Mbinu 5 za kuanza na kukuza biashara kwa mtaji mdogo

image: valeague.com
Leo katika kipengele hiki tutaona jinsi ya kukabiliana na changamoto hii. Lakini kabla hatujaona ni nini cha kufanya, hebu tusome maoni ya msomaji mwenzetu.
Nilikuwa nimeajiriwa na Wazungu fulani. Walipoondoka nilianza kigenge cha laki mbili sasa naendelea mdogo mdogo. Changamoto yangu ni kukuza na kupata duka la jumla. tatizo ni wapi nitapata mtaji usiozidi milioni kufikisha malengo yangu, nitumie njia gani maana kigenge changu pato lake halizidi 40 kwa siku, naomba ushauri nifanyeje. M.P
Kama tulivyosoma alichoandika msomaji mwenzetu hapo juu, ameanza biashara na mtaji kidogo na sasa changamoto yake ni kuikuza biashara hiyo zaidi. Hapa tutashirikishana baadhi ya mambo ya kufanya ili kuweza kukuza biashara hii na kufikia mafanikio makubwa.

1. Jipe muda, biashara haitaweza kukua haraka kama unavyofikiri

Uzuri wa kuanza biashara na mtaji kidogo ni kwamba kila mtu anaweza kufanya hivyo. Lakini pia urahisi huu wa kuanza biashara kwa mtaji kidogo unafanya ukuaji wa biashara kuwa wa taratibu sana. Hivyo unapofanya biashara yoyote ambayo unaanza na mtaji kidogo ni muhimu ukajipa muda ili kuweza kukuza mtaji wako. Usiwe na tamaa ya kutaka kukuza biashara hii haraka, unaweza kuingia kwenye maamuzi ambayo yatakugharimu zaidi. Endelea kufanya biashara yako huku ukijifunza zaidi na kuangalia kila fursa ambayo unaweza kuitumia kukuza biashara yako.

2. Kuza mtaji wako taratibu

Kwa mtaji huo mdogo ambao umeanza nao biashara, endelea kuukuza kila siku. Usiendeshe biashara kwa kula kila kipato unachopata, badala yake tenga sehemu ya akiba irudi kwenye biashara yako. Fanya hivi kwa nidhamu ya hali ya juu sana na unahakikisha kila unapopata faida sehemu inarudi kwenye biashara yako. Pia endelea kuangalia kwa mazingira uliyonayo na kwa biashara unayofanya ni kwa jinsi gani unaweza kukuza mtaji wako zaidi. Kama utafikiria hili kila siku, hutakosa majibu ambayo yatakusaidia.

3. Punguza gharama za biashara na za maisha pia

Kuwa kwenye biashara haimaanishi kwamba ndio una uhuru wa kufanya chochote unachotaka na fedha za biashara hiyo, kwa sababu tu ni zako. Wewe sasa upo kwenye wakati mgumu wa kukuza biashara yako huku ukiwa huna njia nyingi za kufanya hivyo. Hebu kwa sasa punguza kabisa gharama zako za kibiashara na za maisha pia. Kama kitu sio muhimu sana basi usikigharamie. Punguza matumizi yote ambayo ni ya anasa tu na sio kwa ukuaji wa biashara. Katika kupunguza gharama zako za biashara na maisha, jijengee nidhamu nzuri sana ya fedha. Usitumie fedha kiholela tu, kuwa na mahesabu na sababu kwa nini umetumia fedha fulani, hasa kwa matumizi ambayo sio ya kawaida.

4. Angalia watu ambao unaweza kushirikiana nao

Baada ya kuiendesha biashara yako vizuri na ukaona inaenda kwa faida, unaweza kuangalia watu ambao unaweza kushirikiana nao kwenye biashara hiyo. Kuna watu wengi ambao wanaweza kuwa na mtaji lakini hawana muda wa kufanya biashara. Lakini pia watu hawa wanataka mtu ambaye wanaweza kumwamini. Hivyo kama unaweza kuaminika angalia watu unaoweza kushirikiana nao kibiashara. Andaa mpango mzuri ambao utamshawishi mtu ni jinsi gani yeye atafaidika kama atawekeza kiasi kidogo kwenye biashara yako. Ikiwa unaendesha biashara yako kitaalamu itakuwa rahisi zaidi kushawishi watu kushirikiana na wewe.

