NEC yazungumzia malalamiko kuwa kuna vyama vimepitiliza gharamza za kampeni


Haya! Mgombea Ubunge ACT-Wazalendo amwombea kura Lowassa

Mgombea ubunge wa ACT - Wazalendo kwa Jimbo la Arusha Mjini, Estomih Malla jana baada ya kupanda jukwaani alimwombea kura za ndiyo mgombea urais Tanzania kupitia CHADEMA, Edward Lowassa.

Akihutubia mkutano wa kampeni uliokuwa na lengo la kunadi pia sera na kumwombea kura mgombea wa chama chake, Bi. Anna Mnghwira, katika Uwanja wa Stendi Kubwa, mkoani Arusha alisema:
“Jamani naombeni mtambue kuwa mimi ni msomi ambaye nina shahada (Hakuitaja ni ya nini), kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikitumia elimu yangu kwa faida ya familia yangu tu baada ya kufukuzwa udiwani na Chadema, sasa naombeni mnichague ili niitumie pia kuwatumikia kwa kuwaletea maendeleo yaliyoshindikana kupatikana kwa miaka mitano,”  “Mimi ni mkweli, nipeni ridhaa ya kuwaongoza na msisahau kumpa ridhaa ya kuwa rais mheshimiwa Edward Lowassa, naamini hamtajutia kura zenu,” alisema Malla.
Alipoulizwa baada ya kumaliza mkutano wake kwa nini amemnadi Lowassa badala ya mgombea urais wa chama chake, Malla hakutaka kujibu bali alipanda gari lake na kuondoka.
 • Habari hii imenukuliwa kutoka kwenye gazeti MWANANCHI

Facebook and EU satellite operator team up to deliver broadband to Africa


European satellite operator Eutelsat Communications and social media giant Facebook said today (5 October) they are working jointly to deliver satellite broadband Internet to connectivity-hungry sub-Saharan Africa.

The firms revealed they have reached a multi-year agreement with satellite communication firm Spacecom to use the entire broadband payload of the AMOS-6 satellite due to come on stream in the second half of next year and provide coverage for large swathes of sub-Saharan Africa, after identifying "pent-up demand for connectivity".

Eutelsat said in a statement the project would offer access "using affordable, off-the-shelf" hardware, sharing capacity with Facebook in regions often lacking access to reliable fixed and mobile terrestrial networks.

"Satellite networks are well suited to economically connecting people in low- to medium-density population areas," Eutelsat added.

The capacity will enable Eutelsat to step up its broadband activity in sub-Saharan Africa that was initiated using Ku-band satellites to serve professional users.

Eutelsat is establishing a new company based in London that will steer its African broadband vision and business. The company will be led by Laurent Grimaldi, founder and former CEO of Tiscali International Network, and will focus on serving premium consumer and professional segments.

Facebook two years ago launched Internet.org, an initiative to accelerate connectivity in poorly covered regions and unveiled plans to work with partners in Africa to improve both satellite and terrestrial capacity for rural areas.

"Facebook's mission is to connect the world, and we believe that satellites will play an important role in addressing the significant barriers that exist in connecting the people of Africa," Chris Daniels, Internet.org vice president, said in a statement.

"We are looking forward to partnering with Eutelsat on this project," Daniels added.

Eutelsat chairman and CEO Michel de Rosen said: "We are excited by this opportunity to accelerate the deployment of our broadband strategy and to partner with Facebook on a new initiative to provide Internet access services in Africa.

"Eutelsat's strong track record in operating High Throughput Satellite systems will ensure that we can deliver accessible and robust Internet solutions that get more users online and part of the Information Society."

Taarifa ya Wizara leo Oktoba 5, 2015 kuhusu Mahujaji

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa masikitiko makubwa imepokea jina la Bw. Khamis Juma Shamte hujaji kutoka Tanzania aliyefariki dunia kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015. Kifo cha Bw. Shamte kinafanya idadi ya vifo vya Watanzania kufuatia tukio hilo kufikia watu nane (8) hadi sasa.

Aidha, Wizara imepokea jina la Bi Hawa Amrani Khamis aliyekuwa amepotea tangu siku ya ajali hiyo ambaye amepatikana akiwa mzima na aliweza kuungana na Mahujaji wengine na kurejea nyumbani tarehe 02 Oktoba, 2015.

Vile vile orodha ya majina ya majeruhi wote wa ajali ambao bado wapo hospitali imetolewa. Hadi sasa kuna Mahujaji wanne (4) wa Tanzania ambao wanaendelea kupatiwa

matibabu katika hospitali mbalimbali za Saudi Arabia na hali zao zinaendelea vizuri. Mahujaji hao ni Bi. Hidaya Mchomvu, Bi. Mahjabin Taslim Khan na Bw. Ahmed Abdalla Jusab. Pia, kuna mgonjwa mmoja ambaye aliugua tangu alipowasili Madina akitokea nchini anayeitwa Mustafa Ali Mchira ambaye bado amelazwa katika Hospitali ya Ansari Madina katika chumba cha wagonjwa mahututi. Bw. Mchira hakujeruhiwa kwenye ajali ya mkanyagano.

