Chart: Most dangerous foods for dogs


Chart source: thebark.com (first seen at Lifehacker)

Call for applications: Queen's Young Leaders Awards


The Queen’s Young Leaders Award recognises exceptional people aged between 18-29 from across the Commonwealth, who are taking the lead in their communities and using their skills to transform lives. 
The search is now on for the winners of 2016. 

Are you: 
– working to support others? 
– creating positive change? 
– raising awareness of issues affecting your community? 

We’re looking for applicants working on a wide range of issues. The 2015 winners were working on projects including education, climate change, gender equality, disability equality, mental health and youth unemployment. 

Applications are now open. 

Visit www.queensyoungleaders.com for more information about the programme and how to apply #TheSearchIsOn @QueensLeaders

Winners of this prestigious Award will: 
● Receive a year of training and mentoring from The University of Cambridge 
● Take part in a one-week residential programme in the UK 
● Network with senior political and business leaders in the UK 
● Receive their Award from Her Majesty The Queen at Buckingham Palace

Picha za kampeni ya CCM Rukwa


Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM, Mhe. Mizengo Pinda akimtambulisha mgombea Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika ndani ya uwanja wa Nelson Mandela jioni ya leo.


Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Sumbawanga mjini mkoani Rukwa, ndani ya Uwanja wa Nelson Mandela kwenye mkutano wa kampeni,pichani nyuma ni Waziri Mkuu Pinda akishuhudia tukio hilo.Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa atawatumikia kwa nguvu zake zote, na hatokuwa na simile kwa watendaji wazembe.


Wananchi wa Sumbawanga mjini wakiwa wamefurika ndani ya uwanja wa Nelson Mandela wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akimwaga sera kwa wananchi


Wananchi wa Sumbawanga mjini waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Nelson Mandela jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliwahutubia.


Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mhe. Pinda akimtambulisha Dkt Magufuli kwa wananchi wa Kata ya Majimoto,wilaya ya Mlele mkoani Katavi kwenye mkutano wa Kampeni.


Umati wa wananchi wa Kitai wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli lipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano wa Kampeni.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Maji moto wilayani Mlele mkoani Katavi.


Umati wa wananchi wa Namanyere walayani Nkasi mkoani Rukwa wakiwa wamefurika wakimsikiliza Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli lipokuwa akiwahutubia jioni ya leo kwenye mkutano huo wa Kampeni


Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mjini tayari kuwahutubia wakazi wa mji huo.


Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Nelson Mandela.


Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Nelson Mandela.


Mgombea Ubunge wa jimbo la Mpimbwe,Dkt Pudenciana Kikwembe akimwombea kura Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Majimoto wilayani Mlele mkoani Katavi.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi jukwaani anaewania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Nkasi Ndugu Ali Keissy, mbele ya wananchi wa Namanyere wilayani Nkasi jioni ya leo kwenye mkutano wa Kampeni.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akimnadi jukwaani anaewania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Nkasi Ndugu Ali Keissy, mbele ya wananchi wa Namanyere wilayani Nkasi jioni ya leo kwenye mkutano wa Kampeni.


Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Nelson Mandela jioni ya leo.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa mji wa Namanyere wilayani Nkasi (hawapo pichani),kabla ya kuanza kuwahutubia kwenye mkutano huo wa kampeni. Katikati ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mhe. Mizengo Pinda pamoja na anaewania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Nkasi Ndugu Ali Keissy


Moja ya bango lililobebwa na baadhi ya wafuasi wa CCM ndani ya uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga jioni ya leo.


Kada wa CCM Mzee Chrisant Mzindakaya akiwahutubia wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk.John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Nelson Mandela.


Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Nelson Mandela jioni ya leo.


Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa Sumbawanga mjini kwenye mkutano wa kampeni ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa atawatumikia kwa nguvu zake zote, na hatokuwa na simile na watendaji wazembe.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe akiwapungia wananchi alipokuwa akiwasilia katika Kata ya Maji moto alipokwenda kuwahutubia wakazi wa kata hiyo wilayani Mlele mkoa wa Katavi.kulia kwa mgombea ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mhe.Pinda


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe akiwapungia wananchi alipokuwa akiwasilia katika Kata ya Maji moto alipokwenda kuwahutubia wakazi wa kata hiyo wilayani Mlele mkoa wa Katavi.kulia kwa mgombea ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mhe. Pinda


Wakifurahia jambo


Wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia kwenye mkutano wa kampeni ndani ya uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lunyala,wilayani Nkasi alipokuwa akielekea mjini Namanyere kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa kampeni.


