Hapa uko usalama kweli? Hatari hii!Mjadala wa mtizamo wa wenyenchi walioko vijijini kuhusu uchaguzi 2015


Hotuba ya Magufuli - Tangamano, TangaMgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt John Pombe Magufuli akifafanua jambo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika katika viwanja vya Tangamano jioni ya leo mjini Tanga.


Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tanga kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya angamano,jioni ya leo ambapo aliahidi kuboresha Bandari ya Tanga, kujenga Viwanda vya matunda na samaki ili kuweza kupunguza tatizo kubwa la ajira kwa vijana.


Naibu Waziri wa Sheria na Katiba,ambaye pia ni mgombea Ubunge viti maalum upande wa akina Mama mkoa wa Tanga (UWT),Mh Ummy Mwalimu akimuombea Kura za kutosha mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ili aweze kuibuka mshindi na kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.


Wakazi wa mji wa Tanga waliofika kwenye mkutano huo wakishangilia jambo.


Nyomi la watu


Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akihutubia wakazi wa mji wa Tanga kwenye mkutano wa kampeni za CCM.


Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Tanga na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwenye viwanja vya Tangamano kwenye mkutano wa kampeni za CCM,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao.


Dkt Magufuli akisisitiza jambo mbele ya maelfu ya wananchi (hawapo pichani) jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika uwanja wa Tangamano.


Naibu Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akihutubia wakazi wa Tanga mjini kwenye mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano.


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba na Naibu Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano wa kampeni jioni ya leo katika uwanja wa Tangamano,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alihutubia na Kumwaga sera zake kwa wananchi,ikiweno na kuomba ridhaa ya kuwaongoza katika miaka mitano ijayo.


Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Mzee Yusuph Makamba akihutubia wakazi wa Tanga mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika ndani ya viwanja vya Tangamano.


Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na kuwaomba wananchi hao wajitokeze kwa wingi Oktoba 25 na kumpigia kura ya ndio ili aibuke mshindi na kupewa ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa mji wa Tanga waliofika kwenye mkutano hadhara wa kampeni,uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya Tangamano mjini humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
  • Picha tumeshirikishwa na Ahmad Michuzi aka Michuzi Jr/Jiachie Blog, Tanga

Tyler Perry meets Tanzanian children with albinism living in a NY home he funded

ATLANTA -- Tyler Perry recently met with a group of Tanzanian children with albinism who are living in a home the filmmaker helped fund.

Perry representative Keleigh Thomas Morgan said Monday he donated $200,000 three years ago to help build a four-bedroom house in New York for a group of children who had been mutilated for their body parts. The children attended Perry's "Madea on the Run" play Thursday night at Manhattan's Beacon Theatre, where they met him backstage.

The children will stay there while they receive medical treatment in the United States.

Perry donated after watching a special featuring Elissa Montanti, a Staten Island woman who runs the non-profit Global Medical Relief Fund for children affected by war and natural disasters.

Montanti recently brought the children with albinism to the U.S. from Tanzania.

Mradi wa kuzalisha gesi katika mabwawa ya maji taka na vyoo Vingunguti


Mratibu wa Mradi wa kuzalisha gesi ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa 4 katika fani ya Uhandisi wa Mazingira, Chuo Kikuu cha Ardhi John Rutahirwa Akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu moja ya mtambo wa kukusanyia maji taka kutoka majumbani eneo la mradi wa kuzalisha gesi Vingunguti.Gesi hiyo itaanza kutumika mwezi Desemba mwaka huu.


Wakazi wa mtaa wa mji mpya, kata ya Vingunguti, Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wako mbioni kuanza kunufaika na mradi wa uzalishaji wa gesi inayotokana na maji taka ya vyoo vyao na yale ya yaliyo katika mabwawa makubwa ya kuhifadhia maji taka yaliyo katika eneo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo unapojengwa mradi wa majaribio wa kuzalisha Gesi, Mratibu wa Mradi huo ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa 4 katika fani ya Uhandisi wa Mazingira, Chuo Kikuu cha Ardhi John Rutahirwa amesema kuwa wananchi wataanza kutumia gesi itakayozalishwa kuanzia mwezi Desemba mwaka huu.

