[update] Agizo la TCRA kwa watoa huduma za utangazaji

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UFAFANUZI WA TANGAZO LILILOTOLEWA TAREHE 11 SEPTEMBA, 2015 KUHUSU VIPINDI VINAVYORUSHWA MOJA KWA MOJA WAKATI WA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu tangazo lake lililotolewa kwenye vyombo vya habari tarehe 11 Septemba, 2015 kuhusu vipindi vinavyorushwa moja kwa moja wakati wa kampeni za uchaguzi
mkuu. 

Ufafanuzi huu unatolewa kutokana na maoni mbalimbali ya wadau wakitaka ufafanuzi kuhusu tangazo hilo.

Mamlaka inatoa ufafanuzi kama ifuatayo:-

a) Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015 ni Kanuni mbayo ipo kwa mujibu wa Sheria kama ilivyotolewa na Gazeti la Serikali la Tarehe 26 Juni, 2015. Kanuni hizi zinalenga kuweka utaratibu mzuri wa kutangaza shughuli za kampeni na
uchaguzi mkuu kuwa wa amani na utulivu;

b) Wadau wa sekta ya utangazaji walishirikishwa katika maandalizi ya Kanuni hizi wakiwemo vituo vya utangazaji tarehe 28 Oktoba, 2014, Mitandao ya kijamii tarehe 11 Novemba, 2014, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo tarehe 19 Desemba, 2014 na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 14 Aprili, 2015;

c) Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inasisitiza kuwa vyombo vinavyotoa huduma ya utangazaji vina wajibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu uchaguzi bila ubaguzi ili wananchi wenyewe waelimike na hatimaye wafanye maamuzi sahihi kwa hiari yao kuchagua kiongozi anayefaa;

d) Mamlaka inafafanua na kusisitiza kuwa vyombo vya utangazaji vinakumbushwa kuzingatia Kanuni za Huduma za Utangazaji ISO 9001:2008 CERTIFIED (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015, hususani Kanuni zifuatazo;-

4. Kila mtoa huduma za maudhui atahakikisha kwamba:-

(f) haruhusu utangazaji wa jambo lolote linalohamakisha na kuwagawa watu katika hali ya uchochezi;

(h) Utangazaji wa chaguzi unadhamiria kusisitiza ustahiki wa chaguzi na kuhimiza ushiriki wa wananchi wote katika mchakato wa uchaguzi;

(i) wakati wa kipindi cha chaguzi habari zilenge juu ya masuala muhimu na yenye maslahi kwa wananchi sio tu kutangaza matukio ya vyama vya siasa au wagombea;

5. Kila mtoa huduma za maudhui atahakikisha kwamba vipindi na uwasilishaji wake:-

(b) haujihusishi na kumkashifu au kumuumbua mgombea au mtu mwingine yeyote au kauli mbaya juu ya uadilifu wa mtu;

(d) kipindi kisiwe na lugha ya kashfa, chuki au kufuru au lugha yoyote (au toni ya lugha) inayoweza kuchochea vurugu au maasi;

(e ) kipindi kisiwe na kauli zinazoweza kumuudhi mtu yeyote kwa sababu ya jinsia, jinsi, mbari, rangi, tabaka, imani au mahali pa asili.

(f) matangazo ya vyama vya siasa yatakuwa yale tu ambamo vyama vinajitahidi kuelezea sera, mipango na malengo yake.
Hivyo basi, haikuwa lengo la taarifa hiyo kumzuia mtu yoyote kushiriki vipindi vya moja kwa moja (live Programmes) iwapo Kanuni zilizotajwa hapo juu zitafuatwa na kuzingatiwa.

Vituo vya utangazaji vinatakiwa kufuata kikamilifu Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015 na kwamba vituo vya utangazaji vitawajibika na matokeo ya maudhui ya matangazo ya moja kwa moja ambayo hayatozingatia Kanuni.

Mamlaka inatoa wito kwa vituo vya utangazaji kutumia weledi katika maamuzi ya kihariri kuchanganua kipi kinafaa kutangazwa kwa maslahi ya Taifa.

