Polisi inawashikilia "WanaCHADEMA" 10Katika hatua nyingine Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Camilius Wambura, jana alilithibitishia Nipashe kuwa wamewakamata vijana 10 wanaodaiwa kuwa ni wanachama Chadema huku wakiwatawanya wengine zaidi ya 100 baada ya kuandamana bila kibali maeno ya Moroco jijini Dar es Salaam wakimtaka Dk. Slaa asiondoke katika chama hicho.

“Ilikuwa majira ya saa saba mchana tulipopata taarifa kuwapo kwa kundi la watu katika eneo la Morocco waliokuwa wakitokea maeneo ya barabara ya Mwai Kibaki na Ali Hassan Mwinyi wakielekea Magomeni ndipo tulipowatawanya lakini walikaidi amri hivyo tukalazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya,”alisema.

Alisema baada ya saa moja walipokea taarifa kuwapo kwa kundi la vijana hao katika ofsi za makao makuu ya Chadema Kinondoni na kulazimika kwenda na walipofika walikuta baadhi ya vijana wamekamatwa na makamanda wa chama hicho.


Karatasi za kupigia kura kuletwa kutoka Afrika Kusini

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema asilimia kubwa ya maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu yamekamilika, huku karatasi za kupigia kura zikitokea Afrika Kusini.

Aidha, tume hiyo imesema gharama za awali kwa ajili ya ununuzi wa vifaa mbalimbali kama vile wino, fulana, kofia, karatasi za kura, vibanda vya kupigia kura na vifaa vya kufungashia katika uchaguzi huo hadi sasa zimefikia Sh. bilioni 31.25.

Imesema dola za Marekani 6, 145, 882.92 sawa na Sh. bilioni 13.1 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya ununuzi karatasi hizo za kura. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Manunuzi na Menejimenti ya Lojistiki wa Nec, Eliud Njaila, wakati akizungumza na Nipashe, jijini Dar es Salaam jana.

Alisema karatasi hizo zinatarajia kuanza kuwasili nchini Septemba 29 hadi Oktoba 15, mwaka huu.

Alisema gharama za vifaa hivyo ni tofauti na zile zilizotumiwa na tume hiyo kwa ajili ya kununulia mashine 8,000 za Biometric Voters Registration (BVR) na shughuli nzima ya uandikishaji kwenye Daftari la Wapigakura nchi nzima, ambazo kwa mujibu wa Nec ni Sh. bilioni 133.

Tume hiyo pia ilisema Sh. bilioni 85 zilitumika kulipa posho waandikishaji, wataalamu wa mashine hizo, kutengeneza kadi, karatasi, wino na vifaa muhimu wakati wa uandikishji kwenye daftari hilo nchini kote. Alitaja kampuni iliyoshinda zabuni ya wazi ya kutengeneza karatasi hizo kuwa ni Uniprint ya nchini Afrika Kusini ambayo alisema ina uzoefu mkubwa katika kazi hiyo kwani ndiyo iliyoshinda zabuni ya kutengeneza vifaa hivyo katika uchaguzi mkuu nchini humo wa Tanzania wa mwaka 2005.

Iwe ametumiwa au amejituma: Hoja zake za uongo kwa nini na kama kweli zinatuathirije?

JUZI, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Dk. Wilbrod Slaa, alijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya takriban mwezi mmoja hivi wa ukimya, na kuibuka na zile alizodai kuwa ni vielelezo (ushahidi) juu ya tuhuma mbalimbali zinazomkabili Edward Lowassa.

Katika mtindo ule ule uliozoeleka wakati akiwa Mbunge wa Karatu, Dk. Slaa alizungumza kwa ufasaha na kwa kujiamini huku akisapotiwa na nyaraka zake mwenyewe za kuthibitisha tuhuma hizo dhidi ya mgombea urais wa Ukawa.

Aliyoyazungumza si mageni sana masikioni mwa Watanzania wengi, ila ni msisitizo tu wa kile kilichokuwa kikidaiwa cha kutokuwapo ushahidi wa tuhuma kadhaa zilizokuwa zikielekezwa kwa Lowassa zinazoweza kusababisha kushitakiwa kwake au kumpotezea sifa za kuwa Rais bora wa Tanzania.

