Wakuu wote wa Wilaya...


Tangazo la kuitwa kwenye usaili Polisi

TANGAZO KWA UMMA.

JESHI LA POLISI TANZANIA LINAWAITA KWENYE USAILI WAHITIMU WALIOORODHESHWA WA SHAHADA, STASHAHADA NA ASTASHAHADA. USAILI UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE 03.09.2015 HADI TAREHE 04.09.2015 KUANZIA SAA MBILI ASUBUHI HADI SAA KUMI JIONI KATIKA MAENEO YAFUATAYO:-
·         FANI YA UTAWALA, UCHUMI, USIMAMIZI WA SHERIA NA UTEKELEZAJI [BALE], UALIMU, UANDISHI HABARI, UHANDISI MADINI [MINING ENGINEERING], UGAVI, LUGHA, USHAURI NASIHI, KATIBU MUKTASI, LAND SURVEY CATHOGRAPHER NA GEOMATICS WATAFANYA USAILI KATIKA CHUO CHA TAALUMA YA POLISI DAR ES SALAAM [DPA] KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI JIJINI DAR ES SALAAM.

·         MAFUNDI MAGARI, MATENGENEZO YA PIKIPIKI, MAFUNDI MATENGENEZO YA UMEME WA MAGARI [AUTO ELECTRICAL], MAFUNDI RANGI ZA MAGARI, MAFUNDI MAGARI, MAFUNDI USHONAJI,MAFUNDI BODY ZA MAGARI NA MADEREVA. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA POLISI UFUNDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.


·         MATENGENEZO YA KOMPYUTA, FAX & PHOTOCOPY MACHINES NA MAWASILIANO YA REDIO [DIPLOMA IN RADIO COMMUNICATION], USAILI WAO UTAFANYIKA NYUMA YA KIKOSI CHA UFUNDI YAANI TEHAMA KEKO CHINI.

·         WAKEMIA, BAILOJIA [MOLECULAR BIOLOGY] USAILI UTAFANYIKA MAKAO MAKUU YA POLISI YALIYOPO MAKUTANO YA BARABARA YA OHIO NA GHANA JENGO LINALOTAZAMANA NA POSTA HOUSE.


·         KADA ZA AFYA USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA AFYA KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.

·         MANAHODHA NA MAFUNDI MITAMBO WA MELI, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA WANAMAJI KILICHOPO KARIBU NA JENGO LA MAHAKAMA YA RUFAA.

·         DAKTARI WA WANYAMA, USAILI WAO UTAFANYIKA KATIKA KIKOSI CHA MBWA NA FARASI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.

·         MAFUNDI AC ZA MAJUMBANI, ARCHITECTURE DRAFTMAN, QUANTITY SURVEYORS, CIVIL ENGINEER, WELDING & FABRICATION, UMEME WA MAJUMBANI, PAINTING, ALUMINIUM & GLASS WORK, PLUMBING, MOSONRY, MOTOR REWINDING, HYDRO GEOLOGY DRILLING WELL, REFRIGERATION & AIR CONDITIONING. USAILI WA KADA HIZI UTAFANYIKA KIKOSI CHA POLISI UJENZI NDANI YA KAMBI YA POLISI BARRACKS KURASINI KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.

·         FANI ZA BENDI, BRASS BENDI, WOODWIND, STRING JAZZ NA PERCUSSIVE, USAILI WAO UTAFANYIKA KIKOSI CHA BENDI KILICHOPO KANDO KANDO YA BARABARA YA KILWA KURASINI DAR ES SALAAM.

·         FANI YA URUBANI,USAILI  UTAFANYIKA  KIKOSI CHA ANGA KILICHOPO UWANJA WA NDEGE NDOGO WA ZAMANI WA J.K.NYERERE DSM.

