Wanajeshi 3 wa UN kutoka DRC kushitakiwa kwa kubaka watoto Jam. Afr. Kati

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itawafungulia mashtaka askari wake watatu waliotuhumiwa kwa ubakaji nchini Jamhuri ya Afrika ya kati ambao ni sehemu ya ujumbe wa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.

Kauli hiyo imetolewa Alhamis wiki hii na waziri wa sheria wa Congo, Alexis Thambwe Mwamba, akibainisha kuwa tayari amemuagiza Jenerali [Joseph] Ponde, mwendesha mashtaka mkuu wa vikosi vya kijeshi nchini humo kufungua mashitaka hayo kulingana na msingi wa madai ya Umoja wa Mataifa.

Akizungumza na shirika la habari la Ufaransa AFP, Alexis Tambwe mwamba ameongeza kuwa DRC haitaweza "kuvumilia" vitendo kama hivyo, na kwamba askari waliohusika watalazimika kurejeshwa nchini humo kukabiliana na mahakama ya kijeshi.

Imeripotiwa kwamba wanawake watatu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wamebakwa na askari watatu wa Congo, mdogo wao akiwa na umri wa miaka 15, huku wakishinikizwa kutotoa siri, huku mwingine akidaiwa tayari kuwa mjamzito wakati mwingine akikiri kuridhia uhusiano huo.

Jeshi la DRC ndilo pekee lina askari wake mjini Bambari ambapo matukio hayo yanaripotiwa na ambako hivi karibuni, ujumbe wake unatarajiwa kuwasili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuchunguza tuhuma hizo zinazodaiwa na kikosi cha Congo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwa ni njama na uongo.

Mwanzilishi wa chama cha siasa afukuzwa chamani

Jean-Marie Le Pen
Jean-Marie Le Pen
Kamati tendaji ya chama cha FN kimetangaza Alhamisi jioni wiki hii kwamba kimemfukuza katika chama hicho Jean-Marie Le Pen. 
Jean-Marie Le Pen, mwenye umri wa miaka 87, mmoja wa waanzilishi wa chama cha FN, aliongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka 40.

"Jean-Marie Le Pen alikua anakabiliwa na kesi za kinidhamu baada ya kutoa kauli ziliozua utaua kuhusu Shoah", limesema tangazo hilo la chama cha FN.

Kabla ya kusikilizwa na kamati tendaji ya chama cha FN, Jean-Marie Le Pen alikuwa alitoa wito kwa chama kuungana. Jambo ambalo halikufanyika. Katika taarifa fupi, chama cha FN kimetangaza Alhamisi jioni kufukuzwa kwa kiongozi wa kihistoria katika chama. " Kufuatia mkutano uliofanyika leo, kamati tendaji ya chama cha FN, iliokutana kwa kujadili suala la nidhamu, imetoa na kuamua katika idadi kubwa inayohitajika, kumfuta katika chama Bw Jean-Marie Le Pen kwenye uanachama wa wa chama cha FN ", limesema tangazo hilo.

Jean-Marie Le Pen aliitishwa kwa mara ya kwanza Alhamisi mchana na kamati tendaji ya chama iliyokutana kwenye makao makuu ya chama katika mji wa Nanterre. Alitazamiwa kujibu zaidi ya maswalikumi natano, ikiwa ni pamoja na kauli ziliozua utata kuhusu vyumba vya gesi viliochapishwa katika gazeti la kila wiki la Rivarol na matusi ya mara kwa mara dhidi ya binti yake akiwa pia rais wa chama cha FN, Marine Le Pen na mshirika wake wa karibu Florian Philippot. Wawili hawa hawakuwepo katika mkutano huo, ili isonekani kuwa wameshinikiza kamati hiyo kuchukua uamzi. Baada ya muda wa saa tatu wakijadili hali hiyo, kamati tendaji ulichukua uamzi wa kumfuta katika chama cha FN kiongozi wa kihistoria wa chama hicho Jean-Marie Le Pen.

Kufukuzwa huko kunakuja baada ya miezi mitano ya malumbano ya ndani kati ya baba na binti yake. Mwishoni mwa mwezi wa Mei, kamati tendaji ya chama cha FN ilimsimamisha na kuitisha mkutano mkuu wa chama kupitia njia ya posta ili kumfuta katika nafasi yake kama rais wa heshima wa chama cha FN. Jean-Marie Le Pen aliwasilisha kesi hiyo mbele ya mahakama ambayo ilichukua uamzi wa kumrejesha katika nafasi yake. Adhabu yake ilifutwa katika masuala ya kiutaratibu.

