[video] Prof. Kitila Mkumbo azungumzia kura ya maoni ya TwawezaTADIP yatoa matokeo ya utafiti wa tathimini ya wagombea Urais 2015


IPSOS yatoa matokeo ya utafiti wa tathimini ya wagombea Urais 2015


Helikopta ya CCM yaanza kazi: Mwigulu, Kigwangalla, Bashe - Tabora

Chama Cha Mapinduzi hii leo kimerusha helikopta yake ya kwanza kwenye kila pembe ya nchi kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu kwenye nafasi zote za Udiwani, Ubunge na Urais. Kazi ya kupasua anga hilo linaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Ushindi Ndg. Mwigulu Nchemba ambaye katika Jimbo lake la Iramba kwa asilimia 98 amejihakikishia ushindi wa kishindo hapo tar. 25.10.2015

Mkutano wa Lowassa Mirerani - Simanjiro - Manyara


Agizo la CUF kwa CHADEMA kuhusu majimbo ya Nachingwea, Mtama


2 minutes video on How to make an ice cream bread


Snippet! Report on Tanzania opinion poll conducted in 5 regions

''The Opinion Poll conducted by Nanos Research Institute [the reputable Research Institute in Canada], shows that CCM Presidential Candidate Hon. John Magufuli has been left far behind the CHADEMA/UKAWA candidate Hon. Edward Lowassa. The ABC News quoted the report named ''TZ Opinion Poll Report, page 23'' that Lowassa is leading by 64% , Magufuli 31% and other candidates well below 05%. Number of sample size taken were 20,000 people from all 5 cities of Tanzania (Mwanza, Dar, Tanga, Arusha and Mbeya). The same institution will conduct another Opinion Poll in Rural Tanzania areas and provide report before the end of September. This study is funded by the government of Canada through Canadian International Development Agency (CIDA)''.

[update] Taarifa rasmi kuhusu Mkuu wa Jeshi, Jenerali MwamunyangeKUMEKUWAPO UVUMI WENYE KUUPOTOSHA UMMA KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NCHINI AMENUSURIKA KIFO BAADA YA KUWEKEWA SUMU KATIKA CHAKULA NA HIVI SASA AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN ILIYOPO NAIROBI, NCHINI KENYA, HUKU WENGINE WAKIDAI KUWA YUKO NCHINI INDIA KWA MATIBABU.

TAARIFA HIZO NI UONGO WENYE KILA DALILI YA KUTENGENEZWA KWA LENGO LA KUWATIA HOFU WATANZANIA JUU YA USALAMA WA KIONGOZI HUYU WA JUU WA MAJESHI YETU.

UKWELI NI KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI, JENERALI DAVIS MWAMUNYANGE NI BUKHERI WA AFYA NA HAYUPO NCHINI KENYA WALA INDIA KAMA ILIVYOENEZWA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII NA VYOMBO VYA HABARI.

TUNAPENDA KUWATOA HOFU WANANCHI KUWA TAARIFA HIZO NI UZUSHI MTUPU KWANI JENERALI MWAMUNYANGE ALIONDOKA NCHINI TAREHE 22 SEPTEMBA 2015, SAA 10.45 JIONI KWA NDEGE YA SHIRIKA LA NDEGE LA EMIRATES KUELEKEA ROME, ITALIA KWA ZIARA YA KIKAZI KUFUATIA MWALIKO WA MKUU WA MAJESHI WA JAMHURI YA ITALIA, JENERALI CLAUDIO GRAZIANO. TUNAPENDA KUWAHAKIKISHIA WANANCHI KUWA JENERALI MWAMUNYANGE PAMOJA NA UJUMBE WAKE WANAENDELEA NA ZIARA HIYO KAMA ILIVYOPANGWA NA AMESIKITISHWA NA UVUMI HUO.