MUHIMU:
1.      MWOMBAJI AFIKE KWENYE USAILI AKIWA NA NAKALA HALISI YA VYETI VYOTE VYA MASOMO/TAALUMA [ACADEMIC TRANSCRIPT (S)/CERTIFICATE (S) YAANI KIDATO CHA NNE, SITA, CHUO NA CHETI CHA KUZALIWA. KIAPO CHA KUZALIWA HAITAKUBALIWA.
2.      MWOMBAJI ALIYEITWA KWENYE USAILI ATALIPIA GHARAMA ZA UPIMAJI AFYA SHILINGI ELFU KUMI (10,000/=), USAFIRI, CHAKULA NA MALAZI KWA MUDA WOTE WA ZOEZI LA USAILI.
3.      AMBAYE HATAHUDHURIA USAILI KUANZIA SIKU YA KWANZA HATAPOKELEWA.
ILI KUPATA/KUONA ORODHA YA MAJINA, TEMBELEA www.policeforce.go.tz
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Two types of foods that make a Complete Breakfast explained


Muadhini akamatwa kwa kusema assalatu hayrun minal Facebook

Muadhini mmoja amekamatwa nchini Misri kwa kuongeza maneno katika adhana ya sala ya asubuhi

Alikamatwa mjini Kafr al-Dawar Kaskazini mwa Misri baada ya kusikika katika vipaza sauti vya msikiti wa Rahmat akisema akisema assalatu hayrun minal Facebook badala ya 'assalet├╝ hayrun minennaw' kama ilivyo katika utamaduni wa Kiislam katika wito wa sala ya asubuhi.

Assalatu hayrun minannaw kwa Kiarabu humaanisha kuwa sala ni bora kuliko usingizi, lakini muadhini huyo  alibadilisha na kusema kuwa sala ni bora kuliko Facebook.
[via TRT Kiswahili]

Lowassa aahidi elimu bure hadi Chuo Kikuu na malipo ya madeni ya mishahara

Lowassa ameahidi kutumia fedha itakayopatikana katika uzalishaji wa gesi kama sehemu ya kutekeleza ahadi ya elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi Chuo Kikuu. Amesema akiwa Rais wanafunzi hawatalipa chochote na elimu itakuwa bora na atahakikisha walimu na watumishi wengine wa Serikali wanalipwa madai yao yote.

Ameyasema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa kituo cha polisi cha mji wa Makambako.

Lowassa alisema pia atatumia fedha zitakazopatika katika zao la pamba huku akihoji zilivyotumika fedha ambazo serikali ya awamu ya nne imekopa kutoka nchi wahisani.

Kwenye mkutano huo, Sumaye alitumia mtindo wa kuwauliza wananchi, “CCM” huku wakimjibu “Ni shiiiida”, kueleza mambo matatu yaliyofanywa na serikali ya CCM na kusababisha watanzania waishi kwa matabaka.

“Tumetengeza ilani kiboko ambayo ndani ya miaka mitano Tanzania yetu itabadilika, lazima tupunguze tabaka kati ya tajiri na masikini kwa uchumi wa pamba, chai, dhahabu na gesi kwa nini tushindwe. Mkitupa ridhaa na Mungu akikubali tukakwenda kasi na tutakuwa na maendeleo.

Sumaye alisema Watanzania wamepata shida mpaka kufikia wakati wanaamini shida ni sehemu ya maisha yao, huku akisema nchi ya Libya iliingia katika matatizo kwa sababu utawala uliokuwepo ulikataa kuwapisha wengine kuongoza nchi na kukandamiza watu.

Soma zaidi habari hii kesho kwenye gazeti la MwananchiWatuhumiwa wa EPA waachiwa huru

Washitakiwa watano wameachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kutokukutikana na hatia iliyowashitaku kuwa walijipatia takribani shilingi nilioni 5.9 kutoka kwenye Benki Kuu ya Tanzania (BoT) .