Hadi kufikia tarehe 03 Oktoba, 2015, Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia kwa kushirikiana naTanzania Hajj Mission na Vikundi vilivyopoteza Mahujaji umefanikiwa kupata majina ya Watanzania 32 ambao bado hawajapatikana. Orodha ya Majina na Vikundi vyao ni kama ifuatavyo:-

KIKUNDI CHA KHIDMAT ISLAMIYA
 1. Abdul Iddi Hussein
 2. Awadh Saleh Magram
 3. Burhan Nzori Matata
 4. Yussuf Ismail Yussuf
 5. Saleh Mussa Said
 6. Adam Abdul Adam
 7. Archelous Anatory Rutayulungwa
 8. Farida Khatun Abdulghani
 9. Rashida Adam Abdul
 10. Hamida Ilyas Ibrahim
 11. Rehema Ausi Rubbaga
 12. Faiza Ahmed Omari
 13. Khadija Abdulkhalik Said
 14. Shabinamu Ismail Dinmohammed
 15. Salama Rajabu Mwamba
 16. Johari Mkesafiri Mwijage
KIKUNDI CHA TCDO
 1. Alwiya Sharrif Abdallah
 2. Hafsa Sharrif Saleh Abdallah
KIKUNDI CHA AHLU DAAWA
 1. Masoud Juma
 2. Issa Amiri Faki
 3. Juma Jecha Dabu
 4. Nassor Mohammed Hemed
 5. Mohammed Awadh Namongo
 6. Juma Yussuf Bajuka
 7. Said Habibu Ferej
 8. Khadija Hamad
 9. Rahma Salim
 10. Hadija Abdallah Sefu
 11. Farida Khamis
 12. Nuru Omar Karama
 13. Laila Manunga
 14. Saida Awadh
Zoezi la kuwatambua Mahujaji wa Tanzania ambao bado hawajaonekana linaendelea. Serikali ya Saudi Arabia imetoa picha nyingine zipatazo elfu moja (1,000) kwa ajili ya kuangalia Mahujaji waliofariki dunia katika ajali hiyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

05 Oktoba, 2015

Mabadiliko ya Ratiba ya Mikutano ya Kampeni za Uchaguzi wa Rais 2015

Kuhusu taarifa za kufariki dunia kwa Waziri mwingine

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali inapenda kukanusha taarifa kutoka Kwenye baadhi ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Viwanda na Biashara amefariki dunia nchini India alikokuwa anatibiwa.

Taarifa Rasmi ya serikali kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata Chembe ya ukweli. Mhe. Dkt. Kigoda bado yupo nchini India Katika Hospitali ya Apollo katika Jiji la New Delhi anakoendelea kupatiwa matibabu.

Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015 na tangu kipindi hicho amend eleza kupata matibabu katika hospitali Hiyo ya Apollo.

Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari nu Mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa serikali.

Imetolewa na Assah Mwambene,
Msemaji Mkuu wa serikaliAnaomba msaada wa kufahamu chuo kinachotoa masomo jioni

Update/Taarifa mpya: Erine, unashauriwa na wadau hivi:

Mashine Mwalali: Just check Institute of Finance Management (IFM) -
Aliraza Bandali: Depending on type of course but TIOB, FTC and Learn IT.
---------

Nimechaguliwa kwenda kusoma Mzumbe mwaka 2014 - 2015 lakini kwa sababu nipo kazini, na napenda nipate chuo kitakachokuwa na masomo ya jioni, kwa mfano TIA.

Tafathali naomba msaada juu ya hili niweze kuanza shule mwaka huu.

Asante sana.

Erine

Majambazi sugu 6 wakamatwa na kukiri kumwua Polisi wa kikosi maalum, Pallangyo

JESHI la Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam limewakamata majambazi sugu sita waliohusika kumuua Afisa wa Polisi ASP Elibariki Pallangyo, aliyekuwa akifanya kazi katika kikosi maalum cha kupambana na majambazi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova ambapo alisema kuwa majambazi hao wanaongozwa na Omary Salehe maarufu kama Bonge Mzito walifanya tukio hilo Agosti 4 mwaka huu nyumbani kwa Marehemu huko Yombo.

Kova amewataja majambazi hao kuwa ni Omary Salehe (39), Saidi Saidi Mzee (37), Rashid Waston(21), Ramadhan Salum (38), Bakari Salim Rashid (38), na Hamisi Hamisi (24) ambao wote walikubali kuhusika katika mauwaji hayo kwa makusudi.

Amesema kuwa majambazi hao walienda kwa ASP Pallangyo na kumvamia usiku wa manane akiwa amelala na familia yake na kumuua mbele ya familia nzima ikishuhudia.

