Katuni na vibonzo...


The major dress code terms one should know

Dress codes are everywhere: work, conferences, weddings, birthday parties, cocktail parties, etc. Unfortunately, not all of us are so fashion-inclined to know what every single term means in regards to proper attire. These are the major dress code terms you should know:
 • Casual: Can also be called “informal.” Essentially, this means that anything goes...almost. 89
 • Smart casual: This can also be called “casual dressy” or “dressy casual.” For men, that might mean a nice pair of trousers—or very nice jeans—with a polo or button-up shirt. For women, the same thing, but a nice knee-length skirt is acceptable as well. Usually it’s best to avoid shorts, old pairs of jeans, and t-shirts for this dress code.
 • Business casual: Generally speaking, women should wear a skirt or dress with a hem past the knee, or tailored dress pants with a button-down or blouse. Men should wear dress pants or khakis, with a collared shirt and a belt. See some examples.
 • Garden attire or beach formal: This means you should “dress to impress,” but consider the environment when you select your outfit. If it’s “beach formal,” sandals and other open-toe style shoes are acceptable. For “garden attire,” Female guests should wear wedge heels or flats so they don’t sink in the dirt or grass. Depending on the time of year, a “garden attire” gathering could mean light colored linen for men and summer dresses for women.
 • Cocktail attire: Sometimes called “cocktail chic” as well. You should be well dressed (no shorts, sandals, or t-shirts), but there is usually some wiggle room for personality. Still, both men and women should aim for darker colors. Men should wear dark suits (with or without a tie), dress pants with dress shirts, and even a nice pair of jeans with a sport coat or jacket. Women should wear knee-length skirts or dress pants with a nice sweater or blouse, or go for the classic “little black cocktail dress.”
 • Festive: This is usually the dress code for holiday parties and other themed get-togethers. It’s best to aim for cocktail level attire with a holiday twist. Be creative, but maybe leave the Santa hats and elf ears at home.
 • Business formal: You’ll usually find this dress code being used for business lunches or conferences. Guys should be in a suit and tie, and gals should be in a tailored dress or pantsuit..
 • Semi-formal: Men at least wear a darker colored business suit and tie (vest optional). Women can go with a little black cocktail dress or a long dressy skirt with a nice top. Dress shoes are expected. Basically, the main difference between “black tie optional” and “semi-formal” dress code is that this one isn’t sorta-kinda asking you to wear a tuxedo or evening gown.
 • Black tie optional: This is interchangeable with “formal attire,” but is still slightly less formal than “black tie.” For men, this means that a tuxedo isn’t required, but a dark suit and tie is considered appropriate for the occasion. For women, a dress or pantsuit in a dark, neutral tone is acceptable. Even a cocktail-length dress can be perfectly fine as long as isn’t too colorful or flashy.
 • Creative black tie: A combination of “black tie” with trendy or whimsical items. While tuxedos and dresses are still recommended, you can combine them with colored shirts, patterned bow ties, and slightly flashier cocktail dresses fit in this dress code. Depending on the occasion, it could also mean different styles of footwear. Things like cowboy boots, bolo ties, and cowboy hats might be appropriate, for example.
 • Black tie: This is considered to be the second highest level of formal attire. This is usually the kind of dress code you’ll be given for weddings or special life events (like an anniversary party). Men should wear a tuxedo with a black bow tie, cummerbund, and a nice pair of leather dress shoes. Women should wear a long evening gown or cocktail dress in a dark, neutral color like brown or black.
 • White tie: Can also be called “ultra-formal” because this is considered the highest level of dress code. Men should wear a white bow tie, black coat with tails, and a white pique vest over a white formal dress shirt. Women should wear long, formal evening gowns, and gloves when enjoying cocktails and dancing (then removed during dinner). If you get an invitation that says “white tie attire only,” you know this is a very formal occasion.
Source: Lifehacker

RealSimple: How to remove every type of stain [infographic]


Source: www.realsimple.com

Scholarship: African Centre for Migration and Society, Univ. of Witwatersrand, SA

In-Region Scholarship Programme – African Centre for Migration and Society, University of the Witwatersrand, South Africa (ACMS) • DAAD

Postgraduate training aiming at university staff development and public sector demand of academically trained personnel.
Who can apply?
Nationals from any country in Sub-Sahara Africa, except from South Africa.
What is supported?
Master of Arts in Forced Migration Studies
Duration of funding
One year
Value
 • Monthly allowance
 • Travel allowance
 • Tuition fees
 • Health insurance
Selection
Applications have to be submitted to ACMS only. Applications sent directly to DAAD will not be considered.
More detailed information
For more details and application requirements please refer to ACMS.

How to make peanut butter at homeCCM yaahidi ikishinda itahakikisha mgambo hawawakamati wafanyabiashara wadogo

Angela Kairuki mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya taifa akizungumza katika mkutano wa mgombea mwenza
Joachim Mushi, Arusha

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kikifanikiwa kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kitahakikisha mgambo wa halmashauri ya jiji hawawasumbui kwa kamatakamata za wafanyabiashara ndogondogo ambao wengi wao ni akinamama pamoja na vijana.

Kauli hiyo imetolewa leo na mgombea mwenza nafasi ya urais tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika mkutano uliofanyika uwanja wa Kilombero Jimbo la Arusha Mjini na kuhudhuriwa na umati wa wanaCCM na wananchi wengine.

Akinadi ilani ya CCM alisema chama hicho kimeandaa utaratibu mzuri wa fursa kwa akinamama na vijana wanaofanya biashara ndogondogo hivyo itakuwa ni marufuku kwa mgambo wa jiji kukamata biashara za akinamama na vijana wanaojitafutia ridhiki mjini.
"...Iwapo CCM itafanikiwa kuingia mjini naomba wale mgambo ambao uishi kwa kutegemea kukamata kamata bidhaa za akinamama watafute kazi nyingine ya kufanyanya...hatutaki mgambo wa kufanya kazi hizo ni marufuku," alisema mgombea huyo mwenza wa CCM, Samia Suluhu.

Alisema Ilani ya CCM imepanga kujenga viwanda vya kuchakata madini ili kuhakikisha vijana wanapata ajira na kuweza kukuza vipato vyao, na kufufua viwanda vilivyosimama kikiwemo cha 'General Tyre' ikiwa ni mpango wa kumaliza tatizo la ajira kwa vijana.

