Mnyororo wa utajiri


Ngoja niwape mchapo halafu nitaendelea kidogo. Jana nilikwenda mtaa mmoja hapa Iringa mjini unaitwa Wilolesi. Huko nilikwenda kutazama kiwanja ambacho kinauzwa. Nilipofika kulenikaonana na bwana mmoja ambae huwa ninaonana nae mjini mara kwa mara; na ndie muuzaji wa eneo hilo. 

Kiwanja hiki alipewa na babu yake ambae alishafariki miaka ya nyuma. Alinieleza kuwa anakiuza sio kwa sababu nyingine isipokuwa anataka fedha ili akanunue nyumba nyingine huko Dodoma. Anyway, kilichonifurahisha ni historia ya eneo hilo. Alikuwa muwazi, kuwa babu yake alikinunua mwaka 1982 kwa shilingi elfu sita kutoka kwa mwenyeji mmoja. Leo hii anakiuza kiwanja hicho milioni 470! Nilichoka! Pointi ni nini hasa?....ni kwamba; kuna mambo ambayo ukiyatenda leo wajukuu zako watakuja kuchekerea, lakini kuna mambo usipoyafanya leo basi watoto na wajukuu zako watakuja kutukana kaburi lako na kuuliza ulikuwa unawaza nini wakati .

Nilipoishia nilitoa mfano wa Yesu Kristo uliohusu talanta, ya kwamba kuna ambae alipata talanta 5, mwingine 2 mwingine 1. Nikaeleza kwamba kuna mantiki ya makundi matatu ya watu katika mfano huo. Yaani wafanyakazi, wafanyabiashara na wale walio iddle a.k.a wasio na kazi...

Kwanza niwafahamishe kwamba ni kosa kiimani, ni kosa kijamii na tena ni kitokwenda sawa kwako binafsi kusema ama kudhani kwamba hakuna kitu cha kufanya, kusema hakuna fursa, kusema hakuna ajira, kusema mshahara ni mdogo na hata kudhani kwamba hakuna njia ya kutokea...

Kwa nini ni kosa? Ni kwa sababu Mungu alipoumba dunia hakukuwa na serikali hii ina maana alitaka ufanikiwe hata pasipo serikali. Kulalamikia serikali kutokukumbuka kwa ajira ama mshahara mdogo, itabidi upigwe viboko!...

Tuache hapo kidogo hebu twende kwenye wafanyakazi na wafanyabiashara. Usisahau kuwa tunaongelea mnyororo wa utajiri. Na ninarudi kwenye mfano wa talanta kidogo. Huyu investor alietoa hii mitaji (talanta) aliwaambia wale waliopewa kwamba wafanye biashara wazalishe faida.

Nini kilitokea? Jamaa mwenye 5 akazalisha nyingine tano na jamaa mwenye 2 akazalisha nyingine 2 maana yake wali double mitaji, right?! Haya hebu tumcheki huyu aliepewa moja. Huyu jamaa aliepewa moja akaenda kufukia eti kwa madai kwamba talanta moja haitoshi kufanya chochote cha maana! Sikiliza mwenye talanta alichomwambia, akamwambia "ulishindwa kuweka talanta hii moja hata kwa watozao riba?" Usichoke ati na huu mfano, nakuja sasa kwenye pointi ninayotaka uinyake. Kwa lugha nyingine ni kwamba badala ya kufukia tu hela aliyopewa(ile talanta) ingekuwa jambo la maana angeiweka kwa hao watozao riba a.k.a benki. Ngoja nitokee hapa kukupeleka ninapotaka ufike.

Hivi si unafahamu kazi ya benki? Okei, kazi ya benki ni kuwakutanisha wenye hela lakini hawana mawazo na wale wenye mawazo isipokuwa hawana hela; kwa kuwakutanisha huko benki inazalisha faida kupitia alieweka hela benki na uthubutu wa aliekwenda kukopa benki. BENKI inampa nini anaeweka hela benki? Inampa kitu kiitwacho riba ambayo ni ndogo ukilinganisha na thamani ambayo ile hela inazalisha.

Hebu pozi kidogo! Hebu rudi kidogo kwenye ule mfano wa talanta, halafu tujiulize swali: kwa nini yule bwana aliewapatia jamaa zile talanta hakuwapa option ya kuziweka hela benki(kwa watozao riba)? badala yake tunaisikia hiyo option mwishoni kabisa baada ya yule jamaa aliepewa talanta moja kushindwa kuifanyia chochote na kuifukia?

Hadi hapa tunaona kwamba kuweka hela benki ni kusema, "jamani.eheee mimi ni hela hapa ila nimeshindwa jinsi ya kuzitumia mimi kama mimi; hivyo naomba mnisaidie katika kufikiri namna gani zitumike".

Ukishawakabidhi, benki wanakupa masharti makali. Kwanza watakwambia ili tukupe riba fulani hela yako lazima ikae miezi mitatu, sita, tisa n.k. Yaani hata uwe na shida aje jamaa hawacheki na wewe, wanakula bati mpaka ule muda ufike. Kiufupi wanakuwa na urafiki na wewe unapoenda kuwapatia ila baada ya hapo wanaendelea kukunyanyasa mpaka utakapozitoa hela zako. Tupo jamani?....

Wengine wameshaanza, ohooo Sanga, unatuleta kwenye benki na wakati umesema unaongelea wafanyakazi nawafanyabiashara. Wangapi kati yenu mnafahamu kwamba neno talanta mbali na kumaanisha fedha pia linamaanisha kipaji/karama/uwezo/maarifa n.k?

