African Democracy: A Conversation with Tanzania's President Jakaya Kikwete


Scheduled for Sep 21, 2015

Kikwete Speaks on International Day of Peace

After 10 years as president of The United Republic of Tanzania, Jakaya Kikwete will hand office to a successor to be chosen next month in what is expected to be the country’s most closely contested election. On the International Day of Peace, September 21, President Kikwete will discuss the challenges and opportunities for consolidating democracy and development in Africa.

Almost 23 years after the establishment of multiparty democracy in Tanzania, the October 2015 election is being tightly contested between the governing Chama Cha Mapinduzi (CCM) and a united opposition. The vote provides an opportunity for Tanzania to uphold its reputation as a country committed to peaceful transition of power. And a credible, transparent Tanzanian vote will advance democratic progress in Africa just months after Nigeria’s first-ever electoral transfer of power.

President Kikwete’s preparation to leave office under Tanzania’s two-term limit comes as Burundi, the Democratic Republic of the Congo and other African countries face turmoil over leaders’ efforts to remain in office.

President Kikwete will speak in Washington before addressing the United Nations Heads of State meeting in New York. His speech and discussion at USIP is co-sponsored by the National Democratic Institute, the International Republican Institute, and the International Foundation for Electoral Systems.

Join the conversation on Twitter with #KikweteDC

Maisha hayana rimoti

MAISHA HAYANA RIMOTI KUSEMA UTAIBONYEZA MARA UNAPOYAHITAJI MAISHA MAZURI NA YAKAJA. AMKA NA UTENDE, UBADILISHE MAISHA YAKO. 

Kila binadamu chini ya jua ana uhuru wa kuchagua; kufanikiwa au kutofanikiwa.

Mafanikio hayamfuati mtu shida tumezaliwa nazo maana sote tulizaliwa tukiwa watupu na mengine yote tuliyonayo yawe mazuri au mabaya tumeyapata tukiwa hapa duniani.

Uamuzi wa kufanikiwa au kutofanikiwa upo katika matendo yetu ambayo ni mazao ya fikra na matamshi yetu. Hakuna binadamu ambaye hana matendo, kila sekunde tunatenda jambo fulani la lazima au si la lazima, baya au zuri.

Haikwepeki lazima kila binadamu atende; atake au asitake. Mafanikio yetu au kushndwa kwetu kupo katika matendo hayo maana kila sekunde mtu hufikiri, hutazama, husikiliza, hutembea, huongea, n.k.

Katika matendo hayo ndiposa mtu hutenda kwa faida au kwa hasara, hujenga au hubomoa, hufikiri kulaani au kubariki, hutazama matambiko au mbinu za mafanikio, husikiliza mema au maovu n.k. Katika uchaguzi wa nini tutende na nini tusitende ndipo ilipo njiapanda ya kushinda na kushindwa.

Kwa namna hii imekupasa kujiuliza katika matendo yako unayotenda mangapi yanakuinua na mangapi yanakushusha? Mangapi unatenda kwa ajili ya kesho yako na mangapi unatenda kwa ajili ya kesho ya wengine huku ukiamini unaitendea haki kesho yako? Ukitafakari vizuri utagundua wapo watu wanamaliza hata wiki nzima hawajatenda matendo yanayojenga kesho yao ili kuibomoa au kuisusa.

Jiulize pale unapobishana kwa jazba kuhusu nani mkali kati ya Mesi na Ronaldo, Man Pacquiao na Mayweather, Ali Kiba na Diamond n.k unakuwa umeijenga kesho yako kwa namna gani? Jiulize unapolalamika kutaka uonewe huruma unakuwa umeijenga kesho yako kwa mtindo gani? Kuna wakati watu wamekuwa mashabiki wa mambo yasiyowahusu toka mwanzo mpaka mwisho wa wiki, Januari mpaka Desemba bila hata wao wenyewe kujijua.

Fikiri upya kuhusu matendo yako. 

ALOYCE MROPE, 
Che Mrope Wa Mrope (fb), 
Mbeba Maono (fb page) 
0787641417/0766656626/0715366010

NEC yajibu tahariri ya Mhariri wa gazeti Mwananchi


[video] Bashe azungumza


[audio] Kipindi cha Jukwaa Langu, Septemba 14, 2015Kipindi hiki hukujia kila Jumatatu kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu Uchguzi Mkuu wa Tanzania 2015.

Hii ni sehemu ya pili ya kipindi kilichosikika Septemba 14, 2015.

Kutoka Tanzania tuliungana na Jonathan Samiya na Nyakia, ambaye ni mmoja wa wakuu wa Itifaki wa kampeni za Dk Magufuli.

Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, Clare Ng'owo, Ali Badawy na Shamis Abdulla.

Kwenye line tulikuwa na Jeff Msangi, Dk Patrick Nhigula na Arthur.

Ugomvi wa picha ya mgombea Urais yasababisha auawe

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Manushi Kibosho, Wilaya ya Moshi Vijijini ameuawa saa chache baada ya ugomvi unaohusishwa na kuchanwa kwa picha ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.