Anaongeza kuwa mtuhumiwa namba moja Bw Salehe alikutwa na bastola aina ya Revolver iliyofutwa namba na baada ya kuhojiwa alidai kuwa silaha hiyo ndiyo iliyotumika katika tukio hilo.

Kamishna Kova amesema mtuhumiwa huyo alijaribu kuwa toroka Polisi kwa kuwadanganya kuwa ameficha silaha nyingine mahali na kutaka kukimbia lakini polisi walimuwahi na kumpiga risasi iliyopelekea akutwe na umauti.

"Mtuhumiwa mwingine huyu Waston tumemkamata na silaha aina ya Shortgun iliyokatwa mtutu ambayo waliitengeneza kihenyeji ikiwa na risasi nne na betri nne zilizounganishwa kwaajili ya kulipua baruti,"amesema Kova

Katika tukio lingine Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wengine saba wa ujambazi wanaojihusisha na kuratibu matukio ya uvamizi wa vituo vya polisi pamoja na ugaidi ambao watano kati yao ni familia moja ya ukoo wa Ulatule.

Kamanda Kova amesema kuwa watuhumiwa hao wanahusika na matukio ya kupanga na kuratibu uvamizi wa vituo vya polisi ambapo pia wamekuwa wakiendesha kambi za mafunzo huko mkoani Morogoro kwa kutumia fedha walizokuwa wakijipatia kwa njia ya udanganyifu.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Siad Mohamed Ulatule (67),Ramadhan Ally Ngande(29),Hamis Mohamed Salum Simba Ulatule (51),Ally Mohamed Salum Simba Ulatule (65),Nassor Suleiman Ulatule (40), Seleman Abdallah Salum Ulatule (83) na Said Abdullah Chambeta (40).

"Jeshi la polisi limefanya operesheni hii kuhakikisha tunakomesha kabisa vitendo vya uvamizi wa vituo vya polisi pia tuna lengo la kuwaondolea wananchi hofu ya vitendo vya kigaidi nchini,"amesema Kova.
PRESS RELEASE 
05/10/2015
 • MAJAMBAZI SUGU SITA WALIOMMUA AFISA WA POLISI ASP ELIBARIKI PALLANGYO WAKAMATWA. WAPATIKANA NA SILAHA MBILI.
 • WATUHUMIWA WA UGAIDI WAZIDI KUKAMATWA KATIKA OPARESHENI KALI INAYOENDELEA. SABA WASHIKILIWA POLISI KANDA MAALUM. PIA ZIMEKAMATWA BUNDUKI NNE NA RISASI 18
Jeshi la Polisi kanda maalum ya dar es salaam wamefanikiwa kuwakamatwa majambazi sugu sita walioshiriki katika mauaji ya ASP Elibariki Palangyo huko nyumbani kwake Yombo Makangarawe tarehe 04.08.2015.

Waliokamatwa ni: 
1) OMARY [email protected] MZITO (39) MKazi wa Mtoni mtongani ambaye ni Kiongozi wa kundi hilo
2) SAIDI SAIDI MAZINGE (37) Mkazi wa Tegeta Kibaoni
3) [email protected] DODO(21) MKAZI WA Vingunguti
4)RAMADHANI [email protected] 38 mkazi MBAGALLA KIBURUGWA
5) BAKARI SALIM [email protected] MALENDA (38) Mkazi wa Mbagala kizuiani
6) HAMISI HAMISI @ FREEMASON 24 Mkazi wa Mbezi Mwisho

Afisa huyo wa ngazi ya juu katika jeshi la Polisi alikuwa anafanya kazi Mkoani Morogoro katika kikosi Maalum cha kupambana na majambazi aliyekuja nyumbani kwake Dar Es salaam. Alikuja DSM kwa ajili ya kusalimia familia na ndipo alipovamiwa na majambazi usiku wa manane wakati amelala na familia yake.

Aidha mtuhumiwa namba mmoja alikutwa na silaha bastola aina ya revolver iliyofutwa namba na baada ya mahojiano. aidha mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa ni marehemu kabla ya kufariki alijaribu kuwatoraka askari kwa kukimbia alijeruhiwa na hatimaye alifia njiani wakati akipelekwa hosptalini.

Pia inasemekana marehemu alipotezana na familia yake miaka mitani iliyopita akiwa kwenye harakati ya ujambazi. Pia bonge mzito alikuwa akitafatwa na Polisi kwa matukio mazito ya ujambazi wa kutumia silaha na mauaji ambaye pia amehusika katika mauaji ya afisa wa Polisi nyumbani kwake usiku wa manane na kumuua mbele ya familia yake ikishuhudia.

Pia mtuhumiwa RASHIDI [email protected] DODO alikamatwa maeneo ya Vingunguti tarehe 01.10.2015 akiwa na silaha aina ya Shortgun ilikatwa mtutu na kutengenezwa kienyeji ikiwa na risasi nne na betri mbili zilizounganishwa kwa ajili ya kulipua baruti.

Watuhumiwa wengine watano watapelekwa mahakamani baada ya kuperuzi na kukamilika kwa upelelezi wa shauri hilo.

WATUHUMIWA WA UJAMBAZI WANAOJIHUSISHA WANAOJIHUSISHA NA UGAIDI WAPATAO SABA WAKAMTWA, SITA KATI YAO NI WAFIMILIA MOJA 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na mikoa ya jirani pamoja na vyombo vingine vya dola limeendelea kufanya oparesheni ya kuwatafuta na kisha kuwakamata wale wote wanaojihusisha na matukio ya kupanga na kuvamia vituo vya Polisi, kuua askari/raia kisha kupora silaha jambo linaloashiria vitendo vya kigaidi.

Oparesheni hii ni kali na ya aina yake kwa madhumuni ya kukomesha kabisa vitendo vya uvamizi wa vituo vya Polisi na wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine lazima wakamatwe ili sheria uchukue mkondom wake. Oparesheni hii pia ina lengo la kuwaondolea hofu wananchi dhidi ya vitendo vya kigaidi nchini na kwamba wananchi waendelee kutoa taarifa juu ya watu kama hao ili nchi yetu iendelee kuwa na amani na utulivu. Majina ya watuhumiwa waliokamatwa ni kama ifuatavyo:

1. SIAD S/O MOHAMED ULATULE @ USO WA SIMBA, Miaka 67, Mkazi wa Mandimkongo, Mkuranga mkoa wa Pwani.
2. RAMADHANI S/O ALLY NGANDE, Miaka 29, Dereva wa Bodaboda, Mkazi wa Kongowe.
3. HAMIS S/O MOHAMED SALUM SIMBA ULATULE, Miaka 51, Mkulima, Mkazi wa Mamdimkongo, Mkuranga, Pwani.
4. ALLY S/O MOHAMED SALUM SIMBA ULATULE, Miaka 65, Mkulima, Mkazi wa Mamdimkongo, MKuranga, Pwani.
5. NASSORO S/O SELEMAN ULATULE, Miaka 40, Mkulima, Mkazi wa Mamdimkongo, Mkuranga, Pwani.
6. SELEMAN S/O ABDALLAH SALUM ULATULE, Miaka 83, Mkulima, Mkazi wa Mamdimkongo, MKuranga, Pwani.
7. SAID S/O ABDULLAH CHAMBETA @ Mzee wa Fasta, Miaka 40, Mfanyabiashara wa Mitumba, Mkazi wa Yombo Makangarawe. Mtuhumiwa namba 1,3,4 na 5 ni wa familia moja inayojihusisha na vitendo vya ujambazi pamoja na vya kigaidi.

Tunawashukuru sana watanzania wazalendo na wenye mapenzi mema na nchi yao kwa kutoa ushirikiano wa hali na mali ambao umesaidia kupata mafanikio yote haya. Tunawaomba waendelee kulisaidia Jeshi la Polisi kwa kuendelea kutoa taarifa ili oparesheni hii iwe yenye ufanisi zaidi.

KUKAMATWA KWA BUNDUKI SMG MOJA NA SHORTGUN MBILI, BASTOLA MOJA PAMOJA NA RISASI 14
 
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa MUSSA S/O MALAKI AKUTI, Miaka 30, fundi wa magari, Mkazi wa Mbagala Charambe kwa kukutwa na bunduki aina ya “Chinese 56 SMG” yenye namba 563845189 ikiwa na magazine moja na risasi 14. Mtuhumiwa huyu alikamatwa tarehe 28/09/2015 maeneo ya Mbagala Sabasaba, Temeke jijini Dar es Salaam baada ya Polisi kupokea taarifa kutoka kwa raia wema.

Bunduki hiyo ambayo aliiweka chini ya kiti cha pikipiki aina ya BOXER yenye namba T269 AUX inayosemekana kutumika katika matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Upelelezi unaendelea ili kuwakamata watuhumiwa wengine ili sheria iweze kuchukua mkondo wake kutokana na tuhuma zinazowakabili.

Katika muendelezo wa kuwasaka washirika wa MUSSA MALAKI, alikamatwa mtu mmoja kwa jina la AMON @ MTU MFUPI na simu yake ilianza kufuatilia ndipo wenzake walimpigia simu wakimtaka wakutane maeneo ya Tabata ili wakapore fedha kule Sinza Bigbon.

Askari walienda na mtuhumiwa maeneo ya Tabata na kuanza kuwafuatilia hao majambazi. Majambazi waliposhtukia mtego huo walianza kurushiana risasi ndipo jambazi mmoja alipigwa risasi na kufariki palepale. Alipopekuliwa alikutwa na Bastola aina ya FATIN-43 yenye nambari T0620-10J00413.

Ufuatiliaji uliendelea ndipo alipokamatwa JOSEPH S/O WAMBURA aliyekuwa akimfuatilia mteja aliyekuwa anachukua fedha benki. JOSEPH ALipopekuliwa alikutwa na karatasi ya kuchukulia fedha benki (pay-in-slip). Mtuhumiwa alikiri kuwa hiyo mbinu wameitumia kwa muda mrefu kumbe dhumuni ni kuwaangalia watu wanaochukua fedha nyingi benki kisha yeye huwasiliana na wenzake ili wawapore fedha.

Wakati huo huo, imekamatwa bunduki nyingine aina ya SHOTGUN/GOBOLE baada ya mtu mmoja aliyekuwa anafuatiliwa na polisi kushtukia mtego na kutupa fuko la kiroba alilokuwa kisha kutokomea kusikojulikana. Lilipopekuliwa fuko hilo ilikutwa bunduki hiyo inayoonekana ilifukiwa ardhini.

Bunduki hii ilikamatwa tarehe 28/09/2015 huko kijiji cha MKULIWINI, Kata ya Bupu Mkoani Pwani baada ya polisi kupata taarifa na kuweka mtego wa kumkamata mtuhumiwa. Bado msako wa kumtafuta unaendelea ili kubaini wapi alikuwa anaipeleka silaha hiyo na kwa dhamira gani.

Aidha, katika msako wa kuwakamata majambazi wa kutumia silaha mnamo tarehe 30/09/2015 huko Vingunguti nyumbani kwa mtuhumiwa JUMA S/O MALIMBIKA ilikamatwa silaha aina ya SHOTGUN iliyotengenezwa kienyeji (GOBORE) inayotumia risasi za shotgun. Taarifa za awali zinaonyesha kuwa bunduki ilipelekwa hapo na mtuhumiwa aitwaye RASHID S/O WATSON, Miaka 28, Mkazi wa Vingunguti ambaye amekamatwa kwa mahojiano zaidi ili kuubaini mtandao wa majambazi hao kwa lengo moja tu la kuusambaratisha.

POLISI YAOKOA MALI ILIYOIBIWA YENYE THAMANI YA TSHS 159,000,000/=

Mnamo tarehe 16.06.2015 majira ya saa 02:00 usiku, huko barabara ya Nyerere Jeshi la polisi kanda maalum Dsm lilipokea taarifa toka kwa ndugu FORD s/o MUSHI (40) mkazi wa Sinza aligundua kuvunjiwa ghala analotumia kuhifadhia bidhaa mbalimbali za dukani zikiwemo Fridge piece 133, Home Theatre idadi 582, kabati za nguo 17, bidhaa zote zenye thamani ya Tsh 159,680,000/=

Aidha Polisi kwa ushirikiano na taarifa mbalimbali za kiintelijensia walifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja anayefahamika kwa jina la ABAS s/o RAMADHANI(31) mfanyabiashara mkazi wa Kiwalani (w)Temeke.

Baada ya mahojiano mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio hilo na baada ya upekuzi alikamatwa na bidhaa zote zilizoibiwa pia aliwataja watuhumiwa wengine alioshirikiana nao ambao ni ALLY s/o SELEMANI SALIMU(37) mfanyabiashara mkazi wa Yombo(w)Temeke ambaye naye alikiri na kueleza kuwa baada ya kuvunja ghala hilo bidhaa zote walienda kuhifadhi kwa mtu aitwaye RICHARD S/o MARIDADI maarufu kwa jina la MUDY MKINGA (34) mkazi wa Chamazi alipopekuliwa tarehe 01/10/2015 saa 06:45 aubuhi katika nyumba ya kulala wageni itwayo MBILWA GUEST iliyoko Bugurunini Malapa ambapo vipo vyumba anavyovitumia kama ghala ndipo bidhaa zote zilizoibiwa zilipatikana pale. Watuhumiwa wote wanahojiwa na watapelekwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

MAKOSA YA USALAMA BARABARANI

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani kimeendesha oparesheni maalum kuaznia tarehe 15/09/2015 hadi 04/10/2015 ya kuzuia, kukamata na hatimaye kuwachukulia hatua madereva wazembe wanaendesha vyombo vya moto hivyo kukiuka sheria za usalama barabarani.

Makosa mbalimbali yalifuatiliwa ikiwa ni pamoja na ubovu wa magari, kuzidisha abiria, kukatisha route, uendeshaji wa hatari, matumizi mabaya ya barabara, kutokuwa na leseni, pamoja na makosa mengineyo. Katika makosa hayo, madereva mbalimbali walionywa, na wengine walitozwa tozo kulingana na utaratibu wa kisheria na makosa yao.

Kutokana na tozo zilizotozwa zimekusanywa jumla ya fedha za kitanzania shilingi MILIONI MIA TANO TISINI NA MOJA, MIA SABA SABINI ELFU TU (TShs. 843,260,000/=).

Lengo la oparesheni hii ya kikosi cha usalama barabarani si kukusanya fedha bali ni kuwakumbusha madereva wote wanaotumia barabara kutii sheria za usalama barabarani bila shuruti. Tinawahimiza watumiaji wote wa barabara kuzingatia hili kwa vitendo.

S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.

Kitabu (eBook) kipya kuhusu Uchaguzi Mkuu


Kitabu hiki kinahusu Uchaguzi Mkuu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, utakaofanyika Oktoba 25, 2015. Kinachambua chaguzi kuu zilizopita, na mazingira ya sasa ambapo uchaguzi huu unafanyika.

Kadhalika, kitabu hiki kinachambua michakato ya kambi kuu mbili katika kupata wagombea wake wa urais. Kambi hizo ni Chama tawala CCM na UKAWA, na wagombea wao Dkt John Magufuli (CCM) na Edward Lowassa (UKAWA).

Katika uchambuzi huo, kitabu kinaangalia nafasi na vikwazo kwa kila kambi na mgombea wake. Lengo kuu la kitabu hiki ni kuwapa Watanzania uelewa wa kutosha kuhusu zoezi zima la Uchaguzi Mkuu, sambamba na kuzielewa kambi hizo kuu na wagombea wake, ikitarajiwa kuwa itawasaidia kufanya maamuzi sahihi siku ya kupiga kura.

Link ya kitabu katika formats nyingine za kusoma kwenye simu au tablet ni hii http://kbuuk.com/kb/book/4993/uchaguzi-mkuu-tanzania-2015-.shtml

Ajali na kifo cha Mch. Mtikila: Taarifa ya Polisi

TAARIFA YA POLISI KUHUSU KIFO CHA MCHUNGAJI MTIKILA

Mnamo tarehe 04/10/2015 majira ya saa 05:45hrs huko Msolwa Kata ya Bwilingu barabara kuu ya Dar es Salaam – Morogoro, Wilaya ya Ki-Polisi Chalinze, Mkoa wa Pwani. Gari No. T.189 AGM aina ya Toyota Corolla likiendeshwa na George Steven Ponera miaka 31, mkazi wa Mbezi Mwisho Dar es Salaam liliacha barabara kisha kupinduka na kusababisha kifo cha Christopher Mtikila miaka 62, mpangwa, mchungaji wa Kanisa la Assemblies, na mwenyekiti wa Chama cha siasa DP mkazi wa Kinondoni “B” Dar Salaam.

Katika ajali hiyo, watu watatu waliokuwamo ndani ya gari hilo na marehemu Mchungaji Mtikila walijeruhiwa ambao ni Ally Mohamed miaka 42 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam, yeye alipata maumivu shingo, mabegani na kifuani, mwengine ni Patrick Mgaya miaka 37 ambaye ni mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God mkazi wa Mbagala Dar es Salaam ambaye alikuwa na michubuko midogo usoni na kuumia kichwani, pamoja na George Steven miaka 31 mkazi wa Mbezi Dar es Salaam ambaye alipata michubuko kidogo eneo la mabegani. Majeruhi wote walipatiwa matibabu katika Kituo cha afya Chalinze na badae wawili kati yao katika Hospitali teule ya Tumbi na waliruhusiwa kutokana na hali zao kuendelea vizuri.

Baada ya kutokea kwa hiyo ajali, timu maalum ilifika katika eneo la tukio kwa ajili ya ufuatiliaji wa ajali hiyo ikiongozwa na Mkuu wa utawala wa Traffic kuu Dar es Salaam SACP J. Kahatano, pamoja na mimi mwenyewe, Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Mkoa wa Pwani na kuwashirikisha wataalamu wa Forensic Makao Makuu ya Polisi ACP Kashindye na Dokta A. Makata.

Uchunguzi wa mwili wa marehemu tayari umefanyika, na taarifa ya Daktari aliyefanya uchunguzi huo katika Hospitali ya Rufaa tumbi Kibaha jana tarehe 04/10/2015 umeonyesha kuwa, kifo cha marehemu kimesababishwa na kuvunjika kwa mbavu nane (8) upande wa kushoto na kuingia kwa damu kwenye mfumo wa hewa na kusababisha kushindwa kupumua.

Kabla ya ajali hiyo kutokea marehemu na wenzake tarehe 02/10/2015 jioni waliondoka Dar es Salaam kwenda Mkoa wa Njombe na kufika tarehe 03/10/2015 alfajiri kwa ajili ya kampeni za Chama chao cha DP. Wakiwa huko walipata ajali kwa kugonga magari mawili yaliyopata ajali na kusababisha uharibifu wa gari lao.

Kulingana na taarifa ya Mkaguzi wa magari ya tarehe 03/10/2015 huko Njombe walishauriwa walitengeneze kwanza kabla ya kulitumia tena.

Tarehe 03/10/2015 saa 21:30hrs waliondoka Njombe kwenda Dar es Salaam na ilipofika saa 05:45hrs katika eneo la Msolwa ndipo wakapata ajali hii.

Uchunguzi uliofanywa kwa kukagua tukio na kuwahoji majeruhi walionusurika (katika eneo hilo hakuna watu wengine walioshuhudia tukio hilo kwa kuwa si eneo la makazi ya watu, ni mbuga). Ajali hii imeonyesha kuwa imesababishwa na sababu zifuatazo:
 1. Mwendo kasi, dereva mwenyewe anakubali kwamba alikuwa mwendo kasi licha ya kuwepo kwa alama zinazooonyesha kwenda mwendo wa Km 50 kwa saa. Aidha baada ya kuacha barabara kuu, gari hilo lilikwenda umbali wa mita 125 kabla ya kupinduka hali inayoashiria kuwa lilikuwa kwenye mwendo kasi.

 2. Uchovu wa dereva kutokana na safari ndefu kwa kuendesha gari mchana na usiku kucha kabla ya kuanza safari walikuwa wakishughulikia matengenezo ya gari hilo ambapo hakupata muda wa kupumzika.

 3. Kutofunga mkanda ya usalama. Katika uchunguzi inaonyesha marehemu hakufunga mkanda kwa kuwa alirushwa nje kupitia kioo cha mbele (wind screen).

 4. Ubovu wa gari. Gari hilo lilipata ajali tarehe 03/10/2015 na moja ya sehemu muhimu iliyoharibika ni mfumo wa usukana (steering system) yawezekana halikupata matengenezo kikamilifu na hivyo kuchangia kutokea kwa ajali hiyo.
Hivyo nitumie fursa hii kuwaomba wananchi kuwafichua maderva wanaokwenda mwendo kasi kupitia namba 08007575 ama 0715 009953 au 0658 376012. Aidha niwatake madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani na kwa wale watakao kaidi Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani hatutasita kuwachukulia hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengi.

Asanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani

Kamishina Msaidizi Jafari Ibrahim.

Internet Top 20 Countries by end of June 2015

TOP 20 COUNTRIES WITH HIGHEST NUMBER OF
INTERNET USERS - JUNE 30, 2015
#
Country or Region
Population,2015 Est
Internet Users
Year 2000
Internet Users
June 2015
Penetration
(% Population)
% Growth
2000 - 2015
1
China1,361,512,53522,500,000
674,000,000
49.5 %
2,895.6 %
2
India1,251,695,5845,000,000354,000,000
28.3 %
6,980.0 %
3
United States321,362,78995,354,000
280,742,532
87.4 %194.4 %
4
Brazil204,259,8125,000,000
117,653,652
57.6 %
2,253.1 %
5
Japan
126,919,659
47,080,000
114,963,827
90.6 %
144.2 %
6
Russia146,267,2883,100,000
103,147,691
70.5 %
3,227.3 %
7
Nigeria
181,562,056
200,000
92,699,924
51.1 %
46,250.0 %
8
Indonesia
255,993,674
2,000,000
73,000,000
28.5 %
3,550.0 %
9
Germany81,174,00024,000,000
71,727,551
88.4 %
198.9 %
10
United Kingdom64,767,11515,400,000
59,333,154
91.6 %
285.3 %
11
Mexico
121,736,809
2,712,400
59,200,000
48.6 %
2,082.6 %
12
France
66,132,169
8,500,000
55,429,382
83.8 %
552.1 %
13
Egypt
88,487,396
450,000
48,300,000
54.6 %
10,633.3 %
14
Philippines
109,615,913
2,000,000
47,134,843
43.0 %
2,256.7 %
15
Iran81,824,270250,000
46,800,000
57.2 %
18,620.0 %
16
Turkey77,695,9042,000,000
46,282,850
59.6 %
2,214.1 %
17
Vietnam94,348,835200,000
45,579,922
48.3 %
22,690.0 %
18
Korea49,115,19619,040,000
45,314,248
92.3 %
138.0 %
19
Bangladesh168,957,745100,000
44,625,000
26.4 %
44,525.0 %
20
Italy60,795,61213,200,000
37,668,961
62.0 %
185.4 %
TOP 20 Countries4,914,224,361268,086,400
2,417,603,537
49.2 %
801.8 %
Rest of the World2,346,396,75792,899,092
852,887,047
36.3 %
818.1 %
Total World Users7,260,621,118360,985,492
3,270,490,584
45.0 %
806.0 %
NOTE: Top 20 Internet User Statistics were updated for June 30, 2015. 

The Top Twenty Page shows the list of the 20 top countries in the Internet ordered according to the number of users in each country. There will surely be some surprises in this list. Let's look at the table and analyze the information.

First in the list is China with 674 million estimated Internet users, in second place is India with 354 million Internet users. The USA is now third in the world, with 281 million Internet users. China, India and the United States are by far the top three countries in Internet with a total of over 1,308 million Internet users.

Next comes a group of 3 countries with almost 336 million Internet users. They are Brazil, Japan and Russia. Internet use in these three countries is well established and mature. Japan has over 90% Internet penetration.

It is interesting to point out that the group of the Top 20 Internet countries has grown from 268 million users in year 2000 to 2,417 million users in 2015, a 801.8% increase in 15 years.

Another interesting fact is that the Top 20 countries comprise 73.9% of all the Internet users in the world. By the way, Internet users is a good example of the Pareto Principle, also called the 80/20 rule. About 80% of all the Internet users is contained in 20% of the world countries.

Enrique de Argaez, CEO
Miniwatts Marketing Group
www.internetworldstats.com

TAKUKURU yazindua jengo la ofisi zao MbeyaMkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini, Dkt. Edward Hoseah akizungumza katika sherehe za uzinduzi wa jengo la ofisi mpya ya TAKUKURU Mkoa wa Mbeya ambapo amesema kuwa Taasisi hiyo imeweza kufanikiwa kupambana na rushwa kwa kiasi kikubwa ambapo jumla kesi kubwa za rushwa 1,993 kuanzia mwaka 2004-2015 zimeweza kufunguliwa ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 81 ikilinganishwa na kesi 384 zilizokuwepo miaka 10 ilioyopita (1995-2004) .

Rais Kikwete akutana na Rais Uhuru na kuzuru kaburi la Mzee Jomo Kenyatta


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Nairobi leo Jumatatu October 5, 2015 alipokwenda kwa mapokezi rasmi ya ziara yake pamoja na mazungumzo na hatimaye kuaga

Value of Dual Citizenship for African’s wishing to take advantage of opportunities within Africa and abroad

It is estimated that only around 1% of the world’s population have two or more passports, making dual citizenship an exclusive privilege

JOHANNESBURG, South Africa, 5 October 2015/ --  “No man is an island” is the theme of this year’s upcoming Investment Agenda, being held in Johannesburg on the 20th of October.Leading investors, asset managers and industry experts will assemble to examine the prevailing economic and political environment in Africa and its impact on investment strategy in 2016.

In light of this conference, Monarch&Co International
emphasizes the value of dual citizenship, especially for African’s wishing to take advantage of opportunities within the continent and abroad. Holding the passport of another country can open opportunities for business, education, healthcare and visa-free travel for investors and their families.

Monarch&Co International are specialists in residency and citizenship by investment programmes and currently have a wide portfolio of countries around the world for investors to choose from. Among the countries that offer the best benefits are, Antigua & Barbuda, Cyprus (EU), Grenada, Malta (EU), Mauritius, Portugal (EU), St Kitts & Nevis, the UK (EU) and the USA.

According to statistics, it is estimated that only around 1% of the world’s population have two or more passports, making dual citizenship an exclusive privilege. While in the past it was only possible for people to attain dual citizenship through their ancestry or emigration, many countries have now made it possible for applicants to gain residency or citizenship through various investment programmes without ever having to emigrate.

By making a substantial investment into either a business venture or the purchase of real estate, investors can apply for residency and / or citizenship in a foreign country. James Bowling, CEO of Monarch&Co, says that investors are particularly interested in obtaining citizenship in countries that are members of the European Union (EU). This is largely due to the benefits afforded to EU citizens including right of free movement, settlement and employment across all EU member states. Whilst Bowling agrees that the EU offers unparalleled opportunity, other countries can offer similar and / or different benefits that may better suit other investor requirements. These countries can include the USA, Grenada and Antigua & Barbuda. Therefore, the choice of country really concerns the primary reason for investment, explains Bowling.

Bowling highlights five advantages of gaining dual residency and / or citizenship:

A Lifestyle Hedge

The lifestyle benefits that investors could reap include access to better basic services such as healthcare, education, security and transport.
A Financial Hedge

A hard currency investment is a good currency hedge. “Many are looking for investment options that allow them to financially hedge against future economic uncertainty in their home country. Some of the programmes offer investors returns of up to 6.5% as well as buy-back guarantees once they qualify for citizenship – allowing investors to earn returns in foreign currency - these countries include Grenada and Antigua and Barbuda.

Unrestricted Travel

Freedom of travel is one of the major benefits of these programmes. “Many of our clients incur huge travel inconveniences when travelling abroad owing to the conditions set on them by virtue of the passport that they carry.  Visa applications are both costly and time consuming and generally an irritating nuisance. Through residency and citizenship programmes, investors can gain travel benefits through obtaining another citizenship that has fewer travel restrictions and visa requirements,” says Bowling.

Tax Breaks

Bowling points out that by gaining a second citizenship, investors are also able to enjoy tax breaks as well as the possibility of improved personal and corporate tax exposure. “The extent of these benefits would depend on the new jurisdiction’s offering and incentives as well as where the client makes their primary tax residence.”

Family Security

Investors who are looking for better schooling opportunities for their children, a safe environment in which to raise their families, or just a better quality of life, are attracted by the benefits of dual citizenship.

“There are many reasons why dual residency and citizenship appeals to many investors, but mostly it revolves around the second passport, which is their key to a world of free movement, greater flexibility, and legal tax reduction,” Bowling concludes.

Media contact :
Bridget Meyer
International Marketing Manager
e: [email protected]
t: +27 (0)11 322 4400