Mndeme: Tuambiane ukweli wa kinachoitwa saisa za ukanda

Sehemu ya Pili: Tuambiane Ukweli kinachoitwa Saisa za Ukanda

A: Utangulizi
Nianze makala hii kwa kusema kwamba nikiwa nimeshaandika sehemu kubwa ya makala hii, nimekutana na makala ya ndugu Julius Mtatiro ambaye ni mwanachama wa CUF na mgombea ubunge jimbo la Segerea, akielezea kwamba siku ya jana amepokea simu kadhaa za viongozi wakuu serikali, wakijenga hoja za ukanda hasa baada ya Mhe. Sumaye kuhamia upinzani (iko hapa). Makala ya Mtatiro imenishtua sana kusikia kwamba kuna watu ndani ya serikali wanafanya kila mbinu "eti watu wa kaskanzini wasiingie Ikulu". Makala yake imenipa sababu moja ya zaidi kumalizia makala yangu kwani jambo hili ni zaidi ya hatari.

Uchaguzi mkuu umewadia na ni wakati mwingine wa watanzania kujiandaa kisaikologia kusikia kila aina ya matusi, vijembe, shutuma, na lugha zenye lengo mbaya juu ya umoja wa nchi yetu. Sisemi haya kama mtabiri bali nasimulia tu yale ambayo tayari tumeshaanza kuyaona na kuyasikia tangu  Jaji Lubuva na timu yake wapulize kipenga cha uchaguzi. Imekua kawaida kwenye siasa za nchi yetu kwamba tunaposhindwa kushindana kwa hoja na misingi au tunapogundua hoja zetu hazina mashiko, basi kimbilio letu ni ama lugha za kuchafuana, kutukanana, kudhalilishana au kujenga chuki kwenye mioyo ya wananchi dhidi ya tunaowaona kama maadui zetu kisiasa.
B: Hoja za Ukanda na ukweli kuhusu Ushawishi wa kimaeneo na makundi ya kijamii
Mojawapo ya hoja za ubaguzi zinazouzika sana kwenye siasa ni ile inayoitwa Siasa za Ukanda. Imekua kawaida sana kusikia baadhi ya wanasiasa au vyama vya siasa vikishutumiwa kwamba ni vya kikanda au ukabila na hivyo tusiwaunge mkono maana malengo yao sio mazuri kwa umoja wa taifa letu. Pamoja na kwamba wazo hili la kupinga ukanda na ukabila ni sahihi na jema, ila ushahidi unaotumiwa kama msingi wa hoja hii ni dhaifu sana, hautumii ukweli na unapingana na uhalisia wa mambo ambayo katika jamii yoyote ile yako wazi na ndivyo yalivyo. Mojawapo ni hili la ushabiki wa kisiasa unaoitwa wa kikanda, kimkoa au kikabila.

NI kawaida katika maisha, mtu anapokua na ushashiwi (influence), nguvu ya ushawishi wake huanza kuonekana kwa kuwaathiri wale walio karibu nae. Walio karibu nae, inategemea na aina ya ushawishi aliona nao. Kuna mtu mwingine ushawishi wake unaishia kwa familia yake tu, wengine eneo ushawishi wake unapofika. Kwa upande mwingine, ushawishi unaweza kuwalenga na kuonekana katika katika kundi fulani kwenye jamii; kwa mfano kundi la kidini, wasanii, wanamichezo, fani na kadhalika. Ndiyo mana wako watu wanamfahamu vema Diamond Platinum lakini hawajui chochote kuhusu Rose Mhando ambaye jina lake ni maarufu miongoni mwa kundi la dini. Ndiyo mana Profesa Shivji ni maarufu sana miongoni mwa wanazuoni lakini wako watanzania ambao ukitaja jina lake watakuuliza iwapo ni mwekezaji. Kwa wanaofuatilia diplomasia ya kimataifa wamemtambua Balozi Dk. Maiga na kazi kubwa aliyofanya akituwakilisha Umoja wa Mataifa wakati kun waliomsikia kwa mara ya kwanza alipojitokeza kugombea ubunge.
Siasa ya vyama vingi ilipoanza mwaka 1992 katika nchi yetu, CCM kilikua ni chama kilichoshika hatamu na kikiwa na mizizi kila kona ya nchi yetu. Watu walikijua na kukiheshimu chama kuliko hata serikali na fahari ya utaifa iliendana na uanachama ndani ya CCM. Kwamba CCM ni chama chenye wapenzi au wanachama kila kijiji cha nchi yetu sio  muujiza, sio mafanikio wala sio uvumbuzi: zaidi sana tungeshangaa isingekua hivyo. Tungeshangaa kwa sababu kilikuwa pekee kabla ya vingine vyote kikiwa na mfumo imara wa uongozi ambao hadi leo kuna watu wanashindwa kuutofautisha na mfumo wa uongozi serikalini.
Vyama vya upinzani vilianzishwa na watu wachache waliojitoa muhanga kuleta fikra mbadala ya utawala wa nchi kinyume na chama dola. Ni dhahiri kabisa kama nilivyosema hapo juu, kwamba watu hawa kwa kuanzia mawazo yao yalikubalika na kupata upenzi na ushabiki maeneo walikotoka. Ilikua rahisi watu waTabora kumwelewa na kuwasikiliza akina James Mapalala walioanzisha chama cha CUF kuliko watu wa Masasi. Ilikua rahisi watu wa Kilimanjaro kuelewa na mawazo ya kina Mzee Mtei  wa CHADEMA kuliko watu wa Mlalo kule Lushoto. Wale walioanzisha chama cha ZUF ambacho baadaye kilikuja kuungana na cha bara kufanya CUF ili kikizi matakwa ya kimuungano, ni wazi kwamba walieleweka kirahisi kule Zenji kuliko wangepeleka ujumbe wao kule Bunda.
Kwa minajili hiyo, ni wazi kwamba vyama hivi villipoanzishwa vilipata washabiki na wapenzi maeneo ya waanzilishi wao kuliko maeneo mengine ya nchi yetu. Ndiyo mana cha cha UDP cha kina Mzee Cheyo kimekua na nguvu wilaya yake ya Bariadi kuliko maeneo mengine na amekua mbunge wa wilaya hiyo kwa muda mrefu. Ndiyo mana CHADEMA kilianza kwa kuwa na wapenzi zaidi Kilimanjaro kuliko maeneo mengine ya nchi. Wakati Mrema akiwa NCCR alipata washabiki wengi Kaskazini mwa nchi na ninakumbuka hata wilaya yangu ya Arumeru kipindi kile ilipata mbunge aliyeitwa Kisanga ambaye hakua mwenyeji wala hakujuliakana lakini alichaguliwa kwa kua aligombea kupitia NCCR. Nakumbuka mbunge huyu kwa miaka  yote mitano sidhani kama hata aliwahi kurudi kutushukuru wananchi na hicho ndiyo kikawa kifo cha NCCR Arumeru na kukosa wapenzi. Ndiyo mana chama cha NLD cha Dr. Makaidi kimekuwepo miaka mingi lakini watanzania wengi wameanza kukisikia kama chama hai baada ya kujiunga na kundi la UKAWA. Chama hiki hadi sasa kina nguvu na utambulisho mkubwa kule Masasi ambapo ndiko anatoka Makaidi na wakati wa bunge la Katiba, Mzee huyu kwa uhalali kabisa alijimwaga bungeni akiwa na mke wake kama wawakilishi halili wa chama chao kwenye bunge lile. Mifano ni mingi.
C: Hali Ikoje tulikoiga mfumo wa Demokrasia
Swala la vyama vya siasa kuwa na ushawishi kwenye eneo au maeneo fulani pekee au zaidi kuliko mengine kwenye nchi za kidemokraisa sio jambo la ajabu na haliko Tanzania pekee. Hata nchi zilizoendelea zenye ukomavu wa kidemokrasia na zisizo na makabila katika jamii zao, zinadhihirisha ukweli huu. Nitoe mifano katika nchi 2 zenye mifumo ya kimuungano kama sisi:
 1. Uingereza:
  1. Katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi May mwaka huu, pamoja na vyama vikuu vya Labour na Conservative, kulikua na vyama vidogo ambavyo vingine vina wanachama wachache chini ya 1,000 na majina yao yanaakisi eneo kinapotoka.
  2. Wabunge karibu wote kutoka Scotland walioko kwenye bunge la makabwela (house of Common) wanatoka chama kimoja cha Scottish National Party (SNP). Chama hiki hakina mbunge hata mmoja kutoka Wales, Northern Ireland wala England na sina hakika hata kama kina wanachama kwenye maeneo hayo. Kwa nini? Kilianzishwa huko na kilikuja na ajenda ya kutetea zaidi maslahi ya Waskotishi katika muungano wa nchi ya Uingereza .
  3. Hata vyama vikuu vya Labour na Conservative havina ushahiwishi sawa maeneo yote. Conservative kinachoongoza serikali kwa sasa hakina mbunge hata mmoja toka Northern Ireland na Scotland. Hata ndani ya England, kuna maeneo kama ya katikati na Kaskazini Magharibi mwa nchi pamoja na jiji la London, miaka yote yanajulikana ni ngome ya chama cha wafanyakazi (Labour). Hii imetokana na ukweli kwamba maeneo haya ndiyo yalikua ngome ya mapinduzi ya viwanda na hivyo kujaa wafanyakazi zaidi. Pia inajulikana kwamba chama cha Conservative kina wapenzi zaidi maeneo ya vijijini walipo wakulima na wale waingereza wa asili.
Picha1: Ramani hii inaonesha matokeo ya uchaguzi wa bunge la Uingereza mwaka 2015 yakionesha jinsi vyama vya siasa vilivyo na ushawishi kulingana na maeneo. Hali hii sio ya mwaka huu peke yake bali inahakisi ushawishi wa vyama hivi hata miaka mingine.