Mwalimu huyo, Demetus Dastan (33) maarufu kwa jina la Kidule, aliuawa Jumamosi iliyopita usiku na mwili wake kukutwa katika shamba la mtu aliyetajwa kuwa ni Joackim Massawe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani alisema kabla ya kuuawa, mwalimu huyo alikuwa amekwenda kunywa pombe katika klabu moja hapo kijijini. Inadaiwa kuwa akiwa klabuni, kulitokea ubishani kati yake na mtu mwingine uliotokana na kuchanwa kwa picha ya Lowassa ambao ulikwenda mbali na kusababisha wapigane.

Kamanda Ngonyani alisema waliamuliwa na wateja wengine waliokuwapo na baadaye mwalimu huyo aliondoka kurejea nyumbani na hakuonekana hadi mwili wake ulipookotwa.

Baadaye mwili wake ulikutwa shambani ukiwa na michubuko kidogo kwenye mguu wa kulia karibu na goti na shati lake likiwa limechanikachanika.

Polisi wamewakamata watu wawili akiwamo mmiliki wa klabu hiyo na mtu mwingine anayedaiwa kuwa aliongozana naye kurudi nyumbani huku mtu waliyepigana naye akiendelea kusakwa.

Mnyika amzungumzia Dk Slaa kama "Samson na Delila"

Akizundua ofisi za CHADEMA huko katika mtaa wa Saranga juzi, Mgombea Ubunge wa Kibamba kwa tiketi ya chama hicho na UKAWA, John J. Mnyika amewataka wananchi waache kumkebehi au kumkashfu Dk Willibrod Slaa akimfananisha na hadithi ya "Samson na Delilah" inayopatikana kwenye Biblia (imenukuliwa hapo chini).

Akiwahubiria wananchi hao kuhusu mkasa wa Samsoni, akisema alikuwa na nguvu nyingi, lakini zilikuwa na siri ambayo Wafilisi waliangaika kuijua wakamtumia Delilah, akafanikiwa kuijua ndipo wakamtoboa macho na kumtesa, lakini kuna siku aliota nywele akalipa kisasi.

“Mwacheni Dk Slaa aende zake, ipo siku Mungu akimbariki nguvu itamrudia yatatokea ya kutokea,” alisema.

Hatua ya Mnyika kumtetea Dk Slaa ilikuja baada ya kuwasikia baadhi ya wanachama wakimwita msaliti.

Kisa cha Samson na Delila kilivyoandikwa katika Biblia Takatifu, kitabu cha Waamuzi


1  Samsoni akaenda Gaza, akaona huko mwanamke kahaba, akaingia kwake.
2  Watu wa Gaza wakaambiwa, ya kwamba, huyo Samsoni amekuja huku. Wakamzingira, wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, Na tungoje mpaka mapambazuko, ndipo tutamwua.
3  Basi Samsoni akalala hata usiku wa manane, akaondoka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing'oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hata kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.
4  Ikawa baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika bonde la Soreki, jina lake akiitwa Delila.
5  Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.
6  Delila akamwambia Samsoni, Tafadhali uniambie asili ya nguvu zako nyingi, na jinsi uwezavyo kufungwa, ili uteswe.
7  Samsoni akamwambia, Wakinifunga kwa kamba mbichi saba ambazo hazijakauka bado, hapo ndipo nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu.
8  Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamletea kamba mbichi saba zisizokauka, naye akamfunga nazo.
9  Na yule mwanamke alikuwa na watu katika chumba cha ndani, wakimwotea. Basi akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Ndipo akazikata zile kamba kama vile uzi wa pamba ukatwavyo ukiguswa na moto. Basi hiyo asili ya nguvu zake haikujulikana.
10  Delila akamwambia Samsoni, Tazama, umenidhihaki, na kuniambia uongo; sasa tafadhali, niambie, waweza kufungwa kwa kitu gani?
11  Akamwambia Wakinifunga tu kwa kamba mpya ambazo mtu hakufanya kazi nazo, hapo ndipo nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu.
12  Basi Delila akatwaa kamba mpya akamfunga nazo, akamwambia, Wafilisti wanakujia, Samsoni. Na wale wenye kuotea walikuwa katika chumba cha ndani. Naye akazikata, akazitupa kutoka mikononi mwake kama uzi.
13  Delila akamwambia Samsoni, Hata sasa umenidhihaki, umeniambia maneno ya uongo; niambie sasa, waweza kufungwa kwa kitu gani? Akamwambia, Ukivifuma hivi vishungi saba vya nywele za kichwa changu katika mtande wa nguo.
14  Basi akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Naye akaamka usingizini, akaung'oa ule msumari, na ule mtande.
15  Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi.
16  Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa.
17  Ndipo alipomwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu, nitakuwa kama wanadamu wenzangu.
18  Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia yote aliyo nayo moyoni mwake. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.
19  Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka.
20  Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa Bwana amemwacha.
21  Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.
22  Lakini zile nywele za kichwa chake zikaanza kukua tena baada ya kunyolewa kwake.
23  Kisha wakuu wa Wafilisti wakakusanyika ili kumtolea sadaka Dagoni mungu wao, na kufurahi; maana walisema, Mungu wetu amemtia Samsoni adui wetu mikononi mwetu.
24  Na hao watu walipomwona wakamhimidi mungu wao, maana walisema, Mungu wetu amemtia mikononi mwetu huyu adui wetu, aliyeiharibu nchi yetu na kuwaua watu wengi miongoni mwetu.
25  Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili.
26  Samsoni akamwambia yule kijana aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate kuzitegemea.
27  Basi nyumba ile ilikuwa imejaa watu waume kwa wake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu waume kwa wake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza.
28  Samsoni akamwita Bwana, akasema, Ee Bwana MUNGU, unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.
29  Kisha Samsoni akazishika nguzo mbili za katikati ambazo nyumba ile ilikaa juu yake, akazitegemea, moja kwa mkono wake wa kuume na moja kwa mkono wake wa kushoto.
30  Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale aliowaua wakati wa uhai wake.
31  Ndipo ndugu zake, na watu wote wa nyumba ya baba yake wakatelemka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya Sora na Eshtaoli, katika kiwanja cha kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka ishirini.