5. Rasimisha biashara yako ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kupata mkopo

Hata kama biashara yako ni ndogo kiasi gani, irasimishe. Iendeshe kisheria kwa kuwa na namba ya mlipa kodi na hata leseni pia. Hivi vitakuwezesha wewe kutambulika na taasisi za kifedha pale utakapohitaji msaada zaidi wa kifedha. Mkopo kwenye taasisi za kifedha ni chanzo muhimu ila usikimbilie kama bado hujaweza kuiendesha biashara yako kwa faida. Hakikisha umeiweka biashara yako vizuri kwanza na inajiendesha kwa faida ili unapochukua mkopo unajua unauweka wapi na kuendelea kupata faida zaidi. Kuikuza biashara pale ambapo umeanza na mtaji kidogo ni kitu ambacho kinawezekana. Ila unahitaji kujitoa na kujenga nidhamu kubwa. Unahitaji kufanya kazi zaidi ya wafanyabiashara wengine, unahitaji kuwa mbunifu wa hali ya juu na pia unahitaji kujijengea uaminifu. Ukishajua wewe biashara yako ni ndogo na inahitaji kukua, basi hakikisha kila mara unaumiza akili yako ifikirie njia zaidi za kuikuza. Na kama utaweza kufanya hivi basi utaziona fursa nyingi zilizokuzunguka za kuikuza biashara yako.

Mrembo aonesha umahiri wake wa kumiliki mpira kwa danadana


Daktari mbakaji / Doctor abuseSherehe ya miaka 10 ya Michuzi Blog


[picha] UKAWA wazindua kampeni za CUF ZanzibarMgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF - Zanzibar, Nassor Mazrui, wakati akiwasili katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia, Kibanda Maiti, Zanzibar leo Septemba 9, 2015.

Mdahalo: Vyama vya siasa vitajadili elimu na afya

Tarehe: Jumapili Septemba 13 2015

Muda: 7:00 – 10:00am (Saa saba mchana hadi saa kumi jioni)

Mahali: Ukumbi wa Julius Nyerere International Conference Centre (JNICC) – Posta

Midahalo hii inalenga kuvipa vyama vyote fursa ya kunadi Ilani zao na kwa wananchi kuuliza maswali muhimu yatakayo pelekea maamuzi yao katika uchaguzi. Vyama vinavyoshiriki ni vile vyenye wagombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar na wagombea Ubunge angalau majimbo 65.

Midahalo hii itarushwa moja kwa moja na Star TV na Redio RFA. 

Vyombo vya habari vinakaribishwa kushiriki lakini lazima wajiandikishe kabla ili kufanya hivyo. Tafadhali tuma barua pepe kwa [email protected]

UNESCO Statement on World Literacy Day

Dar es Salaam Office

Message from Ms Irina Bokova, Director-General of UNESCO, on the occasion of International Literacy Day, 8 September 2015

Every year, on September 8th, we raise the flag for literacy as a human right, as a force for dignity, and as a foundation for cohesive societies and sustainable development.

This message is especially vital this year, when States will adopt a new agenda for education and development to guide the next 15 years. Promoting literacy must stand at the heart of this new agenda. By empowering individual women and men, literacy helps to advance sustainable development across the board -- from better healthcare and food security to eradicating poverty and promoting decent work.

There has been progress across the world since 2000, but steep challenges remain. Today, 757 million adults still lack basic literacy skills -- two thirds are women. The number of out-of-school children and adolescents is on the rise, standing at 124 million worldwide – while some 250 million children of primary school age are failing to master basic literacy skills even in schooling.

We cannot allow this to continue. Literacy is essential to reach the proposed sustainable development goal to promote “inclusive and equitable quality education and lifelong learning for all.” THE END FROM THE UNESCO DG.

Moving from the preceding Global picture, the situation in Tanzania the UNESCO Sub Saharan Africa ( SSA) EFA, 2014 Report shows that the country has made limited progress with a 4 % gain from 69% in 2000 to 73% in 2012. This is significantly lower than the 9% progress on average in SSA (from 58 to 67% in the same period). In that regard this is the EFA Goal which Tanzania has made the least progress.

