikubaliana na utaratibu huo hadi pale tutakapobadilisha sheria zetu.


MBILI:
HP kashindwa kuwa mkweli katika uwasiliashaji wa hoja zake. Tabia moja kubwa ya UKWELI (truth) ni kutokua na tafsiri nyingi na kujikita katika uhalisia (reality) katika kiwango chake cha juu kabisa (in the light of its ultimate cause). Ukweli una rangi moja inayokubalika na wale wanaoutambua.  Kama vile haitoshi, mwanadamu anaweza kuusimamia ukweli pale tu anapokua na ufahamu uliotokana na uzoefu sahihi (relevant experience) katika kile anachokitazama kama ukweli (Unaweza rejea machapisho yanazungumzia misingi ya taaluma ya filosofia kujiridhisha). Kw aminajili hii ninachelea kuamini iwapo ukweli wa ndugu HP una siafa hizi. Kwa nini?
Unapomsikiliza katika uwasilishaji wake kujibu hoja za msingi za ndugu Mtatiro juu ya usafi na uchafu wa wanasiasa na hasa EL na mgombe wa CCM, unaona kabisa kwamba tafsiri yake ya ukweli inageuka. Unaona kwa uwazi namna anavyojenga hoja kutetea mgombea wa CCM huku akimkandamiza EL. Unaona jinsi anavyoibuka na tafsiri ya ajabu ya kwamba makosa yanayofanywa na mawaziri hayawahusu wala hayawachafui wao bali yanamchafua Waziri Mkuu kwa kuwa ndio msimamizi wao. Hili ni jambo la ajabu sana kwamba Waziri Mkuu anatakiwa kuwa ama malaika wa nuru au giza kuhakikisha anajua kila kitu kinachofanywa na mawaziri wake na manaibu kila siku katika utendaji wa kazi zao ili kuzuia wasifanye makosa atakayoyabeba yeye huku wao wakibaki salama. HP anatuambia kwamba mawaziri wanaoshutumiwa na matumizi mabaya ya madaraka, ufujaji wa mali za umma, uzembe kazini na kujitanua bila hofu kwa rasilimali za nchi, hawana makosa na ni wasafi kama maji ya chupa maana uovu wao uko kwa kiongozi wao. Kwa tafisiri hii, nilitegemea HP asimamie dhana ya UKWELI kwa kusonga mbele na kusema, Waziri Mkuu ni msaidizi wa Rais na kateuliwa na Rais. Yaani ni mtu Rais aliyemwamini kuliko wote kiasi cha kumfanya kuwa msaidizi mkuu wa utekelezaji wa majukumu yake na hivyo basi naye makosa yake yote na walioko chini yake hastahili kuyabeba hata chembe bali yanakwenda mikononi mwa Rais. Hii ndio tafsiri ya hoja ya HP anapojitahidi kujificha chini ya kivuli cha mikono yake mwenyewe kuhusu maadili na ukweli.
Pili katika hili na kwa kuzingatia sifa ya UKWELI, je huu ndio ukweli wote anaoujua HP? Anachokiita maovu ya EL ndio uzoefu wake wote wa uovu anauojua pia dhidi ya mgombea wa CCM na serikali kwa ujumla? Na kama sio, kwa nini wao haji kuwavua nguo hadharani kama EL? Na kwa nini ukweli wake uwe na tasfiri zaidi ya moja? Kama shida ni "katiba ya wananchi", kati ya EL na serikali yote ya CCM, ni nani amekwamisha katiba hiyo kwa mikono na miguu?
http://api.ning.com/files/6vIMLmuhUcoziHDiqFelayd3rDhFRTYcjfRMnqLereV4fED5H8C16r8yFLe*u99XkLes2hB7avn*oGi0eJlBYptkJQU-6NKQ/WaziriMkuumstaafuEdwardLowassa..JPG?width=650
TATU:
Dhana ya UKWELI na HAKI katika kauli za ndugu HP, inaonekana pia anapozungumzia utajiri. HP anatuaminisha kwamba utajiri ni kitu kibaya na tajiri ni mtu wa kuepukwa na kuogopwa. Anajenga hisia kwamba watu wenye mali kwenye jamii sio watu rafiki kwa wanyonge, sio watu wenye mapenzi mema na taifa lao, sio watu wa kuaminika, ni watu wa kuogopwa na hawastahili kutuongoza. Mojawapo ya chuki ya dhahiri na misingi ya hoja za HP dhidi ya EL ni shutuma kwamba Laigwanani huyu wa kimasai ni TAJIRI KUPINDUKIA. Naita kauli yake kama shutuma maana kwenye makala ya jana nilihoji uhalisia/ukweli wa kauli hii ambayo tumeshauzoea kwa muda mrefu. Nilihoji ni kwa nini HP na serikali, haituambii huyu mtu ana utajiri gani, kiasi gani, uko wapi, umepatikanaje (maana anaitwa mwizi na fisadi) na kwa nini hajashughulikiwa?