Aidha alisema mpango mwingine ambao upo kwenye ilani ya CCM ni kushughulikia tatizo la mikataba ya ajira ya madereva wa magari madogo na makubwa, "...Tukifanikiwa kuingia Ikulu kazi ya kwanza tutakayoipa Wizara ya ajira ni kuhakikisha inafanya kazi ya kushughulikia mikataba ya ajira kwa madereva wa magari madogo na makubwa," alisema Bi. Suluhu.

Aliongeza Serikali ya CCM itaunda ufuko wa maji kuakikisha huduma za maji zinakuwa za uhakika kwani Mkoa wa Arusha unashughuli nyingi na idadi ya watu inakuwa kila uchao. Serikali ya CCM imepanga kushughulikia suala la rushwa na vitendo vya ufisadi, uzembe ili kuhakikisha kasi ya maendeleo inaongezeka.

Awali kabla ya mkutano wa Arusha Bi. Suluhu alifanya mikutano katika majimbo ya Hai, Siha na Arumeru yaliyopo mikoa ya Kilimanjaro kabla ya kuingia Mkoani Arusha. Akiwa katika majimbo hayo mgombea aliinadi ilani ya CCM pamoja na kuwanadi wagombea ubunge na madiwani wa CCM wa maeneo hayo.

Ambapo alisema Serikali ya CCM imepanga kuboresha huduma za afya, elimu, uwezeshaji wa vijana na akinamama ikiwa ni pamoja na kutenga shilingi milioni 50 kwa kila kijiji kwa ajili ya kuwainua akinamama na vijana.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.

Baadhi ya wananchi na viongozi wa wafugaji wa kimasai wakifuatili kutano

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.


Baadhi ya wanachama wa CCM wakimkabidhi zawadi katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia SuluhuAggrey Mwanri akizungumza na wapiga kura wake

Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini.

Agrey Mwanri (kushoto) akifuraiya jambo na Bi. Ummy Mwalimu (kulia) kwenye mkutano wa B, Samia Suluhu

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.

Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.

Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.

Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.

Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu, Arusha Mjini.

Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara Moshi Mjini.
 • Tumeshirikishwa taarifa hii na TheHabari.com

Dk Magufuli ashambulia Momba, Tunduma na Ileje


Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Tunduma waliofurika kwa wingi katika uwanja wa shule ya msingi Tunduma,mkoa wa Mbeya mapema leo mchana, kwenye mkutano wa kampeni wa kuwaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika kipindi cha awamu ya tano, ambapo uchaguzi unatarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Siku ya Shafi Adam Shafi - Mjadala 5/9/2015 @SomaBookCafé


Umewahi kusoma kazi yoyote kati ya hizi?
 • "Kasri ya Mwinyi Fuad"
 • "Kuli"
 • "Vuta Nkuvute"
 • "Haini"
 • "Mbali na Nyumbani"
Baada ya kuzisoma, umewahi kuwa na hamu ya kukutana, kubadilishana mawazo na kujadiliana na mwandishi wake?

Taasisi ya “Kitabu kwa Maendeleo Tanzania (KMT)” kwa kushirikiana na “Soma Book Café” inawaletea "Siku ya Shafi Adam Shafi". Washiriki wa siku hii watapata nafasi ya kuzijadili kazi za mwandishi huyu nguli wa fasihi na kubadilishana naye mawazo na uzoefu.

Mjadala utafanyika siku ya tarehe 5/9/2015 kwenye Mkahawa wa Soma (Soma Book Café)
Kwa maelezo zaidi juu ya mjadala huu piga: 0653619906 (Ado) au 0712568699 (Jasper)

KITABU NI SILAHA
KITABU KINA RAHA!
 • Imewasilishwa Wanazuoni na Ado Shaibu

Kimbunga cha kweli Siha chavamia mkutano wa Mama Samia


Lighter moments: WhatsApp vs Lion

Wife: baby can you kill a lion for me ?

Hubby : No baby, try something else.

Wife: May I go through your WhatsApp?

Hubby : Where is the lion you were talking about?

Tarifa: Marufuku wawania Urais Tanzania 2015 kurusha helikopta bila kibaliMAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA

TANGAZO KWA UMMA

MATUMIZI YA HELIKOPTA MAENEO YA HADHARA NA MIKUSANYIKO YA WATU

 1. UTANGULIZI
  1. Tangazo hili linatolewa kwa lengo la kutoa mwongozo kwa watoa huduma za helikopta, marubani wake na umma kwa ujumla kuhusiana na hatua za kiusalama zinazopaswa kuzingatiwa inapolazimika kutoa huduma ya usafiri wa helikopta hapa nchini, hususani, maeneo ya mbali (vijijini) ambapo huduma za uongozaji ndege hazipo au sio maeneo maalum yaliyotengwa kwa ajili ya helikopta kutua (mahsusi kwa helikopta au viwanja vya ndege kwa ujumla). Tangazo hili limetolewa baada ya Mamlaka kugundua kwamba kumekuwa na matumizi mabaya ya huduma hizi kinyume na kanuni za usafiri wa anga nchini na weledi unaozingatia taratibu za kitaaalamu na miongozo katika usafiri wa anga.
  2. Mamlaka inatambua kwamba matumizi ya helikopta wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 yanatarajiwa kuongezeka na kuna uwezekano wa kuleta athari za kiusalama kwa maisha ya watu na mali pamoja na watumiaji wa vyombo hivi. Pia vitendo vya kuning’iniza vitu kama mabango ya matangazo mbalimbali kwa kutumia ndege (helikopta ikiwemo) yanaweza kuleta hatari endapo sheria na taratibu zinazohusiana na matumizi hayo hazitazingatiwa.
  3. Tangazo hili linatolewa kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mkuu chini ya Sheria Namba 80 ya Usafiri wa Anga na kanuni zake zinazohusiana na masuala ya usafiri wa anga nchini zilizowekwa kwa lengo, hususan, kuhakikisha usalama katika matumizi ya vyombo vya usafiri wa anga sambamba na kulinda usalama wa umma na mali wakati wa matumizi ya vyombo husika.
  4. Watoa huduma za usafiri wa helikopta au ndege na marubani wake wanaokodishwa kutoa huduma wakati wa kampeni, na mtu yeyote anayetarajiwa kutumia huduma hiyo wanakumbushwa kuhakikisha wanazingatia kanuni za usafiri wa anga na ikibidi kuomba kibali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania. Kanuni zinapatikana kupitia tovuti yetu kwa anuani ya: www.tcaa.go.tz; na endapo utahitaji maelezo ya ziada au miongozo zaidi usisite kuwasiliana na Mamlaka.
 2. CHETI CHA NDEGE KWA USALAMA WA KURUKA – AIRWORTHINESS CERTIFICATE
  1. Helikopta yeyote itakayotoa huduma katika kampeni za kisiasa lazima iwe ina cheti halisi cha usalama wa kuruka kilichotolewa na mamlaka husika ya helikopta ilikosajiliwa. Kwa hapa nchini cheti hicho ni lazima kiwe kimetolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga. Na cheti hicho ni lazima kiwe kimetolewa kwa ajili ya helikopta yenye usajili na mahsusi kwa kazi ya kubeba abiria ambayo inaweza kutumika kwa shughuli nyingine zozote. Kwa tangazo hili helikopta nyingine yeyote ile isiyokuwa na sifa hiyo haiwezi kutumika kufanya biashara ya usafiri wa abiria katika kampeni.
  2. Endapo helikopta itakuwa ina usajili wa nje ya Tanzania, mtu anayetarajia kuitumia hapa nchini ni lazima apate kibali cha kuiingiza nchini na kuitumia kwa usajili wa nchi iliyotoka kama ilivyoainishwa katika Waraka wa Mamlaka unaoainisha taarifa za usafiri wa anga – Aeronautical Information Circular (AIC 08/09). Hakikisha unapoomba kibali uwe umekidhi vigezo vya waraka huu ikiwa ni pamoja na kuwasilisha nakala za nyaraka zinazopaswa kuwasilishwa zikiwemo cheti cha usajili wa ndege, cheti cha ndege kwa usalama wa kuruka, cheti cha leseni za radio za ndege, cheti cha bima, makubaliano/mkataba wa kukodisha ndege hiyo, utaratibu wa kufanya matengenezo ya ndege hiyo, leseni za marubani, na ushahidi wa karibuni wa matengenezo ya ndege hiyo.
 3. TARATIBU ZA USALAMA WA UENDESHAJI
  1. Mahitaji ya jumla ya kiuendeshaji

   Matakwa ya marubani na uendeshaji unatakiwa kufuata maelekezo husika yaliyomo kwenye Kanuni inayohusiana na uendeshaji, yaani, The Civil Aviation (Operation of Aircraft) Regulations. Rubani Mkuu anawajibika kuhakikisha kwamba vituo vya Mamlaka vya kuongoza ndege vinavyohusika katika eneo atakalokuwepo au kwa utaratibu wa uongozaji ndege, wanakuwa na taarifa za mpango wake mzima wa safari husika kwa siku au wakati husika.

   Njia itakayotumiwa na rubani izingatie matakwa ya kuepuka kuruka chini ya kiwango cha umbali unaotakiwa hasa katika maeneo yenye watu wengi yakiwemo maeneo yaliyopangwa kufanyika kwa mikutano husika.

   Tahadhari ni lazima zichukuliwe wakati wa kuelekea kutua, kutua kwenyewe na hata wakati wa kuondoka, hasa ikizingatiwa kuwa kuna uwezekano wa wananchi kuikimbilia helikopta au eneo la utuaji. Katika hali yeyote ile rubani hapaswi kutumia chombo chake kukusanya wananchi kwa ajili ya mkutano au kuitumia kwa utaratibu wowote mwingine kinyume na matakwa ya kiurukaji kwa ndege husika.
  2. Usalama wa eneo la kutua na kuruka

   Maeneo yote yatakayotumika kwa ajili ya kutua ama kuruka ni lazima yafahamike mapema. Maeneo ya kuruka ama kutua ni lazima yawe mbali na eneo mkutano utakapofanyika ili kuweza kutoa eneo salama kwa ajili ya kuruka ama kutua kutoka katika mikusanyiko ya watu.

   Maeneo ambayo yatatambuliwa kama ni ya kuruka ama kutua hasa yale ambayo hayajatambulika kisheria kwa kufanyia shughuli hiyo ni lazima yawekewe alama maalum na uzio ili kuzuia watu wasiohusika kusogelea eneo hilo.

   Eneo husika ni lazima lilindwe; rubani mkuu ahakikishe helikopta itakayokuwa imetua eneo hilo inalindwa dhidi ya uvamizi kutoka kwa watu wasiohusika. Hatua maalum za kiulinzi ni vyema kuchukuliwa endapo kutakuwa na ulazima wa chombo hicho kulala katika eneo husika usiku mzima. Kila wakati rubani anapotaka kuruka ni vyema ahakikishe amekagua chombo chake kwa mujibu wa taratibu zinazohusika kwa umakini kabla ya kuanza safari.
  3. Usiamizi wa Chombo kikiwa ardhini na usalama kwa umma

   Mtu mwenye wajibu wa usimamizi wa chombo kikiwa ardhini lazima awe ni mwenye mafunzo ya kutosha na awe anajua madhara yanayoweza kusababishwa na mapanga ya helikopta yanapozunguka. Kwa marejeo zaidi kuhusiaha na hilo tafadhali zingatia yaliyomo kwenye Waraka wa Mamlaka AIC33/2000 unaoelezea masuala ya madhara yanayoweza kusababishwa na mapanga ya helikopta yanayozunguka.