Amesema kazi ya kufanikisha ujenzi wa miundombinu ya mradi huo inaendelea chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Maji Taka (DAWASA) kwa kushirikiana na Wanafunzi wa fani ya Uhandisi wa Chuo Chuo Kikuu cha Ardhi na Taasisi isiyo ya kiserikali ya wanafunzi wanaosomea fani ya uhandisi wa Mazingira (CDI) ya Chuo kikuu cha Cambridge, Uingereza.

Amesema wanafunzi wanaosomea fani ya Uhandisi wa Mazingira wa Chuo Kikuu cha Cambridge, Uingereza kwa kushirikiana na baadhi ya wanafunzi wanaosomea Uhandisi wa Mazingira wa Chuo Kikuu cha Ardhi nchini Tanzania walikuja na wazo na kubuni mradi huo wenye lengo la kuboresha maisha kupitia maji taka.

Amesema chini ya uratibu wa DAWASA yenye jukumu la kusimamia miundombinu ya maji taka na Taasisi ya mikopo la Bridge for change ya Tanzania inayotoa mikopo midogo midogo kwa wananchi walianza kufanya mapitio kwa kila nyumba ili kuona namna wanavyoweza kutumia changamoto ya maji taka katika eneo hilo kwa kuigeuza kuwa fursa.

Amefafanua kuwa wakihusisha wataalm wa mradi na viongozi wa mtaa wa vingnguti mji mpya, walianza kuzungumza na kujadiliana na wakazi wa eneo hilo ili kuwezesha kazi ya kuunganisha vyoo vyao katika mtandao wa mabomba ya kusafirisha maji taka kuelekea kwenye mtambo wa kuzalisha gesi.

Amefafanua kuwa chini ya mradi huo maji taka yote kutoka kutoka katika nyumba zilizounganishwa kupitia mabomba yanakusanywa na kusafirishwa moja kwa moja kwenye mtambo wa kuzalisha gesi.
Kwa upande wake Mtaalam anayehusika na ujenzi, mafunzo na usimamizi wa mfumo wa mradi huo ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya Uhandisi wa Mazingira Chuo Kikuu cha Ardhi Rukia Yange amesema mradi huo ambao uko kwenye majaribio unalenga kuwapunguzia wananchi gharama za uhifadhi wa maji taka kwa kuwapatia nishati ya gesi kwa gharama nafuu itakayowasaidia kuondokana na matumizi ya mkaa.

Amesema kwa kuanzia utawanufaisha watu 150 wa eneo hilo na kuongeza kuwa kuanzia Desemba mwaka huu wataanza kuiweka gesi hiyo katika vifungashio maalum vitakavyoanza kusambazwa majumbani mwao tayari kwa matumizi.

Amesema gesi hiyo itamwezesha mwananchi kuitumia kwa kipindi cha mwezi mmoja na kupunguza matumizi makubwa ya mkaa na uharibifu wa mazingira.

Aidha, amesema gharama za mwananchi kuunganishwa katika mfumo huo inaanzia shilingi 150,000/ kwa wale walio na vyoo vinavyoruhusu mfumo huo na shilingi 700,000/= kwa mwananchi anayetaka kujengewa choo kipya katika eneo lake la makazi gharama ambazo hulipwa kidogo kidogo kupitia utaratibu wa mikopo nafuu ulioanzishwa.

Naye Meneja Uhusiano wa DAWASA Bi. Neli Msuya akifafanua kuhusu mradi huo amesema suala la ujenzi wa miundombinu ya kuchukualia maji taka na matumizi ya gesi itakayozalishwa litakwenda sambamba na utoaji wa elimu kwa wananchi hao juu ya matumizi na uhifadhi wa gesi hiyo.

Amefafanua kuwa DAWASA inaendelea kuendesha mafunzo ya uzingatiaji wa usalama katika matumizi ya gesi hiyo pamoja na suala la usafi, utunzaji na ulinzi wa miundombinu ya kusafirishia maji taka iliyojengwa katika eneo hilo ili iweze kudumu kwa kipindi kirefu.

