[Update] NEC yazungumzia hatma ya kupiga kura waliopoteza vitambulisho

Taarifa mpya kutoka kwenye gazeti MTANZANIA:

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema waliopoteza vitambulisho vya kupigia kura wataweza kupiga kura endapo watakuwa na taarifa ya polisi na majina yao kuwamo katika daftari la mpiga kura.

Hayo yalielezwa Dar es Salaam jana na Kamishna wa NEC, Mary Stelalongwe alipotoa ufafanuzi kuhusu watu wanaozunguka mitaani kuandika namba za vitambulisho vya wapiga kura.

Alionya kuwa kufanya hivyo ni kosa ingawa alisema NEC haina taarifa rasmi ya matukio hayo.


Wakati zaidi ya robo tatu ya vifaa vinavyohitajika vikiwa vimewasili nchini, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema inaangalia namna ya kuwasaidia waliopoteza vitambulisho vyao kushiriki kupiga kura.

Kauli hiyo imetolewa baada ya idadi ya watu wanaotoa taarifa za kupotelewa na vitambulisho vya kupigia kura pamoja na wanaowasilisha vitambulisho vilivyookotwa kwa tume kuendelea kuongezeka kila siku licha ya uhakiki na uhamishaji wa taarifa za mpiga kura kumalizika mapema mwezi huu.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari wa NEC, Clarence Nanyaro amesema ni changamoto kwa tume kutokana na wingi wa watu wenye tatizo linalofanana na hatma yao ya kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba.
“Kwa wale waliojiandikisha na wakahakiki majina yao lakini wamepoteza vitambulisho tutaangalia namna ya kuishawishi tume itafute jinsi ya wao kushiriki kupiga kura kwasababu majina yao yapo kwenye datfari na yatarudishwa vituoni. Watakachotakiwa ni kuwa na ripoti ya upotevu huo kutoka polisi (Loss report),” 
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) cha tume hiyo kinaendelea na kupakia taarifa za watu wote waliojiandikisha na Nanyaro amewatoa shaka wale ambao mpaka sasa wanaambiwa hawaonekani kwenye kumbukumbu.

Nanyaro amewataka wawe na uhakika wa kushiriki uchaguzi na kubainisha: 
“Kuna wale ambao wakihakiki taarifa zao kwa njia ya simu wanaambiwa hawatambuliki. Wasiwe na wasiwasi. Kazi ya kuingiza majina yote kwenye mtandao inaendelea na baada ya muda mambo yatakuwa sawia. Kama wanavitambulisho, inatosha kuwatambua hivyo wawe na subira’
Imenukuliwa kutoka gazeti la MWANANCHI

Hatua 8 za kuchukua unapokosa matokeo mazuri ya unachofanya


Kuna wakati katika maisha yako unaweza ukajikuta unafanya kila kilicho sahihi kwako ili kupata matokeo unayotaka, lakini kitu cha kushangaza matokeo hayo unakuwa huyapati. Ni kweli unaweza ukawa unafanya kazi kwa bidii, una mipango na umejiandaa vizuri, lakini kila ukiangalia bado havikuridhishi na havifanyi kazi sawasawa.
Ukweli huu unakuja kuuthibitisha mwenyewe kila unapotazama mabadiliko makubwa hayatokei ikiwa ni pamoja na kutengeneza pesa za kutosha, zaidi unajiona kama uko palepale. Kwa hali hii inapokutokea inakuwa ni rahisi sana kutaka kukukatisha tamaa. Hiyo yote inakuwa hivyo ni kwa sababu unakuwa unashindwa kujua wapi ulipokosea kama ni uwezo wote umeuweka hapo lakini matokeo huyaoni.

Kwa hiyo kwa vyovyote vile unakuwa unaona mipango yako au kile unachokifanya kimeshindwa. Hivyo basi, akili yako yote inakuwa inapiga sana kelele na kukuambia kuwa ni lazima kubadilisha njia nyingine kwa hili haliwezekani tena. Hali inaweza ikawa imekukuta kwa namna moja au nyingine, unapokumbana nayo unafanyaje?