Katika hili, nimuulize HP, utajiri ni kiasi gani cha mali? Na je, kwa kuwa tu mimi sijui HP kapata wapi pesa za kununua suti nzuri anazovaa kila mara, basi nina haki ya kumwita mwizi, mla/mtoa rushwa, fisadi? Ni kweli kwamba watu wote wenye mali mitaani tunajua wamezipataje? HP anajua chanzo wa mali za viongozi wote wa serikali na usafi wao? Ukweli wa HP katika dhana ya umiliki wa mali uko wapi? Je, shida ni kumiliki mali au ni kumiliki mali zisizo halali? Na kama mtu anamiliki mali zisizo halali, taratibu na sheria zetu zatuambia nini kifanyike dhidi yake?


Ninamuunga mkono ndugu HP kwamba katika utafutaji wa mali, ni vema sana tukasisitiza maadili na usafi. Ni vema jamii (na hasa vijana) ikajengewa misingi ya kutotamani mali wasizoweza kueleza wametoa wapi; kutamani kutajirika kwa njia yoyote ile kwa haraka; na kuwa waaminifu katika majukumu na kazi zao za kujipatia kipato. Na ili kujihakikishia haya yanatokea ni lazima tujenge misingi imara ya kitasisi na kimaadili mingoni mwa watumishi, taasisi na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha kunakua na udhibiti wa mianya yoyoye inayoruhusu matajiri wa kuibukia kama uyoga.


Pamopja na taadhari hii, katika nchi kama yetu tunayojitambulisha wapambanaji dhidi ya umaskini, tutakua tunajenga dhana potofu sana kuwaaminisha watu kwamba utajiri ni kitu kibaya na cha kuogopwa. Ni hatari sana kuwa na watu wanaomwona kila mwenye mali ni mwizi, fisadi, mkwepa kodi au mnyang'anyi. Kwa kuwa mimi sina mali, hainipi kibali kuwatazama wenye mali kuliko mimi kwamba sio watu waungwana na hainipi kibali cha mimi kuwa mshitaki na hakimu juu ya usafi wao tena nikiwa sina vielelezo. Kufanya hivi ni kutowatenda HAKI wale wenye uwezo wa kifedha/mali na kuwafanya wajione ni watu waovu, wasiofaa na wasiokubalika ndani ya jamii zetu. Kufanya hivi ni kukosa kuwa wakweli kwamba hakuna anayeupenda umaskini na hakuna anayeuchukia utajiri: basi tu maisha ndivyo yalivyo kwamba wengine yamewaendea vema na wengine yamewawekea ukuta, ama kwa kupenda wao au sababu zingine wasizoweka kukabiliana nazo. Mitazamo kama hii ndio inayowafanya hata vibaka kuona kila mwenye kagari kake, au simu, au kanyumba basi amewaibia huko serikalini na hivyo wanaamia kwake kwenda kutwaa kilicho chao. HP hatuambii ukweli kuhusu dhana ya utajiri na hawatendei haki wale wenye utajiri katika jamii yetu.


Nitaendelea na sehemu ya tatu.


