Magazetini Agosti 29, 2015

LHRC yazungumzia kauli ya Mkapa "wapumbavu, malofa"


Ya Uchaguzi Mkuu: TCRA yatoa onyo kwa TBC1 na kuipiga faini Magic FM


MAMLAKA ya mawasiliano nchini (TCRA) imekipa onyo kali kituo TBC 1 kwa kosa la kubagua kusoma taarifa zinazohusiana na UKAWA.

Hukumu hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za TCRA na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Bgoya alisema kamati hiyo imebaini TBC one imekiuka sheria ya utangazaji ya mwaka 2005 pamoja na sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015 kwa kufanya upendeleo wa vyama katika taarifa zake.

Alidai katika kipindi cha "Jambo Tanzania" kilichorushwa tarehe 15 mwezi huu majira ya saa 12 asubuhi hadi saa tatu, katika kipingele cha uchambuzi wa magazeti mtangazaji wa kipindi hicho alikuwa anayasoma magazeti huku akiruka kusoma habari kuu husika. Alisema Mtangazaji huyo alipokuwa anachambua gazeti la Majira na Nipashe alidanganya umma jambo ambalo amedai ni kosa.

Bgoya alitaja makosa hayo kuwa ni wakati mtangazaji huyo alipokuwa anasoma gazeti la Majira ukurasa wake wa mbele alisema habari kubwa ni “CCM yazidi kuwaumbua wanaomfuata lowassa” wakati habari kubwa ilikuwa inasomeka hapo ni ile inayosema “Mbeya kwafurika”, huku picha ya gazeti hilo likionyesha picha ya umati watu pamoja na mgombea wa Urais, Edward Lowassa akihutubia.

Alisema mtangazaji huyo pia alifanya kosa jingine kama hilo pia wakati akisoma gazeti la Nipashe ambapo alisema habari iliyopewa uzito wa kipekee ni “Mbarawa atoa sheria ya mitandao” ambapo habari iliyopewa uzito ilikuwa ni ile “Mafuriko Mbeya” na sio aliyokuwa anaisoma yeye.

Alisema mtangazaji huyo alisikika akisema: “Gazeti la Majira, habari iliyopewa uzito wa pekee yasema: ‘CCM yazidi kupuuza wanaomfuata Lowassa. Yafananisha wanaohamia Ukawa na dizeli chafu… habari kwa kina ukurasa wa nne.”

Alisema kwenye gazeti la Nipashe, habari iliyopewa uzito wa juu ilikuwa na kichwa cha habari: “Mafuriko Mbeya” ambayo ilikuwa na picha ya Lowassa lakini mtangazaji wa kipindi alisikika akisema habari iliyopewa kipaumbele ni “Mbarawa kutoa elimu ya mitandao.”

Akimnukuu mtangazaji huyo, Bgoya alisema; “Gazeti la Nipashe, habari iliyopewa umuhimu wa pekee ni ‘Mbarawa atoa elimu ya mtandao’ …habari hii inapatikana ukurasa wa ndani.”
Alisema baada ya kamati yake kubaini makosa hayo waliwasiliana na Mkurugenzi wa TBC 1 Bwana Clement Mshana ambaye alitoa utetezi wake kwenye kamati hiyo akisema mtangazaji huyo hakufanya kosa kwa kuwa alikuwa hajaridhika na taarifa zilizokuwa zimeandikwa kwenye magazeti hayo.

Mshana alizidi kujitetea akidai kuwa hata mtangazaji huyo asingesoma habari ile lakini picha iliyokuwa inaonekana kwenye magazeti hayo tayari mtazamaji alikuwa ameshajua kwa hiyo haikuwa na ulazima wa kusomwa.

Aliendelea kutoa utetezi wake kwa kudai TBC1 inatoa taarifa zenye umuhimu wa kitaifa na katika kutangaza wanalindwa na taaluma ya uandishi wa habari ambapo mtangazji hatarusha taarifa yoyote hewani kama ana wasiwasi nayo.
“Nilipoulizwa niliambiwa mtangazaji alikuwa na wasiwasi na ile picha kama ni sahihi au kama imekuwa ‘doctored’ … kwa hiyo kilichomsukuma ni kwamba hata asipoisoma wanaoangalia televisheni wanaona sio lazima yeye atoe sauti yake kusisitiza hicho ambacho amekuwa na shaka nacho,’’ 
alisema Mshana.

Naye Mwanasheria wa TBC1, John Mapinduzi alisema hakuna kanuni yoyote iliyokiukwa katika shauri hilo kwa sababu mtangazaji alitoa taarifa kama zilivyochapishwa kwenye gazeti.

Bgoya alisema baada ya kusikiliza upande wa TBC 1 walibaini kuwa kituo hicho kilikiuka sheria ya utangazaji ambayo inavitaka vituo vyote vya utangazaji nchini kuripoti taarifa kwa kutokuwa na upendeleo wowote.

Alisema kamati imefikia uamuzi wa kuipa onyo kali TBC 1 na endapo wataendelea, mamlaka hiyo haitasita kuwachukulia hatua kali zaidi.

Aidha Bgoya alisema Kamati hiyo pia ililazimika kukipiga faini kituo cha Magic FM ya Sh2.5 milioni kwa kukiuka Kanuni za Huduma za Utangazaji (maudhui) ya 2005 Na.6(2)(b),6(2)(c) na 6(3)

Alisema kituo hicho kilijadili katuni zilizochorwa kwenye gazeti moja la Julai 7 mwaka huu na kuzifananisha na wagombea urais kwa kuwataja majina ikiwa ni pamoja na kuhusisha dini na masuala ya kishirikina.