Hukumu iliyowaachia huru imesomwa leo na Hakimu Sundi Fimbo kwa niaba ya jopo la mahakimu 3 waliokuwa wanasikiliza kesi hiyo. Fimbo alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi tisa wa upande wa mashtaka pamoja na utetezi , watuhumiwa wanaachwa huru kutokana na upande wa mashtaka kushindwa kuyathibitisha mashitaka sita pasina shaka.

Washitakiwa walioachiwa huru ni Kada wa CCM, Rajabu Maranda, mfanyabiashara Ajay Somani na wafanyakazi wa BoT, Ester Komu, Bosco Kimela na Iman Mwakosya. Walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kuwasilisha nyaraka za uongo na kusababisha hasara.

Katika kesi hiyo watuhumiwa walishitakiwa ifuatavyo:
 • Maranda na Ajay: Kula njama na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. 
 • Maranda: Kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. 
 • Ester Komu, Iman Mwakosya na Bosco Kimela: Kusababisha hasara.
Habari kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, soma kesho kwa kina zaidi.

5 tips on how to reduce chances of acohol abuse, drug addiction

If you grew up in a family of substance users, you know that your risk for developing an addiction to drugs or alcohol is greater because of this hereditary factor. But what exactly are your risks? And is there anything you can do to reduce your risk?

The bottom line is that there are still a lot of uncertainties when it comes to assessing drug and alcohol risks as they relate to family history. The good news is that even if you come from a family with a troubled history, or a history of addictions, that does not mean you will automatically become an addict. The risk is higher, but there are ways to prevent that from happening. You can choose to be proactive and greatly reduce your addiction risk.

Here are a 5 suggestions to reduce your addiction risk:

 1. Avoid under-age drinking or substance use; early-onset of use increases risk
 2. Choose abstinence or carefully monitor your consumption
 3. Avoid associating with heavy drinkers or substance users
 4. Manage your psychological health; seek assistance from a mental health provider if you are highly stressed, anxious or depressed
 5. Participate in workplace or school prevention programs
Read the full post (including intervention strategies) at recovery.org
 • Shared to us by Mellisa "Mel" who says "I'm a writer and I'm also a recovering addict."

Italy donates cancer screening facility to Mbweni hospital

The government of Italy through its charitable organization, Ruvuma Onlus Limited, has donated a mobile Mammography Facility to help screening breast cancer at Mbweni Hospital in Kinondoni District, Dar es Salaam Region.

The 80,000 euro facility was officially handed over yesterday by the Ambassador of Italy to Tanzania, Mr Luigi Scotto.

Speaking at Mbweni Hospital, the Head of Radiology Department at the Ocean Road Cancer Institute, Dr Yekebeth Uuhahula, thanked the sponsors for donating the machine, saying that it shall enable early treatment of women who suffer from that disease.

"The facility has come at the right moment, when we plan to carry out Breast Cancer awareness campaign in October, this year.

The facility shall help women get early treatment," she said. She added that breast cancer is still a big challenge in Tanzania, because majority of women fail to turn up for early treatment. She said most women go for healing when the cancer has already advanced.

"Over 400 women who were screened at Ocean Road Hospital last year had signs of breast cancer and among them, 200 had already been affected by the disease.

On the other hand, the Italian envoy said the facility would help Tanzania women detect breast cancer at an early stage before symptoms develop.

"Prevention is better that cure, the availability of the machine will enable women get treatment if detected to have the disease," he said.

Breast cancer is the second most common cancer in women. in Tanzania, Dr Uuhuhela said breast cancer was the second killer disease after cervical cancer.
 • Story by Anne Robi via The DailyNews, Tanzania 

Dk Lwaitama ajiunga CHADEMA

Azaveli Lwaitama
Azaveli Lwaitama
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kimemkabidhi kadi ya uanachama pamoja na katiba ya chama hicho, Dk. Azaveli Lwaitama ambaye amesema kujiunga kwake kutamfanya aendelee na harakati za ukombozi kwa wananchi malofa na wapumbavu.