Kwa mwanasiasa aliyedumu kwa zaidi ya miaka 10 kwenye nafasi ya Katibu Mkuu wa chama kikubwa kama Chadema, anayeheshimika ndani na nje ya nchi, kusimama hadharani na kuzungumza mambo mazito kama hayo, haistahili kumpuuza hata kidogo.

Iwe ametumika, ametumiwa au amejituma bado hoja zake zinapaswa kuchukuliwa kwa tahadhari nzito na kuzijadili kwa kina ili kupata majawabu sahihi kwa kuwa yeye si Mtanzania wa kawaida sana kwani amekuwa kwenye uongozi wa juu ndani ya siasa kwa miaka mingi sana na kwa vyovyote vile kuna anayoyafahamu.

Hatutaki kuamini hata kidogo kwamba chuki binafsi kati ya watu hawa wawili, Dk. Slaa na Lowassa, ni miongoni mwa mambo yaliyomsukuma kuzungumza kama alivyozungumza juzi au uchu wa madaraka na ukubwa ndio uliosababisha hayo yote kuwekwa hadharani.

Hoja ni je, yana ukweli kiasi gani? Kama ni ya uongo, ni kwa nini aliyatoa hadharani? Kwa nini asishitakiwe kwa kuhatarisha amani? Na kama yana ukweli, utaathiri vipi mustakabali wa kisiasa na kijamii wa taifa letu?

Haja za Dk. Slaa na maswali haya ndivyo vinavyotufanya kuwataka wahusika (Lowassa na wenzake) watoe majawabu, wajisafishe ili kuondoa shaka mioyoni mwa Watanzania na kudhihirisha uadilifu wao kwa taifa.

Tanzania restarts talks for $800 million of loans to support Shilling


Tanzania will resume discussions for $800 million of loans from international lenders after abandoning an earlier plan as borrowing costs increased during the Greek debt crisis, the nation’s finance minister said.

Tanzania has been selling foreign currency -- as much as $10 million a month -- to support the shilling, Saada Mkuya said on Wednesday in the commercial capital, Dar es Salaam. The demand for dollars in East Africa’s second biggest-economy has been stronger than the central bank’s ability to support the local shilling, which hit a record low against the dollar in June.

“We are holding another round of talks with investors in London next week,” Mkuya said. “The delay to secure the loan has caused scarcity of dollars in the market.”

The nation had agreed on $800 million of loans from Rand Merchant Bank and China Development Bank Corp. to underpin its currency and plug the budget shortfall, Joseph Masawe, the Bank of Tanzania’s head of economic research and policy, said in June. A month later, the government shelved plans for $600 million in credit from South Africa-based Rand Merchant.
High Rates

Tanzania postponed the plans after other African nations borrowed at “very high rates driven by the Greece situation,” Mkuya said. She didn’t specify whether next week’s talks will be with the two lenders.

The country’s net international reserves stood at $4 billion in June, down from $4.2 billion a year earlier, according to central bank data.

The shilling has weakened 19 percent against the dollar this year and is the worst-performer in Africa after Zambia’s kwacha, Uganda’s shilling and Madagascar’s ariary, according to data compiled by Bloomberg. It traded unchanged at 2,150 against the dollar on Thursday.

Inflation may maintain its upward trend if the shilling keeps declining against the dollar, said Mkuya. The inflation rate rose to 6.4 percent in July compared with 4 percent at the start of the year, while the shilling has lost about a fifth of its value since then.

“There is imported inflation,” she said. “If we go on like this, in the long run, unfortunately, inflation will increase.”

Some investors are nervous about next month’s presidential and parliamentary elections, Mkuya said, without elaborating. President Jakaya Kikwete is stepping down after serving for a maximum of a decade.

“While we are lucky to always hold elections peacefully, we are seeing most investors holding back during this time,” she said.

Serikali inachofanya Mtanzania anaporudishwa (deported)


Nitaunda tume kushughulikia matatizo ya wakulima na wafugaji - Lowassa


Docstoc is closing


If you have any documents stored/shared at Docstoc, you may want to download a copy before the end of November this year as per the notice sent out by the company (see below)...
Docstoc : Service Discontinuation Notice
Hi nukta77,
Thank you for being a valued Docstoc.com free account user. We regret to inform you that Docstoc will be closing down effective December 1, 2015. At that time, we will automatically be closing all accounts.
If applicable to your account, please make sure to visit the site no later thanNovember 30th, 2015 to retrieve copies of any documents you previously uploaded to your account.
If you have any questions between now and November 30th, please email us at [email protected].
The Docstoc Team
(DLUL)

Wazungumza na AzamTv: Prof. Lipumba; Dk Slaa9 Best scientific tips on how to study and pass exams


Maelezo ya Sumaye kuhusu 'bomu' la uuzaji nyumba za Serikali


Rostam Aziz atoa taarifa kuhusu tuhuma za Dk Slaa kwake


Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz, amemvaa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akimuita kuwa ni mtu mwongo, mbinafsi na mpotoshaji mkubwa.