[video] Lissu amjibu Rais Kikwete kuhusu mmiliki wa Richmond

Suala la Richmond imekuwa moja ya agenda za CCM katika kampeni za kuwania Urais wa Tanzanai 2015 hasa baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa aliyejiuzulu wadhifa huyo kwa kashfa hiyo, kuhamia upinzani.

Kila sehemu ambako mgombea urais wa CCM anakwenda, suala hilo limekuwa likiibuliwa, huku Lowassa akisema yeye hakuhusika, bali alijiuzulu kuiokoa Serikali isianguke kwa kuwa ulikuwa uamuzi wa wakubwa.

Wakati akiwaaga wananchi wa Kigoma katika Uwanja wa Lake Tanganyika juzi, Rais Jakaya Kikwete aliesema anashangazwa na Mwanasheria wa CHADEMA, Tundu Lissu kumtaka amtaje mhusika wa Richmond wakati mwenye Richmond yupo na anatembea naye mikoani na kumtaka Lissu amtaje: 

“Endapo Tundu Lissu atashindwa kumtaja mwenye Richmond, nitatoka hadharani na kumtaja mwenyewe,” 

Video iliyopachikwa hapo chini ina kauli iliyotolewa na Lissu siku moja tu baada ya Rais Kikwete kuzungumza...
Mwenyekiti ashikiliwa kwa kumvunja mguu mama aliyekuwa anadai kibatari chake kwenye mkutano wa kampeniKamati yaagiza aliyebomoa nyumba zaidi ya 140 Chanika akamatwe

Kamati ya Ulinzi na Usalama Dar es Salaam pia imeagiza kukamatwa kwa Joseph Mwakajinga ambaye anadaiwa kutekeleza agizo la kubomoa nyumba za wananchi bila ya kuwa na idhini ya kibali cha mahakama katika eneo ambalo awali lilikuwa ni pori.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ni Mkuu wa Mkoa huo, Said Meck Sadiq amesema Serikali inachunguza tukio hilo la kubomolewa kwa nyumba zaidi ya 140 katika mtaa wa Vikongoro kwenye kata ya Chanika mkoani Dar es Salaam na kusababisha mamia ya kaya kubaki bila makazi.

Kitendo hicho kilicholaaniwa na Sadiq kilitokea Septemba 11 mwaka huu ambapo wakazi wa eneo hili wamedai walioendesha zoezi hilo walipora mali walipokuwa wanabomoa nyumba na kuwaweka rumande baadhi ya vijana katika kituo cha polisi cha Sitaki Shari, Ukonga.

Mkuu wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, Kamishina Simon Sillo amesema kuwa uchunguzi unafanyika na kuwataka watendaji la jeshi hilo kufanya kazi kwa kuzingatia wa sheria.Basi la METRO (Dar - Rombo) lapata ajali Manga na kuua 5

Watu watano (wanaume 3, wanawake 2 - mtu mzima na binti), wakiwemo 3 wa familia moja wameaga dunia baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali lilipohama njia katika eneo la Manga wilayani Handeni, mkoani Tanga, mwendo wa saa tano adhuhuri.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Tanga, Zuberi Mwombeji amewaomba ndugu na jamaa wa abiria wa basi basi la kampuni ya Metro lenye namba za usajili T442 DAF waliokuwa wakitokea Dar es Salaam kuelekea Rombo, Kilimanjaro wajitokeze katika kituo cha afya cha Mkata ili kuwatambua marehemu na majeruhi 39 waliolazwa hospitalini hapo.

Kamanda Mwombeji alisema dereva wa gari hilo hakuweza kupatikana kwa kuwa alitoroka baada ya ajali.

Call for applications: $200K for 2 Yrs: HIV funding opportunity
Request for ProposalsFunding to support innovative biomedical research projects exploring the potential for HIV eradication.

Total Cost Maximum: $200,000

Performance Period: 2 years (February 1, 2016 – January 31, 2018)

You must request application credentials by October 9, 2015 (click here for request form)
 
LOI Submission Deadline: October 14, 2015, 3:00 PM EDT

Click here to see the RFP for detailed information about this funding opportunity

BACKGROUND
amfAR wishes to support basic, pre-clinical, clinical, and especially translational research exploring the mechanisms whereby HIV infection persists; the chronic nature of viral reservoirs and latency; and barriers to the eradication of HIV, with the potential goal of ultimately curing HIV infection.
Specific areas of interest fall within the following four categories:
  • Determine the location of persistent reservoirs of HIV in tissues, cell subsets or within cells
  • Determine the cellular and viral mechanisms and kinetics that establish and/or maintain HIV persistence
  • Develop, compare, or validate assays to measure persistent infection
  • Develop and test strategies to safely eliminate or control viral reservoirs (in the absence of ART)
Eligibility
Principal investigators:
  • Must hold a doctoral level degree
  • Must be affiliated with the applicant institution
amfAR grants are made to nonprofit organizations worldwide. Applicant investigators need not be U.S. citizens, and there are no restrictions as to age, color, creed, gender, medical condition, handicap, national origin, parental status, political affiliation, race, religion, marital status, or sexual orientation.

Man drops dead in Arusha after hearing child rape ordeal


It took a team of policemen to rescue a man who was about to be killed by an irate mob of people who surrounded him after allegedly defiling a nine-year old girl who also happened to be speech and hearing impaired.

The suspect, 'Balozi,' said to be in his 50s, allegedly defiled the helpless girl who cannot speak and without the ability to cry for help. The victim is a pupil at the Meru Primary School's special stream for disabled children.

But as the rowdy commotion escalated within the Olevolosi Street of Sinon Ward in the outskirts of Arusha City, where the incident took place, the girl's uncle, Laurent Lobikoki (Lelo) who was lying sick inside, got up to find out what the fuss was all about.

"When he heard that, 'Balozi' had 'raped' his niece, he dropped down and died," said the head of the family, Peter Lobikoki Laizer adding that the sad incident has just become a double tragedy for them. "My brother died on the spot, look here is the medication that he was taking," he said.

Apparently, the late Lobikoki, was helping as the girl's father, despite the fact that the child belonged to his sister. This is due to the fact that nobody knew where the actual father was.

It is reported that the suspect had summoned the girl into his room and afterwards the child came out limping and crying. A woman known as Joyce Peter carried her to the nearest dispensary for check-up before she was referred to the regional Mount Meru Hospital, where it was proven that indeed she was raped.

Speaking through a special sign language interpreter, the girl told the police that, the suspect had tied both arms behind her back, before proceeding to defile her in his room.

The suspect has been living in the same enclosure (boma) with the girl's family since 1986 when he was welcomed to stay with them more less like a family member.

The Olevolosi area Chairman, Adrian Mswata, said while indeed, Laurent could have possibly died of heart attack, upon hearing the bad news, he would rather not have the issue connected with the incident, because the deceased had been sick in the first place.

Mswata added that, the suspect once had a wife but they divorced and she left both the man and house taking their children with her. Police are still investigating the matter and soon the suspect will be taken to court.

Tangazo la nafasi za kujitolea Tanzania Agricultural Modernization Association


TANGAZO LA NAFASI ZA KUJITOLEA

Tanzania Agricultural Modernization Association (TAMA) ni asasi ya kijamii isiyokuwa ya kiserikali inayojishughulisha na uendelezaji wa kilimo na mazingira wezeshi nchini Tanzania. Ofisi zetu zipo Jengo la TEPU House, Mjini Bukoba, Mkoani Kagera.

Toka mwanzoni mwa mwaka huu 2015, tunao Mpango wa Kujitolea kwa vijana wanaohitimu Chuo Kikuu katika fani mbalimbali. Vijana hupata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo: Tasks Management, Risks Mitigation Plans at work place, Program Management, Strategic Thinking and Planning, Resource Mobilization and Proposal Writing Skills. Mpaka sasa zaidi ya vijana 6 wamenufaika na fursa hii na tayari wamepata ajira katika taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi nchini.

Utaratibu wa kukaa na Wafanyakazi hao ni muda wa miezi 3 tu, baada ya hapo mfanyakazi yupo huru kuondoka. Pia, tunatoa Vyeti (Testimonials) kama Hati za Utambuzi/Uthibitisho. Hivi sasa tunazo nafasi 4 za Kujitolea kwa vijana waliohitimu Elimu ya Chuo Kikuu (Shahada) katika fani mbalimbali, na hawajapa ajira yoyote. Waliosoma Kilimo, Mazingira, Mipango na Maendeleo ya Jamii watapewa kipaumbele zaidi. Tunapokea waombaji kutoka mikoa mbalimbali nchini LAKINI ni muhimu ukawa na mahali pa kuishi Mjini Bukoba, Mkoani Kagera kwa sababu TAMA haitahusika na gharama zozote za kuishi Bukoba.

Kwa taarifa zaidi kuhusu TAMA tembelea tovuti yetu: www.tamatz.org. aidha, kwa maelezo zaidi kuhusu nafasi hizi, wasiliana nasi kupitia email: [email protected]; . Tunafurahi kufanya kazi na wewe, tukupatie uzoefu wa kazi. Tunaamini utafurahi zaidi kuwa na sisi! Karibuni sana!

Imetolewa na,

Idara ya Rasilimali Watu
TAMA, 15th September 2015.
www.tamatz.org

Kampeni hazichezi mbali na huku! Sababu? Wapiga kura zaidi ya 50% wapo katika mikoa hii 10

Mapema mwezi huu, ofisi ya Taifa ya Takwimu ilitoa makadirio ya idadi ya watu wanaotarajiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015. Idadi ya wapiga kura wa mwaka huu inakadiriwa kuwa watafika million 24.2 nchi nzima. Taarifa hiyo ilikuwa ikitoa makadirio ya idadi ya watu wanaostahili kupiga kura katika majimbo ya uchaguzi Tanzania kwa mwaka 2015. 

Itakumbukwa kwamba, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, idadi ya wapigakura waliojiandikisha ilikuwa 20,137,303. Hata hivyo, watu walioshikiri kupiga kura katika mwaka 2010 walisemeana kuwa 8,626,283 sawa na asilimia 42.84 ya wapiga kura wote waliojiandikisha.

Makadirio ya idadi ya wapiga kura katika mikoa mbalimbali yanatokana na uchambuzi wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012. Kwa mujibu wa sensa, Tanzania itakuwa na watu wapatao 48,522,229 ambapo watakaokuwa na umri wa kupiga kura watakuwa ni watu 24,252,927 endapo watu wote wanastahili watakuwa walipata fursa ya kujiandikisha kupiga kura. Hata hivyo pamoja na kwamba taarifa iliyotolewa na tume taarifa iliyotolewa na tume July 17, 2015 ikionyesha kukamilika kwa zoezi katika mikoa 17, inaonyesha uwiano wa moja kwa moja na takwimu za makadirio zilizotolewa na ofisi ya taifa ya Takwimu, taarifa ya tume inaonyesha kufika makaridio ya ofisi ya takwimu kwa zaidi ya asilimia 100.

Mwanzo wakati watangaza nia wa nafasi ya urais wakitafuta mwadhamini kabla ya kupitishwa na vyama vyao na hata baada ya vyama kupitisha wagombea rasmi, kuna mikoa ambyo haikuachwa kutembelewa. Hata sasa wakati vyama vikipita kuwatambulisha wagombea urais wake haswa cha chama tawala na UKAWA, kuna mikoa ambayo imekuwa ni target muda towe. Suala hili lilinifanya ni jaribu kufanya ufuatiliaji na uchambuzi mdogo wa kitamwimu kuelekea otoba 25.

Wazungu husema politics is a game of numbers, yaani ushindi wa kisiasa ni mchezo wa takwimu. Hii ina maana kwamba mwanasiasa haswa katika nafasi ya urais lazima atambue mahali ama makundi ya kijamii yenye watu wengi zaidi na ajikite katika mikakati ya kuwafika wapiga kura hao. Ni muhimu ikafahamika kwamba kuna maeneo yenye waiga kura wengi zaifi lakini yanaweza kuwa ma majimbo machache zaidi. Haya huwa ni maeneo ya kimkakati kwa kura ya urais.

Ikiwa watu million ishirini na nne nukta 3 (24,252,927) watakuwa wamejiandikisha na watapatiwa fursa ya kupiga kura basi zaidi ya nusu ya watu hao ambao ni kumi na tatu nukta 5 (13,520,000). Mkoa wa Dar es Salaam wenye majimbo nane utaongoza ukiwa na wapiga kura million 3 ukifuatiwa na Mbeya itakayokuwa na wapiga kura milioni 1.5. Mkoa wa Mwanza utakuwa na tatu ukiwa na wapiga kura milioni 1.4 na Morogoro itakayokuwa mkoa wa nne kwa wapiga kuwa wengi ambao ni sawa na milioni 1.3.Mkoa wa Kagera utakuwa katika nafasi ya 5 ukiwa na wapiga kura milioni 1.2 ukifuatiwa na Mkoa Tabora ambao unakadiriwa idadi ya wapiga kura milioni 1.1. katika orodha hiyo pia kutakuwa na Mkoa wa Tanga ambao una idadi sawa na mkoa wa tabora (milioni 1.1) na pia Dodoma katika nafasi ya nane ikiwa na wastani wa wapigakura milioni moja. Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ikiwa na wapiga kura laki tisa na elfu sabini sita (976,000) na laki tisa elf arobaini na nne (944,000) ndio inakamilisha mikoa yenye kumi bora za wapig kura.