Naamini wengi mnaelewa. Kwa hiyo unapokuwa na kipaji/karama/uwezo/maarifa; una machaguo matatu. 1) Kufanya biashara 2) Kuweka kwao watozao riba 3) Kufukia ama kukaa bila kufanyia chochote. Sijui mnanipata? Ngoja nitoe mfano: ukisomea ualimu unakuwa umepata uwezo/ujuzi/ wa kufundisha, right? Basi hapo una options tatu: kuufanyia biashara ujuzi huo, kupeleka ujuzi wako kwao watozao riba ama kupotezea uwezo wako (kukaa bila kufanya chochote).

Sasa tuje hapa. Unapochukua vyeti vyako vya ualimu na kwenda kutafuta ajira, maana yake ni kwamba umepeleka ujuzi wako kwao hao watozao riba! Yaani ni kwamba umeshindwa kufikiria cha kufanyia ujuzi wako hivyo umeona ni bora umkabidhi mwajiri afikirie namna atakavyotumia ujuzi wako, huku akikupa riba kidogo.

Riba ni mshahara na wote tunafahamu kuwa mishahara ni kasehemu kadogo ka thamani unayozalisha hapo kazini. Yaani wewe huna tofauti na yule alieweka hela benki kwa miezi mitatu akilipwa riba ya asilimia 3 wakati benki wanazalisha faida ya asilimia 18 hadi 30 kupitia hela yako hiyo hiyo. Ujuzi wako, profeshno yako, umeamua kuikabidhi kwao hao watozao riba, a.k.a waajiri! Tunakwenda sawa?

Sasa nakuuliza swali la ufahamu. Unadhani ni kwa nini options ya kuweka talanta benki haikushauriwa miaka 2000. Kwani unadhani kuweka hela benki ni vibaya? Wala hata siyo vibaya! Ahaa, labda hujaelewa. Je, unadhani kuukabidhi ujuzi wako kwa watozao riba a.k.a waajiri ni jambo baya? Akhuuu! Wala sio baya! Lakini unajua kwa nini? Ni kwamba sio option ya kwanza ya mashujaa. Naomba niishie hapa kwa leo. Nitaendelea ili niconnect na ufanyabiashara, ufanyakazi na namna unavyotakiwa kutoka.
Asanteni sana kwa kunisikiliza, tuonane wakati ujao.

Albert Sanga. 
Iringa

Misingi 6 iliyo siri ya watu wenye mafanikio ya kudumu

Ili uweze kufanikiwa, ni lazima kujiwekea misingi imara ya kimafanikio itakayokuwa ikukuongoza kila siku. Bila kuijua misingi hii mapema sitashangaa kuona maisha yako yakibaki kuwa yaleyale bila ya kubadilika sana. Kwa kujiwekea misingi hii, inauwezo wa kufanya maisha yako kubadilika kwa sehemu kubwa sana.

Kama misingi hiyo ipo, ni nini kinachokuzuia wewe kufanikiwa sasa? Bila shaka hakuna. Unachohitajika kukifanya ni kutumia misingi hiyo mpaka kufanikiwa. Uwezo na nguvu za kubadilisha maisha yako kwa kadri unavyotaka unao. Kwa kuijua misingi hii, kwako itakuwa chachu ya kukusaidia kuweza kusonga mbele na kujijengea maisha ya mafanikio makubwa:-

Je, misingi hiyo ni ipi?

Hii Ndiyo Misingi 6 Muhimu Ya Kujiwekea, Ili Kujenga Mafanikio Ya Kudumu


1. Kaa mbali na watu hasi


Kama vile ambavyo ilivyo kompyuta inaweza ikaharibiwa na virusi na kuharibika kabisa, hata wewe maisha yako yanaweza kuharibiwa vivyohivyo lakini ikiwa una watu hawa hasi wengi wanaokuzunguka. Unapokuwa na watu hasi inakuwa ni rahisi sana kwako kuweza kuua mipango na malengo mazuri uliyojiwekea.

Ninajua watu hawa wanaweza wakawa ni rafiki zako au ndugu kabisa, lakini hiyo haina namna tena kwako, zaidi ya kuachana nao. Ikiwa utaendelea kung’ang’ania kuwa na watu hawa hasi utarudishwa nyuma sana katika maisha yako. Ili kuokoa maisha yako ni lazima kukaa mbali nao na kutafuta marafiki chanya watakaokupa hamasa ya kufanikiwa zaidi. Kukaa mbali na watu hasi ni msingi mzuri kwako unaotakiwa kuujua.

2. Wekeza kila siku katika maisha yako


Huu ni msingi muhimu sana kujiwekea ili kuwa na mafanikio ya viwango vya juu. Kama katika maisha yako unawekeza kila siku, tambua baada ya muda kidogo kuanzia sasa utakuwa mbali sana kimafanikio. Pengine unaweza ukaanza kusema ‘oooh mimi sasa sina pesa, sina mtaji hili halinihusu nitawekeza vipi sasa hapa?’

Sikiliza, hauhitaji kuwa na pesa ili kuwekeza. Anza na kuwekeza kwanza kwenye akili yako kwa kujifunza kupitia vitabu au semina mbalimbali. Maisha yako yatakuwa ya thamani sana kila utakavyozidi kufanya uwekezaji huu. Maarifa utakayoyapata huko kwani yataweza kukusaidia kuwekeza katika maeneo mengine na kufanikiwa zaidi pale utakapopata mtaji unaouhitaji.

