How to fold a suit jacket and pack for travel without wrinkles


Taarifa ya walioitwa kwenye usaili TBS


Shirika la Viwango Tanzania linapenda kuwatangazia waombaji wa nafasi za kazi zilizotangazwa 25.5.2015 katika kada zifuatazo, kuwa usaili wa mahojiano utafanyika tarehe 28 na 29 Septemba 2015 katika ofisi za TBS, Ubungo Dar es Salaam:-
 1. Standards Officer II (Pharmacy),
 2. Standards Officer II (Microbiology and Chemistry)
 3. Standards Officer II (Animal Science) 
 4. Quality Assurance Officer II (Microbiology with Chemistry)
 5. Quality Assurance Officer II (Laboratory Science and Technology)
 6. Inspector II (Food & Biochemical Engineering)
 7. Quality Assurance Officer II (Food & Biochemical Engineering) 
 8. Quality Assurance Officer II (Petroleum and Gas)
 9. Metrologist II (Legal and Industrial Metrology)
 10. Metrologist II (Physics)
 11. Chief Procurement Officer
Tafadhali bofya hapa kupakua nakala ya orodha ya walioitwa na taarifa zaidi za mambo ya kuzingatia.

Nani kasema Janeth haambatani na Magufuli na kufanya kampeni?


Mke wa Mgombea Urais wa CCM,Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu.


Wakazi wa Chato wakishangilia kwa shangwe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika shule ya sekondari Chato,jioni ya leo mkoani Geita.


Mke wa Mgombea Urais wa CCM, Mama Janeth John Magufuli akipeana mkono na Mgombea Ubunge wa jimbo la Chato,Dkt Meedad Kalemani mara baada ya kuwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt Magufuli kuwa Rais wa awamu ya tano,pichani kati anaeshuhudia ni Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli.


Mama Janet Magufuli, mke wa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari kuhutubia mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na mamia ya wananchi muda huu. 


Mke wa Mgombea Urais wa CCM, Mama Janeth John Magufuli akiwasalimia wananchi wa Chato na kuwaomba ridhaa ya kumchagua Dkt John Pombe Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika awamu ya tano,kweney uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuwafanyika Oktoba 25 mwaka huu.


Sehemu ya maelfu ya wananchi katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari mkutano wa kampeni


Sehemu ya maelfu ya wananchi katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Chato mkoani Geita tayari mkutano wa kampeni.
 • Picha: Ahmad Michuzi, Jnr/Jiachie blog.

Tanzania NEC calls on police to investigate political militia groups


Arusha (Tanzania) (AFP) - Electoral authorities in Tanzania on Saturday called on police to investigate fears that some political parties were preparing to train militia groups ahead of next month's national elections.

The concern has emerged as campaigning heats up prior to the October 25 polls, in which the long-time ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM) party's candidate John Magufuli is hoping to succeed President Jakaya Kikwete.

But Magufuli, 55, is facing what is seen as the tightest electoral race in the east African nation's history, with the main opposition parties uniting around ex-prime minister Edward Lowassa, 61, who recently defected from the CCM.

"The Commission has received information that certain political parties were preparing to give military training to more than 1,500 youth in order to cause trouble during the elections," Damian Lubuva, the National Election Commission's president, said in a statement.

"Even if this information only comes from one camp, the Commission requests the police to investigate and take the necessary action," it added, without naming any particular party.

"No party is allowed to use such a militia. It is against the law."

The statement also came after one person was killed earlier this month in a clash between CCM supporters and the main opposition Chadema party.

The ruling CCM party has dominated politics since modern Tanzania was formed in 1964, and currently has two-thirds of seats in parliament.

But it has been weakened by internal splits and a string of graft scandals, and recently suffered defections of high-profile members -- including ex-prime minister Frederick Sumaye and former home affairs minister Lawrence Masha -- to the opposition coalition.

Tanzania is one of the region's most stable countries, and Kikwete is also standing down at the end of his second and final mandate -- in contrast to President Pierre Nkurunziza in neighbouring Burundi whose bid to stay in office sparked weeks of violence and a coup attempt.