   Ni wajibu wa Rubani mkuu na mhusika aliyekodisha helikopta kuhakikisha wananchi wanakuwa salama na mbali na helikopta. Matumizi ya kizembe na yasiyo ya kiweledi ya helikopta yatakayohatarisha usalama wa wananchi yatachukuliwa kama ukiukwaji wa kanuni za usafiri wa anga na Mamlaka itawachukulia hatua kama ilivyoanishwa kwenye kanuni hizo.
  4. Kuchukua na kuangusha vitu ardhini na kupeperusha mabango angani

   Huduma hizi zinaweza kufanywa na helikopta na hata ndege zingine za kawaida. Kabla ya kufanya shughuli za namna hiyo, mmiliki wa chombo ni lazima ahakikishe anakidhi vigezo vya Kanuni za Usafiri wa Anga kwa huduma hizi, yaani, The Civil Aviation (Aerial Work) Regulations na pia awe amepatiwa kibali kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga kwa kazi hiyo. Mmiliki wa ndege yeyote anayefanya shughuli za namna hii bila ya kuzingatia vigezo vya Kanuni hizi atachukuliwa hatua.
  5. Kutoa taarifa za matukio

   Rubani Mkuu ni lazima aandike taarifa ya matukio na kuiwasilisha Mamlaka ya Usafiri wa Anga kama ilivyoanishwa kwa mujibu wa kanuni za usafiri wa anga hususan, kanuni za 52, 74,75 na 76 zilizomo kwenye Kanuni ya The Civil Aviation (Operation of Aircraft) Regulations. Wananchi nao wanatakiwa kutoa taarifa ya tukio lolote waliloliona hatarishi kwa mujibu wa kanuni namba 262 ya Kanuni iliyotajwa.

   Mamlaka itafuatilia na kuchunguza taarifa inazozipokea na kuchukuwa hatua stahiki ili kuhakikisha kuwepo kwa usalama wa kiuendeshaji, watu na mali.
 4. HITIMISHO
  Ili kulinda usalama wa wananchi, wamiliki na marubani wote wanapaswa kuhakikisha wanazingatia Sheria ya Usafiri wa Anga pamoja na Kanuni zake. Rubani anayeendesha chombo ni lazima ahakikishe anatumia weledi wa hali ya juu katika matendo yake.

  Mamlaka inawahakikishia wananchi/umma kwa ujumla kwamba haitosita kuchukuwa hatua stahiki kama zilivyoanishwa kisheria na kanuni za usafiri wa anga iwapo mapungufu ya usalama yatajitokeza.
Imetolewa na
Charles M. Chacha
Kaimu MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA

[update] UKAWA yazungumzia barua inayowazuia kufanya mkutano Jangwani

[update/taarifa mpya Agosti 27, 2015]

Tumaini Makene akizungumza na wanahabari Agosti 27, 2015
Tumaini Makene akizungumza na wanahabari Agosti 27, 2015
Malalamiko ya vyama vinavyounda UKAWA ya kakatazwa kutumia uwanja wa Jangwani kuzindua kampeni yameanza kufanyiwa kazi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na taarifa zilizotolewa na Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya CHADEMA Bw. Tumaini Makene imesema kuwa shughuli hiyo itafanyika kwenye uwanja huo kama ilivyokuwa imepangwa.

Bw. Makene ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la vijana la vyama vinavyounda UKAWA na waandishi wa habari ambao pia viongozi hao wametumia nafasi hiyo kuiomba tume ya uchaguzi kuwakemea viongozi na watendaji wa serikali kufanya kazi za siasa kwa lengo la kukibeba chama tawala.

Viongozi hao wa vijana wamesema hatua ya viongozi na watendaji wa serikali ya kujihusisha moja kwa moja na kampeni za CCM huku wengine wakitumia rasilimali za umma na vyombo vya dola kukandamiza vyama vya upinzani inathibitisha ukweli wa malalamiko yao.

Naye Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ametaka Watanzania kujitokeza kwa mamilioni katika uwanja wa Jangwani kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni zao.
MUENDELEZO! Taarifa tunazozipata muda huu ni kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeondoa zuio la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala...
Posted by Julius S. Mtatiro on Wednesday, August 26, 2015


MKURUGENZI wa Manispaa ya Ilala, Claud Mpelembwa amezuia mkutano wa uzinduzi wa Kampeni za Urais, mgombea wa Urais wa Tanzania anayeiwakilisha UKAWA kupitia CHADEMA, Edward Lowassa kufanyika katika viwanja vya Jangwani kwa madai ya uwanja huo kuwa na matumizi mengine.

Pamoja na kuwepo kwa barua hiyo kutoka kwa mkurugenzi wa Ilala, Umoja wa wadai Katiba ya Wananchi (UKAWA) umesisitiza kuwa ratiba ya mkutano wao utakuwa kama walivyopanga, eneo, muda na tarehe ile ile.

Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, James Mbatia aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali imekataa ombi lao la kufanyia mkutano kwenye viwanja vya Jangwani bila ya kuwa na sababu za msingi.

Mbatia amesema waliandika barua ya 22 Agosti, 2015 kutumia viwanja vya Jangwani lakini mkurugenzi amewazuia kutumia viwanja hivyo kwa madai kuwa tayari umeshalipiwa na mtu mwingine, ambaye hakutaka kumtaka kwa sababu zao binafsi.

“Tumefanya juhudi zote za kiungwana ili tuweze kupewa viwanja hivyo ikiwemo kuomba kumjua aliyelipia ili tufanye naye mazungumzo lakini serikali ilikataa kutupa jina la mtu huyo. Tutafanya mkutano Jangwani,” amesema Mbatia.

Mwenyekiti huyo amesema hii ni mizengwe inayoanzishwa na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kujaribu kuzuia mafuriko ya mgombea wa UKAWA, lakini hilo haliwezekani kwa kuwa kwenye nguvu ya umma hakuna kinachoweza kuzuilika.

“Hivi ni vitendo vya kishetani vinavyofanywa na serikali na vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani kwa wananchi. Tunahitaji utulivu ili tujenge Tanzania yetu, hatupo tayari kuona damu inamwagika kama ilivyokuwa kwa nchi nyingine,” amesema Mbatia.

Pia Mbatia amemtaka Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Damian Lubuva afanye kazi kwa kusimamia misingi ya haki bila ya kupendelea chama chochote cha siasa.

Mbatia amesema katika uzinduzi wa kampeni za CCM wiki iliyopita, kiongozi mwandamizi wa serikali alitoa kauli za matusi na kejeli, mkutano huo ulivunja kanuni za uchaguzi kwa kupitiliza muda uliopangwa, lakini Lubuva hakusema chochote mpaka sasa.

“CCM chini ya Rais Kikwete (Jakaya) ndiyo walikuwa wa kwanza kuvunja sheria kwa kupitiliza muda wa kampeni, lakini pia walitoa maneno ya kejeli na matusi, lakini cha ajabu si serikali wala Tume iliyokemea matukio hayo,” amesema Mbatia.