Ufunguo: Rangi ya Bluu: Conservative: Nyekundu/ maruni: Labour, Njano: SNP, Kijani: Green, rangi zingine ni vyama vingine vidogovidogo.
https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/3/3e/2015UKElectionMap.svg/2000px-2015UKElectionMap.svg.png
D: Marekani: Picha 2 inaonesha matokeo ya uchauzi wa mwaka 2012
  1. Marekani ni muungano wa nchi au majimbo 50 na ina vyama vingi vya siasa ingawa vinavyojulikana zaidi ni Democratic na Republican. Vyama hivi vina ushawishi unaotofautina kutoka jimbo moja kwenda lingine. Wakati Democratic wana wafuasi zaidi kutoka yale maeneo ya watu weusi na miji yenye mchanganyiko wa watu kama New York na wapenzi wengi ni watu wa kipata cha chini na cha kati, Republican wako zaidi majimbo ya watu weupe na wapenzi wengi ni matajiri wanaokumbatia mfumo upebari
  2. Chaguzi za Marekani miaka yote zinajulikana kutawaliwa na kinachoitwa Blue States (ngome ya Democratic) na Red States (ngome ya Republican). Pamoja na kwamba wingi wa kura kila chama inachopata hutofautina kila chaguzi, lakini bado ushawishi a upenzi wa vyama kwenye majimbo ni dhahihiri kila uchaguzi.

Sheria ya vyama vingi, haivipi vyama vya siasa mamlaka ya kulazimisha wananchi kuwa wanachama bali watu wanatakiwa kujiunga na vyama vya siasa kwa hiyari yao wenyewe. Hivyo Mzee Cheyo au Makaidi na vyama vyao wasingeweza kulazimisha watu wa mikoa mingine wajiunge na vyama vyao ili visionekane ni vya maeneo machache pekee.  
https://sundipmeghani.files.wordpress.com/2012/01/usmap2.png
Picha2: Matokeo ya kura za Urais wa Marekani mwaka 2012
Pamoja na ukweli wa nchi mbili hizi ambao ndiyo viranja wa demokraisa duniani, huwezi kusikia watu wake wakitengana na kuonana maadui kwa vigezo hivi. Huwezi kusikia wakati wa kampeni wanatoa lugha za kuonesha kwamba ni dhambi/uadui/ugaidi na hatari kwa nchi kwa chama kuwa na wapenzi wengi wa eneo na hivyo kukosa uhalali wa kuongoza. Kwa nini? Ni kwa sabau hayo sio mambo ya msingi na hakuna anayeweza kuamua ugawanyiko wa upenzi wa kisiasa kwa vyama miongoni mwa wananchi kwanbi sababu zingine ni za kiasili kabisa na kuzichokonoa ni kutafuta uchonganishi na uchochezi usio na maana. Ni ajabu kwamba, wale wanazi na wafahidhina wa kabila, udini na ukanda, kwa makusudi kabisa, wanaupuuzia ukweli na uhalisia wa jambo hili na badala yake wameamua kuviandama baadhi ya vyama kwamba ni vya kikabila, kiukanda na kidini.