Rejea:
  1. Siku ya 2 ya Mjadala wa HP na Mch Msigwa: sehemu ya kwanza: https://www.youtube.com/watch?v=-KvqAyxnWkU na sehemu ya pili: https://www.youtube.com/watch?v=fteTqyCOcrI
  2. Siku ya 3 ya mjadala wa HP na ndugu Mtatiro: sehemu ya kwanza: https://www.youtube.com/watch?v=GBhYacfvGuc na   sehemu ya pili: https://www.youtube.com/watch?v=8E-5WxBxzfQ
  3. TUKI (2013). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press, Oxford


Mwalimu MM ni mhadhiri Katika kitengo cha Sayansi ya ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mtafiti wa mifumo ya TEHAMA (ICT) katika Huduma za Afya (Health Informatics). Unaweza kuwasiliana naye kupitia [email protected] Blog: http://mwalimumm.blogspot.com

When to use Who/Whom - The Comma Queen explains


Ngoma Africa, Asia Idarous-Khamsin katika hafla ya Kongamano II la Diaspora


Ngoma Africa band yenye makazi yake nchini Ujerumani na Mama wa Mitindo Asia Idarous-Khamsin "wamenogesha" hafla ya Kongamano la Pili la Diaspora lililofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Agosti 15, 2015.

Ngoma Africa band walituma CD yenye nyimbo kali mbili za kumuaga Rais Kikwete.

Mama wa Mitindo alifanya onesho maalumu la mavazi ya Kiafrika.

Eat less calories in total to burn fat, lose weight - Study


via The NPR

You may also want to read: This is What Happens to Your Body When You Stop Exercising
and Were Carbs A Brain Food For Our Ancient Ancestors?

Mgawanyo wa UKAWA kwenye Majimbo ya Ubunge 2015

UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI (UKAWA)

MGAWANYO WA MAJIMBO YA UBUNGE KWA VYAMA VINAVYOUNDA UKAWA KATIKA UCHAGUZI MKUU 2015

Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), uliasisiwa wakati wa Bunge Maalum la Katiba mwaka 2014, lengo likiwa kuunganisha nguvu za Wabunge wote wa Bunge hilo kwa ajili ya kusimamia na kutetea maoni ya wananchi yaliyowasilishwa kupitia rasimu ya pili ya Katiba iliyotayarishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

UKAWA ulihusisha wabunge kutoka vyama mbalimbali vya upinzani na baadhi ya wabunge kutoka kundi lililojulikana kama la 201. Baadaye, UKAWA ulibaki na wabunge na Viongozi kutoka vyama vya NLD, NCCR – Mageuzi, CUF na CHADEMA.

Ikumbukwe kwamba viongozi wakuu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) walikubaliana tangu mwaka 2014 kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 UKAWA utasimamisha mgombea mmoja katika kila ngazi ya Uchaguzi kuanzia Rais wa Jamhuri ya Muungano, Rais wa Zanzibar, Mbunge, Mwakilishi na Diwani katika maeneo yote ya nchi.

Azma na ndoto ya viongozi, wanachama wa vyama washirika wa UKAWA na Watanzania ni kuhakikisha Serikali ya CCM inaondoshwa katika majimbo yote, na kuingiza Serikali mpya ya UKAWA.

Baada ya Majadiliano ya muda mrefu, kuhusu kuachiana majimbo ya Ubunge, vyama vinavyounda UKAWA vimefanikiwa kuachiana majimbo kama inavyoonekana katika orodha.

1. Mara

1. Rorya CDM
2. Tarime Mjini CDM
3. Tarime Vijijini CDM
4. Musoma Vijijini CDM
5. Butiama CDM
6. Bunda Mjini CDM
7. Mwibara CDM
8. Musoma Mjini CDM
9. Bunda Vijijini CDM

2. Simiyu

1. Bariadi CDM
2. Maswa magharibi CDM
3. Maswa mashariki CDM
4. Kisesa CDM
5. Meatu CDM
6. Itilima CDM
7. Busega CUF

3. Shinyanga

1. Msalala CDM
2. Kahama Mjini CDM
3. Kahama Vijijini CDM
4. Shinyanga Mjini CDM
5. Kishapu CDM
6. Ushetu CDM

4. Mwanza

1. Ukerewe CDM
2. Magu CDM
3. Nyamagana CDM
4. Kwimba CUF
5. Sumve CUF
6. Buchosa CDM
7. Sengerema CDM
8. Ilemela CDM
9. Misungwi CDM