Rostam alieleza hayo katika taarifa yake jana kwa vyombo vya habari kuhusiana na tuhuma zilizotolewa na Dk. Slaa dhidi yake jijini Dar es Salaam juzi, alipozungumza na vyombo vya habari kuelezea mambo kadhaa zikiwamo sababu za kujiondoa ndani ya Chadema.

Dk. Slaa alidai kuwa mwaka 2009 baada ya kutaja orodha ya mafisadi 11 nchini katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwembeyanga, Dar es Salaam, Rostam alimpigia simu na kumtishia maisha.

Dk. Slaa pia alidai juzi katika mkutano wake na vyombo vya habari uliorushwa na vituo vitatu vya runinga kuwa Rostam anaifadhili Chadema.

Katika taarifa yake jana, Rostam alisema: “Nilimsikiliza Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Willibrod Slaa jana (juzi) alipokuwa akizungumza katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
“Kwa mara nyingine kama ilivyo hulka yake miaka yote, Dk. Slaa kathibitisha pasipo na shaka kwamba yeye ni mbinafsi na mpotoshaji mkubwa.”
“Nimesikitishwa na kushtushwa japo sikushangazwa hata kidogo na hatua ya Slaa ambaye sasa anaonekana kukubuhu kwa uzushi kutoa matamshi ya namna hiyo.
Sijapata hata mara moja kuwa na mawasiliano na Dk Slaa wakati wowote. Madai yake kwamba eti nilimtisha ni ya kupuuzwa na yasiyo na msingi hata kidogo,” 
Rostam alieleza kuwa ni jambo lisiloingia akilini hata kidogo kwa watu wanaomfahamu Slaa kwamba anaweza kumtishia maisha na yeye akakaa kimya bila kuchukua hatua ya kwenda polisi na kumshitaki halafu anakaa na jambo hilo kwa miaka yote hadi juzi ndipo alisema hadharani.
“Ili kuthibitisha madai yake hayo, namtaka Dk. Slaa kujitokeza hadharani na kutoa ushahidi wa jambo hilo”
Huu ni uongo mwingine wa dhahiri. Namtaka Dk. Slaa kutoa ushahidi pia katika madai yake haya.
“Ni huyu huyu Dk. Slaa ambaye mwaka 2010 alizusha kwamba eti mimi, tukiwa na Rais Jakaya Kikwete na Edward Lowassa tulikutana katika hoteli ya La Kairo, Mwanza na kupanga njama za kumuibia kura zake za urais,” alisema na kuongeza:
“Wakati Slaa akitoa madai hayo ya uongo, mimi nilithibitisha kwamba wakati huo nilikuwa Afrika Kusini na Rais Kikwete akiwa Lindi huku Lowassa akiwa Arusha. Ni wazi kwamba tusingeweza kukutana La Kairo kama alivyodai yeye.”
Kwa mujibu wa Rostam, Dk. Slaa kuna wakati alimzushia hadi Rais Kikwete alipodai kwamba alisafiri kwa usiku mmoja kwenda China kumtoa mwanaye aliyekuwa amekamatwa na vyombo vya usalama, kisha kurejea Dar es Salaam usiku huo.
“Ni Slaa huyu huyu ambaye mwaka 2010 wakati wa kampeni alifikia hatua ya kuutangazia umma wa Watanzania kwamba kulikuwa na malori yaliyobeba kura za CCM ambazo zingesaidia ushindi wa wizi yaliyokamatwa Tunduma. Malori hayo yalipokaguliwa yalibainika kuwa na mizigo ya kawaida,” 
aliongeza katika taarifa hiyo.