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAREHE 13/09/2015

-----------------

TAARIFA KWA WATOA HUDUMA ZA UTANGAZAJI

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa taarifa kuwa kuanzia leo tarehe 10 Septemba 2015, na katika kipindi chote cha kampeni za uchaguzi mkuu 2015, watu ambao sio wagombea wa udiwani, ubunge, urais, wasemaji rasmi wa vyama au watu wasioteuliwa na vyama vya siasa kama wawakilishi hawataruhusiwa kushiriki katika vipindi vya moja kwa moja (Live Programmes) vinavyohusu shughuli za uchaguzi vitakavyorushwa na vituo vya utangazaji.

Utaratibu huu unazingatia Kanuni Za Huduma Za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji Wa Uchaguzi Wa Vyama Vya Siasa), 2015, Kanuni ya 4 (f), (h), (i), 5(b), (d), (e) and (f).

Hatua hii inachukuliwa na Mamlaka ili kuweka utaratibu mzuri wa kufanya kampeni za uchaguzi ziwe za amani na utulivu.

Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya kituo cha utangazaji kitakacho kwenda kinyume na utaratibu huu..

IMETOLEWA NA:
Mkurugenzi Mkuu
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

Tarehe 11/09/2015

Wapandishwa kizimbani kwa kutengeneza tovuti za kutapeli wakitumia majina ya taasisi, viongozi, wanasiasa

SUSPECTED Designers of Fraudulent Credit and Loan Websites, Maxmillian Rafael Msacky (second left) and Patrick James Natala (third right) at the Kisutu Resident Magistrate’s Court in Dar Es Salaam on Friday, 11 September 2015, faced with 10 charges including producing Fake Websites identified as “Jakaya Kikwete Foundation (State House), TCRA Foundation, AkibaSaccos Social Company, Social Credit and Loans Company, Ridhiwani Social Company, Hisa Tanzania, Zitto Kabwe Foundation, Vicoba Tanzania and Wekeza Fund”.The suspects who also allegedly used fake names to register SIM Cards denied all charges before Resident MagistrateEmelliusMchaulo and remanded until 24th September 2015 when the case comes up for another mention.
(Photo: TCRA)

Watu wawili, Patrick Natala na Maxmillian Msacky wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 10 yakiwamo ya kughushi, kutengeneza tovuti feki na mifumo ya mtandao kwa kutumia majina ya Taasisi, viongozi na wanasiasa.

Akiwasomea hati ya mashtaka leo Wakili wa Serikali, Theophil Mutakyawa akishirikiana na Wakili Mwandamizi Mkuu wa TCRA, Johannes Kalungura walidai kuwa washtakiwa hao walitengeneza tovuti feki kwa kutumia majina ya Taasisi ya Jakaya Kikwete Foundation (Ikulu), TCRA Foundation, Akiba Saccos Social Company, Social Credit and Loans Company, Ridhiwani Social Company, Hisa Tanzania, Zitto Kabwe Foundation, Vicoba Tanzania na Wekeza Fund.

Mutakyawa amedai kuwa washtakiwa hao wametengeneza tovuti hizo feki kati ya Januari na Aprili 2014 jijini Dar es Salaam kinyume na kifungu cha 122 (b) cha sheria ya Kielektoliniki na Mawasiliano ya Posta namba 3 ya 2010.

Mbali na mashtaka hayo, Mshtakiwa Msacky yeye anadaiwa kuwa kati ya 2006 na 2024 kwa njia ya udanganyifu alighushi cheti cha Sekondari namba 0421130 chenye indexi namba S 0260-0001.
Iliendelea kudaiwa kuwa kati ya 2005 na 2014 mshtakiwa huyo alighushi cheti kingine cha Sekondari namba 0217951 chenye indexi namba S 0310-0532,akionyesha ni halali na kwamba vimetolewa na Baraza la Mitihani Tanzania wakati akijua kuwa ni uongo.

Washtakiwa hao wamekana mashtaka na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi bado haujakamilika na washtakiwa kupelekwa rumande hadi Septemba 28, 2015 itakapotajwa.

Akizungumzia tukio hilo, Mkurugenzi wa Sheria wa TCRA, Elizabeth Nzage amesema kati ya Aprili na Juni katika mwaka wa fedha wa 2014/2015 walipata malalamiko toka kwa wananchi kuhusu kuwepo kwa makampuni feki yaliyokuwa yakidai kuwa yanatoa mikopo kwa muda mfupi.