WIZARA YA ULINZI YA JESHI LA KUJENGA TAIFA IMESIKITISHWA NA TABIA HII YA UZUSHI INAYOPINGANA NA WELEDI NA KANUNI ZA UANDISHI KATIKA TASNIA YA HABARI. NI DHAHIRI TABIA HII INAIDHALILISHA TASNIA YA HABARI NA WANAHABARI WANAOZINGATIA WELEDI NCHINI. TUNAPENDA KUCHUKUA FURSA HII KUKEMEA TAARIFA ZA AINA HII ZISIZOKUWA NA TIJA KWA TAIFA LETU NA ZILIZOLENGA KUWASUMBUA NDUGU, JAMAA, MARAFIKI NA WATUMISHI WENYE MAPENZI YA DHATI NA JENERALI MWAMUNYANGE.

TUNAWAASA WANAHABARI KUTOZITUMIA VIBAYA KALAMU ZAO NA UHURU WALIONAO KWA NAMNA YOYOTE ISIYOKUWA NA TIJA KWA TAIFA LETU. AIDHA, WIZARA NA TAASISI ZAKE WAKATI WOTE ZIMEKUWA TAYARI KUTHIBITISHA JAMBO LOLOTE AU KUTOA UFAFANUZI PALE ULIPOHITAJIKA. INASTAAJABISHA KUONA WALIOANZISHA UZUSHI HUO NA KUUENEZA HAWAKUWA TAYARI KUOMBA UTHIBITISHO WA NAMNA YOYOTE. JAMBO HILI LINATIA SHAKA JUU YA NIA YA MTU AU KIKUNDI KILICHOANZISHA UVUMI HUO. 

WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA TAASISI ZAKE ZITAENDELEA KUTOA USHIRIKIANO WA DHATI KWA WANAHABARI WENYE NIA YA DHATI YA KUJENGA NA KUILETEA SIFA TASNIA YA HABARI KWA KUZINGATIA WELEDI. UHURU WA VYOMBO VYA HABARI UWE NI UHURU WENYE KUZINGATIA WAJIBU ULIOBAINISHWA KATIKA MAADILI NA KANUNI ZA UANDISHI WA HABARI.
MWISHO, TUNAWATAKA WALIOANZISHA UZUSHI HUO KUMUOMBA RADHI JENERALI MWAMUNYANGE KAMA ISHARA YA USTAARABU NA KUTAMBUA KUTELEZA KWAO. KUTOFANYA HIVYO ITATAFSIRIKA KUWA NI KUKIRI KUWA KUENEZA UZUSHI HUO HAIKUWA KUTELEZA, BALI ILIKUSUDIWA KWA DHAMIRA FULANI, NA HIVYO KUSHAWISHI HATUA ZAIDI KUCHUKULIWA.

JESHI NA WIZARA ZITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA MAMLAKA HUSIKA KUWABAINI WATU WALIOHUSIKA KUUTUMIA VIBAYA UHURU WA HABARI NA HIVYO KUUPOTOSHA UMMA NA KULETA USUMBUFU KWA FAMILIA YA JENERALI MWAMUNYANGE, JESHI NA TAIFA KWA UJUMLA.

Imetolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na JKT
September 26, 2015.


Jenerali Mwamunyange akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.


Jenerali Mwamunyange akiteta jambo na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.

Jenerali Mwamunyange Italia
Jenerali Mwamunyange akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.

Taarifa zinazosambaa kumhusu Mkuu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) Jenerali Davis Mwamunyange zilizosambaa kwenye mitandao ya jamii kwamba amekula chakula chenye sumu na amekimbizwa jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu hazina ukweli wowote. Ni uzushi.

Kwa mujibu wa taarifa za familia ya Jenerali Mwamunyange pamoja na makao makuu ya jeshi ambazo Globu ya Jamii imezisaka na kuzipata, kiongozi huyu wa JWTZ hivi sasa yupo nchini Italia kwa ziara ya kikazi ya siku tisa kama anavyoonekana pichani, hajambo kabisa na yu bukheri wa afya.

Hii ni changamoto kwa wakala wa mawasiliano nchini (TCRA) ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa ukimya wake wa kutochukua hatua thabiti kudhibiti uongo kama huu kwa kuwatafiti, kuwabaini na kuwachukulia hatua watu kama hawa wenye nia ya kuleta taharuki na machafuko nchini.