Magufuli aahidi "mahakama maalumu ya mafisadi na wala rushwa"

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi,Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi katika viwanja vya Nzovwe mjini Mbeya jioni ya leo, kwenye mkutano wa kampeni ya kuwaomba ridhaa Watanzania ya kuwaongoza katika awamu ya tano
Dkt Magufuli amesema kuwa serikali atakayoingoza atakapopata ridhaa ya kuingia Ikulu,itazifanya huduma za Afya kuwa bora na kuwabana wahudumu wa afya wenye tabia ya kuchukua dawa na kuziuza kwa watu binafsi.

TMA yakanusha taarifa ya utabiri wa hali ya hewa kesho

TAARIFA KWA UMMA

28/08/2015

Kuanzia mida ya saa 7 mchana tarehe 29/08/2015 Jumamosi, kutakuwa na mvua kubwa sana maeneo yote ya Pwani, Dar es Salaam, Unguja, Mtwara na Tanga.

Pia mvua hiyo itaambatana na Upepo mkali sana ambao utakuwa unavuma kwa 123.7km/hr kutoka Kusini Mashariki kuelekea Ukanda wa Kaskazini.

Wananchi mnahaswa kutulia majumbani kwenu kwa muda huo hadi hali itakapo tulia kufikia tarehe 31/08/2015.

Pia watumiaji wa vyombo vya usafiri kama magari madogo, pikipiki, baiskeli na bajaji mnashauriwa kutotumia vyombo hivyo kwani Upepo utakuwa mkali sana kwa siku tatu hizo na unaweza kuhatarisha Usalama Barabarani.

Imetolewa na;
MAMLAKA YA HALI YA HEWA (TMA) - TANZANIA.
Morogoro Road, Ubungo Plaza, 3rd Floor
P.O.Box 3056,
Dar Es Salaam,
Tanzania,
Fax: +255 222460735, +255 2460700
Email; [email protected]
Website; Https://www.metro.go.tz/

Mdahalo wa vyama vya siasa kujadili suala la Utaifa

Tarehe: Jumapili Septemba 6, 2015

Muda: 9:00 alasiri – 11:00 jioni (saa tisa hadi saa kumi na moja)

Mahali:
Ukumbi wa Julius Nyerere International Conference Centre (JNICC) - Posta

Wageni waalikwa


Vyama vitano vya siasa tulivyochagua ndivyo vuilivyokuwa na wagombea wengi zaidi (ngazi ya ubunge na udiwani) kwenye uchaguzi mkuu ujao. Vimealikwa kutuma wataalam wao kushiriki midahalo itakayojadili maeneo muhimu yanayohusu wananchi. Wawakilishi hawa watahojiwa na jopo la wataalam wa sekta husika.

Midahalo hii itarushwa moja kwa moja na Star TV na Redio RFA

Kujiandikisha ni muhimu. Tafadhali tuma jina na chombo cha habari husika kwa [email protected] or call +255 768 129974

Uelewa wa wananchi juu ya mchakato wa uchaguzi

Tukio: Uzinduzi wa Ripoti ya Sauti za Wananchi | Uelewa wa wananchi juu ya mchakato wa uchaguzi

Tarehe: Jumatano Septemba 2, 2015

Muda: 4:00 – 5:00 asubuhi (saa nne hadi saa tano)

Mahali: Ofisi za Twaweza, (Barabara ya Mafinga, Imetazamana na Benki ya Stanbic Kinondoni)

Msemaji Mkuu: Aidan Eyakuze - Mkurugenzi Mtendaji, Twaweza

Maoni ya wananchi kuhusu ugunduzi wa gesi

Twaweza inapenda kukualika katika Uzinduzi wa Ripoti ya Sauti za Wananchi | Maoni ya wananchi kuhusu ugunduzi wa gesi

Muda: 5:00 asubuhi - 7:00 mchana

Tarehe: Jumanne Septemba 1, 2015

Mahali: Makumbusho (Imetazamana na IFM)

Wageni waalikwa: 
  • Peter Bofin - Oxfam Tanzania na Kenya
  • Ludovick Utouh - Mkaguzi Mkuu Mstaafu
  • James Mataragio - Mkurugenzi Mtendaji, TPDC
  • John Ulanga - Makamu wa Raisi, Ofisi ya Sera na Ushirika, BG Tanzania

Ukiwa na haraka Mbweni JKT jiandae kupiga mbizi

Gari likivuka eneo la mkondo wa bahari, ambapo pia ndipo panapojengwa daraja hilo hatua chache mkono wa kulia kutoka gari linapopita. Maji yakijaa hapo hakuna kupita wala kuvuka.
UPIGE mbizi. Ndivyo unavyoweza kusema msemo huu kama unahitaji kupita haraka haraka katika eneo la Mbweni JKT, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, mahala panapojengwa daraja la kuvukia watu kwa miaka mitatu sasa, halina dalili za kukamilika hivi karibuni. Ni eneo tata. Ni eneo linalokera na kusumbua watu mno. Mbaya zaidi, ni eneo lililozunguukwa na majumba ya watu wenye ukwasi au ukubwa wa majina ya viongozi waliojenga katika eneo hilo. Eneo linalojengwa daraja hilo ni kwenye mkondo wa maji unaotokea baharini.

