Taarifa nzima ya habari ChannelTEN Septemba 28, 2015
Yaliyojiri magazetini leo Septemba 29, 2015

Waliochaguliwa kujiunga na Vyuo vya Afya

MATOKEO YA AWALI KWA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA VYUO VYA AFYA


1. Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kujiunga na kozi mbalimbali za afya kwa ngazi ya Cheti (Astashahada) na Diploma (Stashahada) kupitia Mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kuwa, Uteuzi wa awali umefanyika na waombaji 9306 kati ya 21228 wameteuliwa kujiunga na vyuo mbalimbali. Matokeo ya uteuzi huo yanapatikana katika kurasa binafsi (Profiles) za waombaji.

2. Waombaji wote ambao wamechaguliwa katika awamu hii wanapaswa kuthibitisha kuwa wataripoti katika vyuo walivyopangiwa na mwisho wa kuthibitidha ni Ijumaa tarehe 16 Oktoba 2015. Iwapo muombaji hatathibitisha, nafasi hiyo itatolewa kwa mwingine. Kuweza kuthibitisha bonyeza hapa.

3. Kwa wale ambao bado hawajapangiwa vyuo, kurasa binafsi zenu zina maelezo yenye sababu za kutopangiwa chuo katika awamu hii na maelekezo ambayo unatakiwa kuyatekeleza ili mfumo utakapochakata uteuzi wa awamu nyingine siku ya Jumatatu 19 Oktoba 2015 idadi kubwa zaidi ya waombaji iweze kupangiwa vyuo kwani hadi sasa nafasi zipatazo 11566 hazijajazwa.

Imetolewa na:

Katibu Mtendaji
Baraza la Taifa la Elimu yaUfundi (NACTE)
27 Septemba 2015

Two of 100 don't understand you, so what? Be content!

When you find yourself overwriting, embracing redundancy and overwhelming people with fine print, you're probably protecting yourself against the 2%, at the expense of everyone else. (And yes, it might be 10% or even 90%.... that's okay).

When we hold back and dumb down, we are hurting the people who need to hear from us, often in a vain attempt to satisfy a few people who might never choose to actually listen.

It's quite okay to say, "it's not for you."
Seth Godin via blog

Mndeme: Tanzania tuna migodi ya thamani kuliko dhahabu na gesi

Unapoutazama ulimwengu kiuchumi, unagawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni nchi tajiri, nchi za kipato cha kati na nchi za kipato cha chini (high-income, middle-income and low-income countries). Ninapenda kutumia vigezo vya kipato kutofautisha makundi haya kuliko kile cha "nchi maskini na nchi tajiri" kwa kuwa sio kweli kwamba nchi zote zenye kipato cha chini ni maskini na zote zenye kipato cha juu ni tajiri. Utajiri na umaskini wa nchi ni zaidi ya kuzalisha mali zinazohesabika kama mapato. Huu ni msimamo wangu na sio lazima ukubaliane na kanuni na tafsi za wachumi wabobezi au wanasiasa. Nyingi ya nchi zinazoitwa tajiri, zimepata utajiri huo kwa kupora mali kutoka nchi zinazoitwa maskini kwa hila na ujanjaujanja wa aina nyingi wanaoulinda na mifumo na kisheria zinazoitwa za kimataifa. Mara nyingine, wanalazimisha nchi zenye rasilimali zijitungie na kujiwekea sheria mbovu zinazawapa wao uhalali wa kuja kupora huku mukiwatazama na kuwapigia makofi kwa jina la uwekezaji.Tofauti kubwa kati ya nchi za kipato cha juu na zile za kipato cha chini inaweza kutazamwa zaidi katika tofauti ta maendeleo ya kiviwanda na tafiti za sayansi na kiteknolojia (elimu). Nchi tajiri zimepiga hatua kubwa katika tafiti za kisayansi na hivyo kuwa na maendeleo makubwa ya kiteknologia na viwanda na kupelekea kuwa wazalishaji wa bidhaa nyingi, ambazo mwisho wa siku, soko lake kubwa ni nchi zisizo na uwezo huo (za pato dogo). Siyo hivyo tu, bali maendeleo haya ya kisayansi na teknolojia yamewafanya kupiga hatu kubwa ya ujenzi wa miundombinu ya kila aina yenye kuboresha hali za maisha ya watu wao, kujitafutia kipato, pamoja na uhakika na ubora wa huduma za kijamii (afya, elimu, maji, nishati, usafiri, nk).