Dk. Lwaitama ambaye ni Mwalimu mkongwe katika Vyuo Vikuu amesema yeye tangu mwaka 1976 alikuwa ni mwanachama mfu wa CCM kutokana na kutolipia kadi yake jambo ambalo amesema ni kutokana na kuwa na chama ambacho ni cha ukandamizaji.

Akizungumzaia kuhusu mgombea Urais wa Tanzania 2015 kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA, Edward Lowassa, amesema mgombea huyo ndiye anayefaa kushika nchi kutokana na uwezo wake wa kufanya kazi kwa umakini zaidi.

[video] Kanye West: "I have decided to run for president"Serikali kushirikiana na Asset Holding kuimarisha reliSERIKALI kwa kushirikiana na kampuni ya reli ya Asset Holding imejizatiti kuimarisha miundombinu ya reli itakayogharimu shilingi trilioni 16/= katika kuleta maendeleo endelevu hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa uchukuzi Mhe. Samuel Sitta amesema kuwa mkakati wa kuimarisha reli katika maeneo mbalimbali hapa nchini utayanufaisha maeneo ya  Songa Mpiji, Mtwara hadi Mbambabay, Songea hadi Mchuchuma na mradi mpya wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Bagamoyo.
"Lengo la miradi hii ni kuhakikisha kuwa tunaleta maendeleo ya kiuchumi kwa kujipatia fedha za kigeni ambazo zitatokana na usafirishaji wa mizigo nje ya nchi" 
amesema Sitta na kuongeza kuwa miradi hiyo inatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa tisa ambapo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ataweka jiwe la msingi tayari kwa utekelezaji.

Aidha, alibainisha kuwa kuimarisha miundombinu ya reli kutasaidia kurahisisha usafirishaji wa mizigo yenye uzito mkubwa kama mafuta, makaa ya mawe na chuma ndani na nje ya nchi.
 • JenikisaNdile – Idara ya Habari, Maelezo

AMJIBU SUMAYE

Sitta amemjibu Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, aliyeituhumu serikali ya Rais Kikwete kuwa imewafumbia macho watendaji walioisababishia hasara nchi zaidi shilingi bilioni 220 kwenye ununuzi wa mabehewa yanayotajwa kuwa ni feki.

Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za wizara yake, Sitta amesema watendaji wote waliohusika na kashfa hizo watafikishwa mahakamani muda wowote kutoka sasa baada uchunguzi kukamilika.

Aliongeza kwamba kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo imeshakamilisha kazi yake na kuonesha kulikuwa na uzembe kwa watendaji wa shirika la reli (TRL) uliosababisha kununuliwa kwa mabehewa hayo.

Aidha amesema kuwa kamati hiyo ilikwenda hadi nchini India kuichunguza kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited ambayo ndiyo watengenezaji wa mabehewa hayo mabovu na kubaini kampuni hiyo iliyopewa zabuni ilikuwa haina sifa.

Hata hivyo, Sitta ameongeza kuwa kamati hiyo ilibaini kampuni hiyo haikuwa na sifa na watendaji TRL walikiuka kanuni za manunizi ya serikali kwa kitendo chao cha kutoa fedha zote kwa kampuni hiyo kabla hawajaleta mabehewa.

Viongozi wanaotuhumiwa katika sakata hilo kuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Kipallo Kisamfu; Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosowile Ngosomiles; Mhasibu Mkuu Mbaraka Mchopa; Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Kampuni, Jasper Kisiraga; na Meneja Mkuu wa Manunuzi, Ferdinand Soka.
 • DENIS MTIAMA/GPL

CCM yaahidi hospitali Ikungi na bandari kavu Manyoni

Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni ulofanyika Wilaya ya Ikungi.
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa kampeni ulofanyika Wilaya ya Ikungi.
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu ameendelea kunadi ilani ya chama chake huku akiahidi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ikungi pamoja na ujenzi wa bandari kavu wilayani Manyoni endapo wananchi watakipa ridhaa ya kuunda serikali mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015.