E: Uhanga wa CHADEMA
Kwa muda mrefu sasa, baadhi ya vyama hasa CHADEMA kimekua mhanga na kikiandamwa sana na hoja ya ukaskazini na ukabila. Unapokaa chini na kutizama ukweli wa hoja hii unashindwa kuona uhalisia. Uongozi wa CDM kwa maana ya kamati kuu una watu kutoka mikoa mingi na kutoka pande zote za muungano. Katika bunge lililolamaliza muda wake, chama hiki kina wabunge wa kuchaguliwa toka Mwanza, Mara, Kigoma, Dar, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Rukwa, Shinyanga, Singida, na Iringa. Sote twajua kwamba mikoa yote hii ni ngome kubwa ya CCM lakini chama hiki kimeweza kuwa na ushawishi, wanachama na wapenzi hata kuweza kupata wabunge. Sasa unaposikia hizi hukumu za kwamba hiki ni chama cha watu wa Kaskazini, unajiuliza hivi mikoa yote ya Tanzania imekua Kaskazini? Kwani kuna tangazo la Rais la karibuni lililobadilisha muundo wa mikoa?

Chama cha CUF kina wabunge nadhani 2 tu wa kuchaguliwa katika bunge lilopita kutoka bara na wengine wametoka visiwani. Je CUF ni chama cha kanda gani? CCM kwa miaka mingi sasa haina wabunge kule Pemba kama CDM na CUF wasivyo na wabunge mkoa wa Dodoma, hivi CC nacho ni chama cha kikanda kwa kukosa ushawishi Pemba na kuwa na ushawishi mdogo kule Kigoma?
Ukifikiria mambo haya vizuri, unaweza kuona kabisa kwamba sio tu hayana ukweli bali ni mpango mzima wa kujenga chuki, mgawanyiko na hisia za kihasama miongoni mwa watanzania. Utagundua haya ni mapepo machafu ya chuki na uadui ambayo yanapandikizwa na wafahidhina wanaotaka kutumia kila mbinu chafu kutafuta kupendwa au kuungwa mkono kisiasa kwa gharama za amani ya nchi yetu. Huku ni kujenga chuki na uchonganishi miongoni mwa wananchi. Nilisema kwenye makala iliyotangulia kwamba watu hawa wanaotuhubiria ukanda, ukabila na udini ni wa kukataliwa, kuzomewa na kudharauliwa na watanzania wote wanaoipenda nchi yao.
Nitaendelea na sehemu ya mwisho kueleza athari za mitazamo ya kikanda Tanzania
Mwalimu MM ni mhadhiri katika kitengo cha Sayansi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mtafiti wa mifumo ya TEHAMA (ICT) katika Huduma za Afya (Health Informatics). Unaweza kuwasiliana naye kupitia [email protected] na kusoma makala zake kupitia: mwalimumm.blogspot.com

Majaji wa Miss Tanzania USA wamvua taji Doreen na kumvika Aeesha nje ya ukumbi

Aeesha Kamara
Aeesha Kamara sasa ndiye mshindi wa Miss Tanzania USA pageant
Doreen Panga kutoka New York usiku wa Aug 22, 2015, alivuliwa taji la Miss Tanzania USA na majaji wa shindano hilo nje ya ukumbi taji alilolivaa kwa dakika 45 na kumvika Aeesha Kamara wa Maryland kwa madai kwamba Doreen Panga hakua chaguo lao.

Majaji hao Peter Walden, Elaine Roecklein, Tee Thompson, Bertini Huemegni, Tina Semiti Magembe, Mayor Mlima, Uche Ibezzue wakiongozwa na Michael Lewis McBride kwa pamoja walikataa kukubaliana na mshindi aliyetangazwa na kufanya kikao nje ya ukumbi wakati watu wakiondoka ondoka huku nao wakisikitishwa na maamuzi ya kutangazwa mshindi ambaye hawakumtarajia.

Kama majaji wangekaa kimya basi masahabiki wa shindano hilo wangepelekea lawama kwa majaji.Jaji Dr. Secelela Malecela japo kwamba alipingana na Doreen Panga kutangazwa mshindi lakini hakukubaliana na majaji wenzake Doreen avuliwe taji na apewe Aeesha Kamara aliyekua chagua la majaji wengine, yeye alipendekeza kwa kua kosa lishafanyika waachane nalo wahakikishe mwakani halitokei tena. Wazo lake lilipingwa na majaji wenzake pale pale.

Shindano hilo lilianza vizuri kwa nyimbo za Taifa za Marekani na Tanzania zilizoongozwa na watoto Brian akiwa kwenye kinanda na dada yake Briana akiwa kwenye kipza sauti,

Baadaye walitambulishwa ma miss wa kesho watoto wa DMV wenye umri wa miaka 9 na 12 na baada ya hapo waliingia malikia wenyewe huku wakisindikizwa na wimbo wa Diamond wa mdogo mdogo na baadaye kujitambulisha kwa majaji.

Washiriki wa miss Tanzania USA walikua Rechel Mujaya kutoka Atlanta, Joyce Mkapa toka New York, Doreen Panga toka New York, Aeesha Kamara toka Maryland, Aziza Gama toka Maryland na Brenda Panga toka New York. Washiriki walianza shindano kwa kujielezea wakifuatia na shindano la vipaji na baadae kujibu maswali ya majaji.

Pia katika shindano hilo kulikua na burudani mbalimbali akiwemo Mr Tz ambaye aliitambulisha singo ya wimbo wake mpya uliotoka mwei uliopita, Wasanii wengine walikua kutoka Ivory Coast na Jamaica.

Baada ya hapo ndipo kulitangazwa mshindi kuwa ni Doreen Panga ushindi ambao waliowengi hawakukubaliana nao wakiwemo majaji na mkurugenzi na mwanzilishi wa Miss Africa USA ambao walisikika wakinong'ona huku wakiulizana imekuaje bila kupata majibu.

Wakati majaji wakiwa nje ya ukumbi wakitafakali imekuaje tumeacha shughuli zetu tumekuja hapa tunatoa maamuzi sasahihi halafu mtu anatuzarau maamuzi yetu. Mashabiki walianza kuondoka baada ya shindano hilo kufikia ukingoni na wengine wakimtupia lawama wandaaji kwa kuvurunda shindano.