Wananchi wengine waliohojiwa na Globu ya Jamii wanahoji kama kweli TCRA ipo na ina vifaa vya kisasa iliyodai wanavyo kuwabaini watu kama hawa, na kwa nini hawajafanya kweli toka sheria ya mitandao (Cyber Law) iliyoanza kutumika.

"Endapo kama TCRA watashindwa kumnasa mhusika wa uongo huu wa kuogofya, inabidi mamlaka husika iangalie upya ajira ya watendaji wake maana kama taasisi nyeti kama JWTZ inaguswa na wao wakae kimya tu basi ujue kuna tatizo ambalo inapaswa Serikali ilifanyie kazi", amesema msomaji mmoja wa Globu ya Jamii katika maoni yake.
Jenerali Mwamunyange mara baada ya kuwasili na kupokelewa na mwenyeji wake Rome, nchini Italia.
Tumeshirikishwa taarifa hii na Michuzi/"Globu ya Jamii"


Serikali inayoweka sheria yenyewe na kuzikiuka yenyewe


Sidhani kama kuna ubaya kwa watu wanaopenda kufuatilia siasa na mienendo ya kampeni kujumuika katika mikutano mbalimbali kuwasikiliza wagombea nyadhifa za uongozi katika maeneo yao na nchi nzima kwa ujumla.

Nadhani ni njia sahihi ya kuweza kuwasikia wagombea kuendana na eneo na tukio husika, kuliko kusubiri kusikiliza vipande tu kupitia vyombo mbalimbali rasmi na visivyo rasmi vya habari.

Ili watu waweze kuhudhuria mikutano hiyo kwa wingi, bila shaka ni sahihi kabisa kutumia vyombo vya usafiri kwa mtu binafsi au kama kundi, ili kurahisisha shughuli nzima.

Linalonitatiza katika mwenendo huu, ni hili la Serikali kupiga marufuku mara kadhaa usafirishaji watu na abiria kwa kutumia vyombo visivyo rasmi kwa usafiri wa abiria kama vile magari ya kubebea mizigo na wanyama.

Agizo la kusitisha mara moja kubeba abiria kwa kutumia vyombo hivi lilitolewa hasa baada ya kutokea ajali huko Dodoma, Mbeya na Arusha. Iweje lifumbiwe macho katika nyakati hizi za kampeni ambapo watu wanakuwa wamejaa mhemuko na mshawasha wa kisiasa kiasi cha kuwa kama waliorukwa na akili?

Tutasubiri mpaka ajali itokee ndipo tuseme, "Mapeni ya Mungu" na kuomba walazwe pema wakati tulishaumizwa nayo na tunaiona hatari yake wakati huu?

Hatutakaa tuendelee kama tunavyotaka ikiwa sisi ndiyo watunga sheria na kisha wakiukaji wa sheria zenyewe. Hatuna msimamo. Ni mambo kama haya yanayosababisha watu wakose imani na viongozi na Serikali.

Kuhusu kauli ya Magufuli: Serikali yangu askari akipiga jambazi mwenye silaha kwa risasi hashtakiwi

John Magufuli
John Magufuli

MAGUFULI NA MAJAMBAZI

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr John Magufuli akichaguliwa huenda nchi yetu ikashuhudia mapambano dhidi ya polisi na wananchi yakiongezeka kwa sababu serikali yake itaruhusu polisi kuuwa wananchi kwa kisingizio cha ujambazi.

Dr Magufuli katika kampeni zake kwenye uwanja wa Mashujaa mkoni Mtwara 02 Septemba 2015 alikaririwa na vyombo vya habari akisema kuwa serikali yake haitamshitaki polisi yoyote atakayemuua jambazi mwenye silaha.

Dr Magufuli alikaririrwa akisema ‘serikali yangu askari akipiga jambazi mwenye silaha kwa risasi hashtakiwi. Kila mara (majambazi) wanavamia vituo vya polisi, mbona hawavamii kambi za jeshi, jeshi la kujenga taifa au Ukonga FFU maana polisi wana nidhamu sasa wanawaonea na kuwaua’.