In addition, the 2014 ‘Adult Literacy Survey Report for Tanzania Mainland’ of the Ministry of Education and Vocational Training reveals that out of 236 adult literacy learners only 31.5% could read, write, and compute simple arithmetic correctly. Whereas, 39% could not read, write and compute at all. These findings depict a worse situation implying that the actual illiteracy rate may be around 39%.

Undoubtedly, this is a big hindrance to achieving any national and international education targets as well as desired socio-economic development. Hence, all education stakeholders ought to join hands in curbing this problem if Tanzania is reach the Middle Income Level by 2025 as envisioned in its 2025 Vision.

Matokeo ya ukaguzi wa kushitukiza wa TBS wa Solar Power Panels

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Shirika la viwango Tanzania limekuwa likifanya ukaguzi wa kushitukiza wa bidhaa zilizopo sokoni na viwandani mara kwa mara, lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zinakidhi matakwa ya kiwango cha bidhaa husika wakati wote. 

TBS kwa kushirikiana na Taasisi ya Nishati Jadididu (TAREA) iliamua kufanya ukaguzi wa kushitukiza kufuatia malalamiko mengi kuhusiana na ubora wa vipande vya umeme nuru katika soko la Tanzania ili kutatua tatizo. Mnamo tarehe 23-06-2015, TBS ilifanya ukaguzi wa Umeme Nuru (Solar Power panels) katika maeneo yafuatayo;

Keko- Mwanga, Mtaa wa Msimbazi, Mtaa wa Congo. TBS ilibaini baadhi ya wasambazaji walikuwa na bidhaa za umeme nuru zilizo chini ya kiwango nyingi zikitokea nchini China. 

Jumla ya vipande vya umeme nuru 1321 kutoka duka na ghala la Regal Solar Ltd vilizuiwa kuuzwa; na 164 kutoka duka la Nishati Electronics Ltd pia vilizuiwa kuuzwa baada ya ubora wake kutiliwa shaka mpaka matokeo ya maabara yatakapotoka. Na vile vile wakaguzi walichukua sampuli kutoka duka la Keoali Power & Equipments Co.Ltd.

Matokeo ya maabara yalitoka na kuonesha kuwa sampuli hizo zilizochukuliwa katika maduka tajwa zimefeli.

Tafadhali bonyeza linki ifuatayo kwa maelezo zaidi: press_conference_-_solar_panel.pdf

Taarifa ya kuitwa mafunzoni - Idara ya Uhamiaji

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

IDARA YA UHAMIAJIKUITWA MAFUNZONI

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anawatangazia wote waliofaulu usaili wa nafasi za ajira ya Konstebo, Koplo na Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji ulioendeshwa katika Kambi na Vikosi vya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuwa wanatakiwa kuripoti Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji, Mtaa wa Loliondo Kurasini Dar es salaam Siku ya Alhamisi, Tarehe 10 Septemba, 2015 kwa ajili ya maandalizi ya safari ya kwenda kujiunga na Shule ya Polisi- Moshi hapo Tarehe 11 Septemba, 2015.

Mahitaji na vifaa muhimu wanavyopaswa kuandaa na kuwa navyo huko Shule ya Polisi Moshi ni pamoja na:
  • Mashuka mawili (2) rangi ya blue bahari (light blue);
  • Chandarua chenye upana wa futi 3;
  • Nguo za michezo (track suit nyeusi, T-shirt ya rangi ya blue na raba za michezo);
  • Pasi ya mkaa;
  • Ndoo moja;na
  • Pesa ya tahadhari Shilingi 50,000/= na
  • Nauli ya kuwawezesha kufika Shule ya Polisi Moshi.
Atakayesoma tangazo hili amjulishe na mwingine.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA
KAMISHNA JENERALI WA UHAMIAJI
LEO TAREHE 08 SEPTEMBA, 2015

Call for applications: Training on Experimental Design and Statistical Analysis

CALL FOR APPLICATIONS TO ATTEND A TRAINING COURSE ON EXPERIMENTAL DESIGN AND STATISTICAL ANALYSIS, 19TH - 23RD OCTOBER 2015 

Sokine University of Agriculture (SUA) in collaboration with the Technical University of Denmark, National Institute of Aquatic Resources (DTU- Aqua) under BSU II are implementing a project entitled “Strengthening Research and Teaching Capacity for Sustainable Development of aquaculture in Tanzania. One of the objective of this project is to strengthen research skills at SUA through providing training on research methodology and statistical analysis. 