3. Kuwa wewe kama wewe


Kuna wakati wengi wetu huwa ni watu wa kutaka maisha ya kuwapendezesha wengine. Nikiwa na maana kutaka kuishi maisha kama wengine wanavyoishi. Hiki ni kitu hatari sana kwako kwa sababu unakuwa unaishi kwa kufuata bendera ama wengine wanavyoishi na kujikuta unakuwa mtu wa kupoteza mwelekeo.

Ili uweze kuishi kwa mafanikio ni vizuri ukajijengea msingi wa kuishi maisha yako ukiwa wewe kama wewe. Kwa kuishi wewe kama wewe itakulazimisha kutambua unataka nini kwenye haya maisha, ni lini utafikia mipango yako uliyojiwekea na unataka kitu gani kikusaidie kufikia malengo yako. Huo ndiyo msingi muhimu pia kuujua kwa ajili ya mafanikio yako ya leo na kesho.

4. Jiwekee mipaka katika maisha yako


Ishi maisha yako kwa kujiwekea mipaka. Usije ukaruhusu kila mtu kuingilia maisha yako kwa jinsi anavyotaka hata awe ndugu wa karibu kiasi gani. Bila shaka umeshawahi kuona watu ambao maisha yao yanaharibiwa kutokana na kuingiliwa na watu walio karibu nao. Na hii yote imekuwa ikitokea kutokana na wahusika kushindwa kujiwekea mipaka iliyoimara katika maisha yao.

Mipaka hii unatakiwa ujiwekee katika maeneo mabalimbali kama vile katika muda, kazi zako za kawaida na wakati mwingine kwenye biashara zako unazozifanya. Kwa kufanya hivyo watu wako wa karibu watakuwa hawako huru sana kuingilia yale maeneo uliyojiwekea mipaka maana wakifanya hivyo watajua utakuwa mkali au hutakubali kiurahisi. Hiyo itakusaidia kukujengea msingi mwingine imara wa mafanikio yako.

5. Kuwa king’ang’anizi wa mafanikio


Kwenye maisha yako kitu ambacho hutakiwi kukiruhusu ni kushindwa kiurahisi. Kama ikitokea umeshindwa katika jambo kwa namna moja au nyingne, jaribu kutafuta njia ya kulifanya jambo hilo kwa namna ya tofauti mpaka kufanikiwa. Unapokuwa king’anga’nizi wa mafanikio huo utakuwa msingi bora kwako unaojitengenezea wa kufikia mafaniko makubwa.

Maisha ni kusonga mbele. Ng’ang’ania mafanikio yako mpaka uyaone hata kwa gharama yoyote ile. Usiruhusu kitu kikakukatisha tamaa. Kama unafikira za nyuma unazoziweza kwa kudhani kuwa ulikosea eneo fulani ni bora ukaachana nazo fikra hizo kwa sasa, kwa sababu hazitakusaidi kitu chochote zaidi ya kukwamisha wewe. Yaliyopita yamepita, songa mbele.

6. Jijengee ukomavu wa fikra


Ili uweze kufanikiwa inatakiwa ifike mahali fikra zako ziwe zimekomaa na kuweza kutambua kila hali inayojitokeza katika maisha na jinsi ya kuweza kukabiliana nayo. Kwa mfano, inapotokea kushindwa au ukakosea katika jambo fulani, unakabiliana vipi na kushindwa huko bila kuumia au kujiona hufai na kisha kuendelea mbele?

Hakuna kingine zaidi ya wewe kuwa na ukomavu fulani wa fikra utakaokuwezesha kusonga mbele. Ukomavu huu ni rahisi kuupata, utaupata tu ikiwa wewe ni mtu wa kujifunza mambo mbalimbali ya kimafanikio kama unavyofanya sasa hivi. Bila kufanya hivyo hutaweza kuhimili mawimbi mengi ya maisha yanayojitokeza kwa upande wako.

Kumbuka hii ni sehemu ya misingi ambayo unaweza ukajiwekea kama nguzo ya mafanikio yako. Lakini, kwa kutumia kijitabu chako kidogo cha kujifunzia unaweza ukaongeza misingi mingine ambayo unaona kwako inafaa kukuongoza katika safari ya mafanikio. Bila kujiwekea misingi binafsi, utayumbishwa sana katika maisha kwa mambo mengi na itakuwa ngumu kufanikiwa.

Tunakutakia kila la kheri katika safari ya mafanikio, endelea kuwashirikisha wengine kutembelea mtandao wa DIRA YA MAFANIKIO kila siku kwa kujifunza na kuhamasika zaidi.

Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,

"Mama Langa" Venus Kimei azindua kampeni za Udiwani Mikocheni


Hawaruhusiwi kutumia rasilimali za umma kwenye kampeni za kisiasa isipokuwa...

Katika ukurasa wa mbele na wa tano wa Gazeti la Nipashe, toleo 0578604 la tarehe 12 Septemba, 2015 kumechapishwa taarifa kwamba “Sefue; Marufuku kutumia magari ya serikali kwenye kampeni”

Katika taarifa hiyo, imeelezwa kwamba Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema “Ni kosa kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kutumia rasilimali za serikali yakiwemo magari katika mikutano ya kampeni ya Chama cha Mapinduzi (CCM).”

Alichosema Katibu Mkuu Kiongozi ni kwamba Watumishi wa Umma wakiwemo Wakuu wa Mikoa na Wilaya hawaruhusiwi kutumia rasilimali za umma yakiwemo magari kwenye kampeni za kisiasa isipokuwa wanapokuwa katika utekelezaji wa majukumu yao kiserikali.

Aidha, watumishi wa Umma wanaotaka kushiriki katika katika kampeni za kisiasa ama kugombea nafasi yoyote ya kisiasa sharti wajiudhulu nyazifa zao za utumishi wa umma.

