Faida za mbilimbi


Nilikuwa natafuta jina rasmi la "mbilimbi", haja yangu ikiwa ni kujua endapo mmea huu unafahamika na faida za matumizi yake mwilini. 

Kwetu Tanzania, mbilimbi si geni kwa wakazi wa Pwani kwani hutumika sana katika kutengeneza chachandu/achali na utaikuta kwenye meza za wachuuzi kwa ajili ya kutia ugwadu kwenye mihogo ama viazi vya kukaanga (chips/french fries -- kama ilivyo mabungo, pilipili-chumvi) n.k. na pia hutumika kuungia ladha vyakula mbalimbali.

Huku mtandaoni nimekuta wapo ambao wanakausha na kuhifadhi kwenye paketi na kuuza (bofya hapa kuona Amazon.com au eBay.com), nikajisikitia kuwa ni habati gani mbaya tuliyo nayo kwetu tuna vingi lakini kuvifanyia ujasiriamali kwa juhudi na maarifa tunashindwa. Pengine tusingizie ni tatizo la mfumo na mkazo wa elimu na woga.

Baadhi ya mapishi (recipes) mbalimbali ya mbilimbi yanapatikana katika tovuti ya fruitsinfo.com


Zifuatazo ni baadhi tu ya faida za mbilimbi mwilini (zimenukuliwa kutoka onlyfoods.net):
Health Benefits
Bilimbi offers some of the best health benefits. The fruit is popular worldwide for its sour flavor and is also used as a spice in cooking some of the delicious seasonal dishes.
 • It is capable enough for eliminating phlegm and reducing heat from the body.
 • It has anti-inflammatory properties.
 • It is advised for treating high blood pressure and the treatment is quite effective.
 • For reducing the pain of cavities, cucumber tree is used.
 • The juice extracted from bilimbi fruit is effective in eliminating cough.
 • The fruit is good for treating rheumatism.
 • It is effective in treating acne.
Uses
The tree as well as the fruit is used for several purposes. 
Edible uses
 • The juice of this fruit is tangy and refreshing.
 •  Apart from that, bilimbi is used as a spice in cooking delicious and appetizing curries.
 • It is used instead of mango for preparing chutney and is preserved.
Medicinal uses
Bilimibi tree as well as the fruit is full of medicinal properties.
 • The leaves are applied as a paste on itchy skin.
 • Malayans use the leaves for treating venereal diseases.
 • Leaves are also used for treating cold and cough.
 • Paste of the pickled bilimbi is applied over the body to get rid of fever.
 • A syrup prepared from the fruit helps in getting rid of fever.
 • The fruit also helps in stopping rectal bleeding and eliminating internal hemorrhoids.
Other uses 
 • The wood is frequently used in carpentry. 
 • The fruit juice has high concentration of oxalic acid, useful for bleaching.
Side Effects
Consumption of bilimbi is good for our health but overconsumption can lead to digestion problems.


Flaviana Matata ateuliwa Balozi wa Hiyari wa Utalii Tanzania

Dk Adelhelm James Meru akimkabidhi Flaviana Matata barua ya kuchaguliwa kwake huku kaimu Mkurugenzi Devota Mdachi akishuhudia, katika ofisi za Wizara hiyo.

Mwanamitindo wa Kimataifa anayefanyia kazi zake za nchini Marekani, Flaviana Matata amechagulia na Wizara ya Mali Asili kuwa Balozi wa Hiyari 'Good Will Ambassador' kwa kipindi cha miaka mitatu kwa dhumuni la kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania ndani na nje ya nchi.

Flaviana ambaye juzi alikuwa mmoja kati ya shuhuda wa kushuhudia wizara ya maliasili na utalii wakizindua rasmi tangazo litakalokuwa linatangaza vivutio vya Tanzania nje ya anchi, alitawazwa leo hii na Katibu Mkuu Dk Adelhelm James Meru aliyemkabidhi kwa niaba ya Waziri, Mheshimiwa Lazaro Nyalandu huku Kaimu Mkurugenzi Madam Devota Mdachi akishuhudia.

Kampeni za Lowassa/UKAWA Kibamba, KaweWimbo kwa ajili ya Lowassa kwa Uchaguzi Mkuu 2015

Kampeni za Mbatia/UKAWA Vunjo - Marangu Mtoni


Msafara wa pikipiki ukimsindikiza mgombea Ubunge katika jimbo la Vunjo kupitia chama cha NCCR-Mageuzi na UKAWA, James Mbatia wakati wa kwenda kufanya uzinduzi wa kampeni katika jimbo hilo.
Msururu wa magari ukimsindikiza mgombea huyo.


Maeneo mbalimbali aliyopita mgombea huyo alipokelewa na makundi mbalimbali ya watu waliokuwa wamesimama kando ya barabara wengi wao wakiwa ni kina mama.


Katika maeneo mengine wananchi walisimamisha msafara wake na kusalimia kwa muda kabla ya kuendelea na safari.


Shughuli zilisimama kwa muda katika maeneo mbalimbali angalao kutoa nafasi japo kupunga mkono kwa mgombea huyo.


Msafara ukielekea uwanja wa michezo wa Chuo cha Ualimu cha Marangu kwa ajili ya uzinduzi wa mkutano wa kampeni.


Makondakta na madereva wa daladala katika eneo la Marangu Mtoni wakisalimiana na mgombea ubunge katika jimbo la Vunjo, James Mbatia.
Hii ndivyo ilivyokuwa katika eneo la Marangu Mtoni.