Katika makala yetu ya leo nimekuwekea mambo ya kufanya kama kile unachokifanya hakikupi matokeo unayoyataka. Kwa kufanya mambo hayo yatakusaidia kuweza kuendelea mbele hata kama ulihisi umekata tamaa. Kikubwa cha kufanya ni kuweza kuyafanyia kazi ili yakusaidie kupata mwelekeo, nguvu na dira mpya ya kukufikisha kwenye mafanikio unayoyahitaji.

Yafuatayo Ni Mambo 8 Ya Kufanya Kama Kile Unachokifanya Hakikupi Matokeo Unayoyataka.
 1. Chukua muda kila siku kutafakari ni kwanini hupati matokeo unayoyataka. Angalia ni wapi unapokosea hata kama kila kitu unacho kisha jirekebishe na endelea kung’ang’ania mpaka uyaone mafanikio yako.
 2. Tafuta msaada kwa kupata ushauri kwa watu uliokaribu nao. Watu hao hakikisha wawe ni wale wanaofanya kile kinachoendana na wewe. Kwa ushauri wao watakupa uzoefu wao ambao utakusaidia kuendelea kusonga mbele kwa mtindo tofauti badala ya kuacha.
 3. Kuwa makini na watu wanaokuzunguka katika kipindi hiki. Ni rahisi wakakukatisha tamaa na kukwambia wewe tena ndiyo basi huwezi tena. Kwa maneno yao unaweza ukaamini na ukachukulia huo ndiyo ukweli na ukajikuta umekwama.
 4. Badili mipango yako upya jinsi ya kufanya hicho kitu ulichokuwa ukikifanya kwa namna ya tofauti tena. Ukibadili hiyo mipango na kuboresha zaidi katika maeneo mengine unaweza ukapata matokoe uliyokuwa ukiyahitaji kwako hapo mwanzo.
 5. Badili mipango yako upya jinsi ya kufanya hicho kitu ulichokuwa ukikifanya kwa namna ya tofauti tena. Ukibadili hiyo mipango na kuboresha zaidi unaweza ukapata matokoe uliyokuwa ukiyahitaji kwako hapo mwanzo.
 6. Chukua muda kiasi wa kukaa chini na kutuliza akili yako na kufanya tahajudi (Meditation) ili kuipa akili yako nguvu zaidi ya kufanya kazi kwa ubunifu mkubwa.
 7. Kama ulikuwa ni mtu wa kufanya mambo mengi ni bora ukabadili mwelekeo wako na kuanza kuweka nguvu na uwezo wako wote kwenye kitu kimoja mpaka kikupe matokeo chanya unayoyahitaji.
 8. Kumbuka mafanikio hayaji tu kwa urahisi wakati mwingine yanakuja kwa kutumia kanuni ya ung’ang’anizi. Hivyo basi ng’ang’ana mpaka upate matokeo unayoyataka. Inapotokea mambo yamegoma jaribu tena na tena mpaka mlango wa mafanikio utafunguka.
Kuwa tayari kubadilika na kufanyia kazi mambo hayo muhimu ili kubadili hatima ya maisha yako. Hata hivyo kama kitu hicho ni kweli unaona kabisa huwezi kukibadli basi ni vyema ukaangalia namna nyingine ya kufanya ambayo itakuwa nafuu kwako kuliko kung’ang’ania sana ambako kunaweza pengine kukupeleka kubaya.

Tukutakia ushindi katika safari ya mafanikio yako na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kujifunza na kuhamasika kila siku.

Kwa makala nyingine nzuri karibu pia katika DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuboresha maisha.

Imani Ngwangwalu,
0713 048035, [email protected].

Mapitio ya magazetini Septemba 22, 2015


Mnyororo wa utajiri - Sehemu ya pili


Ukitaka kufanikiwa ambatana na waliokusudia kufanikiwa. Kundi hili naamini tumekusanyika watu tuliodhamiria kufanikiwa, kwa hiyo ukiwa hapa uwe na uhakika kwamba upo mahali sahihi kabisa.