Tanzania huenda ikawa mzalishaji namba 1 wa graphite duniani


Maoni ya Askofu Kilaini kuhusu tuhuma za Dk Slaa dhidi yao


Maoni ya Prof. Mbele kuhusu aliyosema Dk Slaa

Hotuba ya Dr. Wilbroad Slaa Kuacha Siasa


Kuhusu hotuba ya Dr. Slaa kwa waandishi wa habari akitangaza kuondokana na siasa, mengi muhimu yamesemwa na wenye upeo na tafakari nzito kunizidi. Ila nami kama raia mwingine yeyote, nina uhuru kamili wa kuongelea suala hili, kama mwananchi anavyoongea mtaani, ambayo ni haki yake.

Napenda nianze kwa kujikumbusha kwamba kwa miaka mingi, CCM wamekuwa wakimbeza Dr. Slaa, kwamba ni mzushi na mropokaji. Alipoanza kusema kuna ufisadi, CCM walimkatalia katakata, wakasema ni mzushi. Baadaye, vijana wa UVCCM wakawa wanafanya kibarua cha kumtukana Dr. Slaa.

Sasa, baada ya huyu mzushi na mropokaji kutema cheche juzi, mbele ya waandishi wa habari, nasubiri kuwasikia CCM wanasemaje. Wakisema tumpuuze kwa vile ni mzushi na mropokaji, basi ina maana kuwa UKAWA hawana sababu ya kukosa usingizi wala kujibishana naye. Kwa nini mtu ukose usingizi kwa sababu ya maneno ya mtu anayefahamika wazi kuwa ni mzushi na mropokaji?

Nitawashangaa CCM iwapo watashangilia mashambulizi ya Dr. Slaa dhidi ya Lowassa na UKAWA. Nitawashangaa.

Dr. Slaa amewaponda kabisa CCM. Sio tu kwa jinsi alivyoifananisha CCM na choo kichafu, bali kwa kauli yake kwamba serikali ya CCM ni waoga wa kuwachukulia hatua watuhumiwa wa ufisadi. Amesema kuwa CCM ni mfumo unaofuga mafisadi. Sio hivyo tu, bali amewaumbua pia wabunge wa CCM, kwamba hawasomi wanayopaswa kusoma.

Alivyosema hayo kuhusu wabunge wa CCM, nimekubaliana naye kabisa, kwani nami nilishaandika kuhusu wabunge hao nikiwaita mbumbumbu. Ushahidi ulikuwa jinsi walivyotoroka midahalo wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010. Midahalo inaheshimiwa na watu wote wenye akili, lakini mbumbumbu hawaelewi umuhimu wake.

Umbumbumbu wa wabunge wa CCM umejidhihirisha tena na tena kwa tabia yao ya kuzomea Bungeni, na tabia ya kuunga mkono chochote kinachosemwa na serikali ya CCM. Kwa hayo yote, ninaichukulia kwa uzito upasao kauli ya Dr. Slaa kuwa wabunge wa CCM hawasomi.

Dr. Slaa hajawaonea CCM kwa hilo. Nakumbuka ule mwaka Mwalimu Nyerere alipojiandaa kung'atuka uenyekiti wa CCM, alizunguka nchi nzima akikagua uhai wa chama hicho. Inaonekana hakuridhika, kwani kuna siku alisema kuwa wako watu katika CCM ambao hata mtihani kuhusu "Azimio la Arusha" hawawezi kupasi. Kwa hivyo Mwalimu alishabaini umbumbumbu katika CCM tangu miaka ile ya katikati ya themanini na kitu.

Sasa, nikijumlisha hayo yote, nakuta kwamba Dr. Slaa ametuambia kuwa Tanzania inaendeshwa na mbumbumbu wasiosoma. Inaendeshwa na vipofu. Hilo ni janga kwa Taifa. Halafu ukiongezea na lile wazo la kuwa CCM ni kama choo kichafu, unaona wazi kuwa Dr. Slaa amemwaga hadharani mambo mazito dhidi ya CCM.

Sasa katika hali hii, nikiangalia wagombea wawili wa urais, yaani Magufuli na Lowassa, naona kuwa tafsiri ya kauli za Dr. Slaa ni kuwa UKAWA wamemtoa Lowassa chooni, lakini Magufuli ameng'ang'ania kubaki chooni. Ningekuwa mpiga kura, kura yangu ningempa huyu Lowassa aliyelopolewa kutoka chooni kuliko huyu Magufuli ambaye amepania kufia humo chooni.