Ameeleza kuwa mbali na mradi wa kuzalisha gesi DAWASCO kwa kushirikiana na wadau wa matumizi ya Nishati endelevu na uhifadhi wa mazingira inatarajia kuanzisha mradi wa kuzalisha mbolea itakayotokana na maji taka yaliyohifadhiwa katika eneo hilo.

“DAWASA tukishirikiana na wadau mbalimbali tuna mpango wa kuyatumia maji taka haya yaliyohifadhiwa kuzalisha mbolea itakayotumiwa na wakulima katika shughuli za kilimo,tunalenga kuibadilisha changamoto hii ya maji taka kuwa fursa itakayowanufaisha wananchi badala ya kuwa kero kwao” Amesisitiza.

Wakiuzungumzia mradi huo baadhi ya wakazi wa mtaa wa mji mpya ambao vyoo vyao vimeunganishwa kwenye mfumo wa kusafirishia maji Taka wamesema mradi huo ni ukombozi katika maisha yao kwa kuwa umewapatia vyoo bora na kuwaondolea adha na gharama ya uhifadhi wa maji taka waliyokuwa wakiipata hapo awali kutokana na ujenzi holela wa makazi yao.

Wameongeza kuwa mradi huo umewasaidia katika uhifadhi wa mazingira na kuondoa tatizo la utiririshaji wa muda mrefu wa maji taka uliosababishwa na uwepo wa mifumo mibovu ya vyoo vyao.
Wamesema kuwa kutokana na uimarishaji wa mifumo ya kusafirisha maji uliofanywa na DAWASA kwa kushirikiana na Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Cambrige (CDI) na Taasisi ya utoaji wa mikopo ya Bridge for Change wameondoa hofu waliyokuwa nayo ya kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu na kutoas wito kwa wananchi katika maeneo mengine kujiunga na mradi huo.


umanne Saidi Fundi ujenzi wa vyoo na msimamizi wa mradi wa majaribio wa Biogasi Vingunguti akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu kazi ya ufungaji wa miundombinu ya kuzalisha gesi katika eneo la Vingunguti.

Mtambo wa kuzalisha Gesi katika katika eneo la Mradi wa Majaribio eneo la Vingunguti unaokusanya maji taka moja kwa moja kutoka katika makazi ya wananchi.Mtambo huo kwa mujibu wa maelezo ya watalaam wa mradi huo una uwezo wa kukaa ardhini kwa kipindi cha miaka 50.

Moja ya choo cha kisasa kilichojengwa katika moja ya familia kwa ajili ya mradi wa kuzalisha Gesi katika eneo la Vingunguti.

Eneo la Mtaa wa mji mpya Vingunguti ambako mabomba ya kupitishia maji taka kutoka kwenye vyoo vya wananchi ambayo huenda moja kwa moja kwenye mtambo wa kuzalishia gesi.
  • Taarifa ya Aron Msigwa – MAELEZO. Dar es salaam.

Ngoma ya Lowassa kijijini Geita


Report on Retail Potential on Africa: Tanzania leads East Africa

atkearney.PNG

PRESS RELEASE

Retail potential on African continent confirmed

- AT Kearney’s 2nd African Retail Development Index reconfirmed the continent’s retail potential

- Gabon (#1), Botswana (#2) and Angola (#3) in particular provide retailers with diverse options for retail expansion

- Nigeria drops from #2 to #4 it is still a market to consider, while Tanzania leads the pack in East Africa

JOHANNESBURG, South-Africa, September 8, 2015-- The 2015 African Retail Development Index has been released today  that reveals the most attractive developing markets across Africa for expansion. It discusses the growth in the middle class in Africa, increased consumerism, the spread of malls, land being taken up for development for retail purposes and Sub-Sahara’s young and connected middle class that is growing fast and still deciding on its favourite brands.
  
The report reveals :
  • The African Retail Landscape – what the retail market in SSA looks like today
  • ARDI 2015 ranking incl. South Africa’s ranking and the opportunities for its retailers in the rest of SSA
  • Right Approaches to Africa – which countries provide the best opportunities and how does this link to retail maturity stages?