Wataalam wa kiuchumi wanatushauri kwamba, ili nchi iweze kuendelea, pamoja na mambo mengine ni lazima iweze kuwa na viwanda angalau vidogo na vya kiwango cha kati ambavyo vitaweza kubadilisha malighafi zinazopatikana katika nchi husika kuwa bidhaa zinazotumika. Mfano mzuri ni viwanda vinavyoweza kusindika vyakula na vinywaji vya matunda; kutengeneza mavazi kutokana na pamba; kutengeneza viatu na bidhaa zitokanazo na ngozi, nk. Historia ya uchumi wa dunia hasa ndani ya miaka 30 iliyopita imjenga tofauti kubwa sana kati ya nchi za kipato cha juu na cha chini na kuzifanya nchi za kundi la pili kuwa na wakati mgumu sana wa kuendelea kiviwanda kama njia kuu ya kupiga hatua za maendeleo. Kuna maelezo mengi ya kwa nini hali hii imekuwepo lakini ushahidi ni mkubwa kwamba nchi zilizoendelea kiviwanda na teknologia zimekua sababu kubwa ya kuzifanya nchi maskini kushindwa kupiga hatua. Kuna mifumo mingi ya kifedha, kiuchumi, kibiashara, uwekezaji na kisiasa ambayo imezifanya nchi maskini zisisogee na hivyo kuendelea kuwa wanyonge mbele ya nchi tajiri. Naomba nisiingie ndani sana katika hili maana kuna maelezo mengi, magumu na sababu zingine zinaleta maumivu ya kihisia.Mifumo hii ya uchumi unaondeshwa na kuamuliwa na nchi tajiri ni mgumu sana kuuvunja au kuupindua kwani waliouweka wamejenda misingi mikubwa sana yenye nguvu katika kila nyanja ya maisha. Kwa mfano, nchi zenye nguvu ya kiuchumi, zimeingiza baadhi ya dhana na kuzifanya kuwa vigezo vya kimataifa (international standards) ambazo nchi maskini ikivikeuka zinajikuta katika hali ngumu. Mojawapo ya vigezo hivyo ni msisitizo wa misingi ya kiutawala wa kidemokrasia; zinazoitwa haki za binadamu; mahusiano ya kibiashara; na mengine. Kinachoumiza zaidi ni ukweli kwamba, vigezo hivi vyote vinaungwa na wenye uwezo kwa kuzingatia maslahi yao na kisha nchi maskini zinalazimishwa kuzikumbatia na kuzilinda kisheria bila kujali misingi na tamadunia zao ambazo zinatofautina na anaowaletea taratibu hizo. Mambo haya yameiweka nchi maskini katika wakati mgumu na kujikuta zimejiingiza kwenye mikataba mibaya na mahusiano mabovu ya kibiashara. Haya yamepelekea kuendelea kuua uwezo wao wa kujitegemea na wakati huohuo kushuhudia utajiri na rasimaliza za nchi zao kuchotwa na kuwaacha wakiwa hawana chochote cha kuwanufaisha kwa muda mrefu. Tanzania inahusika sana katika hili na mifano ni mingi ya jinsi tulivyoumizwa na tunavyoendelea kuumizwa na mifumo hii.

Tufanyaje?

Serikali yoyote makini inayoangalia hali ya kiuchumi ya wananchi wake na taifa kwa ujumla na kuwa wakweli bila uyeyushaji wa kisiasa, ni lazima ikubali ukweli kwamba hawawezi kufurukuta kirahisi katika mazingira haya na ni lazima wajiulize swali la pili: tunafanyaje? Je, tuna mbadala?