Kwa upande mwingine Mbatia amelitaka jeshi la polisi kuacha kutumiwa na CCM, kwa kuwazuia baadhi ya wagombea wa chama fulani huku chama kingine kikiachiwa kufanya kile ambacho wengine wamekatazwa.

Mbatia amesema kitendo cha Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova kupiga marufuku ziara za Lowassa kutembelea kwenye masoko, hospitali na sehemu nyingine, huku wagombea wa CCM wakifanya ziara hizo kwa kusindikizwa na jeshi hilo.

“Leo Lowassa (Edward) alikuwa atembee kwenye hospitali jijini Dar es Salaam, lakini Kova amezuia, huku Mgombea Mwenza wa CCM, Samia Suluhu akisindikizwa na polisi kutembelea hospitali za Rombo, Kilimanjaro. Hii siyo haki,” amesema Mbatia.

Mbatia amewatoa hofu watanzania, kuwa hawatafanya kampeni za uvunjifu wa amani bali wao watahubiri amani, na siyo kama CCM wanavyohubiri vita na kuwatisha wananchi juu ya uvunjifu wa amani.
 • Taarifa kwa maandishi imenukuliwa kutoka MwanaHALISI Online
 • Nakala ya barua imepatikana kutoka WhatsApp


Taarifa kuhusu kampeni za kisiasa katika maeneo ya huduma za afya

Tumepokea taarifa kuwa wapo baadhi ya wagombea uongozi kuamua kutembelea Hospitali kama sehemu ya kuendesha kampeni za uchanguzi. Kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya huduma za afya, Hospitali ni sehemu inayopokea na kulaza wagonjwa wenye matatizo mbalimbali ya muda mrefu na muda mfupi. Pia yapo magonjwa yanayohitaji uangalizi wa karibu, na wakati mwingine huhitaji kutumiwa mitambo maalumu ya kuimarisha afya za wagonjwa.

Aidha, ikumbukwe kuwa katika mazingira ya sasa Duniani kote, Tanzania ikiwa ni mojawapo, yapo magonjwa mapya na yanayojitokeza upya (emerging and re-emerging diseases) ambayo mengine ni ya kuambukiza na ya milipuko.

Kutokana na hali hii wizara inapenda kutoa maelekezo kama ifuatavyo:-

Hospitali na vituo vingine vya kutolea huduma za Afya visitumike kwa madhumuni ya kuendeshea shughuli za kisiasa. Hii itasaidia kuzuia kupata magonjwa ya kuambukiza au kuingia hospitali na magonjwa ya kuambukiza. Hivyo ni vizuri kuchukua tahadhali kubwa hususan kipindi hiki ambacho kuna ugonjwa wa Kipindupindu.

Wizara inatambua umuhimu wa wagonjwa kutembelewa na ndugu na jamaa zao kwa lengo la kuwajulia hali. Katika mazingira haya utaratibu utaendelea kuwepo kama unavyofanyika nyakati nyingine kwa kuwa mgonjwa, anayo haki ya msingi ya kufarijiwa anapokuwa hospitalini na hata nyumbani, isipokuwa tu katika magonjwa ya kuambukiza.

Pale itakapoonekana kuwa baadhi ya wagombea wa nafasi za uongozi wana haja ya kutembelea hospitali kwa madhumuni tofauti na yale ya kuwajulia wagonjwa hali zao, itabidi waombe kibali maalumu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii . Wizara itakubali au kukataa maombi hayo kutokana na uzito wa ombi litakalowasilishwa pamoja na hali ya magonjwa yaliyopo katika eneo na hospitali au kituo husika cha kutoa huduma za Afya.

Tunapenda kusisitiza kwamba taarifa hii ina lengo la kuwazesha wagonjwa waliopo hospitalini kuendelea kupata huduma katika mazingira ya amani na utulivu. Hospitali na vituo vingine vya kutolea huduma za Afya nchini visitumike kama sehemu ya kuendeshea kampeni za siasa kwa vile ni maeneo maalumu ya kutolea huduma za Afya kwa mujibu wa Sera ya Afya na miongozo ya kutoa huduma za Afya.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
WIZARA YA AFYA

Marekani yakabidhi ruzuku ya mil. 173/= kwa Watanzania

Balozi wa Marekani nchini Mark Childress amekabidhi ruzuku yenye thamani ya shilingi milioni 173 kwa vikundi na mashirika ya kijamiii 14 yanayofanya kazi ya kuboresha maisha ya Watanzania kupitia shughuli za maendeleo.

Ruzuku hiyo inatarajiwa kuwanufaisha wananchi wa kipato cha chini zaidi ya 5,000 katika mikoa 12 na kuboresha huduma za kijamii ikiwemo afya, elimu, mazingira na maendeleo ya uchumi.

Kwa mujibu wa Ubalozi wa Marekani, lengo la ruzuku hiyo ni kusaidia vikundi na mashirika ya Kijamii, ambayo hutoa misaada ya moja kwa moja inayolenga kuboresha maisha ya jamii husika kupitia mfuko wa Balozi wa Kusaidia Miradi ya kujitegemea ya Jamii.

Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress, amesema mradi huo wa kuwezesha vikundi vya kijamii, na utasaidia kupunguza tatizo la umaskini kutokana na ushirikiwshwaji wa wananchi katika shughuli za maendeleo ya uchumi.

Baaadhi ya wananachi waliopata ruzuku hiyo,wamewataka watanzania kutumia nafasi walizonazo kwa kuwasadia watu wenye shida mbalimbali ili waweze kuondokana na umaskini na kuwa na Taifa lenye watu walio na ushikamano katika maswala ya kiuchumi..

Mfuko wa Balozi wa Marekani kusaidia miradi ya kujitegemea ya jamii ulianzishwa wakati wa muhula wa kwanza wa Utawala wa Mwalimu Julius Nyerere.Kwa miaka 50 sasa mfuko huo umeweza kuboresha maisha ya Watanzania.

Askari mbaroni kwa kuongoza wenziye wakalipe kisasi kwa raia

Polisi mkoani Manyara inamshikilia askari mmoja wa jeshi la Magereza wilayani Babati mkoani Manyara kwa tuhuma za kuwashawishi wenzake 10 kuwavamia wakazi wa eneo la Kijiweni Mrara wilayani humo na kuwapiga pamoja na kuharibu mali zao.