Kwa wanaofahamu tabia za mikondo hii ya baharini watakuwa wanaelewa. Na wasiofahamu ni kwamba, linakuwa na tabia za kujaa maji na kupungua kila wakati. Kwa mfano, mtu anaweza kupita saa tatu asubuhi akakuka hakuna maji mengi. Lakini dakika kadhaa mbele, maji mengi yanajaa kutokea baharini. Ukifanya mkosi, ukiwa na haraka ya kuendelea na shughuli zako, ndipo hapo unapopaswa upige mbizi.
Hapa ndipo panapojengwa daraja hili.
Uyavulie nguo, upite. Na ikiwa na una gari, huna budi kusubiri kwanza yapunguwe kama si kuisha kabisa maji hayo. Au utafute njia nyingine za kukufikisha eneo unaloelekea, ingawa njia hiyo ina usumbufu mkubwa wa muda na gharama nyingine pia. Ni kutokana na hilo, serikali kwa kupitia Halmashauri ya Wilaya Kinondoni, inapaswa kupigia jicho kuu eneo hili. Iangalie tatizo ni nini? Mbona daraja hilo halikamiliki kwa miaka mingi sasa. Hakuna kinachoendelea. Watu wanapata tabu. Mbaya zaidi ni eneo linalovutia na kusisimua, maana haiwezekani mtu ajenge nyumba mamilioni ya shilingi wakati njia ya kumfikisha kwake haieleweki eleweki. Ni wazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni pamoja na DC Paul Makonda wanapaswa kuliangalia suala hili kwa kina.

Kama serikali haina fedha za kukamilisha mradi huo iwachangishe wananchi wake, maana hii adha wanayokutanaa nayo ya kupiga mbizi si nzuri. Inapoteza muda. Inadhalilisha pia. Ikiwa mtu anasafiri nje ya nchi, anawahi uwanja wa ndege, anaweza kushindwa kusafiri kwa kuchelewa ndege yake kama atafika kwenye eneo hilo na kukuta maji yamejaa. Ni aibu na fedheha kubwa. Mtaa umezunguukwa na majumba ya mamilioni ya shilingi. Mtaa umezaja watu wengi wenye nazo, viongozi wakubwa, lakini njia wanayopita inapitika kwa vipindi vya maji kujaa na kuisha. Hii haiwezekani. Serikali iliangalie hili la mradi wa daraja la Mtaa Mbweni JKT, ambalo nalo pia linajengwa chini ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
  • Taarifa hii tumeshirikishwa na Kambi Mbwana, Dar es Salaam

Freeman Mbowe's article at The HuffingtonPost: A dangerous shift against democracy in Tanzania

Last Saturday, we in Tanzania kicked-off our official campaign season that will culminate in elections at the end of October. Twenty four million Tanzanians are registered to vote to elect a new President, Parliament, and local government Councilors.

Unfortunately the day after, the government kicked-off a more ominous campaign: to stifle the democratic hopes and aspirations of the people of Tanzania by making a mockery of free and fair elections.

We in Tanzania and the supporters of democracy throughout the world must not allow this to happen.

Tanzania is the largest nation in east Africa, blessed with abundant resources and hardworking people. We are a young nation, gaining independence just over a half-century ago. Ours is a peaceful history, not marked by the coups and ethnic conflicts that have afflicted other countries in the region.

For our entire history as a sovereign nation, Tanzania has been ruled by only one party, Chama Cha Mapinduzi (CCM), the Party of the Revolution. In 1992, for the first time, a multi-party political system was instituted. Since then, the opposition parties have grown gradually stronger.

In the last election in 2010, my party, Chadema (the Party of Democracy and Progress) received almost 30% of the vote, with the combined opposition receiving 40%.

For the upcoming election, the four biggest opposition parties united to create the Ukawa coalition and agreed to support one person for president. Our candidate, the popular former Prime Minister Edward Lowassa, crossed over from CCM, stating the change Tanzania needs will not be brought about through a ruling party that has been in power for 50 years. With strong candidates across the nation, the united opposition has created the real possibility, if elections are free and fair, that the people of Tanzania will vote out the CCM on October 25th.

Moved by fear of losing, the ruling party is now resorting to undemocratic methods to maintain its grip on power. First, they passed a Draconian election expenses act which forbids the importation of any campaign materials, including flags, vehicles and finances, 90 days before the polling date. This deadline fell three weeks before the party's official nomination day. How can any candidate purchase materials before they know they are the official nominee?

On Monday, the police arrested 19 Chadema youths who were signing up supporters. They were arrested for the simple act of public campaigning. When the former Home Affairs Minister Lawrence Masha went to the police station to request their release, they arrested him, too.

The next day, the police ruled that our candidate Lowassa could not meet with the public. CCM was shocked by the public reception the former prime minister received when he drove on a bus to bring attention to the desperate need for better public transportation in Dar es Salaam, Tanzania's largest city.

Increasingly, the police are blocking our campaign's travel routes and disallowing our campaign plane from using airports. They have refused to grant our rally permits in the very grounds CCM held a rally only a few days before.

Finally, the government announced on September 1st, they will begin enforcing its free-speech suppressing "Cyber Security Act," which makes it a crime to criticize the government in emails or across social media.

By disallowing free speech and the right to assembly, and by arresting our youth for simply campaigning, the ruling party is clearly seeking to thwart the will of the people. We who have worked so hard to bring democracy to Tanzania will not accept this. We ask the support of people in the US, in Europe, in the rest of Africa and across the world to exert pressure on the government to allow both active healthy campaigns and free and fair elections.

We all applauded President Jakaya Kikwete, who after serving two-terms, is freely stepping aside, as required by the constitution. But we call on him as head of the government to allow free and fair elections, and if CCM is voted out, to allow a peaceful and orderly transition. A real multi-party democracy demands nothing less.