Ili kutoendelea kuwa wahanga wa mifumo kandamizi ya uchumi wa kidunia inayozinyima nchi maskini kuendelea, ni lazima zirudi kwenye msingi (drawing board) na kuangalia ubunifu mbadala wa kujikwamua kwenye umaskini. Hili ni lazima lifanyike kwa umakini mkubwa sana ili kuona ni maeneo gani kika mazingira yetu twaweza kuyatumia kujikwamua na kubadili hali

za maisha yetu bila kuhitaji msaada wa mtu au nchi nyingine. Sio hivyo tu, bali tuweze kufanya hivyo huku tukiwapa wanyonyaji nafasi ndogo sana ya kutuingilia na tutumie rasilimali zetu tulizonazo ikiwa ni pamoja na wataalamu wetu tuliowandaa sisi wenyewe. Tukiweza hilo, tutakua na uwezo hata wa kujenga mahusiano sahihi na nchi zingine yenye usawa katika aina ya ushirika tunaojenga kuliko huu wa sasa.

Nchi makini zilizopitia mazingira haya ya uonevu wa kiuchumi, zimetumia njia hizi na zinafanikiwa sana. Miongoni mwa nchi hizo ni pamoja na China, India, Korea ya Kusini na Brazili. Kwa mfano, kwa kutambua umuhimu wa ushindani wa kimataifa na kujiandaa vuma kupambana na washindani (maadui!!) wa kiuchumi, China inapeleka raia wake zaidi ya milioni ishirini (20,000,000) kila mwaka kusoma kingereza nje ya nchi yao. Sio hivyo tu, ukienda vyuo vikuu vya nchi za Ulaya zinzosifika kwa elimu bora, utashangaa na wingi wa wanafunzi wa shahada za uzamili na uzamivu toka chini za Asia na hasa China. Nimeshuhudia baadhi ya programu za uzamivu (hasa biashara na uhandisi) kwenye baadhi ya vyuo, vikiwa havina hata mwanafunzi mmoja wa nchi husika na badala yake ina mamia ya wanafunzi toka China. Vijana hawa wanapomaliza, hawatafuti kuzamia kubaki ulaya, bali wanarudi kwenye nchi zao kupeleka ujuzi huu na kushindana kikamilifu.Nchi ya Korea Kusini ambao uchumi wao unatisha kwa kutegemea viwanda hasa eneo la vifaa vya kielkroniki, kila mwaka linapeleka mami ya vijana kufanya shahada za uzamivu (PhD) katika vyuo bora kabisa duniani Marekani na Ulaya. Vijana hawa wanasomeshwa kwenye vyuo hivi kwa gharama kubwa ya serikali zao kwa lengo la kupeleka ujuzi sahihi wa ushindani kujenga nchi yao.

Nchi ya India, pamoja na maeneo mengi ya uazalishaji yakiongozwa na kilimo cha kisasa, imewekeza katika biashara ya tiba (medical tourism) kwa kuhakikisha imesomesha wataalamu bora; kutengeneza madawa; kujenga hospitali za kisasa; na kutengeneza vifaa bora vya tiba. Ndio maana imekua kimbilio la tiba na inavuna mabilioni ya fedha toka karibu nchi zote za kiafrika kwa idadi kubwa ya wagonjwa wanaopelekwa kupata tiba kila mwaka. Huduma hii sio tu kwamba imeipa India umaarufu na kuongeza kipato cha moja kwa moja, bali imetengeza wingi wa ajira na mapato yatokanayo na huduma zingine zitakazohitajika na watu wanaofuata tiba. Nchi zingine zinazoona mbali kama vile Omani na Dubai, zimeanza kuwekeza kwenye eneo hili la tiba pamoja na kwamba wanafanya vizuri sana kwenye maeneo mengi ya uzalishaji. Wamegundua kwamba katika dunia ya kisasa, tiba sio huduma tu bali ni biashara na uwekezaji unaolipa kwa uhakika.Sina haja ya kueleza ni kwa jinsi gani Brazil wametumia mpira wa miguu (football) kama uwekezaji usiohitaji mtaalamu wala msaada toka nje na ni kwa jinsi gani umpira umeitambulisha nchi hii katika uso wa dunia na kuwa ajira ya muhim na njia ya mapato kwa wengi. Mifano ni mingi ya jinsi nchi zinazoibukia zinafanya hivyo kwa ubunifu unaokwepa utegemezi wa nchi tajiri na kutumia ubunifu wao. Hata hivyo ngoja nijirudi kwa ninachotaka kusema kuhusu nchi yangu pendwa ya Tanzania.

Tuanzie wapi?