Majaji walipokua wakijadiliana wafanye nini walikuja na kuazimia kwa kauli moja lazima wampe ukweli mwandaaji kwamba hawakufurahika na kilichotokea ndani ya ukumbi. Mwandaaji wa Miss Tanzania USA aliitwa ndipo majaji wakatoa dukuduku lao na mwandaaji akajitetea kwamba mshindi amesema hataweza kushiriki mashindano hayo na ameamua kumpa taji mshindi wa pili ambaye alikua Aziza Gama, baada ya kusikia hayo majaji walimwita Doreen Panga na kumuuliza sababu yake ya kutaka kumvisha taji mshindi wa pili ni nini yeye akawajibu ni kutokana na kazi zangu ninazofanya hospitali sitaweza kupata muda wa ushiriki kwa hiyo badala yake nitampa taji mshindi wa pili.

Majaji walishindwa kuafikiana na Doreen na kuamua kupiga kura upya ndipo wote kwa pamoja kasolo Dk Secelea Malexela walimchagua Aeesha Kamara kwamba ndiye aliyestahiki kuvigwa taji na ndio aliyekua chaguo lao.

Doreen Panga akavuliwa taji na kuvikwa Aeesha Kamara huku Doreen akionesha kutokubaliana na majaji lakini wao ndio waamuzi wa mwisho na kitendo walichokifanya ni kulinda heshima yao.

Sasa Miss Tanzania USA ni Aeesha Kamara, mshindi wa pili ni Aziza Gama na mshindi wa tatu ni Joyce Mkapa.
Miss Africa 2014-15 akipata picha ya pamoja na Doreen Panga baada ya kuvikwa taji la Miss Tanzania USA 

Miss Africa 2014-15 akipata picha ya pamoja na Aeesha Kamara baada kuvikwa taji na maamuzi ya majaji ambao hawakukubaliana na mshindi aliyetangazwa kwanza.

Tumeshirikishwa taarifa hii na Kwanza Production

Kilometa za barabara zaidi ya elfu sita zajengwa nchini katika miaka 10Sumbawanga -- NAJIWEKA vyema kwenye kiti na kutazama nje kupitia dirishani. Japokuwa giza limetanda majira haya ya saa 4:30 usiku, lakini ninaweza kuhisi jinsi basi hili nililopanda la kampuni ya Majinjah linavyotafuna lami.

Abiria mwenzangu wa jirani ananiambai tutaingia saa sita kasoro usiku mjini Sumbawanga mjini. Nafarijika japo uchovu ni mwingi, maana kuketi kwenye basi kwa saa takriban 15 siyo mchezo ingawa tulipata nafasi mara kadhaa za kupumzika 'kuchimba dawa' na kupata mlo.

“Barabara yote ni lami tupu ndugu yangu, kasoro tu ni haya matuta kutoka Tunduma hadi Sumbawanga, lakini yamesaidia kupunguza mwendokasi,” ananieleza.

Tunduma tumeondoka kama saa tatu hivi kuzikabili kilometa 222 hadi Sumbawanga, lakini safari hii ya kutoka Dar es Salaam inayokadiriwa kuwa na umbali wa kilometa 1,000 imekuwa siyo ndefu licha ya uchovu wa kiuno na mgongo kutokana na kuketi tangu saa 12 alfajiri. Faraja pekee ni kwamba ninatumia siku moja tu kufika Sumbawanga, tofauti na miaka mitano iliyopita ambapo nililazimika kutumia siku mbili huku nikiingia gharama za ziada za kulala Lodge pale Mbeya kutokana na kutokuwepo na usafiri wa uhakika kutokana na ubovu wa barabara.

Wakati huo, ukilala Mbeya unalazimika tena kuamka mapema kuwahi basi ambalo licha ya kuondoka saa 12 alfajiri, bado litafika Sumbawanga saa 8 mchana.

Jirani yangu ananiambia kwamba sasa unaweza kwenda na kurudi Sumbawanga mara mbili ukitokea Mbeya kwani mabasi ni mengi na njia ‘inateleza’.

“Wametukomboa sana, magari hayajazi kama zamani, unasafiri kwa raha na kwa wakati – muda wowote unaotaka,” ananieleza.

Ndiyo. Nakumbuka safari moja wakati nikitokea Sumbawanga jinsi basi lilivyokuwa limejaza abiria mpaka sehemu ya kupita ikakosekana. Walioketi walikuwa wachache kuliko waliosimama, sasa piga hesabu lilikuwa na abiria wangapi! Hata kondatka mwenyewe alilazimika kupita kwa kuinama juu ya siti ili kwenda nyuma kuwapanga abiria waliosimama na kuchukua nauli. Ilikuwa ni hatari.

Lakini leo barabara hii imetandikwa lami na imekuwa sehemu ya barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 6,276 ambazo zimetengenezwa na utawala huu wa Awamu ya Nne, huku sehemu kubwa yabarabara hizo ikiwa imesimamiwa na Dk. John Pombe Joseph Magufuli kama Waziri wa Miundombinu.

Nimezunguka karibu nchi nzima nikifanya habari za uchunguzi kwa miaka kumi iliyopita. Mazingira ya wakati ule na ya sasa ni tofauti kabisa, maeneo ambayo yalikuwa hayafikiki, hivi sasa hali ni nzuri.

Tangu Januari hadi Juni 2015 pekee nimezunguka karibu kilometa 20,000 hapa nchini. Nimezunguka nikitokea Iringa kwenda Arusha kupitia Dodoma-Singida hadi Manyara; nimezunguka kutoka Dar es Salaam-Kiteto-Kondoa hadi Babati; nimepita Babati-Kondoa-Mayamaya hadi Dodoma; nimepita Mwanza-Shinyanga-Tabora-Mpanda hadi Sumbawanga mpaka Mbeya; nimetoka Dar es Salaam-Njombe-Songea hadi Mbambabay; nimetoka Mwanza-Musoma hadi Sirari; nimezunguka Mwanza-Sengerema-Geita hadi Bukoba; nimetoka Bukoba kupita Kahama hadi Dar es Salaam; nimetoka Shinyanga-Maswa-Bariadi hadi Lamadi; na maeneo mengine mengi kwa miezi sita.

Hakika nilichokiona kinastahili kupongezwa kwamba kimefanyika. Ingawa barabara kadhaa zimesimama kutokana na kukosekana kwa fedha kufuatia msukosuko wa wafadhili kushindwa kutoa fungu, lakini nyingi kati ya hizo zimekamilika na kuiunganisha vyema Tanzania.