The course on experimental design and statistical analysis will introduce the participants to the best practices in modern scientific method and statistical analysis. The course will highlight the iterative nature of scientific investigation, and the use to simple models as a platform for hypothesis development. The course will consist of lectures, practical work, plenary discussions and presentations. 

Learning outcomes After the course participants will be able to: 
 Formulate a hypothesis on a relevant scientific topic according to good scientific practice. 
 Plan and design an experiment to test a hypothesis. 
 Construct a simple conceptual model to synthesize a scientific problem. 
 Carry out various statistical tests and identify their strengths and weaknesses. 
 Use an iterative approach to redesign experiments and tests in a scientifically robust manner. 
 Present and critically evaluate experimental results and hypotheses. 

Target group: 
The targeted groups include PhD students and Junior/ Mid-career members of academic staff (Assistant Lecturers and Lecturers holding MSc/MA) at SUA. 

The course will be facilitated by 
Sigrun Jónasdóttir - Senior Research Scientist, DTU Aqua, Denmark 
Andre Visser - Professor, DTU Aqua, Denmark 
Marja Koski - Senior Research Scientist, DTU Aqua, Denmark 

How to apply: 
Send an email indicating your interest and willingness to participate to Prof. Sebastian Chenyambuga ([email protected] / [email protected]) and copy to Dr. Hieromin Lamtane ([email protected] / [email protected]). Please indicate your official name, department and occupation (i.e. PhD student/Lecturer). 

Deadline for receiving applications: 5 th October 2015. 

Selected participants will be informed by e-mail on 9 th October 2015.

Source: http://www.suanet.ac.tz/phocadownload/statistical.pdf

Mfalme Letsie III aanza ziara Tanzania


Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamilius Membe (Mb.), akisalimiana na Mfalme Letsie III wa Lesotho, muda mfupi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, kabla ya kuelekea Jijini Arusha kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa Dunia kuhusu Uimarishaji wa chakula (Global Summit on Food Fortification, na kuanza ziara ya siku tatu kuanzia leo 08 hadi 11 Septemba 2015.


Mhe. Bernard Membe (Mb), akifanya mazungumzo na Mfalme Letsie III wa Lesotho, kabla ya kuelekea Jijini Arusha kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa Dunia kuhusu uimarishaji wa chakula (Global Summit on Food Fortification).

Taarifa ya NEC: Maamuzi ya rufaa za Wabunge na Madiwani

Taarifa ya DAWASCO kuhusu tuhuma za kumwaga maji taka

SHIRIKA la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) limewatahadharisha wananchi kuepuka taarifa za uzushi zilizoripotiwa na vyombo kadhaa vya habari juu ya usambazaji maji machafu kwenye line za mabomba ya wateja wa Dawasco.

Akizungumza na gazeti hili, Kaimu Meneja Uhusiano wa Dawasco , Bi Everlasting Lyaro alisema taarifa hizo za uzushi zimesambazwa na watu wachache ili kuchafua taswira ya shirika hilo na pia kuihusisha Dawasco moja kwa moja na mlipuko wa kipindupindu ulioingia jijini.

“Tunawatahadharisha wateja wetu kuwa ubora wa maji unaozalisha na Dawasco unakidhi vigezo vyote kwa matumizi ya binadamu na viumbe hai, hatuwezi kuzalisha maji yenye kuleta madhala kwa wananchi kwani hata haki za binadamu haziruhusu kufanya hivyo ” alisema Lyaro.

‘Ukweli wa maeneo yanayolalamikiwa kama vile Ilala mitaa ya Sharif shamba na Buguruni ni kuwa kuna kampuni za uchimbaji mifereji bado hatujabaini kama ni ya watu binafsi au za Manispaa. Wao walichimba mifereji ya majitaka karibia na mabomba ya wateja walio na line za Dawasco za majisafi hivyo kutiririsha majitaka kwenye mfumo wa majisafi. Ikapelekea maji machafu kuingia kwenye line zao na kupelekea mabomba ya maji yanapofunguliwa zinakutana na yale maji machafu yaliyokatwa kutoka kwenye mifereji” aliongezea Lyaro.