Freeman Mbowe is a Member of the Tanzania Parliament, Chairman of Chadema, and leader of the opposition.

Follow Freeman Aikaeli Mbowe on Twitter:www.twitter.com/freemanmbowe

cross-posted from the HuffingtonPost

[video] Dawa mpya ya kulevya "Flakka" inavyo-mess up watumiaji


Nchi ya Marekani sasa inapambana na dawa mpya hatari ya kulevya inayofahamika kama Flakka.

Maelezo mafupi kutoka katika tovuti ya Gawker yanasema:
Flakka (2013 - Present)
What it is: Alpha-Pyrrolidinopentiophenone, a synthetic stimulant
How it's done: Vaping, snorting, eating, smoking
Reported effects: Murderous rage, paranoia, ultra-violence, running around screaming
Is it real: Yes—multiple reported instances of individuals arrested while high on flakk
Peak year: 2015! NOW! RIGHT NOW! WE'RE SMOKING THIS SHIT TONITE!
Famous victim: Naked intersection guy
Flakka tayari imesababisha madhara makubwa katika jimbo ka Florida kiasi cha kusababisha Serikali ya Marekani kushikwa na hofu ya dawa hiyo kuzagaa katika majimbo mengine nchini humo.

Wataalamu wa tiba wameshangazwa na hali inayomtokea mtu anapokuwa katumia dawa hiyo ambapo  mtu hupiga kelele na kujizungusha huku akionekana kama mwendawazimu. Kadiri muda unavyokwenda, mtumiaji wa dawa hiyo huonekana kama mgonjwa wa kifafa.

Daktari Nabil el-Sanadi alifahamisha katika muungano wa hospitali ya Broward Health kuwa mtumiaji wa dawa hiyo hupatwa na ndoto za kutisha na kudai kukimbizwa na viumbe wa ajabu.

Ndani ya meizo 10, tayari watu 30 katika kitongoji cha Broward wamekwishafariki kutokana na matumizi ya Flakka.


Tanzania yasaini makubaliano na EU ya kuleta waangalizi katika Uchaguzi Mkuu 2015

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, na Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregondi, wakisaini Hati ya Makubaliano ya kuruhusu waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kuingia nchini kufuatilia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.
Na REUBEN MCHOME via blogu ya Mambo ya Nchi za Nje ya Tanzania

Umoja wa Ulaya (EU) utatuma timu ya waangalizi yenye wajumbe 128 nchi nzima katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2015. Hayo yalibainishwa wakati wa uwekaji saini wa Makubaliano ya awali ya kuruhusu timu hiyo kati ya EU na Serikali ya Tanzania uliofanyika kwenye Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tarehe 28 Agosti 2015. Uwekaji saini huo umefanywa na Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na kwa upande wa EU ulifanywa na Mhe. Filiberto Ceriani Sebregondi, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania.

Akizungumza baada ya uwekaji saini wa Makubaliano hayo, Balozi Sebregondi alieleza kuwa EU imekuwa ikituma timu hiyo kwa nchi washirika ambazo zina historia nzuri ya demokrasia. Aidha, nchi hizo zina dhamira ya dhati ya kukuza mahusiano na EU kwa kuruhusu waangalizi wafanye majukumu yao katika hatua zote za uchaguzi kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa uchaguzi unakuwa wa haki na huru.

Balozi Sebregondi aliendelea kueleza kuwa timu kama hiyo ambayo wajumbe wake wanakuwa Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya, ilitumwa katika uchaguzi wa mwaka 2010 ambapo iliutangaza kuwa ni huru na haki. Timu pia ilitoa ushauri na maelekezo ya namna ya kufanya maboresho katika hatua mbalimbali za uchaguzi.

Kwa upande wake, Balozi Mulamula aliikaribisha timu hiyo kuja Tanzania na alisema kuwa jukumu la Wizara yake ni kuratibu na kuhakikisha kuwa wajumbe wa timu hiyo wanatekeleza majukumu yao kama ilivyokubalika kwenye Makubaliano ya Kimataifa. Aliongeza kuwa maelezo ya undani wa shughuli ya timu hiyo wakati wa uchaguzi yatatolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ambao pia watasaini makubaliano ya utekelezaji wa kazi ya timu hiyo.

Taasisi nyingine za Kimataifa zinazotarajiwa kutuma timu za uangalizi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 ni pamoja na Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, na Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania, Mhe. Filiberto Sebregondi, wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya kuruhusu waangalizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Ulaya (EU) kuingia nchini kufuatilia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu. Hati hiyo ya makubaliano imesainiwa leo, 28-08-2015, katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo.Mkasa wa kusikitisha kuhusu Susanna, mpigania haki za ardhi za wakazi Loliondo

Hii ni simulizi ya kusikitisha kuhusu mwanaharakati wa mazingira kutoka Sweden, Susanna Nordlund, ambaye amekuwa akifanya harakati dhidi ya uporwaji wa ardhi na manyanyaso kwa wakazi wa Loliondo.

Kilichonigusa katika harakati za Susann ni ukweli kwamba ni raia wa kigeni anayepigani haki za Watanzania lakini amekuwa akifanyiwa hujuma na unyanyaswaji mkubwa.

Chini ni stori yake kama nilivyoitafsiri kwa idhini yake:


My late computer in Wasso before being arrested. Samsung in Nairobi established that the hard drive was taken.
Ripoti fupi jinsi nilivyokamatwa Loliondo:

Niliwekwa rumande siku mbili katika kituo cha polisi cha Loliondo na pia nilikaa rumande usiku mmoja katika kituo cha polisi cha Arusha.