Nilipita wakati fulani ilipoanza kutengenezwa barabara hii, nadhani ilikuwa mwaka 2011 nikiwa katika harakati zangu za kuandika habari za maendeleo vijijini. Barabara hii ilimegwa katika vipande vitatu ili kuharakisha ujenzi wake na kuzingatia ubora.

Kipande cha kwanza kilikuwa kutoka Tunduma hadi Ikana chenye urefu wa kilometa 63.2 ambacho kilijengwa na kampuni ya Consolidated Contractors Group kwa gharama ya Dola 82.521 milioni; Kipande cha pili chenye urefu wa kilometa 64.2 kilikuwa kutoka Ikana hadi Laela na kilijengwa na kampuni ya China Newera (64.2km Ikana-Laela) kwa Dola 46.812 milioni; na kipande cha mwisho kilikuwa kutoka Laela hadi Sumbawanga chenye urefu wa kilometa 95.31 ambacho kilijengwa na kampuni ya Aarsleff-Interbeton J.V kwa gharama ya Dola 130.038 milioni. Kwa hiyo kilometa zote 222.71 ziligharimu jumla ya Dola 259.371 milioni ambazo ni fedha za wahisani na fedha za ndani.

Ni fedha nyingi sana lakini haziwezikuzidi thamani halisiya barabara hii ambayo licha ya kuwakomboa wananchi wa pembezoni hasa katika mikoa ya Mbeya, Rukwa na Katavi, lakini pia itasaidia kuiunganisha Tanzania na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa sababu ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilometa 112 kutoka Sumbawanga-Matai hadi bandari ya Kasanga katika Ziwa Tanganyika unaendelea chini ya kampuni ya China Railway 15th Bureau Group Corporation - CR15G kwa gharama ya Dola 80.912 milioni.

Dk. Magufuli, ambaye sasa ni mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), anazifahamu karibu barabara zote nchini na hatua zilikofikia. Alipoingia kwa mara ya kwanza bungeni mwaka 1995 baada ya kushinda katika jimbo la Chato akiwa na miaka 36 tu, Rais Benjamin Mkapa akamteua kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Miundombinu. Kazi ya Ubunge na unaibu waziri ilimpeleka salama hadi mwaka 2000.

Uchaguzi wa mwaka 2000 ulipoitishwa, Dk. Magufuli aligombea na kushinda kwa mara ya pili. Rais Mkapa akamteua kuwa Waziri wa Wizara ya Miundombinu, wadhifa aliodumua nao hadi kipindi cha uongozi wa Mkapa kilipomalizika.

Mwaka 2005 alishinda ubunge kwa mara ya tatu, lakini safari hii aliingia katika orodha ya wabunge waliopita bila kupingwa. Rais Jakaya Kikwete akamteua kuongoza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hadi mwaka 2008 alipohamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambayo aliiongoza hadi mwaka 2010.

Mwaka 2010 akagombea tena ubunge, lakini safarihii akapambana na mgombea wa Chadema, Rukumbuza Vedastus Albogast ambaye alitoa upinzani mkubwa ingawa hatimaye Magufuli alishinda kwa asilimia 66.39 dhidi ya asilimia 26.55 za mpinzani wake. Rais Kikwete akamrudisha katika Wizara ya Ujenzi ambako yuko hadi hivi sasa.

Tangu kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, wengi walikuwa wakimtaja Magufuli kwamba anafaa kuwania urais, lakini yeye alikaririwa akisema wakati huo kwamba hana mpango huo.

Hata makada wenzake walipoanza kuonyesha nia kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka huu, yeye hakuwa na papara na iliwashangaza wengi Mei 29 alipoamua kujitosa kimya kimya, akachukua fomu na kuondoka, bila mbwembwe wala madoido kama walivyofanya wengine.

Wanaomfahamu wanasema nguvu yake kubwa iko kwenye elimu yake, lakini kukaa muda mrefu kwenye wizara zake na mambo makubwa aliyoyafanya katika wizara alizopata kuziongoza, pamoja na uwezo wake wa kutoa maamuzi magumu kila mara vinampa sifa ya kuwa rais anayefaa katika kipindi hiki ambacho rushwa, ufisadi na ukosefu wa maadili vimetamalaki.

Udhaifu wake pekee unaotajwa na walio karibu yake ni kufanya maamuzi ya haraka, jambo ambalo linaweza kurekebishwa kwa kuwa ndani ya Taasisi ya Urais kuna washauri makini.

UJENZI WA BARABARA

Katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya awamu ya nne, barabara zenye urefu wa jumla ya 6,276.82km zimejengwa kwa gharama ya Dola 102,654.98 milioni, nyingi kati ya hizo zikiwa za lami na hivyo kuutengeneza mtandao imara wa miundombinu ya barabara.

Kujengwa kwa barabara hizo kumerahisisha hata usafiri ambapo leo hii magari ya abiria na mizigo kutoka Dar es Salaam kwenda Musoma, Mwanza, Kagera na Kigoma hayahitaji kuzunguka Nairobi bali yanakwenda moja kwa moja.

Hivi sasa usafiri wa kutoka Dar es Salaam kwenda Sumbawanga ni wa siku moja badala ya siku mbili, kama ilivyo kwa usafiri wa Dar es Salaam kwenda Mbinga, jambo ambalo miaka 10 iliyopita lilikuwa ndoto.

Asilimia 90 ya miradi hiyo imesimamiwa na Dk. Magufuli akiwa Waziri wa Miundombinu katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015na bado miradi mingine inaendelea kujengwa japo imesimama kidogo kutokana na ufinyu wa bajeti.

Kampuni za Kichina zimepata mikataba mingi ya ujenzi. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, kampuni 14 kutoka China zimeingia jumla ya mikataba 58 ya ujenzi wa kilometa 3,140.85 yenye thamani ya Dola 1.75 bilioni.

Kampuni ya China Henan International Cooperation Group Co., Ltd. (CHICO) ambayo ilipata mkataba wenye thamani ya Dola 206 milioni kutoka Wakala wa Barabara Zambia kujenga barabara ya Mansa-Luwingu yenye urefu wa kilometa 175, peke yake imeingia mikataba 13 nchini Tanzania ya barabara zenye urefu wa kilometa 705.2 zikiwa na thamani ya Dola 490.26 milioni.

