Mchungaji Mtikila afariki ajalini

Gari alimopata ajali Mch. Mtikila
Mwenyekiti wa chama cha siasa (Democratic Party - DP) nchini Tanzania, Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia alfajiri ya leo katika ajali ya gari iliyotokea kwenye kijiji cha Msolwa, Chalinze mkoani Pwani, alipokuwa safarini akitokea kwake mkoani Njombe.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Jafari Ibrahim amethibitisha hilo na kusema watu wengine watatu waliokuwa katika gari hilo wamekimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.


Mtikila alizaliwa Ludewa Mkoani Njombe, huko kusini mwa Tanzania, mwaka 1950. Pamoja na shughuli za siasa, Mchungaji Mtikila ni mwanzilishi na mkuu wa kanisa la Kipentekoste la Full Salvation Church.

Mchungaji Mtikila amekuwa pia alijihusisha na harakati za haki za binadamu kwa kupitia kitengo cha haki za binadamu cha kanisa hilo kiitwacho Liberty Desk.

Mwanzoni mwa miaka ya 90, mchungaji Mtikila alijipatia umaarufu mkubwa katika siasa za Tanzania kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuongea, upinzani wake dhidi ya muundo wa muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, madai yake kuhusu uhujumu wa uchumi unaofanywa na wahindi (ambao anawaita Magabacholi), na kesi mbalimbali za kikatiba alizokuwa akifungua katika mahakama za Tanzania.

Kwa muda mrefu chama chake cha DP hakikuweza kupata usajili wa kudumu kutokana na kukataa kwake kutambua Zanzibar.

Alikuwa akisisitiza kuwa chama chake ni cha Tanganyika na sio Tanzania. Hata hivyo Mtikila alibadili msimamo wake katika miaka ya karibuni kwa kukubali kutafuta wanachama toka Zanzibar (kama sheria ya uchaguzi inavyotaka) na hivyo chama chake kuweza kupata usajili wa kudumu.

Mwaka 1997, Mbunge wa Ludewa kwa tiketi ya CCM wakati huo, Horace Kolimba aliitwa na Kamati Kuu ya chama chake mjini Dodoma kwenda kujibu mashtaka ya ndani ya chama juu ya kauli ambazo alikuwa akizitoa kwamba “CCM imepoteza mwelekeo”, baadhi ya viongozi wa chama chake walimchukulia kama msaliti na wengine wakimuona kama mtu aliyethubutu kusema ukweli bila kumhofia Nyerere. Hata hivyo, Kolimba alifariki hukohuko Dodoma katika siku ambazo alikuwa akihojiwa.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ilipotangaza uchaguzi mdogo, ndipo Mtikila alikihama chama chake cha DP akajiunga na Chadema na kuomba ridhaa ya kugombea. Mtikila ni mzaliwa wa Ludewa na alifanya hivyo kwa sababu chama chake cha DP kilikuwa kimenyimwa usajili.

Uchaguzi ulifanyika Mei 25, 1997 na kumpa ushindi mgombea wa CCM Profesa Chrispin Haule Che Mponda ambaye alipata kura 20,111 dhidi ya 8,386 za Mtikila. Mgombea wa NCCR ambayo haikuwa imejijenga vilivyo Ludewa, Barnabas Kidulile, alipata kura 1,271.

Baada ya kushindwa uchaguzi huo, Mtikila alisikika akihitilafiana na Chadema hadharani huku akitoa shutuma nzitonzito, akafukuzwa kwenye chama hicho na ndipo akaendelea kuwekeza nguvu kwenye mipango ya kukamilisha usajili wa chama chake.

Mbio za urais

Mtikila alianza harakati za kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2005 kwa tiketi ya DP. Alikuwa kati ya wagombea 10 katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huo. Katika uchaguzi huo, alipata asilimia 0.27 ya kura zote, akiwa nyuma ya Jakaya Kikwete wa CCM (asilimia 80.28), Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF (asilimia 11.68), Freeman Mbowe wa Chadema (asilimia 5.88), Augustine Mrema wa TLP (asilimia 0.75) na Dk Sengondo Mvungi wa NCCR (asilimia 0.49).