Serikali yetu kwa muda mrefu sasa imekua na mipango na mikakati mingi ya kujikwamua kwenye umaskini na kuijengea nchi uwezo wa kujitegemea. Mipango na mikakati hii ni mizuri tu na inaonesha nia njema kabisa ndani ya mioyo na mawazo ya waliyoiandaa. Hata hivyo tukubali kwamba mingi ya mikakati hii haijaleta matokeo tarajiwa. Kuna ambayo imekufa kabla ya utekelezaji wake; kuna ambayo imekua ni mifuko iliyotoboka ya kupoteza mabilioni ya fedha; kuna ambayo inasonga kwa kujikangoja; na kuna michache inaleta mafanikio yanayotia moyo. Nisingependa kuwa msemaji wa serikali katika makala hii kuelezea ni miradi na mikakati ipi imefanikiwa au imesindwa kuleta mafaniko. Sina ujasiri wa kufanya hivyo kwa sasa hasa ukizingatia ni kipindi cha kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu.

Pamoja na mikakati iliyoko, ambayo mingi inaendeshwa na nchi tajiri kwa namna mbalimbali (inategemea ufadhili wao; tau tunaiga wanachofanya wao; au unategemea ushauri na utaalamu wao; au wanatulazimisha kuitekeleza kwa malengo yao); ninaamini kuna vitu hatujavitazama kama rasilimali na kama tumefanya hivyo hatujavuka toka kwenye mtazamo kwenda kwenye vitendo. Katika makala hii, nataka nizungumzie maeneo matatu au manne ambayo ninashawishika tuna uwezo mkubwa sana wa kuyafanyia kazi, kuyaendeleza na kuyatumia kuboresha hali ya maishayetu. Makuzi na uzoefu niliopitia umenifundisha kutodharau mambo madogo na kutotamani mambo makubwa wakati madogo yamenishinda au sijafanikiwa kuyatekeleza. Kwa minajili hiyo, naamini katika dhana ya kukua, kuendelea na kufanikiwa hatua kwa hatua ili kuwa na maendeleo endelevu kwa mtu binafsi, jumuiya ya watu, na taifa pia. Historia ya watu na nchi nyingi zilizofanikiwa zinaonesha na kulithibitisha hilo. Siamini sana katika mafanikio ya kushtukiza, kusaidiwa, kuoteshwa, au ya miujiza isiyo na maelezo maana yana madhara yake. Hivyo ninataka nizungumzie maeneo matatu ambayo kwa udogo wake yanaweza kubadili mwelekeo wa baadhi ya mambo na kuleta maendeleo ya kichumi ya mtu mmoja mmoja na taifa, na kulijengea taifa letu sifa za kipekee kama zile tunazozifuata kwenye nchi nyingine.

Maeneo hayo sio mageni na nitakua muongo nikisema naleta uvumbuzi au ugunduzi mpya. Ninachotaka kufanya ni kuyaelezea katika mtazamo unaweza kumfanya angalau mtu mmoja kuyatazama kiuchumi/uzalishaji-mali, badala ya kuyatazama tu kwa mazoea kama huduma za kijamii. Sababu ya kufanya hivyo unajengwa katika msingi wa kwamba nchi yetu iko katika mazingira yenye fursa za kipekee (strategic position and opportunities) ukilinganisha na nchi nyingi zinazotuzunguka. Hivyo, tunaweza kutumia fursa hizo kujijenga sisi wenyewe na kuwafanya wengine watuone kama kimbilio lao kwenye baadhi ya mambo hivyo kutuletea mapato kwa watachokifuata kwetu.

Endelea kunisoma kwenye makala itakayofuata.

---
Mwalimu MM ni mhadhiri katika kitengo cha Sayansi ya Kompyuta ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na mtafiti wa mifumo ya TEHAMA katika Huduma za afya (Health Informatics). Unaweza kuwasiliana naye kupitia [email protected]

Tanzania Oil and Gas Almanac launches today

(image via WhatsApp)
On Tuesday 29th September 2015 FES Tanzania will launch the Tanzania Oil and Gas Almanac and present other tools aimed at promoting transparency in Tanzania's oil and gas sector.