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe (hayupo pichani) akiwahutubia wakazi wa kata ya Maji moto,wilayani Mlele mkoani Katavikwenye mkutano wa kampeni.
  • MICHUZI JR-RUKWA

Polisi Dar yaonesha picha ya anayetuhumiwa kufadhili uvamizi vituo vya polisi

Suleiman Kova akionesha picha ya mtuhumiwa huyo
Hatimaye Jeshi la Polisi Tanzania (PT) limeanika picha ya mtu anayedaiwa kuwa ndiye mfadhili mkuu wa matukio mbalimbali yanayohusishwa na ugaidi likiwemo lile la mauaji ya watu saba kwenye Kituo cha Polisi Sitaki Shari, Dar lililotokea saa 5 usiku, Julai 12, mwaka huu na yale mapigano ya Amboni, Tanga.

Mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Ally Mtozen Hery ambaye anadaiwa kuishi kwa kujibadili kama kinyonga kwa muonekano wa sura, wakati mwingine huvaa mavazi ya kike ili asijulikane kirahisi.

Akizungumza na Uwazi juzikati, Kamishna wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema uchunguzi uliyofanywa na kikosi kazi cha jeshi hilo umebaini kuwa, mtuhumiwa huyo ana mtandao mpana na ndiye mfadhali mkuu wa matukio mbalimbali ya uvamizi, mashambulio na uporaji wa silaha yanayotokea nchini.

Kova aliongeza kuwa, hivi karibunim Hery amehusika katika kufadhili tukio la Amboni Tanga, Mkuranga, Sitaki Shari na mengineyo lakini hatimaye jeshi la polisi kwa kutumia kikosi cha intelijensia kimeweza kubaini nyendo zake na kuinasa picha yake hiyo.

“Tunachotaka mtu huyo ajitokeze mara moja na kujisalimisha polisi, kwani hata afanyaje lazima tutamkamata tu,” alisema Kamishna Kova.

Akaongeza: “Ile milioni 50/= iliyotangazwa na IGP Ernest Mangu sasa imefikia mahala pake kwa mtu atakayeweza kusaidia kupatikana kwa mtuhumiwa huyo.”

Kova aliendelea kusema mtuhumiwa huyo wakati mwingine hupenda kutembelea Pemba, Tanga, Dar na ukanda mzima wa Pwani.Katika mahojiano na Kamishna Kova alisema hadi sasa, watuhumiwa tisa wanashikiliwa na jeshi hilo kutokana na tukio la Stakishari.

“Si vyema kuwataja kwa majina tunaowashikilia kwa sababu za kiupelelezi lakini hadi sasa kwa jitihada za jeshi letu makini tunawashikilia watuhumiwa tisa na mahojiano yanaendelea,” alisema Kova.

Mbali na mtuhumiwa huyo kusakwa na jeshi la polisi, mtuhumiwa mwingine aliyekuwa akisakwa na jeshi hilo amejisalimisha polisi akiwa na wake zake wawili na sasa anahojiwa kwa kina.

Aliongeza kusema mtuhumiwa huyo aliyejisalimisha polisi aliwahi kuwa mtumishi ndani ya jeshi la polisi lakini alifukuzwa kazi mwaka 1998 kutokana na kutoeleweka kwa nyendo zake.

Polisi huyo aliyeachishwa kazi akiwa na cheo cha Sajenti anafahamika kwa jina maarufu la Mzee Mzima ambapo akiwa kazini kitengo cha redio (999) ambacho hushughulikia matukio ya uhalifu kwa haraka nyendo zake zilikuwa hazieleweki ndani ya jeshi hilo.

“Hatuwezi kuvumilia damu za askari wetu zikipotea bure. Ni lazima tuhakikishe kazi tunaifanya ipasavyo na hao watuhumiwa tisa tunaowashikilia wanaendelea kutupa taarifa muhimu,” alisema Kova.
  • Imeandikwa na Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa via GPL

[audio] Kipindi cha Jukwaa langu cha Jumatatu Agosti 24, 2015

Kipindi hiki hukujia kila Jumatatu, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2015.

Hii ni sehemu ya kwanza ya kipindi kilichosikika Agosti 24, 2015...Sehemu ya pili..


Majimbo 5 ya CCM iliyokwishaweka kibindoni

Huku kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu zikiwa ndiyo kwanza zimeanza, tayari CCM imepata wabunge watano waliopita bila kupingwa.

Wabunge hao na majimbo waliyopita bila kupingwa ni
  1. Abdallah Chikota - Nanyamba (Mtwara) 
  2. Rashid Shangazi - Mlalo (Tanga)
  3. January Makamba - Bumbuli (Tanga)
  4. Jenista Mhagama - Peramiho (Ruvuma) 
  5. Deo Filikunjombe - Ludewa (Njombe)
Orodha imenukuliwa uktoka kwenye gazeti la Mwananchi la Jumanne, Agosti 25, 2015. Hata hivyo, gazeti la NIPASHE la Jumatano, Agosti 26, 2015 linaripoti ifuatavyo:

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekata rufani katika majimbo matatu ya Bumbuli, Mlalo na Ludewa baada ya pingamizi zake kutupiliwa mbali.

Pingamizi hizo zilitupiliwa mbali na Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo hayo na hivyo kuwatangaza wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamepita bila kupingwa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatala, alisema tayari wamewasilisha rufani na wanasubiri uamuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na wanaamini haki itatendeka.

Alisema Jimbo la Ludewa, Msimamizi wa Uchaguzi, alidai kwamba katika fomu ya mgombea wa CHADEMA haikuwa na fomu namba 10, huku mgombea akisema aliwasilisha kila kitu kinachohitajika ikiwamo fomu hiyo.

Kibatala alisema baada ya kufuatilia, ofisi ya msimamizi ilibaini kwamba wao ndiyo walifanya uzembe katika kuihifadhi. Alisema sababu za kutupiliwa mbali pingamizi katika majimbo mengine, hazikuwa na msingi hususan Majimbo ya Bumbuli, Mlalo, Peramiho, Handeni Mjini na Chalinze na hivyo kulazimika kukata rufani.

Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Salum Mwalimu, alisema sababu za wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo hayo kutupa pingamizi hizo, siyo za msingi na inaonekana wamepanga kuwabeba wagombea wa CCM wapite bila kupingwa.

Akizungumza na Nipashe, Mkurugenzi wa Uchaguzi Nec, Ramadhani Kailima, alisema hakuwapo ofisini wakati rufani hizo zinapelekwa, lakini alisema anaamini zitafanyiwa kazi.

“...lakini kama wamesema wameleta, yamepokelewa na yatafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria.

Nec ndiye muamuzi wa mwisho katika suala hilo na ikishatoa uamuzi hauwezi kupingwa popote ikiwamo mahakamani labda yawe ni jinai yanayohusisha matusi au rushwa,” alisema.

[video] Kubenea azungumzia alivyokamata shahada bandia 100 za kupigia kura

Kubenea | Mdee
MGOMBEA Ubunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, amedai kuwa zaidi ya kadi milioni mbili za kupigia kura zinatengenezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kwa ajili kuongeza kura za ziada za kukiwezesha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushinda katika uchaguzi Oktoba 25, mwaka huu.

Kubenea alidai tayari amepata kadi 100 ambazo alidai amepatiwa baadhi ya maafisa wa Tume ambao walimuahidi kumpatia kadi nyingine zaidi.
“NEC wameweka mkakati wa kukisaidia CCM kupata ushidi katika kufanikisha hilo wametengeneza kadi ambazo hazijajazwa taarifa zozote ambazo wanatarajia kuzitumia kwa kuingiza taarifa za watu ambao hawastahili ili wapige kura,”
“Tunashukuru kuna wasamaria wema ndani ya NEC ambao hawakubaliani na hujuma hizo, wameamua kutuambia na wametuahidi kutupa kadi nyingine zaidi, na huyo aliyenipa hizi 100 aliniambia hata nikitaka kadi hizo 100,000 atanipa.”
Kubenea alisema tayari amekabidhi kadi hizo kwa mwanasheria na kwamba kabla ya kuzikabidhi, aliapishwa kwanza.
“Naomba NEC iache kufanya kazi za CCM, kama itaendelea kufanya hivi itaipeleka nchi kwenye machafuko, tunaomba ifanye kazi kwa uadilifu na ninamuomba Mwenyekiti wa Tume hiyo asiipeleke nchi pabaya, hatutaki kuona watu ambao hawakuandikishwa wanaingizwa kwenye daftari,” 
Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji, Damian Lubuva, alisema hawezi kuzungumzia chochote kwa kuwa hajaziona kadi hizo.
“Kama CHADEMA wamesema kadi hizo ni za kwetu ni vema wangezileta kwetu ili tuone kama kweli ni zetu, kwa kuwa wamezungumza hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari na mimi sijaziona kadi hizo siwezi kuzungumza chochote mpaka nidhibitishe”
“Hata nikizungumza hapa itaonekana tunabishana Tume na CHADEMA, wao kama kweli wanazo watuletee tuthibitishe.”
Naye mgombea ubunge wa Kawe, Halima Mdee, aliitaka Tume hiyo kuhakikisha inahakiki taarifa za wananchi katika vituo vya kupigia kura walivyojiandikishia na si katika kata.

Alisema taarifa ambazo amepata ni kwamba baadhi ya ofisi za wakurugenzi wameambiwa na NEC kwamba wananchi wao watahakiki taarifa zao katika ofisi za kata na si katika vituo walivyojiandikishia kama inavyotakiwa kutokana na uchache wa vitabu.

Jaji Lubuva alisema changamoto za uhakiki wa wapiga kura ni suala ambalo linashughulikiwa kwa kushirikiana na wakurugenzi na kwamba watahakikisha kila aliyejiandikisha anahakikiwa.Salim Kikeke katika mazungumzo na "Baragumu" la ChannelTENNEC yarejea maagizo yake kwa vyama vya siasa kuhusu upinzani


Uchaguzi Mkuu 2015: Yaliyojiri mwishoni mwa juma la Agosti 22Mama Suluhu afanya kampeni kwa wakazi wa Moshi


Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu akihutubia maelfu ya wananchi kwenye mkutano wake wa kampeni aliofanya kwenye Viwanja vya CCM Majengo, jimbo la Moshi mjini mkoani Kilimanjaro, leo.

Wananachi wakimpongeza mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya CCM Majengo jimbo la Moshi mjini Mkoani Kilimanjaro leo.


Wananchi wakishangilia kwa furaha wakati mgombea mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani, alipohutubia mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya CCM Majengo, jimbo la Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro leo.


Mwananchi akishangilia kwa nguvu zake zote, mgombea mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassani, alipohutubia mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya CCM Majengo, jimbo la Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro leo.


Sehemu ya umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa kampeni


Wananchi wakijimwayamwaya Uwanjani wakati wa mkutano huo


Wananchi wenye mkutano huo wakinyoosha mikono kuahidi kuwachagua wagombea wa CCM, katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, tangu mgombea wa Urais, Dk John Magufuli, Wabunge na madiwani
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akishiriki kucheza ngoma, wakati kikundi cha kina mama kutoka Moshi Mjini kilipotumbuiza wakati wa mkutano huo


Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CM, Mama Samia Suluhu akiwafurahia wananchi waliokuwa wakiselebuka mbele yake kwa furaha wakati wa mkutano huo.


Vijana wakitoa burudani wakati wa mkutano huo


Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM akimshukuru Mzee, Omari Mwariko (65) , baada ya mzee huyo kumkabidhi zawadi ya picha za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Mzee Kawawa , wakati wa mkutano huo


Mgombea mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, akizitazama vema picha alizokabidhiwa na mchoraji huyo, Mzee, Mwariko


Kamanda wa Umoja wa Vijana, Kinondoni Dar es Salaam, Angela Kairuki, akishauriana jambo na Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia, wakati wa mkutano huo wa kampeni


Mgombea Ubunge jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya CCM, Devis Mosha akimwaga sera wakati wa mkutano huo


Mama Samia, akimpongeza Devis Mosha kwa hotuba nzuri


Mbunge wa kuteuliwa, mkoa wa Tanga, Ummy Mwalimu, akiwaombea kura wagombea wa CCM, Dk. John Magufuli kwa upande wa Urais na wabunge na madiwani, wakati wa mkutano huo.


Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Nkenge, mkoani Kagera, Asupta Mshama, akiwaasa wananchi kuacha kuhama vyama baada ya kukosa nafasi za uongozi wanazoomba, alipohutubia mkutano huo, akisema " Mbona mimi licha ya kuwa ni mwanamke, baada ya kukosa nafasi ya kugombea ubunge kutokana na kura kutotosha nimetulia ndani ya Chama changu? Lakini wanaume wazima tena wengine wazee, wamekosa nafasi eti wanahama!"


Mbunge wa Afrika Mashariki Angela Kizigha akizungumza, kumkaribisha mgombea Mwenza, Mama Samia kuzungumza, wakati wa mkutano huo. Katikati ni Katibu Mkuu wa UWT Amina makilagi


Mgombea mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama Samia akiwanadi wagombea wa Ubunge, Davis Mosha (Moshi Mjini), Innocent Meleck (Vunjo) na Dk. Siril Chami (Moshi Vijijini) wakati wa mkutano huo.


Wadau wakifuatilia hali ya mambo wakati wa mkutano huo.
  • Picha na maelezo tumeshirikishwa na Bashir Nkoromo