Ukiachilia mbali mikoa hiyo kama kama nilivyoainisha hapo awali, mikoa mingine ambayo inatarajiwa na kichocheo kikubwa katika ushindi wa kura za urais ni pamoja na Mara (834,000), Geita (808,000), Ruvuma (783,000), Mtwara (773,000), Shinyanga (762,000), Manyara (741,000), na Simiyu (714,000). Mikoa inayotarajiwa kuwa na wapiga kura wachache zaidi ni pamoja na Mkoa mpya wa Katavi (271,000), Mkoa wa Mjini (347,000), Kaskazini Unguja (104,000), Kaskazini Pemba (103,000), Kusini Pemba (95,000) na Kusini Unguja (69,000).

Nadhani sasa watu wanaweza kuelewa kwa nini ziara za wagombea urais zimekuwa zikilenga mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na Zanzibar. Upande wa Zanzibar pamoja na kwamba mikoa yake inawapiga kura wachachewachache lakini Zanzibra yote kwa ujumla kama upande mmoja wa muungano una ushawishi mkubwa katika kukubalika kwa mgombea na kupelekea ushindi. Ni mbinu pia kwa mwanasiasa yoyote kuonyesha hitaji la kupata kuungwa mkono na wanzanzibar haswa ikizingatiwa kuwa kipindi ya zoezi la kutafuta katika mpya ya muungano ilijitokeza sana. Kukubalika kwa mgombea pande zote za muungano ni muhimu sana sio tu kwa kupelekea ushindi wa kuingia ikulu bali pamoja na uwezo wa mtu anayetaka kuwa rais kuweza kuitawala nchi pale atakapokuwa amefanikiwa kuingia madarakani.

Imeandikwa na Constantine Deus via WeWrite
Constantine ni mtafiti na mchambuzi

UNDP Climate Change Storytelling Contest
PRESS RELEASE

UNDP Climate Change Storytelling Contest: Oxfam supports journalists’ participation with additional fellowships

The authors of the top five prize-winning stories will be invited to attend and cover the COP21 UN climate summit in Paris


JOHANNESBURG, South-Africa, September 15, 2015/ -- Oxfam will support the Voice2Paris global storytelling contest launched in August by the United National Development Programme (UNDP) by providing three additional fellowships for participating journalists to cover the UN Conference on Climate Change, COP21, in Paris in December. Oxfam’s contribution to the contest aims at encouraging journalists’ participation in climate change reporting and raising public awareness of climate actions.

“The contest is a fantastic opportunity to create awareness of the harmful impacts of climate change on communities, and of potential opportunities in climate-vulnerable developing countries. This is also a great opportunity for young journalists to strengthen their perception of climate change and to frame it not merely as an environmental issue but also as an issue of social justice and poverty alleviation” said Wang Binbin, Manager of the Climate Change and Poverty Team, Oxfam Hong Kong.

The storytelling contest targets writers 35 years and under from developing countries who want to contribute – locally and internationally – towards greater public awareness of climate change.

The authors of the top five prize-winning stories will be invited to attend and cover the COP21 UN climate summit in Paris. UNDP will support the top two winners and Oxfam, as a special partner in the contest, will cover travel costs and per diem for writers of the next three best stories worldwide.

“We welcome the partnership with Oxfam, as it gives UNDP concrete support to expand the voices of vulnerable countries, helps depict the reality of climate change globally, and gives a new generation of journalists a chance to get heard during COP21” said Jo Scheuer, Director, Climate Change and Disaster Risk Reduction at UNDP’s Bureau for Policy and Programme Support.

Stories can be submitted in English, and in Arabic, Chinese, French and Spanish with an English translation, on a rolling basis until October 11th, 2015. Guidelines for participating are available on the UNDP Geneva website: http://www.europe.undp.org/content/geneva/en/home.html

The stories, once screened and scored, will be published on UNDP’s website and disseminated through partners’ channels to ensure maximum outreach and to support the call for an ambitious agenda for climate action to be endorsed at COP21.

APO (African Press Organization) (http://www.apo-opa.com), Deutsche Welle and Oxfam Hong Kong are special partners of the contest.


Participating organizations: African Network of Environmental Journalists (http://www.unep.org/roa/AboutROA/tabid/7000/Programmes/EnvironmentalJournalists/tabid/51359/Default.aspx), Care International (http://www.care-international.org), China Dialogue (https://www.chinadialogue.net), Global Call for Climate Action (http://tcktcktck.org), International Center for Journalists (http://www.icfj.org), Global Village of Beijing (http://www.gvbchina.org.cn), Innovative Green Development Program (http://www.igdp.cn), InterNews (https://www.internews.org), Pacific Islands News Association (http://www.pina.com.fj), RNTC (https://www.rntc.nl), RTCC/Climate Home (http://www.rtcc.org), Secretariat of the Pacific Regional Environment Programme (http://www.sprep.org) and University of the South Pacific (https://www.usp.ac.fj).