Sikuruhusiwa kuwasiliana na mtu yeyote, kompyuta yangu iliharibiwa, na badala ya kuelekwa kortini, nilifukuzwa Tanzania.

Wiki iliyopita safari yangu ya hivi karibuni huko Loliondo -sehemu ya dunia ambayo siku zote ipo akilini mwangu- ilikatishwa ghafla baada ya mtu fulani kuniripoti kwa mamlaka za eneo hilo. Nilipania kukutana na watu ambao hawapo online lakini wana taarifa kuhusu vitisho dhidi ya ardhi yao vinavyofanywa na 'wawekezaji.'

Niliwasili Wasso kwa basi tarehe 20 Juni mwaka huu, na sikuwa na mengi ya kufanya wakati ninatafuta gari la kuelekea vijijini. Nilipata ofa moja nzuri lakini dereva akadai kuwa haendi kwenye vijiji hivyo mchana. Hatimaye tarehe 23 nilipata gari kwenda Kirtalo kwa nusu siku. Nikiwa njiani, nilipata ujumbe kwamba mmoja wa madereva wa kampuni ya utalii ya Thomson Safaris alimpigia simu kijana mmoja kumweleza kuwa ameniona na rafaki yangu flani katika nyumba ya wageni ya Domel. Nilikutana na watu hapo Kirtalo, rafiki yangu alibaki hapo, na nilirudi Wasso na dereva. Njiani, tulikutana na gari lililokuwa na Diwani wa Oloipiri 'rafiki wa wawekezaji' William Alais. Mpango wangu ulikuwa kwenda Mondorosi na Sukenya siku inayofuata.

Nilirudi nyumba ya kulala wageni na kuingiza kwenye kompyuta niliyoelezwa na watu huko vijijini lakini baadaye nikaptiwa na usingizi. Nilipoamka, tayari ilikuwa usiku na nikaenda kupata chakula katika nyumba ya kulala wageni ya Honest, hasa baada ya kuona mengi hapo Domel. Gari moja liliwasili, na waliokuwa ndani ya gari hilo walishuka na kuniijia. Afisa Uhamiaji Angela aliniuliza ninafanya nini Tanzania na akataka kuona hati yangu ya kusafiria. Nilimweleza ratiba yangu ya safari na mipango yangu, bila kumtajia dhima yangu kufahamu kuhusu waporaji ardhi ya wafugaji.

Nilikuwa na nakala tu ya hati yangu ya kusafiria, na niliombwa kufuatana na maafisa Uhamiaji na askari polisi kwenda Oloip nilipokuwa nakaa. Nilijaribu kutuma meseji wka marafiki lakini nilinyang'anywa simu yangu. Niliambiwa kuwa Idara ya Uhamiaji ilikuwa ilikuwa ikinifahamu vema kutokana na taarifa za mtandaoni, jambo lililonipa ahueni nikidhani ningeweza kusimulia maoni yangu kuhusu kinachoendelea. Nilifahamishwa kuwa niko chini ya ulinzi na kutakiwa kupakia vitu vyangu. Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Hashimu Shaibu Mgandilwa, ambaye nilimtambua baada ya kumwona katika vyombo vya habari, alikuwepo pia, japo hakujitambulisha, na alikuwa akiongea na maofisa wa Uhamiaji. Wakati tunaondoka hapo kwenda kwenye gari la Idara ya Uhamiaji, kitambu cha kuandikisha wageni kilichukuliwa, na nikapelekwa kituo cha polisi cha Loliondo.
Baada ya kufika kituo cha polisi, niliambiwa kuwa sababu ya kukamatwa kwangu ni kuwa niliingia Tanzania kama mgeni haramu.

Mwaka 2010, nilitembelea Loliondo kama mtalii kuwauliza watu kama Thomson Safaris- kampuni ya Kiamerika ya kutembeza watalii ambayo inadai kumiliki ekari 12617 za ardhi ya Wamasai, na kudaiwa kuwanyanyasa watu- inaendana na ilichoandika kwenye tovuti yake. Nilipatwa na shauku kuhusu suala hili baada ya maongezi mtandaoni. Mengi kwenye tovuti ya kampuni hiyo si ya kweli, lakini pia nilifanya kosa la kumuuliza Afisa Mtendaji wa Kata ya Soitsambu , ambaye alimpigia simu aliyekuwa Mkuu wa Wilaya wakati huo, Elias Wawa Lali, ambaye alinijibu siku iliyofuata.

Siku iliyofuata, nilifuatwa na polisi na kupelekwa katika Kamati ya Usalama. Nilituhumiwa vitu mbalimbali, kama vile kufanya utafiti bila kibali. Hati yangu ya kusafiria ilichukuliwa na ilinibidi kwenda Uhamiaji Arusha kuichukua, ambapo huko nako niliambiwa kuwa mie ni 'mgeni haramu' na kutakiwa kuondoka nchini humo.

Baada ya hapo ndio nilianzisha blogu yangu - Mtizamo kutoka kwenye kichuguu cha mchwa (A view from a Termite Mound) - kuhusu 'wawekezaji' huko Loliondo ambao ni tihshio kwa haki za ardhi - Thomson Safaris na wengine wanaofahamika zaidi OBC kutoka Falme za Kiarabu- ambao wamekuwa wakijitahidi kuishawishi serikali ya Tanzania kutangaza kilometa za mraba 1500 jirani na Mbuga ya Taifa ya Serengeti kuwa ni eneo lililohifadhiwa, na kuiondoa jamii ya Kimasai katika eneo hilo lenye umuhimu mkubwa kwa maisha yao. Mwaka 2009, suala hili lilipelekea wanavijiji kuondolewa kwa nguvu baada ya kurudi tena katika eneo hilo.