Hizi ni pamoja na barabara za Singida-Iguguno (76km) yenye thamani ya Dola 20.55 milioni; Sekenke-Shelui (33km) yenye thamani ya Dola 12.51 milioni; Mwandiga-Manyovu (60km) wenye thamani ya Dola 32.54 milioni; Kigoma-Kidahwe (35.7km) kwa Dola 19.56 milioni; Bonga-Babati (19.20km) kwa Dola 11.95 milioni; Tabora-Urambo (42km) kwa Dola 31.17 milioni; Kyaka-Bugene (59.1km) kwa Dola 51.6 milioni; Dareda-Minjingu (84.6km) kwa Dola 51.6 milioni); Kidahwe-Uvinza-Ilunde (76.6km) kwa Dola 47.5 milioni; Isaka-Ushirombo (132km) kwa Dola 88.223 milioni; Kilwa Road Phase III (1.5km) kwa Dola 3.4 milioni; Nyanguse-Musoma (85.5km) kwa Dola 3.3 milioni; na Kagoma-Lusahunga (154km ) kwa ubia na kampuni ya CRSG kwa gharama ya Dola 116.2 milioni.

China Sichuan International Cooperation Co., Ltd (SIETCO) inajenga barabara zenye urefu wa 283.9km zenye thamani ya Dola 123.03 milioni ambazo ni Isuna-Singida (63km) kwa Dola 18.5 milioni; Tarakea-Rongai-Kamwanga (32km) kwa Dola 8.8 milioni; Iringa-Migori (95.1km) kwa Dola 51.123 milioni; na Migori-Fufu Escarpment (93.8km) kwa Dola 44.7 milioni, wakati kampuni ya CICO inajenga barabara ya Nangurukuru-Mbwemkuru yenye 95km kwa thamani ya Dola 23.82 milioni.

Kampuni ya China Geo-Engineering Corporation International Ltd (CGC INT'L) inajenga barabara zenye urefu wa 525.9km zikiwa na thamani ya Dola 151.2 milioni. Barabara hizo ni Shelui-Nzega (112km) kwa Dola 12.6 milioni; Kyamorwa-Buzirayombo (120km) kwa Dola 29.822 milioni; Manyoni-Isuna (54km) kwa Dola 18.4 milioni; Arusha-Namanga (104.2km) kwa Dola 49.64 milioni; Chalinze-Tanga Phase I (125km ) kwa Dola 25.9 milioni na ndiyo kampuni iliyojenga Daraja la Mkapa (Daraja la Umoja 10.7km) linalounganisha Tanzania na Msumbiji kwa gharama ya Dola 14.9 milioni.

Katika orodha hiyo, ipo kampuni inayomilikiwa na serikali ya China, Hydropower Engineering and Construction Company (SINOHYDRO) ambayo ilipata mikataba 12 nchini Tanzania ya ujenzi wa barabara zenye urefu wa jumla ya 779.95km zenye thamani ya Dola 434.36 milioni. Barabara hizo ni Sengerema-Usagara (40km) kwa gharama ya Dola 21.724 milioni; Buzirayombo-Geita (100km) kwa Dola 25 milioni; Geita-Sengerema (50km) kwa Dola 24.034 milioni; Dodoma-Mayamaya (43.65km) kwa Dola 25 milioni; Manyoni-Itigi-Chaya (89.3km) kwa Dola 66.56 milioni; Puge-Tabora (56.1km) kwa Dola 35.085 milioni; Handeni-Mkata (54km) kwa Dola 34.81 milioni; Korogwe-Handeni (65km) kwa Dola 38.4 milioni; Katesh-Dareda (73.8km) kwa Dola 38.94 milioni; Singida-Katesh (65.1km) kwa Dola 31.34 milioni; Tanga-Horohoro (65km) kwa Dola 42.43 milioni; na Peramiho Junction-Mbinga (78km) kwa Dola 48.444 milioni.


CHIKO ilijenga barabara ya Sam Nujoma jijini Dar es Salaam yenye urefu wa 4km kwa thamani ya Dola 7.9 milioni, China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) ilipata mikataba minne ya kujenga barabara zenye urefu wa 145.6km kwa thamani ya Dola 95 milioni. Barabara hizo ni Magole-Turiani (48.6km) kwa Dola 25.43 milioni; Tabora-Urambo (52km) kwa Dola 36.3 milioni; Dumila-Rudewa (45km) kwa Dola 25.5 milioni na Jangwani Depot kwa ajili ya mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar es Salaam (BRT) kwa Dola 7.81 milioni.


Wakati wakandarasi walipokuwa wanajenga daraja hili katika eneo la Miangalua kwenye barabara ya Tunduma-Sumbawanga mwaka 2011. Barabara hiyo sasa imekamilika.


Barabara ya Mwanza-Musoma iko katika hali nzuri.


Ujenzi wa barabara ukiendelea katika baadhi ya miradi nchini.


Ujenzi wa barabara ya Iringa-Dodoma umekamilika kwa asilimia 95, bado maeneo machache tu likiwemo hili la Mlima Nyang'oro ambapo Wachina wameuchonga ili kupunguza kona katika umbali wa kilometa 15.

Miradi mbalimbali ya barabara zilizojengwa na zinazoendelea kujengwa unaweza kuiona kwa kubofya hapa.
 • Tumeshirikishwa taarifa hii na Daniel Mbega, brotherdanny.com. Simu: 0656-331974)

Balozi mpya wa Tanzania nchini Marekani na Mexico awasili Washington, DC


Balozi mpya atakayeiwakilisha Tanzania nchini Marekani Mhe Wilson Masilingi akiwa amefuatana na Mkewe Marystella Masilingi pamoja na mwanae Nelson Masilingi wawasili kituoni kwake Washington DC, awali ya hapo Mhe Wilson Masilingi alikua Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi.


Mhe. Wilson Masilingi mara baada ya kutua Washington DC akisalimiana na atakayekuwa dereva wake Virgilio Paz maarufu kama Bong.


Safari ya Mheshimiwa Balozi pamoja na mama ikianza kuelekea hotelini ambapo atapumzika kwa muda kabla ya kuingia nyumbani kwake Bethesda, Maryland.


Mhe. Wilson Masilingi mara baada ya kufika Hotelini kwake akisaidiwa mlango na Afisa wa Ubalozi Swahiba Habib Mndeme.