With Sub-Saharan African brimming with potential being one of the few markets with annual GDP growth of more than 5%.  AT Kearney’s 2015 African Retail Development Index (ARDI) reconfirms the potential of many nations throughout Africa—not just oft-discussed markets like Nigeria and Ghana, but also small, dynamic markets such as Gabon, the ARDI’s top-ranked market and home to Sub-Saharan Africa’s highest GDP per capita, and also mid-sized and fast-growing countries such as third-ranked Angola.
The report begins with a look at entry strategies for Sub-Saharan  Africa, followed by an in-depth analysis of the top 14 countries.

The authors are available this week to share their views of the report & insights on:
  • The outlook for the retail sector for 2015/2016
  • South Africa's retail sector vs other emerging markets such as India, Brazil, etc

The 2015 ARDI ranks the top 15 Africa countries according to market attractiveness for retail expansion. The ARDI is a useful framework for retailers because it not only identifies the markets in Africa most attractive for retail expansion today, but those that offer the most potential.

The Index identifies three distinct differences in stages of retail advancement in the Top 15 countries—basic, developing, and mature—with only Southern Africa falling into the mature bracket. They are characterized by having a formal shopping culture, international and growing private label exposure, innovation, and stable and transparent pricing. In this market, the key purchase drivers are convenience and quality.

Mirko Warschun, AT Kearney partner and leader of the firm’s consumer industries and retail practice for Europe, Middle East, and Africa (http://www.atkearney.com), noted that Nigeria (#4) moved down the index, despite its market size and room for growth. “Nigeria has massive room for growth in formal retail with 25 new shopping centres in development,” said Warschun. “True spending, however, remains comparatively low as the ‘true middle class’ is a lot smaller relative to the smaller countries ranked higher.”

With its tremendous potential and strong economic projections, however, Nigeria is still a market to consider.

While Tanzania (#5) has dropped a notch, it was the largest and most stable of the East African Community countries and remained an attractive retail market said Warschun. “Tanzania is in the early stages of development, and therein lies the opportunity,” he said. “This unsaturated market has one of Africa’s fastest growing retail sectors, boosted by new shopping malls.”

Bart Van Dijk, AT Kearney partner and leader of the firm’s consumer industries and retail practice in Africa, said that it was instructive to think of Africa as a set of opportunities that can be augmented and added onto one another, rather than just one singular opportunity. “How you pick among the opportunities depends on your offering,” he said. “Retailers with a basic offering should target the large cities and countries because scale will be important, while retailers with a wider assortment should target higher average income countries including the smaller ones.”

The ARDI is based on four dimensions: market size, market saturation, country risk, and time pressure, and ranks the potential and urgency of moving into each country accordingly.

2015 ARDI Results (see chart)
The ARDI’s top 15 highlights some interesting developments. Two small countries—Gabon and Botswana—are ranked first and second, while Ethiopia, with Africa’s second largest population, barely cracks the top 15. The ARDI report includes a summary of all 15 countries in the Index, recommendations for the Cash and Carry retail model, and commentary on the opportunity presented by the East African Community—Kenya, Tanzania, Uganda, and Rwanda.

The report also provides entry strategy recommendations for each stage—Basic, Developing, and Mature.

Mike Moriarty, AT Kearney partner and leader of the firm’s Global Consumer Institute, concluded, “Success in Africa requires analysis, understanding, and the flexibility to customize, but for those willing to take the risk, the rewards are plentiful.”

Download a copy of the full report at: www.atkearney.com

Contact:                                
Nicole Chamberlin
HWB Communications
+27 (0)21 421 0430
+27 (0)79 192 0105

About the Authors:  
Marieke Witjes (+27 63 309 7802 )– Her ability to recognize and realize change, both from a market and consumer perspective as well as an organization and employee angle, she’s been A.T. Kearney for over 7 years working on strategic assignment across industries. She is a member of A.T. Kearney’s global strategy practice, focusing mainly in consumer driven industries. Prior to this, she obtained a master’s degree in international economics and worked in India and Uganda. She has always been passionate about emerging economies and growth opportunities, explaining her move from the Netherlands to South Africa.  