Wapiga kura wanajiuliza, kama kabla hajachaguliwa Dr Magufuli anaanza kuwaweka wananchi roho juu kiasi hiki, je akichaguliwa mapambano kati ya wananchi na vyombo vya dola yataongezeka kiasi gani?

Wananchi wanauliza swali hili kwa sababu ingawa hivi sasa hakuna polisi anayeruhusiwa kuhukumu watuhumiwa wa makosa mbali mbali ikiwa ni pamoja na watuhumiwa wa ujambazi, lakini umma umeshuhudia polisi wakiwauwa watu hovyo hovyo kwa tuhuma za ujambazi.

Wanauliza je Dr Magufuli akichaguliwa na polisi wakiruhusiwa rasmi kuwauwa watuhumiwa wa ujambazi—ni wananchi wangapi wasio na hatia watakaosukiwa zengwe la ujambazi na kuishia kuuwawa kikatili na polisi?

Hivi Magufuli ambaye amekuwa kiongozi wa serikali kwa zaidi ya mika 20 hajui kwamba polisi siyo mahakama na kwamba polisi haipaswi kutoa hukumu ya kifo kwa raia?

Wakati mgombea Dr Magufuli akitoa ahadi kwamba kwenye serikali yake polisi ndio watakaotoa hukumu ya kifo kwa watuhumiwa wa ujambazi; Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelekeza kuwa ni mahakama kuu ndiyo yenye mamlaha ya kutoa hukumu ya kifo.

Zaidi wananchi wanajiuliza, nchi itakuwa katika hatari kubwa kiasi gani Dr Magufuli akichaguliwa ambapo ataruhusu polisi kujichukulia sheria mkononi kuwauwa wananchi ambao pengine maisha magumu yametumbukiza kwenye ujambazi?

Lakini pia wananchi wanajiuliza je Dr Magufuli uchambuzi wake wa masuala ya kijamii umempa jibu kwamba polisi wakiwauwa ‘’majambazi wenye silaha’’ ndio utakuwa mwisho wa mapambano kati ya wananchi na polisi?

Pengine Dr Magufuli anapaswa kujielimisha kujua kuwa chanzo cha ujambazi siyo wananchi na wala siyo polisi. Kadhalika chanzo cha mapambano katika ya polisi na wananchi siyo polisi wala wananchi
Dr Magufuli anapaswa mapambano kati ya polisi na wananchi wa ni kiashiria kimoja cha kuonyesha athari ya mfumo wa serikali ya CCM wa kutajirisha watawala na kufukarisha wananchi wengi.

Anapaswa kufahamu kwamba CCM baada ya kulitupa Azimiao la Arusha bila kuweka mbadala wake katika zama hizi mpya za utandawazi wizi ambapo mfumo wa uchumi unaotamba duniani baada ya ukomunisti kufa ni wa upebari ambao unaruhusu mtu uwezo wa kupata apate hata kama kwa wizi na wa kukosa afie mbali.

Matokeo yake sasa nchi yetu Tanzania ina kikundi kidogo cha watawala waliotajirika vya kutisha kwa kujigawia kibepari fedha za wananchi na mali za nchi (kutumia ujambazi wa kalamu na sheria) huku mamilioni ya wananchi wakiwepo polisi ambao hali zao za maisha ni mbaya wakitumia mbinu mbali mbali safi na chafu ukiwepo ujambazi ili maisha yaende.

Hali hii ni hatari kwa mustakabali wa amani ya nchi yetu. Lakini cha kushangaza ni kwamba Dr Magufuli hajui kwamba hata pale mamilioni ya wananchi walipotaka kuisaidia nchi kuondoa mfumo huu wa utawala unaozalisha makundi mengi ya kihalifu katika jamii—majambazi, panya road, wezi wa kutumia kalamu na sheria na kadhalika, CCM na serikali yake walikataa.

Wananchi walipendekeza Katiba Mpya CCM na serikali yake ikakataa kata kata na kuyazika maoni hayo pale Dodoma tena kwa mbwembwe na kutukana wananchi mwaka 2014.