Kupitia taarifa hii, Watumishi wa Umma na wa Kisiasa wanaombwa kuzipuuza taarifa hizo potofu zilizoandikwa na gazeti la Nipashe na wanashauliwa kufuata maelekezo yaliyomo kwenye Waraka wa Mkuu wa Utumishi wa Umma Namba 1 wa Mwaka 2015. Walaka huu unaeleza bayana utaratibu na jinsi Watumishi wa Umma wanavyoweza kushiriki katika kugombea ama kufanya kampeni za kisiasa na utaratibu pindi mtumishi wa umma anataka kugombea nafasi ya kisiasa.

Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo
13 Septemba, 2015

Habari iliyochapishwa katika gazeti la NIPASHE "Sefue: Marufuku kutumia magari ya serikali kwenye kampeni."

Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue amesema ni kosa kwa wakuu wa mikoa na wilaya kutumia rasilimali za serikali yakiwamo magari katika mikutano ya kampeni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kadhalika, Sefue amesema walimu katika vyuo vikuu vya umma wanaruhusiwa kufanya ama kujihusisha na masuala ya siasa kwa kuwa baadhi yao wanakuwa wanafanya utafiti.
Hata hivyo, kuhusu viongozi hao kutumia magari yao ambayo ni ya serikali katika mikutano ya CCM, Sefue alisema hajapata ushahidi kamili, lakini alisema ni kosa kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma.
Alitoa kauli hiyo baada ya baadhi ya wakuu wa wilaya na mikoa kuonekana katika misafara ya wagombea wa CCM wakifanya kampeni huku wakitumia magari ya serikali.
Pamoja na gazeti hili kumtajia baadhi ya mikoa na wilaya ambayo viongozi hao walionekana kutumia magari ya serikali kwenye kampeni za CCM, Sefue alisisitiza kwamba hajapata ushahidi.
Katika maeneo mbalimbali viongozi hao ambao kwa mujibu wa katiba ya CCM ni wajumbe wa kamati za siasa katika wilaya na mikoa yao, wameonekana katika mikutano ya kampeni za CCM, wakiwa na magari ya serikali yakiwa na nembo ya DC ama RC.
Akizungumza na Nipashe Ikulu juzi muda mfupi baada ya Rais Jakaya Kikwete kupokea tuzo mbili kutoka taasisi ya East Africa Book of Records ya nchini Uganda, Sefue alisema walimu katika vyuo vikuu ambao ni madokta na maprofesa, hawafungwi kushiriki siasa.
Hata hivyo, wakati Sefue akitoa ufafanuzi huo, Profesa Mwesiga Baregu aliwahi kusimamishwa kazi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kile kichodaiwa kujihusisha na siasa ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akiwa mjumbe wa kamati kuu.
Alisema watumishi wa serikali wameganyika katika makundi mbalimbali wapo wanaoruhusiwa kushiriki siasa na ambao hawaruhusiwi wakiwamo makatibu wakuu wa wilaya, yeye mwenyewe, lakini wapo ambao hawafungwi na kanuni hizo utumishi wa umma.

Here is the University of Cambridge engine that predicts your psychological profile using Facebook

Prediction results said Subi Nukta's age was 28 and more satisfied with life than 54% of the population.


If interested, you can check yours at applymagicsauce.com/test.html


Get rid of annoying toolbar from your computer with AdwCleaner


If your Windows computer has an annoying toolbar that can not easily be uninstalled, you can get rid of is using AdwCleaner.

AdwCleaner is a free removal tool for :
  • Adware (ads softwares)
  • PUP/LPI (Potentially Undesirable Program)
  • Toolbars
  • Hijacker (Hijack of the browser's homepage)
It works with a Search and Delete mode. It can be easily uninstalled using the mode "Uninstall".
It's compatible with Windows XP, Vista, 7, 8, 8.1, 10 in 32 & 64 bits.

Be sure you install the real AdwCleaner from toolslib.net because there is a fake AdwCleaner and you can learn more about it at howtogeek.com

[watch] Italy's struggle to process swelling tide of refugees


Mifugo ya Wamasai yaharibu mashamba ya wakulima Kilimanjaro


Gazeti la An-Nuur Septemba 11 - 17, 2015

Rais Kikwete ateua na kuhamisha wakuu wa mikoa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wakuu wawili wapya wa mikoa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wakuu wa Mikoa ambao wanawania ubunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue inasema kuwa katika uteuzi wake, Rais Kikwete amemteua Ndugu Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Ndugu Jordan Rugimbana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Aidha, Rais Kikwete amewahamisha wakuu wawili wa mikoa – Ndugu Mwantumu Bakari Mahiza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Ndugu Saidi Magalula ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitokea Mkoa wa Tanga.

Ndugu Magalula anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Stella Manyanya anayewania ubunge mkoani Ruvuma pia.

Ndugu Makalla ambaye alipata kuwa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Morogoro na Naibu Waziri wa Maji anachuku anafasi iliyoachwa wazi na ndugu Leonidas Gama ambaye anawania ubunge mkoani Ruvuma.

Ndugu Rugimbana ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Mahiza.

Uteuzi na uhamisho huo ulianza Jumamosi, Septemba 12, mwaka huu, 2015 na wakuu wapya wa mikoa wataapishwa kesho kutwa Jumatano, Septemba 16, 2015, Ikulu, Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

14 Septemba, 2015

Orijino Comedy: Masanja Mkandamizaji alivyomtambulisha Magufuli Tabora


Wimbo wa Taifa ulioimbwa na The Dar Choral Society & Orchestra


Song: Mungu Ibariki Afrika by Enock Sontonga
Arranged by Prof. Imani Sanga
Conducted by Hekima Raymond

Dk Barnabas: Serikali ijayo; Maboresho ama Mabadiliko?

