[audio, video] Dk Slaa azungumza kwenye StarTv

Magazetini Septemba 5, 2015

Malalamiko ya mabango kuchanwa na la mwania Urais lililoamriwa kushushwa
Katuni za @Kipanya - Ya mwisho ndiyo iliyochapishwa
Vya Lowassa vilivyojadiliwa leo: Picha Kigoma; Video ya mchakamchaka; Utabiri wa Shk. Yahya

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akipokea saluti kutoka kwa Askari Polisi, wakati alipowasili kwa Helkopta, kwenye Uwanja wa Nguruka Kati, Uvinza, Mkoani Kigoma kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo, leo Septemba 4, 2015. (picha imepigwa na Othman Michuzi/Mtaa kwa Mtaa blog - bofya hapa kuona nyingine)Ahadi ya CCM: Serikali kutoa mil.150/= kwa wajasiriamali kila Kata Dar

Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza kwenye Viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es Salaam.

SERIKALI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imepanga kutoa shilingi milioni 150 kwa kila Kata ya Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwawezesha wajasiriamali kimikopo ili kukuza biashara zao. 

Kauli hiyo imetolewa na mgombea mwenza wa CCM katika mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Mbezi Centre jijini Dar es Salaam. 

Alisema ili kuboresha huduma za afya Jimbo la Kibamba Serikali imedhamiria kujenga hospitali kubwa itakayofanya kazi saa 24 pamoja na kuboresha huduma nzima za afya katika hospitali hiyo wakiwemo wataalam. 

Aliongeza kuwa Serikali kupitia mradi mkubwa wa maji safi na salama imepanga kuongeza huduma za usambazazi maji kwenye eneo la Kibamba na kiujumla mradi mzima utakapokamili hali ya upatikanaji maji itapanga kutoka asilimia 65 ya watu hivi sasa hadi kufikia asilimia 95 jambo ambalo litamaliza kero kabisa ya maji Jijini Dar es Salaam. 

Hata hivyo Serikali ya CCM imepanga kuyapima maeneo ya viwanja na kuyakabidhi kwa wananchi jimboni humo ili kuwawezesha wamiliki kuyatumia kama dhamana pamoja na kuwalipa fidia wananchi 8,365 wa Mloganzila ili kupisha uendelezaji wa eneo lililoitajika kwa maendeleo. 

Mgombea mwenza alifanya mikutano yake ya kunadi ilani ya CCM katika Jimbo la Kinondoni maeneo ya Mbezi, Mburahati, Mwananyamala na Msasani (Namanga) jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu kwenye uwanja wa Mbezi Centre Kata ya Mbezi jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu kwenye Viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es Salaam.

Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akiwanadi wagombea udiwani wa Jimbo la Kawe kwenye mkutano wa kampeni ulofanyika kwenye Viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es Salaam


Meya wa Kinondoni, Yusuf Mwenda akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es Salaam.

Hawa Ng'umbi akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Jimbo la Kawe kwenye mkutano wa kampeni ulofanyika kwenye Viwanja vya Barafu Mburahati jijini Dar es Salaam.

Ahueni? Hukumu ya gazeti la MwanaHALISI Mahakama Kuu


Jaji Salavatory Bongole wa Mahakama Kuu ya Tanzania ametoa hukumu na kulipa ushindi gazeti la MwanaHALISI baada ya mahakama hiyo kujiridhisha kuwa Waziri wa Habari na Utamaduni, Dk Fenella Mukangara hakufuata taratibu la kukifungia chombo hicho cha habari.

Wakili wa Kampuni ya Hali Halisi Publisher, Rugemaleza Mashamala amesema ingawa hawajapewa hukumu mkononi lakini kutokana na ushindi waliopewa na mahakama ni halali na wana haki ya kuendelea na uchapishaji.

Hata hivyo alisema ni lazima upande wa serikali waone uamuzi wa kimaandishi uliotolewa ili kujiridhisha na kuendelea na taratibu nyingine. [via gazeti la MWNANCHI]


MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imesema Waziri wa Habari, Dk. Fennela Mkangara hakufuata utaratibu wa kisheria katika kulifungia gazeti la MwanaHALISI Julai 30 miaka mitatu iliyopita.

Jaji Salvatory Bongole amesema Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 aliyoitumia kufungia gazeti hilo lililokuwa linachapishwa kila Jumatano na kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL), inaelekeza kuwa pamoja na hatua nyingine kutaka maelezo ya utetezi kwa mchapishaji.

Katika uamuzi wa shauri lililofunguliwa mara baada ya MwanaHALISI kufungiwa, Jaji Bongole amesema gazeti hilo liko huru kuchapishwa kuanzia sasa.

Jaji huyo amesema pamoja na uamuzi huo, kampuni iliyolalamika imepewa mafao yote iliyoyaomba katika kufungua shauri hilo la mapitio ya uamuzi wa Waziri – prerogative orders.

Miongoni mwa maombi ya faida ni HHPL kulipwa gharama za kesi pamoja na fidia kutokana na hasara iliyopatikana kwa muda wote wa gazti hilo kuwa kifungoni.

Wakati Waziri alipofungia gazeti la MwanaHALISI, alieleza kwamba sababu ni kuandika habari na makala za uchochezi.

Habari hasa iliyoikera serikali hata kujilazimisha kuchukua hatua hiyo katili, ilikuwa ni iliyohusu uchunguzi wa tukio la kutekwa na kuteswa hadi karibu na kifo kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (TMA), Dk. Steven Ulimboka.

Dk. Ulimboka alikumbwa na mkasa huo mnamo Juni 2012 alipotekwa usiku eneo la TAZARA, karibu na viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, ambako aliitwa na mtu aliyemtaja kuwa ni ofisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu, ambaye alikuwa na mawasiliano ya karibu naye kwa saa kadhaa siku chache na usiku huo siku ya tukio.

Daktari huyo aliyekuwa mtumishi wa taasisi ya Marekani nchini, alifika eneo la Tazara akifuatana na daktari mwenzake aitwaye Deo, ambaye mara baada ya tukio hilo, wakati wa alfajiri, alimpigia simu Mhariri wa MwanaHALISI, Jabir Idrissa, kumjulisha kuhusu kutekwa kwa Dk. Ulimboka.

Kufuatia habari za kuachiwa huru kwa MwanaHALISI, Mhariri huyo amesema amefurahishwa na uamuzi wa mahakama ya Tanzania, kwa kuwa umethibitisha kosa la serikali la kujichukulia maamuzi mkononi chini ya kuvunja sheria ilizoahidi kuzilinda.

“Nimefurahi sana kuthibitishiwa kwamba serikali ilikosea katika kufungia gazeti. Uamuzi wa Jaji umesema waziri hakufuata hatua za kisheria alizopaswa kuchukua kabla ya kufungia gazeti, ikiwemo ya kuwapa wamiliki na mhariri nafasi ya kujitetea,” amsema Idrissa.

“Lakini pia uamuzi huu unatakiwa uwe funzo muhimu kwa utawala kwamba hauwezi kudumu na kudumu kwa msisitizo wa kuhifadhi na kufurahia sheria zilizopitwa na wakati ambazo miaka kadhaa nyuma zilishatangazwa kuwa ni sheria kandamizi,” alisema.

Mhariri amesema anawasiliana na mmiliki na mchapishaji wa MwanaHALISI, kampuni ya HHPL, kukamilisha taratibu za kuchapisha toleo la kwanza haraka iwezekanavyo. Gazeti hilo lilikuwa likichapishwa mara moja kwa wiki siku ya Jumatano.

Kwa muda wote ambao gazeti hilo linatumikia kifungo, viongozi waandamizi serikalini, akiwemo rais Jakaya Kikwete, wamekuwa wakitamba kuwa hawatavumilia gazeti linalochapisha habari za uchochezi.

Waziri huyo aliyefungia MwanaHALISI anagombea ubunge katika jimbo la Kibamba, akikabiliana na ushindani mkali wa John Mnyika (Chadema) ambaye ni mwakilishi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Mkurugenzi Mtendaji wa HHPL, Saed Kubenea yeye anagombea ubunge jimbo la Ubungo kupitia Chadema pia akiwakilisha UKAWA. [via MwanaHALISI Online]

How to make a cheese-cake using a mug in a microwave in 5 minutes

See more videos at Hello Lana's channel

Mashehe Watanzania waliotekwa DRC wazungumzia yaliyowasibu


Kilichomlaza Lema rumande jana


Mgombea ubunge jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na UKAWA, Godbless Lema na wenzake wanne wameachiliwa kwa dhamana leo baada ya kushikiliwa na polisi tangu jana.

Polisi mkoani Arusha waliwakamata watuhumiwa hao jana jioni mara baada ya kuzindua kampeni ya kuwania ubunge katika jimbo hilo katika Shule ya Msingi Ngarenaro.

Wakisomewa mashtaka katika mahakama ya Arusha, Lema amedaiwa kulizima gari lake wakati wakitokea kwenye mkutano wa kampeni, hali iliyowafanya wafuasi wake kuanza kulisukuma hivyo kusababisha maandamano pasipo kuwa na kibali cha polisi. Lema na wenzake wameyakana mashtaka dhidi yao. [via Mwananchi]

"Star Tv matatani kwa kumchafua Lowassa"


5 things you have to stop saying if you want to achieve your goal

1. “It’s too late.”

No matter who you are, no matter what you did, no matter where you’ve come from, you can always change and become an improved version of yourself. Peace, strength and understanding will come to you when you manage to tune out the noisy judgments of others, in an effort to better hear the soft and steady hum of your own inner strength. And once you hear it, you will realize that it’s not too late to be what you might have been.

2. “If only I was stronger, smarter, more attractive, etc.”

The absolute worst loneliness is to not be comfortable with yourself. It’s always better to be true to yourself, and risk incurring the ridicule of others, rather than trying to live a lie, only to gradually earn your own self-contempt. Remember, almost everything that happens to you is a direct reflection of what you believe about yourself. You can’t possibly outperform your level of self-esteem. You can’t draw from yourself more than you think you are worth.

3. “What I have to say is not that important.”

Silence makes the inner battle much harder and longer. Speak your truth. Let it out… before it kills you! Honestly, this is one of the saddest things about so many people’s life situation – their most important thoughts and feelings often go unspoken and barely understood.

4. “The less risks I take, the less regrets I will have.”

You miss 100% of the shots you never take. Choices, chances and changes – start making them. You must make a choice to take a chance, or your life will never change. In the end, more so than the mistakes we make along the way, we regret the chances we didn’t take, relationships we were afraid to have, and the decisions we waited too long to make.

5. “I’ll start tomorrow.”

Many great things can be done in a day if you don’t always make that day tomorrow. Don’t let your fear of making a mistake stop you. A life spent making mistakes is not only more enjoyable, but more useful than a life spent waiting around.

Marc and Angel 
Hack Life

Muhtasari wa maamuzi ya NEC kuhusu rufaa za Wabunge na Madiwani


Dk Slaa azungumzia: Kukutana na Mwakyembe; Ulinzi UwT; Picha; Lissu

SIKU moja baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, kutangaza kuachana na siasa na kushusha tuhuma kwa chama chake, maaskofu wa Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), imebainika kuwa kabla ya kuzungumza na waandishi wa habari alikutana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiwamo Dk. Harison Mwakyembe.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Dk. Slaa ambaye alimshambulia mgombea urais wa Chadema chini ya mwamvuli wa Ukawa, Edward Lowassa, alikiri kukutana kwa takribani saa mbili na Dk. Mwakyembe akisema lengo lilikuwa ni kujikumbusha taarifa ya Richmond na ndipo alipopata ujasiri wa kutamka aliyoyasema.

“Hivi kukaa kwangu na Mwakyembe kuna kosa gani? Je, ni dhambi? Watanzania sijui kwanini huwa hawataki kuelewa mambo, mimi nilionana na Mwakyembe kabla ya kuanza mkutano wangu na waandishi wa habari, na tulikaa kuanzia saa nne asubuhi hadi sita mchana.

“Katika suala la Richmond hakuna ‘source ya information’ (chanzo cha habari) zaidi ya Mwakyembe na ndiyo maana nilikaa naye…nilirudia kufanya utafiti.

“Sasa anayeshangaa Dk. Slaa kuongea na Mwakyembe nadhani kwa bahati mbaya akili yake haina upeo wa kutosha, kwa sababu unapofanya ‘research’ (utafiti) lazima urudi kwenye ‘source’ (chanzo) ya hilo jambo na ndiyo maana nilikuwa na jeuri ya kuzungumza kwa kujiamini,” alisema Dk. Slaa.

USALAMA WA TAIFA


Dk. Slaa pia alikiri kusindikizwa na usalama wa taifa akisema alifanya hivyo kwa sababu tangu amejiuzulu ukatibu mkuu wa Chadema, amekuwa akitishwa hivyo alitoa taarifa polisi kwa ajili ya kulindwa.

“Nikiwa pale mkutanoni nilihoji kama polisi wapo ili tu watu wajue kuwa pale kuna usalama, nilisema kabisa kwamba hakuna kipindi nilichopata vitisho kama hiki, kuliko hata wakati nilipotangaza ‘list of shame’ pale Mwembeyanga, hivyo nilitoa taarifa polisi ili nilindwe.

“Tangu nimejiuzulu ukatibu mkuu, nyumba yangu imekuwa ikilindwa na polisi. Polisi ni maadui zetu, lakini kuna wengine ni wazuri kwa ajili ya usalama,” alisema Dk. Slaa.

Kabla ya kufanyika kwa mkutano huo, baadhi ya taarifa zilizokuwa zikizagaa zilidai kuwa umeandaliwa na watu wa CCM na Serikali.

MTANZANIA ilipomuuliza Dk. Slaa kuhusu suala hilo, hakuwa na jibu la moja kwa moja.

GHARAMA ZA MKUTANO [bofya hapa kutizama video]

Alipoulizwa juu ya gharama alizotumia kufanya mkutano wake kwenye Hoteli ya Serena na kuurusha moja kwa moja kwenye vituo takribani vitano vya televisheni, wakati akisema yeye ni masikini, Dk. Slaa alihoji: “Hivi kwa uzito wa hotuba ile ulidhani ningefanyia Manzese?”

Gharama za kurusha matangazo ya moja kwa moja kwenye baadhi ya televisheni nchini, zinaanzia Sh milioni 6 kwa saa na mkutano wa Dk. Slaa ulirushwa kwa takribani saa moja na nusu.

Hivyo gharama za kurusha matangazo hayo kupitia televisheni hizo achilia mbali ukumbi, redio zilizorusha moja kwa moja, luninga mbili zilizorudia matangazo hayo juzi usiku na kampuni iliyoandaa mkutano huo ni takribani Sh milioni 45.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Dk. Slaa alisema yeye si mtu mwenye uwezo na hata fedha zake huwa zinatumiwa na mke wake kukijenga chama, hivyo yeye na familia yake huishi kwa kula mihogo.

Jana MTANZANIA ilipomtaka Dk. Slaa ataje gharama ya mkutano huo na nani amegharamia, alisema: “Bado nasubiri gharama za mkutano wangu na kampuni inayofanya kazi hiyo wakiniletea nitakwambia.

“Niliamua kufanya mkutano ule kwa kuwa Taifa limegawanyika katika sehemu mbili, wengine ni wale wanaounga mkono ufisadi ambapo ndiyo wanatumia fedha kufanya jambo lolote, kundi jingine ni lile ambalo linapinga, na ndiyo maana nikawatahadharisha Watanzania wawe makini na mafisadi,” alisema Dk. Slaa.

PICHA NA LIPUMBA, MWIGULU
Akizungumzia kuhusu picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii akiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba na Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck, alisema picha hiyo ni ya tangu rais huyo alipokuja nchini.

“(Anacheka) Yaani ninawashangaa sana Watanzania…hivi watu tukimbiane? Lakini bahati mbaya picha hiyo ni ya siku nyingi, tangu rais wa Ujerumani alipokuja nchini, na siku ile Mwigulu alikuja kuiwakilisha Serikali, mimi niliwakilisha chama changu na Lipumba aliwakilisha CUF,” alisema Dk. Slaa.

AMJIBU LISSU [bofya hapa kusikiliza]

Pamoja na mambo mengine, alimtaka Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu afanye utafiti kabla ya kuzungumza chochote na vyombo vya habari.

“Lissu amekuwa mtu wa kukurupuka…hivi alijua mimi niko wapi, kwa anachofanya anapoteza ‘credibility’ yake, na mtu makini anafanya tafiti kabla ya kutoa ‘press’. Sasa aende kwenye kumbukumbu ya chama na atoe vocha yoyote iliyosainiwa halafu aniambie kuwa nilichukua mshahara wa chama,” alisema.

Akizungumzia kuhusu nyumba anayoishi, Dk. Slaa alisema alichangiwa na rafiki yake ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hivyo alimtaka Lissu aweke hadharani uthibitisho wowote kama nyumba hiyo ni ya chama.

“Hivi mtu ukichangiwa nyumba ndiyo umelipiwa na chama? Nyumba yangu nilichangiwa na rafiki yangu Mbowe, sasa Lissu aweke hadharani kama nyumba ni ya chama,” alisema.