Nzage amedai kuwa wahusika hao walitumia majina ya wanasiasa na pia kujifanya ni viongozi na wamiliki wa taasisi hizo na kwamba makumpuni hayo yanaandaa shughuli za kuchangisha fedha.
  • (Taarifa ya mandishi: Mwananchi)

Salma Moshi awalipia wasanii Bima ya Afya katika Jukwaa la Sanaa

Mwandishi maarufu Khadija Khalili (mwenye daftari) akifuatilia mada

Jukwaa La Sanaa la BASATA wiki hii lilipata wazungumzaji wa aina yake na kulifanya kuwa jukwaa lililochangamka na kuwa na mazungumzo ya zaidi ya masaa matano. Wasanii takriban 70 walikaa wakichambua maada mbalimbali kuhusu mustakhabari wa sanaa katika nchi yetu. Jambo ambalo liliingiza changamoto katika jukwaa hili, ni kuweko katika meza kuu wasanii wawili ambao walianza sanaa nchini na hatimae kuhamia ughaibuni ambako ndiko wanaishi kwa sasa.

Wasanii Salma Moshi aliyekuwa akijulikana kama Salma Nyoka, msanii wa kwanza wa kike kuchezea nyoka katika jukwaa, na ambaye alikuwa kiongozi wa vikundi vilivyotamba kama DDC Kibisa Cultural Troupe Super Mama Cultural Troupe na Ujamaa Cultural Troupe, na Abbu Omar, mwanamuziki aliyewahi kupigia bendi kama Urafiki na UDA Jazz ambae kwanza alihamia Kenya na kupiga na kurekodi na makundi kama Simba wa Nyika na Les Wanyika na pia kurekodi album kadhaa akiwa na kundi lake ambaye hatimae alihamia Japan ambako amekuwa akiishi kwa kupiga muziki na akiwa na waTanzania wengine kama Lista na Fresh Jumbe.

Mazungumzo yaligusia nyanja mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kuwa na mikataba kabla ya kazi, kuboresha kazi ili kuweza kuuza nje, namna ya kujitambulisha duniani kwa kuwa na websites na blogs, na pia serikali kubadilika na kuweko mfumo wa uongozi wa sanaa kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa. Katika mkutano huo, John Kitime Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki aliongelea fursa ya Bima ya Afya kwa wasanii, ambapo Salma Moshi alijitolea kuwalipia nusu ya ada wasanii wanne, na kumlipia bima kamili Mzee Kassim Mapili ambaye kwa sasa anasumbuliwa na moyo na figo. Abbu Omar pia aliamua kulipia Bima yake na kueleza kuwa katika nchi ya Japan ni lazima kila mwananchi kuwa na Bima ya Afya, kwani ugonjwa hauji kwa taarifa na matibabu ni gharama kubwa.

Mkutano huo ulianza saa tano na kulazimishwa kusimamishwa saa kumi, kwani wasanii bado walikuwa na mengi ya kuwauliza wasanii hawa nguli walioweza kuendeleza maisha ughaibuni kupitia sanaa.


Mwenyekiti wa CHAMRUMBA akiwa na Mzee Mapili


Salma Moshi na Mzee Mapili


Abbu Omari mwanamuziki aishiye Japan


Salma akiwa na baadhi ya wasanii aliowalipia sehemu ya Bima ya Afya

Nyerere: How much does the President earn?


The President doesn't earn $192,000 per month. How much does he earn?


State House has refuted claims that President Jakaya Kikwete earns $US192,000 as salary per month. I thought the statement would say how much he actually earns. It did not. That, apparently, is within the legal protection enjoyed by public servants that maintains that salaries of public servants is confidential information.

Despite that, I note that the press release mentions that the newspaper that published the erroneous information could have used proper channels to obtain accurate information. And that is a change from the past when it appeared to me that any citizen inquiring about a public official's pay would have been told to find some other work to do.

Opposition presidential candidate Edward Lowassa is promising to slash the presidential salary considerably if elected in October's general elections although I do not know whether voters should read more politics than resolve in his promise.

I thought I should write something about my attitude on the secrecy surrounding these salaries but realised I had already written about it in 2013. Here's what I wrote then. What is your opinion?

We all have at least someone in our lives in The Dunning–Kruger effect


The Dunning–Kruger effect is a cognitive bias wherein relatively unskilled individuals suffer from illusory superiority, mistakenly assessing their ability to be much higher than is accurate. Conversely, highly skilled individuals may underestimate their relative competence, erroneously assuming that tasks that are easy for them also are easy for others.