Alisema kuwa baada ya kupokea malalamiko hayo tulichukua hatua kadhaa moja ni kuchukua sampuli za maji hayo na kwenda kuyapima na kurudi kufunga maji hayo yasiendelee kutoka. Baada ya upimaji sampuli ile na kukuta siyo salama tulitenga line (isolate) ya majisafi ya Sharif Shamba hadi hapo tatizo litakapotatuliwa na mamlaka husika.

Tuhuma za Dawasco kusambaza maji machafu ziliripotiwa mapema wiki hii huku zikihusishwa zaidi na athari za ugonjwa wa kipindupindu unaoendelea kushika kasi jijini Dar.

Dr. Mazrui to teach Kiswahili at Carleton, Canada

Dr. Abdulwahid Mazrui
Dr. Abdulwahid Mazrui
The School of Linguistics and Language Studies is pleased to announce that they have added an impressive new member to their team. Dr. Abdulwahid Mazrui (PhD, Indiana University), co-author of the prominent book Swahili: A Complete Course for Beginners, will be teaching two introductory Kiswahili courses for 2015-2016 academic year – LANG 1010A, Intro to Language 1: Kiswahili (Fall) and LANG 1020A, Intro to Language 1: Kiswahili (Winter).

These courses will cover oral skills and basic reading and writing skills. There will also be an important emphasis on cultural practices of Swahili-speaking people.

Kiswahili (which is the Swahili word for the language, although it is increasingly used in English as well) is one of many Bantu languages spoken by more than 60 million people throughout central and eastern Africa, and is an official language of Kenya, Tanzania, Uganda, and the Democratic Republic of the Congo. It is also an official language of the African Union and is the second language of some 135 million more people, making it the most widely used language in sub-Saharan Africa. Remarkably, the 2006 Canadian Census reported 27,795 Ki-Swahili speakers were living in Canada.

Kiswahili has had an interesting evolution that spans centuries. Although it is African in origin, the language has been influenced by contact with Arabic, Persian, German, Portuguese, English, and French.

Much like the language he teaches (which is also his first language), Dr. Mazrui’s career path has had a significant global flavour.

“I was born and raised in a small island off the eastern coast of Africa called Pemba, which is part of Zanzibar in Tanzania, explains Mazrui. “I started teaching Kiswahili to Peace Corps volunteers in Tanzania in 2002. I then went to Indiana University for about 10 years to teach Kiswahili and did my postgraduate studies there as well and also taught Kiswahili at University of Illinois at Urbana-Champaign.”

Mazrui has been passionate about teaching language to others for as long as he can remember. As a multi-lingual individual, he is aware of the challenges of learning a new language, but is also very familiar with the sense of triumph and reward attached to acquiring a new dialect.

“English was my favorite subject. So much so that I wanted to learn English so that I could teach others. I also learnt Spanish while I was in high school and had a firsthand experience in learning a totally foreign language in Zanzibar. This has helped me a lot in my teaching.”

Upon completing his PhD in Linguistics at Indiana University, Mazrui moved to Ottawa with his family. He is thrilled to be sharing Kiswahili with students at Carleton. Mazrui, whose research interests include Sociolinguistics, Second Language Phonology, Second Language Acquisition and African Literature, is known for his teaching dynamism – often implementing creative methods and techniques to teach the particularly challenging aspects of a given language.

He sees many advantages for Carleton students who are interested in acquiring Kiswahili.

“Kiswahili is one of the widely spoken language in Africa. It is a very useful and an instrumental language for those who want to do research in that region.”

“The language also has some very interesting linguistics features to research. One of the many reasons it is fun to teach Kiswahili is to watch as students realize that they already know some Kiswahili words. Students tend to pick up Kiswahili rather quickly because it is written just as it is spoken.”

He added, “the students will be more familiar on the unique culture of the Swahili people and of the Swahili speaking countries. This hopefully widens their interest in the areas where Kiswahili is spoken.”