Diaspora Montgomery County yamuaga Balozi Amina S. Ali


Bwn. Daniel Korona akisherehesha hafla futi ya kumuaga Balozi wa Umoja wa Afrika aliyemaliza muda wake Mhe. Amina Salum Ali iliyoandaliwa na Jumuiya ya Diaspora kutoka Afrika wanaoishi Montgomery county iliyofanyika siku ya Jumatano Sept 2, 2015 Silver Spring, Maryland.
Kulia ni mwongozaji maswali Bi. Soffie Ceesay ambaye ni mwanachama mwanzilishi wa Montgomery County's African Affairs Advisory Group na African Immigrant Caucus akimuuliza Mhe. Amina Salum Ali maswali mbalimbali likiwemo nini anajivunia kwenye uongozi wake kama Balozi wa kwanza wa Umoja wa Afrika nchini Marekani. Balozi Amina Salum Ali alieleza ni ushirikiano wa nyanja mbalimbali mabazo nchi za Afrika zimenufaika na kupata mafanikio na uhusiano wa AU na Marekani kwa kuwezesha kupata Balozi wao nchini Marekani na kikubwa kabisa katika historia ya AU na yeye kama Balozi kuwezesha Rais Barack Obama kwa mara ya kwanza katika historia kama Rais wa Marekani kuhutubia Umoja huo.


Isiah Leggett ambaye ni Montgomery County Executive akimtunukia cheti Mhe. Balozi Amina Salum Ali


Balozi Amina Salum Ali akitoa shukurani zake ambapo leo anaondoka kurudi Tanzania baada ya kumaliza muda wake kama Balozi wa kwanza wa Umoja wa Afrika nchini Marekani kazi aliyoifanya tangia 2006.


Wahudhuriaji


Wageni waalikwa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.

Illicit flow of funds moves thousands of millions of dollars in Africa - Thabo Mbeki


PRESS RELEASE

Mbeki is now head of the High-Level Panel on Illicit Financial Flows From Africa created by the United Nations Economic Commission for Africa and the African Union

LUANDA, Angola, September 3, 2015/ -- The continent of Africa loses over 50 thousand million dollars each year as a result of the illicit flow of funds, former president of South Africa Thabo Mbeki told the meeting of the Group of African Governors affiliated with the World Bank and the International Monetary Fund, known as the African Caucus.

"Africa faces the great challenge of large volumes of capital leaving the continent illicitly – money that our continent needs to address the challenges of development. We, as Africans, have an absolute obligation to act on this to ensure that the rest of the world (the destination of these illicit movements of funds), by acting together, will help stop this drain of resources which belong to the continent that needs them so badly," said Thabo Mbeki.

Mbeki is now head of the High-Level Panel on Illicit Financial Flows From Africa created by the United Nations Economic Commission for Africa and the African Union, which did exemplary work and analysed the magnitude of the problem on the continent, producing a report now known as the "Mbeki Report".

The former President of South Africa maintains that it is possible to put an end to these issues with proper monitoring of the transactions of large commercial companies. Moreover, he points out that in order to combat this phenomenon interventions are needed from institutions such as tax authorities, customs, central banks, financial intelligence units for combating money laundering, audit and anti-corruption authorities and the police.

It is clear to Thabo Mbeki that there is also a need for appropriate legislation to give these institutions the mandate they need to cooperate in the fight against illicit capital outflows and so that countries can also cooperate at the regional level, given that some of these outflows move across shared borders.

"Our governments lose large amounts of revenue owed to the state due to the unlawful outflow of significant capital that we need for development," he pointed out.

Thabo Mbeki says that it is imperative to build the global architecture required for a focussed offensive to put an end to these illicit outflows, within the framework of UN processes, in order to avoid a piecemeal approach to the problem and to enable supervision by an appropriate UN body.

SOURCE: Ministry of Finance of Angola

Mtanzania aliyeko Afrika Kusini anawatafuta ndugu zake Tanzania


Exim Bank Korea yaikopesha Serikali $91 mil kwa ujenzi wa Selander bridge

Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali na wajumbe kutoka Benki ya Exim ya Korea baada ya kusaini hati ya mkataba wa makubaliano ya mkopo wa dola za Kimarekani milioni 91.032 zilizotolewa na Benki ya Exim ya Korea kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Selander leo jijini Dar es Salaam. (picha: Eleuteri Mangi-MAELEZO)