Ugiriki kupiga kura mara ya tano katika miaka sita baada ya Tsipras kujiuzulu

Waziri Alexis Tsipras ametangaza kujiuzulu wadhiwa wake Alhamis jioni ili kufungua njia ya uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa hivi karibuni.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika ifikapo Septemba 20.

Tsipras alifahamisha katika kituo cha televisheni mkuwa serikali yake itafikisha barua yake ya kujiuzulu kwa rais wa Ugiriki.

"Katika muda mfupi, nitakwenda kwa Rais wa Jamhuri na kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwangu na kujiuzulu kwa serikali yangu ", Alexis Tsipras alisema.

Waziri Mkuu ameongeza kwamba ametaka kuwasilisha kwa raia wa Ugiriki kila kitu alichofanya tangu kuchaguliwa kwake ili aamue upya.

Alexis Tsipras hakuwa na uamzi mwengine wa kuchukua kwani anakabiliwa na mvutano uliozushwa na zaidi ya wabunge arobaini tangu kupitishwa kwa mpango wa tatu wa msaada kwa Ugiriki wa Euro bilioni 86 wiki iliyopita. Tawi hili la mrengo wa kushoto la Syriza limedhoofisha idadi kubwa ya wabunge alionayo, ambayo imepunguza wabunge 119 kwa jumla ya wabunge 300 wa Bunge la Ugiriki, na hivyo kuzuia sheria ya baadaye kuwasilishwa Bungeni.

Alexis Tsipras amelazimishwa kufuata utaratibu kwa kuwasilisha kwa rais Prokopis Pavlopoulos barua ya kujiuzulu kwa serikali na kuingia katika kampeni za uchaguzi kwa kipindi cha mwezi mmoja. Kaimu Waziri Mkuu atakua -- kwa mara ya kwanza katika historia ya Ugiriki -- mwanamke, Vassiliki Thanou, mwenyekiti wa Mahakama Kuu.

Raia wa Ugiriki watarejea kupiga kura kwa mara ya tano katika kipindi cha miaka sita.

Jeshi la Polisi lapiga marufuku vikundi vya ulinzi katika vyama vya siasa


CCK yawafungulia kesi Mwenyekiti NEC na Mwanasheria Mkuu wa Serikali


Kauli ya Jaji, Brig. Jen. Mch. Ramadhani kuhusu matokeo ya mchujo CCM

Aliyechukua fomu za kuwania Urais wa Tanzania 2015 kwa tiketi ya CCM, Jaji mstaafu Augustine Ramadhani amesema anaheshimu matokeo ya uteuzi wa mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM):
“Malezi yangu nimelelewa katika mahakama, sheria na jeshi tena wa ngazi ya juu, hivyo huwa tunaheshimu na kutii uamuzi wa ngazi za juu,”
“Tangu mchakato huu umalizike sijawahi kuzungumza chochote, ninyi waandishi wa habari mnanitafuta ... nianze kuzungumza na hamtanipata,”
“Amani tuliyonayo tumekuwa tunaisisitiza iendelee kwa kuwa ni muhimu kwa maendeleo yetu,” 
Jaji Ramadhani (mwanajeshi mstaafu wa cheo cha Brigedia Jenerali) amenukuliwa na gazeti la Mwananchi aksiema hayo kwenye kongamano la uhusiano wa dini na amani lililoandaliwa na Shirika la World Vision.

Sarakasi katika majimbo yaliyoachiwa CHADEMA

UAMUZI wa vikao vya juu vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwapitisha wagombea ubunge bila ridhaa ya wanachama huenda ikaathiri mwenendo wa uchaguzi katika Jimbo la Bunda.

Taarifa kutoka jimboni humo zinasema kwamba uteuzi wa Esther Bulaya aliyeanguka kwenye kura za maoni jimboni humo, umekipasua chama hicho baada ya viongozi wote wa juu jimboni humo kusimamishwa kazi na baadaye kutangaza kuachia madaraka.

Esther alikuwa Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kabla ya kuamua kukimbilia CHADEMA ambako aliangushwa na kada wa upinzani Bunda Mjini, Pius Masururi, lakini akarejeshewa kijiti cha kugombea jimbo hilo na Kamati Kuu ya CHADEMA.