Another neighbour, Kenya, was also hit by post-election tribal violence in 2007-2008 which left more than 1,000 dead.

Tanzania, with over 50 million people, is east Africa's most populous country, with economic growth of more than seven percent, according to the World Bank.

Despite advances, the country remains very poor by regional and international standards, the World Bank says, with agriculture the key sector, providing a quarter of gross domestic product and employing three-quarters of the population.

Gazeti la MwanaHALISI kuuzwa tena mitaani kuanzia kesho

Saed Kubenea, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers LTD, inayochapisha na kusambaza gazeti la MwanaHALISI akionesha waandishi wa habari (hawapo pichana) nakala ya gazeti la MwanaHALISI litakalotoka kesho.

Gazeti lililokuwa limefungiwa miaka 3 iliyopita, MwanaHALISI limechapwa na kesho litakuwa mtaani nchi nzima kwa ajili ya mauzo -- inaripoti tovuti ya MwanaHALISI Online

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Hali Halisi Publishers (HHPL) inayomiliki na kuchapisha gazeti hilo, Robert Katula nakala moja ya gazeti itauzwa kwa Sh. 1,000.
“Tumeamua kuongeza kidogo bei kwa sababu mbalimbali lakini. Kubwa zaidi ni kupanda kwa kasi kwa gharama za uchapishaji” 
Wakili wa MwanaHALISI, Dk. Rugemeleza Nshala amesema gazeti liko huru kuchapishwa baada ya taratibu za kisheria baada ya uamuzi kukamilika.
“Jaji ametoa amri kwamba wahusika kutoingilia kamwe shughuli za uchapishaji wa gazeti la MwanaHALISI na shughuli za kampuni ya Hali Halisi Publishers. Zuio limetolewa dhidi ya vitendo vyovyote vya kuwanyanyasa na kuwatishia waleta maombi ikiwa ni pamoja na kutowafungia au kusimamisha uchapishaji wa gazeti la MwanaHALISI”
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi Publishers, Saed Kubenea amesema kwa muda wa miaka mitatu ambao gazeti lilifugwa kampuni yake imepata hasara hivyo kusababisha shughuli za kampuni hiyo kudolola.
“Kwa muda wa miaka mitatu, mwezi mmoja na siku tano kwa makadilio ya hasara tuliyopata ni Sh. 6.8 bilioni. Kitu kinachoskitisha ni kwamba fedha hizo ni za walipa kodi wa nchi hii. Ni fedha ambazo zinapaswa kwenda kuboresha huduma za afya, elimu, kuchimba visima na kujenga barabara,”
Aidha, Mhariri wa MwanaHALISI, Jabir Idrissa ameitaka serikali kutunga sheria ambayo itawalazimisha viongozi wake wanaoisababishia hasara kulipa hasara hizo badala ya fedha za walipa kodi kutumika.
“Waziri Fenella anataka kwenda bungeni kutunga sheria wakati ameshidwa kufuata sheria. Zipo nchi ambazo hasara kama hizi anarudishiwa ofisa wa serikali aliyezisababisha” 

Picha za Meshack akijiandaa kwa kilimo cha parachichi

Nimekuta mjasiriamali Meshack Maganga ameandika katika ukurasa wake wa Facebook, nikaisambaza kwa faida ya wengine...

Not long ago my wife Rose Ambali said, " It's good to be something you feel in your heart. That's where it all begins. She said, you won't complain so much about work, because it will be something you enjoy no matter what. 

Sasa Leo nilienda sokoni kwa mama muuza Parachichi, nikamuomba Parachichi zilizoharibika.

Kwanza alinishangaa. Akaniuliza "Mwanangu mbona yameoza? Nikamwambia hayo yaliyooza ndiyo ninayataka, akanipatia bure.

  

Nimefika nyumbani nikaanza kazi ya kuyamenya na kuyasafisha. Wakati ninaendelea kusafisha hizi mbegu za parachichi, nikamkumbuka mama, mentor wangu na mjasiriamali Haika Lawere aliyewahi kuniambia kwamba ' Ukitaka kutoka sehemu moja hadi nyingine kijasiriamali badilika, tenda zaidi ya unavyoongea'....!Kuna vitu unavifanya bila kutumia pesa nyingi, mfano hizo mbegu za parachichi nimepewa bure, labda nauli ya daladala kutoka nyumbani shilingi mia 4 na kurudi mia 4. 