Mhe. Balozi Wilson Masilingi akisalimiana na baadhi ya Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliofika kumlaki pichani ni mmoja wa Maafisa Andrew Mugendi Zoka.


Mama Marystella Masilingi naye hakua nyuma kusalimiana na baadhi ya Wafanyakazi na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania.


Mhe. Wilson Masilingi akiwa na bashasha tele kuona kwa jinsi gani Tanzania House walivyo na upendo na kuonyesha ushirikiano wao wa dhati kwenye tukio hilo muhimu.


Mhe Wilson Masilingi alifuatana na mtoto wake, Nelson Masilingi.


Maafisa wa Ubalozi Swahiba Mndeme pamoja na Alfred Swere wakiteta jambo kidogo.


Mhe Balozi Wilson Masilingi pamoja na Familia yake kwenye picha ya pamoja na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta.


Mhe Wilson Masilingi alipata fursa kidogo kutembelea mitaa ya jijini akiwa ameongozana na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta


Baadhi ya Wafanyakazi na Maafisa wa Tanzania House wakiwa Hotelini alipofikia Mhe Wilson Masilingi.
 • Picha: Kamera ya Ubalozi.

Wanaojidai wao ni chama cha ukombozi ni wapumbavu, malofa - Mkapa


Maoni ya Polepole kuhusu Sumaye kuhamia UKAWA

Mtatiro: Kaskazini wana mkakati wa kwenda Ikulu...

SIMU ZA KUUDHI: ETI WATU WA KASKAZINI WANA MKAKATI WA KWENDA IKULU! UPUUZI MTUPU!


Ndugu zangu, leo nimepigiwa simu zingine mbili za kuudhi sana, na jana nilipigiwa simu moja ya namna hiyo, na WANAOPIGA SIMU HIZI ni viongozi wakubwa kabisa katika nchi hii. Kwanza walikuwa wanataka OPINION yangu juu ya SUMAYE kujiunga na UKAWA, kila mmoja kwa wakati wake niliwajibu kuwa ni kitendo cha kidemokrasia na pia ni kitendo cha kuonesha kuwa CCM imefika kwenye ANGUKO KUBWA.

Wakubwa hawa kila mmoja kwa staili yake walianza kutaka kuniaminisha kuwa kitendo hicho kina maana kuwa watu wa Kaskazini (hasa wakitajwa WACHAGA) kuwa wanaungana ili kuchukua uongozi wa nchi. Wakubwa hao wakaendelea kunieleza kuwa mimi ntakuwa mmoja wa watanzania watakaounga mkono MKAKATI WA WACHAGA kuingia Ikulu? Simu hizi za kijinga zimeniudhi sana na leo nimeamua kuziandika hapa.

Wakubwa hao mmoja mmoja nimewajibu kwa uwazi kabisa kuwa ni WANAFIKI, WAOGA, WAKABILA na WATU WANAOTAPATAPA kwa kuhofia kuwa CCM ikiondoka madarakani nyadhifa zao walizopewa bila kuwa na sifa zitawaondoka. Sikuficha.

Na pili nimewaeleza kwa uwazi kuwa wao huko Serikalini ndio wanaoeneza UKABILA na UBAGUZI. Nimewakumbusha tuhuma nzito za UGAIDI na UISLAMU ambazo wamejaribu kwa miongo kadhaa kukitwisha Chama Cha Wananchi CUF, nimewakumbusha juu ya tuhuma za UKRISTO na MFUMO Kristo ambazo wamekuwa wakiibambikiza CHADEMA, nimewakumbusha mambo mengi ya kipuuzi yanayopikwa kwa sababu tu CCM ni lazima iokolewe, iendelee kubakia madarakani na kunyonya nchi hii ibakie mashimo matupu huku wakubwa wakitunza vijisenti vyao huko kwenye akaunti za nje, ambazo zilipewa kibali cha kuendelea kuwepo na Rasimu ya Katiba inayopendekezwa, baada ya ile ya Warioba kupiga marufuku akaunti hizo.

Tatu, nimewaeleza juu ya UPUUZI kuwa Lowassa anatekeleza mkakati wa watu wa kaskazini! Lowassa alianza mbio za kuutaka urais ndani ya CCM mwaka 1995 hadi leo ameendelea na "ndoto" na mbio hizo. Huyu ni mtanzania na ana haki ya kutimiza ndoto zake kwa kufuata sheria na utaratibu. Kama CCM na SERIKALI haiwataki hao WATU wa Kaskazini na WACHAGA mbona wamejaa serikalini kwenye vyeo vikubwa vikubwa? Mbona imewaacha wakawa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, mbona wamekuwa wabunge na mawaziri hadi wamekuwa mawaziri wakuu?

Hiyo kaskazini inayopigwa vita mbona ndiyo iliwatoa watu kama kina SOKOINE ambao mfano wao haujapata kutokea hadi leo hii? Nani anataka kuaminisha watanzania kuwa Rais wa Tanzania anapaswa kutoka Kusini, Mashariki na Magharibi na kwamba huko KASKAZINI ni mwiko kutoa Rais? Huu ni upuuzi wa hali ya juu na lazima tuukemee. Uungwaji mkono wa mgombea wa UKAWA umekuwa wa ajabu na wa kutisha huko Zanzibar, Mbeya, Mwanza n.k. Je, wale wanaompokea ni watu wa kaskazini? Ni wachaga? Ni upuuzi sana kufikiri KINYUMENYUME namna hii!

Watanzania wakae chini wawapime watu wanaogombea urais hivi sasa, waangalie rekodi zao, waangalie tuhuma walizowahi kukumbana nazo na uhusika wao, waangalie mazuri yao na mabaya yao, waangalie mifumo ambayo wagombe wamo na kama wanaweza kuleta mabadiliko ya nchi wakiwa humo, waangalie ukaribu wao na wananchi na waangalie uwezo wao wa kuwa viongozi wakuu wa nchi ambayo itafanya maamuzi haraka, kupga vita uzembe na kusonga mbele. Watanzania leo kamwe wasikubali kuanza kutishwa na "visimu uchwara" ati "vinapiga mkwara" ati watu wa kaskazini wana mkakati wa kwenda ikulu. TUZIPIGE VITA SIMU ZA NAMNA HIYO na KAMPENI CHAFU NAMNA HIYO.