We also thank the global network of climate vulnerable countries active in the Climate Vulnerable Forum (http://www.thecvf.org) currently chaired by Philippines for its support.

Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of United Nations Development Programme (UNDP).

For more information, please contact:

Sarah Bel - UNDP Communication Specialist
[email protected]
+41 22 917 8544

SONG Yang - Oxfam Hong Kong Senior Communication Officer
[email protected]
+86 13141326211

Social media:
Hashtag #Voices2Paris

For frequent updates follow also Twitter @UNDPGeneva and @TheCVF

Uzinduzi wa ripoti ya Twaweza kuhusu Uchaguzi Mkuu 2015

Jumanne, Septemba 22, 2015 saa nne asubuhi hadi saba mchana (10:00am – 1:00pm), Makumbusho (imetazamana na IFM)

Twaweza inakualika katika uzinduzi wa 

Ripoti | Uchaguzi 2015


Mwendesha mada: Aidan Eyakuze, Mkuu, Twaweza

Wageni waalikwa (tbc)
  • Generali Ulimwengu - Raia Mwema
  • Maria Sarungi - Compass Communications
  • Dr Alexander Makulilo - Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Muda: 10:00am – 1:00pm (Saa nne asubuhi hadi saa saba mchana)
Tarehe: Jumanne Septemba 22, 2015
Mahali: Makumbusho, (Imetazamana na IFM)

Kutakuwa na muda maalum utakaotengwa kwa ajili ya maswali na mahojiano kwa waandishi wa habari.

Mbatia, Selasini, Komu 'wavamia' Moshi Vijijini


Rais Kikwete ateua Mganga Mkuu wa Serikali, Naibu Mwanasheria Mkuu, Mtendaji Mkuu NDC

Rais Kikwete amemteua Profesa Muhammed Bakari Kambi kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.

Taarifa iliyotolewa Jumatatu, Septemba 14, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza tokea Jumatano, Septemba 9, 2015.

Kabla ya uteuzi wake, Profesa Muhammed Bakari Kambi alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tiba na Afya Shirikishi cha Muhimbili, Dar es Salaam.

Vile vile, Rais Kikwete amemteua Ndugu Mlingi Elisha Mkucha kuwa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC). Uteuzi huo ulianza Jumatano, Septemba 9, mwaka huu, 2015.

Taarifa iliyotolewa Jumatatu, Septemba 12, 2015 na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Ikulu, Dar es Salaam imesema kuwa Ndugu Mlingi Elisha Mkucha ni mwanasheria kwa taaluma na mwajiriwa wa NDC kwa miaka 14 iliyopita ambako ametumikia katika nafasi mbali mbali mpaka akawa Kaimu Mtendaji Mkuu.

Ndugu Mkucha anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ndugu Gideon Nassari aliyestaafu kwa mujibu wa sheria.

Wakati huo huo, Rais Kikwete amemteua Dkt. Tulia Ackson kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuanzia Jumatano, Septemba 9, mwaka huu, 2015.

Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Tulia Ackson ni Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
14 Septemba, 2015

Walioteuliwa na Rais Kikwete kuwa Mabalozi na Wakurugenzi wapya Wizara ya Mambo ya Nje


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Bi. Victoria Richard Mwakasege aliyekuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Burundi. Balozi Victoria R. Mwakasege anaiwakilisha Tanzania nchini Malawi. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 16 September, 2015


Balozi Mwakasege akisaini kiapo chake mbele ya Mhe. Rais Kikwete


Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Mwakasege vitendea kazi


Mhe. Rais Kikwete (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mwakasege na familia ya Balozi Mwakasege


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi.Zuhura Bundala kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais (Diplomasia) anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Samweli Shelukindo.


Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Bundara vitendea kazi


Mhe. Rais Kikwete (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Bundala na familia ya Balozi Bundala


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Innocent E. Shiyo kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara hiyo


Balozi Shiyo akisaini kiapo chake mbele ya Mhe. Rais KikweteMhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Shiyo vitendea kazi


Mhe. Rais Kikwete (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Shiyo na familia yake


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Afisa Ubalozi Mkuu, Ubalozi wa Tanzania, Muscat, Oman, Bw. Abdallah Kilima kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Balozi Kilima naye akisaini kiapo chake mbele ya Mhe. Rais Kikwete


Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Kilima vitendea kazi


Mhe. Rais Kikwete (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Kilima na familia yake


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ubalozi wa Tanzania, Kampala, Uganda Bi. Anisa Mbega kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Balozi Mbega naye akisaini kiapo chake mbele ya Mhe. Rais Kikwete
Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Mbega vitendea kazi


Mhe. Rais Kikwete (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mbega na wanafamilia.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa Mratibu wa Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu Bw. Baraka H. Luvanda kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Balozi Luvanda naye akisaini kiapo chake mbele ya Mhe. Rais Kikwete


Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Luvanda vitendea kazi


Mhe. Rais Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Luvanda na familia yake

Balozi Irene Kasyanju (wa kwanza kulia), akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje Balozi Celestine Mushy (katikati) na wakwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Haji Kombo walipokuwa katika hafla ya uapisho wa Mabalozi na wakurugenzi wapya


Wakurugenzi wasaidizi Idara ya Utawala na Rasilimali watu wakifuatilia zoezi la uapisho wa Mabalozi na Wakurugenzi likiendelea


Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Asha Rose Migiro (katikati) ambaye alikuwepo kwenye sherehe hizo akisalimiwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia). Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Liberata Mulamula (Kushoto).