(picha via twitter.com/sikika1)

“Mwaka ujao nitakuwa Jerusalem”
Waisrael waishio nchini mwao na wengine wengi waliotawanyika karibu kila pembe ya dunia hii wanao msemo wao maarufu usemao “Shana Haba B├Łerushalem” unaoaminika kuanza kutumika wakati wa Karne ya 11. Msemo huu hufasiriwa kwa Kiingereza kama “Next Year in Yerusalem” ama kwa Kiswahili cha haraka tunaweza kusema “Mwaka ujao nitakuwa Jerusalem”. Ijapokuwa usemi huu ni maarufu wengi wanakubaliana na fasiri ya kwamba mwaka ujao Jerusalem itajengwa upya na kuwa kitovu cha imani kwa watu wote duniani. Pia Jerusalem ya mwaka ujao ndipo ambapo Mwenyezi Mungu atajidhihirisha zaidi kwa wanadamu na watu wote wataishi kwa raha na furaha. Hivyo wanaamini na kutarajia kwamba mwaka ujao utakuwa bora kuliko mwaka unaoondoka. Hata hivyo sio Waisrael wote wanaokubaliana na fasiri hii ya msemo huu mkongwe na maarufu.
Tofauti ya mawazo na fikra za Waisrael juu ya msemo wao huu mkongwe na maarufu vinashabihiana na mawazo na fikra za Watanzania wengi katika maisha yetu ya kila siku. Watanzania wengi tunaamini kwamba kesho itakuwa bora kuliko leo. Kimantiki ndivyo inapaswa kuwa hivyo kwamba kesho iwe bora kuliko leo.
Wakati huu tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu kuchagua Raisi, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani fikra za kuitaka kesho iliyo bora zinachipuka zaidi. Fikra za kuitaka kesho yenye jamii iliyostawi kielimu, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa ndio inatawala mawazo yetu. Fikra ya kufanya maamuzi yatakayofanikisha kesho tunayoitamani inaendelea kupata msukumo zaidi kila tunapoitazama jana yetu na leo yetu. Hivyo basi, ni wazi Watanzania tunatumia msemo wa “mwaka ujao nitakuwa Jerusalem” pengine bila ya kutumia maneno haya kama yalivyojipanga sisisi. Maana ni wazi tunaitaka kesho iliyo bora.
Kesho iliyo bora ya Watanzania imemezwa na ilani za vyama vya siasa. Ilani hizi ndio hasa mkataba kati ya wagombea uongozi na Wananchi. Wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi kupitia vyama hivi vya siasa wamekuwa wakinadi yaliyoandikwa kwenye ilani za vyama vyao. Ingawa takribani  vyama 8 vinashiriki uchaguzi mkuu mwaka huu, ni CCM na UKAWA (muungano wa vyama vine – CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD) ndio vinaonekana kuchuana kwa karibu sana. Mchuano mkali baina ya CCM na UKAWA unaibua swali la msingi kwa Mtanzania la: je “mwaka ujao nitakuwa Jerusalem” kupitia CCM ama UKAWA?.Ni imani yangu kwamba majibu ya swali hili yatatofautiana.
Hata hivyo itakuwa na maana zaidi ikiwa tutaulizana maswali mengine ya msingi kama: Je, ni nini tofauti ya itikadi ya siasa ya uchumi ya CCM na UKAWA?; Je, kuna tofauti ipi ya mfumo wa uzalishaji mali unaopigiwa chapuo na CCM na UKAWA?; vilevile kwa kwa nini CCM wanaahidi maboresho na UKAWA wanaahidi mabadiliko? Bila shaka yapo maswali mengi ya msingi tunayopaswa kujiuliza kabla hatujathibitisha kwa hakika kwamba “mwaka ujao nitakuwa Jerusalem”.
Itikadi ya uchumi wa soko huria
Kwa vile CCM na UKAWA wanatumia ilani zao kujinadi. Ni vema kutafuta majibu ya maswali yetu haya kupitia ilani zao. Jambo linalosisimua ni kwamba, ilani hizi mbili zina akisi kwamba CCM na UKAWA wote ni waamini wa uchumi wa soko huria (Free Market Economy). Fasiri rahisi ya uchumi wa soko huria ni kwamba, uzalishaji mali viwandani na mashambani, pamoja na utoaji wa huduma za kijamii utaongozwa bei ya soko. Jukumu la serikali litakuwa ni kusimamia wazalishaji na watoa huduma pamoja na kukusanya kodi.


Katika hili, ilani ya CCM inaainisha kwamba chama hiki kimefanikiwa kutekeleza kanuni za soko huria. Kwa mfano, “serikali imeondoa ukiritimba wa TANESCO kuwa mzalishajina msambazaji pekee wa umeme hapa nchini”(p.61). Vilevile “vituo vya kutolea huduma ya Afya vimeongezeka kutoka 6,260 mwaka 2010 hadi vituo 7,014 mwaka 2015. Pia kuna kliniki 89 zinazohamishika (huduma za mkoba) katika mfumo wa utoaji wa huduma za wazazi, meno, macho, moyo na sukari ambazo huendeshwa na madaktari bingwa” (p.67).