Nilirudi tena mwaka 2011 na 2013 bila matatizo yoyote lakini nimekuwa nikipata zaidi taarifa kuhusu adha zinazowakabili wakazi wa maeneo hayo kupitia watu wanaotumia mitandao ya kijamii (social media). Blogu yangu ni nyenzo muhimu kwa sababu sio tu serikali na 'wawekezaji' wanasambaza taarifa potofu bali pia taasisi na watu wanaopinga unyanyasaji huo wamekuwa wakichanganywa na taarifa potofu. Wenyeji wa Loliondo wanaopinga vitisho kuhusu ardhi yao wamekuwa wahanga wa unyanyasaji mkubwa, hususan kutuhumiwa kuwa ni Wakenya, lakini tishio kubwa zaidi ni kutoka kwa baadhi ya wakazi wanaonufaika na unyanyasaji huo kwa urafiki wao na 'wawekezaji.'

Baada ya kufikishwa kituo cha polisi Loliondo, nilitakiwa kuorodhesha vitu vyangu vyote. Lieleza bayana kuwa ninaamini kukamatwa kwangu kulitokana na 'siasa chafu' kuhusiana na suala la ardhi, na kwamba wanaopaswa kukamatwa ni hao wanaohatarisha maisha ya wanavijiji. Hata hivyo, niliambiwa nipo chini ya ulinzi, na sina haki yoyote. Afisa Uhamiaji Angela alinieleza kuwa nitapatiwa simu yangu siku inayofuata. Kisha nikaingizwa rumande nikiwa na kikoi changu ambacho nilikitumia pia kama blanketi. Nililala kwenye sakafu ya zege kwenye selo yenye kiza. Baadaye nilipewa chupa ya maji ya kunywa ambayo nilitumia kunawa uso, lakini sikunywa maji mengi kwa vile selo haikuwa na choo. Baadaye niliona ndoo inayotumika kama choo.

Loliondo ni sehemu yenye baridi nyakati za usiku, na madirisha ya selo hayakuwa na glasi bali nondo tu. Kulikuwa na mbu wengi na sikuwa na kinga ya kuzuwia mbu (mosquito repellent). Nilikuwa mfungwa wa kisiasa. Nilitetemeka kwa baridi, lakini maneno kutoka Kirtalo kuhusu blogu yangu yalinipa nguvu. Unyanyasaji dhidi yangu ulikuwa kama kichekesho, na baadhi ya watu walionyesha dalili za kuniunga mkono.

Asubuhi, nilipewa kifungua kinywa na kuruhusiwa kwenye bafuni, na kupatiwa maji ya kunawa uso kabla ya kurudi selo. Kwenye kuta za selo, kulikuwa namnaandishi kadhaa yaliyoashiria baadhi ya mahabasu walikuwemo humo bila mlo kwa siku kadhaa. Baadaye, nilichukuliwa na Angela kwenda ofisi ya Uhamiaji kuchukuliwa maelezo yangu. Alikuwa mkarimu kwangu na kunipatia peremende. Nilitoa maelezo yangu, na kueleza nilichokuwa ninafanya Loliondo, lakini bila kutaja majina kwa kuhofia watanyanyaswa. Angela alinieleza kuwa nitapelekwa kwenye nyumba ya kulala wageni kuoga kabla ya kupelekwa Arusha. Hata hivyo, alionekana kutofahamu kabisa kuhusu suala la haki za ardhi.

Nilirudishwa kituo cha polisi na kusubiri kwa muda mrefu wakati maofisa Uhamiaji wanafanya kikao na Mkuu wa Wilaya. Nilipata mlo na kuendelea kusubiri. Baadaye nilirudishwa tena rumande.

Mkuu wa Wilaya wa zamani, Elias Wawa Wali, alifanya kazi yake kibadhirifu akiitumikia serikali na 'wawekezaji' dhidi ya wanavijiji lakini hakuonekana kuwa na dhamira ya kufanya mabo mbaya zaidi. Mtangulizi wake, DC Hashimu Shaibu Mgandilwa, alikuwa na mawazo ya ajabu kabisa, kwa mfano kuwaamuru viongozi wa chini yake kutembea umbali wa kilometa nane kutoka Wasso hadi Liliondo, na kuishia kutupwa rumande baada ya askari mmoja mla rushwa kupigwa na wanakijiji Mei 6 mwaka huu.

Ilikuwa usiku nilipoamshwa, ANgela alikuja akiwa na bosi wake na mtu mwingine, na tuliondoka sote kuelekea Arusha. Tulipofika Olduvai nilipatiwa vitu vya kufanya usafi mwilini na baadaye tulisimama katika hoteli ya kifahari ya Serena Lodge kupata kifungua kinywa. Sina hakika kama gharama zililipwa kwa fedha za walipakodi wa Tanzania au na hoteli hiyo. Niltamani kuona ana angalau mtalii anayeonekana kama Mswidi lakini haikuwezekana. Nilitaraji kuwa albda taarifa zangu zimeshafika Ubalozi wa Uswidi.


Tulipofika Arusha, sikurejeshewa simu yangu. Angela, yule afisa Uhamiaji, alikagua vitu vyangu na kukuta orodha ya majina, na hilo halikumfurahisha. Ilikuwa ni orodha tu ya majina ya watu ambao nilipanga kufanya maongezi nao.

