Now you can Block sender and Unsubscribe from mailing list in Gmail

Gmail announced a week agi that now you can block specific email addresses in Gmail on the web and on Android. See "how to" in the gif picture below.

Future mail from the blocked person will go to the spam folder.

You can always unblock in Settings.Also, the unsubscribe option that was available on web, is now available on Android. You will now be able to opt out of eligible mailing lists directly from the Gmail app. Majina ya walioitwa TBS kwenye usaili wa kuandika

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limewatangazia waombaji wa nafasi za kazi zilizotangazwa terehe 25.5.2015 na tarehe 05.01.2015 katika kada kadha wa kadha, kuwa usaili wa kuandika utafanyika tarehe 30 Septemba 2015 hadi tarehe 03 Oktoba 2015 katika chuo kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam.

Magufuli abadili staili! Video hii hapa...Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akifanya mazoezi jukwaani akijiandaa kujinadi kwa wananchi katika Mji wa Makambako, mkoani Njombe leo, jambo ambalo lilizua vifijo, nderemo na vigelegele kutoka kwa wananchi waliofurika kwenye mkutano huo wa kampeni.

How to stop mails from RedPlum/Valassis and ValpakFor RedPlum/Vlassis go to: www.valassis.com/about-us/contact-us.aspx

Valassis Direct Mail, Inc.
Consumer Assistance
PO Box 249
Windsor , CT 06095
1-800-437-0479For Valpak go to: www.coxtarget.com/mailsuppression/s/DisplayMailSuppressionForm

Valpak
1 Valpak Ave. N.
St. Petersburg, FL 33716
1-727-399-3000

Scholarship tenable in Peoples Friendship University of Russia 2015/2016

Scholarship Tenable in Peoples Friendship University of Russia (PFUR) 2015/2016| Print |
1.0  Call for Application:
Applications are invited from qualified Tanzanian for undergraduate, Masters and Doctorate, Scholarships tenable in Peoples Friendship University of Russia (PFUR) in Russian Federation for the year 2015/2016

2.0 Qualification:

2.1 Application for Undergraduate programme must:-

 • Have completed and passed Advanced Certificate of Secondary Education;
 • Candidates not exceed  25 years by September, 2015;
 • Have obtained and passed not below “C”  grade in the relevant subjects and No “F” in any subject of Advanced Secondary education, Examination or Secondary Education Examination
 • Not be admitted in any Higher Learning Institution (Local Foreign);  and
 • Have a good Health.

2.2  Applicants for MastersProgramme must:-

 • Have undergraduate degree with GPA not less than 3.5;
 • Not be older than 35 years of age by September, 2015; and
 • Have a good Health.
2.3  Applicants for Doctorate Programme must:-
 • Have a master’s degree with GPA not less than 3.5;
 • Not be older than 40 years of age by September, 2015; and
 • Have a good Health.
3.0  Financial Arrangements:

Application for Loan:

Need selected candidates must apply for loan from Higher Education Students Loan’s Board to cover air ticket, fees and maintenance costs.

4.0 Mode of Application:

 • All applications must attach certified photocopies of Academic Certificates, Transcripts and birth Certificate;
 • Applicants must indicate reliable contacts telephone number and E-mail.

5.0 Application and closing data:

Application  letter, together with certified copies of relevant Certified copies of relevant certificates and documents must reach the Embassy of the Russia Federation in Tanzania not more than 30th September, 2015 and copy to:-

Permanent Secretary,
Ministry of education and Vocational Training,
P.O. Box 9121,
DAR ES SALAAM.

6.0  Courses and Fees:
Amount of fees and more information open http:/rudn.ru/en

Source: http://www.moe.go.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=1827:scholarship-tenable-in-peoples-friendship-university-of-russia-pfur-20152016&catid=1:latest-news

TCU invites applications from Tanzanians for 2015 Commonwealth Scholarships

Commonwealth Scholarships Tenable in the United Kingdom for the year 2015

The Tanzania Commission for Universities as a nominating agent in the country for the Commonwealth scholarships is inviting applications from qualified Tanzanians for Masters and Doctorate degrees tenable in the United Kingdom in the year 2015.