Jaco Prinsloo (+27 83 980 2614) is a principal with A.T. Kearney who has more than 12 years of consulting and industry experience in consumer goods. He focusses on rapid operational improvement, post-merger integration and turnarounds for private equity and corporate clients. His work experience spans Europe, Asia and Africa. Recent emphasis has been on supporting growth in Africa through a combination of market entry strategies, route to market configurations and new factory developments. Prior to joining A.T. Kearney he managed the supply chain for a large European consumer goods company and drove their performance to world class.

About the Study
The Africa Retail Development Index ranks Sub-Saharan Africa countries on a 0-to-100 point scale: the higher the ranking, the higher the potential and urgency to enter the country. The countries considered for the rankings were pre-selected based on three criteria – a country risk of 35 or higher in the Euro money country-risk score, population size greater than 1.5 million, and GDP per capita (PPP) of more than $1,000. The ARDI scores are based on Country and Business Risk (25 percent), Market Size (25 percent), Market Saturation (25 percent), and Time Pressure (25 percent).

About AT Kearney
A.T. Kearney (www.atkearney.com) is a leading global management-consulting firm with offices in more than 40 countries. Since 1926, we have been trusted advisors to the world's foremost organizations. A.T. Kearney is a partner-owned firm, committed to helping clients achieve immediate impact and growing advantage on their most mission-critical issues. For more information, visit www.atkearney.com

About the A.T. Kearney Global Consumer Institute
The A.T. Kearney Global Consumer Institute is a worldwide network of professionals and executives. The Institute combines proprietary and public data resources with local knowledge to deliver strategic and operational insights to executives in consumer-facing industries seeking long-term growth and competitive advantage. For more information, please contact [email protected]

SOURCE 

A.T. Kearney (Pty) Ltd

Taarifa ya CCM kuhusu kauli ya Lowassa Kanisani

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katika hali ya kushangaza na kusikitisha tarehe 6/09/2015 siku ya Jumapili mjini Tabora mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema Ndg. Edward Lowassa aliamua kutumia udini kuomba kura.

Ndg. Lowassa akihudhuria ibada katika kanisa la Kilutheri (KKKT) mjini Tabora amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii akidai kuwa, kwa kuwa toka nchi ipate uhuru hajawahi kutokea Rais kutoka dhehebu la Kilutheri hivyo mwaka huu ni zamu ya Walutheri.

Chama Cha Mapinduzi kinalaani matumizi ya lugha zinazoligawa Taifa letu kwa misingi ya udini, ukanda, ukabila na ubaguzi wa aina yeyote kisa tu kutafuta madaraka.

Kauli hii ya Ndg. Lowassa licha ya kuwa ni kinyume na Sheria za Uchaguzi za nchi yetu, kinyume na Kanuni za Maadili ya Uchaguzi zilizosainiwa na vyama vyote, lakini ni kinyume kabisa na mila na desturi za Kitanzania katika kuhakikisha Taifa hili linabaki kuwa Taifa moja lenye umoja, amani na mshikamano.

Kwa mfano, Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2015, yaliyotolewa na Tangazo la Serikali Na. 294 la tarehe 27/7/2015 chini ya kifungu cha 124A cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura ya 343, ukurasa wa 5 kifungu 2.1(k) kinasema:-

"Viongozi wa vyama vya siasa, wagombea au wafuasi wao wahakikishe kuwa majengo wanayotumia kufanya kampeni sio ya Ibada. Vile vile, vyama vya siasa vihakikishe kuwa havitumii viongozi wa dini kupiga kampeni kwa ajili ya vyama vya siasa au wagombea wao".

Lakini katika maadili hayo hayo, ukurasa wa 7, kifungu 2.2(i) kinasema:-

"Vyama vya siasa au Wagombea hawaruhusiwi kuomba kupigiwa kura kwa misingi ya UDINI, UKABILA, JINSIA AU RANGI."

Kwa kuwa Ndg. Lowassa siku hizi tabia ya kusahau inaongezeka kwa kasi nimeona ninukuu vifungu hivi kwa rejea yake na wenye tabia kama yake.

Lakini matamshi hayo ni uthibitisho tosha kuwa Ndg. Lowassa, Chama chake cha CHADEMA na vyama vinavyomuunga mkono chini ya UKAWA ni wabaguzi, wachochezi na waroho wa madaraka wasiojali masilahi mapana ya nchi yetu. Kwao madaraka ni muhimu kuliko nchi yetu.