Ninaendelea na mada yangu ya mnyororo wa utajiri, sitakuwa na wasaa wa kurudi nyuma isipokuwa kwa ufupi ni

kwamba nilikueleza kwamba mnyororo wa utajiri ni uhakika wa wewe, watoto wako na wajukuu zako kuwa safi kiuchumi kutokana na bidii, misingi na mambo utakayoyafanya sasa na hapo baadae.

kimsingi ni kwamba una aina mbili ya maisha ambayo watu wanaishi
1. Kufanya kazi kwa ajili ya kujitosheleza wao binafsi
2. Kufanya kazi kwa ajili ya kuwatosheleza wengine. Nikiongeleza kujitosheleza namaanisha kuwa mtu anafanya kazi kwa ajili yake, watoto wake na pengine nduguze basi!

Tunapoongelea mnyororo wa utajiri tunakusudia ile namba 2 ambapo mtu anafanya kazi kwa ajili ya kuwatosheleza wengine. Swali la kujiuliza ni hili, je, picha gani inakujia kichwani kila unapopata mshahara? (kama umeajiriwa)

Je inakuja picha ya kulipa madeni, kulipa kodi, kununua chakula, halafu hela inakata kabla picha nyingine haijaonekana? Kama wewe ni mfanyabiashara, mjasiriamali ama huna ajira, je, nini kinakuja kichwani mwako unapoitazama kesho yako?Kama unaiona familia yako pekee huko ni kuishi ama kupanga kuishi kwa kujitosheleza na kama unaona picha zaidi ya hapo basi huenda unafikiria wengine.

Mtu mwingine ataniuliza, kuna haja gani nifikirie kuwatosheleza wengine? Ama atanieleza kuwa kila mtu atajijua kivyake! Siri iliyopo ni kwamba, hakuna mtu anaeweza kufanikiwa isipokuwa amewafikiria wengine.

Muuza genge anapata faida kwa sababu amewafikiria wanaohitaji mahitaji ya nyumbani. Mwenye basi anapata faida na maendeleo kwa sababu anawafikiria wenye shida ya kusafiri. Mama Ntilie asingepata faida isipokuwa amewafikiria wenye njaa.

kwa maana hii utaona kwamba mafanikio ama niseme maendeleo ni matokeo ya kujituma ama kulazimishwa kuwafikiria wengine. Nimesema kujituma ama kulazimishwa kuwafikiria wengine kwa maana kuwa mafanikio ni ama uvutiwe kufanikiwa au ulazimishwe kufanikiwa.

Ndio! mafanikio yeyote ya maana(makubwa) hayaji mpaka uwe umevutiwa kufanikiwa ama umelazimika kufanikiwa. Kuna wakati ambapo unafanikiwa kwa kuvutiwa na waliotangulia kufanikiwa na kuna wakati shida na matatizo vinakulazimisha kufanikiwa!

Hii dhana ya kufanikiwa kwa kujituma/kuvutiwa na kufanikiwa kwa lazima kwa kimishenari wanasema push-pull power. Mifano ya hii dhana unaweza kuipata kwa makabila mawili, wakinga na wachaga. (Wachaga na wakinga wenzangu msimaindi kwa kuwa nimewataja)
Sehemu kubwa ya Wachaga huwa wanadhamiria kufanikiwa kutokana na kuiangalia mifano ya waliowatangulia. Kwao (walio wengi) kinachowafanya kupambana na maisha sio ugumu wa maisha uliopindukia, bali ni kiu ya kufika kukubwa zaidi ya ama sawa na waliomtangulia. Historia ya wakinga ipo tofauti kidogo. Kwao hawa dini ilichelewa, elimu ilichelewa; kwa hiyo familia nyingi zilikuwa katika umasikini uliopindukia.

Kilichokuwa kikiwafanya wakinga wotoke huko milima ya ukingani kwenda kutafuta vibarua kama manamba kwenye mashamba ya chai, mkonge, n.k ilikuwa ni maisha magumu yaliyokuwa yakiwatandika .

Wengi wao walikuwa hawana namna, ni eidha wabaki huko Ukingani na wafe kwa njaa na maisha magumu ama watoke na kwenda kutafuta ili waishi! Hii ya wakinga ndo inaitwa push power na ile ya wachaga inaitwa pull power.

kwa kusema hivyo haimaanishi kwamba hakuna wachaga wanaotoka kwa push power, ama wakinga wanaotoka kimaisha kwa pull power, isipokuwa nimesema sehemu kubwa ya wachaga na nikasema hivyo kukuonesha namna wakinga wengi walivyotoka kihistoria .Pointi yangu sio kutaka uwajue wachaga ama wakinga, bali nataka uone mazingira mawili yanayoweza kukutoa kimaisha.