Raia wa kigeni wakichukua taswira za mgombea Ubunge katika jimbo la Vunjo, James Mbatia.
Mgombea Ubunge katika jimbo la Vunjo, James Mbatia akiwa ameongozana na mkewe, Catherine Mbatia na mototo wao Chelsea wakiingia katika uwanja wa michezo wa Chuo cha Ualimu Marangu kwa ajili ya mkutano wa ufunguzi rasmi wa kampeni.
 • Tumeshirikishwa na Dixon Busagaga / (0755 659929) 

[video] Kubenea amzungumzia Dk Slaa mkutanoni Kyela, Mbeya


Taarifa ya NEC kuhusu ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi 2015


KTAARIFA KWA UMMA

KUHUSU VYAMA NA WAGOMBEA KUZINGATIA MAADILI YA UCHAGUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI YA MWAKA 2015

Kama mnavyofahamu Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani zimeanza tangu tarehe 22 Agosti, 2015 na zinaendelea hadi tarehe 24 Oktoba, 2015.
Ni jambo linaloeleweka kwamba mchakato wa Kampeni na wa Upigaji Kura unatawaliwa au kuongozwa na Sheria, Katiba na Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015.
Katika kipindi hiki tangu Kampeni zianze, nafurahi kusema kwa niaba ya Tume kuwa kwa ujumla, Kampeni zimeenda vizuri.  Karibu mikutano yote imefanyika katika hali ya utulivu na amani. Hatujapata taarifa ya mkutano wa Kampeni ambao umevurugwa kwa fujo zozote.  Kwa hilo napongeza Vyama vyote vya Siasa.
Hata hivyo, kutokana na mikutano hiyo nchini ya Kampeni, ngazi ya Urais, Ubunge na Udiwani yamejitokeza mambo ambayo ni kinyume kabisa na Mwongozo wa Maadili ya Uchaguzi wa Rais Wabunge na Madiwani wa mwaka 2015 uliotiwa saini na Vyama vyote vya Siasa tarehe 27 Julai, 2015.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yamejitokeza katika Kampeni hizo:-
(i)           Kutozingatia muda wa kumaliza Mikutano ya Kampeni
Kuna baadhi ya Vyama ambavyo katika mikutano yao vimekiuka Kipengele hiki kwa kufanya mikutano zaidi ya saa 12.00 jioni.  Kuendelea kufanya Mkutano wa Kampeni zaidi ya muda huo ni ukiukwaji wa Kipengele cha 2.1 (c) cha Maadili ya Uchaguzi  wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 kinafafanua kuwa Mikutano yote ya Kampeni itafanyika kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
(ii)        Kubandika mabango ya Kampeni, matangazo au Mchoro wowote kwenye maeneo yasiyoruhusiwa au bila idhini ya wahusika
Baadhi ya Vyama vimeanza kubandika mabango, michoro na picha za Wagombea wao katika majengo au vyombo vya usafiri vya watu binafsi au Taasisi mbalimbali bila idhini ya wamiliki husika.
Napenda kuwakumbusha kuwa, kwa mujibu wa Kipengele cha 2.2. (g) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, hairuhusiwi kufanya hayo bila idhini ya wamiliki husika.
(iii)      Kuchafua, kubandua au kuharibu matangazo au picha za Kampeni za Vyama vingine
Tume imeanza kupokea malalamiko kutoka baadhi ya Vyama kuwa, mabango au picha za Kampeni za Vyama vyao yanabanduliwa au kuchafuliwa na wafuasi wa Vyama vingine.
Ni vema Vyama vya Siasa na Wagombea wakumbuke kuwa Kipengele cha 2.2 (f) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, kinapiga marufuku Chama kingine kuchafua, kubandua au kuharibu matangazo au picha za Kampeni za Vyama vingine.
(iv)       Matumizi ya lugha zisizo za staha
Tume imepokea malalamiko kuwa, katika Mikutano mbalimbali ya Kampeni katika ngazi zote, kumeanza kujitokeza baadhi ya viongozi wa Vyama, Wagombea au wafuasi wao kutumia lugha zisizo za staha wakati wa Mikutano ya Kampeni katika ngazi mbalimbali.
Lugha zisizo za staha zinajumuisha matusi, kejeli, kashfa n.k.  Kipengele cha 2.2 (b) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015, kinakataza Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wagombea wao kutumia lugha zisizo za staha katika harakati zote za Kampeni hadi upigaji Kura.  
Wajibu wa Vyama vya Siasa na Wagombea
Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wagombea wana wajibu wa Kisheria wa kuyaheshimu, kuyasimamia na kuyatekeleza Maadili hayo kwa mujibu wa Kipengele cha 2.1. (b) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015. Viongozi wa Vyama vya Siasa na Wagombea wana jukumu la kuwaelimisha, kuwahamasisha na kuwasisitiza wanachama wao kutekeleza Sheria ya Uchaguzi (ikumbukwe kuwa Maadili ya Uchaguzi yametungwa chini ya Kifungu cha 124A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343)
Adhabu za ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi
Napenda kuwakumbusha Vyama vya Siasa na Wagombea kuwa, ukiukwaji wa aina yoyote wa Maadili unaweza kusababisha Chama au mgombea kupewa adhabu kama zilivyoainishwa katikaKipengele cha 5.10 (a-f). Adhabu hizo ni pamoja na:
1.    Chama au Mgombea aliyekiuka maadili kuelekezwa kuomba msamaha hadharani.
2.    Kupewa onyo au karipio.
3.    Kumtangaza kupitia vyombo mbalimbali vya habari na taarifa kwa Umma mgombea au Chama kilichokiuka Maadili.
4.    Chama au Mgombea kusimamishwa kuendelea kufanya Kampeni.
5.    Chama au Mgombea kuzuiliwa kutumia vyombo vya habari.
6.    Chama au Mgombea kulipa faini kuanzia kiwango cha 100,000/- 500,000/- na 1,000,000/- kutegemea ngazi ya Kamati husika.
Katika kipindi hiki cha Kampeni, Chama au Mgombea akipewa mojawapo ya adhabu hiyo kunaweza kuathiri Kampeni zake za kuelekea Uchaguzi wa Rais, Wabunge au Madiwani.
Hitimisho.
Napenda kunukuu Kipengele cha 1.4 cha Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 ili kila Chama kione umuhimu wa kuwahimiza wagombea na wanachama wao kuzingatia Maadili katika harakati zao za kujinadi. Nanukuu:
“[……] kila mgombea atajaza Fomu Na. 10 kuthibitisha kuwa ataheshimu na kutekeleza Maadili ya Uchaguzi. [….] Mgombea atakayekataa kusaini Maadili haya atakataliwa au kuondolewa kushiriki katika Uchaguzi kama Mgombea.”
Maana yake ni kwamba kila Chama, Mgombea na Wanachama kwa ujumla wana wajibu kuheshimu taratibu zote za Kampeni hadi kupiga Kura.
Yote yaliyokatazwa katika Maadili yazingatiwe na Vyama vyote.  Kama nilivyosema hapo awali Tume imepata malalamiko kuwa baadhi ya Vyama na Wagombea wamekiuka Maadili ama kwa kuzidisha muda wa Kampeni, au kuchana na kuharibu mabango, au kutumia lugha chafu isiyo na staha; Haya yote Tume inakemea kwa nguvu sana na kusihi Vyama vyote na Wanachama wao wote kuheshimiana, waeleze sera zao bila kukashifiana.
Lengo na matumaini ya Tume ni kuwa na Kampeni za utulivu na hatimaye wananchi kuwa na hali ya utulivu na amani ili Uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu.  Kwenye hali ya utulivu na amani wananchi wataweza kupiga Kura ya utulivu ili kuamua viongozi wanaowataka.  Hiyo ndiyo Demokrasia.
Nimalizie kwa kuwakumbusha Vyama vyote kuzingatia Maadili ya 2015.  Tume isilazimishwe kuchukua hatua za kutoaadhabu kwa Vyama na Wagombea.  Busara itumike katika mikutano yote ya Kampeni.
Inawezekana, wote tukidhamiria, “Play your Part”.
Jaji (Mst.) Damian Z. Lubuva
MWENYEKITI