Askari anayeshikiliwa na polisi ni Konstebo Jackson ambaye inasemekana aliwashawishi wenzake baada ya yeye kupigwa na wakazi hao wakati akiamua ugomvi wa vijana katika eneo hilo

Mganga Mkuu wa hosptali ya mji wa Babati Dokta Antipas Swai amekiri kupokea majeruhi katika hosptali hiyo ambao wanadai kupigiwa na askari magereza na kusababishiwa majeraha mbalimbali katika miili yao.

Baadhi ya majeruhi waliolazwa wanasema walikuwa wakipigiwa na vyuma hivyo kupelekea kuumizwa sehemu mbalimbali na kulazimika kupelekwa hospitali kwaajili ya matibabu. Mbali na hayo, baadhi ya majeruhi katika tukio hilo wamealalamika pia kwa upotevu wa baadhi ya mali zao zikiwemo fedha.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi Lingnus Tibisubwamu anasema pamoja na kumshikilia askri aliyeongoza wenzake kuwapiga wanachi, upelelezi zaidi unafanyika kuhusu chanzo cha tukio hilo. Inasemekana hii ni mara ya pili ndani ya kipindi cha miaka mitatu askari wa gereza la Babati kuhitilafiana na wananchi wa eneo la Kijiweni Mrara.

[audio] Ngoma mpya ya Nuru The Light: ‘L’


Ukimya wa miaka miwili wa Nuru The Light ulikuwa na makusudi mahsusi ya kutaka kubadilisha upepo wa muziki wa Tanzania. Ameutumia kutengeneza muziki tofauti, mzuri na utakaokuwa na ladha inayoishi kwa miaka mingi zaidi kwenye masikio ya wapenzi wa muziki.

Na sasa anarejea kwa kishindo kwa kuachia wimbo anaouelezea kama wenye utofauti mkubwa na muziki uliopo kwenye mzunguko wa nyimbo zinazochezwa kwenye redio.

Nuru anasema hakutaka ujio wake kutoka kwenye ukimya wa miaka miwili uwe wa kawaida na ndio maana ametumia muda mrefu kutengeneza kazi yake mpya aliyoipa jina ‘L’.

“Hii kazi nimeanza kuifanya tangu January,” anasema Nuru. “Ni nyimbo ambayo nimeirekodi sana. Nimefanya nyimbo nyingi lakini zaidi ni nyimbo mbili ambazo nilitaka uwe ujio wangu mpya.”

Anasema wimbo ‘L’ ndio ulioonekana kupenya zaidi na kuwa na sifa zote za kutimiza azma yake ya kurejea kwa mshindo mkuu. “Huu ni ujio mpya, kitu tofauti ambacho mimi kama Nuru nimewahi kufanya,” amesisitiza muimbaji huyo.

“Nadhani nilitaka kufanya kitu ambacho watu watasema ‘ohh kaja kitofauti tena kama vile nilivyokuja na Muhogo Andazi.”

Muimbaji huyo anaeleza kuwa L ni herufi iliyo na mambo mengi chanya na ya furaha kwenye maisha yake na ameitumia kama jina la wimbo kuyawakilisha.

“L inaweza kuwa Love, Life, Light, ni vitu chanya,” anaeleza.

Nuru amedai L ni wimbo uliotayarishwa nchini Sweden lakini aliamua kuja kuifanyia video nyumbani chini ya muongozaji mkongwe wa video, Adam.

Hii inakuwa ni video yake takriban ya tano kuwahi kufanya na muongozaji huyo.

“Nakumbuka kabisa video yangu ya kwanza Walimwengu ilikuwa ni mimi na Adam, tukasafiri tukaenda Zanzibar na nadhani tulielewa kutoka kwenye siku hiyo na ikawa imekuwa rahisi kwangu kufanya kazi naye.”

Nuru amedai kinachompa faraja zaidi ni kuwa pamoja na kutokuwa na kazi mpya kwa kipindi cha miaka miwili, bado mashabiki wamekuwa wakiwasiliana naye kumuulizia kuhusu kazi mpya.

“Nina furaha kwamba mashabiki wamekuwa wakisubiri na sasa muda umefika wa wao kuweza kusikiliza wimbo mpya.”

Usikilize wimbo huo wa mapenzi na wenye mahadhi ya ‘reggae tamu’ ambao bila shaka unajibu la swali la kwanini anasema huu ni ujio mpya.

MISATAN to sharpen bloggers, editors’ right to information, election reportingBy Gasirigwa GS

The Media Institute of Southern Africa (MISA) Tanzania Chapter in association with the Centre for ICT Policy promotion in Africa (CIPESA) will tomorrow train a selected number of bloggers and editors on Right to Information with special focus on this year’s general election.

Editors and bloggers will be taught on the safest ways to access information and report responsibly during campaigns and the entire election period. Attention will be directed to the Cyber crime and the Statistics Acts which are already in effect and have dire consequences on media practice.

Participants will also be introduced to ‘The Broadcasting Services (Content) (The Political Party Elections Broadcasts) Code 2015’ which was gazetted on June 26, 2015. Bloggers, SMS pollsters, and broadcasters in general will seriously be affected by this Code. The Code was developed by the Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA).

About 20 selected Dar es Salaam-based editors and bloggers have confirmed to take part in this one-day workshop, scheduled for tomorrow Thursday the 27th of August at Kebbys Hotel in Dar es Salaam.

Similar training was held two weeks ago in Mwanza and drew participants from Geita, Mara and Mwanza itself. The Mwanza training specifically targeted journalists who basically cover rural areas.

MISATAN and CIPESA believe that the media needs to responsibly serve the public in a way that will provoke positive engagement and subsequent improvement in the political administration of the country.

Zanzibar Diaspora yapongezwa kwa kusaidia elimu

Afisa wa Elimu Zanzibar Bw Suleiman Yahya Ame (kulia) akionesha makala ya kitabu
Na Abou Shatry Washington DC

Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani (ZADIA), imepongezwa kwa kusaidia gurudumu la maendeleo ya elimu visiwani Zanzibar.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu Zanzibar Bw. Suleiman Yahya Ame wakati wa kupokea mchango wa vitabu vya Ufundi na Mafunzo ya Amali uliotolewa na ZADIA kwa ajili ya shule za ufundi visiwani humo.

Akizungumza kama mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika mjini Zanzibar, Bw. Ame pia aliwashukuru Wanadiaspora hao kwa kuendeleza juhudi za kujenga jamii iliyoelimika Zanzibar.

Aliendelea kusema "Tukiwa na mahitaji makubwa ya vitabu katika shule zetu, vitabu hivi vimewasili katika wakati mwafaka, na tunashukuru kwa msaada huu", na kungoeza kuwa juhudi kama hizi zitasaidia kuigeuza Zanzibar kuwa jamii inayojitosheleza kiajira.

Alizitolea wito shule zilizofaidika na vitabu hivyo kuvitumia vizuri kwa lengo la kuisaidia Zanzibar kufikia malengo yake ya kielimu.

Bwana Ame alimalizia kwa kuitolea wito ZADIA kupanua zaidi mfumo wa misaada yake ya kielimu na kujumuisha ujenzi wa madarsa na vitabu vya taaluma nyengine ambazo Zanzibar ina upungufu mkubwa, kama vile taaluma ya Fedha na nyenginezo.

Naye Mwenyekiti wa ZADIA Bwana Omar Haji Ali, alisisitiza azma ya jumuiya yake ya kuendeleza juhudi za kusaidia maendeleo Zanzibar.

Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na mwakilishi wa ZADIA Zanzibar Bwana Mussa Shehe kwenye hafla ya makabidhiano ya vitabu hivyo, Bw. Ali alisema "ZADIA, tangu kuanzishwa kwake imekuwa msitari wa mbele katika harakati za kusaidia maendeleo Visiwani Zanzibar katika nyanja tofauti."

Aliendelea kutamba kwa kusema kuwa, "Kwa vile ZADIA inaelewa kuwa daima maadui wakubwa wa maendeleo ya jamii wamekuwa wakivinjari kuzorotesha maendeleo hayo, basi jeshi letu siku zote liko imara kupambana na maadui hao ambao ni maradhi, ujinga na umaskini, na kuhakikisha kuwa milele hawatothubutu kujaribu kuyachokoza maendelea ya Wazanzibari.

Aidha, Bwana Ali alisisitiza kuwa msaada huo wa vitabu siyo mwisho wa juhudi za ZADIA katika kusaidia sekta ya Elimu Zanzibar, bali ni mwendeleo wa mapambano dhidi ya adui ujinga.

Alielezea matumaini yake kuwa msaada huu utakuwa ni changamoto kwa jumuiya nyengine za Wazanzibari ulimwenguni kushiriki katika kusaidia maendeleo Zanzibar.

Bwana Omar aliwashukuru WanaZaida wote walioshiriki katika kufanikisha msaada wa vitabu hivyo, pamoja na shirikika la Goodheart-Willcox la nchini Marekani kwa ukarimu wao.

Hafla hiyo ya makabidhiano ya vitabu, pia ilihudhuriwa na maofisa wa ngazi za juu kutoka Wizara ya Elimu Zanzibar, Maofisa wa Idara ya Diaspora katika Ofisi ya Rais wa Zanzibar, wawakilishi wa Vyuo vilivyokusudiwa kufaidika na msaada huo pamoja na wawalikishi wa vyombo mbalimbali vya habari vilioko Zanzibar.

Madaktari kutoka India kupambana na ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa kwa WatotoKutokea kwa ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa (CHD) kunatazamwa kwa usawa kwa duniani kote, pamoja na kutofautiana kati ya mikoa na nchi kutokana na maumbile, mazingira na mabadiliko ya kiepijenetiki. Takriban watoto 8 kati 1000 wanaozaliwa wakiwa hai wanazaliwa na CHD duniani kote. Takwimu hii kwa ujumla inaaminika zaidi. Hata hivyo, kutokana na ukosefu wa takwimu sahihi katika bara la Afrika, watoto walioathirika na CHD barani Afrika inaweza kuwa wengi sana.

Watoto wenye ugonjwa wa moyo wanaweza kuonesha dalili wakati wa kuzaliwa. baadhi ya dalili hizi ni pamoja mtoto kubadilika rangi na kuwa wa bluu, mtoto kupumua kwa kasi, jasho nyingi, kuvurugika kwa mapigo ya moyo, kushindwa kula ambapo husababisha kushindwa kuongezeka uzito na mtoto kupata maambukizi katika mfumo wa upumuaji mara kwa mara. Wakati mwingine, hii inaweza kugundulika kwa kuhakikisha unamuona daktari wa watoto wachanga mara kwa mara. Tatizo lolote katika moyo linaweza kubadilisha namna moyo unavyosikika. Sauti hizi zisizo za kawaida zinaweza kugunduliwa na daktari kwa kusikiliza kutumia kifaa maalumu cha ‘stethoskopu’. Kuna baadhi ya matukio ambapo vichanga na watoto wadogo wanakuwa wakizimia, kuonyesha kwamba wako katika hali ya kushindwa kwa mizunguko upumuaji.

Watoto, hasa walio chini ya umri wa siku 28 na vichanga ambao wako chini ya umri wa mwaka mmoja hawachukuliwi kama vijana, hivyo kuwafanyia upasuaji moyo kwao ni changamoto. Inapaswa kuzingatiwa kuwa moyo wa mtoto anapozaliwa unakuwa na ukubwa wa ngumi yake. Kutokana na muundo wake unaochanganya, watoto wachanga hukabiliwa na kiwango kidogo cha ufanyaji kazi wa moyo na hivyo kupata uharibifu kwa viungo vingine muhimu ikiwa ni pamoja na mapafu, figo na ini. Hivyo, kwa asili upasuaji wa moyo ni mgumu zaidi.

Kutokana na ugumu wa upasuaji kwa mtoto, Dkt. Neville A.G Solomon Mshauri, Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Moyo kwa Watoto wa Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai anaona kwamba mbinu zinazojumuisha mambo mbalimbali zitumike ili kuwa na mafanikio. Ili kufanya kwa usahihi upasuaji na marekebisho bila kuharibu miundo yoyote muhimu, mpasuaji ni muhimu kuusimamisha moyo wa mtoto, kukata usambazaji wa damu kwenye moyo na kukausha damu yote ili aweze kuona vema miundo ya ndani. Pamoja na utaratibu huu mgumu, wakati wa upasuaji ni wa muhimu na makini sana. Ugumu huongezeka kadiri upasuaji unapochukua muda mrefu. Ni muhimu kwa timu nzima kufanya kazi katika hali ya maelewano kwa lengo la pamoja la kuokoa maisha.

Wakati mtoto anapohisiwa kuwa na ugonjwa wa moyo hatua ya awali ya kuchunguza hili ni kwa kufanya vipimo kama vile kuchukua X-ray ya kifua na ECG ambapo husaidia kuthibitisha uchunguzi. Mionzi ya sauti ya moyo (ECG) mara nyingi husaidia katika uchunguzi. Hii itatoa taarifa za kutosha kwa ajili ya mtaalamu na / au mpasuaji wa moyo na kuamua namna matibabu yanavyopaswa kufanyika. Kama vipimo vya ziada au zaidi vinahitajika, takwimu hizi zinaweza kupatikana kwa njia za uchunguzi kama wa kutumia katheta ya moyo na ‘anjiografia’, CT na MRI ‘anjiogramu’ ya moyo.

Uboreshaji wa hatua hizi za uchunguzi umeongezeka ubora wa upasuaji kwa watoto. Daktari mpasuaji au mtaalamu wa moyo sasa utakuwa na mwongozo wa pande tatu za ugonjwa wa moyo kabla ya utekelezaji wa wake. Hii inatoa mpango bora wa upasuaji usiokabiliwa na matatizo wakati wa upasuaji na kwa hiyo matokeo ya upasuaji kuwa bora zaidi na yenye mafanikio zaidi.

Kuna tiba kadhaa ambazo zinapatikana kwa sasa. Baadhi ya hizi ni pamoja na mbinu ya kutumia matundu madogo na upasuaji wa moyo kwa kuufungua na kuufunga. Mbinu ya matundu huweza kukamilika kwa siku moja tu na hii inaweza kufanywa na wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu wa magonjwa ya moyo kwa watoto. Utaratibu huu unahitaji kupatikana kwa vifaa vinavyowezesha kuipata mashimo midogo ya moyo ambayo imefungwa na valvu na kujificha ndani sana. Kwa mbinu hii mtoto hapati maumivu ya kukatwa. Utaratibu huu hauhitaji mashine ya upumuaji kuwekwa au mtoto kuwekwa katika chumba maalumu cha wagonjwa mahututi mtoto anaweza kupona kwa haraka zaidi na kurudi shule na hata kushiriki katika michezo.

Namna nyingine za matibabu ambazo zinaweza kutumika kwa watoto wenye hali mbaya zaidi ya moyo ni ile ya kuufungua na kuufunga moyo yaani (upasuaji). Upasuaji huu unaweza kufanywa kwa watoto wachanga wenye umri wa masaa manne hadi matano au wenye gramu 800. Kutokana na utata wa hali hii, umuhimu wa kutumia timu shirikishi unasisitizwa zaidi. Hata mtaalamu wa upasuaji awe mjuzi sana, atahitaji msaada kutoka kwa timu.

Watu kadhaa wanahusika katika mchakato huu. Wauguzi wanashiriki katika kuwahudumia watoto ambao wamefanyiwa upasuaji wa moyo. Madaktari wa watoto wanashiriki kuwahuduma baada ya upasuaji kama vile kudhibiti maumivu, kudhibiti maambukizi na msaada wa kisaikolojia na teknolojia ya kisasa inaruhusu usahihi zaidi katika uchunguzi. Hii ni sehemu muhimu zaidi kuhakikisha maisha ya mtoto yanaendelea.

Kwa mujibu wa Dkt Neville A.G Solomon wa Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai, kinga ni bora kuliko tiba. Kuna njia nyingi ambazo mtu anaweza kujaribu na kuzuia ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa. Kliniki (ya mjamzito) kupata kipimo maalumu kitaalamu ‘echocardiography, ambacho hutumika kuchunguza moyo wa mtoto akiwa ndani tumbo la mama. Daktari bingwa wa Moyo unaweza kutambua kasoro za moyo mapema wiki ya kumi na nane ya ujauzito. Kwa hiyo ‘echocardiogram’ itawezesha wazazi kufanya maamuzi sahihi juu ya mustakabali wa mtoto kama kuna kasoro zilizogundulika katika moyo.

Njia nyingine ambayo inaweza kuzuia au kupunguza hatari kwa kuepukana ndoa kati ya ndugu wa damu, kwa mama kuacha kutumia baadhi ya madawa, na kuepuka mionzi wakati wa ujauzito huweza kumfanya mtoto kuzaliwa na kasoro katika moyo na pia mama kuepuka maambukizi. Njia ya kawaida ya kuepuka ugonjwa wa baridi yabisi katika moyo wa mtoto ni kwa kupatiwa matibabu ya maambukizi katika koo kwa wakati kwa kutumia antibiotiki.

Timu ya wataalamu wa magonjwa ya moyo kwa watoto Hospitali ya Apollo Chennai inaona fahari kubwa kupambana dhidi ya maradhi ya moyo kwa watoto duniani kote. Hii imewezekana kutokana na uvumbuzi mashine za mawimbi ya sauti zinazobebeka na za ukubwa wa kompyuta ndogo (mpakato). Hii Inawawezesha kufika sehemu za mbali zaidi duniani na kuchunguza kasoro na magonjwa ya moyo.

Baada ya upasuaji ingawa watoto wengi hutibiwa kikamilifu bado watahitaji ufuatiliaji kwa miaka ijayo. Baadhi wanaweza kuhitaji kurudiwa upasuaji hata hivyo wengi hawatahitaji dawa tena na kuwa na uwezo wa kuendelea na maisha ya kawaida kama watoto wengine. Wataweza wa kuishi wakiwa afya kwa muda mrefu maishani bila matatizo.

Inachangiwa na:

Dk Neville A.G Solomon
Mshauri, Mtaalamu Upasuaji wa Moyo kwa Watoto & Watu Wazima na Mkuu wa Idara ya Upasuaji Moyo kwa Watoto
Hospitali ya Watoto Apollo, Chennai.