Having Dr. Mazrui on its roster is yet another reason that The School of Linguistics and Language Studies at Carleton University has earned its reputation as world-class language learning institution. Dr. Mazrui joins a small army of some 40 passionate full and part-time language instructors in the Modern Languages program, teaching American Sign Language, Anishinaabemowin (Ojibwe), Arabic, Chinese, German, Italian, Japanese, Korean, Portuguese, Russian and Spanish.
  • Source: carleton.ca (shared to us by a fellow wavuti.com reader)

Eight Africa's Ministers of Energy &Finance in Beijing to outline current investment opportunities

aipf.jpg

PRESS RELEASE

‘2015 – a turning point for Africa and Foreign Direct Investment.  8 of Africa’s Ministers of Energy and Finance gather in Beijing to outline current investment opportunities’

The 4th Annual Africa Infrastructure and Power Forum will take place in Beijing, China 15-16th October 2015

BEIJING, China, September 9, 2015-- 2015 marks a turning point for African investment. The need to address the continent’s energy deficit, and the critical requirement to connect those living without access to electricity, is undisputed - 13% of the world’s population live without electricity, versus 48% of the global population who live in Africa. 

This year Africa will have witnessed 19 elections, and the formation of many new governments. Many of these administrations will seek to improve living conditions through access to electricity, and subsequently, added employment opportunities. Despite the headwinds caused by lower oil and commodity prices, and weakening currencies across sub-Saharan Africa, progress continues to be made.  Nigeria witnessed the most notable investment deal in recent weeks, with Africa’s largest privately held business – Dangote - signing a $4.34 billion deal with China’s Sinoma, an indication of Nigeria's infrastructural ambition.  In the same period, another of the world’s fastest-growing economies, Kenya, has earmarked $55.6 billion for infrastructure development. Kenya’s road network urgently needs improvement - essential for trade and tourism, indispensable lines of inward investment. 

Global investor demand for African opportunities were displayed this month when one of the world’s largest private-equity funds - The Abraaj Group - announced it had raised $1.4 billion, indicating the dawn of billion-dollar African private-equity funds searching for greater returns than offered by alternative, saturated markets.  Of 119 African investor deals, there has only been one default in the past decade. 

However, of all interested parties looking to invest in Africa this year, there has been one nation consistently seeking to improve infrastructure and power development on the continent - China.  As of 2011, China’s investment in Africa was 4.3% of its global trade (Asia represented 60.9%, Latin America 16% and Europe 11.1%).  By 2009, 45.7% of China’s cumulative foreign aid of $256.29 billion had been dispensed to Africa.

The growth of China-Africa trade is revolutionising African development, stimulating crucial upgrades of the continent’s infrastructure and power development - highlighted in June when Tanzania awarded a consortium of Chinese railway companies projects valued at $9billion. 

EnergyNet are delighted to announce the 4th Annual Africa Infrastructure and Power Forum (http://www.africa-infrastructure-forum.com), taking place in Beijing, China 15-16th October 2015.  This important meeting once again partners with the China Africa Development Fund, who will be seeking new projects to receive some of the $5billion under their management.

Standard Bank, Africa’s largest bank, will be joining the meeting this year as forum sponsor.  David Humphrey, Head of Infrastructure and Power, Standard Bank, recently commented that “the conference brings together some of the foremost figures in infrastructure, as well as key policymakers from Africa. Continued and increasing investment in infrastructure is crucial to the development of African nations, and Standard Bank is well placed to play a leading role in connecting investors with opportunities across the continent.  We are delighted to be sponsoring the conference for the second year in a row, and we look forward to seeing our customers and stakeholders in Beijing.”

At the Forum there will be 11+ project presentations featuring major opportunities, including:
•          The East to West Landbridge - LAPSSET Corridor
•          East African Standard Gauge Railways
•          Dry port development in Ghana
•          Unbundling of state utilities in Liberia
•          Gas-to-Power investment opportunities in Mozambique and South Africa.