Akizungumza na Radio Mazingira FM ya mjini hapa juzi muda mfupi kabla ya kuelekea Nairobi, Kenya, Masusuri alisema ameachana na Chadema na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Nimeshindwa kuvumilia uonevu huu na ninawaomba wote waliokuwa wakiniunga mkono Chadema, kumpigia kura Wasira (mgombea wa CCM, Stephen),” alisema Masusuri na kuongeza:
“Mbowe (Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman) huwa anasisitiza kuwa asiyefanya kazi na asile. Sasa inakuaje mimi niliyeanza kulitengeneza jimbo hili tangu mwaka 2013 leo niachwe, achukuliwe ambaye hajakifanyia chochote chama?
“Mwanachama mwenye wiki moja tu hata mkutano mmoja wa hadhara hajahutubia leo anapewa nafasi kubwa kuliko sisi!”
Tayari wana CHADEMA saba wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Masururi nao wamejiunga na CCM jana.

CHADEMA iliwasimamisha uongozi Mwenyekiti wa Jimbo la Bunda, Samwel Imanani; Katibu Mwenezi, Emmanuel Malibwa na Katibu wa Wilaya, Rita Tosile ambao pamoja na madai mengine, wanatuhumiwa kutumiwa na CCM kukidhoofisha chama hicho.

Taarifa za kusimamishwa kwao zilithibitishwa na Katibu wa Jimbo la Bunda, Daniel Charles.

Hata hivyo, wanachama wa CHADEMA waliokuwapo ofisi za chama hicho jana waliliambia Raia Tanzania kuwa wanaunga mkono hatua ya Makao Makuu kuwasimamisha viongozi wao.
“Hata Masusuri mwenyewe, tulishamshitukia muda mrefu kuwa anatumiwa na Wasira, kwa hiyo bora alivyoondoka,” 
alisema mwanachama mmoja akionekana dhahiri kumuunga mkono Esther.

Baadaye, kiongozi mmoja aliyesimamishwa na baadaye kuamua kuachia ngazi, Rita, alidai kuwa Masururi alionewa na kwamba sasa CHADEMA wajiandae kushindwa kwenye Uchaguzi Mkuu.
“Nimeachia ngazi kwa kuwa ninajua chama hiki sasa kitashindwa kwenye uchaguzi. Sasa makamanda waliokipigania chama kwa muda mrefua wanaachwa, badala yake wanakuja wageni.
“Uongozi wa taifa unapasawa kuheshimu uamuzi wa wananchi waliompa ushindi wa kwanza mgombea kwenye kura za maoni ni si vinginevyo,” 
alisema Rita.

[Habari inayoshabihiana na hii inapatikana pia kwenye gazeti la MWANANCHI]

Sarakasi Jimbo la Mbarali

Liberatus Mwang'ombe akionesha fomu ya kuwania Ubunge Mbarali 2015, aliyoichukua NEC (picha zaidi bofya hapa)
Wakati hali ya Bunda ikiwa hivyo, Mwandishi Wetu kutoka Mbarali mkoani Mbeya anaripoti kwamba makumi ya wananchi wilayani humo jana walizingira Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya (DED) wakishinikiza Modestus Kilufi apewe fomu za kugombea ubunge.

Kilufi ni Mbunge anayemaliza muda wake ambaye ameondoka CCM na kujiunga na Chadema hivi karibuni na kisha kupewa jukumu la kutetea nafasi yake Mbarali.

Lakini kabla hajakwenda Mbarali, uongozi wa CHADEMA Wilaya ulimwandikia barua Msimamizi wa Uchaguzi wilayani humo ambaye pia ni DED, Adam Mgoi, kumtambulisha Liberatus Mwang’ombe kuwa ndiye mgombea ubunge na kuchukua fomu hizo juzi.

Jana, Mwang’ombe alikula kiapo mahakamani na wakati akijiandaa kuzirejesha fomu zake, ndipo msafara wa Kilufi aliyeongozana na viongozi wa Chadema Mkoa ulipowasili wilayani humo na kwenda moja kwa moja ofisi za CHADEMA.

Alipowaona wageni hao, Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mbarali, Peter Mwashiki, alilazimika kuikimbia ofisi huku wanachama wakimkimbizi na kumtaka kumpeleka Kilufi kwa Msimamizi wa Uchaguzi.

Baada ya kushindwa kumpata Mwasiki, Kilufi akiongozana na makumi ya wanaCHADEMA, walikwenda ofisini kwa DED lakini nako waligonga mwamba kwani msimamizi huyo aliamua kufunga ofisi akiwaacha nje wafuasi wa CHADEMA, Kilufi na uongozi wa mkoa.
“Wananchi wanamtaka Kilufi agombee ubunge kwani hawana imani na Mwang’ombe. Wanadai kuwa huyu amefanya mipango na mwekezaji (shamba la mpunga lenye mgogoro na wananchi) ilia je kumlinda baadaye,” 
walisikika wananchi wakimlalamikia DED.

Hata hivyo, ofisi za NEC ambazo zipo chini ya Mgoi hazikufunguliwa hadi jana jioni huku wananchi wakiapa kutoondoka eneo hilo hadi ‘kieleweke’.

Katibu Mwenezi ACT – Wazalendo ahamia ADC

Katibu Mwenezi wa ACT – Wazalendo mkoani Iringa, Daudi Masasi amekihama chama hicho na kujiunga na ADC kisha kuchukua fomu ya kuwania ubunge Iringa Mjini, limeripoti gazeti la Mwananchi la Ijumaa, Agosti 21, 2015.

Masasi ambaye alishindwa kwenye kura za maoni zilizompa ushindi mgombea kupitia chama hicho, Chiku Abwao amejiondoa baada ya rufaa yake ya kupinga ushindi wa Abwao kukwama.

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Iringa Mjini, Ahmad Sawa alisema hadi sasa makada sita kutoka vyama mbalimbali wamechukua fomu kuwania kiti hicho. Aliwataja wagombea wengine kuwa ni Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) anayetetea kiti chake, Frederick Mwakalebela (CCM ), Chiku Abwao (ACT - Wanzalendo), Paulina Mgimwa (CHAUSTA) na Robeet Kisinini (DP).

Madiwani CCM Maswa wahamia TADEA

CCM Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imepata mtikisiko baada ya katibu wake mwenezi, Jishuli Nchala na wanachama wanaodaiwa kuwa ni zaidi ya 200 wakiwamo wawili waliokuwa madiwani, kukihama na kujiunga na TADEA, limeandika gazeti la Mwananchi la Ijumaa, Agosti 21, 2015.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana baadhi ya wanachama hao walisema wamechukua hatua hiyo kwa kuwa CCM kimetawaliwa na vitendo vya rushwa, chuki na udugu na kusababisha kukosekana kwa demokrasia.

Waliokuwa madiwani ambao wamejiunga na TADEA ambacho umaarufu wake wilayani hapo umeongezewa nguvu na aliyekuwa Mbunge wa Maswa Magharibi aliyejiunga nacho hivi karibuni ni Godi Kibinza wa Kata ya Kulimi na Sabi Kabangila wa Kata ya Nguliguli.
“CCM ya leo si ile ya zamani tuliyoachiwa na Mwalimu Nyerere, kwa sasa huwezi kupata uongozi ndani ya chama hasa ile ya kuwatumikia wananchi mpaka utoe rushwa,” 

alisema Kibinza.

Kabangila aliyekuwa amegombea udiwani na kushindwa katika kura za maoni alisema:

“Tumetoka CCM kwa sababu ya wizi wa waziwazi katika uchaguzi, wanafunga magoli ya mkono watu wakiwa wanaona, sasa tumekuja huku upinzani. Lazima tuwashughulikie mpaka waachane na wizi wao.
Wanachama hao walipokewa na Katibu wa TADEA Wilaya ya Maswa, Luhende Mipawa katika ofisi ya chama hicho mjini Maswa aliyesema sasa ni wakati wa wapinzani kuweka nguvu ya pamoja na kuiondoa CCM madarakani.

Aliyekuwa Meya Bukoba ahamia NCCR-Mageuzi akitokea CCM

Aliyewahi kuwa Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dk Anatory Amani amehama CCM na kujiunga NCCR – Mageuzi baada ya juhudi za kujiunga CHADEMA kushindikana, linaripoti gazeti la Mwananchi la Ijumaa, Agosti 21, 2015.

Baada ya kutangaza uamuzi huo, jana alikwenda kwa Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi katika Kata ya Kagondo na kukabidhiwa fomu za kugombea udiwani katika kata hiyo.