Baada ya hapo ilifuatia kusubiri kwa muda mrefu. Koo ilikuwa imenikauka na nilikuwa na uvimbe kufuatia kung'atwa na mbu. Nywele zangu, ambazo kwa kawaida huzisha kila usiku, zilikuwa ovyo ovyo. Nilijilaza kwenye benchi, na baadaye nikasikia mlango ukifunguliwa. Wanasheria waliotumwa na Onesmo Olengurumwa wa Kituo cha Haki za Binadamu waliwasili. Niliwaeleza kilichotokea na wakaniambiwa watashughulikia nipate dhamana ikiwezekana. Nilishakuwa nimewekwa rumande kitambo sasa na haikuwa haki kuninyima mawasiliano na watu wengine. Nilitaraji kuwa baada ya kutoka rumande itafuatia kesi mahakamani.

Baada ya muda mrefu nilielezwa kuwa nitarudishwa kituo cha polisi. Muda wote huo nilipokuwa nasubiri, sikupewa taarifa yoyote kuhusu inachoendelea. Ufahamu wangu mdogo wa Kiswahili ulichangia pia kutoelwa kinachoendelea. Niliwekwa tena rumande. Humo rumande nilkutana na mahabusu wengine, Sidamu aliyedai ni mtaalam wa wizi kwenye ATM na Mary aliyeiba maji kwa ajili ya kumwagia kwenye shamba lake.

Saa kadhaa baadaye nilichukuliwa kwenda ofisi ya Uhamiaji na kuchukuliwa alama za vidole. Mchana, nilifahamishwa kuwa mie ni 'mgeni haramu' na sintoruhusiwa tena kuingia Tanzania. Niliambiwa kwamba kitu pekee ninachoweza kufanya ni kuandika barua Wizara ya Mambo ya Ndani. Niliomba majina ya watu ninaoweza kuwasiliana nao kwa barua-pepe lakini sikupewa, na sikurudishiwa simu yangu.

Nilisindikizwa hadi Namanga, nikiwa kati ya watu wawili katika gari. Mpakani Namanga kulifuatia kusubiri kwingi na kupigwa picha. Niliomba nakala ya hati ya kutangazwa 'mgeni haramu' lakini sikupewa. Nilisema kwamba ningerejea tena siku moja, na afisa mmoja wa Uhamiaji alimweleza mwenzie, "haogopi kitu."

Baada ya kuingizwa Kenya nilipatiwa simu yangu, na dereva mkarimu alinipeleka hotelini. Nilapata fursa kuangalia mitandao ya kijamii na kulikuwa na taarifa za kukamatwa kwangu. Pia nilipata wasaa kuwafahmisha ndugu na jamaa kuwa nimeachiwa huru. Familia yangu haikufahamishwa lolote nilipokamatwa, na maofa wa Ubalozi wa Uswidi hawakuruhusiwa kuwasiliana nami bila idhini yangu (ningewezaje kutoa idhini ilhali walizuwia mawasiliano yangu na mtu yeyote yule?)

Kompyuta yangu ambayo huwa nayo muda wote iligoma kuwaka. Kesho yake nilimpata mtaalam wa kompyuta hapo Namanga ambaye alibaini ilikuwa na matatizo.

Tarehe 30 nilifahamishwa kuwa mwandishi mmoja, Manyerere Jackton ameandika kwa kirefu kuhusu mimi katika gazeti la kila wiki la Jamhuri. Kesho yake niliweza kuiona habari husika........ na ilikuwa na uongo mwingi. Kama nilivyotarajia, mwandishi huyo alijaribu kunifarakanisha na Tina Timan ambaye sijawahi kukutana nae. Huyu ni anayelezwa kuwa ni mwanaharakati kutoka Kenya, japo amekuwa akiishi Tanzania kwa muda mrefu na ana watoto hapo. Mwandishi huyo amekuwa akichochoea vitu vingi dhidi ya wanavijiji wa Loliondo.

Manyerere- au mtoa habari wake- alidai kuwa nilisema kwamba ningehakikisha serikali ya Uswidi inakata misaada kwa Tanzania kama seriali haitoendelea kunisumbua. Licha ya kwamba sina uwezo huo, lakini kila anayenifahamu anajua nisingeweza kusema maneno kama hayo. Kitu pekee nilichosema kuhusu nchi yangu ni katika nchi yoyote yenye demokrasia, mtalii nanaweza kuongelea siasa na mtu mwingine, baada ya kuambiwa pale kituo cha polisi kuwa "hakuna sehemu yoyote duniani mtalii anaruhusiwa kuongelea siasa." Huu ni unafiki wa hali ya juu katika nchi ambayo ni mhanga wa ukoloni mamboleo.

Katika habari hiyo, Kamishna wa Uhamiaji Abdullah Khamis Abdullah alimpongeza DC Mgandilwa kwa 'kudumisha amani wilayani kwake.' Sio tu uwepo wa Mkuu wa wilaya ni zao la ukoloni bali pia afisa huyo amekuwa akiwatenda wanavijiji kama ilivyokuwa zama za ukoloni.

Mwandishi huyo alinituhumu kuwa mie na 'washirika wangu' tumekusanya mabilioni ya shilingi kwa ajili ya wafugaji wanaonyanyaswa na kuzifadhili NGO za kuchochea vurugu katika vijiji husika. Sijawahi kuksanya fedha zozote wala kutoa chochote kwa NGO. Mie ni bloga tu.

Tishio baya zaidi ni kuwapeleleza wanavijiji wote wanaonisaidia, na kwa kukosa mwelekeo,miongoni mwa wahanga ni mmiliki wa nyumba ya kulala wageni niliyofikia kama mteja mwingine yeyote yule.Itanilazimu nimlipe fedha zake za huduma ya malazi, kupitia huduma ya kuta fedha ya Western Union, mara baada ya kurudi nyumbani, kwani nilichukuliwa kutoka sehemu hiyo ghafla.