The Scholarships include:
 • One year taught Masters courses or equivalent degrees 
 • Doctorate degrees, of up to three years duration 
Qualifications 

1. Applicants must be holders of Bachelor or Masters degrees; 
2. Applicants for Masters must have Bachelor degree of GPA not less that 3.5; and 
3. Applicants for Doctorate degrees must have a B Grade Masters degrees or a GPA of 4 or above at Masters level. 

Mode of Application: 
 • All applications should be made directly to the Commonwealth Secretariat and should online using the following link: http://cscuk.dfid.gov.uk/apply/scholarships-developing-cw 
 • It is important that applicants should read and understand all given instructions when filling the application forms, and should attach all necessary attachments such as certified copies of academic certificates, transcripts, birth certificates and submit online through the above mentioned link. 
All applicants who wish to be nominated by the Tanzania Commission for Universities, should print one hard copy of completely filled application form, attach with certified photocopies of academic certificates, transcripts, birth certificates and submit them to the address below before 31st October, 2015. 

The Executive Secretary, 
Tanzania Commission for Universities, 
P.O. Box 6562, 
DAR ES SALAAM.

Jinsi ya kupata tisheti za "Go Big Or Go Home"


Go Big Or Go Home...! 

Rafiki zangu wengi walinipigia Simu na kuniandikia jumbe fup ifupi, wakiniomba niwapatie Tisheti Zenye hii slogan ya "Go Big Or Go Home"

Wengi wameniambia kwamba zinawapa moto wa kukazania malengo yao. Hata kama mtu anajisikia uvivu akikumbuka hii slogan anapata nguvu ya kusimama.

Tisheti hizi zinapatikana sasa kwa kuwasiliana na Mona Jona, Afisa Masoko wetu 0715812572. Mwandikie ujumbe mfupi atakuelekeza jinsi ya kupata tisheti yako.

Nilipokea maoni ya kufanya marekebisho; Nitayafanyia kazi. Asanteni sana sana.

To me life is a classroom. Dream beyond. Be your own aspiration. The Choice is up to you nobody else. Go Big Or Go Home.

Katika yote uliyochagua maishani kuwa mtendaji, usikubali kuyaishi maneno, ishi matendo. 


Meshack Maganga

[video] Mdahalo wa wawakilishi wa vyama vya siasa kuhusu Uchumi na Usawa

[video] Simba vs Yanga - Mechi nzima ya Jumamosi 26.09.2015Wamsimamisha Magufuli na kuanza kuita Lowassa
Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia gharika ya wananchi wa Makambako mkoani Iringa ambako alipita leo kumalizia viporo vya mkoa huo kwenye kampeni zake.

Wananchi kwa maelfu wakimsikiliza Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia huko Makambako mkoani Iringa ambako alipita leo kumalizia viporo vya mkoa huo kwenye kampeni zake.Wagombea wa nafasi mbalimbali wa Mafinga wali-Magufulika mbele ya Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli katika jimbo la Mafinga mkoani Iringa ambako alipita leo kumalizia viporo vya mkoa huo kwenye kampeni zake.

Mgombe ubunge jimbo la Mafinga Mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Cosato Chumi, aki-Magufuli-ka

Mgombea Ubunge Jimbo la Mufindi Kaskazini, Mahamudu Mgimwa akidhihirisha kuwa yupo fiti.
 • Picha: Ahmad Michuzi, Jnr.

Magufuli aanza kuwataja kwa majina wale "CCM mchana, UKAWA usiku"

 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Shinyanga mjini Ndugu Stephen Massele kwenye mkutano wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya Kambarage.

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, jana aligeuka mbogo baada ya kuamua kuwataja hadharani watu wanaohujumu kampeni zake kwa kujifanya mchana wako pamoja na usiku wakigeukia upande wa upinzani.

Akiwahutubia wananchi wa mkoani Shinyanga jana katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage, Dk. Magufuli, alisema kuna mamluki wanaokihujumu chama hicho katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Dk. Magufuli aliwataja hadharani baadhi ya makada hao ambao wamekuwa wakiipigia kampeni CCM mchana na usiku wakiwapigia wapinzani.

“Kuna baadhi ya wana-CCM wanatujuhumu sana, wengine nawajua hata majina yao bahati nzuri huwa sisemi uongo bali ukweli, kuna huyu Gasper mchana tunakuwa naye CCM lakini usiku anaungana na wapinzani,” alisema.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Dk. Magufuli ilipokelewa kwa mshangao na baadhi ya wananchi na wanachama waliokusanyika uwanjani hapo, kwa kuwa baadhi ya makada hao walikuwa wameketi jukwaa kuu wakifuatila hotuba yake.

Mwandishi wa habari hizi alimshuhudia meneja kampeni wa mgombea huyo, Abdallah Bulembo, akimfuata Magufuli na kumnong’oneza, ghafla Magufuli alibadilisha na kudai msaliti ni Gasper Anthony wala si Gasper Kileo aliyetajwa awali.

Hata hivyo, Magufuli baada ya kumaliza hotuba yake alimfuata kada huyo na kumkumbatia huku akimtuliza na kuendelea na msafara wake.

Kada huyo aliyetajwa kuwa msaliti anadaiwa awali kuwa mpambe wa mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa, anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba (UKAWA).

Akizungumza katika mkutano huo wa kampeni, Kileo alisema alimuunga mkono Lowassa akiwa CCM, lakini kwa sasa anamuunga mkono mgombea urais wa chama hicho, Dk. Magufuli na wala kwa kilichotokea hatarajii kukihama chama.

Akiwahutubia mkoani Shinyanga, Magufuli amesema hashangai wananchi kuanza kumwita rais kwa sababu hata yeye anajua kuwa ndiye atakayeibuka na ushindi mnono kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Alisema wagombea wengine wa nafasi ya urais ni wasindikizaji tu kama walivyo wapambe wa kwenye harusi.

Taarifa ya Ikulu: Tanzania kupata mabilioni mengine ya MCC

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Sasa ni Rasmi: Tanzania kupata mabilioni mengine ya MCC
 • Yafaulu mtihani wa kupata bilioni 992.8 za kuboresha sekta ya umeme
 • Yafanikiwa baada ya kutimiza masharti yote likiwemo la kupambana na rushwa
 • Zitaanza kutolewa mwakani baada ya kupigiwa kura na Bodi ya MCC
Tanzania imetimiza masharti yote ya kupatiwa raundi ya pili ya fedha za maendeleo kutoka Shirika la Maendeleo ya Milenia la Millennium Challenge Corporation (MCC) la Marekani na itaanza kupata na kunufaika na mabilioni hayo ya fedha baada ya wajumbe wa Bodi ya MCC kupiga kura ya kuidhinisha kutolewa kwa fedha hizo chini ya Mpango wa MCC-2.

Habari hizo njema zimetangazwa Jumamosi, Septemba 26, 2015, kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, na Mtendaji Mkuu wa MCC, Bi. Dana J. Hyde katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya JW Marriot Essex House, New York, na kuhudhuriwa na watumishi waandamizi wa MCC akiwamo Bwana Kamran Khan, Makamu wa Rais wa Operesheni za MCC. Rais Kikwete yuko New York kuhudhuria shughuli za mwaka huu za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.“Hongera Mheshimiwa Rais kwa sababu nchi yako, Tanzania imetimiza masharti yote ya kupata fedha nyingine chini ya mpango wa MCC - 2, ikiwa ni pamoja na uongozi wa MCC kuridhika kuwa Tanzania inachukua hatua za dhati kupambana na rushwa,” Bi. Hyde amemwambia Rais Kikwete na viongozi wengine wa Tanzania akiwamo Waziri wa Nchi za Fedha wa Zanzibar, Mheshimiwa Yusuf Omar Mzee.

Bi. Hyde amemwambia Rais Kikwete kuwa Bodi ya MCC, katika mkutano wake wa Septemba 17, mwaka huu na chini ya Mwenyekiti wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Bwana John Kerry, imeafiki kuhusu kipengele pekee kilichokuwa kimebakia katika masharti ya kupata fedha za MMC kuwa ni kweli Tanzania inakabiliana ipasavyo na rushwa na kuchukua hatua stahiki kukabiliana na janga hilo la rushwa.

MCC imetoa taarifa ya kuthibitisha kuwa Tanzania imetimiza masharti ya kuiwezesha kufaulu kupata raundi ya pili ya fedha za maendeleo na pia imetoa taarifa ya kuthibitisha kuwa ni kweli Bodi ya MCC imeridhishwa na hatua zinazochukuliwa kukabiliana na rushwa.

Tofauti na fedha nyingi zinazotolewa na wafadhili wengi duniani, fedha za MCC hazitakiwi kurudishwa na nchi inayopewa fedha hizo na pia nchi husika hupewa uhuru wa kuchagua aina ya miradi ya maendeleo ambayo inaitaka igharimiwe na fedha hizo.

Miongoni mwa wajumbe wengine wa Bodi ya MCC ni pamoja na Waziri wa Fedha wa Marekani ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi, Mwakilishi wa Biashara wa Marekani duniani, Mwendeshaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), nafasi ambayo kwa sasa anaikaimu Bwana Alfonsi Lenhardt, Mtendaji Mkuu wa MCC Bi. Hyde na Rais wa Taasisi ya International Republican Institute (IRI) Balozi Mark Green.

Mabalozi Lenhardt na Green walikuwa mabalozi wa Marekani katika Tanzania wakati wa majadiliano, upitishaji na utekelezaji wa MCC–1.

Bi Hyde amesema sasa linalobakia ni kwa wajumbe wa Bodi kupelekewa muhtasari wa kuidhinisha mabilioni hayo kwa Tanzania ambayo chini ya mpango wa uwekezaji wa MCC–2 yatakwenda katika kuboresha huduma za umeme katika Tanzania ikiwa ni pamoja na kusambaza umeme katika vijiji vingi zaidi nchini. Kiasi cha asilimia 46 ya Watanzania kwa sasa wanapata umeme kutoka asilimia 10 ya mwaka 2005 na sehemu kubwa ya asilimia hiyo imetokana na msaada wa MCC-1.

Chini ya Mpango huo wa pili wa MCC, Tanzania itapatiwa kiasi cha dola za Marekani milioni 472.8 (sawa na sh. bilioni 992.80). Kwa kutilia maanani kiasi cha dola milioni 698 (sawa na sh. trilioni 1.46) ambazo zilitolewa chini ya MCC-1 basi Tanzania itakuwa imepata jumla ya dola za Marekani trilioni 2.45 za maendeleo kutoka Marekani katika kipindi cha miaka 10 tu iliyopita. Fedha za MCC-2 zitaanza kutolewa mwakani, 2016.

Kiasi kilichotolewa kwa Tanzania wakati wa MCC-1 ndicho kilikuwa kiasi kikubwa zaidi ambacho kimepata kutolewa na Marekani chini ya Mpango huo wa Millennium Challenge Corporation na kwa kupita MCC-2 Tanzania itakuwa ni nchi ambayo itakuwa imepata kiasi kubwa cha fedha za maendeleo chini ya MCC duniani.

Fedha zilizotolewa chini ya MCC -1 zilitumika kujenga Barabara za Tunduma-Sumbawanga, Tanga-Horohoro na Namtumbo-Songea-Mbinga.

Aidha, fedha hizo zilitumika kujenga upya mfumo wa huduma za maji kwa ajili ya miji ya Dar es Salaam na Morogoro na zilitumika kusambaza umeme katika vijiji vya mikoa 10 ya Tanzania Bara.
Fedha hizo vile vile zilitumika kutandaza njia ya pili ya kusafirisha umeme chini ya Bahari ya Hindi kati ya Bara na Tanzania Visiwani na pia zilitumika kujenga barabara zote kuu za Kisiwa cha Pemba na baadhi ya barabara za Unguja kwa kiwango cha lami.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
27 Septemba, 2015

Taarifa ya Mkuu wa Habari Simba, Haji Manara kwa washabiki

TAREHE 26-9-2015 jana jumamosi kulifanyika mechi ya ligi kuu ya vodacom Tanzania bara baina y a klabu yetu ya Simba na timu ya Yanga.

Kwenye mchezo huo timu yetu imepoteza mchezo huo kwa kufungwa goli mbili kwa bila.

Tumeanza kuandika hvyo hapo juu kwa maksudi kuonyesha sisi Simba tumeyakubali matokeo hayo ya dakika tisini za mchezo na tutumie nafasi hii kiungwana kabisa kuwapongeza watani wetu wa jadi kwa ushindi huo walioupata.

Pili tumshukuru mungu kwa kutuwezesha kumaliza mchezo huo salama nahapa mungu ashukuriwe sana pamoja na wapenzi wetu pia.sababu washabiki wetu wameonyesha utulivu wa kiunamichezo kwa kutokufanya fujo yoyote licha ya mwamuzi wa mchezo huo Israel Nkongo kuharibu mchezo kwa makusudi.

Nkongo kwa dhamira ya kusudi jana aliamua kuwatoa wachezaji wetu mchezoni kwa kuanza kugawa kadi kwa wachezaji wetu pasi na sababu na kwa rafu zilezile kuacha wachezaji wa Yanga kucheza bila kuwaonya.

Kilichoshangaza washabiki wote waliokuwa uwanjani na walioangalia kwenye televisheni ni kumuacha mchezaji wa Yanga Donald Ngoma kuendelea na mchezo ilhali alimpiga kichwa cha maksudi mchezaji wetu Hassan Kessi!

Mbali ya vitendo hvyo wachezaji wetu wametulalamikia kutukanwa na mwamuzi wa mchezo huo Nkongo.

Tunaamini Tff watachunguza malalamiko yetu na kuchukua hatua stahiki kwa mwamuzi huyo ambaye kila mtu aliyeuona mchezo huo anakiri kuwa alishindwa kuumudu.

Mwisho na kwa umuhimu wa kipekee klabu ya Simba inaendelea kuwashkuru washabiki kwa utulivu wao licha ya vitendo vya mwamuzi huyo ambavyo vingeweza kabisa kuharibu amani iliyokuwepo uwanjani jana.

Tunawaomba waendelee kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho uongozi wenu umewaandikia TFF na bodi ya ligi ambazo tunaamini zitatenda haki..

Reclaming our glrory
Simba nguvu moja

Imetolewa na Haji S.Manara
Mkuu wa habari wa Simba

Simba sports club
27-9-2015

Nb.mchezo dhidi ya yanga ushapita na sasa tunajipanga kwa game ijayo.

Tunawaomba wapenzi wetu mjitokeze kwa wingi kwenye mechi yetu dhidi ya Stand united jtano ijayo ya tarehe 30-9-2015

Lowassa aahidi 'one stop centre' kupunguza urasimuMgombea urais kwa tiketi ya CHADEM anayewakilisha UKAWA Edward Lowassa amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano atahakikisha kuwa serikali yake inaanzisha kituo maalum cha jamii 'one stop centre' kitakachokuwa kikitoa huduma kwa umma sehemu moja ili kupunguza urasimu katika kupata huduma hizo.

Lowassa akiwa katika mkoa wa 20 wa mikutano ya kampeni ya kuomba ridhaa ya watanzania kumchagua kuwa rais wa awamu ya tano leo akitumia njia ya barabara katika azma yake ya kuwafikia wananchi wote hata wa vijijini, alifanya mikutano mitano -- Kata za Rundugai, Shirimatunda, Machame Mkwakwasi, Masama Mula na baadaye kuzindua kampeni katika mkutano uliofanyika Boma Mjini. -- katika Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro ikiwa na lengo la kuzindua kampeni za mgombea ubunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe. [taarifa via ChannelTEN]


Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akipokelewa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Freeman Mbowe, wakati alipowasili eneo la Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Mpira wa Machame, Jimbo la Hai, Mkoani Kilimanjaro Septemba 26, 2015.


Picha zote tumeshirikishwa na Othman Michuzi/Michuzi Jr2/Mtaa kwa Mtaa blog.