Kiburi na jeuri ya watawala wa serikali ya CCM kukataa ushauri wa wananchi kutengeneza Katiba Mpya inayotokana na maoni ya wananchi ili kupunguza pengo la utajiri kati ya watawala na wananchi ndiyo sababu ya wananchi kuikataa CCM hata kama CCM itafanya propaganda na ufisadi kuonyesha inapendwa.

Tena wananchi wanajua kuwa Dr Magufuli akichaguliwa kuwa Rais maana yake ni kwamba serikali ya CCM kuendelea kuwa madarakani na hivyo ujambazi hautakwisha kwa kuuwa majambazi.

Badala yake amani ya nchi itawekwa rehani kwa sababu kwa polisi kuua majambazi—hasira ya wananchi itaongezeka siyo tu dhidi ya polisi bali dhidi ya kila chombo ambacho serikali itakitumia kudhibiti umma unaotamani madadiliko ya mfumo wa uongozi unaowafanya wananchi kuwa maskini na kudhalilishwa na vyombo vinavyopaswa kuwalinda raia.

Kwa hiyo vema CCM wakati huu wa kampeni isijidanganye, iwe ni kwa kutumia tafiti za kimkakati ama propaganda nyingine zozote kuwa wanakubalika kwa mamilioni ya wananchi wanaoteseka kwa umaskini na hivyo eti watashinda uchaguzi.

CCM na mgombea wao wa Urais Dr Magufuli wanapaswa kuwa na miwani itakayowaelekeza kuona kuwa kitendo cha wananchi wenye silaha (majambazi) kuvamia kituo cha polisi na kuuwa polisi, ni ishara tosha ya amani kutoweka nchini –maana ni mwanzo wa vita kati ya wananchi na polisi—kati ya wananchi na serikali yao.

Hii ni ishara tosha kwamba wananchi wameichoka serikali ya CCM iwe inaongozwa na Dr Magufuli au mwanamuziki maarufu nchini Diamond au mwana CCM yeyote mwingine atakayedhaniwa ni kivutio kwa wananchi.

Kadhalika CCM wanapaswa kufahamu kuwa kwa wananchi wengi kushabikia upinzani ni ishara nyingine tosha kwamba wananchi wameichoka CCM na serikali yake. Hivyo suluhisho siyo kuuwa upinzani, bali nchi kuweka mfumo mpya wa utawala ambao misingi yake wananchi wamependekeza kwenye Rasimu ya Katiba Mpya.

Kwa hiyo kama kweli CCM na serikali yake wanaitakia mema Tanzania yetu ---hasa amani ya kweli unaotokana na wananchi wengi kuridhika na maisha badala ya viongozi peke yake kuwa matajiri wa kukufuru, ni vema na ni muhimu sana wakaheshimu maamuzi ya wananchi watakayoyafanya kupitia sanduku huru la kura hapo tarehe 25 Oktoba mwaka huu 2015. Mungu ibariki Tanzania.

Note: Ninaruhusu yeyote mwenye kutaka kuisambaza, kuichapisha Makala hii afanye hivyo. Lengo sote tushiriki kuijenga Tanzania yetu.

Ananilea Nkya
E-mail: [email protected]

Askari wakamatwa kwa kumuua mdhamini wa mtuhumiwa kesi ya wizi wa fedha kwa mtandao

Polisi mkoani Mbeya inamshikilia Mkuu wa kituo kidogo cha Polisi Ikata mkoani humo, Steven Rajab pamoja na askari mgambo wawili waliofahamika kwa jina moja moja, Labani na Kafurafumbi, kwa kutuhumiwa kumpiga Simioni Mndolwa na kusababisha kifo chake siku nne baadaye.

Kamanda wa Polisi Mbeya, Ahmed Msangi amesema kuwa watuhumiwa wanashikiliwa kwa mahojiano huku kituo hicho kikiwa kimefungwa hadi hapo watakapopelekwa askari wengine.