Mwalimu Nyerere alituasa sana kabla hajafa, kwamba hatutamchagua mtu kwa sababu ya kanda yake, kwa sababu ya kablia lake, kwa sababu ya dini yake na kwa sababu ya rangi au kipato chake. Tutamchagua mtu kwa sababu ya sifa zake. Magufuli na Lowassa wote wana sifa lakini mmoja wao ana sifa kuliko mwingine, tumpekue huyo na tumpe uongozi wa taifa hili ambalo halimo mikononi mwa watu maalum, ni letu sote na maamuzi ni yetu sote.

Na wale waliokuwa wanaituhumu CUF na Uislamu na CHADEMA na Ukristo na kama tuhuma hizo zina ukweli (JAPO NI ZA KIPUUZI) sasa watambue kuwa waliotuhumiwa kwa Ukristo na waliotuhumiwa kwa Uislamu sasa wameungana pamoja na kazi iliyoko mbele yao ni KUIONDOA CCM MADARAKANI.

Nawapiga marufuku viongozi wote serikalini wanaojaribu kupiga simu hizi za UKABILA, wakome mara moja kwa sababu wananchi wakiwasikiliza na kuanza kufanya mambo kikabila sote hatutakuwa salama.

Imeandikaw na
Julius Mtatiro,
Dar es Salaam,
+255787536759 (text message and whatsup only), [email protected]

Serikali yamiliki asilimia 100 za hiza za General Tyre

Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kumiliki kiwanda cha kutengeneze magurudumu ya magari cha General Tyre kwa asilimia 100 baada ya kununua hisa 26 zenye thamani ya dola moja milioni kutoka kwa kampuni ya Continental AG.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya Msajili wa Hazina wakati wa makabidhiano ya nyaraka za ununuzi wa hisa hizo Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue anasema jitihada za kuhakikisha kuwa serikali inamiliki hisa hizo zilianza tangu mwaka 2012 kwa kufanya mazungumzo ya awali na mwekezaji.
“Kufuatia hatua hii ya kuweza kumiliki hisa kwa asilimia 100 sasa tutakuwa na fursa ya kuzalisha magurudumu yetu wenyewe na hivyo kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kilichokuwa kikitumia kununua magurudumu kutoka nje” 
Aidha anaendelea kufafanua kuwa hatua itakayofuata ni kutamfuata muwekezaji atakayeshirikiana na Shirika la Maendelao la Taifa (NDC) katika kuzalisha magurudumu kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

Balozi Sefue anampongeza Rais Mhe. Jakaya Kikwete kwa kufanikisha zoezi zima la kuhakikisha serikali inamiliki hisa za kiwanda cha General Tyre kwa asilimia 100 na hivyo kufufua uchumi wa jiji la Arusha na Taifa kwa ujumla.

Naye Msajili wa Hazina Lawrence Mafuru anasema mpaka serikali kuweza kumiliki hisa hizo ni hatua kubwa sana kutokana na vikwazo mbalimbali vilivyokuwa vikiwekwa na mwekezaji wa kiwanda hicho kilichoanzishwa mwaka 1969.
“Haikuwa kazi rahisi kumiliki hisa hizi bila ya jitihada kubwa iliyofanywa na serikali katika kumshawishi mwekezaji baada ya kuona hana kuwa hakuwa tayari kuwekeza na hivyo kurejesha umiliki kwetu” 
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Uledi Musa, anaeleza kuwa kiwanda hicho kitatoa fursa za ajira zaidi kitakapoanza kuzalisha tofauti na awali ambapo kiliweza kuajiri wafanyakazi 360.

Wakazi wa Mwembeladu wakikagua taarifa zao BVR katika mbao

BAADHI ya wananchi katika wilaya ya Chake Chake wakiangalia majina ya wagombea Ubunge wa majimbo la yaliyomo ndani ya wilaya hiyo, nje ya Ubao wa matangazo wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kisiwani Pemba. (picha: Abdi Suleiman, PEMBA via  ZanziNews blog.)
WANANCHI wa Shehia ya Muembeladu wakiangalia majina yao katika daftari la wapiga kura wa lililobandikwa katika kituo cha kujiandisha cha skuli ya muembeladu kuangalia majina yao kama yako sawa (picha: ZanziNews blog)

Machali amwekea pingamizi mgombea Ubunge kutoka CCM

Mgombea Ubunge Jimbo la Kasulu Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Moses Machali, ameweka pingamizi la uteuzi wa mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Daniel Nsanzugwanko, kwa madai kuwa hafai kuwa mgombea baada ya kujaza fomu kuwa amezaliwa tarehe 15/08/2015.

Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 10 jioni baada ya wagombea wengine kuona fomu yake kwenye ubao matangazo wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu.

Machali alitoa pingamizi hilo jana kwa Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu, Fatina Hussein, kwa madai kuwa kutokana na mgombea wa ubunge kupitia CCM, Nsanzugwanko kujaza fomu kuwa alizaliwa tarehe hiyo, mwaka huu, hafai kuwa mgombea.

Kwa mujibu wa Machali, kisheria ni kosa kwa mtu mwenye umri chini ya miaka 21 kugombea nafasi ya ubunge, lakini pia kwa kosa hilo ambalo ni la kisheria ni wazi msimamizi wa uchaguzi anapaswa kutomteua mgombea huyo wa CCM ambaye kwa mujibu wa Machali, Nsanzugwanko ameapa kiapo kinachoonesha umri wake ni siku sita.

Alisema katika mazingira hayo amepoteza sifa za kuteuliwa kuwa mgombea na suala hilo halihitaji mjadala.

Hata hivyo, katika hatua iliyowashangaza wananchi ni pale Mkurugenzi huyo kutaka kubandua fomu hiyo ili abandike nyingine.

Akifafanua kuhusu hatua hiyo, Hussein alisema, juzi majira ya saa 10 jioni alibandika fomu kwenye ubao kama sheria inavyosema na ilionekana Nsanzugwanko alijaza fomu kuwa alizaliwa mwaka 2015.

Fatina alisema baada ya wagombea kubaini kuwa fomu ya mgombea wa CCM imekosewa aliwaambia wachukue fomu za pingamizi.

Mkurugenzi huyo aliwataka wagombea kuwa na amani na utulivu na kwamba fomu zitalindwa na uchaguzi utafanyika kwa haki.

Kwa upande wake CCM Nsanzugwanko alipoulizwa kuhusu tarehe hiyo ya kuzaliwa alijibu kwa kifupi: “ Je wewe unaamini, kwa heri.”

 • via Nipashe Jumapili

Streaming LIVE online: Ufunguzi wa kampeni za CCM