5. Geita

1. Bukombe CDM
2. Busanda CDM
3. Nyang'wale CDM
4. Chato CDM
5. Mbogwe CDM

6. Kagera


1. Karagwe CDM
2. Kyerwa CDM
3. Bukoba Mjini CDM
4. Bukoba Vijijini CUF
5. Nkenge NCCR
6. Muleba Kaskazini CDM
7. Muleba Kusini CDM
8. Biharamulo CDM
9. Ngara NCCR

7. Mbeya

1. Lupa CDM
2. Songwe CDM
3. Mbeya Mjini CDM
4. Kyela CDM
5. Rungwe CDM
6. Busekelo CDM
7. Ileje NCCR
8. Mbozi Mashariki CDM
9. Momba CDM
10. Mbeya Vijijini CDM
11. Tunduma CDM
12. Viwawa CDM

8. Iringa

1 Ismani CDM
2 Kalenga CDM
3 Mufindi kaskazini CDM
4 Mufindi Kusini NCCR
5 Iringa Mjini CDM
6 Kilolo CDM
7 Mafinga Mjini CDM

9. Njombe

1 Njombe Kaskazini CDM
2 Lupembe CDM
3 Wanging'ombe CDM
4 Makete CDM
5 Ludewa CDM
6 Makambako CDM

10. Rukwa

1 Nkasi Kusini CDM
2 Kwela CDM
3 Nkasi Kaskazini CDM
4 Sumbawanga Mjini CDM
5 Kalambo CDM

11.Tanga

1 Handeni Mjini CUF
2 Handeni Vijijini CUF
3 Kilindi CDM
4 Pangani CUF
5 Tanga Mjini CUF
6 Muheza CDM
7 Bumbuli CUF
8 Mlalo CUF
9 Lushoto CUF
10 Korogwe CDM
11 Korogwe Vijijini CDM
12 Mkinga CUF

11. Kilimanjaro

1. Rombo CDM
2. Same Magharibi CDM
3. Same mashariki CDM
4. Vunjo NCCR
5. Moshi Vijijini CDM
6. Moshi Mjini CDM
7. Hai CDM
8. Siha CDM

12. Arusha

1 Arumeru Mashariki CDM
2 Arumeru Magharibi CDM
3 Arusha Mjini CDM
4 Longido CDM
5 Monduli CDM
6 Karatu CDM
7 Ngorongoro CDM

13. Manyara

1 Simanjiro CDM
2 Mbulu Vijijini CDM
3 Hanang CDM
4 Babati Mjini CDM
5 Babati Vijijini CDM
6 Kiteto CDM
7 Mbulu Mjini CDM

14. Dar es Salaam

1. Ubungo CDM
2. Kawe CDM
3. Kinondoni CUF
4. Ukonga CDM
5. Ilala CDM
6. Temeke CUF
7. Kibamba CDM
8. Mbagala CUF

15. Pwani

1 Bagamoyo CUF
2 Chalinze CDM
3 Kibaha Mjini CDM
4 Kibaha Vijijini CDM
5 Kisarawe CUF
6 Mkuranga CUF
7 Rufiji utete CUF
8 Mafia CUF
9 Rufiji Kibiti CUF

16. Morogoro

1. Kilosa CUF
2. Mikumi CDM
3. Morogoro Kusini CDM
4. Morogoro Kusini Mashariki CUF
5. Kilombero CDM
6. Mlimba CDM
7. Mvomero CDM
8. Ulanga Magharibi CDM
9. Ulanga Mashariki CDM
10. Morogoro Mjini CDM

17. Dodoma

1. Kondoa Mjini CUF
2. Kondoa Vijijini CUF
3. Chemba CUF
4. Kibakwe NCCR
5. Kongwa CDM
6. Dodoma Mjini CDM
7. Bahi CDM
8. Chilonwa CDM
9. Mtera NCCR

18. Singida

1 Iramba Magharibi CDM
2 Iramba Mashariki CDM
3 Singida kaskazini CDM
4 Singida Mashariki CDM
5 Singida Magharibi CDM
6 Manyoni magharibi CDM
7 Manyoni Mashariki CDM

