Moshi Mjini: Kinana, Sendeka wafungua kampeni kwa Uchaguzi Mkuu 2015


Pride FM Reggae Time: Justin KalikaweNi zaidi ya miaka 12 sasa tangu kuondokewa na mwanamuziki mahiri wa Reggae kutoka nchini Tanzania, Justine Kalikawe.

Kwangu ni kumbukumbu “mbichi” ya kuondoka kwake, kwa kuwa alifariki tukiwa kwenye mkakati wa kufufua hamasa na umuhimu wa muziki wa reggae nchini.

Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2003. Mwaka ambao ulikuwa na mambo mengi saana kwangu. Ndio mwaka ambao nikiwa na Dj Fax (wakati huo sote tukiwa 100.5 Times Fm) tulipanga mikakati ya kuwa na kipindi bora zaidi cha reggae jijini Dar (ambako radio hiyo ilikuwa ikisikika).

Na nakumbuka tulipanga kukutana na kushauriana na wadau mbalimbali wa reggae nchini kuhusu namna tunavyoweza kushirikiana kuunyanyua muziki huo uliolenga katika kuelimisha, kuburudisha na kuikomboa akili ya jamii ya wanyonywaji. Ni katika harakati hizo nilipoweza kuonana na kufanya mahojiano na wasanii kama Jah Kimbute, Ras Inno na nikakosa nafasi kuonana na Justine Kalikawe ambaye alikuwa akikosekana kutokana na ratiba yake ya kurekodi. Hivyo nikawa "namvizia" ili kujua muda ambao hashiriki kurekodi nimpate naye aweze kuizungumzia tasnia ya Reggae nchini Tanzania.

Bahati mbaya Justine aliondoka na kwenda nje ya nchi kwa zaiara ya kimuziki na aliporejea hakukaa muda mrefu akakutwa na mauti. Huo ndio ukawa mwisho wa ushiriki wake katika mkakati huo.

Lakini wakati anafariki, nilikuwa likizo Bukoba, hivyo siku hiyohiyo nilipata taarifa zilizonishtua sana, lakini nikazikubali na kuanza mikakati ya kushiriki mazishi yake, jambo ambalo nililifanikisha.

Lakini….

Justin Kalikawe ni nani?
UKAWA Mbarali waungana na ACT-Wazalendo kwa ajili ya Ubunge tu

Wapiga kura huko Mbarali wameamua kuungana na kuunda umoja wao kwa ajili ya kushinda kiti cha Ubunge tu, ili jimbo libaki kwa Modestus Kilufi, mgombea kutoka ACT-Wazalendo.

Wakizindua kampeni zao, wamesema wameamua kufanya hivyo baada ya UKAWA (CHADEMA, CUF, NLD na NCCR-Mageuzi) kushindwa kupata mgombea mmoja anayekubalika na vyama vyote vinavyounda umoja huo.

Kilufi ni nani? Bofya hapa na pia hapa ili usome kwa ufupi taarifa ziliyotangulia kumhusu.

Uzinduzi wa kitabu: Lingala-SwahiliUzinduzi wa Dar Kavasha Club pamoja na uzinduzi wa kitabu cha kujifunza Kilingala unafanyika leo tarehe 05-Sep-2015 kuanzia saa 12 jioni katika ukumbi wa MRC Mikocheni, ukumbi ulio nyuma ya Shopperz Plaza. Uzinduzi huo unasindikizwa na burudani kutoka kwa wana Bana Marquis bendi inayoongozwa na mwanamuziki Tshimanga Kalala Assosa, ambaye pamoja na kuwa ni kati ya wanamuziki waliokuweko katika enzi ya uanzishwaji na ukuaji wa mtindo wa Kavasha, akiwa mwanamuziki wa bendi kama Negro Success, Lipualipua, Orchestra Kamale, na Orchestra Fuka Fuka. 


Uzinduzi huu ulikuwa ufanyike mwezi wa 5 lakini ukaahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku ambapo uzinduzi huo ulipangwa kufanyika.

Kiingilio cha onyesho hili ni BURE. Hakika tukio hili ni la aina yake katika tasnia ya muziki wa dansi.
  • Tumeshirikishwa taarifa hii na John Kitime

Kubenea asema "Dk. Slaa... uvumivu umenishinda. Sitaruhusu..."

Saed Kubenea
Saed Kubenea
Katika taarifa yake kwa Mwanahalisi Online, Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd (HHPL) wachapishaji gazeti la MwanaHALISI, (ambaye amechimba kwa undani sakata la Richmond lililotokea mwaka 2007) amesema: 

NIMEMSIKILIZA kwa makini, Dk. Willibrod Slaa, aliyekuacha Ukatibu mkuu wa Chadema na katibu wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) akizungumza katika mahojiano na kituo cha telebisheni cha Star TV.

Dk. Slaa ambaye ni msomi wa thiolojia, amemtuhumu Mgombea Urais anayewakilisha UKAWA, Edward Lowassa kwamba ni fisadi na hafai kuchaguliwa na wananchi.

Ikiwa ni mara yake ya pili kutokeza hadharani tangu aliposusa kufanya kazi za katibu mkuu katikati ya mwezi Julai mwaka huu, ameeleza kwanza Watanzania wamchague “Mgombea mwenye nafuu ya ufisadi...” akamtaja John Pombe Magufuli.

Kwa taarifa mpya aliyonayo na ambayo aliitumia katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumanne iliyopita, kuhusu sakata la Richmond, aliipata kutoka kwa Dk. Harrison Mwakyembe, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati Teule ya Bunge, juu ya Richmond.

Kubenea amesema ameshindwa kuvumilia taarifa anazozitoa Dk. Slaa kuhusu sakata hilo na sasa ataeleza anachokijua kuhusu sakata la Richmond na msukumo uliopo hata Dk. Slaa kujitokeza wakati huu wa kampeni za uchaguzi katika mlengo wa kumshambulia na kumchafua Lowassa.
“Niliamua kutojibizana na Dk. Slaa – rafiki yangu wa miaka mingi – katika mradi wake huu. Lakini kwa hapa alipofika, uvumivu umenishinda. Sitaruhusu mtu mzima, anayejiita padri na ambaye alitaka kuwa rais wetu, kuendelea kulindanganya taifa na kuwapotosha wananchi.

“Hivyo basi, nimeamua kuanzia leo hii, kukabiliana na Dk. Slaa kwa kila kona ili ukweli ufahamike. Kwa kuanzia, leo hii – Jumamosi, naelekea mkoani Mbeya ambako nitahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara katika jimbo la Kyera, linaloshikiliwa na Mwakyembe, swahiba mpya wa Dk. Slaa.

“Nikiwa Mbeya nitaeleza ukweli wa kilichotokea na kile ambacho Dk. Slaa anakificha.

“Aidha, nikirejea Dar es Salaam, nimepanga kuitisha mkutano na waandishi wa habari, kueleza ukweli uliokamilika kuhusu Dk. Slaa na mkewe Josephine Mushumbuzi na sababu ya yeye kususia chama.”

Picha za Rashid Mwishehe “Kingwendu” aliponadiwa kwa Ubunge Kisarawe


Umati wa watu ukiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Majengo wilayani Bagamoyo.i uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kisarawe mkoa wa Pwani.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed (kulia) akiteta jambo na mgombea wa jimbo la Kisarawe, Rashid Mwishehe “Kingwendu”


Mgombea mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Juma Duni Haji akiwahutubia mamia ya wakazi wa Kisarawe katika mkutano wa kampeni.


Mgombea ubunge jimbo la Kisarawe, Rashid Mwishehe “Kingwendu” akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni.


Juma Duni Haji akimtambulisha mgombea ubunge wa jimbo la Kisarawe, Rashid Mwishehe “Kingwendu” wakati wa mkutano wa kampenzi uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Kisarawe mkoa wa Pwani.

Juma Duni Haji akiwahutubia mamia ya wakazi wa wilayaya Bagamoyo wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Majengo.


Mgombea ubunge jimbo la Kisarawe, Rashid Mwishehe “Kingwendu”
  • Picha: Francis Dande