Hizo mbegu nitazipeleka shambani. Kila mti wa parachichi utaniletea pesa miaka michache ijayo. Zaidi ya hapo, miche itakayozidi nitaiuza kwa wakulima wenzangu watakaohitaji. 

Mche wa kawaida wa parachichi huuzwa shilingi 700/= hadi 1,000/= kwa Iringa. Lakini Nikizifanyia "Bading" nitauza kwa shilingi 3,000/=. Mtaalamu wa kufanya hiyo kazi yupo Ndugu Nicolaus Kulanga . Hii ni pesa na ni ajira kamili kwangu. Kumbuka nimeokota sokoni. Miparachichi ikifanyiwa bading huanza kutoa matunda baada ya miaka mitatu hadi miaka minne. 

I wish I could tell you that the rest is history. Tanzania is a great country; the harder you work, the luckier you get. Na kama alivyoniambia mkulima mwenzangu Hadija Jabiry (Mama B' Ministry) kwa msisitizo kwamba soma Yoshua 1: 9 ' Je si Mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na Moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike'... 

Na uchaguzi unabakia mikononi mwangu, kuwa hodari na moyo wa ushujaa ama kufadhaika. 

The cost of continuing to not get this knowledge is up to you. Nobody else.

Go big or go home and watch Tv.

Imani: Aina 10 za biashara (business ideas) za kufanya sasa

Je, Unahitaji Kufanya Biashara Na Hujui Ni Biashara Ipi Ya Kufanya? Soma Hapa Kujua Ni Biashara Ipi Ya Kuifanya Sasa


Wapo watu ambao mara nyingi hujiuliza ni biashara gani wafanye katika maisha yao ambayo itaweza kuwaingizia pesa nyingi ya kutosha. Ni wazo ambalo hutokea kutokana na pengine kuona kila biashara wanayoitazama kwa wakati huo kama hailipi. Hali hiyo husababisha mkanganyiko mkubwa wa mawazo ambao husababisha wabaki njia panda.

Kama imeshawahi kukutokea hali kama hii kwa namna moja au nyingine makala hi ni muhimu sana kwako kuisoma. Kwa kusoma makala hii inakuonyesha kwa uwazi orodha za biashara ambazo unatakiwa uzifanye ukiwa katika mazingira uliyopo. Karibu kila biashara ipo hapo, kazi ni kwako kuchagua mojawapo unayoipenda na kuifanya, acha kulalamika tena kuwa huelewi nini cha kufanya.
Twende kwa pamoja kuzijua biashara hizo ambazo unauwezo wa kuzifanya na kukufikisha kwenye mafanikio makubwa:-

1. Kutengeneza na kuuza chaki

Hii ni moja ya biashara nzuri unayoweza kuifanya na soko lake liko juu. Unaweza ukanunua mashine yako za kutengeneza chaki na kisha ukaanza kuzisambaza kwenye stationary au mashuleni. Uzuri wake mashine hizi za kutengenezea chaki gharama yake pia sio kubwa sana ni ya kawaida tu ambayo hata wewe unaweza kuimudu. Hii inaweza ikawa ni sehemu mojawapo ya kuingizia kipato chako.

2. Kufungua duka la kuuza asali


Uzuri wa bidhaa hii muda mwingi soko lake lipo juu. Ni biashara ambayo unaweza ukaifanya kwa kuagizia asali kutoka kwa wakulima kama nilivyo mimi na kisha kuanza kuiuza moja kwa moja katika vipimo vinavyotakiwa.

Kama huwezi kufungua duka hili unaweza ukafanya mbadala wake ukaenda kutengeneza mizinga wewe mwenyewe na kuwafuga. Pia hii ni biashara ambayo ni nzuri kwako kukuingizia kipato kikubwa kwa urahisi.

3. Kuanzisha biashara ya kuuza vyakula katika matamasha mbalimbali

Hapa siyo lazima uwe na Hotel au Mgahawa ndiyo uanzishe biashara ya namna hii. Kikubwa unahakikisha unakuwa makini na sherehe katika eneo ulilopo. Kama ni kuweka mawakala watakao kusaidia kukujulisha kuwa eneo fulani kuna sherehe ya aina fulani na siku fulani itakuwa nzuri zaidi kwako kuchangamkia tenda hizo mapema.

4. Kujenga nyumba za kulala wageni

Kama mtaji wako unaruhusu hii ni moja kati ya biashara nzuri kuifanya. Ni biashara ambayo hahitaji kukimbizana sana ukishamaliza kujenga, zaidi unatakiwa kuweka mfumo sahihi wa kusimamia na kuanza kuingiza pesa. Na kwa bahati nzuri kwa Tanzania yapo maeneo mengi ambayo yanauhitaji mkubwa wa huduma hii. Ni Biashara nzuri kuifanya hata kama umri umeenda, kwa sababu haihitaji mkimbizano mkubwa.

5. Kutengeneza matoroli/mikokoteni na kuikodisha

Katika hili hapa unatakiwa kutengeneza kwa idadi unayoitaka na unamwachia kijana ambaye anaikodisha huku ukiendelea na majukumu mengine. Unaweza ukaiona ni biashara ndogo lakini fuatilia kwa waliowekeza nguvu na mawazo yao hapo wakwambie kile wanachokipata utashangaa.

6. Kuazisha huduma ya AIRTEL MONEY, MPESA, TIGOPESA, EZYPESA

Hakuna ubishi hii ni moja ya huduma ambayo imezagaa kila eneo na watu wengi wanaihitaji. Kikubwa ni juhudi yako na kuzingatia eneo uliloweka biashara yako liwe hasa la mzunguko mkubwa zaidi kukuwezesha kufanya biashara hii vizuri.

7. Kupamba maharusi na kumbi za harusi/sherehe

Pia unaweza ukajiingiza hapa na kushughulika na kupamba tu maharusi. Kama hujui sana ni kitu cha kujifunza pia, kisha unachangamkia sherehe zinazojitokeza mjini.

8. Kuanzisha kilimo cha kisasa

Wengi wanaposikia kilimo kichwa kinakataa. Lakini ikiwa utawekeza kwenye kilimo cha kisasa na cha kitaalamu ambacho unategemea kumwagilia zaidi, uwe na uhakika unatoka. Yapo mazao mengi unaweza ukalima lakini mojawapo ni kitunguu. Inaweza ikawa ni njia rahisi ya kufikia mafanikio yako kuliko unavyofikiri.

9. Mashine za kusaga na kukoboa nafaka

Pia unaweza ukajitengenezea kipato chako na kuwa kikubwa na cha uhakika kwa kufunga mashine hizi. Kila siku watu wanahitaji kula hivyo ukifunga mashine hizi ni rahisi sana kupata wateja wa kuwauzia unga na kupata faida. Na uzuri mahindi ya kusaga yanapatikana maeneo mengi kwa wingi kama kule Kibaigwa (Dodoma), Gairo(Morogoro), Kiteto(Manyara) na maeneo mengine mengi kama Iringa na mbeya.

10. Yadi kwa ajili ya kupaki magari

Kitu unachotakiwa hapa ni kununua kiwanja na kukigeuza kuwa yadi ambapo magari yanakuwa yanapaki iwe kwa kulala au kwa muda. Kila gari linalokuwa linapaki linakuwa linatozwa kiasi fulani cha pesa ambacho kinakuwa ndiyo hiyo huduma unayoitoa.

Zipo aina nyingi sana za biashara ambazo unaweza ukazifanya na kukuingizia kipato. Katika Orodha ya kipande cha makala hii kinachoendelea zimebaki biashara zaidi 110 ambazo sijaziweka hapa kutokana na ufinyu wa nafasi. Kuzijua zinazoendelea na ufafanuzi wake unaweza ukaniandikia email kwenda [email protected] nitakutumia mara moja.

ILA KAMA YOTE HAYO UTASHINDWA KUPATA LA KUFANYA WEWE UTAKUWA UMESHAPOTEA, ENDELEA NA UTARATIBU WAKO WA KUILAUMU SERIKALI.

Tunakutakia ushindi katika safari yako ya mfanikio, ila kumbuka daima tupo pamoja mpako maisha yako yaimarike.

Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035

Video nzima ya #MkikiMkiki: Mdahalo ulioshirikisha ACT-Wazalendo, ADC, UKAWA na UPDP


Video ya mdahalo wa pili wa #MkikiMkiki kuhusu UTAIFA uliowashirikisha wawakilishi kutoka ACT-Wazalendo, NCCR-Mageuzi (UKAWA), ADC na UPDP.


Joto la Uchaguzi Mkuu baina ya wafuasi, wagombea Ubunge Mbeya


Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi akiwa sambamba na dereva wake akibishana na wafuasi wa Chama cha Mapinduzi baada ya kuvamia eneo lao la mkutano wa kampeni za Ubunge katika kata ya Ghana.


Vijana wa boda boda wanaomuunga mkono Joseph Mbilinyi wakizuiliwa na Green Guard wa CCM.


Baadhi ya viongozi wa CCM wakimsihi Joseph Mbilinyi kutoendelea na safari yake na badala yake ageuze lakini bado aliendelea na maamuzi yake.
Wanachama wa CCM waliokuwa kwenye mkutano wa kampeni wakilizuia gari la Joseph Mbilinyi kupita katika eneo hilo
Joseph Mbilinyi akiwasili eneo ambalo CCM wanafanyia mkutano na kukutana na umati wa wanaccm waliomzuia kupita

WATU 9 wamejeruhiwa na gari na pikipiki kuharuibiwa vibaya kutokana na vurugu zilizotokea baina ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na Chama cha Mapinduzi(CCM).

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa lilitokea juzi majira ya saa kumi na moja jioni eneo la Mbata – Buchani, Kata ya Ghana jijini hapa.

Alisema tukio hilo lilitokea wakati mgombea ubunge Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CCM, Sambwee Shitambala akiwa na wafuasi wake, wapenzi wa chama hicho alikuwa akifanya mkutano wa kampeni katika eneo hilo kwa mujibu wa ratiba yake.

Alisema mgombea huyo akiwa katika mkutano huo, mgombea ubunge jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Joseph Mbilinyi alikuwa akipita eneo hilo akiwa na msafara wake kuelekea maeneo ya Nsoho kwenye mkutano wa kampeni.

Kamanda Msangi alisema kutokana na kitendo hicho wafuasi wa CCM ambao walionekana kuwa wengi hadi eneo la barabara hivyo kupelekea msafara wa Mbilinyi kutoweza kupita eneo hilo hali iliyopelekea kuzuka kwa vurugu zilizopelekea kujeruhiwa kwa watu na uharibifu wa mali.

Aliwataja majeruhi wa vyama hivyo vya siasa kuwa ni Robert Kerenge (58) Katibu wa CCM Wilaya ya Mbeya, Salum Mwansasu (35) mkazi wa Majengo (CCM), Atupele Brown (39) mkazi wa Ghana (CCM), Rose Nelson (30) mkazi wa Majengo (CCM),Sakina Salum (25) mkazi wa Ghana (CCM), Malanyingi Matukuta (31) mkazi wa Forest (CCM), Agabo Mwakatobe (44) mkazi wa Ghana (CHADEMA), Jailos Mwaijande (23) mkazi wa Itiji (CHADEMA) na Gabriel Mwaijande, dereva wa mgombea Ubunge (CHADEMA).

Kamanda Msangi aliongeza kuwa katika vurugu hizo gari la mgombea ubunge jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya Chadema Joseph Mbilinyi aina ya Toyota land cruiser yenye namba za usajili T161 CPP liliharibiwa kioo cha mbele, taa moja ya nyuma upande wa kushoto na kioo cha upande wa dereva kwa kupigwa mawe.

Alisema pia pikipiki zenye namba za usajili T332 CHV aina ya T-better na T383 CSE aina ya Skymark ziliharibiwa kwa kuvunjwa side mirror za upande wa kushoto na zipo kituo cha polisi kati.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa ratiba ya kampeni za uchaguzi iliyotolewa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa tarehe 17.09.2015, ilikuwa ikionyesha Chadema saa 4 asubuhi hadi saa 9 alasiri walitakiwa kufanya mkutano Kata ya Nsoho na saa 9 alasiri hadi 12 jioni walitakiwa kufanya mkutano Kata ya Maendeleo wakati Ccm kwa mujibu wa ratiba walitakiwa kufanya kampeni Kata ya Itende saa 2 asubuhi hadi saa 7 mchana na saa 7 mchana hadi saa 12 jioni mtaa wa Mbata, Kata ya Ghana ambapo tukio hili lilipotokea.

Alisema upelelezi unaendelea ikiwa ni pamoja na kupeleka jalada la uchunguzi kwa mwanasheria wa serikali ili waliohusika katika vurugu hizo wafikishwe mahakamani.


Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Mbeya mjini, Sambwee Shitambala akizungumza katika mkutano wa kampeni kata ya Ghana


Meneja Kampeni wa Mgombea Ubunge Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CCM, Charles Mwakipesile akimnadi mgombea Sambwee Shitambala


Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM Mbeya mjini, Philimon Mng'ong'o akiwaongoza wafuasi na wapenzi wa Chama hicho kuimba nyyimbo za hamasa
Baadhi ya wanachama wa CCM waliojitokeza kusikiliza sera za mgombea ubunge

MGOMBEA Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi(SUGU) ambaye pia anatetea nafasi yake alijikuta katika wakati mgumu baada ya kushuhudia gari lake likipopolewa kwa mawe na wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Tukio hilo lilitokea baada ya Sugu akiwa na msafara wa vijana wa bodaboda wakipita eneo anbalo Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM, Sambwee Shitambala alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni katika kata ya Ghana jijini Mbeya.

Sugu na msafara huo walifika eneo hilo kwa kile kilichodaiwa walikuwa wakielekea Kata ya Nsoho majira ta saa kumi na nusu jioni ambapo alizuiliwa na wafuasi wa CCM ambao walimwamuru kupita njia nyingine lakini alikaidi na kulazimisha kupita kwa nguvu ndipo vurugu zilipoibuka na kuvunjwa kwa vioo vua gari ya mbunge huyo.

Hata hivyo baada ya kufanikiwa kupenya Mbilinyi alirudi tena baada ya saa moja akiwa amebadilisha gari huku akiwa ameongeza idadi ya vijana wa bodaboda ambao walikuwa wameshika silaha mbali mbali yakiwemo marungu ambao makada wa CCM baada ya kuona hivyo waliamua kuwapisha kuendelea na safari yao.

Baadhi ya wananchi waliokuwepo eneo la tukio walisema alichokifanya Sugu ni ukorofi kwani alikuwa ameshamaliza mkutano wake wa Kampeni katika Kata ya Nsoho hivyo kitendo cha kurudi kulikuwa na ishara ya vurugu na kwamba njia za kuelekea eneo hilo zipo zaidi ya mbili hivyo alikusudia kufanya fujo.

Akizungumzia sakata hilo, Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Wilaya ya Mbeya Mjini, Philimon Mg’ong’o alisema kwa sasa hawako tayari kuvumilia vitendo vya vurugu ambavyo Chama chake kimekuwa kikitendewa na vijana wa Chadema wakiongozwa na mgombea wao.

Naye Meneja wa kampeni wa Ngombea Mbunge wa CCM, Charles Mwakipesile alisema Sugu pamoja na wafusi wake wa Chadema wamepanga kuharibu ratiba ya CCM ya kufanya kampeni jambo ambalo hawatakubali kufayiwa hivyo na badala yake wataendelea na kampeni na hawako tayari kwajibu kwa sasa bali adhabu yao ni Oktoba 25 mwaka huu.

Aliongeza kuwa hata mabadiliko wanayoyahubiri kila siku ni kuwaondolea amani wakazi wa Mbeya na kuwapeleka kwenye vurugu ambazo dalili zake zimeanza kuonekana kabla ya uchaguzi mkuu na kwamba wakazi wa Jiji la Mbeya wanayonafasi ya kuchagua amani ama vurugu.

Kwa upande wake Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM), Sambwee Shitambala, alisema hizo vurugu zilizofanywa na Sugu ziliandaliwa siku nyingi hivyo wanachofanya ni utekelezaji tu ambapo hadi sasa aneshavamia mikutano mitatu ya CCM ikiwa ni pamoja na kujipitisha pitisha wakati Mgombea Urais wa CCM Dk. Magufuli alipokuwa akihutubia katika viwanja vua Ruanda Nzovwe.

Alisema yote hayo majibu yake wanayo wakazi wa Jiji la Mbeya kwa kuamua kuchagua kati ya fujo au amani na kuingeza kuwa endapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge wa Mbeya mjini atahakikisha amani inapatikana ili machinga, Bodaboda, mama ntilie na wafanyabiashara waendeshe shughuli bila bugudha zozote.

Alisema atahakikisha viwanda vinafufuliwa ili vijana wengi wasio na kazi waweze kupata ajira ikiwa ni pamoja na kupunguza uhalifu kwa vijana wanaokosa kazi na kuzurura mitaani pia kuboresha miundombinu ya barabara zikiwemo kilomita kumi alizoahidiwa na mgombea Urais endapo atapita.

Picha za maonesho ya ndege za kivita


Maonesho ya ndege za kivita na vifaa vingine kutoka majeshi ya Marekani, yamefanyika siku Jumamosi, Septemba 19, 2015 na kuhudhuriwa na maelfu ya watazamaji.

Maonesho hayo yasiyo na kiingilio, yaliambatana na maadhimisho ya miaka 100 ya jeshi la maji nchini hapa.

Hongereni vijana wadogo Briana Kagemuro na Bryan Mwombeki

Briana Kagemuro na Bryan Mwombeki wakiwa katika picha ya pamoja na walimu wao wa mchezo huo mapema leo siku ya Jumamosi Septemba 19, 2015 baada ya kushinda makombe yao.

Vijana wenye asili ya Kitanzania Briana Kagemuro na Bryan Mwombeki wameonyesha umahiri wa mchezo wa Tennis uliofanyika leo Jumamosi, September 19,2015 katika viwanja vya nyumbani kwao South East Tennis and Learning Center, South East Washington, DC.

Briana Kagemuro alikuwa katika kinyanganyiro cha Wasichana wenye umri wa miaka 12 Singles (Girls 12 singles) ambapo alimshida Isabella De Leo 6-4, 6-4; Cassi Chen 7-6, 6-3, 10-6 na Asha verma 6-4, 6-4.

Naye Bryan Mwombeki alipata kombe lake la ushindi la wavulana wenye umri wa miaka 10 (USTA) (Boy's 10 Singles) dhidi ya Jason De Silva 4-0,4-0, Arbert Vardimisky 4-3, 4-1; Aarush Rajanala 4-1, 4-2.

Bryan Mwombeki


Briana Kagemuro

Balozi mpya wa Tanzania - Marekani akabidhi hati za utambulisho kwa Rais Obama


Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa na Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama mara baada ya kukabidhi hati za utambumbulisho (White House). Washington DC siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.


Mhe. Wilson Masilingi Pamoja na Familia yake wakiwa Katika nyuso za furaha mara baada ya kukabidhi hati za utambulisho Ikulu ya Marekani(White House) siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015. Kutoka kushoto ni Mtoto wa Balozi ndugu Nelson Masilingi, Rais wa Marekani Barack Obama, Balozi Wilson Masilingi, pamoja na Marystella Masilingi. Mke wa Balozi.


Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wilson Masilingi na familia yake mara baada ya kurudi nyumbani kwake Bethesda, Maryland alipotoka kukabidhi hati za Utambulisho kwa Rais Barack Obama siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.
 • Picha tumeshirikishwa na Kamera ya Ubalozi via Kwanza Production