Sehemu ya III: Maoni ya Mndeme kuhusu aliyosema Polepole

Maoni yangu juu ya Kauli na Misimamo ya Ndugu Humphrey Polepole katika Kipindi cha Mada Moto Channel Ten: Sehemu ya Tatu


Kama nilivyoahidi jana, leo ninaendelea na sehemu ya 3 ya makala yangu ambayo kwayo ninajaribu kujibu hoja na misimamo ya ndugu Humphrey Polepole (HP) kupitia vipindi vya MADA  MOTO cha Channel Ten. Katika vipindi hivyo vitatu kwa mfululizo, ndugu HP alitumia muda mwingi kuongelea udhaifu wa vyama vinavyoundaa UKAWA hasa kwa kitendo chao cha kumpokea raia mmoja wa kitanzania kutokea wilaya ya Monduli aitwaye Edward Lowasa (EL). Hoja kuu ya ndugu HP ni kwamba Ndugu EL ni mtu mchafu, fisadi, mwenye utajiri usio halali, na asiyefaa kupewa nafasi ya ongozi. Pamoja na uhuru wa ndugu HP katika utoaji maoni, niliona mapungufu makubwa katika uwasilishaji wake hasa kwa kitendo cha kukiuka maadili anayoyasimamia, kutokutenda haki dhidi ya mtanzania mwenzake, kutokua mkweli katika anayoyasimamia na kutofuata misingi ya kisheria ya nchi yetu. Katika kuanisha kasoro nilizoziona kwenye uwasilishaji wa ndugu HP niliandika sehemu ya kwanza kwa kueleza dhana ya MAADILI (Rejea hapa (bofya));  jana nikaandika sehemu ya pili kuhusu dhana ya UKWELI na HAKI (Rejea hapa (bofya)); na leo nitaongelea dhana ya MAGEUZI na MABADILIKO ambayo ilichukua sehemu kubwa ya madajala wake na ndugu Mtatiro. Ninakusihi usome makala mbili zilizotangulia ambazo ni msingi wa hiki niachokwenda kuandika leo ili upate mtiririko wenye mantiki tarajiwa.
Nimetafakari namna nzuri ya kuchambua hoja za ndugu HP juu ya mabadiliko na mageuzi niimepata shida kuweka mawazo yangu sawa. Nimeona napata ugumu sana kuchambua hoja zake bila kufafanua dhana ya mabadiliko na mageuzi kiuhalisia na kitaaluma kidogo ili kujenga kile kwenye lugha ya kikoloni wanaita "premise" (msingi) wa hoja zangu. Hivyo nitachambua kidogo kuhusu mabadiliko na mageuzi kabla sijaweka uchambuzi wangu kuhusu hoja za ndugu HP.
http://blogs-images.forbes.com/learnvest/files/2014/06/behavior-change-expert-questions.jpg
DHANA YA MABADILIKO NA MAGEUZI
Katika mjadala kati ya ndugu HP na ndugu Mtatiro, HP alipinga kwa hoja kwamba nchi yetu haihitaji mabadiliko ya mfumo wa utawala bali inahitaji mageuzi kwa maana kwamba kubadili tu serikali kwa kuitoa CCM madarakani na kuweka vyama vya upinzani hakuwezi kuleta tija. HP alijaribu kuonesha kwamba mabadiliko ya serikali siyo jambo la msingi kwa sasa kama namna ya kuendelea kuubeba msimamo wake wa kwa nini anampinga mgombea wa UKAWA pamoja na umoja huo kupewa nafasi ya kuongoza. HP kasema hatuhitaji mabadiliko bali tunahitaji mageuzi lakini hakujenga hoja kugusia mageuzi hayo yatapatikanaje ni nani anatakiwa ayalete. Kabla sijaeleza undani wa hoja yake labda ni vema kwanza tutazame maneno haya ili tuweze kuyaweka katika muktadha wa hoja za HP na tunapoelekea uchaguzi wa mwezi October mwaka huu.


 • Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la 2013 haina neno mabadiliko (wingi) ila ina neno badiliko (umoja). Neno BADILIKO linatafsiriwa kama "change" kwa lugha ya kikoloni na lina maana ya, "hali inayokuweko baada ya kutokea mageuzi fulani". Badiliko linatokana na kitendo cha ku-badilisha ambacho ni kurudisha kitu ulichokichukua awali na kuchukua  kingine. Hii yaonesha kwamba waweza kuyaelezea mabadiliko kama kitendo (process of change) na kama matokeo ya maamuzi ya kubadilika (the situation soon after the action of change).
 • Kwa upande mwingine neno MAGEUZI (Transformation) limefafanuliwa kama, "mabadiliko ya jamii ya kisiasa, kitamaduni na kiuchumi". Lugha ya kikoloni (kingereza) imetoa tafsiri pana zaidi ya neno "TRANSIFORMATION" kama MABADILIKO KAMILI (complete change) ambapo ni kubadili namna au muonekano au muundo wa jambo au kitu fulani kwa malengo ya kutengeneza kipya (Rejea Oxford Advanced Learneres Dictorinary toleo la mwaka 2006).
http://www.worldreligionnews.com/wp-content/uploads/2014/11/human_evolution.jpg
Ukitazama maneno haya mawili utaona kwamba yana husiano mkubwa. Huwezi kuwa na MAGEUZI bila MABADILIKO na huwezi kufikia MAGEUZI bila kuanza na MABADILIKO. Yaani, mageuzi ni hatua inayofuata mabadiliko au inayotanguliwa na mbadiliko. Kwa upande mwingine, unaweza kufanya mabadiliko bila lengo la mageuzi kulingana na uhitaji. Kwa mfano, twaweza kusema Tanzania tumechoka kuongozwa na wazee au vijana (bila kujali  wanatoka chama gani) na wakati umefika sasa tuongozwe na vijana au wazee (kuanzia rais, wabunge na madiwani). Ajenda hii ukiitazama huoni uhitaji wa mageuzi maana haizungumzii lengo pana la mabadiliko haya zaidi ya kutaka RIKA TOFAUTI katika uongozi. Pia uhitaji huu hausemi kitu kuhusu kuchoshwa na chama au mfumo wa endeshaji nchi au katiba au sheria. Hivyo mabadiliko hayo yatatupeleka kubadili tu watu lakini tutaendelea na hali iliyoko.
Huwezi kupuuzia umuhimu wa mabadiliko katika kufikia mageuzi lakini unaweza kufanya mabadiliko bila mageuzi. Kwamba mabadiliko yatafikia megeuzi tarajiwa (iwapo yapo) au la hilo ni swala lingine na halina nguvu sana kunapokua na kiu ya mabadiliko kama nitakavyoeleza baadaye. Ukitazama kwenye tafsiri utaona kwamba MAGEUZI ni hitimisho la mchakato wa MABADILIKO (complete change). Mageuzi ni zao la mwisho la mabadiliko na tunapoongelea mageuzi katika taifa hili sio swala la uchaguzi pekee na sio jambo la muda mfupi. Inaweza kuchukua miaka mingi sana kufikia mageuzi jamii inayoyataka kwani kuna harakati na mambo mengi sana ha kubadilisha ili kufikia. Ngoja nizame kidogo kwenye dhana ya mabadiliko.


MABADILIKO
Mojawapo wa maeneo niliyoyapitia kwa maana ya taaluma na majukumu ya kikazi ni eneo la "sayansi ya menejimenti ya mabadiliko" (kikoloni wanaita Change Management"). Mabadiliko ni kati ya dhana inayokabili kila eneo. Maisha ya kila siku ya kibinafsi, familia, kitaasisi, kisiasa, kitaaluma, kibiashara na mengine, yamejaa ama watu wenye kiu ya mabadiliko au muendelezo wa mabadiliko katika kutaka kuboresha mambo. Mara nyingine kiu kubwa ya mabadiliko inawafanya watu hata kutojua ni aina gani ya mabadiliko wanayoyataka na inapofikia hatua hii tunajua kwamba shida sio hamu ya mabadiliko bali shida ni kuchoshwa na hali au mazingira waliyoko sasa. Mazingira hayo yamekua sio rafiki tena kwao na hivyo wanatamani chochote kinachoweza kuwatoa toka hayo mazingira hata kama hawajui kitawaweka kwenye mazingira gani ukilinganisha na waliyoko sasa. Wale walioko kwenye ndoa watakua wameshawahi kukutana na wakati ambapo unaona kabisa kuna kitu hakiko sawa kwenye mahusiano yenu na munatakiwa kubadilika lakini hamuna lugha ya kuelezea haya mabadiliko  mtu awaelewe vema.


Kuna aina mbili za mabadiliko:
 1. Mabadiliko rasmi au ya kupangwa (Kikoloni wanaita Planned Change). Haya ni aina ya mabadiliko ambayo mtu au kundi la watu linaona uhitaji wa mabadiliko na kukubaliana kwamba kuna haja ya kufanya mabadiliko. Wanakaa nchini ha kuoredhesha kwa undani kile wanachotaka kibadilike na namna ya kukibadili. Hii ni pamoja na kungalia gharama (cost) na athari (risks) zinazoweza kujitokeza katika mabadiliko hayo na namna ya kukabiliana nazo ili kufikia mabadiliko tarajiwa. Mara nyingi ni ngumu kuyaona haya yote wakati wa mipango ya kubadilika lakini huwa tunashauri kwamba wahusika waangalie kwa undani kila kitu na kila eneo ambalo litagushwa na mabadiliko husika ikiwa ni pamoja na kupima ni kipi kitakua na uzito kati ya hasara na faida. Kama gharama a mabadiliko ni kubwa kuliko faida basi ni bora kutokufanya aina ya mabadiliko kusidiwa na hivyo ama kuendelea na hali iliyoko  au kutafuta aina nyingine ya babadiliko ambayo yatakua na faida zaidi


  1. Katika mfumo huu wa mabadiliko ni lazima kutafakari vema iwapo kiu ya kubadilika inahitaji mabadiliko makubwa kwa maana ya kubadilisha kila kitu au mfumo ulioko au kunahitajika tu marekebisho machache ya mfumo ulioko. Ukichukulia mfano wa nyumba, kabla ya kuamua kuingia gharama za kuvunja nyumba unayoishi kwa sasa na kujenga mpya kwa kuwa ni ya zamani, ni vema utazame kama utastahimili gharama hizo au la ili usijenge ukaishia kwenye msingi. Pili unaweza kutazama iwapo kuna unalazima wa kujenga upya ua ufanye tu marekebisho makubwa/madogo ya nyumba unayoishi ili kuiboresha kukidhi mahitaji maalumu, viwango na nafasi. Mara nyingi serikali na taasisi zake hufanya mabadiliko makubwa bila kufanya hizi tathmini za kina na hata wakifanya hawahusishi "vichwa sahihi" na matokoe yake mabadiliko mengi hayana tija, mengi yanaishia njiani na mengi yameleta hasara kubwa na mtambuka.


  1. Aina hii ya mabadiliko inafuata mtiririko na mipango thabiti (systematic aproach to change) ili kufikia malengo na kunakua na ufuatiliaji wa karibu wa kila hatua ili kuyapima mabadiliko husika na kutizama iwapo kuna ulazima wa kubadili baadhi ya mikakati/mambo yaliyo kwenye mipango kwa kutoendana na na uhalisia.


  1. Aina hii ya mabadiliko utekelezaji wake ni halisia zaidi katika taasisi zenye uongozi na malengo maalamu kama vile makampuni ya kibishara ambapo wanaweza kupima faida ya mabadiliko kwa kutizama uboreshaji wa huduma zao, uzalishaji na faida wanayoipata itokanayo na mabadiliko.


  1. Moja ya changamoto ya mabadiliko haya ya kupanga ni ucheleweshwaji wa mabadiliko au kufanyika taratibu sana kwani menejimenti inachukua kila aina ya tahadhari kuhakikisha haifanyi makosa. Pia kuna uwezekano wa baadhi ya watu ndani ya taasisi kuchelewesha mabadiliko hayo kwani yanaleta hofu kwao. Hofu hii hutokana na ukweli kwamba mambo hayatakua kama walivyozoea siku zote iwapo mabadiliko yatafanyika. Yanaweza ziba miaya ya mapato (halali au haramu); yanaweza kuongeza wingi wa kazi; yanaweza kuwabana au kuwahitaji kuwa na elimu na ufanisi zaidi; na mara nyingine hata kubadilishwa vitengo au kuachishwa kazi kabisa iwapo utaonekana huna nafasi kwenye mfumo mpya. Kwa mfano, mabenki yalivyoanza kutumia mifumo ya kompyuta katika shughuli zote za fedha, wale wote waliokua na "aleji" na kompyuta ama walitafutiwa kazi zingine au walipoteza kabisa kazi. Wako wenye vyeo walivyovikalia kwa muda mrefu lakini ilibidi wawapishe wenye ujuzi.


  1. Kitendo hiki cha watu kuchelewesha au kuzuia mabadiliko kufanyika kama yalivyopangwa, kwa lugha ya kikoloni kinaitwa "Resistance to Change" (Ugumu wa mabadiliko). Kizuizi hiki ni kigumu sana kukabiliana nacho hasa iwapo wale wanaotakiwa wawe sehemu ya utekelezaji wa mabadiliko ni sehemu ya wenye maamuzi katika taasisi kwani watafanya kila liwezekanalo maslahi au udhaifu wao usikumbwe na kimbunga cha mabadiliko. Hii ndio sababu kubwa inayofanya kuwe na ugumu sana kufanya mabadiliko kwenye taasisi za serikali/umma ukilinganisha na kwenye sekta binafsi. Kwenye sekta binafsi menejimenti inapokubaliana kufanya mabadiliko haitizami sana mitazamo na maoni ya watendaji na utekelezaji wake unatakiwa ufanyike kama ilivyopangwa kwani wanakua wamefanya kazi kubwa iliyoangalia kila eneo, gharama na changamoto. Ambaye hataki mabadiliko hayo anapewa uchaguzi wa ama kutii au kutizama mlango wa kutokea ulipo. Serikali kuna mbwembwe nyingi zisiruhusu mabadiliko na wako watumishi hasa vigogo ni heri uwaue kwanza ndio ubadili walichokizoea. Mtu ambaye kazoea anashinda ofisini akinywa chai na vitrumbua na kusoma gazei, akichoka analala au anapaka kucha rangi; halafu leo umwambie ofisi zote zinakwenda kufungwa CCTV camera kutizama utendani kazi, atatumia kila mbinu na ufahamu kuzuia huo mradi usitekelezeke. Mukimshinda basi atakata hata waya au kuzima umeme kila siku ili mtambo usifanye kazi.


  1. Nifupishe kipengele hiki kwa kusema kwamba mabadiliko ya iana hii sio halisia yanapokua yanayotakikana katika mazingira ambayo siyo ya kimkakati na kikanuni. Pia sio halisi katika mazingira ambayo anayetaka kuyaleta mabadiliko hayo hana maamuzi ya mazingira yanayoathiri mabadiliko (the change agent has little or no control of the factors affecting the anticipated change). Ni ngumu sana kutekeleza mabadiliko kwa mtindo huu katika mazingira ya mtu binafsi, katika familia na mabadiliko ya kijamii kama vile yahusiyo siasa na mabadiliko ya serikali.


 1. Aina ya pili ya mabadiliko ni mabadiliko yasiyo rasmi au yanayotokea bila kupangwa (kikoloni wanaita unplanned change).  Haya ni mabadiliko ambayo hutokea bila kupanga au kuamuliwa na watu. Mara nyingi mabadiliko ya aina hii hutokea kwenye jamii au kundi la watu dhidi ya menejimenti kama ni kwenye kampuni / taasisi au watawala iwapo ni kwenye mifumo kisiasa Kinachosukuma mabadiliko haya mara nyingi ni hali ya kutoridhika na mazingira ya kazi; kutoridhishwa na uonevu toka kwa walio juu; kutoridhishwa na huduma za kijamii; uonevu; unyanyasaji; mateso na dharau toka kwa watawala; hali ngumu za maisha; nk.


  1. Kiu ya mabadiliko haya huwa ni kubwa sana na inaendesha sana hisia za watu kiasi kwamba ni vigumu sana kuzipuuzia hisia hizo hivyo huamua kufanya kila liewekanalo kudai mabadiliko popote inapowezekana. Inapokua ni kwenye taasisi au makampuni, unaweza kuyaona madai haya kwa njia nyingi kama vile kugoma kufanya kazi au kutofanya kazi kwa kujituma; kuandamana; uharibifu / wizi wa mali za taasisi; na mengine mengi. Kama ni dhidi ya watawala wa nchi watu wanaweza kuandamana, kulalamika sana na wanapopata nafasi ya kuchagua serikali mpya "wanafanya maamuzi magumu"


  1. Mara nyingi ni ngumu kujua nani hasa kaanzisha mkakati au mipango ya kudai mabadiliko ya aina hii. Ingawa mara zote kunakua na aiNa ya uongozi kwenye kundi hili katika kudai mabadiliko, ukweli ni kwamba uongozi huo unakua umejitokeza baada ya harakati za kudai mabadiliko kuanza. Mara nyingine uongozi unajitokeza baada ya wengine kuumia, kupoteza kazi/nafasi na hata kupooteza maisha. Na uongozi huu unaweza kutokeza kwa wahusika kujiteua wenyewe au kuteuliwa papo kwa hapo na kundi. Kundi huwa tayari kumchagua yeyote wanayeona ana ujasiri, ushawishi na uwezo wa kuwasemea na kuyadai mabadiliko bila kuogopa (yaani wanataka mtu aliye tayari kujilipua kwa niaba ya wengine). Kwa hali hii, vigezo vinavyotumika kupata uongozi huu vyaweza kuwa ni tofauti sana na vile vinavyotumika kupata viongozi kwenye maeneo mengine.


  1. Mabadiliko haya hutokea kwa haraka sana na kwa  watawala au wenye maamuzi  huchukuliwa kama aina fulani ya uasi usiostahili kuvumiliwa.


  1. Kama nilivyosema awali, mara nyingine wahusika kutokana na jazba, hasira, miheuko, hisia kali, hofu na mengine, hata hawajui ni nini hasa wanakihitaji (yaani hawana specific demands) ila kilio chao ni mabadiliko, Yeyote anawajibika kujibu au kusikiliza hitaji la kundi hili hujiweka kwenye mazingira mabaya na magumu ya kukabiliana na changamoto zitokanazo na "nguvu ya mabadiliko" iwapo ataonesha kupuuzia kilio chao. Kwa kuwa wanakua hawana mahitaji maalum, iwapo kiu yao itasikilizwa na wakafanikiwa kujikuta kwenye mbadiliko ndipo huanza kujipanga na kutazama taratibu zitakazofaa katika mazingira hayo mapya ya mabadiliko.


  1. Kwa upande wa pili, mabadiliko haya yasiyopangwa yanaweza kutokea au kulazimika kufanyika hata kwenye taasisi/ kampuni zenye mifumo inayoruhusu "planned change". Taasisi au kundi, laweza kujikuta kwenye wakati au mazingira ambapo kuna mambo yanalazimisha waachane na mazoea fulani na kuruhusu mambo mapya. Kwa mfano, taasisi ambazo zilizoea kufanya mambo yake kwa mifumo ya karatasi, kwa sasa wapende au wasipende, wanalazimika kutumia mifumo ya kompyuta na intanenti kwani kila wanayewasiliana naye katika utekelezaji wa kazi zao anatumia mifumo hii.


Mfumo wa kutuma na kupokea fedha kwa kutumia simu za mikononi ulipoingia watu wengi sana walikua hawana simu za mikononi wala hawajapanga kuwa nazo. Na hata walizokua nazo walikua wagumu kukubali kuzitumia kwa matumizi ya kutuma na kupokea fedha. Hata hivyo, nguvu ya mifumo hii, iliwalazimisha watu wengi kuwa angalau na "line" ya simu watakayoitumia kupokea na kutuma fedha. Wafanyabiashara na makampuni yalijikuta yanalazimika kuanza kutafuta namna mpya ya kupokea malipo kwa kupitia simu za mikononi maana kinyume chake ilikua ni kupoteza mapato au wateja. Haya ni mabadiliko yasiyopangwa yanayolazimishwa na mabadilo ya kimazingira ambayo wahusika hawana budi kuyatii.
Nifupishe sehemu hii kwa kusema kwamba sehemu kubwa ya mabadiliko katika maisha yetu ya kila siku hufuata mfumo wa mabadiliko yasiyo rasimi/yasiyopangwa (unplanned change). Watu binfsi, familia, kampuni, taasisi, na serikali hujikuta katika mkumbo wa kubadilika bila kupanga au kubadilishwa pale wanapoleta ubishi. Mojawapo ya mifumo ambayo siku zote hufuata utaratibu huu kote duniani ni mabadiliko ya kiuongozi wa serikali zinazofuata mfumo wa kidemokrasia. Kote duniani hakuna nchi watu wanachagua chama cha siasa au kiongozi fulani kwa kupanga, kuweka mikakati, kupima gharama na hasara na mengine yanayoendana na hayo. Watu hubadilisha serikali, vyama na watu wa kuwaongoza kwa kuamua kwamba wanataka mabadiliko. Mabadiliko hayo hufanyika kama kauli au ishara ya wao kujieleza kwamba wamechoka; wana hasira; wana maumivu; "wameboreka"; wamekinaika na kilichopo; wameshindwa kuvumilia ubaya na mateso ya watawala; hawaridhiki na huduma mbaya za kijamii na hali ya maisha; wamedanganywa; na sababu zingine nyingi.
Nilimwambia rafiki yangu mmoja aliyetafuta kugombea ubunge kupitia CCM na kukutwa na "panga la ukatwaji", kwamba inapofika kwenye kipindi cha uchaguzi, hata nafasi ya sera, misingi na mwelekeo wa vyama vya siasa (ideologies) huwa ni finyu sana na watu wachache sana huzitumia kufanya maamuzi. Maamuzi ya wamchague nani au chama gani inapofikia wakati wa uchaguzi hayafanyiki tena kichwani bali huamini moyoni hadi baadaye sana baada ya uchaguzi.
Kwa kua kipengele hiki kimekua kirefu, ninakomea hapa na nitaendelea na sehemu ya nne kuhakisi uchambuzi huu kwenye hoja na misimamo ya ndugu HP katika eneo hili na ujumla wa mtazamo wake kwa EL na UKAWA kama kundi la vyama vya siasa.


Rejea:
 1. Siku ya 2 ya Mjadala wa HP na Mch Msigwa: sehemu ya kwanza: https://www.youtube.com/watch?v=-KvqAyxnWkU na sehemu ya pili: https://www.youtube.com/watch?v=fteTqyCOcrI
 2. Siku ya 3 ya mjadala wa HP na ndugu Mtatiro: sehemu ya kwanza: https://www.youtube.com/watch?v=GBhYacfvGuc na   sehemu ya pili: https://www.youtube.com/watch?v=8E-5WxBxzfQ
 3. TUKI (2013). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Oxford University Press, Oxford
 4. Oxford Advanced Learners Dictionary (2006), New 7th Edition. Oxford


Mwalimu MM ni mhadhiri Katika kitengo cha Sayansi ya ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mtafiti wa mifumo ya TEHAMA (ICT) katika Huduma za Afya (Health Informatics). Unaweza kuwasiliana naye kupitia [email protected] Blog: http://mwalimumm.blogspot.com

Rais Kikwete, Dk Magufuli wamfariji mjane wa Mzee Mazongera

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka mchanga kaburini huku Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli akisubiri zamu yake wakati wa mazishi ya Marehemu Iddi Ubwa Mazongera aliyekuwa Diwani wa Kata ya Yombo Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani aliyefariki jana na kuzikwa leo kwenye makaburi ya Kichangani, Bagamoyo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli wakimfariji mjane wa Marehemu Iddi Ubwa Mazongera aliyekuwa Diwani wa Kata ya Yombo Wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani aliyefariki jana na kuzikwa leo kwenye makaburi ya Kichangani, Bagamoyo. Katikati ni Mama Salma Kikwete
Picha: Ikulu

Kasuku ashitakiwa kwa kumtusi mtu

Polisi nchini India wameripotiwa kuzuia kasuku mmoja anayedaiwa kumtusi mwanamke mmoja mzee mapema leo hii.

Mmoja wa maafisa wa polisi wa India alitoa maelezo na kusema kwamba wamechukuwa hatua hiyo ya kumzuia kasuku kwa lengo la kumfanyia majaribio ili kuthibitisha iwapo ni ‘mkorofi’.

Mwanamke huyo mzee kwa jina la Janabai Sakharkar mwenye umri wa miaka 75, aliwasilisha kesi yake kwa polisi baada ya kughadhabishwa na matusi yaliyotolewa mara kwa mara na kasuku huyo kila alipomuona.

Sakharkar pia aliekezea kidole cha lawama kwa jirani yake ambaye ni mfugaji wa kasuku huyo kwa madai ya kumfunza matusi aliyomtolea.

Licha ya madai hayo kutolewa, kasuku huyo alionekana kukaa kimya kila alipojaribu kuzungumzishwa matusi yaliyorudiwa zaidi ya mara moja na polisi.

Hatimaye polisi waliamua kufutilia mbali kesi hiyo na kumsalimisha kasuku huyo kwa idara ya wanyama na misitu. [via TRT Swahili]

Tanzania to reopen its embassy in Khartoum

August 17, 2015 (KHARTOUM) - The United Republic of Tanzania has decided to reopen its embassy in Khartoum, two decades after it was shut down.

The Tanzanian foreign ministry undersecretary, Liberata Mulamula, on Monday has conveyed her government’s decision to her Sudanese counterpart, Abdel-Ghani al-Nai’m.

The two officials discussed ways for promoting the bilateral cooperation in the trade, economic and cultural domains besides the exchange in the training of diplomats and coordination in the regional and international forums.

They stressed the need for forming joint ministerial committees between the two countries as well as forming another committee for political consultation between the two ministries to lay the foundations for the development of bilateral relations in all fields.

It is worth mentioning that Tanzania has shut down its embassy in Khartoum more than two decades ago for economic reasons.

The Sudanese diplomat, for his part, briefed his Tanzanian counterpart on the security and political developments in the country besides the ongoing consultations among the Sudanese government, United Nations and the African Union on the exit strategy for the hybrid peacekeeping mission in Darfur (UNAMID).

via SudanTribune

I've been peeling bananas wrong way, now I do it right (like monkeys)

How monkeys do it (the right way)
 1. Locate the top (the end of the banana opposite from the stem).
 2. Pinch the top off and peel it back to open one side.  This is where you will be starting to open up the banana without bruising or mashing it. 
 3. Peel back the other remaining parts.
 4. Now eat your banana and enjoy!
The video below shows how it's done...
ATCL yaanza tena safari za Mwanza mara mbili kwa juma

Abiria wakishuka toka kwenye ndege ya Shirika la Ndege la Taifa, Air Tanzania (ATCL) katika uwanja wa ndege wa Mwanza Jumamosi jioni 
SHIRIKA la ndege la taifa (ATCL) limerejesha safari zake kuelekea mkoani Mwanza ikiwa ni sehemu ya mpango wa shirika hilo kupanua huduma kwa wateja wake hapa nchini.

Safari ya kwanza ya shirika hilo kuelekea mkoani Mwanza ilifanyika mwishoni mwa juma lilopita kwa kukutumia ndege yake aina ya CRJ- 200, baada ya safari hizo kusimama tangu mwezi Agosti mwaka mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Uwanja wa ndege wa Mwanza, Kaimu Afisa Uhusiano wa Shirika hilo, Bi Lily Fungamtama alisema uamuzi wa kurejesha safari hizo umezingatia mahitaji ya wateja wa shirika hilo.
“Tumepokea maombi mengi kutoka kwa wateja wetu wakiwemo wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kwa kuhusisha majiji haya mawili. Kwa kuwa ATCL ni shirika mama la ndege hapa nchini tukafanya kila jitihada kuhakikisha tunarejesha safari zetu kuelekea jijini Mwanza,’’ 
alibainisha Fungamtama huku akiongeza kuwa shirika hilo litafanya safari zake mara mbili kwa siku katika siku zote saba za wiki.

Alisema ili kukabiliana na ushindani wa kibiashara dhidi ya mashirika mengine ya ndege yanayofanya safari zake kuelekea mkoani humo, shirika hilo limewekeza zaidi kwenye ubora wa huduma zake sambamba na kutoa huduma zake kwa gharama nafuu.

Akizungumzia na waandishi wa habari mara tu baada ya kuwasili kwa ndege hiyo Uwanja wa ndege wa Mwanza mmoja wa abiria waliosafiri na ndege hiyo Bw. Bakari Hamidu mbali na kushukuru kurejeshwa kwa huduma hiyo pia alionyesha kuridhishwa kwake na ubora wa huduma unaotolewa na wahudumu wa shirika hilo.
“Nimefurahishwa sana na kurejeshwa wa huduma hii na zaidi nimefurahishwa na huduma nzuri zinazotolewa kwa abiria na wafanyakazi wa shirika hili. Kwa hilo lazima niwapongeze,’’ 
alisema Bw. Hamidu.

Pamoja na kurejesha safari hizo za mkoani Mwanza, shirika hilo pia kwa sasa linatoa huduma zake kuelekea mikoa ya Kigoma, Mtwara na visiwa vya Comoro kwa kutumia ndege yake aina ya CRJ-100.
“Tunatarajia mambo yatakuwa mazuri zaidi baada ya kukamilika kwa ukarabati wa ndege yetu nyingine aina ya De-Havilland Dash 8 Q300 inayoendelea na ukarabati mkubwa kwenye karakana iliyopo kwenye uwanja wa Kimataaifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam’’ 
aliongeza Fungamtama.

Tayari 3 wamefariki kwa kipindupindu Dar, 34 wamelazwa


Watu watatu (wanawake 2, mwanaume 1) wamefariki dunia na wengine 34 wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala na hospitali ya Mburahati jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kipindupindu.

Hospitali ya Sinza Palestina imeripotiwa kuwa na wagonjwa walio na dalili za ugonjwa huo zaidi ya 50.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Bw. Paul Makonda amezitaja Kata zilizoathirika na ugonjwa huo kuwa ni Kijitonyama, Kimara, Manzese, Tandale, Saranga, Makumbusho na Mwananyamala.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, amesema kuna ripoti ya wagonjwa waliolazwa 71 hadi sasa, na kwamba Wilaya ya Ilala na Temeke bado hazijakumbwa na ugonjwa huo.


Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, Mganga Mkuu wa Minispaa hiyo, Dk. Aziz Msuya, amesema kuwa mgonjwa wa kwanza aligunduliwa katika maeneo ya Kijitonyama kwa Ally Maua na kufia nyumbani kwake katika eneo hilo na kuambukiza ndugu zake wawili ambao walikufa wakati wanapelekwa Hospitali.

Dk. Msuya amesema kumetayarishwa kambi za muda katika Hospitali za Kijitonyama, Mwananyamala na Sinza Palestina pamoja na kambi kuu iliyopo katika Hositali ya Mburahati. Amewataka wananchi wa Jiji hilo kuchukua tahadhari kwa kuweka mazingira safi kunywa maji yaliyochemshwa na kujiepusha kula vyakula vilivyopikwa katika mazingira yasiyo safi na salama.

“Ukipata huu ugonjwa tutakupa dawa lakini kwa sasa tumetoa dawa katika maeneo yale ambayo tumeona yameathirika zaidi ambayo ni Manzese na Kijitonyama. Tumeshazipa dawa kaya zile ambazo tunazitilia mashaka kwamba zinawezikawa zimepata maambukizi, na wale waliopo katika maeneo mengine ambayo sio maeneo hayo niliyokutajia hapo awali, wanapoona hizo dalili za kutapika na kuhara basi wafanye haraka kukimbia Hospitali.”

Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini, Dk. Rufaro Chatora, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amethibitisha kupokea taarifa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ikiijulisha WHO kuwepo kwa ugonjwa huo, na kwamba ugonjwa huo uliibuka tangu Agosti, 15, 2015.

Hata hivyo, ametaja maeneo yaliyobainika kuwa na wagonjwa hadi sasa kuwa ni Tandale, Kijitonyama, Saranga, Kimara, Manzese, Makumbusho na Mwananyamala.

Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, inafanya uchunguzi wa kina katika Wilaya ya Kinondoni ambayo ndiyo imeshambuliwa kwa sasa na ugonjwa huo kwa kasi ambapo pia timu hiyo itaendelea kutoa njia za kujikinga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Musa Nati, amesema watu wengine ambao hadi sasa idadi yao haijathibitishwa wamethibitika kuugua kipindupindu na wamelazwa katika hospitali hizo za manispaa hiyo. Ameeleza kuwa wodi mbili zimetengwa katika hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya wagonjwa wenye dalili hizo.

Mathalani, amesema wameanza kuchukua tahadhari kwa kupuliza dawa katika maeneo yaliyoripotiwa kuwa na mlipuko wa ugonjwa huo.


Historia ya kipindupindu Dar es Salaam

Ugonjwa wa kipindupindu umekuwa ukiutesa mara kwa mara mkoa wa Dar es Salaam kila mwaka licha ya jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali licha ya kila mwaka ugonjwa huo ambao umekuwa ukilipuka na kuwaathiri watu wengi na wakati mwingine kupoteza maisha.

Mamlaka za serikali zimekuwa zimekaririwa mara kadhaa na vyombo vya haabri kuwa zinachukua hatua kwa kuweka tahadhari mbalimbali kwa lengo la kudhibiti kipindupindu. Miongoni mwa hatua hizo ni kuzuia mikusanyiko ya watu kama sherehe, misiba na unywaji wa pombe za kienyeji.

Hata hivyo, pamoja na hatua hizo na nyingine nyingi kumekuwepo na hatua ya upigaji marufuku uuzaji wa vyakula katika maeneo yasiyoruhusiwa hali ambayo inatajwa kusababisha ugonjwa huo wa kipindupindu kuendelea kuutesa mkoa huo kila mwaka.

Kufuatia hali hiyo, Halmashauri ya Jiji hilo, imelazimika kufungua kambi maalumu za kuhudumia walioathirika na ugonjwa huo, katika Manispaa za Temeke, Kinondoni na Ilala ili wanaporipotiwa wagonjwa wapatiwe tiba kwa haraka.

Waziri aliyejaribu kunyang'anya karatasi ya matokeo amkubali na kumuunga mkono mshindi

Dk Titus Kamani
Dk Titus Kamani
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani -- ambaye video ilimwonesha akitaka kumpokonya karatasi msoma matokeo -- aliyekuwa mgombea Ubunge katika jimbo la Busega Mkoani Mwanza, amekubali matokeo yaliyotangazwa Kamati Kuu ya CCM ya uteuzi wa Dk Raphael Chegeni.

Uchaguzi huo ulikumbwa na vurugu na kurudiwa yapata mara tatu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dk Kamani amesema uchaguzi huo wa uligubikwa na hila, udanganyifu na vurugu kiasi cha kusababisha kutoaminiana kati ya wagombea.

Huku akiwa na wagombea wenzake katika jimbo hilo, wamesema hivi sasa wameamua kuondoa tofauti zao na kujikita katika kuleta umoja katika jimbo hilo ili waweze kukiletea ushindi Chama Cha Mapinduzi.


Call for applications: Global Health Program for Fellows and Scholars

Applications accepted through Support Centers

Program Overview


The Global Health Program for Fellows and Scholarsprovides supportive mentorship, research opportunities and a collaborative research environment for early stage investigators from the U.S. and low- and middle-income countries (LMICs), as defined by the World Bank, to enhance their global health research expertise and their careers. (See The World Bank Country and Lending Groupsto identify countries with low- or middle-income economies.)
Support Centers

Support Centers (funded in part by Fogarty through competitive grants) identify postdoctoral Fellows and doctoral Scholars. See each Support Center website for application deadlines, eligibility, program areas and additional information.
The Global Health Program for Fellows and Scholars is based on the success and experience of the Fogarty International Clinical Research Scholars and Fellows (FICRS-F) Program.

Please visit each of the Support Center websites for application materials, eligibility criteria, program areas and additional information.

Applications for 2016-2017 fellowships are due Nov 1, 2015

Call for applications: Fogarty Emerging Global Leader Award (K43)

Announcement(s)

Deadlines

 • ​Upcoming deadlines: December 16, 2015, December 14, 2016, and December 14, 2017

Eligibility


 • Only low- or middle-income country (LMIC) institutions are eligible.
 • Candidates must be LMIC citizens.
 • Candidates must hold an academic junior faculty position or research scientist appointment at the LMIC applicant institution and must have been in this position for at least one year at the time the application is submitted.
 • Candidates are required to have both U.S. and LMIC primary mentors.
 • Research should take place primarily in the LMIC.
 • Individuals who have already received independent research funding are not eligible.
 • Applicants should demonstrate that they are committed to an independent research career and justify the need for three to five years of mentored research experience in order to become an independent research scientist.
 • View full eligibility details in the program announcement and refer to FAQs.
Info source: www.fic.nih.gov

Call for applications: Wellcome Trust Seed Awards in Science

The purpose of the scheme is to enable researchers to develop a novel idea to a point where it may compete for a larger award from the Wellcome Trust or from another source. Eligible activities include pilot studies, scoping studies, preliminary data gathering, proof-of-principle studies, planning sessions and meetings of collaborative networks. The Trust encourages applications for interdisciplinary research across its Sciences, Humanities and Social Sciences and Innovations funding.

Amount: Seed awards are worth up to £100,000 and are mainly for up to two years.

Eligibility: 
 • Hold an appointment at an eligible institution in the UK, Republic of Ireland or alow- or middle-income country.
 • Not be based at a core-funded research institute
 • Receive personal salary support from your host institution for the duration of the award, which must not come from welcome trust funding.
 • Not have held substantive funding for research in the 12months before the application closing date.
Closing date: October 22, 2015.

More information is available at: www.wellcome.ac.uk

Jeff Msangi na Darmatus Nambai katika Jukwaa Langu wakijadili Demokrasia na Mabadiliko

Kipindi hiki ambacho kinakujia kila Jumatatu, kinajadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2015.

Katika kipindi hiki utasikia mjadala wetu na wageni Jeff Msangi kutoka Toronto, Canada na Darmatus Nambai aliyehudhuria studioni, kuhusu "Demokrasia na Mabadiliko" tunapoelekea kwenye uchaguzi nchini Tanzania.

Karibu...

Majina 32 ya kamati ya CCM ya kampeni za Uchaguzi 2015TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa jana Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imekamilisha kazi ya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto.

Wagombea ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika majimbo hayo ni pamoja na Ndugu Jonathan Njau (Singida Mashariki) na Ndugu Emmanuel Papian John (Kiteto).

Aidha Kamati Kuu imefanya uteuzi wa Kamati ya Kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015 ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana. Wajumbe wa Kamati hiyo ni kama ifuatavyo;-

1. KAMATI YA KAMPENI YA CHAMA CHA MAPINDUZI 
 1. Ndugu Abdulrahman Kinana - Mwenyekiti 
 2. Ndugu Rajab Luhwavi - Makamu Mwenyekiti - Bara 
 3. Ndugu Vuai Ali Vuai - Makamu Mwenyekiti - Z'bar 
 4. Ndugu Sofia Simba 
 5. Ndugu Mohamed Seif Khatib 
 6. Ndugu Asha-Rose Migiro 
 7. Ndugu Samwel Sitta 
 8. Ndugu Nape Nnauye 
 9. Ndugu Mwigulu Nchemba 
 10. Ndugu Harrison Mwakyembe 
 11. Ndugu January Makamba 
 12. Ndugu Amina Makillagi 
 13. Ndugu Christopher Ole Sendeka 
 14. Ndugu Stephen Wasira 
 15. Ndugu Abdallah Bulembo 
 16. Ndugu Hadija Aboud 
 17. Ndugu Mohamed Aboud 
 18. Ndugu Lazaro Nyalandu 
 19. Ndugu Issa Haji Ussi 
 20. Ndugu Waride Bakari Jabu 
 21. Ndugu Mahmoud Thabit Kombo 
 22. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha 
 23. Ndugu Maua Daftari 
 24. Ndugu Stephen Masele 
 25. Ndugu Pindi Chana 
 26. Ndugu Shaka Shaka 
 27. Ndugu Makongoro Nyerere 
 28. Ndugu Bernard Membe 
 29. Ndugu Sadifa Juma Khamis 
 30. Ndugu Antony Diallo 
 31. Ndugu Livingston Lusinde 
 32. Ndugu Ummy Mwalimu 
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye, 
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
18/08/2015