Balozi Mwakasege (kushoto), Balozi Bundala (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Diaspora Bi. Rosemary Jairo wakiwa katika picha ya pamoja na nyuso za furaha mara baada ya kumaliza kuapishwa kuwa Mabalozi


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Itifaki Bw. James Bwana (kushoto) akimpongeza Balozi Zuhura Bundala (kulia) mara baada ya kuapishwa kuwa Balozi.


Bi. Mindi Kasiga (kushoto) akimpongeza Balozi Mbega (kulia) mara baada ya kuapishwa kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa


Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wapya pamoja na Waziri Membe, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.


Mabalozi wapya wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu Balozi Liberata Mulamula (wa nne kushoto mstari wa mbele), Naibu Katibu Mkuu Balozi Simba Yahya (wa tatu kutoka kushoto), Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Juu na chini ni Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wakiwasubiri Mabalozi wapya kuwasili Wizarani hapo mara baada ya kuapishwa. 


Maafisa Mambo ya Nje wakiwa na maua wakisubiri kuwakabidhi Mabalozi wapya kama ishara ya pongezi na kuwakaribisha Wizarani.


Sehemu nyingine ya watumishi wa Wizara hiyo wakiwatizama Mabalozi (hawapo pichani) wakiwasili Wizarani hapo mara baada ya kuapishwa Ikulu


Balozi Mwakasege akifuatana na Mabalozi wenzake kuteremka kwenye Basi maalumu lililoandaliwa kwaajili yao wakiwasili Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mara baada ya kuapishwa kuwa Mabalozi


Balozi Mwakasege (kushoto) akipokea maua kutoka kwa Afisa Mambo ya Nje Felista Rugambwa (kulia)


Balozi Samweli Shelukindo aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika naye akipokea maua kutoka kwa Afisa Mambo ya nje Eliet Magogo, mara baada ya kuwasili Wizarani.


Balozi Luvanda naye akipongezwa na Balozi Irene Kasyanju mara baada ya kuwasili Wizarani hapo.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.), katikati akipongezwa na Watumisho wa Wizra ya Mambo ya Nje kwa uongozi mzuri katika Wizara hiyo.


Waziri Membe akizungumza neno huku watumishi wa Wizara hiyo wakimsikiliza
  • Picha: Reginald Philip


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Victoria Richard Mwakasege kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Mwakasege alikuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Burundi. 

Aidha, Rais Kikwete amemteua Msaidizi wa Rais wa Diplomasia, Balozi Samwel Shelukindo kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Kimataifa.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue pia imesema kuwa Rais Kikwete ameteua Ndugu Zuhura Bundala kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais (Diplomasia) kujaza nafasi iliyoachwa na Ndugu Shelukindo. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Bundala alikuwa Mkurugenzi Msaidizi na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Afrika. 

Taarifa hiyo iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015, imesema vile vile kuwa Rais Kikwete amewateua wakurugenzi wengine wanne wa Wizara hiyo ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimatiafa na kuwapandisha cheo kuwa mabalozi.

Walioteuliwa ni Ndugu Abdallah Kilima ambaye anakuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Kilima alikuwa Afisa Ubalozi Mkuu, Ubalozi wa Tanzania, Muscat, Oman. 

Ndugu Baraka H. Luvanda ambaye anakuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Luvanda alikuwa Mratibu wa Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu. 

Ndugu Innocent E. Shiyo ambaye anakuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Shiyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Idara hiyo hiyo.
Bibi Anisa K. Mbega ambaye ameteuliwa kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Mbega alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ubalozi wa Tanzania, Kampala, Uganda.

Uteuzi huo wote umeanza leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Balozi Mteule Victoria Richard Mwakasege
Balozi Mteule Victoria Richard Mwakasege

Balozi Samwel Shelukindo
Balozi Samwel Shelukindo

Balozi Mteule Zuhura Bundala
Balozi Mteule Zuhura Bundala

Balozi Mteule Abdallah Kilima
Balozi Mteule Abdallah Kilima


Balozi Mteule Baraka H. Luvanda
Balozi Mteule Baraka H. Luvanda

Balozi Mteule Innocent E. Shiyo
Balozi Mteule Innocent E. Shiyo

Balozi Mteule Anisa K. Mbega
Balozi Mteule Anisa K. Mbega