1. Kama unadhani umeshafika kimaisha, huna namna itakayokutoa hapo kwenda mbele isipokuwa umetumia pull power, yaani kwa hiari yako uwatazame walio mbele yako na udhamirie kufanya sawa ama zaidi yao
2. Kama unapitia kwenye kipindi kigumu kimaisha, ni muda mzuri wa kuamua ikiwa ufie hapo ama uinuke na kupambana

Hata hivyo katika mazingira yote mawili hapo juu, no. 1 na no. 2, msingi wa kutoka hapo ni wewe kuwafikiria wengine. Kwa mfano kama unadhani umeridhika, labda kwa sababu una kazi nzuri na mshahara mkubwa ambao unatosha kusomesha watoto wako na kujihudumia na wale wanaokuzunguka; ili utoke hapo itabidi uwafikirie wagonjwa ili upate hamasa ya kujenga hospitali, uwafikirie watoto ili upate hamasa ya kujenga shule yako, uwafikirie yatima ili uanzishe kituo cha kuwalea, uwafikirie abiria ili ununue mabasi ama ndege, na orodha inaendelea.

Unajua kinachowafanya watu waridhike na kuona kana kwamba wameshafika na kumaliza katika maisha ni kwa sababu ya mawazo na ndoto za kibinafsi. Ukiwa na ndoto kubwa na mawazo ya kuwafikiria wengine, huwezi kufika mahali ukasema hela zimekutosha ama ukapumua eti ukajiona umefika...

kama wewe ni mwalimu jaribu leo kuwaza kumiliki shule yako uone kama utaridhika na huo mshahara wa ualimu. Kama wewe upo kwenye shirika la kimataifa, jaribu kuwaza kufungua shirika lako mwenyewe siku moja huko mbeleni, uone kama mshahara na marupurupu wanayokupa yatakuzuzua.

Mimi huwa nashangaa hata ninapomkuta daktari amebweteka na kuridhika na kibarua chake, moyoni huwa najua kwamba huyu daktari karidhika kwa sababu kichwani mwake hakuna hospitali kubwa na ya maana.Nafahamu kuwa kundi kubwa la watu lipo hapa no. 1 moja, ambapo wameridhika na hatua walizofikia, wanapumua, wanajiona wamefika.

Hata katika sababu no. 2 ya kutakiwa kukufanya ufanikiwe, yaani push power; uhalisia ni kwamba kufanikiwa kwako kutategemea namna unavyowafikiria wengine. Kama ilivyokuwa kwa Wakinga, hatua ya kwanza unapokwama na unapokuwa huna namna nyingine ni kufikiria wanaokuzunguka.

Unafikiria: ni kweli maisha yamenipiga, lakini nikibaki hapa bila kuinuka na kupambana itakuwaje wanangu, itakuwaje mke wangu, itakuwaje wadogo zangu n.k.

Albert Sanga. 
Iringa

Jinsi Shetani alivyo na maslahi na umaskini


NDANI YA KILA MTU UNAYEMFAHAMU KUNA MTU MWINGINE USIYEMFAHAMU:

Kila binadamu ana utu wa nje na utu wa ndani. Utu wa nje unaweza kuwa imara kuliko utu wa ndani na utu wa ndani unaweza kuwa imara kuliko utu wa nje.

Vyovyote iwavyo hatima ya maisha ya mtu huamuriwa na  utu wa ndani. Huko ndiko mtu hufanya tafakari na kuchukua maamuzi ya mwisho. Maana yake ni kuwa utu wa ndani ukiwa mlegevu hata maamuzi ya mtu yatakuwa malegevu na matokeo atakayopata mtu huyo ni malegevu pia.

Kuna wengine unaweza kuona ni jitu lenye afya njema na nguvu nyingi lakini utu wake wa ndani ukawa dhaifu sana na hapo ndipo utasikia, "huyu mambo yake hayaendani kabisa na jinsi alivyo".

Kuna mwingine ana afya njema na ni pandikizi la mtu na utu wa ndani ni imara basi watu watamsifu kwa kusema, "vile unavyomuona na ndivyo alivyo mpaka 'rohoni'".