Imeeelezwa na ndugu wa marehemu pamoja na mwenyekiti wa kijiji kuwa, marehemu alifikwa na mauti kutokana na majeraha aliyoyapata alipopigwa kutokana na kutokuonekana kwa Nebati Nkwale, anayekabiliwa na kesi ya wizi wa fedha kwa njia ya mtandao ambaye marehemu alikuwa amemdhamini. Nkwale alitokomea kusikofahamika baada ya kupewa dhamana.

Mke na watoto wa marehemu wameripoti kuwa walifika mara kadhaa kituoni hapo wakiomba kuondoka na Mndolwa wakati akiwa bado hai ili atibiwe lakini hawakuruhusiwa hadi watoe dhamana ya shilingi laki tano za dhamana.

Mke wa marehemu ameeleza kuwa walilazimika kuuza ng’ombe ili kupata kiasi cha fedha kilichotakikana. Baada ya kufanikiwa kumpatia dhamana na kufanikiwa kumfikisha nyumbani, hali ya mgonjwa ilikuwa dhoofu kiasi cha kushindwa kuzungumza. Alipelekwa hospitali ni Mbozi Mission ambapo aliandikiwa rufaa na kwenda hospitalini Mtwara ambapo alikata roho akiwa katika chumba cha mapokezi.


Dr Lwaitama's 3 questions regarding Twaweza's findings

Azaveli Lwaitama
Azaveli Lwaitama

I agree with Risha completely that on the statistical errors issue there is not much to argue against the Twaweza results. I have however three supplementary problems:

(1) why did Twaweza boradcast the dissemination of the results by live television broadcast which is something they have never done before.

(2) why did TWAWEZA not wish to wait till they had had another opinion survey at the end of Septemberbefore they broadcast these clearly counter-intuitive opinion poll results . Delay till the end of this month, a mere two weeks away, would have allowed Twaweza to guard against having the results technically bias by the fact that an opinion survey between 19 August and 7 or 8 September would be influenced by the fact from 12 July to 4 August the public had no way of knowing Lowasa would be a Presidential candidate and that in many ways the news that he was a candidate begun to spread like fire only after the launch of the Chadema Presidential Election campaign on 29 August , more than 20 days after the end of the Twaweza opinion survey...people who are finding the Twaweza opinion poll results hard to believe are basing their doubts on impressions formed after 29 August when Lowasa's name begun to spread as a presidential candidate on everyone' lips... The TWAWEZA poll would seem to have targeted that period of more than one full month after the name of Magufuli was in the news as the unchallenged contestant of the presidential race...12 July to 19 August and almost a month (about 20 days) before Lowasa launched his official presidential campaign on 29 August.

(3) finally since most informed Tanzanians associate Twaweza with Prof Kitila Mkumbo and Hon Zito Kabwe as Twaweza research consultants, and since these two have a vested interest in ensuring that the Chadema Presidential candidate does not win, one thought Twaweza would state clearly that these two were not in any way involved in decisions regarding WHEN to conduct the survey and WHETHER to broadcast the results of a survey conducted in late August and early September LIVE toward the end of September just when Chadema's Presidential candidate would seems to have caught the public eye in the media as a possible winner of the race?

Twaweza may indeed have been scientific in its conduct of the survey and the computation of its results, but can it avoid the charge of perhaps having allowed itself to be used politically by taking the decisions it took on the points have I raised above? I would love to hear to Twaweza has to say on this score. My trust in the integrity of Aidan Eyakuze is left intact but a tinny bit shaken , especially after reading Chambi Chachage's posting in Kswahili that I attach herewith. I believe Twaweza will do its best to response to thse queries of its admirers like me.

Mwl. Lwaitama

Taarifa mpya kuhusu mtoto aliyepotea na house-girl


Taarifa mpya kutoka kwa familia ya Jullu inasema kuwa mtoto wao Loveness Coletha aliyepotea na yaya wake amepatikana na mzazi wake amesafiri kwenda jijini Mwanza kumchukua.

Tunashukuru wote waliojumuika kuifariji familia kwa maneno ya kutia moyo, walioguswa na kuombea matumaini kwa sala, wote waliosambaza ujumbe kwa njia mbalimbali na zaidi sana, kwa watendaji wote wa mamlaka husika waliofanya kazi yao katika kufanikisha hili.

Asanteni!


Taarifa ya BAKWATA: Majina ya Mkenya, Watanzania waliofariki Mena katika hija

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Bismilah Rahman Raheem

Assalaam alaykum warahmatullahi wa barakaatuhu.

Taarifa hii inahusu tukio lilitokea jana Mina Saudi Arabia wakati mahujaji wakielekea kwenye Jamaraat, palitokea msongamano mkubwa (stampede) na kupelekea mahujaji zaidi ya 700 kufariki na mamia kadhaa kujeruhiwa.

Tayari tumethibitisha kutokea vifo vya watu watano waliotokea Tanzania miongoni mwao mmoja ni raia wa Kenya na wengine wanne ni Watanzania.

Watanzania waliotambuliwa hadi jana usiku wametajwa kuwa ni Bi Mwanaisha Hassan Juma, Mkungwe Suleiman Hemedi na Sefu Saidi Kitimla.

Mwanamke mwingine mmoja Mtanzania jina halijaweza kupatikana hadi Alhamisi usiku wakati tukiandaa taarifa hii.

Raia wa Kenya ametambuliwa kwa jina la Bi Fatuma Mohammed Jama.

Kuna taarifa ya mahujaji wanawake wawili ambao hadi Alhamisi usiku walikua hawajapatikana hivyo hatukua na uhakika juu ya usalama wao hadi tutakapowaona ama kupata taarifa zao.

Ifahamike kuwa majina yamepatikana kupitia vitambulisho vyao ambavyo wahanga wa tukio hili waliweza kuvichukua kutoka kwenye miili ya marehemu.

Nimepokea taarifa za majeruhi miongoni mwa mahujaji wetu wa Tanzania na baadhi ya majeruhi hao nimeonana nao mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini.

Vilevile nimeagiza maafisa wetu wa Bakwata nilionao hapa Mina kuendelea kufuatilia habari na taarifa za mahujaji wetu katika hospitali na sehemu za kuhifadhia maiti.

Nimefanya hivyo ili niweze kuwa na uhakika juu ya usalama wa mahujaji wetu.

Katika kipindi hiki cha taharuki kubwa tunafanya mawasiliano na wizara husika hapa Saudi Arabia kwa kushirikiana na serikali yetu kupitia ubalozi wetu hapa Saudi Arabia.

Natambua uwepo wa mkanganyiko wa taarifa ambazo zinazidisha taharuki kwa ndugu na jamaa wa mahujaji wetu.

Nachukua fursa hii kuwaomba ndugu na jamaa wa mahujaji kuwa watulivu na kuwa na subra katika wakati huu mgumu sana kwetu sote.

Tunaendelea kufuatilia kwa karibu sana na Insha Allah mara tu tukipata taarifa za uhakika basi tutawafahamisha.

Kutokana na idadi ya maiti kuwa kubwa serikali ya Saudi Arabia wanaendelea na zoezi la kutambua uraia wa kila mwili ili waweze kutoa taarifa tunatarajia wakati wowote tutakuwa tumepata taarifa zaidi.

Wabillahi Tawfiiq.
Sheikh Abu Bakari Zuberi
Mufti wa Tanzania.
MECCA, Saudi Arabia
25/09/2015

Twaweza invitation: Political Party debate on Economy and Inequality

Twaweza would like to invite you to:

Debate | Political Party debate on the topic Economy and Inequality 


Time: 3:00pm - 5:00pm
Date: Sunday September 27 2015
Venue: Julius Nyerere International Conference Center (JNICC) - Posta

Invited guests

The five political parties fielding the largest number of candidates in the elections (at constituency or ward level) have been invited to send their experts to outline their visions and plans for these critical areas. These representatives will be interrogated by a panel composed of sector experts drawn from civil society.

These debates will be broadcast live by Star TV and Radio RFA.

Registration for this event is essential. Please send your name and media outlet to [email protected] or call +255 768 129974.