Zaidi ni kwamba ilani inaainisha kuwapo kwa maeneo ambayo CCM haikufanya vizuri sana. Kwa mfano kuwapo kwa hitaji la “kuongeza kiwango cha uunganishaji umeme (Connection level) kutoka asilimia 36 mwaka 2015 hadi asilimia 60 ifikapo mwaka 2020 (p.61); pia ilani imeanisha hitaji la “kukarabati, kujenga na kupanua miundombinu katika vyuo vya mafunzo ya afya na kushirikisha Sekta Binafsi katika uendeshaji wa vyuo”. Kwa mifano hii michache ya kufanikiwa na changamoto zilizoikabili serikali ni dhahiri kwamba CCM inalazimika kufanya maboresho.


Kwa kipimo cha itikadi ya uchumi wa soko huria, ilani ya UKAWA inaahidi mabadiliko. Hapa inaanisha kwamba matatizo ya nchi yetu yamesababishwa na “udhaifu wa kimuundo, kiutendaji na kiuongozi uliojengwa na Chama Cha Mapinduzi kwa zaidi ya miaka 50”(p.5). Ilani ya Chadema ina ahidi kubadilisha muundo, utendaji na uongozi wa nchi. Hii ni ruya (vision) nzuri. Hata hivyo ilani haisemi ni namna gani mabadiliko haya yanayoahidiwa yatafanyika. Pia ilani haielekezi ni namna gani mabadiliko haya yanayoahidiwa yatajibu mahitaji ya itikadi ya uchumi wa soko huria ambayo ni itikadi mama ya CHADEMA.

Mfumo wa Uzalishaji.


Mbali na itikadi, lipo swali la aina ya mfumo wa uzalishaji mali unaopigiwa chapuo na CCM na UKAWA. Hapa ilani zote mbili zinabainisha kwamba sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, madini, mafuta na gesi ndizo sekta mama zitakazotumika kukuza uchumi wa nchi yetu.


Katika hili, Ilani ya CCM inaainisha umuhimu wa ushirikishwaji wa sekta binafsi ili kuboresha uchumi kisekta. Yapo maeneo kadhaa ya mafanikio yanaanishwa. Kwa mfano, “Jumla ya miche 3,500,000 ya mikarafuu imeoteshwa katika vitalu mbalimbali vya Serikali. Kati ya hiyo miche 2,216,328 yenye thamani ya shilingi bilioni 4.4 imetolewa kwa wakulima bila ya malipo. Kiwango cha uzalishaji wa karafuu kimeongezeka kutoka tani 2,673 mwaka 2010 hadi kufikia tani 5,340 mwaka 2014. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 50”(p. 102).


Vile vile ilani ya CCM inaainisha changamoto zilizomo. Kwa mfano,  hitaji la “kuhamasisha Sekta Binafsi kujenga viwanda vya usarifu wa mazao ili kuongeza thamani na ubora wa mazao ya mboga na matunda, nazi na karafuu ili kukuza kipato cha wakulima na kurahisisha upatikanaji wa soko; “(p. 103). Ni dhahiri changamoto hizi zinaibuka kutokana na jitihada za serikali kushirikiana na sekta binafsi ili kukuza uchumi.


Kwa upande wa UKAWA, ilani inaelekeza kwamba serikali itakuwa mhimili wa kufufua na kuimarisha viwanda (p.44). Hapa swali linabakia, ikiwa serikali ndio itakuwa muhimili wa kufufua na kuimarisha viwanda, serikali ya UKAWA itawezaje kujibu mahitaji ya itikadi ya uchumi wa soko huria? Vile vile ilani ya UKAWA ina ahidi ya dhamira ya “kubadili mfumo wa Uchumi wa nchi ili kuhakikisha kuwa mfumo wa uchumi wa Tanzania unakuwa ni wa soko-jamii (social market economy), ambapo nguvu za soko zitatumikia jamii kwa serikali kuweka uwiano wa mapato unaohakikisha huduma za kijamii zinapatikana kwa ufanisi” (p.49). Kimsingi sera hii sio sera mpya maana imekuwa ikitekelezwa na CCM kwa muda mrefu. Pengine agenda ya mabadiliko ya muundo, uongozi na utekelezaji yasiyosemwa na UKAWA yanalo jibu la kadhia hii.


Maboresho ama Mabadiliko?

Agenda ya CCM kuahidi maboresho baada ya kubaini mapungufu kwenye utekelezaji wa Ilani ya 2010-2015 ni hoja inayohitaji kutazamwa kwa ukaribu zaidi ili kutambua nia ya dhati ya CCM katika kusukuma maendeleo ya nchi yetu. Wakosoaji wa hoja hii ya CCM wanadai kwamba CCM imeshindwa kuleta maendeleo ya nchi yetu kwa haraka hata baada ya kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50. Pengine wakosoaji hawa wanazo sababu nyingi kutetea madai hayo. Watetezi wa hoja dhidi ya CCM kuomba ridhaa ya uongozi kwa miaka mitano ili kuboresha penye mapungufu ni kwamba, miaka zaidi ya 50 iliyopita Taifa letu limepitia mengi ya kujivunia. Kubwa zaidi ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na awamu ya kwanza ya kupigania uhuru wa nchi za kusini mwa Afrika. Bila shaka wapo wakosoaji watakaohoji sababu za Tanzania kushiriki kwa hali na mali katika ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika.


Agenda ya UKAWA kuahidi mabadiliko ya muundo, uongozi na utekelezaji  vilevile agenda inayohitaji kutazamwa kwa undani ili kutambua msingi na namna muafaka ya kufikia mabadiliko haya. Sababu kubwa ya kutazama msingi wa mabadiliko haya ni kujiridhisha kwamba misingi ya matatizo yetu inayotajwa ndio hasa inayokwamisha maendeleo yetu. Maana mbali na misingi hiyo inayotajwa bila ushahidi wa kutosha, ni dhahiri kwamba mwelekeo wa utekelezaji wa ilani ya UKAWA hauna tofauti na utekelezaji unaoendelea wa CCM. Kwa mfano, UKAWA hawatupatii ushahidi wa mfano wa mabadiliko hayo ya mfumo na namna ulivyotumika mahali pengine duniani ili kuharakakisha maendeleo kwa kadri yanavyoahidiwa kwenye ilani hii ya UKAWA ya 2015. Ni wapi hasa yalifanyika mabadiliko hayo na kuharakisha maendeleo kwa kasi hivyo?


Hitimisho

Umuhimu wa “mwaka wa mwaka ujao nitakuwa Jerusalem” haupingiki. Hata hivyo ni jukumu la jamii kutambua nini hasa kinachoahidiwa na ilani inayoalika “Maboresho” dhidi ya ilani inayoalika “Mabadiliko”. Ikiwa lengo ni kufika Jerusalem pekee bila kujali kwamba Jerusalem hii itatupatia furaha, basi ni vema tusiende Jerusalem. Ndugu zangu, Watanzania wenzangu, wajibu wetu ni kuilinda na kuitetea nchi yetu. Fursa tuliyonayo mwaka huu binafsi ninaiona kama fursa ya ama kuchagua “Maboresho” (Reform) ama kuchagua “Mabadiliko” (Change). Namna muafaka ya kuchagua kati ya pande hizi ni kupitia mikataba hii maarufu kama Ilani ya Uchaguzi tunayoletewa na Wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi.


Muhimu zaidi ni maswali linalobakia kwamba: inawezekanaje kuwa Jerusalem mwaka ujao bila ya kuzisoma, kuzielewa, kuzichambua, kuzichanganua na kuzipima Ilani za CCM na UKAWA washindani wanaochuana vikali? Zipi faida na hasara za kuchagua Maboresho yanayosemwa dhidi ya Mabadiliko yasiyosemwa?


Tafakari. Tujenge Taifa.


Barnabas Mbogo
P.O.Box 6243
Nyamagana
Mwanza

Twitter @drbmbogo

Kauli ya Sumaye kuhusu tuhuma za mashamba

Sumaye katika ufunguzi wa kampeni za UKAWA Ubungo

Akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni za ubunge wa Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, alisema kwa sasa hakuna njia au mtu atakayeweza kuifufua CCM.

Sumaye alisema wamezunguka maeneo mengi ya nchi kila walipokuwa wakienda wamebaini Watanzania hivi sasa wanahitaji mabadiliko na hawana mpango wa kuongozwa tena na CCM.

Aidha Sumaye alipingana na wale wanaosema amejiunga Ukawa kwa uchu wa madaraka, na kusema kuwa uchu wake wa kujiunga Ukawa ni kutaka kuing’oa CCM.
“Sikuja UKAWA kutafuta cheo kwa sababu nimeshakuwa waziri mkuu na hata hapa Ukawa hakuna nafasi ninayotaka kwa sababu nafasi ya urais yupo Lowassa na nafasi ya waziri mkuu siwezi kupata kwa sababu sijagombea ubunge ila ninachofanya ni kuhakikisha CCM inaondoka madarakani,” 
Sumaye alisema kwa kuingia kwake UKAWA, amejikuta akipata vitisho kutoka serikalini:.
“suala la kunitisha kuninyang’anya mashamba yangu ni kunikomaza zaidi kwa kuwa naamini suala hilo ni sawa na kumpiga chura teke.” 
via MTANZANIA

Pombe bandia za mil 75/= zilizotoroshwa zakamatwa

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, imekamata pombe mbalimbali bandia za ‘viroba’ aina ya rider, empire, na signature vodka, zilizokuwa zikidaiwa kutengenezwa bila kibali na kiwanda cha Mwanza Lakeline Ltd, zikiwa zimehifadhiwa ghala la kampuni ya Ikohi lililopo jijini Mwanza.

Bidhaa hizo ziligunduliwa katika ukaguzi wa kushtukiza uliofanywa na mamlaka hiyo zikidaiwa kuhifadhiwa katika ghala hilo linalomilikiwa na kampuni ya Ikohi, lakini zikidaiwa zilitoroshwa katika kiwanda cha Mwanza Lake Line, wakati kikifanyiwa ukaguzi na mamlaka hiyo.

Akizungumza na NIPASHE juzi, Mkaguzi wa TFDA Kanda ya Ziwa, Nuru Mwasulama, alisema kiwanda hicho kilichopo jijini Mwanza, hakijasajiliwa kuzalisha bidhaa hizo zilizokamatwa, hivyo kilikuwa kikizalisha kwa njia ya ujanja wakati ‘viroba’ vya kuwekea pombe hiyo vikinunuliwa nchini Uganda.

“Tumechukua hatua ya haraka kukifungia kiwanda hicho na kuzuia bidhaa zake kutokana na kucheza mchezo mchafu na kuhatarisha afya za watumiaji wa bidhaa hizo,” alisema Mwasulama.

Alisema baada ya kufanya msako wa kushtukiza kiwandani hapo, siku ya kwanza hawakufanikiwa kuingia ndani, lakini waliona ‘mzigo’ ukiwa ndani ya kiwanda kupitia dirishani, isipokuwa kilichofanyika ni mmiliki wa ghala la Ikohi kuuhamisha usiku na kuuweka ghalani mwake ili usambazwe kwa walaji bila ya ruhusa ya mamlaka. 