We therefore invite senior government officials, policy makers, members of parliament, representatives of civil society and international organisations as well as journalists to a guided tour around the Tools for Transparency and Information Platforms with presentations from FESTanzania, OpenOil and the Natural Resource Governance Institute.

Please email [email protected] if you are interested in attending this event.
News/Event cross-posted from: fes-tanzania.org

Kwa nini nyumbu wote hawa wamekufa? Hundreds of wildebeest found dead in Tanzania

Update: >>  Statement by Tanzania National Parks on the death of wildebeest

Cross-posting this tragic news from africageographic.com

Hundreds of lifeless wildebeest were spotted this morning in the Mara River in northern Serengeti, Tanzania. The sad sight was captured on phone cameras by safari guides.
The images below can only be described as tear-jerking. The pile of carcasses stretches into the distance and scavenger birds have already started circling the wildebeest.
According to our source on the ground, the authorities have been contacted and the exact cause of death has yet to be confirmed. If the past is anything to go by, the wildebeest chose a crossing point that was too deep.
As an African travel operator with a love for our continent and wildlife inhabitants, the incident saddens us deeply and is a reminder of what happened in 2007 when 10,000 wildebeest died in a mass drowning.

I couldn't resist posting this video: Life lessons from people of all ages


Manifesto ya CUF kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu Tanzania 2015


Jipakulie nakala (pdf) kwa kubofya hapa.


[video] Magufuli aona isiwe taabu, ashuka garini kupitia dirishani


Kiwewe cha watu! Lowassa ashindwa kuhutubia Tangamano, mjini Tanga


Mgombea wa nafasi ya urais kupitia CHADEMA anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda UKAWA, Edwrad Lowassa amelazimika kuahirisha mkutano katika kiwanja cha Tangamano, mjini Tanga baada ya watu wengi kujitokeza na kusababisha msongamano ambao ulihatarisha maisha yao.

Taarifa zinasema kuwa kwa mara ya kwanza shughuli zote zinazofanyika katika mitaa ya barabara ya 4, 5, 6, 7, 8 zililazimika kusimama kwa muda kutokana na hali hiyo.

Juhudi zilizofanywa na viongozi wa UKAWA wakiongozwa Fredrick Sumaye za kujaribu kutuliza hali ya mambo hazikuzaa matunda.


Kauli ya Wizara kuhusu Mahujaji kutoka TanzaniaTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa zaidi kuhusu Mahujaji kutoka Tanzania waliofariki na kujeruhiwa huko Saudi Arabia


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kupitia Ubalozi wake mjini Riyadh, Saudi Arabia imepokea taarifa kuwa hadi kufikia tarehe 27 Septemba, 2015 watu waliopoteza maisha kufuatia tukio la mkanyagano (stampede) wa Mahujaji waliokuwa wakielekea Jamarat kutupa vijiwe huko Mina nje kidogo ya mji wa Makkah, lililotokea siku ya Alhamisi tarehe 24 Septemba, 2015 wameongezeka na kufikia 769 na majeruhi 934.

Aidha, Wizara kupitia Ubalozi huo inaendelea kufuatilia hatma ya Mahujaji wa Tanzania waliopotea katika tukio hilo la ajali ambapo hadi sasa Mahujaji wa Tanzania wapatao 50 bado hawajaonekana. Vikundi wanavyotoka Mahujaji hao na idadi yao ni kama ifuatavyo:-
 1. Ahlu Daawa-Mahujaji 30;
 2. Khidma Islamiya-Mahujaji 16; na
 3. TCDO-Mahujaji 4
Vile vile juhudi za Ubalozi kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission na viongozi wa vikundi vilivyopoteza Mahujaji wao zimefanikiwa kuutambua mwili wa hujaji mmoja aliyefariki dunia anayejulikana kwa jina la Shafi Khamis Ali kutoka kikundi cha Ahlu Daawa. Kutambuliwa kwa mwili wa hujaji huyo kunafanya idadi ya Mahujaji wa Tanzania waliofariki dunia katika ajali hiyo kufikia watano (5).

Pia, Wizara kupitia Ubalozi wake imepokea taarifa ya kupatikana kwa hujaji mwingine anayeitwa Nasra Abdullah akiwa hai naye kutoka kikundi hicho cha Ahlu Daawa.

Kuhusu majeruhi, taarifa kutoka Ubalozini zinaeleza kuwa, hujaji mmoja aliyejulikana kwa jina la Mahjabin Taslim Khan alipata majeraha yaliyopelekea kukatwa mguu na kwa sasa anaendelea kupata matibabu huku hali yake ikiendelea vizuri.

Ubalozi unaendelea na juhudi za kuwatafuta Mahujaji wengine wa Tanzania ambao bado hawajaonekana kwa ajili ya kubaini wale waliofariki au majeruhi wanaoendelea kupatiwa matibabu.

Mahujaji wengine wa Tanzania wapo salama ambapo tarehe 26 Septemba, 2015 walimaliza ibada ya hija na tarehe 28 Septemba, 2015 wameanza safari ya kurejea nyumbani.

Wizara inaendelea kuwaomba Wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati Serikali ikiendelea kufuatilia.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali kwa Umma,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

28 Septemba, 2015

[video] Nape ahutubia leo mkutano wa kampeni Iringa


Lowassa afika Bumbuli, Tanga


Bongo Movie Artists watangaza kutembea nchi nzima kwa bajaj kumnadi Magufuli


Baadhi ya Wasanii nyota wa Filamu hapa nchini wakiongozwa na Jacob Steven a.k.a JB wakiwa wamenyanyua juu mikono yao kwa pamoja ni Ushindi sambamba na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli (wa tatu kushoto),kuonesha kuwa wasanii hao wanamuunga mkono Dkt Magufuli katika mbio zake za kuusaka Urais kwa kutembea nchi nzima kutumia Bajaji zao tano,ambapo Bajaj mojawapo itakuwa na kazi ya kukusanya kadi za wale wanaomua kurudi/kujiunga na chama cha CCM.

Magufuli katika kampeni Iringa

 Ulinzi ukiwa umeimarishwa wakati msafara wa Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli ukitoka kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa baada ya mkutano wa kampeni kumalizikaMnanda sijui mdundiko au mchiriku huu? Wamemtungia Lowassa


Ugonjwa wa bawasiri na namna ya kuuepuka


FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU

Watu wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba

BAWASIRI (HEMORRHOIDS) NI NINI?

Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nnje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe

Ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita hemorrhoids ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles

Tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50

AINA ZA BAWASIRI

Kuna aina mbili za bawasiri

(A) BAWASIRI YA NDANI
 1. Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili 
 2. Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa 
 3. Aina hii imegawanyika katika madaraja manne 
 • DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahal pale panapohusika 
 • DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyew ndani baada ya kujisaidia 
 • DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe 
 • DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi 
(B) BAWASIRI YA NNJE

Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo thrombosed hemorrhoids.

CHANZO CHA TATIZO

Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷
 • Kufanya mapenzi kinyume na maumbile
 • Kuharisha kwa muda mrefu
 • Tatizo la kutipata choo
 • Matatizo yatokanayo na umri
 • Kukaa kitako kwa muda mrefu
 • Uzito wa kupita kiasi
 • Matumiz ya vyoo vya kuketi
DALILI ZA BAWASIRI
 • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa 
 • Kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia 
 • Kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa 
 • Kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo 
 • Kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana 
MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI

Matibabu ya bawasiri hutegemea na aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwa sababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa na anion chip kubandika mahali penye tatizo na kuondoa tatizo hilo.

Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia
 • Kula mbogamboga za majani, matunda na nafaka zisizokobolewa
 • Kunywa maji mengi angalau glasi 6 hadi 12 kwa siku
 • Epuka kukaa chooni kwa muda mrefu
MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI
 • kupata upungufu wa damu (anemia) 
 • Kupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo 
 • hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake 
 • kuathirika kisaikolojia 
 • kukosa moral ya kufanya Kaz kutokana na maumivu makali 
Wasiliana nasi kwa namba 0717035770 AU 0753692612.
Makala hii ya afya imeletwa kwako na JamiiMoja BLOG

Utitiri wa watu katika mkutano wa CUF Micheweni
Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia katika mkutano wa hadhara wa Chama hicho uliofanyika viwanja vya skuli ya Micheweni.


Wafuasi na wapenzi wa CUF wakimsikiliza mgombea Urais wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif katika viwanja vya skuli ya Micheweni.