Bi. Samia alitoa ahadi hizo jana katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Ikungi, wilayani Ikungi ikiwa ni jitihada za serikali ya CCM kuhakikisha inaendelea kuboresha huduma bora za afya kwa wananchi mjini na vijijini.

Alisema serikali watakayoiunda itaendelea kushughulikia kero ya maji katika vijiji vyenye ukame na kuhakikisha kila kijiji kinapata maji safi na salama kwa matumizi, pamoja na kuvipelekea umeme baadhi ya vijiji vya Singida Mashariki ambavyo bado vijafikiwa na huduma kupitia awamu ya pili ya mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kuchochea maendeleo vijijini. Alisema katika kuboresha miundombinu wataikarabati barabara ya Mung'aa kwenda Nkiku ili iweze kupitika na kuwasaidia wananchi wanaoitegemea barabara hiyo.

Akihutubia katika mkutano mwingine wa kampeni Wilaya ya Manyoni, Bi, Suluhu aliahidi ujenzi wa bandari kavu eneo hilo ikiwa ni jitihada za kuongeza nafasi za ajira kwa vijana na kukuza uchumi na maendeleo ya wilaya hiyo. Alisema Serikali watakayoiunda itaunda mfuko wa maji ambao utashughulikia kero za huduma za maji safi na salama kwa wakazi wake.

Aidha watahakikisha vijiji ambavyo bado havina mawasiliano vinapata huduma hiyo ili kuchochea maendeleo ya wananchi katika mawasiliano. Bi. Samia amewataka Watanzania kutofanya makosa ya kuvichagua vyama vingine vya upinzani maana havina muelekeo na kuviita vya kuunga unga.

"...Tusifanye mchezo kwa kuvijaribu vyama vya kuungaunga kuingia madarakani, huwezi kufanya majaribio ya kuonja simu...hivi mlisha ona wapi chama kinasimamisha wagombea ambao sio wao bali wameazimisha kutoka vyama vingine, hivi havitufai hata simu moja," alisema B. Samia Suluhu.
 • Tumeshirikishwa taarifa hii na Joachim Mushi/TheHabari.com

Ilani ya uchaguzi ya CHADEMA: Moshi Mjini

Meneja Kampeni wa mgombea Ubunge katika jimbo la Moshi mjini kupitia CHADEMA na UKAWA, Bw Raymond Mboya akitambulisha mbele ya wanahabari wa mkutano wa mgombea huyo na wanahabari uliofanyika katika hoteli ya Keys.
Na Dixon Busagaga, Moshi
ILANI YA CHADEMA KATIKA MANISPAA YA MOSHI.

1.      ELIMU:
A.     ELIMU YA AWALI:
·         Kuimarisha madarasa ya awali.
·         Upatikanaji wa walimu wa awali.

B.      ELIMU YA MSINGI:
(i)                 Kuongeza matundu ya vyoo katika shule za msingi ndani ya Manispaa ya Moshi.
(ii)               Kujenga silos katika shule mbalimbali za msingi ya kuhifadhi nafaka za shule.
(iii)             Kuongeza nyumba za walimu.
(iv)              Kuongeza madarasa na kukarabati  yaliyopo.
(v)                Kusaidia kulipia michango ya chakula kwa watoto yatima na wanaotoka familia duni
(vi)              Kuimarisha elimu ya computer katika shule zetu za msingi.
(vii)            Kuongeza mtandao wa maji safi kwa shule za msingi.

C.      ELIMU YA SEKONDARI:
·         Kuongeza matundu ya vyoo
·         Kuongeza na kuimarisha miundombinu ya vyumba vya maabara.
·         Kuongeza vyumba vya kulia chakula (mabwalo).
·         Kujenga maktaba katika shule za sekondari.
·         Kupandisha daraji baadhi ya shule za kawaida kuwa za kidato cha tano na sita.
·         Kuhakikisha familia duni na za watoto yatima zinasaidiwa michango mbalimbali ya shule.


(2) AFYA:
·         Kusukuma upatikanaji wa hospitali ya Wilaya.
·         Kuimarisha vyumba vya upasuaji katika vituo vya afya.
·         Kuboresha zahanati.
·         Kujenga vyumba vya kuhifadhia maiti katika vituo vya afya.
·         Kujenga uzio katika vituo vya afya na zahanati ili kudhibiti usalama wa wagonjwa.
·         Kusukuma kusimamia kwa sera ya matibabu ya bure kwa wazee na watoto chini ya miaka mitano.
·         Kuongeza na kuimarisha vyumba vya kuzalishia. (labour ward)
·         Kuongeza nyumba za waganga wa vituo.

(3) MAJI:
·         Kuongeza mtandao wa maji safi na maji taka kwa kushirikiana na mamlaka ya maji safi na maji taka.((MUWSA)
·         Mh: Kata ya Kiboriloni, Longuo B na Rau.

(4) Makundi maalum:
·         Kuboresha miundombinu ya makundi maalum katika majengo ya serikali
·         Kuimarisha na kuboresha miundo mbinu ya shule za watu wa makundi maalum.
·         Kushirikiana na vyama vya watu wenye ulemavu
·         Kushirikiana na Asasi za kiraia zinazohudumia makundi maalum katika jamii

(5) MIUNDO MBINU:
·         Kuongeza mtandao wa barabara za lami kwenye maeneo ya katikati ya mji na
Kata za pembezoni.
·         Kupandisha barabara za kiwango cha vumbi kwenda kiwango cha changarawe(moramu)
·         Kuimarisha barabara mbalimbali ndani ya Kata na Mitaa yake katika manispaa ya Moshi.
·         Kujenga na kuimarisha mfereji wa maji ya mvua katika manispaa ya Moshi ili kulinda barabara za Manispaa.
·         Kujenga vivuko na kumalizia madaraja ndani ya Manispaa ya Moshi.
·         Kuongeza na kuimarisha mtandao wa taa za barabarani.

 (6) UCHUMI:
(A) AJIRA:
(i) Tutaendelea kuboresha ajira zisizo rasmi (informal sector) ili ziwezeshwe kurasimishwa.
·         Kutenga maeneo rasmi
·         Kuzuia matumizi nguvu kwa wajasiriamali wakiwepo wamachinga wadogo.
·         Kuwapa elimu
·         Kuwathamini wafanyabiashara sekta muhimu katika kukuza uchumi wa Moshi.

(ii) Kuendelea kuviwezesha vikundi vya vijana na kinamama kwa kutumia fedha za mfuko wa  vijana na kina mama.


(iv) Kuendelea kuhamasisha uanzishwaji wa vikundi vya vikoba na saccos na kuimarisha       vilivyopo.

(v) Kuendelea kusukuma Serikali Kuu ili kufufua viwanda vilivyo binafsishwa kwa ajili ya kutoa ajira kwa wananchi wa Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.

(vii) Kuendelea kujenga mazingira rafiki na mahusiano mazuri na sekta binafsi ili kusukuma na kuharakisha uwekezaji katika mji wa Moshi kwa ajili ya kuongeza ajira. (Service levy)

(viii) Kulinda na kusimamia matumizi sahihi ya rasilmali za halmashauri ikiwepo kutafuta wawekezaji katika maeneo ya Halmashauri ya Manispaa ya Moshi.

(xi)  Kuendelea kuongeza mapato ya Halmashauri mwaka hadi mwaka kwa kuboresha mfumo wa takwimu za ukusanyaji wa mapato. (Data base)
(B)UTALII:
(i) Kuangalia uwezekano wa kuongeza vivutio vya watalii katika Manispaa ya Moshi ikiwepo kuendeleza mazungumzo na Wizara ya Mali Asili na Utalii ya kuingia ubia na Manispaa ya Moshi ya kuboresha msitu RAU.

(ii)  Kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika hoteli za kitalii za nyota tatu mpaka tano ili kuongeza idadi ya watalii wanaolala katika mji wa Moshi.

(iii) Kuendelea kusukuma uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Moshi (Moshi Airport) uweze kufanya kazi kwa ufanisi .

(iv) Tutaendelea kutetea maslahi ya wapagazi na kushirikiana na vyama vyao.

(C) MCHAKATO WA MANISPAA YA MOSHI KUWA JIJI LA MOSHI.
Kuendelea kumshawishi Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atoe tamko la Moshi kuwa jiji baada ya kukamilisha mchakato wote kwa mujibu wa sheria.

(D)KILIMO:
 kuendelea kuboresha kilimo cha mjini (Urban agriculture) kwa kuimarisha kilimo cha kisasa katika ukanda wetu wa kilimo ndani ya Manispaa ya Moshi ikiwa ni pamoja na uvuvi na ufugaji.

(E) MASOKO:
 Kusimamia uboreshaji masoko ya manispaa ili yafanye kazi kwa ufanisi.

(7) MICHEZO:
(a) Kuendelea kuimarisha viwanja vya michezo katika Manispaa ya Moshi.

(b)  Kuimarisha ushindani wa wanamichezo katika Kata za manispaa ya Moshi ili kuibua vipaji mbalimbali katika michezo ya aina tofauti.

(c) Kuhamasisha wadau mbalimbali kuchangia timu za michezo tofauti katika Manispaa ya Moshi ili kupata timu za michezo mbalimbali zitakazowakilisha manispaa katika michezo ya kitaifa.

(d) Halmashauri ya Manispaa ya Moshi itaandaa sera za michezo inayooanisha michezo na uchumi na michezo na ajira ili kuondoa dhana kuwa michezo ni burudani tu.

(8) MAZINGIRA:
(a) Kuhamasisha upandaji wa miti katika maeneo mbalimbali ya Manispaa.

(b) Kutunza vyanzo vya maji.

(c) Kuendeleza usafi wa mji wa Moshi;

 (i)Kutoa elimu kwa wananchi wa Moshi

 (ii) Kuhamasisha watu kutenga takataka katika vyanzo (separation at source)
(iii) Kufanya takataka kuwa rasilimali na sio uchafu hivyo kuzalisha ajira.
(iv) Kutengeneza gesi asilia (Bio gas) na  mbolea ya mboji
(v)  Kuongeza vitendea kazi kama magari na vinginevyo.
(vi) Uboreshaji wa dampo kuu (land field).

(9) ARDHI NA MIPANGO MIJI:
(a) Upimaji wa maeneo ya makazi kwa kuondoa ujenzi holela.

(b) Kupima maeneo ya halmashauri ya manispaa ya Moshi  kwa ajili ya kupata hatimiliki.

(c) Kusimamia ujenzi unaoendelea na mpango kabambe wa uendelezaji wa mji wa Moshi (Master plan) ya mwaka 2001)

(d) Kuzuia uvamizi wa maeneo ya wazi

(e) Kutengeneza na kusimamia mpango kabambe wa miaka kumi na tano wa kuendeleza mji wa Moshi, utahusisha Kata za Majengo, Bomambuzi, Korongoni, Kiusa,Mawenzi na Bondeni.

(f) Kukabiliana na migogoro ya ardhi inayosababishwa na idara ya ardhi ikiwepo kugawa kiwanja kimoja zaidi ya mtu mmoja.

(g) Kusukuma upatikanaji wa hati miliki kwa wakati.

 MWISHO .