Katika Uchaguzi Mkuu unaotaraji kufanyika Oktoba 25 mwaka huu Mtikila kupitia DP, alichukua fomu lakini alishindwa kutimiza masharti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na jinalake kuondolewa katika orodha ya wagombea Urais.

Kesi za kikatiba ambazo amewahi kufungua ni pamoja kesi ya kutaka wagombea binafsi kuruhusiwa katika uchaguzi Tanzania, wananchi wa Tanzania Bara kuruhusiwa kwenda Zanzibar bila pasipoti, na vyama vya siasa kuruhusiwa kufanya mikutano bila kuomba kibali toka kwa Mkuu wa Wilaya na Polisi.

Mtikila alifungwa kwa mwaka mmoja mwaka 1999 baada ya kupatikana na hatia ya kutoa maneno ya kashfa dhidi ya aliyekuwa katibu mkuu wa CCM, marehemu Horace Kolimba.

Mwaka 2004 alihukumiwa kifungo kilichosimamishwa cha miezi sita kwa kutoa maneno ya kashfa dhidi ya mkuu wa polisi wa wilaya ya Ilala.

Mchungaji Christopher Mtikila, mwaka huu mwezi March alifungua kesi ya kikatiba namba 14 ya mwaka 2015 katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga muswada wa mabadiliko ya sheria kwa ajili ya kuitambua rasmi Mahakama ya Kadhi.

[video] Mitambo, Mabingwa: Ndani ya Taasisi ya moyo ya Jakaya kikwete


Lowassa afika Pemba, ahutubia!Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mumungano wa Tanzania kupitia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) Mh. Edward Ngoyayi Lowassa amewataka wananchi kisiwani Pemba kumkataa na kutomchagua mgombea yeyote anayechezea amani ya nchi kwani nchi hii si miliki ya mtu bali ni mali ya watanzania wote, na kusisitiza kuwa endapo atachaguliwa atahakikisha anapambana na umasikini kwa nyanja zote.

Magufuli afika Sindiga, ahutubia!Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Peoples, mjini Singida, ambapo alilisitiza kwamba akishinda urais ataongeza ajira kwa vijana kwa kuwapa mikopo ya mitaji ya kuanzishia miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi.

View from inside and out of a cruise ship hit by storm


The impact of massive waves that struck a cruise ship during a storm off New Zealand revealed by CCTV footage posted on the internet.

Pacific Sun Cruise liner, carrying 1732 passengers and 671 crew, was caught in a severe storm on July 30, 2008, encountering seven-metre swells and 50 knot winds.


Utetezi na malalamiko ya Mbeya City kuhusu adhabu ya TFF kwa Juma Said "Nyosso"


Bodi ya klabu ya Mbeya City ilikutana tarehe 29.09.2015 kwa dharula kulijadili suala ambalo hivi sasa linaendelea kujadiliwa katika Umma wa wanamichezo nchini likimuhusisha mchezaji wa timu yetu Juma Said maarufu kama “Nyoso” baada ya mchezo kati ya timu yetu na Azam FC uliochezwa tarehe 27.9.2015 katika uwanja wa chamazi.
Katika kikao hicho yafuatayo yaliamuliwa:
  1. Klabu iliunda kikosi kazi kuliangalia suala zima na kikosi kazi hicho kilipewa masaa 86 na kilifanya kazi kwa adidu za rejea zifuatazo:
(a) Kupitia rejea za mchezo husika na kuangalia Mazingira na Asili ya suala zima lililojitokeza.
(b) Kupata Maelezo ya awali ya mchezaji wetu juu ya suala lenyewe.
(c) Kufanya uchambuzi wa kisayansi wa mzizi wa suala analohusishwa mchezaji kwa kushirikisha watalaam wa Ushauri Nasihi na Saikolojia kisha kuishauri Bodi.
Wakati kazi hiyo ikiendelea, Klabu ilipokea nakala ya barua ya adhabu ya mchezaji wetu Juma Said maarufu kama “Nyoso” yenye Kumb:TPLB/VPL/766/15 ya tarehe 30.09.2015.
Kwa Mukhtasari ifuatayo ni taarifa ya klabu baada ya kikosi kazi hicho kuwasilisha taarifa yake.
Klabu inapenda umma wa wanamichezo nchini ukajua kuwa inasononeka sana na matukio yoyote yenye kuupunguzia ladha mchezo wa mpira wa miguu kunakofanywa na mdau yoyote wa mchezo huo.
Mara zote klabu imekuwa ikisisitiza na kusimamia nidhamu ya wachezaji na viongozi muda wote wanapotekeleza majukumu yao.
Katika mchezo wetu wa ligi kuu namba 32 uliochezwa katika uwanja wa Chamazi tarehe 27.09.2015 inadaiwa mchezaji wetu tajwa hapo juu alifanya kitendo cha udhalilishaji dhidi ya mchezaji wa Azam Fc John Bocco.
Tarehe 29.09.2015 kamati ya masaa 72 inayoisimamia shughuli za bodi ya ligi ilikutana na kutoa uamuzi wa kumfungia mchezaji Juma Saidi Nyoso kutocheza mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi milioni mbili kwa kufuata kanuni namba 37(24) za ligi kuu toleo la 2015(Kwa mujibu wa barua TPLB/VPL/766/15 ya tarehe 30.09.2015).
Ufuatao ni uchambuzi wa adhabu iliyotolewa
  1. (a) Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa bodi ya ligi ( Masaa sabini mbili) pamoja na mambo mengine inashughulikia kufanya maamuzi kwa masuala yote ambayo maamuzi yake hayakatiwi rufaa kama yalivyoainishwa katika kanuni namba 74 ya ligi kuu. Kanuni iliyotumika kutoa adhabu 37(24) si miongoni mwa kanuni ambazo hazikatiwi rufaa ni kanuni inayopaswa kutumika na kamati ya Maadili au Nidhamu ambayo kulingana na aina ya kosa linahitaji kuthibitishwa pasipo shaka na pande zote zinazohusika.
(b) Hata kama kanuni waliyoitumia ingekuwa ni sahihi lakini tafsiri ya kanuni hasa maneno AU, NA hayakutumika ipasavyo kwa kuwa walikuwa na uchaguzi wa adhabu lakini adhabu hizo haziendi pamoja kama kamati ilivyo tafsiri. Adhabu imeangalia upande mmoja wa hisia , hivyo kutoa adhabu kubwa bila kuangalia upande wa mchezaji husika. Pia Kamati imeunganisha adhabu zote kwa pamoja wakati kanuni inatoa nafasi ya adhabu moja kwa wakati mmoja.
“37(24) Mchezaji yeyote atakayepatikana na hatia ya kufanya makosa makubwa ya kimaadili au kinidhamu, au ya kibaguzi au yakidhalilishaji au yatakayotafsiriwa kuwa ni ukiukaji mkubwa wa taratibu za mchezo na ubinaadamu atatozwa faini kati ya shilingi milioni moja mpaka milioni tatu au/na kusimamishwa kushiriki michezo mitatu mpaka kumi ya klabu yake yoyote atakayoitumikia katika Ligi Kuu na mashindano mengine rasmi ya TFF au kufungiwa kipindi cha kati ya mwaka mmoja na miwili.”
  1. (a) Klabu inapata shaka juu ya maamuzi ya kamati husika kutokana na kikao kilichotoa maamuzi kiliongozwa na Mwenyekiti wa kamati hii ni Ndugu Said Mohamed ambaye pia ni Mwenyekiti wa Azam Fc. Sisi tuna amini kwamba kwa kuwa yeye ni kiongozi wa Timu ya Azam aliwajibika kujitoa kusikiliza shauri.Lakini hakujitoa na aliendelea kuongoza kikao hicho huku akijua kwamba yeye ni mjumbe mwenye maslahi na upande mmoja (AZAM FC).
(b) Mchezaji anayetuhumiwa (Juma Said Nyoso) hakupewa nafasi ya kusikilizwa na kamati kama misingi ya utendaji haki inavyohitaji (Principle of natural justice), Klabu inaona mchakato mzima wa usikilizaji wa shauri hili umeingia dosari hivyo maamuzi na adhabu iliyotolewa inakosa sifa kisheria.
3 Mazingira ya tukio lenyewe:
(a) Klabu inatilia shaka ushahidi uliotumika na kutafsiriwa na kamati kufanya uamuzi uliotolewa,kuna uwezekano mkubwa kuwa kamati iliangalia picha ya mnato(Still Picture)iliyosambaa punde baada ya mchezo huo na kuzua mjadala miongoni mwa jamii bila kuangalia mazingira mengine ya tukio hilo.
(b) Katika kipande cha picha mwendo(Video) kinachoonesha chanzo cha tukio hilo ni baada ya mchezaji wa Azam FC mwenye jezi namba 20 iliyoandikwa Mudathir kumfanyia madhambi mchezaji wa Mbeya City mwenye jezi namba 10,hii ilikuwa faulo yake ya tatu kwa mchezaji huyohuyo bila kuonywa na mwamuzi,Juma Said Nyoso akiwa kiongozi wa wachezaji wa Mbeya City alimfuata Mwamuzi wa mchezo huo kumueleza kuwa Mudathir amekuwa akimchezea sivyo mchezaji huyo bila kuonywa,ndipo John Bocco alipofika eneo ambalo alikuwepo Mwamuzi,Juma Said Nyoso na mchezaji Mwingine wa Mbeya City Fc aliyevaa jezi namba 15 (Christian Sembuli),John Bocco alimpiga kibao usoni Christian Sembuli(Jezi 15) mbele ya muamuzi, wakati John Bocco akifanya hivyo Mudathir(Jezi 20)alizunguka mgongoni kwa John Bocco na kumvuta sehemu za siri(korodani) za Juma Said Nyoso na akarudi upande wa kulia kwa mwamuzi, wakati Mudathir (20) akifanya hivyo John Bocco alimkanyaga na kumpiga teke Juma Said Nyoso.
Klabu inaamini wanaopaswa kuathibiwa ni wachezaji wa AZam Fc John Bocco na Mudathir(20) waliotengeneza mazingira ya kuharibu taswira ya mchezo wa mpira wa miguu mbele ya macho ya watu waungwana.
Mapungufu ya Jumla ya adhabu iliyotolewa:
  1. Kamati badala ya kutumia Kanuni ya 37.7(F) ambayo haikatiwi Rufaa wakaitumia Kanuni ya 37(24) ambayo inakatiwa Rufaa.
  2. Kamati hawakumpa nafasi ya kujitetea mchezaji husika kwa mujibu wa kanuni ya 37(24).
  3. Mwenyekiti wa kamati hii ni Ndugu Said Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa Azam Fc hakusitahili kuongoza wala kuwemo katika kikao hicho kwa kuwa alikuwa na maslahi na timu ya Azam Fc ambao ndio walio mlalamikia mchezaji Juma Said Nyoso.
Umma wa wanamichezo ujifunze nini kutokana na suala hili?
  1. Mamlaka zinazosimamia mchezo wa mpira wa miguu ni vizuri sasa kutafsiri kwa upana dhana ya “udhalilishaji” katika mpira wa miguu.
Hii inatokana na namna ambavyo suala hili limeripotiwa na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu na wanaharakati,picha za tukio hilo zilisambaa kila uchao.
Klabu inaamini kwa namna wadau walivyolijadili na kulichambua suala hili,lilimdhalilisha zaidi muhusika,kuwekwe utaratibu na chombo ambacho kipewe jukumu la kupitia mashauri na ushahidi wa matukio yanayotafsiriwa kuwa ni ya “udhalilishaji” ili kuendelea kulinda heshima za wahusika katika jamii.
Klabu imewasilisha Tff maelezo ya kutoridhishwa na adhabu aliyopewa Juma Said Nyoso.
Imetolewa na
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC
2/10/2015

Serikali yalaani maoni ya Mhariri wa gazeti Mwananchi

Oktoba 3, 2015 MWANANCHI: Serikali imelaani maoni ya Mhariri wa Mwananchi katika toleo la juzi ikidai yalikuwa na lengo la kupotosha mafanikio ya Rais Jakaya Kikwete na haiba ya Tanzania mbele ya Jumuiya ya Kimataifa.

Madai hayo yalitolewa jana kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assah Mwambene, wakati Mhariri Mtendaji wa Mwananchi akiwa ameomba radhi jana kwenye ukarasa wa tatu wa gazeti hili kuhusiana na maoni hayo yaliyokuwa na kichwa cha habari ‘Rushwa inazidi kutudhalilisha mbele ya dunia’. “Katika ukurasa wa 10 wa gazeti letu jana (juzi), Jumatano, tulikuwa na maoni yaliyokuwa yanasomeka; Rushwa inazidi kutudhalilisha mbele ya dunia.

“Hatukuwa na nia mbaya ya kuonyesha kuwa viongozi wetu wa Serikali walikwenda kuomba msaada Marekani, bali lengo letu lilikuwa ni kuonyesha kwamba Tanzania bila rushwa inawezekana. Tunaomba radhi kwa wote ambao walikwazika na maoni hayo.”

Hata hivyo, licha ya Mwananchi kuonyesha msimamo wake huo, bado Mwambene aliendelea kulilaani akisema maoni hayo yalikuwa na makosa ya uhalisia na kujaa upotoshwaji.

“Kwa lugha ya kawaida tunasema tahariri hiyo imeongea uongo wa wazi, inao ukweli wa nusu na imejaa upotoshwaji ambao tunaamini umefanywa kwa makusudi ili kutia doa mafanikio ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete na haiba ya Tanzania mbele ya Jumuiya ya Kimataifa,” alisema.

Mwambene alisema maoni hayo yanaonyesha ni jinsi gani Mwananchi limejipambanua kuwa halifurahii mafanikio ya Tanzania.

Alisema Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Milenia (MMC) haikuwa imezuia kutoa msaada wa dola 472 milioni za Marekani na kwamba kwenye kikao chake cha Septemba iliipongeza Serikali kwa kufanya vizuri katika vigezo vyote vinavyostahili kupata misaada kupitia MMC.

Alisema isipokuwa MCC walitoa tahadhari kuwa iwapo tathimini ya kupiga vita rushwa itaonyesha Tanzania imeshuka zaidi katika kigezo hicho msaada kwake utaahirishwa.

“Ukweli Bodi ya MCC haikuwa imefanya maamuzi kuhusu kutoa misaada bali ilikuwa imetoa angalizo,” alisema Mwambene.

Alisema Rais Kikwete hakukutana na kiongozi wa MCC nchini Marekani kwa lengo la kumbembeleza aionee Tanzania huruma na kuipatia misaada kama ilivyodaiwa.

Alifafanua kuwa kiongozi huyo aliomba ahadi ya kukutana na Kikwete na kumueleza MCC haina kikwazo kwa Tanzania kupata msaada huo baada ya kufanya vizuri katika kigezo cha kupambana na rushwa.

Hata hivyo alisema tathimini ya upigaji vita rushwa haifanywi na MCC, bali huomba kazi hiyo ifanywe na Benki ya Dunia (WB) na taasisi nyingine duniani. “Hivyo kama ni kubembeleza Rais angeenda Benki ya Dunia,” alisema Mwambene.


MAONI YALIYOLAANIWA

Septemba 30, 2015, MWANANCHI: Hatua iliyokuwa imechukuliwa hivi karibuni na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Milenia (MCC) ya Marekani kuzuia msaada wa Dola 472 milioni kwa Tanzania kwa maelezo kwamba nchi yetu imeshindwa kuchukua hatua za kuridhisha kupambana na rushwa, bila shaka itakuwa iliwasononesha na kuwaghadhibisha wananchi wengi kutokana na aibu ya Tanzania kuonekana mbele ya jumuiya ya kimataifa kama moja ya nchi vinara wa rushwa duniani.

Itakumbukwa kwamba wiki mbili zilizopita, Ubalozi wa Marekani nchini ulitoa taarifa kwa vyombo vya habari kwamba bodi hiyo ya MCC ilionyesha wasiwasi juu ya mwenendo wa mapambano ya Serikali ya Tanzania dhidi ya rushwa, hivyo kuzuia kutolewa kwa fedha hizo hadi itakapofuzu kigezo cha udhibiti wa rushwa katika tathmini ya shirika hilo iliyopangwa kufanyika mwaka ujao.

Kama tulivyosema hapo juu, uamuzi huo wa MCC ulipokewa na wananchi wengi kwa masikitiko makubwa, siyo kwa sababu ya kukosa fedha hizo, bali kutokana na ukweli kwamba nchi yetu iliyokuwa ikiheshimika na kusifika duniani kote kama ya mfano, sasa imo katika kundi la mataifa yanayotajwa kwa rushwa.

Hata hivyo, katika hali nyingine, siku 10 baada ya taarifa hiyo ya Ubalozi wa Marekani, Serikali ilitoa taarifa kwamba Bodi ya MCC imeridhia kuipatia Tanzania msaada huo uliokuwa umezuiliwa na kwamba fedha hizo zitaanza kutolewa mapema mwakani. Taarifa hiyo ilisema kwamba hatua hiyo ilifikiwa wiki iliyopita baada ya Rais Jakaya Kikwete kukutana na viongozi waandamizi wa MCC jijini New York, akiwamo Ofisa Mtendaji Mkuu wa MCC, Dana Hyde na kuelezwa kwamba Tanzania imetimiza masharti ya kupata fedha hizo, kikiwamo kigezo cha kukabiliana na rushwa kilichokuwa kikwazo hapo awali.

Sisi tunasema kama Bodi ya MCC imechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha pasipo kuacha shaka kuhusu dhamira ya Serikali ya Tanzania kupambana na rushwa, hakika inastahili pongezi.

Bodi hiyo ya MCC itakuwa imetambua kwamba fedha inazotoa kama msaada kuendesha miradi ya maendeleo kamwe haziwezi kufanya kazi iliyokusudiwa katika mazingira ya rushwa, ambayo vitendo hivyo vinafanywa kuwa utamaduni katika mifumo ya utendaji wa serikali na taasisi zake ndani ya nchi husika.

Hatua ya Bodi ya MCC ghafla kukubali kutoa msaada huo kwa Tanzania baada ya kuuzuia, bila shaka imeacha maswali mengi kwamba pengine haikuwa imefanya utafiti wa kutosha. Sisi hatuna nia ya kujadili suala hili kwa undani, isipokuwa kusema tu kwamba taarifa zilizotolewa na Serikali ya Tanzania na ubalozi wa Marekani hapa nchini hazijitoshelezi, kwani zinajenga picha kwamba pengine viongozi wetu waliomba kwa MCC na kufanikiwa kufikia makubaliano maalumu mjini New York, hivyo MCC ikakubali kutengua uamuzi wake wa awali. Hata hivyo, hatua hiyo itatoa ahueni kwa Serikali, kwani itatekeleza miradi mbalimbali kama usambazaji wa umeme wa gharama nafuu na uimarishaji wa taasisi zinazosimamia nishati hiyo.

Tunaishauri Serikali ijifunze kutokana na aibu tuliyoipata kutokana na sakata hilo. Jina na sifa ya Tanzania vinazidi kuporomoka mbele ya jumuiya ya kimataifa kutokana na madai ya rushwa. Serikali sasa idhamirie kwamba Tanzania bila rushwa inawezekana. Vinginevyo tutaendelea kudhalilika kama ilivyotokea katika sakata hili la MCC.

Mwl. Kissima - Elimu Inayozingatia Uwezo: Wapi tunakosea?


Picha kwa hisani ya gettingsmart

Elimu inayozingatia uwezo imeshika kasi zaidi kipindi cha hivi karibuni, hususani kwa mataifa ya Ulaya. Nchi kama Marekani imewekeza kiasi kikubwa cha fedha kuhakikisha elimu hii inatumiwa mashuleni na vyuoni ili kuleta ufanisi unaopaswa. Kwa mfano, blogu ya BlackBoardkwa kushirikiana na Baraza la Elimu la Marekani, tayari wameunganakufanya Tafiti za Elimu Inayozingatia Uwezo.

Utafiti wa hivi karibu wa BlackBoard na Baraza la Elimu la Marekani umejaribu kuangalia ni kwa kiasi gani Elimu Inayozingatia Uwezo inavyoweza kutekelezwa na pia manufaa yake kijamii na kisera na namna ambavyo mfumo wa krediti na uwezo unavyotafsiriwa na wadau mbalimbali wa elimu.

Kutokana na ukweli kwamba, kiwango cha elimu nchini Tanzania kwa kipindi kirefu kimekuwa kikidorora kadiri siku zilivyokuwa zinaenda, moja ya muarobaini ulionekana ni kuazima mfumo wa Elimu unaozingatia Uwezo. Hivyo basi, mwaka 2004, Tanzania kupitia Taasisi ya Elimu iliamua kubadili mitaala ya shule za msingi hadi vyuo vya ualimu ili iendane na matakwa ya aina hii ya elimu.

Mtaala uliokuwepo ulionekana umeshindwa kukidhi mahitaji ya sera na mikakati mbali mbali ya kielimu na ya kimaendeleo. Pia, tafiti mbalimbali zilzofanywa na wadau wa elimu ikiwa ni pamoja na Taasisi ya Elimu Tanzania zilionesha umuhimu wa kufanyika kwa mabadiliko ya mitaala ya shule za msingi, sekondari na vyuo vya Ualimu.

Kwa shule za msingi, mitaala inayozingatia ujifunzaji wa kuzingatia uwezo ilianza kutumiaka rasmi mwaka 2006, kwa shule za sekondari na vyuo vya ualimu, mtaala mpya ulianza kutumika rasmi mwaka 2005. Hakuna uhakika kama mabadiliko haya yalihusisha pia vyuo vikuu ambavyo huandaa walimu wa kusimamia utekelezaji wa mitaala mipya mashuleni inayohamashisha ufundishaji na ujifunzaji unaozingatia uwezo.

Hata hivyo, mara baada ya kufanyika mabadili haya ya mitaala, mafanikio katika elimu yameendelea kulegalega kwa kiasi kikubwa. Ni takribani miaka kumi ya utekelezaji wa mitaala inayozingatia Ujifunzaji unaozingatia uwezo. Tumezidi kushuhudia idadi kubwa ya wanafunzi wa shule za msingi wanaomaliza elimu ya msingi bila kujua kusoma, kuandika kuhesabu.

Utafitiwa Twaweza wa mwaka 2012 unaonesha kuwa nchini Tanzania, zaidi ya asilimia 55% ya wanafunzi wa darasa la tatu hawakuweza kusoma hadithi ya Kiswahili ya darasa la pili huku wanafunzi 8 kati ya 10 wa darasa la tatu wakishindwa kusoma hadithi ya kiingereza ya darasa la pili. Pia, utafiti huo unaonesha kuwa, wanafunzi 7 kati ya 10 wa darasa la tatu hawakuweza kufanya hesabu ya kuzidisha ya darasa la pili.

Elimu ya sekondari nchini Tanzania nayo imekuwa ikisuasua kila kukicha. Matokeo ya mitihani Taifa ya kidato cha nne ya mwaka 2012 ndiyo yaliyokuwa matokeo mabaya katika historia ya mitihani ya Taifa inayosimamiwa na baraza la mitihani la Tanzania ambapo zaidi ya asilimia 65% ya watahiniwa walifeli mtihani huo.

Kufuatia kusuasua huku wa elimu, watafiti na wadau mbali mbali wa elimu wamekuwa wakitafiti mfumo huu wa elimu elimu ili kubaini mafanikio, changamoto na kisha kutoa mapendekezo ya nini cha kufanya.

Tafiti nyingi zilizofanyika nchini Tanzania zinaonesha kuwa walimu hawana uelewa wa kutosha kuhusu ufundishaji na ujifunzaji unaozingatia uwezo. Kupitia tafiti hizi, imefahamika kuwa, walimu wengi wa shule za msingi na sekondari hawafahamu nini wanapaswa kutekeleza ili kuhakikisha wanafundisha kwa mujibu wa mitaala ya sasa. Hali kadhalika, tafiti zinaonesha kuwa waalimu wanafunzi wanaotarajiwa kwenda kufundisha mashuleni, hawana uelewa wa kutosha wa kuweza kufundisha kwa kuzingatia matakwa ya ufundishaji unaozingatia uwezo. Pia, hali isiyoridhisha ya mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji inaonekana kuwa ni moja ya mambo yanayopelekea elimu inayozingatia uwezo wa mwanafunzi kuonekana kushindwa.

Wakati tafiti nyingi zinazohusu ufundishaji na ujifunzaji unaozingatia uwezo zikiwa zimeelekezwa zaidi kwa walimu, tuna mswali kadhaa ya kujiuliza.

Kwanza, wahadhiri wa vyuo vikuu wanaufahamu vyema mfumo huu wa ufundishaji na ujifunzaji? Wanapofundisha walimu wanafunzi, fikra zao, ufundishaji wao na maono yao yanasimia kwenye mfumo huu? Vyuo Vikuu nchini Tanzania vinautumia mfumo huu kuwafundisha wanafunzi? Je, vyuo vikuu vinafahamu kwa upana wake misingi ya Elimu Inayozingatia uwezo na inaisimamia ipasavyo kwenye kutoa elimu? Pengine, maswali haya yanapaswa kujibiwa kupitia tafiti.

Hata hivyo, kuna ukweli kuwa, vyuo vikuu vingi vinatumia zaidi njia ya mihadhara kwenye ufundishaji. Labda wingi wa wanafunzi katika darasa moja inaweza kuwa ni moja ya sababu. Swali la kujiuliza ni kama, ufundishaji wa kuzingatia uwezo unaathiriwa na wingi wa wanafunzi darasani. Kujibu swali hili, ni vizuri kwanza tukaifahamu kwanza Elimu inayozingatia ujuzi pamoja na misingi yake. 

Tukutane katika makala ijayo.

Albert Kissima

Tahadhari kwa watumia barabara ya Lua eneo la Njia Panda, Isanga


Kipande cha barabara ya njia Panda Isanga karibu na Hotel ya Lifti Valey jijini Mbeya (LUPA WAY) ambacho kimejengwa upya kwa kuongezewa njia, kimeleta sura mpya jijini hapa lakini kimeleta pia changamoto kwa madereva hasa kwa nyakati za usiku kwani hakuna taa hivyo ni vyema watumiaji wa barabara hii wakajihadhari kwa kutoendesha kwa mwendo kasi ili kuepuka ajali zisizo za lazima.
  • Tumeshirikishwa tahadhari hii na JamiiMoja blog