We welcome the following high-level speakers:
1.         H.E Hon, Henry Rotich, Cabinet Secretary for the Treasury, Kenya
2.         H.E. Hon. Matadi Atadi Nenga Gamanda, Minister of Energy and Water Resources, DR Congo
3.         H.E. Hon Christopher Yaluma, Minister of Energy, Zambia
4.         H.E. Hon Henry Macauley, Minister of Energy, Sierra Leone
5.         H.E. Hon James Musoni, Minister of Infrastructure, Rwanda
6.         H.E. Hon Obeth Kandjoze, Minister of Energy and Mines, Namibia
7.         H.E. Hon Aston Kajara, Minister of Finance in charge of Privatisation, Uganda
8.         Honourable Maria Kiwanuka, Senior Advisor to the President, Uganda
9.         Silas Zimu, Presidential Special Advisor on Energy, South Africa
10.       Chairman Mingqiang Bi, Chairman of the Board of ICBC Standard Bank PLC
11.       Madam Shen Min, Deputy General Manager, Special Financing Department, ICBC Bank

For more information on how to get involved in this meeting, please contact:
Meeting dates: 15-16th October 2015
Venue: Ritz Carlton hotel, Beijing
Contact: Amy Offord, Marketing Manager

Ahadi za CCM: Umeme kila kijiji Ruvuma, viwanda vya mahindi, kahawa

Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini, Martin Mtonda (kushoto) na mgombea udiwani wa CCM.

MGOMBEA mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu ameanza ziara yake mkoani Ruvuma akiinadi ilani ya chama hicho huku akiahidi neema kwa wakulima wa kahawa na mahindi wa mkoa huo.

Bi. Samia Suluhu ambaye amehutubia mikutano mitatu katika majimbo mawili ya mkoa wa Ruvuma yaani Jimbo la Nyasa na Mbiga Vijijini, akizungumza katika mikutano yake amesema serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda itahakikisha inashusha umeme katika vijiji vyote vya mkoa huo kwa awamu ili kuchochea maendeleo ya wananchi.

Alisema kwa kuwa mkoa huo unazalisha mazao ya mahindi na kahawa serikali itahakikisha inaanzisha viwanda eneo hilo vya kusaga na kuandaa unga wa mahindi kwa wakulima na kuwawezesha ili wauze unga na kunufaika zaidi tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo wamekuwa wakilanguliwa.

Alisema viwanda vingine ambavyo Serikali ya CCM itavianzisha ni pamoja na viwanda vya kubangua kahawa na kuiandaa kikamilifu tayari kwa kutumika, jambo ambalo alisema licha ya kuongeza thamani ya zao hilo itaongeza ajira kwa vijana na kuchochea uchumi wa wakulima eneo hilo.

Akizungumzia miundombinu ya barabara ambayo bado ni changamoto kwa mkoa huo hasa vijijini alisema serikali itakayoundwa na CCM chini ya uongozi wa Dk. John Pombe Magufuli pamoja na yeye watahakikisha wanajenga na kuboresha barabara za maeneo hayo ili ziweze kupitika kwa uhakika.

Hata hivyo kiongozi huyo amesema Serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015 imejipanga kuboresha vizuri huduma za afya kuondoa ukiritimba na rushwa, elimu kwa kutoa elimu bure toka darasa la kwanza hadi kidato cha nne pamoja na ujenzi wa mabweni na uwezeshaji vijana na akinamama kiuchumi popote walipo mjini na vijijini.

Ziara ya mikutano ya kampeni ya mgombea mwenza huyo wa urais tiketi ya CCM, inaendelea leo katika Mkoa wa Ruvuma na ataingia Jimbo la Tunduru kuendelea kuinadi ilaya ya chama hicho kuomba ridhaa kwa wananchi ili waweze kurejeshwa madarakani na kuunda dola.


Pichani juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.


Pichani juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.


Baadhi ya wananchi na wanaCCM wa Kijiji cha Maguu wilayani Mbinga wakimsubiri mgombea mwenza wa urais, CCM, Bi. Samia Suluhu.


Pichani juu ni baadhi ya pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zilizompokea mgombea mwenza wa CCM urais, Bi. Samia Suluhu mara baada ya kuingia Wilaya ya Mbinga zikiwa zimeegeshwa pembeni huku mkutano wa hadhara ukiendelea.


Mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya mgombea mwenza, Bi. Asumpta Mshama akizungumza na wanaCCM na wananchi (hawapo pichani) katika Kijiji cha Maguu, Wilaya ya Mbinga.


Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (kulia) akizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu, kabla ya kuanza kuhutubia katika mikutano wake wa kampeni.


Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM ambao ni wenyeji wake mkoa wa Ruvuma.


Mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na mmoja wa vijana walemavu waliohudhuria mkutano wake wa hadhara Kijiji cha Maguu. Bi. Suluhu alimsaidia fedha kijana huyo.