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

Gwajima: Nitafanya mkutano kwa saa moja tu

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ameibuka na kusema atafafanua kila kitu kwa umma kuhusu madai yaliyotolewa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, dhidi yake wakati atakapozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaa kesho.

Amesema moja ya ufafanuzi atakaotoa ni kuhusiana na kubatizwa jina la mshenga na Dk. Slaa wiki iliyopita.

Dk. Slaa alitoa kauli ya kumuita Askofu Gwajima kuwa mshenga Jumanne iliyopita wakati akizungumza na waandishi wa habari, akidai ndiye aliyekuwa amepewa kazi ya kuwaunganisha kati yake na mgombea urais aliyesimamishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chadema, Edward Lowassa.

Gwajima alisema atazungumza na waandishi wa habari kesho kwenye hoteli ya Landmark wakati wa ibada iliyofanyika kwenye kanisa la zamani la Ufufuo na Uzima lililopo Ubungo Maji, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni wiki yake ya pili tangu alipohamia kwenye kanisa hilo baada ya kuhama kutoka viwanja vya Tanganyika Packers alikokuwa akitoa huduma hiyo.

Alisema kwenye mkutano wake na vyombo vya habari atafafanua kuitwa mshenga, jambo ambalo asingeweza kuzungumza kwenye nyumba ya ibada.

“Najua hapa kuna waandishi wa habari wamekuja kujua nilivyokuwa mshenga, lakini kanisa langu siyo sehemu ya majibizano, bali nitafanya mkutano kwa saa moja tu inatosha kabisa kufafanua," alisema.

“Wakati nakuja kanisani nilipofika hapa maeneo ya Ubungo kwenye stendi za daladala, watu waliibuka na kuanza kupiga kelele wakiniita mshenga, mshenga, sasa hii ni ishara tosha, maana ndoa bila mshenga haiwezi kuwa ndoa na mshenga ndiyo mwenye jukumu la kuunganisha kuwa kitu kimoja na ikitokea kuna ugomvi ndiye anayesuluhisha,” alisema na kuongeza:

“Lakini niwaeleze kitu, si mnakumbuka yule Dokta Willibrod Slaa, aliyekuja kupiga magoti hapa mbele ya madhabahu ya kanisa hili Januari Mosi, mwaka huu?" Alisema na waumini wakashangalia huku wakipiga kelele na kusema "sema babaaaaa.”

Alisema mwanzoni mwa Januari, mwaka huu, kanisa hilo lilifunga siku 30 kwa ajili ya kutafuta kiongozi wa kuongoza nchi na kuwaeleza waumini wake kuwa kiongozi atakayeapishwa mwaka huu kuwa Rais, atakuwa pamoja nao kwa kuwa walifunga na kuomba, hivyo atakuwa amechaguliwa na Mungu.

“Hivi mlishawahi kuona mtu anasimama kwenye vyombo vya habari na kusema mambo haya, ukiona dalili kama hizi ujue kwamba ndiyo tayari wameshakwisha," alisema.

Sheria mpya ya makosa ya mtandao mwisho Chumbe?


Wanadiaspora wameelezea wasiwasi wao kuwa sheria mpya ya Makosa ya Mtandao iliyoanza kufanya kazi tarehe mosi mwezi huu nchini Tanzania, huenda ikaishia Chumbe.

Hayo yamekuja kwenye kongamano maalumu lililoandaliwa na Jumuiya ya Wazanzibari Waishio nchini Marekani (ZADIA) kujadili Sheria Mpya ya Makosa ya Mtandao na athari zake kisiasa.

Wageni rasmi katika kongamano hilo lililofanyika kwa njia ya simu walikuwa ni Mwandishi habari Bi Salma Said, na Mwanadiplomasia mstaafu Bw. Muhammed Yussuf Mshamba.

Utata wa kisheria

Akizungumza kwenye kongamano hilo, Bi Salma Said alisema kuwa sheria hii itakuwa na utata kutokana na jinsi ya mchakato mzima wa kuipitisha ulivyokwenda. "Sheria imepitishwa kimabavu, kwani wadau wote hawakushirikiswa, pia ilipitishwa wakati Wabunge wa upinzani wakiwa wametoka Bungeni" alifafanua Bi Salma na kuongeza kuwa Baraza la Wahariri Tanzania liliikataa sheria hiyo na kupitisha azimio la kumshauri rais Kikwete asiitie saini, lakini Mheshimiwa rais aliitia saini.

Kwa upande wake, Bwana Muhammed Yussuf Mshamba ambaye pia ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alielezea wasiwasi wake juu ya uwezekano wa sheria hiyo kutekelezeka kwa vile mfumo uliotumika kuiptisha haukukidhi haja.