Wengine wana miili midogo wanafanya mambo makubwa, wengine umri mkubwa wanafanya mambo ya umri mdogo kabisa, kwa hiyo ni wazi kila binadamu ana mtu wa pili ndanimwe ambaye anaathiri fikra, matamshi, na matendo na hatimaye matokeo ya maisha yake. Katika hali halisi ni nadra sana utu wa nje kuwa bora kama utu wa ndani ni wa ovyo ovyo. Wengine utu wa ndani ni ovyo lakini kwa nje utu wake ni bora, huyo si bora bali anapretend (kujishaua).

Kwa hiyo jukumu la mtu kufanikiwa lazima lianze kujengwa kwa mtu wa ndani yako. Ukiwa imara ndani hata kama nje watakudharau wala hutatishika. Huwezi kusimamia maamuzi mazito ambayo jamii inayaona kinyume na ukabaki imara kuendea malengo yako kama utu wa ndani ni legelege.

Malengo yote ya mafanikio kwanza yanapata upinzani katika ulimwengu wa roho toka kwa shetani na wajumbe wake maana mafanikio yako yanakuondoa katika uwezekano mkubwa wa kunasa katka mitego yake mingi anayoitumia kupitia umaskini.

Kuna vibaka, majambazi, makahaba, machokoraa, ndoa zinazobomoka kupitia umaskini na kwa namna hiyo shetani ana maslahi na umaskini na Mungu hajatuwekea fungu la kushindwa wala umaskini ili kutuepusha na hayo.

Umaskini sio mpango wa Mungu. Kwa hiyo mafanikio yako yanapangwa na shetani na kisha binadamu wasiokutakia mema na ndiposa unapaswa kuwa imara katika utu wa ndani ili usimame imara kuelekea maamuzi yako na kama haupo imara ndani utapiga mbwembwe na mayowe bila kufanikiwa.

Nini kifanyike? 
 1. Jiimarishe katika imani ya kushinda 
 2. Jifunze kufikiri, kutamka na kutenda katika kushinda 
 3. Fanya mafanikio unayoyatarajia kuwa sehemu ya ukombozi wa wale wanaoteswa na kukosa mafanikio kama yale utakayoyapata wewe. Imarisha utu wa ndani kisha uyaendee mafanikio yako. 
Che Mrope wa Mrope, 
Mbeba Maono (fb page), 
0766656626/0715366010/0787641417

Selected Candidates for non Degree orogrammes AY 2015/2016 at SUA

The management of Sokoine University of Agriculture (SUA) has announced the names of candidates selected to join various non-degree programmes for the 2015/2016 academic year which starts on November 2nd, 2015.

Wale twiga wetu walioondoka kwa ndege wameahidi...


Lukuvi agoma kutamka kuzindua Halmashauri maana viongozi ndiyo watendaji


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameacha hali ya kutokufahamika kwenye Wizara hiyo baada ya kusita kutamka maneno ya kuzindua Halmashauri ya 11 ya wapima ardhi katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Wizara hiyo.

Hatua ya Waziri kutotamka uzinduzi rasmi umetokana na kushuhudia viongozi wa Halmashauri hiyo yenye jukumu la kusajili Wapima Ardhi na Wathamini katika kusimamia taaluma na mwenendo wa utendaji katika masuala ya kupima ardhi, ndiyo watendaji wakuu wa Wizara.

Akizungumzia mkanganyiko huo, Waziri Lukuvi amesema haiwezekani yakawepo mazingira ya kutenda haki ikiwa viongozi wenye jukumu la kusimamia Halmashauri hiyo ili iweze kusimamia na kuondoa migogoro katika sekta ya ardhi ndio, hao hao watendaji wakuu katika Wizara hiyo.

Kutokana na hali hiyo, Waziri amependekeza sheria ya kuanzisha halmashauri hiyo ibadilishwe ili kuwaondoa watendaji hao ambao miongoni mwao wanatuhuma za kuhusika na migogoro ya ardhi ili chombo hicho kiongozwe na watu kutoka nje ya serikali.