Hata hivyo, msimamizi msaidizi wa uchaguzi wa kata hiyo, Sharifa Mustafa awali alisita kutoa fomu hiyo, hali iliyozua malumbano.

Baadaye mgombea huyo alipewa fomu baada ya kuonyesha barua ya uthibitisho kutoka NCCR – Mageuzi ambayo ilikuwa imesainiwa na Kamishina wa chama hicho mkoani Kagera, Peterson Muganyizi.

Msimamizi huyo alisema ofisi hiyo ilikuwa imepokea barua mbili tofauti kutoka NCCR – Mageuzi, moja ikisema chama kilikuwa hakijapata mgombea katika kata hiyo na ya pili ya Dk Amani.

Akizungumza katika ofisi hiyo, Dk Amani alisema amechukua uamuzi huo baada ya kutoridhika na kitendo alichofanyiwa ndani ya CCM kwa kuwa aliongoza kwenye kura za maoni lakini akakatwa.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya NCCR Mageuzi, Angelina Mutaihwa alisema Ukawa katika kata hiyo walikuwa hawajateua mgombea lakini baada ya kujadiliana litapitishwa jina moja.

Vyama vilivyoachwa na vilivyoondolewa kuwania Urais Tanzania 2015

Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) imewafuta wagombea urais kadhaa kwa kushindwa kufikia vigezo vilivyowekwa ama kutokurejesha fomu (chama cha AFP) kama ilivyopangwa.

Wagombea waliokatwa na (na vyama vyao katika mabano) ni:-
 1. John Chipaka (ADA-TADEA)
 2. Mchungaji Christopher Mtikila (DP)
 3. Godfrey Malissa (CCK)
 4. Omari Sombi (AFP)
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema kuwa wagombea wa vyama 8 kati ya 12 vilivyochukua fomu, wamekidhi matakwa na hivyo wanaruhusiwa kuanza kampeni rasmi kesho.

Waliopitishwa na NEC (na vyama vyao katika mabano) ni:-
 1. Dk. John Magufuli (CCM)
 2. Edward Lowassa (CHADEMA)
 3. Fahmi Dovutwa (UPDP)
 4. Macmillan Lyimo (TLP)
 5. Chief Lutalosa Yemba (ADC)
 6. Anna Mghwira (ACT-Wazalendo) 
 7. Hashimu Rungwe (CHAUmma) 
 8. Malik Kasambala (NRA)

ACT – Wazalendo yamsimamisha uongozi Katibu

Kutoka Mwanza, Mwandishi wetu Christopher Gamaina, anaripoti kuwa chama cha ACT – Wazalendo Mkoa wa Mwanza kimemsimamisha uongozi Katibu wa chama hicho Jimbo la Ilemela, Omary Shigemelo kutokana na kilichoeleza kuwa ameshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Mwenyekiti wa ACT – Wazalendo Mkoa wa Mwanza, Chacha Okong'o aliliambia gazeti la Raia Tanzania jijini hapa jana, kwamba Kamati ya Uongozi wa mkoa wa chama hicho ikiyoketi Agosti 12, mwaka huu ndiyo iliazimia kumsimamisha katibu huyo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, Katibu huyo anatuhumiwa kukiuka maadili ya uongozi ikiwa ni pamoja na kujihisisha na vitendo vya rushwa wakati wa mchakato wa kura za maoni za ubunge wa Ilemela ndani ya chama hicho.
"(Shigemelo) ulianza jamoeni chafu kugomesha mchakato wa kura za maoni za udiwani katika jimbo la Ilemela… Mwenyekiti wa Mkoa alipokuhoji ulinjibu kwa kejeli na lugha chafu za matusi," 
inasema sehemu ya barua ya kumsimamisha Shigemelo uongozi huo yenye Kumb. Na. ACT/MZA/KM/VOL.II/004/2015 ya Agosti 12, mwaka huu.

List of Africa's Top 100 Research Journals

S/NJournal *h5 Index **JIF
1African Journal of Business Management3631.09
2African Journal of Biotechnology3534.82
3Journal of Medicinal Plants Research3524.73
4International Journal of Physical Sciences2914.82
5South African Journal of Botany2618.73
6African Journal of Microbiology Research2424.08
7South African Medical Journal2421.86
8Scientific Research and Essays2420.96
9African Journal of Agricultural Research2228.14
10African Journal of Pharmacy and Pharmacology2215.45
11African Health Sciences2113.13
12Tropical Journal of Pharmaceutical Research2014.14
13South African Journal of Science1921.64
14South African Journal of Education1915.51
15African Journal of Food Science1911.23
16African Journal of Traditional, Complementary and Alternative Medicines1910.03
17Pan African Medical Journal1816.27
18SA Journal of Industrial Psychology1812.47
19African Journal of Marine Science188.88
20Cardiovascular Journal of Africa187.66
21African Journal of Environmental Science and Technology1710.78
22Nigerian Journal of Clinical Practice177.92
23East African Journal of Ophthalmology175.47
24Middle East African Journal of Ophthalmology175.01
25African Journal of Ecology1618.23
26African Journal of Reproductive Health1612.94
27Educational Research and Reviews1610.85
28African Journal of Plant Science168.43
29African Journal of Psychiatry167.19
30Economic Research Southern Africa Working Papers161.38
31Annals of African Medicine158.05
32Ghana Medical Journal157.75
33Ethiopian Journal of Health Sciences153.76
34Journal of Economics and International Finance147.19
35Alexandria Engineering Journal146.58
36South African Journal of Psychology1416.47
37South African Journal of Human Resource Management143.06
38SAHARA-J: Journal of Social Aspects of HIV/AIDS137.97
39African Journal of AIDS Research139.82
40Ethiopian Journal of Health Development137.61
41Journal of Applied Sciences and Environmental Management137.02
42Journal of Geography and Regional Planning136.63
43Journal of Public Health and Epidemiology135.58
44Journal of Environmental Chemistry and Ecotoxicology133.36
45South African Journal of Economics1215.14
46Koedoe1211.17
47International Journal of Biodiversity and Conservation126.89
48African Journal of Biochemistry Research126.08
49African Journal of Pure and Applied Chemistry125.70
50Annals of Medical and Health Sciences Research125.38
51African Archaeological Review128.84
52South African Journal of Clinical Nutrition125.10
53African Journal of Paediatric Surgery124.50
54Journal of Plant Breeding and Crop Science124.38
55Libyan Journal of Medicine124.19
56South African Journal of Higher Education1112.42
57Journal of Toxicology and Environmental Health Sciences112.67
58South African Journal of Animal Science1111.26
59African Journal of Food, Agriculture, Nutrition and Development119.82
60South African Journal of Geology119.49
61South African Archaeological Bulletin119.15
62West African Journal of Medicine118.10
63Nigerian Journal of Medicine117.52
64Journal of Development and Agricultural Economics116.89
65Ethiopian Medical Journal116.52
66South African Journal of Enology and Viticulture116.26
67Nigerian Medical Journal115.83
68Tanzania Journal of Health Research115.52
69Tunisie Medicale1112.28
70Journal of African Business116.63
71South African Dental Journal115.16
72Bulletin of the Chemical Society of Ethiopia114.94
73Journal of the Egyptian Mathematical Society114.04
74Journal of Microbiology and Antimicrobials102.89
75African Zoology1010.94
76African Crop Science Journal1010.17
77Onderstepoort Journal of Veterinary Research109.93
78Journal of Engineering and Technology Research108.31
79Journal of the Southern African Institute of Mining107.83
80South African Journal of Economic and Management Sciences107.19
81Arab Journal of Nephrology and Transplantation102.08
82South African Journal of International Affairs106.88
83International Journal of Medicine and Medical Sciences106.57
84African Journal of Political Science and International Relations106.33
85Southern African Journal of HIV Medicine106.16
86African Primary Health Care and Family Medicine101.85
87International NGO Journal105.46
88South African Journal of Surgery105.20
89Journal of Ecology and The Natural Environment104.92
90Journal of the Egyptian Public Health Association103.89
91Journal of the Egyptian National Cancer Institute92.83
92South African Family Practice912.33
93South African Journal of Business Management912.19
94South African Journal of Wildlife Research99.38
95Journal of Psychology in Africa99.00
96Journal of the South African Veterinary Association98.52
97HTS Teologiese Studies / Theological Studies97.08
98African Journal of Aquatic Science97.07
99Journal of the Egyptian Society of Parasitology97.00
100African Journal of Medicine and Medical Sciences96.57
See the complete list of African Journals Indexed by Google Scholar in 2015

First seen at Wanazuoni Yahoo! Groups