Hii si mara ya kwanza kwa Ndg. Lowassa, Chama chake cha CHADEMA na makada wenzake kutoa kauli na kufanya vitendo vya kibaguzi, kwa kutumia ukanda na sasa wameamua kutumia udini kama njia ya mkato ya kutafuta madaraka.

Chama Cha Mapinduzi kinaamini huu si msimamo wala utamaduni wa Watanzania, bali ni uroho binafsi wa madaraka wa Ndg. Lowassa na chama chake, hasa baada ya kuona kuwa hoja zake za kutafuta nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi yetu zimekataliwa na wananchi.

Mwalimu aliwahi kutuonya juu ya wanasiasa wanaotumia udini na ukabila kama hoja ya kutaka kupata madaraka kuwa ni wanasiasa walifilisika kisiasa lakini ni watu wa hatari sana kwa mustakabali wa amani, umoja na mshikamano wa nchi yetu.

Hivyo basi, Chama Cha Mapinduzi kinalaani kauli hii na tunaamini inapaswa kulaaniwa na wote wanaoipenda nchi yetu. Lakini CCM inaamini vyombo vinavyohusika na hasa Tume ya Taifa ya Uchaguzi itachukua hatua zinazostahili kuondoa mbegu hii ya kansa inayoletwa na Ndg. Lowassa kwenye nchi yetu. Maneno ya Ndg. Lowassa ni kansa mbaya kwa nchi yetu na lazima yakemewe na kukomeshwa kabisa.

Maneno na vitendo vya Ndg. Lowassa, chama chake, na makada wenzake wa CHADEMA na vyama shirika vya UKAWA toka wameanza kampeni katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu na kwa nyakati tofauti zimejaa ghiriba na ubaguzi uliokithiri. Tabia hizi za Ndg. Lowassa ni moja ya sababu iliyopelekea CCM kutompa nafasi ya kugombea kupitia Chama hichi.

CCM inatoa wito kwa wadau wote na Watanzania wote kuwa ni vizuri kuwa makini wakati huu wa Uchaguzi, kuhakikisha hakuna jambo linaligawa Taifa letu. Tuendeshe kampeni bila kuligawa na kuliangamiza Taifa letu. Tanzania yetu ni muhimu. Tanzania kwanza mengine baadae.

Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
08/09/2015

Rais Kikwete apokea Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete leo amepokea Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika Mashariki kutoka katika taasisi ya East Africa Book of Records yenye makao yake makuu jijini Kampala Uganda.Pichani kiongozi wa Taasisi hiyo Dkt.Paul Bamutize akimkabidhi Rais Kikwete tuzo hiyo wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaanm leo asubuhi.Sambamba na Tuzo hiyo Rais kikwete amepokea tuzo ya kuitambua Tanzania kama taifa bora Afrika Mashariki kwa kudumisha Amani na Utulivu,Huduma bora za jamii,na maendeleo makubwa ya kiuchumi katika kipindi cha miaka kumi. (picha, maelezo: Freddy Maro)Mahojiano ya awali ya Tido Mhando na Dk Slaa


Gwajima amzungumzia Dk Slaa


Video nzima ya Askofu Mkuu wa Kanisa Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima lipoongea na Waandishi wa habari katika hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam, Septemba 8, 2015 akijibu tuhuma za Dk Slaa.


Gwajima akizungumza na waandishi wa habari pamoja na waumini wa kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo, kuhusu kauli mbalimbali alizozitoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chadema Dk.Willibroad Slaa, akimtuhumu yeye kuwa ni mshenga wa Lowassa pamoja na kumpa siri za Maaskofu na wachungaji kuhongwa na Lowassa ambapo alikanusha tuhuma zote.


Baadhi ya waandishi wa habari na waumini wa Kanisala Ufufuo na Uzima wakifuatilia mkutano wa Askofu wa Kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo.


Walinzi waliomzinguka Askofu Gwajima wakisafisha njia.
  • Picha kutoka kwenye blogu ya Said Powa