Mwasulama alisema kiwanda hicho kilipewa kibali na mamlaka kusindika pombe ya ‘viroba’ aina ya simba gine pekee, lakini walikiuka masharti ya leseni na kuzalisha bidhaa ambazo hawakupewa kibali kuzalisha.

Alisema bidhaa zilizokamatwa ni masanduku 1,246 na magunia 25, ambayo thamani yake inakadiriwa kuwa Sh. milioni 75.

Hata hivyo, mmiliki wa ghala hilo, Ikohi alikataa kuzungumza na waandishi wa habari kwa madai msemaji ni mmiliki wa kiwanda cha Mwanza Lakeline, Chola Maginga, ambaye yupo safarini China.

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia asali na mdalasini

Asali ikiwa imechanganywa na mdalasini tayari kwa matumizi 

Wadau wetu wale ambao wanasumbuliwa sana na chunusi (vipele) iwe usoni, kifuani, mgongoni n.k., wanaweza tumia mchanganyiko mzuri wa asali na mdalasini wa unga kwa kupaka angalau mara moja kwa siku.

Asali na mdalasini zinasaidia kuponyesha kwasababu zina tabia za anti-bacterial (zinaua na kuzuia mazalia ya bacteria)

Jinsi ya kufanya:-
  1. Chukua vijiko vitatu (3) vya chai vya asali
  2. Chukua nusu kijiko cha chai cha mdalasini wa unga safi
  3. Changanya pamoja kupata uji uji mzuri
  4. Paka sehemu yenye chunusi na kisha kaa nayo kwa angalau dakika 10-30 kisha osha kwa maji ya uvuguvugu.
ANGALIZO: Mdalasini unaweza kuwasha kwenye ngozi hivyo unashauriwa ujaribu kupaka kidogo kwenye kiganja cha mkono kwanza ili kupata uhakika kua haitakusumbua.

Imeandaliwa na Honey Spring na Jamiimojablog
0683370065 au 0769129351

Uzinduzi wa kampeni za CCM na UKAWA Kinondoni


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kushoto) akimtambulisha Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan(kulia) mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika katika viwanja vya CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni.a , wakati wa uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, katika jimbo hilo, jijini Dar es Salaam.


Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan akizungumza na wananchama na wananchi wa maeneo mbalimbali ya jimbo la Kinondoni waliofurika katika viwanja vya CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni wakati wa uzinduzi wa kampeni.


Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akihutubia umma uliohudhuria uzinduzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CCM.


Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa akimwaga sera za CCM mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika wakati wa ufunguzi wa kampeni za mgombea ubunge jimbo la Kinondoni zilizofanyika waliofurika katika viwanja vya CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akiwasalimia pamoja na kutoa neno kwa wananchama na wananchi waliofika kwenye mkutano huo wa ufunguzi rasmi wa kampeni za mgembea Ubunge jimbo la Kinondoni.


Mgombea udiwani kata ya Mwananyamala Bw. Songoro Mnyonge(kushoto) akitambulishwa kwa wananchi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kulia)


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akimtambulisha Mgombea udiwani wa kata ya Kijitonyama, Ndg. Kamugisha wakati wa ufunguzi wa kampeni za Mgombea Ubunge jimbo la Kinondoni


Mgombea udiwani kata ya Tandale Bw Tamimu akitema vidonge kwa wapinzani.


Bw. Massawe ambaye ni mgombea udiwani kata ya Ndugumbi akizungumza jambo wakati wa mkutano huo


Mgombea Udiwani kata ya Magomeni Ndugu Bujugo akiwaomba kura wananchi waliofika kwenye mkutano huo na pia kuwapigia wabunge pamoja na raisi kupitia chama cha CCM


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge (kushoto) akipokea kadi ya CUF toka kwa bibi ambaye alikuwa ni kada wa chama hicho alidai hajaona manufaa yeyote kuwepo katika chama hicho ambapo alijitoa rasmi na kurudi CCM.


Bibi akiwasalimia wananchama na wananchi waliofika kwenye mkutano huo


Mzee Dalali akihutubia mamia ya watu waliohudhuria mkutano huo ambao mwenyewe alidai umati ulifikia watu laki 250.
Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan akiendelea kumwaga sera
Umati mkubwa ukishangilia wakati wa mkutano


Baadhi ya wananchi waliofika kwenye mkutano huo


Wasanii wa kizazi kipya Tundaman na Bonge la Nyau wakitumbuiza mara baada ya Mkutani kwisha


Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya CCM, Mh. Iddi Azzan akiaga mashabiki wake baada ya kumaliza kuhutubia katika viwanja vya CCM Mwinjuma Mwananyamala jana jioni.

  • Picha na Geofrey Adroph/Pamoja blogMgombea ubunge wa UKAWA kupitia chama cha CUF Maulid Salum Mtulia akihutubia mamia ya watu waliohudhria uzinduzi wa kampeni za ubunge jimbo la Kinondoni leo jioni.

Vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA leo hii vimezindua kampeni za ubunge kwa jimbo la Kinondoni ambapo mamia ya watu walihunduria katika viwanja vya Mapilau. Ukawa wameamua kusimamisha mgombea mmoja kwa kila jimbo toka vyama vya Chadema, CUF, NCCR Mageu na NLDambapo kwa jimbo la Kinondoni Ukawa imemsimamisha Maulid Salum Mtulia.

Bw Mtulia akimwaga sera leo hii jioni Mwananyamala katika viwanja vya Mapilau.  • Picha: Blogu ya Mkala Fundikira