Akizungumza katika kongamano hilo, Bwana Mshamba ambaye aliwahi kuwa mtia nia wa kuwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM alisema "Sheria ile ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini Zanzibar hawakupata nafasi ya kuiangalia".

"Kwa mujibu wa kifungu cha 234 cha Katiba ya Zanzibar, sheria zote zinazopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ambazo zinatakiwa kutumika Zanzibar na Bara, kwa mujibu wa kipengele kile ni lazima Baraza la Wawakilishi la Zanzibar lipewe nafasi ya kuziangalia".

Alisema Bwana Mshamba na kuongeza kuwa, sheria ile ilipitishwa wakati Baraza la Wawakilishi limeshavunjwa na hakukuwa na njia ya kuliitisha angalau kwa kikao cha dharura ili kuweza kuijadili.

Kutokana na hali hiyo, Bwana Mshamba alisema kuwa, sheria ile kwa sasa haiwezi kutekelezeka Zanzibar mpaka Baraza jipya la Wawakilishi litakapochaguliwa na kuipitia.

Alielezea sheria hiyo huenda ikapta upinzani katika Baraza jipya kwa vile mambo yaliyomo ndaniyake yana utata. "Tunajua kuwa suala la mawasiliano, ni swala la Muungano, lakini je ni kwa kiasi gani? Je suala la mtandao linaingia?" Alihoji mwanasiasa huyo, na kuongeza "Kwa mujibu nilivyoelewa, sharia ile ina mambo ya faragha, na Wazanzibari wanayo faragha yao, na wana mambo yao wanataka wayashughulikie wenyewe"

Alitoa wito kwa pande zote kukaa tena na kuipitia na kuijadili sheria hiyo ili kweza kukidhi haja ya kisheria na kuweza kutekelezeka bila kuleta madhara.

Kutokana na utata huo wa kisheria, Mwenyekiti wa Jumiya ya Watanzania katika jiji la Dallas, Bwana Ben Kazora, alihoji uwezekano wa kuwakamata washukiwa wa makosa mtandao ikiwa sheria yenyewe haiwezi kutumika Zanzibar.

'Ni sheria zipi zitakazotumika kuwakamata watuhumiwa, za Tanzania, za nchi watuhimiwa walizo au sheria za kimataifa za mtandao?' alihoji Bwana Kazora.

Uwezo wa Kitaaluma

Licha ya serikali ya Tanzania kujipiga kifua kuhusu uwezo wake wa kusimamia sheria mpya ya Makosa ya Mtandao, washiriki katika kongamano hilo walielezea wasiwasi wao kuwa Tanzania ina uwezo mdogo kiteknolojia kuweza kuisimamia na kuitekeleza sheria hiyo kiutaalamu bila kuleta madhara kwa jamii.

Akichangia mada hiyo, mtaalamu wa sayansi ya kompyuta Dk Hassan Omar Ali, alisema kuwa Tanzania ina uwezo mdogo kiteknolojia kuweza kufuatilia kesi za aina hiyo, na hivyo kuna uwezekano wa watu kubambikizwa kesi na wakawa hawana uwezo wa kujitetea.

"Kama mnavyofahamu, mtu unawekwa ndani unaambiwa uchunguzi bado unaendelea, kwa mambo ambayo tayari tunayaweza, uchunguzi unaendelea kwa miaka, sikwambii kwa mambo ambayo hatuyawezi sasa hivi" alitoa changamoto Dk Hassan aliyeandika kitabu cha "Kompyuta: Jifunze na Ielewe"

Msomi huyo aliyewahi kuandika makala maarufu chini ya kichwa cha maneno: "mawasiliano ya mtandao hayana siri", alionya kuwa uwezekano wa mtu kuweza kukamatwa kwa makosa ya kimtandao upo, ispokuwa tu kwa Tanzania uwezo wake wa kiutaalamu na kifedha ni mdogo.

Mbali na hofu ya upungufu wa wataalamu wa masuala ya mtandao, Wanadiaspora pia walielezea wasi wasi wao juu ya upungufu wa wataalamu wa sheria za mitandao nchini Tanzania.

Akitoa hoja katika kongamano hilo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania katika jiji la Dallas Bwana Ben Kazora, alielezea kofu yake kuwa upungufu wa wataalamu wa fani hiyo huenda ukaleta athari mbaya katika utekelezaji wa sheria hiyo.

"Je wataalamu wetu wako tayari kusimamia sheria hii?" Alihoji Bwana Kazora, na kuelezea hofu yake kuwa huenda suala hili likawa limechochewa kisisasa.

Kutumiwa vibaya sheria ya mtandao

Kwa upande mwengine, wazungumzaji katika kongamano hilo walielezea dukuduku lao kuwa sheria ya mtandao huenda ikatumika vibaya kwa malengo ya kisiasa au chuki binafsi.

Akifafanua baadhi ya vipengele vilivyomo katika sheria hiyo, Bi Salma Said ambaye pia ni mwanaharakati za kijamii, alisema kimantiki tunahitaji sheria kama hii kudhibiti matumizi mabaya ya mtandao, isipokuwa yaliyomo ndani yake yana utata.

"Katika ile sheria, kuna kipengele kinasema, polisi akikushuku tu anaweza kukwambia uende ukawasilishe simu yako Polisi, tena si kwa amri ya mahakama, ni yeye tu askari" alilalamika Bi Salma, na kuongeza kuwa, simu itaakapofika polisi haki ya faragha inapotea, kwani hujui ni nini kitakachopekuliwa katika simu yako.

Kutokana na hali hiyo, kuna uwezekano wa polisi kuitumia vibaya sheria hiyo ili kumtia mtu adabu kutokana na chuki binafsi, alionya Bi Salma.

Akijibu swali lililoulizwa kuhusu iwapo Bunge Maalum la Katiba lilitilia maanani masuala ya faragha, enzi za mtandao na kumlinda mwananchi dhidi ya ubabe wa Dola, Bi Salma ambaye alikuwa ni mjumbe wa Bunge hilo alisema "suala la uhuru wa faragha tulilijadili katika Bunge la Katiba, ingawaje hatukwenda ndani kuhusu mambo ya mtandao", na kuongeza kuwa Katiba imeweka wazi haki zote za raia, na haki za uhuru wa faragha zimo kwenye rasimu zote za Tume ya Jaji Warioba.

Kwa upande wake, akijibu swali hilo, Bwana Muhammed Yussuf Mshamba ambaye alikuwa mjumbe wa Tume ya Jaji Warioba iliyokusanya maoni ya wananchi na kuandaa rasimu ya Katiba Mpya alisema "Katiba hata ya sasa inalinda haki zote za kiraia, lakini serikali imekuwa na desturi ya kupitisha sheria zinazokwenda kinyume na Katiba".

Alifafanua kuwa tatizo si Katiba, bali ni vyombo vinavyosimamia na kutelekeza Katiba, na kusisitiza imani yake kuwa Sheria mpya ya Mtandao itapata upinzani mkubwa katika Baraza la Wawakilishi.

Naye Dk Hemed Suleiman, alitahadharisha kuwa sheria hii inairejesha nyuma Tanzania katika masuala ya kidemokrasia na haki za binadamu.

Akitoa maoni yake katika kongamano hilo, Dk Suleiman alisema "Nina wasiwasi kwamba tusipochukua tahadhari, hii sheria huenda ikatumika kidikteta, na itaturudisha nyuma kutoka hatua tuliyofikia kuelekea kwenye demkrasia zaidi, na matokeo yake ni kuibana demokrasia zaidi".

Alitahadharisha dhidi ya uwezekano wa wanasiasa kuitumia vibaya sheria hii kwa ajili ya kuwakandamiza mahasimu zao kisisasa.

Hoja hiyo pia iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tawi la DMV nchini Marekani, Bwana Kalley Pandukizi ambaye alielezea wasiwasi wake kuwa sheria hii inaweza kutumika vibaya na kuwaathiri watu wengi ambao hawana uelewa wa kutosha wa sheria hiyo.

"Wasiwasi wangu ni kuwa hizi sheria zitakapoanza kutumika zitakuja kuwaathiri watu ambao hawahui athari za hiyo sheria" alisema Bwana Pandukizi na kuendelea kuwa, "Ndiyo maana baadhi ya wanasiasa wameingia wasiwasi na hofu kuwa sheria hii huenda ikawa imetengenezwa mahsusi kwa ajili ya kuweza kuwatisha watu, hususan katika harakati hizi za kisiasa zinazoendelea". Aidha mwanasiasa huyo wa CHADEMA alionya kuwa sheria mpya inakwenda kinyume na haki ya uhuru wa vyombo vya habari na watu kujieleza.

Elimu kwa jamii

Licha ya kuikosoa Sheria mpya ya Makosa ya Mtandao, hata hivyo wazungumzaji katika kongamano hilo liloandaliwa na ZADIA, walikubaliana kuwa iko haja ya kuwa na sheria kama hiyo, lakini isiwe imetokana na utashi wa kisiasa. Aidha walisisitiza umuhimu wa sheria kama hiyo kupitia taratibu zote za kimsingi kabla ya kupelekwa Bungeni. Moja kati ya kasoro za sheria hizo ni ukosefu wa elimu kwa wadau wote.

"Kwa kawaida, sharia kabla haijapitishwa hufanyika semina, lakini sidhani kuwa hilo lilifanyika" Alisema Kada wa CCM, Bwana Muhammed Yussuf Msahamba, na kuongeza kuwa ikiwa kweli viongozi wetu walikuwa na nia ya kulinda mila, silka na tamaduni zetu, basi hakukuwa na haja ya sheria kama hiyo kupitishwa kwa hati ya dharuara.

Akijibu swali kuhusu nini Wanadiaspora wanaweza kufanya kuhusiana na sheria hii mpya, Bwana Mshamba alisema kuwa Wanadiaspora wanaweza kutoa mchango mkubwa kwa kusaidia kutoa elimu kwa jamii kwa kupitia njia mbalimbali.

"Mnayo nafasi nzuri ya kuchangia, kwa njia za makongamano kama hili kuzipitia sharia na kuzichambua" alisema bwana Mshamba na kuongeza kuwa Wanadispora wanaweza pia kulinganisha sheria za nchi wanazoishi na kupeleka uzoefu wao nyumbani kwa kushirikiana na Taasisi za kizalendo.

Kwa upande wake, akijibu swali hilo, Bi Salma Said alisema "Elimu ni muhimu. Ni vizuri kuipitia sheria na kutoa taaluma kwa jamii". Akasisitiza kuwa mwamko na uelewa kwa jamii yetu ni mdogo hususan katika masuala ya mitandao ya kijamii na sheria zake.

Kama hujawahi kufanya yafuatayo endelea kuilaumu Serikali

Mmtanzania yupo hivi:

Anamlaumu Lowassa kwa kuhusika na Richmond.

Anamlaumu Kikwete kwa kuumiza uchumi.

Anailaumu CCM kwa kuuvuruga uchumi wa nchi.

Analaumu kila kinachofanyika hata akikohoa analalamikia serikali. Lakini je umetimiza wajibu wako katika kujenga taifa? Wengi wetu tutasema ndio kwa kua tunalipa kodi. Je kodi inatosha kusema unatimiza wajibu?

Uchunguzi mdogo na wa kipuuzi unaonyesha kwamba watumishi wa serikali na kila mmoja wetu anachangia kwa namba moja au nyingine kuumiza nnchi na mwisho wa siku watu wanailalamikia serikali.

Naomba kama hujawahi kufanya yafuatayo endelea kuilaumu serikali kwani kwa mawazo yangu finyu umetimiza wajibu wako:

1. Je umewahi kutoa rushwa?

2. Umewahi kupokea rushwa?

3. Umewahi kukwepa kodi kwa namna yeyote ile?.

4. Je umewahi kushuka sehemu ya mizani ili gar ionekane haijazidi mzigo na ukapandia mbele baada ya kupita mzani?

5. Umewahi kumwibia mwajiri wako ambae ni serikali ya jamuhuri kwa namna yeyote ile? (kuandika safari hewa, kupeleka invoice ya uongo, kupandisha bei ya bidhaa inayonunuliwa na offisi, kuandika mafuta ya uongo. Kuiibia serikali kwa kutolipa unachotakiwa kulipa, na wizi mwingine wowote ule ambao unadhan haikua sawa kuufanya).

6. Je uwapo kazini unatimiza wajibu wako kama inavotakiwa?

7. Ewe Mwalimu ushawahi kumpa supp mtoto wa watu kwa kuwa ulimtaka kingono na akakukataa?

8. Ushawahi kutumia cheo chako kushawishi ndugu yako kuajiliwa hata kama sifa zake hazitoshi?……hapa unasababisha kukata jina la mtu.

Maswali ni mengi sana lakini ishu ni kwamba tusilalamike katika ngazi ya taifa tuanze kujichunguza sisi kwanza ndo twende kwa wengine. Tubadikike sisi kwanza ndo twende kubadilisha kwingine. Tuwe wazalendo kwenye sehemu zetu za kazi.

Jioni njema. Sioti.

Ebube Oluwafemi Onwuchekwa
Mzumbe University.

Kipaji cha kukokotoa hesabu cha binti aliyeishia STD VII


Vyama 22 vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu 2015


Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa nchini imesema kwamba hakuna chama cha siasa chenye usajili wa kudumu au wa muda kinachoitwa Tanzania Peoples Party (TPP) kinachoshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa mujibu wa Sheria ya Vyama Vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992.

Aidha Ofisi hiyo imesema kwamba hivi sasa kuna vyama 22 ndivyo vinavyoshiriki katika uchaguzi huo.

Kauli hiyo imetolewa leo na Msaidizi wa Msajili wa Vyama Vya Siasa, Sisty Nyahoza, wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye ukumbi wa mkutano wa ofisi hiyo jijini Dar e s Salaam kuhusu vyama vyenye usajili wa kudumu ambavyo vinastahili kushiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Nyahoza alifafanua hayo kutokana na kuwepo kwa taarifa katika gazeti moja la habari hapa nchini, ambalo Septemba 4 ,mwaka huu liliripoti kwa kutumia picha na maneno kuhusu chama hicho katika toleo namba 0455 ukurasa wa tatu.

“Chama hiki kilifutwa kwa mujibu wa sheria kwa sababu kilikiuka masharti ya usajili wa vyama vya siasa,” alisema Nyahoza.

Kwa mujibu wa Nyahoza alisema hicho kilifutwa kutokana na sababu ya kukosa kiongozi kwa kuwa sheria hiyo katika kifungu cha 9 kinasema chama cha siasa kiwe na uongozi wa kitaifa.

Hivyo mwaka 2002 kilishindwa kuchagua viongozi wa chama kwa sababu ya kutokuelewana.

Nyahoza aliongeza kwamba chama hicho, awali kilisajiliwa mwaka 1993 baada Ya kukidhi masharti, lakini kilifutwa kwenye orodha ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu na Msajili wa Vyama Vya Siasa Machi 20, mwaka 2002. Hivyo sasa hivi hakipo kwa mujibu wa sheria.

“Hivyo hivi sasa hakipo kwa mujibu wa Sheria. Kifungu cha 7(3) cha Sheria ya Vyama Vya Siasa sura ya 358 kinakataza taasisi yoyote kufanya kazi kama chama cha siasa bila kusajiliwa na Msajili wa Vyama Vya Siasa,” alisema.

Aidha kifungu cha 8(b) cha sheria hiyo kama ilivyorekebishwa mwaka 2009 kinakataza mtu yoyote kufanya shughuli za kisisa kwa jina la chama ambacho yeye si mwanachama au kiongozi.

Alisema wanaokika vifungu vya sheria hiyo waelewe kuwa wanafanya kosa la jinai, hivyo wanaaswa kuacha mara moja. Pia amewaasa wananchi, wanachama na viongozi wote wa vyama vya siasa kuheshimu na kutii sheria za nchi ili uchaguzi uweze kufanyika vizuri kwa amani na utulivu.


Vyama vinavyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ni 
 1. CCM
 2. CUF
 3. CHADEMA
 4. UMD
 5. NCCR- Mageuzi
 6. NLD
 7. UPDP
 8. NRA
 9. TADEA
 10. TLP
 11. UDP
 12. DEMOKRASIA MAKINI
 13. CHAUSTA
 14. DP
 15. APPT-Maendeleo
 16. Jahazi Asilia
 17. SAU
 18. AFP
 19. CCK
 20. ADC
 21. CHAUMMA
 22. ACT-Wazalendo

Gazeti lachapisha 'mkakati liliounasa' dhidi ya Dk Slaa

Dondoo kutoka kwenye gazeti hilo:
 • “Kukiwa na a well designed damage-control and engagement strategy, Dk. Slaa anaweza kuishia walikoishia akina Michael Nyaruba, James Mapalala, Awesu Daddi na wengineo, enzi hizo.”
 • “Hawa wanapaswa kuandaa majibu dhidi ya maelezo yoyote ya Dk. Slaa, bila kujali usahihi, watafute namna ya kupotosha pale inapobidi ili hatimaye umma upoteze imani na Slaa. Kikosi kinaweza kushiriki vipindi vya mijadala katika redio na televisheni na wakati mwingine kupenyeza hoja zao kwa waandaaji wa vipindi hivyo, na baadaye kuendelea kumu-engage proactively kwa lengo la kuhakikisha anakuwa ignored na political society wa Tanzania na pengine kumfanya aonekane political reform public enemy.
 • “Kikosi-mkakati hicho kinaweza hata kufanya utafiti na ku-expose the inner motives za harakati za Dk. Slaa, zikiwamo zinazomhusu mkewe Josephine. Tunaweza kutafiti taarifa kuhusu mkewe na kuzihakiki, vyovyote itakavyokuwa, kuzianika hadharani kupitia vyombo ya habari rafiki, vinavyounga mkono Ukawa katika kipindi cha kampeni za Uchaguzi Mkuu”
 • “Team ya Kampeni ya mgombea urais wa Ukawa ishauriwe, isijiingize kujibu chochote alichokisema au atakachokisema Dk. Slaa kuhusiana na mgombea urais wa Ukawa au wajumbe wa timu ya kampeni yake. Kama kuna suala au hoja yoyote ipelekwe katika kikosi-mkakati cha wataalamu wa mawasiliano ya kampeni za kisiasa kuandaa na hata kutoa majibu” 

Ya Dk Slaa na Rose Kamili: Siasa vs FamiliaMALUMBANO ya kisiasa nchini yanazidi kupamba moto baada ya mke wake wa zamani wa Katibu Mkuu wa zamani wa CHADEMA Dk Willibrod Slaa, Rose Kamili kuibuka na kusema amesikitishwa na kauli alizozitoa mume wake huyo alipozungumza na waandishi wa habari Septemba Mosi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamili alisema wakati Dk. Slaa anatangaza kung’atuka kwenye siasa alisema amekuwa akila mihogo na familia yake, jambo ambalo si la kweli.

Alisisitiza kuwa japokuwa mihogo siyo chakula kibaya, lakini watoto wake, Elimiana na Linus Slaa hawakuwahi kuishi kwa kutegemea chakula hicho ingawa walitelekezwa na baba yao tangu mwaka 2010.

Kamili ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu wa CHADEMA, alisema Dk Slaa aliwadanganya wananchi aliposema kuwa haongei na mgombea wa urais wa CHADEMA anayeungwa mkono na UKAWA, Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye kuwa siyo kweli kwa kuwa amekuwa akiwasiliana na viongozi hao.

Alisimulia kuwa mwaka 1995 wakati Dk Slaa alipoenguliwa na CCM kugombea ubunge Jimbo la Karatu, alikwenda nyumbani kwa Lowassa kuomba ushauri.

Lowassa alimshauri ajiunge na chama chochote na kuongeza kwamba marafiki zake Dk Slaa nao walimshauri aingie chama chochote.

Alisema anamshangaa anavyosema haongei na Lowassa na kuhoji hizo chuki anazosema yeye kama padri mstaafu zinatoka wapi?

Kwa hakika, Mama Kamili ameshindwa kuonyesha uongo wa Dk Slaa zaidi ya kuidhalilisha familia yake.

Nasema hivyo kwa sababu kauli ya Dk Slaa kuwa alikuwa akishindia mihogo na familia yake ili aisadie CHADEMA ni lugha ya picha ambayo haikuwa na maana kuwa kweli walikuwa wakila mihogo.

Alichokuwa akimaanisha Dk Slaa ni jinsi alivyojitolewa kuisaidia CHADEMA kwa hali na mali ikiwamo kutokuwa karibu na familia yake na hata wakati mwingine kulazimika kutoa fedha zake yake ya mfukoni ili chama hicho kiimarike, lakini hakumanisha familia ilikuwa ikilala njaa.

Sidhani kama Mbunge huyo hajui lugha za alama kiasi kwamba alazimishe kupindisha maneno ya mzazi mwezake kwa ajili ya kunufaisha UKAWA.

Kama Mama Kamili anadiriki kumsema Dk Slaa kuwa anatumiwa kisiasa na CCM kwa kuwa alisema aliyoyasema, anataka kutuambia hata yeye basi anatumiwa na UKAWA kumdhalilisha mzazi mwenzake hadharani?

Ni jambo la hatari sana mama huyu kukubali kuisambaratisha familia yake kwa kukubali kutumika kisiasa kisiasi hicho.

Tuhuma kwamba Dk Slaa ni dhaifu kwa wanawake tena likitolewa mbele ya watoto wake, linaonyesha kuwa Rose Kamili hajakamilika.

Nasema hajakamilika kwa sababu kwa mwanamke ambaye amekamilika huwezi kuwabeba watoto wako wakubwa wenye watoto wao kwenda kumdhalilisha mzazi mwezako katika televisheni.

Hii kwanza inawajengea watoto chuki dhidi ya baba yao na kingine kuwadhalilisha mbele ya jamii.

Kama Rose Kamaili anadai kuwa ametelekezwa na Dk. Slaa tangu mwaka 2010, alipeleka wapi mashtaka ya kutelekezwa ? Je, anataka kuuaminisha umma kwamba Dk Slaa hajali familia yake?

Naamini Rose Kamili ni Mbunge ambaye anajua haki zake kwa vyovyote vile hangeweza kwa muda wote ule kukaa kimya wakati anaonewa, hadi leo ndipo aibuke. Rose Kamili anacheza siasa, tena siasa zenyenye ni nyepesi ambazo hazina mashiko.

Tuhuma nyingine kwamba Dk Slaa kaahidiwa ubunge na uwaziri kama CCM itashinda. Nayo ni hoja nyepesi kwa sababu hivi kiongozi akikosoa CHADEMA lazima awe anatumika ?

Ina maana CHADEMA inaongozwa na malaika ambayo haina matatizo kiasi kwamba ionekane kwamba mtu akiinyoshea kidole kuikosoa tayari huyo anatumika na CCM ?

Nadhani Rose Kamili na watu wengine wenye mwelekeo kama huo wanapaswa kufahamu kwamba kila mahali kuna mazuri na mabaya.

Alichokifanya Padri Dk Slaa kuonyesha hisia zake za kutofautiana na mawazo ya wenzake kuhusu ujio wa mgombea wa urais kupitia Katibu ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa.

Ndiyo maana baada ya kuona kuwa mawazo yake yamezidiwa na wengine wakati akiona kuwa kushiriki katika jambo hilo ni kuumiza nafasi yake aliamua kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wa katibu mkuu wa CHADEMA.

Hiyo ndiyo demokrasia ya kweli kwenye jambo ambalo unaona hukubaliani nalo. Uamuzi wa Dk Slaa sio wa kwanza kufanyika unafanyika katika vyama vingine.

Uamuzi alioufikia aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba wa kujiuzulu wadhifa wake kupinga kukaribishwa kwa Lowassa ndani ya UKAWA, unafanana sana na ule wa Dk Slaa.

Huwezi kusema kuwa viongozi hao wote kwa umoja wao wamehongwa na CCM ili kuihujumu UKAWA. Mbona hivi sasa tunashuhudia makada wengi wa CCM wanahamia UKAWA, ina maana nao wamehongwa ?