Wajumbe wapya wa Halmashauri hiyo wanaongozwa na Justo Lyamuya kama Mwenyekiti na Katibu ni Nassor Duduma, wote ni watendaji katika Wizara hiyo.Taarifa: Waziri kukutana na wananchi kuhusu migogoro ya ardhi Dar es Salaam

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI 

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI INAPENDA KUWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUWA MHE. WAZIRI WA ARDHI ATAPOKEA MALALAMIKO YA WANANCHI WENYE MIGOGORO INAYOHUSU ARDHI KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM TAREHE 22 – 23, SEPTEMBA, 2015 KUANZIA SAA 4.00 ASUBUHI MAKAO MAKUU YA WIZA RA. KATIKA TUKIO HILO, MNATAKIWA KUZINGATIA YAFUATAYO;-

1) TAREHE 22 SEPTEMBA 2015 ATAPOKEA MALALAMIKO YA WANANCHI KWA MANISPAA YA KINONDONI;

2) TAREHE 23 SEPTEMBA 2015 ATAPOKEA MALALAMIKO YA WANANCHI KWA MANISPAA YA TEMEKE NA ILALA;

3) MALALAMIKO HAYO YAWASILISHWE NA MUHUSIKA MWENYEWE NA SIYO MWAKILISHI;

4) MALALAMIKO AMBAYO YAMEKWISHA WASILISHWA MAHAKAMNI HAYATAPOKELEWA. 

KATIBU MKUU
WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

Taarifa: Kamati inakaribisha maombi ya uwakala Miss Tanzania 2016


Prof. Jay na rafikize waburudisha wenyewe kwenye kampeni zake
Taarifa: Rais Kikwete ateua M/Kiti Bodi ya Wanyamapori; Wizara yateua Wajumbe 12

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

TAARIFA KWA UMMA

UTEUZI WA MWENYEKITI NA WAJUMBE WA BODI YA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAMAPORI TANZANIA (TAWA)

Wizara ya Maliasili na Utalii inapenda kuujulisha umma kuwa, Bodi mpya ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tanzania Wildlife Authority -TAWA), imeteuliwa rasmi kuanzia tarehe 09 mwezi Septemba, 2015.

Katika uteuzi huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis Rajabu SEMFUKO kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo.

Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ambao wameteuliwa na Waziri wa Maliasili na Utalii ni:

 1. Dkt. Simon Mduma – Mkurugenzi Mkuu - TAWIRI
 2. Dkt. Fred Manongi – Mhifadhi Mkuu - NCAA
 3. Suzane Charles Ndomba – Mwanasheria – ATE
 4. Bw. Gerald Bigurube – Meneja wa Program Frankfurt Zoological Society – SERENGETI
 5. Dkt. David Manyanza (Mstaafu) Mtaalam wa Maswala ya Wanyamapori
 6. Bw. Benson A. Shallanda – Kamishna wa Sera – HAZINA
 7. Jenerali Samweli Ndomba – Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
 8. Winfrida Nshangeki – Mkurugenzi wa Uratibu wa Sera – TAMISEMI
 9. Abdulrahman Kaniki – Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania
 10. Allan J. Kijazi – Mkurugenzi Mkuu TANAPA
 11. Mr. Herman W. Keraryo – Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori
 12. Abdul Rajab Mhinte – Mkuu wa Idara ya Usalama na Atakayeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
Bodi hii, itaongoza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe ya uteuzi.

Imetolewa na
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali
Wizara ya Maliasili na Utalii
21/09/2015

[video] Lowassa akiwa Chanika aeleza 3 sababu za kuomba Urais


Ndugu 3 wa familia moja waliofariki wakitokea arusini wazikwaPicha za Swahili Fest. Community Picnic, DMV

Mshereheshaji Tuma akielekeza jambo kwenye tamasha la Swhili Fest lililofanyika siku ya Jumapili Septemba 20, 2015 Bladensburg, Water Front iliyopo jimbo la Maryland nchini Marekani. 

CCM yafanya mkutano wa kampeni Micheweni


Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein, akiwa na Mama Mwanamwema Shein, wakisalimiana na Viongozi wa CCM wakati wakiwasili katika viwanja vya mkutano wa Kampeni Micheweni Pemba kwa ajili ya kuendelea na mikutano yake ya kampeni kugombea nafasi hiyo kwa mara ya pili na kuomba ridhaa za Wananchi Pemba kumpigia kura za Ndio katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar.