Mwanakwaya afariki kwenye mkutano wa kampeni

Mkazi wa mtaa wa Mbuyuni kata ya Ng’apa Jimbo la Lindi Mjini, Fatu Jega anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 28, amefariki dunia ghafla akiwa kwenye mkutano wa kampeni.

Fatu alifariki dunia Septemba 21, mwaka huu saa 10:00 jioni wakati wa kampeni ya mgombea udiwani kata ya Ng’apa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwanaidi Mbungo.

Alifariki dunia muda mfupi baada ya kumaliza kuimba nyimbo za uhamasishaji watu kwenye mkutano huo uliofanyika eneo la Lukwania katika kata hiyo.

Baada ya muda wa kuimba nyimbo za uhamasishaji kumalizika, mwanakwaya huyo aliketi chini pamoja na wenzake na kuanza kusikiliza sera kutoka kwa viongozi mbalimbali wa chama hicho.

Wakati baadhi ya viongozi wakiendelea na hotuba za utangulizi, ndipo mwanakwaya huyo aliposikika akisema anawaona watu wa ajabu wakipita mbele ya uso wake na punde si punde, akaanguka chini na kupoteza fahamu.

Mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni, pia ulihudhuriwa na mgombea ubunge wa Jimbo la Lindi Mjini, Selemani Kaunje.

Kitendo hicho kiliufanya mkutano huo kusimama na baadhi ya watu waliokuwapo wakambeba Fatu na kumkimbiza Zahanati ya Ng’apa kwa matibabu.

Hata hivyo, ilibainika kuwa mwanakwaya huyo alikuwa tayari ameaga dunia.

Mganga Mkuu wa Zahanati ya Ng’apa aliyejitambulisha kwa jina moja la Dk. Ally, alithibitisha kutokea kwa kifo cha mwanakwaya huo.

“Ndugu mliomsindikiza, huyu mtu ameshafariki muda mrefu. Urudisheni nyumbani mwili wake kwa taratibu nyingine za mazishi,” alisikika Dk. Ally akiwaambia wana-CCM waliokuwa wamempeleka katika zahanati hiyo, hali iliyoamsha vilio na simanzi miongoni mwao.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Lindi Mjini, Mukhusini Ismail, alisema Chama kimempoteza mtu aliyekuwa tegemeo ndani ya chama chao hususan katika kipindi hiki cha kampeni.

Katibu wa CCM aaga dunia

Ernest Chale
Ernest Chale

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala, Ernest Chale amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu.

Katibu huyo amefariki majira ya saa 5:30 asubuhi jana katika hospitali hiyo.

Alisema kuwa Jumatano ya wiki hii alikuwa anasumbuliwa na shinikizo la damu na Alhamisi alipelekwa katika Hospitali ya Muhimbili na kulazwa wodi ya Mwaisela. Hali yake ilibadilika na hatimaye umauti ukampata.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba Gadafi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Jumatano walikuwa wote kwenye kampeni na hali yake ilibadilika usiku akiwa usingizini.

Lubuva amjibu Mbowe kuhusu Bulembo: Kukataa matokeo ikiwa umeshindwa kihalali ni uhainiMwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana amenukuliwa akisema kuwa NEC imeshitushwa na kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ya kususia uchaguzi mkuu wa mwaka huu kutokana na kauli iliyotolewa katika mkutano wa kampeni za CCM mjini Kigoma na Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya Mgombea urais ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Bulembo, kwamba CCM haitakubali kuiachia Ikulu Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Lubuva alisema kauli ya Mbowe, kiongozi wa chama kikubwa, iliwashitua na katika vipindi vyote vya uchaguzi vilivyopita, hawajawahi kukumbana nayo.

Jaji mstaafu Lubuva alisema baada NEC kufuatilia kauli ya Bulembo, ilibaini kuwa:
“Bulembo katika kauli yake hajasema kwamba hata kama NEC ikitangaza matokeo CCM wakiwa wameshindwa, hawatakuwa tayari kuwaachia Ikulu Chadema. Alikuwa anamaanisha kuwa watawashawishi wapiga kura wao wasiwapigie kura ili wasipate nafasi ya kwenda Ikulu,” 
Alisema kauli iliyotolewa na Mbowe na Bulembo zinakinzana na kwamba:
“Kukataa matokeo ya uchaguzi hata kama umeshindwa kihalali ni uhaini,” alisema Jani Lubuva.
“Hii ni kauli ya kisiasa kama ambavyo CHADEMA nao wamekuwa wakitamka kwamba hii ndiyo awamu ya mwisho kwa CCM kukaa madarakani,” 
Imenukuliwa kutoka NIPASHE

Muhtasari wa mambo 35 muhimu katika iIlani ya CUF Zanzibar


Imani kubwa ya kihistoria tunayoendelea kupewa kupitia ridhaa ya wananchi inaturejesha tena kwao na mpango kazi uliotayarishwa kuirejeshea hadhi na heshima kwa nchi yetu pamoja na kuleta mabadiliko ya haraka ya kisiasa na kiuchumi kwa ajili ya maendeleo ya jamii nzima na taifa letu kuanzia tarehe 25 Oktoba 2015.

1.Tutayarejesha Mamlaka Kamili ya Zanzibar kwa kuimarisha Muungano utakaozingatia Misingi ya Haki, Usawa na Heshima kwa nchi zote mbili zinazounda Muungano huu.

3. Tutajenga Uongozi Mwema kwa Kuimarisha Misingi ya Uhuru, Haki na Maridhiano kwa wananchi wa Zanzibar.

4. Tutailinda, kuienzi, kuendeleza, kuijenga na kuiboresha misingi yote ya Umoja wetu wa Kitaifa ulioasisiwa na viongozi wetu wa kisiasa wa Zanzibar, Dkt. Amani Abeid Amani Karume na Maalim Seif Sharif Hamad tarehe 5 Novemba, 2009 na kupewa ridhaa na wananchi kupitia Kura ya Maoni ya tarehe 31 Julai 2010.

5. Tutapambana kuondosha rushwa, ufisadi, upendeleo, uonevu, ubaguzi na woga ndani ya taasisi zetu pamoja na jamii kwa kurekebisha muundo wetu wa utawala, uwajibikaji, na utendaji katika kazi na utoaji wa huduma sambamba na kupanua viwango vya elimu na uelewa wa kutosha kwa jamii.

6. Tutayaendeleza mashirikiano yetu ya kimataifa (International Relations and Cooperation) na majirani zetu, washirika wa maendeleo, taasisi, nchi wahisani na jumuiya mbali mbali za kimaendeleo kwa lengo la kuifanya Zanzibar inufaike na mahusiano na mashirikiano hayo. Mafanikio ya mashirikiano haya yatatokana na Zanzibar yenye mamlaka kamili ndani ya muungano wa haki, heshima na usawa.

7. Tutatetea haki ya Zanzibar kushirikishwa katika Shirika la Kimataifa la Bahari (International Maritime Organization) pamoja na kusimamia kwa uwazi na kwa mujibu wa sheria za kimataifa mikataba na itifaki mbali mbali za Shirika la IMO ikiwemo suala la usajili wa meli (International Shipping Registry) na fursa zaidi kwa Wazanzibari katika uajiri melini.

8. Tutasimamia na kuitetea haki ya Zanzibar katika sera, mipango na matumizi ya maeneo maalum ya kiuchumi ya bahari kuu (Exclusive Economic Zone) na yale ya madini ya chini ya bahari (Extended Constinental Shelf) kwa faida ya wananchi wa Zanzibar.

9. Tutaingia kwenye uongozi tukiwa na dira ya mabadiliko itakayotupeleka kujenga mashirikiano ya kikanda katika sekta ya uvuvi wa bahari kuu (Regional Deep Sea Fisheries Management).

10. Tutauondoa uonevu na ukiritimba unaofanywa na viongozi na watendaji wachache juu ya haki za msingi za wavuvi wetu wa mwambao na kuhakikisha haki na usawa kwa wavuvi wote ikiwemo wazalishaji wa mwani.
11. Tutahakikisha tunapiga hatua kubwa mbele katika kuijenga nchi, uchumi na jamii yenye fursa ya maendeleo yanayoongozwa na sayansi na teknolojia yakiwemo matumizi endelevu na ya gharama ndogo kwa wananchi ya teknolojia ya taarifa na mawasiliano (Information and Communications Technology).

12. Tutasimamia sera, sheria, na mfumo wa uendeshaji bora wa sekta ya mafuta na gesi (Oil and Gas for Development) ikiwemo ugawaji wa mipaka ya baharini, utafutaji, uzalishaji na mapato yanayotokana na maliasili hizo na kuhakikisha ajira na maslahi kwa wananchi wa Zanzibar.

13. Tutausimamia na kuuendesha uchumi utakaozingatia malengo ya Uchumi Endelevu (Sustainable Development Goals) inayozingatia vipaumbele kwa nchi za visiwa vidogo vidogo na kuendeleza mashirikiano na washirika wetu wa maendeleo katika kufikia malengo hayo.

14. Tutajenga uchumi imara unaokua kwa kasi na unaotoa ajira na tija kwa misingi ya haki na uwiano kwa wote.

15. Tutahakikisha upatikanaji wa ajira kwa wananchi wetu katika sekta zote za kiuchumi za utalii, kilimo, uvuvi, biashara, viwanda, na kukuza huduma za ujasiriamali kwa ajili ya sekta binafsi na sekta isiyokuwa rasmi.

16. Tutaunga mkono na kuusimamia utalii endelevu (Sustainable Tourism) unaojali maslahi ya wananchi, na sio viongozi tu, na kuhakikisha uwiano baina ya wawekezaji na wananchi wa maeneo husika katika utoaji wa huduma za maji, nishati, matumizi ya ardhi, ajira, na fursa nyingine za sekta hii.

17. Tutakuza biashara kwa kupunguza viwango vya ushuru na kodi na kuitangaza Zanzibar kuwa Bandari Huru sambamba na kuimarisha viwanda na miundombinu ya maendeleo ikiwemo ya ujenzi na makaazi, barabara, umeme, maji mawasiliano ya simu, bandari na viwanja vya ndege vya kisasa.

18. Tutaendeleza uzalishaji wa zao la karafuu na usimamizi endelevu wa sekta hii na kutekeleza programu za ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji wa mpunga na miwa katika mabonde yetu.

19. Tutaunga mkono na kushirikiana na wawekezaji na wananchi kuharakisha huduma mbali mbali muhimu (Service Providers) katika uzalishaji wa mazao mbali mbali ya chakula na biashara yakiwemo matunda, mboga mboga, na nafaka kwa ajili ya maslahi ya wananchi.

20. Tutaanzisha Benki ya Uwekezaji ya Zanzibar (Zanzibar Investment Bank) pamoja na kuunda mazingira bora ya kisera na kisheria katika uwekezaji wa mabenki ya kimataifa (Offshore Banking) na makampuni ya kimataifa (Offshore Companies).

21. Tutaufanyia marekebisho ya kitaasisi na kiuendeshaji mfumo mzima wa utoaji wa elimu Zanzibar ili uende sambamba na haja ya kutoa elimu bora na yenye viwango vya kikanda vya Afrika Mashariki na vya kimataifa itakayokuza vipaji na vipawa vya wanafunzi wetu na kuwafanya waweze kushindana katika soko la ajira la kikanda na kimataifa.

22. Tutaboresha maslahi ya wafanyakazi na kuongeza kima cha chini cha mishahara kwa kiwango cha kutosheleza mahitaji pamoja na kuhakikisha maslahi zaidi na bora kwa wastaafu (Pensioners) na wazee (Senior Citizens).

23. Tutawekeza zaidi katika usimamizi bora, upanuzi wa miundombinu, pamoja na viwango vya uhakika vya huduma katika sekta ya afya kwa ajili ya wananchi wetu na kuifanya iwe sekta bora na iliyoimarika.

24. Tutaendelea kupambana na Malaria, UKIMWI, ugonjwa wa presha, moyo, kisukari, kansa, na maradhi mengine yanayoambukiza, yaliyodharauliwa na yasiyoambukiza.

25. Tutapambana vikali na janga la dawa za kulevya kwa kuhakikisha uimarishaji ulinzi na usalama katika viwanja vya ndege.
na bandari zetu, viwango na miundombinu bora katika upekuzi na upelelezi, huduma bora za tiba kwa walioathirika na dawa za kulevya pamoja na elimu ya jamii kuhusu madhara yake.

26. Tutasimamia hifadhi ya mazingira yetu pamoja na kuijenga jamii iliyo tayari na uchumi wenye uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi (Climate Change Adaptation).

27. Tutawekeza katika mipango ya maendeleo ya uchumi na maendeleo ya jamii inayojali utayari wa kujikinga na hatari za majanga ya kimaumbile (Disaster Risk Reduction).

28. Tutatengeneza mpango kazi wa kuanzishwa kwa miundombinu ya kitaifa ya nishati mbadala (Renewable Energy) ikiwemo ya jua, upepo, takataka na biogas itakayochangia katika suala zima la mageuzi katika sekta ya nishati Zanzibar.

29. Tutahakikisha kuwa hifadhi zote za misitu zinalindwa na kuhifadhiwa pamoja na kushajiisha matumizi endelevu ya misitu.

30. Tutatunga sera na sheria mpya za usimamizi wa hifadhi za baharini (Marine Conservation Areas) na kuweka mipaka maalum (zonation) katika matumizi ya maeneo haya ya bahari kwa ajli ya wavuvi, watalii, na shughuli nyingine.

31. Tutaondoa kodi zote kandamizi zinazouathiri utalii wa hifadhi za mazingira na kuweka viwango vipya vya kodi vinavyokubalika kwa maslahi na faida ya wahusika wote.

32. Tutahakikisha utekelezaji kwa ukamilifu wa matamko yote ya kimataifa kuhusiana na haki, wajibu, na dhamana za taifa na jamii kwa wanawake, watoto, na watu wenye ulemavu.

33. Tutaendelea kuuthamini utamaduni na urithi wetu wa kihistoria (Culture and Heritage) na kusaidia katika kukuza malezi bora kwa vijana wetu pamoja na utunzaji wa wazee wetu.
34. Tutatilia mkazo katika uwekezaji na uimarishwaji wa michezo mbali mbali na kutoa fursa kwa vijana wetu katika ngazi zote za ushirikishwaji katika michezo yote.

35. Kwa ridhaa ya wananchi, tutahakikisha tunaiongoza Zanzibar yenye Mamlaka Kamili na inayotoa fursa, haki, na usawa kwa lengo la kujenga nchi yenye neema kwa wote ndani ya Muungano wa haki, heshima na usawa.

Anasema uwanja wa Taifa leo CCM imetoa bure tiketi upande mmoja Yanga ukibinua...
Giving birth in different worlds - Tanzania, Sweden

Photos by Moa Karlberg

The photographs in the series “Hundred Times the Difference,” by the photographer Moa Karlberg, capture, in closeup, the faces of women in the final stages of giving birth. Across the images, there is a range of expressions: grit and sensuality, trepidation and expectation, pain and elation. But in their intimate perspective the photographs emphasize the women’s shared experience—the inward focus and physical determination in their final, transformative moments of becoming mothers.

If you look closely, though, you’ll see signs—the sterile white backgrounds in some photos and patterned fabric in others; a single acupuncture pin in the center of a forehead—that the women in Karlberg’s photographs are having drastically different experiences of giving birth. Half of the pictures were taken in Sweden and half in Tanzania. In the former country, almost all births take place in hospitals, where women have access to supportive midwives who are backed by sophisticated medical technology when needed. In Tanzania, by contrast, only half of births take place in medical facilities, and those that do often occur in places that lack even the most basic amenities.

In a statement about the project, Karlberg, a native of Sweden who travelled to Tanzania in June, with support from the International Women’s Media Foundation, describes the disparity between the scenes she witnessed in the two places. In her home country, “The woman about to give birth is lying on the public hospital’s white sheets. . . . Next to her is her husband, stroking her back, talking to her supportively, helping her to focus on her breathing. Low music comes from the speakers. Water and juice is on the table next to the height-adjustable bed. The woman has her own room and her own bathroom with a tub. Painkillers are available upon request.” In Tanzania, “the woman about to give birth is lying on a bare, rusty bunk, covered in fabrics she brought with her. The water tap is not working, and even if it was, the water would not be drinkable. If she has to urinate there is a bucket on the floor. There is no family member by her side, but three other women, on similar bunks and in various stages of labor, share the room. As they moan, the nurses tell them to be quiet. Since there are no painkillers, the women need to save their strength for the pushing in the end.” As a result of these extreme disparities, and the corresponding difference in the ability to deal with medical complications, the risk of dying during childbirth in Tanzania is a hundred times higher than it is in Sweden.

But despite this cross-national chasm in maternal health, simple explanations of the West-as-best and modernization-as-cure are insufficient. As Karlberg hints in the photo shown in the final slide above—a woman originally from Uganda, giving birth in Sweden—Sweden has experienced a wave of immigrants over the past four decades, many of them refugees from conflict-torn places like Iraq, Eritrea, Somalia, and now Syria. Though Sweden has proved more welcoming than other European nations in the current refugee crisis, the country’s government—influenced by the far-right Swedish Democrats, who received support from one out of every eight voters in the 2014 parliamentary elections—has grown more nativist and stingy about its welfare state. In Tanzania, meanwhile, maternal-mortality rates have improved slightly in recent years as the country has experienced impressive economic growth and extensive foreign aid, but the rates today are the same as they were sixty years ago. In both countries, birth attendants, who are almost all women, are underpaid and overworked.

In Karlberg’s stark photographs, these many inequities seem simultaneously highlighted and erased. Her stunning, unembellished mothers-to-be seem to triumph in ways independent of their immediate surroundings, and notwithstanding the obstacles to empowerment that extend across racial, ethnic, and national lines. Yet the obstacles remain.

Salam za Eid na rambirambi kutoka Zanzibar Diaspora

TAARIFA

Assalamu Alaykum: Kwanza kabisa, napenda kumshukuru Allah Subhanahu Wa Taala kwa kutujaalia kuwa wazima na kuadhimisha Siku Kuu ya Idd Al-Adh-ha ya mwaka 1436H (2015).

Idd Al-Adh'ha ni Siku Kuu kubwa kati ya Siku Kuu mbili katika Uislamu, ni siku ya furaha, kwa familia na jamii kwa ujumla. Kwa niaba ya Uongozi wenu wa ZADIA, naungana na WanaZadia wote, Wazanzibari, na Waislamu kwa ujumla katika kuadhimisha siku hii adhimu.

Kwa vile hii ni Siku Kuu Kubwa, furaha yangu ingekuwa kubwa zaidi katika kusherehekea. Hata hivyo, furaha hiyo imeingia doa kutokana na maafa yaliyowakumba ndugu zetu Waislamu waliofunga safari kwenda kuhiji, kuitikia wito wa Mola Wao Mlezi wa kuizuru Nyumba Yake Tukufu.

Kutokana na hilo, napenda kuchukua fursa hii kutoa salamu zangu za rambirambi kwa Waislamu wote ulimwenguni ambao wamepoteza ndugu, jamaa na marafiki katika maafa hayo.

Tunamuomba Allah awaingize wenzetu waliotangulia peponi kwa Rehma zake. Kama ambavyo, natoa pole kwa Mahujaji wote waliopata ajali na kujeruhiwa, na kumwomba Allah SWT awape afya na uzima na kuwarejea katika familia zao wakiwa katika afya na uzima.

Ndugu Wanazadia na Wazalendo kwa ujumla,

Huku tukiwa tunaendelea kusherehekea Siku Kuu ya Idd Al-Adh'ha, napenda kuwakumbusha kuhusu majukumu ya kila mmoja wetu ya kuendeleza umoja, mshikamano na amani katika Jumuiya yetu na nchi yetu Zanzibar kwa ujumla. Na hakuna njia nyepesi ya kufikia malengo hayo ispokuwa kushikamana na Kamba ya Mwenyezi Mungu.

Tujifunze kutokana na somo la Hijja ambalo Waislamu kutoka sehemu zote duniani hukutan sehemu moja wakiwa katika vazi la aina moja kwa ajili ya kuabudu Mola mmoja, bila kujali kabila, nchi wanazotoka, umri, jinsia, vyeo au tofauti nyenginezo. Wote wako sawa wakiwa na lengo moja.

Siku Kuu hii kwa mwaka huu inakuja ikiwa imebakia si zaidi ya mwezi mmoja kabla Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kuingia katika Uchaguzi Mkuu. Mara tu baada ya kumalizika kwa shamra-shamra za Siku Kuu, akili, macho na masikio yetu yote yataelekea kwenye kampeni za uchaguzi na vioja vyake.

Kwa hivyo, nasaha kwetu sote, wadau wote, kulitumia funzo tulilolipata katika Hijja na Siku Kuu yake kuhakikisha kuwa tunashiriki kwa njia moja au nyengine kuufanya uchaguzi ujao upite kwa salama na amani kama ulivyopita ule uliotangulia wa mwaka 2010. Tukumbuke kuwa Umoja ni nguvu na Utengano ni Udhaifu. Kwa hivyo, kampeni na ushabiki wetu wa kisiasa vyote vilenge kwenye kuendeleza Serikali ya Umoja Wa Kitaifa Zanzibar na kuipa nguvu Zanzibar kuleta maendeleo.

Ikumbukwe kuwa, Malengo Makuu ya ZADIA ni kuleta umoja wa Wazanzibari na Maendeleo yao nje na ndani ya nchi yetu tuipendayo. Hata hivyo, malengo hayo hayawezi kufikiwa bila kuwa na amani, usalama na utulivu ndani ya nchi yetu ya Zanzibar na hata Jamhuri yote ya Muungano wa Tanzania.

Kila mmoja wetu ajaribu kuyalinda malengo hayo kwa kuzingatia kauli ya Bwana Mtume SAW aliposema: "Kila mmoja wenu ni mchunga, na kila mmoja wenu ataulizwa juu ya kile anachokichunga".

Nawatakia Idi Njema, nawapa pole wafiwa na nawaombea majeruhi shifaa.

Omar H. Ali,
Mwenyekiti,
ZADIA.