Mhemuko wa kisiasa uliopo sasa nchini usiwe kikwazo, watu waachwe atoe uamuzi wao wa kuhamia chama kipi ili mradi hawavunji sheria za nchi.
 • Imeandikwa na AHMED KIMBINGO - Kwa nini Rose Kamili si kamili

[video] Aliyoyasema Lowassa ndani ya Kanisa Tabora[video] Yusuf Makamba aanika ya Lowassa, Sumaye 'kama wanabisha watokee'

Dondoo ya yaliyomo...

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba, amesema mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ni fisadi, mwongo na hakerwi na umasikini wa Watanzania na kumtaka kujitokeza hadharani kukanusha hayo na kuwa alitaka kuondoka CCM mwaka 1995 na alimwandikia barua kueleza hayo.

Makamba alisema hayo jana, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, alipohutubia mkutano wa hadhara wa kampeni wa mgombea urais wa CCM, Dk. John Magufuli.
“Anasema ninakerwa na umasikini nitaiendesha nchi mchakamchaka sisi ni mgambo? Haelezi mchakamchaka vipi, umasikini anaosema ni wake si wa wananchi na nitatoa ushahidi.
“Kuna ranchi ya Mkata, kuna kijiji cha Tototwa, Mabwegere, Kiduhi, Tambara, lakini ranchi kampa rafiki yake wa hoteli ya Nam na yeye yumo kama ana uchungu na wafugaji wa Morogoro kwa nini hakuwapa wafugaji wa Tototwa au Mabwegere.
“Anakerwa na umasikini wake.
“Handeni kuna ranchi ya Mzeri wananchi wa Handeni hawana mahali pa kufugia Lowassa akiwa waziri wa Maji na Mifugo alijipa ranchi ya Mzeri na ana ng’ombe anaowatembelea kwa helikopta, huyo ndiye Lowassa anayeomba urais” 
Makamba alisema Monduli, ambako alikuwa Katibu Mtendaji wa CCM kuna ranchi ya Leteni iliyokuwa ya ushirika tangu enzi ya Sokoine, ambayo Lowassa yumo.
“Kwenye shule yumo kwenye bodaboda yumo kwenye daladala yumo. Namuona Dar es Salaam anazunguka, nimekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa miaka 10 hajatembelea mkoa alikuja siku moja tu kutembelea Barabara ya Shekilango, wamachinga hawakuwepo, msongamano haukuwepo anakuja leo kuna nini atoke hadharani ayaseme haya.
“Hata uongo unaweka akiba Lowassa ni muongo anasema amekwenda jeshini na mimi nilikuwepo hataji brigedia aliyekuwepo na mkubwa wake ni nani anasema hatasahau vita ya Uganda aliyetuandika kwenda vitani ni Jakaya Kikwete.
Kuhusu aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, alisema amekuwa waziri mkuu kwa miaka 10 na anampongeza Rais wa zamani Benjamin Mkapa kwa kumvumilia kwa kuwa hana uzuri aliokuwa nao wala uhodari.
“Amehurumiwa hata shule amekwenda baada ya kustaafu. CCM wamesema ili kuwa rais ni lazima uwe na digrii yeye hakuwa nayo, ndiyo waziri mkuu wa kidato cha sita anahurumiwa yeye anatuona sisi wehu.
“Morogoro kulikuwa na shamba la ushirika kabla ya kufika Mvomero lina heka 300 kachukua pamoja na ghala la kijiji, panaitwa Magole, huyo ndiye Sumaye, kwa maana nyingine ni kabaika, ukabaila ni unyonyaji lakini kabaila anatumia sana ardhi.
“Leo anapita analalamika, CCM haina haja ya mwizi wala kabaila. Naweka akiba ili akijitokeza niwe na ya kumwambia, natafuta mahali pengine nimwambie.
Kama Lowassa alikuwa waziri mkuu na hali iko namna hii akiingia ikulu mnabaki na hali gani. Vijana acheni kushabikia, mwenzenu hana haja na umasikini wenu ana haja ya umasikini wake na familia yake.
“Monduli dada yake ndiye amepewa zabuni zote za halmashauri hadi penseli na kama anabisha atokee.
FREDERICK SUMAYE

MEMBER OF PARLIAMENT CV [parliament.go.tz...mpcvs]

GENERAL
EDUCATION
School Name/LocationCourse/Degree/AwardStart DateEnd DateLevel
Gidas Primary SchoolStandard Four19581961Primary School
Single Middle SchoolStandard Eight19621965Primary School
Ilboru Secondary SchoolSecondary Education19661969Secondary School
Egetron Agric. College, KenyaDiploma in Agric. Engineering19701972Diploma
-Technical Studies00000000Advanced Diploma
EMPLOYMENT HISTORY
Company NamePositionFromTo
Prime Minister's OfficePrime Minister1995Todate
Ministry of Agriculture and Cooperative DevelopmentMinister19941995
Ministry of Agriculture and Cooperative DevelopmentDeputy Minister19871994
Ministry of Agriculture and Co-operative DevelopmentDeputy Minister19851990
Arusha Appropriate Tech. ProjectTechnical Coordinator19801982
Rural Energy CAMARTEC - ArushaHead of Department19801982
Kilombero Sugar CompanyWorkshop Engineer and Section Manager19761980
Ministry of AgricultureTutor-Nyegezi Institute of Agriculture19731976
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/LocationPositionFromTo
CCM-Chama Cha MapinduziCommander(Hanang District)1995Todate
CCM-Chama Cha MapinduziMember of National Executive Council1992Todate
CCM-Chama Cha MapinduziMember of Parliament1990To Date
CCM-Chama Cha MapinduziMember of Parliament1985Todate
Chama Cha Mapinduzi (CCM)Member of Parliament - Hanang Constituency19831985
CCM-Chama Cha MapinduziMember of General District Meeting19781980
SPECIAL SKILLS
Skill Name or DescriptionExperienceAcquired Through
JKT(mgambo)1973
Transport Systems1978Mananga Agric. Management Centre-Swaziland
Planning & Control in Agric. Management1978Mananga Agric. Management Centre-Swaziland
Training in Alternative Energy Technologies1982University of Florida-USA