19. Tabora

1 Bukene CUF
2 Nzega Mjini CDM
3 Nzega Vijijini CUF
4 Igunga CDM
5 Igalula CUF
6 Tabora Kaskazini CUF
7 Urambo CDM
8 Kaliua CUF
9 Ulyankulu CDM
10 Sikonge CDM
11 Tabora Mjini CUF
12 Manonga CDM

20. Katavi

1 Mpanda Mjini CDM
2 Mpanda Vijijini CDM
4 Katavi CDM
5 Nsimbo CDM
6 Kavuu CDM

21. Kigoma

1 Buyungu NCCR
2 Mhambwe NCCR
3 Kasulu Mjini NCCR
4 Kasulu Vijijini NCCR
5 Kigoma Kaskazini CDM
6 Kigoma Kusini NCCR
7 Kigoma Mjini CDM
8 Manyovu NCCR

22. Ruvuma

1 Tunduru Kaskazini CUF
2 Peramiho CDM
3 Mbinga Magharibi/Nyasa CDM
4 Mbinga Mashariki/Mbinga CDM
5 Namtumbo CUF
6 Songea Mjini CDM
7 Tunduru Kusini CUF
8 Madaba CDM
9 Mbinga Mjini NCCR

23. Mtwara

1. Newala Mjini CUF
2. Newala Vijijini CUF
3. Tandahimba CUF
4. Mtwara Vijijini CUF
5. Nanyamba CUF
6. Nanyumbu CUF
7. Lulindi NLD
8. Masasi NLD
9. Ndanda NLD

24. Lindi 

1 Mtama CUF
2 Kilwa kaskazini CUF
3 Kilwa kusini CUF
4 Lindi mjini CUF
5 Ruangwa CUF
6 Nachingwea CUF
7 Liwale CUF
8 Mchinga CUF

Mhe. John Mnyika
Kny. Katibu Mkuu – CHADEMA

Mhe. Shaweji Mketo
Kny. Katibu Mkuu – CUF

Mhe. Nderakindo Kessy
Kny. Katibu Mkuu – NCCR

Mhe. Masudi I. Makujunga
Kny. Katibu Mkuu – NLD
---

Katuni na 'meme' za kisiasa tulizopata leo

Picha za "mastaa" wa muziki walivyofanikisha "Democracy in Dar" concertWananchi waliojitokeza katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.Msanii Msagasumu akimwaga sumu kwa wakazi wa Mbagala na Vitongoji vyake waliojitokeza katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.

Shangwe kila kona....

Wasanii wa Bongo Movie nao waliunga mkono harakati za Mabadiliko...

Mhe. Joseph Mbilinyi akiwa na Msanii wa Bongo Moive, Anti Ezekiel.


Wazee wa Isanga Family kutoka Mbeya nao hawakuwa nyuma kutoa ujumbe wao katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.


Msanii AT kutokea Zanzibar akimwaga burudani katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.


Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Joseph Haule “Professa J” (kulia) akiteta jambo na wasanii wenzake Kala Jeremiah (kushoto) na Ney wa Mitego (Kati) katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.

Show love ya wasanii...Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Kala Jeremiah akiwapa wananchi ujumbe katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.

Msanii Ney wa Mitego akitoa burudani katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.


Msanii Roma Mkatoriki akitoa burudani...

Msanii wa Bongo Movie Shamsa Ford nae alikuwepo kusapoti mabadiliko na kuwasisitiza wananchi wajitokeze kupiga kura.
Msanii wa Kizazi kipya, ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu akitoa burudani tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.


Msanii Profesa Jay, ambaye ni mtia nia wa Ubunge kwa jimbo la Mikumi akiburudisha katika tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.


Msanii wa Kizazi kipya, Juma Nature mtoto wa Mbagala akitoa burudani tamasha la 'Democracy in Dar' lililofanyika jana Agosti 16, 2015 Jumapili kwenye viwanja vya Zakhem, Mbagala likiwa na lengo la kuwahamasisha mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani wa Oktoba 25, 2015.

Wasanii Nguri wa Muziki wa Kizazi Kipya, Joseph Haule a.k.a Profesa Jay na Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu wakishow love mara baada ya kumaliza kuwapa elimu na burudani wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake.Marafiki wakifurahi mara baada ya kumalizika kwa tamasha hilo.