Sijui kwanini sikufunguliwa kesi mahakamani. Ingekuwa fursa nzuri kuweka wazi kinachoendelea Loliondo, na kuuliza iwapo watalii hawaruhusiwa kuuliza mwaswali wawapo Tanzania, na iwapo watalii wanaooblogu wanahitaji viza maalumu kuingia katika nchi hiyo.

Sasa dhamira yangu ni kuendelea kuandika kuhusu Loliondo katika uhai wangu wote, na kwa hakika nitarudi tena.

NYONGEZA: Uchunguzi uliofanywa na mafundi wa kampuni ya Samsung umethibitisha kuwa Hard Drive ya kompyuta yangu ilichomolewa nilipokuwa Tanzania.

Pia, Manyerere alinitumia barua pepe kwamba amesoma blogu yangu na anaitetea nchi yake dhidi ya 'ukoloni mamboleo' wangu, akisema 'Tanzania ni kwa ajili ya Watanzania.' Jibu la wazi lilikuwa mshangao kwanini amekuwa akiandika makala mbalimbali za kichochezi dhidi ya wanavijiji wa Loliondo kwa maslahi ya wawekezaji kutoka nje. Badala ya kunijibu swali hilo, mwandishi huyo alijibu haraka kwa kunitumia picha za mtu aliyekuwa akitoa habari Loliondo, na kujigamba kuwa kila nyendo zangu 'haramu' nikiwa huko ilikuwa ikifuatiliwa japo hakubainisha uharamu wa nyendo zangu katika nchi ya kidemokrasia.

Habari hii imetafsiriwa kutoka blogu ya Susanna, kama ilivyoandikwa HAPA. Kadhalika, waweza kuwasiliana na mwanaharakati huyo wa haki za ardhi, kwa barua-pepe [email protected]

MTIZAMO WANGU: Nimemfahamu Susanna kutokana na kuguswa kwake na kujishughulisha kwake na haki za ardhi huko Loliondo. Nina imani wasomaji wengi mnafahamu kuhusu maslahi ya taifa letu yanavyowekwa rehani katika maeneo kadhaa yenye raslimali za taifa letu. Haiingii akilini, mwanaharakati kama Susanna aache shughuli zake huko Uswidi, aende Tanzania kuwachochea wanavijiji. 'Kosa' la dada huyo ni kuwa mtetezi wa wanyonge. Imekuwa kawaida sasa kwa kila anayejaribu kukemea maovu kuitwa adui wa taifa letu. Kwa hakika inaumiza sana kuona watu wanaojali maslahi ya taifa letu wananyanyaswa kiasi hiki na kutangazwa 'maadui wa taifa.'

Evarist Chahali
Kulikoni Ughaibuni blog

Majina ya walioomba mkopo wa elimu HESLB wanaotakiwa kurekebisha taarifa

Mkurugenzi Mtendaji HESLB  Bw. George Nyatega
George Nyatega
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha ya waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016 ambao fomu za maombi zimegundulika kuwa na upungufu na kuwataka kufanya marekebisho kabla au ifikapo tarehe 11 Septemba mwaka huu (2015).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi hiyo leo (Ijumaa, Agosti 28, 2015), jumla ya fomu za waombaji wa mikopo 7,788 kati ya 68,445 zilizopokelewa na kuhakikiwa zimegundulika kuwa fomu zina upungufu na kuwataka waombaji kusoma majina yao katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. George Nyatega, (Pichani) waombaji ambao fomu zao zimegundulika kuwa na upungufu wanatakiwa kurekebisha kabla au ifikapo tarehe 11 Septemba mwaka huu (2015).

“Baada ya kusitisha uombaji wa mikopo kwa njia ya mtandao kwa mwaka wa masomo 2015/2016, Bodi ilianza kufanya uchambuzi wa maombi yote yaliyopokelewa na kugundua kuwa maombi 7,788 ya mikopo yanakosa taarifa muhimu,” inasomeka taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, taarifa muhimu zinazokosekana ni pamoja na sahihi za waombaji, nakala za vyeti vya kuzaliwa vya waombaji, sahihi na picha za wadhamini na baadhi ya fomu za maombi kutosainiwa na wanasheria na maafisa wa serikali za mitaa kama maelekezo yanavyotaka.

“Bodi inawataka waombaji wa mikopo ambao fomu zao za maombi zimegundulika kuwa upungufu, kufika wao wenyewe katika ofisi za Bodi zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam ili kufanya marekebisho katika fomu hizo,” imesisitiza taarifa hiyo na kuongeza kuwa majina waombaji wanaotakiwa kufika katika ofisi za Bodi yanapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz).

Aidha, Bodi ya Mikopo imewakumbusha waombaji wa mikopo kuwa waangalifu na kuchukua tahadhari dhidi watu wasio waaminifu ambao wanaweza kutumia zoezi hilo kuwadai fedha.

HESLB ilianzishwa kwa sheria ya Bunge na 9 ya mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai, 2005 ili, pamoja na majukumu mengine kutoa mikopo kwa wanafunzi wahitaji waliodahiliwa katika taasisi za elimu ya juu.

Aidha, jukumu jingine la Bodi ni kudai na kukusanya mikopo yote iliyotolewa kwa wahitimu wa taasisi za elimu ya juu kuanzia mwaka 1994 wakati Serikali ilipoanza kukopesha wanafunzi.